Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,447
- 7,832
January Makamba: Hakuna uhaba wa mafuta nchini. Hakuna sababu ya kuwa na taharuki. Utaratibu wa kuingiza mafuta unahakikisha kwamba mahitaji yapo wakati wote. Serikali inaendelea kuchukua hatua kuongeza uhakika wa upatikanaji na unafuu wa bei.
Akijibu swali la mdau alieuliza mkanganyiko kati ya mkurugenzi wa TPDC na kauli yake kujichanganya, Makamba amesema yake ni Kauli ya uhakika ya Serikali. Mkurugenzi wa TPDC atatoa taarifa kuhusu taarifa yake kwasababu aliitoa kwenye semina ya wanahabari lakini ni gazeti moja tu ndio limeandika.
Pia amemtaka mkurugenzi wa TPDC aende ofisini kutoa maelezo kabla hajachukuliwa hatua za ziada.
Aidha, amesema Dizeli iliyopo kwenye matenki nchini hadi leo asubuhi ni lita milioni 90.7. Meli inayoitwa SLOANE SQUARE muda huu inashusha lita milioni 60.9 hivyo kupelekea mafuta ya dizeli kuongezeka na kuwa lita 151,694,926 yanayotosheleza kwa siku 24.
Petroli iliyopo kwenye matenki nchini hadi leo asubuhi ni lita 100,345,631. Meli iitwayo JAMES COOK inashusha lita 22,493,188; meli iitwayo JAG PUNIT iko njiani na lita 30,579,019 hivyo kupeleka mafuta ya petroli kuongezeka na kuwa lita 153,417,838 yanayotosheleza kwa siku 34
Pia soma > TPDC: Mafuta yaliyopo yatosha siku 15