Mahakama yamtia hatiani Zitto Kabwe katika kesi yake ya Uchochezi. Atakiwa kutotoa matamshi ya Uchochezi kwa mwaka 1. Asema kukata Rufaa

Amesamehewa kwa kuzusha uwongo na ameambiwa asirudie
Mkuu, si wewe utathibitisha ni uongo au ni kweli. Au alikuwa anafurahisha watu mitandaoni. Au amebaki peke yake.

Jiepushe na kuzungumzia nadharia na vitu usivokuwa na uthibitisho navyo.

Mwache hakimu, mawakili wafanya kazi zao. Mahakama sio sehemu ya hisia.
 
Halafu mbona kama naona zitto is always doing extreme stuffs and he gets away with them stuffs.
Ni kwamba zitto anajua mipaka yake sana au kuna kitu nyuma ya pazia.

Yaani anaweza tu akatoa maneno makali mazitoo mwisho wa siku husikii akapigwa kashkash kama za wapinzani wengine.
Just sinking!
Kama hii kesi nilitegemea angepigwa fine lakini eti asitoe maneno ya uchochezi kwa mwaka mmoja kwahiyo baada ya mwaka wembe ni ule ule.
 
Leo ikiwa ni siku ya Hukumu ya Mbunge wa Kigoma Mjini, Waandishi wenye Press Cards wamekataliwa kuingia kusikiliza hukumu ya Zitto kwa maelezo kwamba si waandishi wa Mahakama.

UPDATE

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Ndugu Zitto ameachiwa huru kwa sharti kwamba asitoe matamshi ya uchochezi katika kipindi cha mwaka mmoja.

Ungesema ukweli tu. Hapo katiwa hatiani na kapewa kifungo cha nje cha mwaka mmoja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Halafu mbona kama naona zitto is always doing extreme stuffs and he gets away with them stuffs.

Ni kwamba zitto anajua mipaka yake sana au kuna kitu nyuma ya pazia.
Yaani anaweza tu akatoa maneno makali mazitoo mwisho wa siku husikii akapigwa kashkash kama za wapinzani wengine.
Just sinking!

Endelea ku-sink!
 
Zito anapenda kuvunja sheria

Uwongo wake na upotoshaji ndio umemfikisha pale

Alikuwa anafurahisha watu mitandaoni amebaki peke yake
Hivi unajua ata Apartheid ilikua sheria halali?
Hivi unajua seditious case ilitungwa mwaka 1952 na mwaka 1954 ilianza kufanya kazi na mchonga ilimtia hatiani?
 
Aise mahakama inakosaje kesi ya kumpa mtu?

Wangempa hata kesi ya kuishi karibu na Ziwa Tanganyika
 
Zito ajifunze sasa aache mambo ya kuzusha mtandaoni

Ipo siku ndumba zake za ujiji zitatunda kufanya kazi aozee jela
Sawa hata meko ajifunze kua tumempa ajira aache kufisadi na kuendesha bunge kama yuko kwao kilimani.
 
Halafu mbona kama naona zitto is always doing extreme stuffs and he gets away with them stuffs.
Ni kwamba zitto anajua mipaka yake sana au kuna kitu nyuma ya pazia.
Yaani anaweza tu akatoa maneno makali mazitoo mwisho wa siku husikii akapigwa kashkash kama za wapinzani wengine.
Just sinking!
Mkuu conviction ya mhe. Huruma shaidi kwa zito ni ya ajabu sana, unaposema nimekuachia huru ila usiseme maneno ya uchochezi ndani ya mda fulani ana maana kwamba amemtia hatiani zito?
 
Mahakama imemuachia huru mh Zitto Kabwe kwa masharti kuwa asikutwe na kosa lolote linalohusiana na masaula ya uchochezi ama kutoa kauli yoyote yenye viashiria vya uchochezi kwa muda wa mwaka mmoja.

Nini maoni yako kwa hukumu hii ya mahakama dhidi ya mh Zitto?

Sio kwamba amewekewa tanzi (mtego) wa kumtia hatiani kutokana ukweli kwamba Mh Zitto ni mwanaharakati na ni wazi kuwa hatoweza kunyamaza kwenye baadhi ya mambo ambayo kwa namna moja ama nyingine si rafiki kwa mustakabali wa taifa letu.
 
Leo ikiwa ni siku ya Hukumu ya Mbunge wa Kigoma Mjini, Waandishi wenye Press Cards wamekataliwa kuingia kusikiliza hukumu ya Zitto kwa maelezo kwamba si waandishi wa Mahakama.

UPDATE

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Ndugu Zitto ameachiwa huru kwa sharti kwamba asitoe matamshi ya uchochezi katika kipindi cha mwaka mmoja.

Pole na hongera ZZK.Ni kipindi kigumu na inawezekana umewekwa katika mtego mkali zaidi. Ngoja tusubiri ya Bi Shost Halima Mdee.
 
Mahakama imemuachia huru mh Zitto Kabwe kwa masharti kuwa asikutwe na kosa lolote linalohusiana na masaula ya uchochezi ama kutoa kauli yoyote yenye viashiria vya uchochezi kwa muda wa mwaka mmoja.

Nini maoni yako kwa hukumu hii ya mahakama dhidi ya mh Zitto
Kama ana kosa kwa nini aachiwe huru kwa mashariti ya kutorudia kosa?
 
Back
Top Bottom