Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,017
- 9,885
Leo ikiwa ni siku ya Hukumu ya Mbunge wa Kigoma Mjini, Waandishi wenye Press Cards wamekataliwa kuingia kusikiliza hukumu ya Zitto kwa maelezo kwamba si waandishi wa Mahakama.
UPDATE
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Ndugu Zitto ameachiwa huru kwa sharti kwamba asitoe matamshi ya uchochezi katika kipindi cha mwaka mmoja.
Zitto kukata Rufaa dhidi ya hukumu yake
TAARIFA KWA UMMA
Chama cha ACT Wazalendo kimepokea kwa mshtuko taarifa ya kutiwa hatiani kwa Kiongozi wa Chama Ndugu Zitto Zuberi Ruyagwa Kabwe ambaye alishitakiwa mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkaazi Kisutu na kukabiliwa na mashtaka matatu chini ya Sheria ya Vyombo vya Habari.
Kwa mujibu wa hukumu iliyosomwa leo na Hakimu Huruma Shaidi, Ndugu Zitto ametiwa hatiani kwenye makosa yote matatu na kuachiwa huru kwa sharti la kutotoa matamshi ya kichochezi katika kipindi cha mwaka mmoja.
Ndugu Wananchi na Wanachama wa ACT Wazalendo, kwa sasa itoshe tu kusema kuwa Chama cha ACT Wazalendo kinapokea na kuyaheshimu maamuzi ya Mahakama ya Hakimu Mkaazi Kisutu yaliyotolewa leo na Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi na kwamba kwa sasa Chama kinasubiri kupokea ushauri wa mawakili wa Ndugu Zitto Kabwe kuhusu tafsiri ya hukumu hiyo na hatua sahihi za kuchukua.
Muda mfupi uliopita, nimeongea na Kiongozi wetu na amenihakikishia kuwa yupo imara na kamwe hukumu hii haitamrudisha nyuma. Mapambano ya kuondoa mfumo kandamizi na uchumi goigoi lazima yaendelee. Aluta Continua!!
Wakati tukiendelea kusubiri tafsiri na ushauri wa wanasheria, nichukue fursa hii kwa niaba ya Chama kuwataka wanachama wote mtulie katika kipindi hiki huku mkisubiri taarifa mbali mbali zitakazotolewa na Chama kupitia viongozi wenu.
Tunachukua fursa hii pia kuwapongeza mawakili wote ambao wamefanya kazi kubwa sana tangu mwanzo hadi mwisho wa kesi hii. Mawakili hao ni Stephen Mwakibolwa, Bonifasia Mapunda, Peter Kibatala, Jebra Kambole na Jeremia Mtobesya.
Asanteni na nashukuru sana!
Dorothy J. Semu,
Makamu Mwenyekiti Bara,
ACT Wazalendo.
29 Mei 2020.