Kamati ya Bunge yapendekeza isiwe lazima kwa Wakurugenzi wa Halmashauri, Miji na Majiji kusimamia Uchaguzi

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,279
9,719
Ndugu zangu Watanzania,

Kamati ya Bunge Utawala, Sheria na Katiba imependekeza kuwa isiwe lazima kwa Wakurugenzi wa Halmashauri, Miji na Majiji kusimamia Uchaguzi.

Pia kamati imependekeza kuwa badala ya kuitwa Tume ya Taifa ya uchaguzi iitwe Tume huru ya uchaguzi.

Kazi iendelee, mama ametufikia na kuwafikia Watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

==============

Kamati ilikuwa ina maoni kwamba Sheria isiweke ulazima kwa Mkurugenzi Mtendaji kusimamia Uchaguzi na badala yake, kuwepo na masharti ya Mtumishi wa Umma mwandamizi ama mtu mwingine yoyote mwenye sifa kuteuliwa kuwa Msimamizi wa Uchaguzi au Msimamizi msaidizi wa Uchaguzi.

Serikali iliona kuwa upo umuhimu wa Wakurugenzi Watendaji kutajwa kwenye sheria kwa kuwa Mahakama ya Rufani ya Tanzania kwenye kesi ya madai na. 138/2019 na Mahakama ya Afrika ya Watu na Haki za Binadamu kwenye kesi ya madai na ziliamua kuwa Wakurugenzi kusimamia Uchaguzi haukiuki masharti ya Katiba wala Mkataba wa Afrika wa Watu na Haki za Binadamu mtawalia.

Ibara ya 6(1) inaeleza kuwa kila Mkurugenzi wa Jiji, Mkurugenzi wa Manispaa, Mkurugenzi wa Mji na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya atakuwa Msimamizi wa Uchaguzi kwa madhumuni ya kuendesha uchaguzi katika Jimbo au Kata

Hawakubaliani na Wakurugenzi wa Halmashauri na watumishi wa umma kusimamia uchaguzi kwa kuwa hawawajibiki kwa tume ya uchaguzi bali wanawajibika kwa Rais na Chama Tawala hivyo wanakosa sifa ya kuwa mamlaka ya uchaguzi huru na haki. Vifungu hivyo vifutwe na Tume iajiri watumishi wake wenyewe

Kamati bado ina maoni kuwa hakuna ulazima wa sheria kuweka sharti kwa Mkurugenzi wa Jiji, Manispaa, Mji na Wilaya kuwa wasimamizi wa uchaguzi au wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi kwa kuwa uzoefu unaonyesha wapo Wakurugenzi kwa sababu mbalimbali wanapoteza sifa za kuwa wasimamizi wa uchaguzi.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kamati ya Bunge Utawala, Sheria na Katiba imependekeza kuwa isiwe lazima kwa Wakurugenzi wa Halmashauri, Miji na Majiji kusimamia Uchaguzi.

Pia kamati imependekeza kuwa badala ya kuitwa Tume ya Taifa ya uchaguzi iitwe Tume huru ya uchaguzi.

Kazi iendelee, mama ametufikia na kuwafikia Watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
Wewe ni bendera fuata upepo.Unapigania tumbo lako tu.
 
Hatutaki porojo za kijinga , tunataka Wakurugenzi wapigwe marufuku , hao ni mamluki wa ccm
Hata ije Tume ya uchaguzi kutoka marekani bado CCM itapita na kushinda kwa kishindo kikuu kitakacho itetemesha Dunia nzima.hii ni kutokana na kuwa na sera nzuri zinazogusa maisha ya watu,pamoja na utekelezaji bora wa ilani yake ambao umekuwa ukibeba na kusheheni mambo na vitu vinavyogusa mahitaji ya watu na wakati. Tofauti na vyama vya upinzani kama CHADEMA havina hata uwezo wa kuandaa ilani ya uchaguzi
 
30 January 2024
Kikao cha Bunge
Dodoma
Tanzania

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge utawala, sheria na katiba Dr. Joseph Kizito Mhagama akisoma maoni ya kamati yake, amesema wanapendekeza sheria isiweke ulazima wakurugenzi kusimamia uchaguzi, kwa kuwa wapo wakurugenzi mji, manispaa, mkurugezi wa halmashauri ya wilaya hawana sifa.....

View: https://m.youtube.com/watch?v=SyqMiHQSZoY
Dr. Joseph Kizito Mhagama akinukuu aya za awali wakati ikiwakilisha muswaada mwezi November 2023, lakini kamati imeona hakuna ulazima kwani kwa sifa mbalimbali zinawafanya wakurugenzi kukosa sifa, hivyo kamati inawasilisha maoni ya marekebisho kuondoa ulazima wa wakurugenzi kusimamia uchaguzi aongeza Dr. Joseph Kizito Mhagama ....
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kamati ya Bunge Utawala, Sheria na Katiba imependekeza kuwa isiwe lazima kwa Wakurugenzi wa Halmashauri, Miji na Majiji kusimamia Uchaguzi.

Pia kamati imependekeza kuwa badala ya kuitwa Tume ya Taifa ya uchaguzi iitwe Tume huru ya uchaguzi.

Kazi iendelee, mama ametufikia na kuwafikia Watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
PUMBAFU! Haiwezekani iitwe 'tume huru ya uchaguzi' bila kufanyika mabadiliko muhimu kama mdau wa uchaguzi ndio anateuwa wasimamizi na wakuu wa tume ya uchaguzi
 
30 January 2024

Mh. Jestina Mhagama : Maelezo ya Serikali na Kamati ya Bunge Juu ya Muswada wa Sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi

View: https://m.youtube.com/watch?v=kolUX3Ccqzg

Waziri wa nchi Ofidi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge Mh. Jestina Mhagama kwa niaba ya mheshimiwa waziri mkuu leo mbele ya Bunge mwezi Januari 30,2024, ...... kuhusu sheria uchaguzi wa rais, wabunge na madiwani leo mheshimiwa rais anaenda kuvunja rekodi katika eneo hili la kukuza demokrasia, anaanza ktk utangalizi Mh. Jesting Mhagama ....

Utaratibu wa mapingamizi, serikali ina leta jedwali la marekebisho ya mswada ....

Masharti ya mgombea wa urais,...mapingamizi, siku ya kupiga rais, mazingira ya upigaji kura n.k rais ili kuondoa utaratibu ambao upo sasa ambapo masharti ya mgombea urais unafanana na zile za wagombea nafasi za ubunge ....

Sura 5 masharti ya kura za udiwiwani serikali inapendekeza marekebisho ...
 
Hata ije Tume ya uchaguzi kutoka marekani bado CCM itapita na kushinda kwa kishindo kikuu kitakacho itetemesha Dunia nzima.hii ni kutokana na kuwa na sera nzuri zinazogusa maisha ya watu,pamoja na utekelezaji bora wa ilani yake ambao umekuwa ukibeba na kusheheni mambo na vitu vinavyogusa mahitaji ya watu na wakati. Tofauti na vyama vya upinzani kama CHADEMA havina hata uwezo wa kuandaa ilani ya uchaguzi
Tokea asubuhi hapa Kariakoo umeme hakuna ni majenereta tu yanafanya kazi je; hiyo ndio sera ya ccm?.
 
Back
Top Bottom