Nyakijooga
Senior Member
- Dec 9, 2018
- 123
- 202
Kesi itakayotolewa uamuzi Leo ni kesi iliyofunguliwa na Mwanaharakati Bob Chacha Wangwe dhidi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo inapinga Vifungu vya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi ambavyo vinaruhusu wakurugenzi kuwa wasimamizi wa uchaguzi, ikidiwa kuwa 'makada wa Chama Cha Mapinduzi' ambacho ni chama tawala hivyo mpeleka maombi anadai kuwa ni vigumu uchaguzi kuwa wa huru na wa haki, lakini pia inadaiwa kuwa vifungu hivyo vinakiuka haki ya usawa mbele ya sheria ikiwa ni pamoja na haki ya wananchi kuchagua viongozi wao wanaowataka kwa uhuru.
UPDATES:
Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu imeagiza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufanya marekebisho ya sheria ya Taifa ya uchaguzi inayotoa uhalali kwa Wakurugenzi (DED) kusimamia uchaguzi.
Uamuzi huo umetolewa kufuatia kutupilia mbali kwa mara nyingine ushahidi wa upande wa Serikali kwenye ile kesi ya kupinga hiyo.
Kufuatia maelekezo hayo mahakama hiyo imeielekeza Serikali ndani miezi 12 kupeleka ripoti ya utekelezaji wa uamuzi huo.
Ikumbukwe Kesi hiyo ambayo uamuzi wake umetolewa leo June 13, 2023, ilifunguliwa na Mwanaharakati Bob Chacha Wangwe dhidi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo inapinga Vifungu vya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi ambavyo vinaruhusu wakurugenzi kuwa wasimamizi wa uchaguzi,
Ambapo mlalakaji alidai kuwa Wakurugenzi hao ni 'makada wa Chama Cha Mapinduzi' ambacho ni chama tawala hivyo kumpelekea uchaguzi kushindwa kuwa wa huru na wa haki. Lakini pia inadaiwa kuwa vifungu hivyo vinakiuka haki ya usawa mbele ya sheria ikiwa ni pamoja na haki ya wananchi kuchagua viongozi wao wanaowataka kwa uhuru.
Inaweza kukumbukwa kwenye uchaguzi wa mwaka 2020 baadhi ya wadau hususani wanasiasa wa vyama vya upinzani Tanzania na Wanaharakati walikosoa vipengere hivyo vinavyotoa mamlaka kwa Wakurugenzi kusimamia uchaguzi, wakitaja Wakurugenzi hao waliokuwa na dhamana kuwa ni makada wa Chama tawala hivyo ilikuwa ni vigumu kwao kusimamia misingi na taratibu za uchaguzi licha ya baadhi ya wengine kuwa na mtazamo tofauti.
Akizungumza kuhusu kesi hiyo mara baada ya uamuzi,Wakili wa upande wa mleta maombi, Jebra Kambole amesema kuwa walichukua uamuzi wa kufungua shauri hilo wakiamini wanaweza kupata haki licha ya kushindwa kwenye mahakama ya rufaa.
“Baada ya kushindwa hiyo kesi mahakama ya Rufaa tuliamini kuna haki zetu hazijawa sawa kwahiyo tukapeleka kesi kwenye mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, kwamba vile vifungu vinavyotoa mamlaka kwa wakurugenzi (DED) vinakiuka mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu”amesema Wakili Jebra Kambore
Ameongeza kuwa “Mahakama imekubaliana na sisi kuwa sheria haijaweka vigezo vya Wakurugenzi hao kusimamia uchaguzi, mahakama imeona kuwa kutokana na kutokuwepo kwa vigezo ni kwamba mtu yoyote anaweza kusimamia uchaguzi. Mahakama imesema Wakurugenzi wasisimamie uchaguzi"
Ikumbukwe Kesi hiyo ambayo uamuzi wake umetolewa leo June 13, 2023, ilifunguliwa na Mwanaharakati Bob Chacha Wangwe dhidi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo inapinga Vifungu vya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi ambavyo vinaruhusu wakurugenzi kuwa wasimamizi wa uchaguzi.