Zitto Kabwe anahutubia Kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama, Februari 12, 2024

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,988
Chama cha ACT Wazalendo kinafanya kikao chake cha kikatiba cha Halmashauri Kuu ya Chama, leo Februari 12, 2024 kwenye Ukumbi wa Halmashauri Kuu wa Hakainde Hichilema uliopo katika ofisi za Makao Mkuu ya Chama, Magomeni Dar es Salaam.

Taarifa ya ACT imeeleza kuwa Halmashauri Kuu inafanyika kwa mujibu wa Ibara ya 74(1) ya Katiba ya ACT Wazalendo ya mwaka 2015 toleo la mwaka 2020.

Hiki ni kikao cha pili cha maamuzi kwa ukubwa baada ya Mkutano Mkuu wa Chama. Wajumbe wanaounda kikao hiki ni Wenyeviti na Makatibu wa Mikoa yote 39 ya kichama kutoka Bara na Zanzibar pamoja na wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama.

Miongoni mwa ajenda muhimu zitakazojadiliwa na kutolewa maamuzi katika kikao hiki ni pamoja na maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Chama Taifa uliopangwa kufanyika kwa siku mbili mfululizo, tarehe 05 na 06 Machi, 2024.

Ajenda nyingine ni kupokea taarifa ya ujenzi wa Chama. Halmashauri Kuu pia itapitia na kutoka na mapendekezo ya maboresho ya Katiba ya Chama kwa kuzingatia maoni yaliyokusanywa kutoka kwa wanachama na wadau mbalimbali wa demokrasia.

Katika hatua nyingine, Halmashauri Kuu itapokea na kupitia mapendekezo ya Sera ya Chama ya Jinsia na kisha kupitisha Sera hiyo inayolenga kuweka misingi ya usawa wa kijinsia katika nafasi na ngazi zote za uongozi wa ACT Wazalendo.


Kiongozi wa ACT Wazelendo, Zitto Kabwe anahutubia umma kupitia Wajumbe wa Halmashauri Kuu.
Zito_page-0003.jpg

Zito_page-0004.jpg

Zito_page-0005.jpg

Zito_page-0006.jpg

Zito_page-0007.jpg

Zito_page-0008.jpg

Zito_page-0009.jpg

Zito_page-0010.jpg

Zito_page-0011.jpg

Zito_page-0012.jpg
 
Kiongozi wa utaratibu asie chuja kwenye medani 🐒

Alifanyaga political blunder moja kali sana uchaguzi mkuu 2020 kumdump mgombea urais wake Bernard Kamilius Membe na kumuunga mkono Puppet 🐒

Hii political mistake itamsumbua sana saikologically maisha yake yote ya siasa 🐒

R.I.P Laigwanan comrade EL
 
Hongereni sana ACT Wazalendo mmeonesha kwa vitendo namna ya kutengeneza CHAMA cha SIASA chenye mifumo, miundo na nguzo. Hakika sasa mnaelekea mahala pazuri sana.
 
Huyu mkongomani mbona kachoka hivi jamani? Sura imeanza kufanana na mkongomani mwenzake Ibrahim Haruna Lipumba
 

Attachments

  • 20240209_070737.jpg
    20240209_070737.jpg
    29.7 KB · Views: 2

Similar Discussions

Back
Top Bottom