Mafuriko makubwa yaikumba Dar es Salaam

Mafuriko makubwa yaikumba Dar es Salaam

Why should I care about maofisi ya serikali? Kwani kila wakati wanaokuwa katika majaribu ya maisha ni hao walioko Azikiwe au walioko Mabondeni? Hivi hapa mada ni kubomoka kwa mabarabara na madaraja au madhira wanayopata watu wa mabondeni? Hivi hata huko unakosema kungekuwa na a cery excellent infrastructure, hao watu wa Jangwani, Msimbazi and the like wangeokoka vipi?

Kwamba kama utashi wa watu ungekuwa ufanye kazi basi kusingekuwa na serikali, serikali mara zote itabaki kuwa mwelekezaji na ni mwananchi mwenyewe ndie mwenye wajibu wa kutekeleza maelekezo! Hata humu majumbani mwetu tunaishia tu kuelekezana na kukaripiana; "acha wizi" "acha uhuni" "acha hiki na kile" lakini tunapokuwa wakahidi hata wazazi nao hututupa mkono vinginevyo jela hivi sasa zingejaa watoto waliopelekwa huko na wazazi wao wenyewe baada ya kuwakaripia hili na lile na baada ya kuona hawasikii wanaamua kuwapeleka polisi! Kama bado ni mtoto mdogo, baba ako atakukanya na usiposikia atakutandika hadi mikwaju lakini ukishakuwa mtu mzima ataishia kukukanya na usiposikia, atakauacha kama ulivyo! Wale watu wa mabondeni ni mijitu mizima na akili zao na wote wanafahamu nini kitawakuta lakini tatizo huwa wanafanya mahesabu, kwamba kati ya siku 365 za mwaka, ni chini ya siku 7 ndizo watahangaika!
Mkuu kujiua ni kosa kisheria, na kama utakamatwa ukawa katika harakati za kujiondoa uhai sheria hiyo itakubana, je kwanini hao wanao jenga kingoni mwa mito sheria hiyo isitumike dhidi yao?
 
Wakuu heshima kwenu;

Wakazi wa jiji la Dar es Salaam wamejikuta tena kwenye sintofahamu kubwa kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha tangia jana.

Maeneo mengi hali ni mbaya kutokana na mvua kunyesha kwa wastani wa saa 14 mfululizo!

Nimetokea maeneo ya Tegeta hali ni mbaya. Nyumba zimejaa maji. Maeneo ya Mbezi kutokea Goba kuna magari yametelekezwa njiani kutokana na maji mengi. Kuna gari dogo ya Toyota (jamii ya saloon kama sikosei) Imetelekezwa hapa Mbezi tangi bovu na imefunikwa na maji yanayotokea huku ukanda wa juu! Pia nyumba nyingi maeneo haya ya Mbezi beach zimezingirwa na maji na zimetelekezwa!

Nimepita Sinza hali ni mbaya sana. Maji yapo kila kona, njia hazipitiki!

Stendi ya Makumbusho asubuhi ya leo ilikuwa na daladala chache sana.

Barabara nyingi zinaongozwa na mataa badala ya askari wa trafic. Mfano mataa ya Chang'ombe kitu ambacho ni nadra sana na ni kutokana na magari kuwa machache sana!

Nasikia pia huko Mbagala hali ni tete kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha.

Emb tujuzane na kwa wale ambao mnaweza kuweka picha pia itasaidia.

Badala ya askari kuokoa raia Tz raia wanaokoa askari
 
Attachments

  • 1431002969012.jpg
    1431002969012.jpg
    15.1 KB · Views: 806
Kufuatia hali kuzidi kuwa tete; Suleiman Kova kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam amewataka wananchi wa mkoa huo kurejea majumbani kwao mapema iwezekanavyo! Barabara nyingi hazipitiki huku mvua kubwa ikiendelea kunyesha!

Kuna wengine majumbani kwao kulivyopata madhara ni bora huko waliko, labda waende kwa ndugu zao
 
Wakuu heshima kwenu;

Wakazi wa jiji la Dar es Salaam wamejikuta tena kwenye sintofahamu kubwa kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha tangia jana.

Maeneo mengi hali ni mbaya kutokana na mvua kunyesha kwa wastani wa saa 14 mfululizo!

Nimetokea maeneo ya Tegeta hali ni mbaya. Nyumba zimejaa maji. Maeneo ya Mbezi kutokea Goba kuna magari yametelekezwa njiani kutokana na maji mengi. Kuna gari dogo ya Toyota (jamii ya saloon kama sikosei) Imetelekezwa hapa Mbezi tangi bovu na imefunikwa na maji yanayotokea huku ukanda wa juu! Pia nyumba nyingi maeneo haya ya Mbezi beach zimezingirwa na maji na zimetelekezwa!

Nimepita Sinza hali ni mbaya sana. Maji yapo kila kona, njia hazipitiki!

Stendi ya Makumbusho asubuhi ya leo ilikuwa na daladala chache sana.

Barabara nyingi zinaongozwa na mataa badala ya askari wa trafic. Mfano mataa ya Chang'ombe kitu ambacho ni nadra sana na ni kutokana na magari kuwa machache sana!

Nasikia pia huko Mbagala hali ni tete kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha.

Emb tujuzane na kwa wale ambao mnaweza kuweka picha pia itasaidia.

Hii ndiyo bongo. Askari anaokolewa badala ya yeye kuokoa.
 
Attachments

  • 1431003129363.jpg
    1431003129363.jpg
    7.5 KB · Views: 2,056
Kiukweli ni balaa!, njia ya Goba Rd kutokea Massana, imekatika, hivyo magari yanapita mtaani kwangu kuzungukia.

Home kwangu maji yamefurika na kufumua ufuniko wa cesspit! maji ya mvua ndia yamejaza cesspit na kureplace contents kutitirishia barabarani!, kiukweli leo ni majanga!.

Ukuta wa Makongo sekondari, umeanguka!. Pale Tangi Bovu, kuna daladala ilitanua kumbe barabara pembeni imelowa, ikaporomoka dala dala hilo limelala mtaroni!. Pale Lugalo kumetokea landslide, pande la udogo limemegeka na kudondokea barabarani!.

Kiukweli leo... sijui!.

Pasco

Pole mkuu, mchungaji katukumbusha kuwa biblia inaelekeza ya kwamba tumshukuru mungu kwa kila jambo.
 
Mbona hadi posta hua mfuriko yanafika kwa hiyo napo wahame
Madhara ya Posta ni madogo ukilinganisha na madhara ya watu wanaoishi mabondeni! Wewe umeshawahi kusikia kwamba Posta kuna watu wamekufa kwa mafuriko? Wanaokufa ni wale wale waliojipeleka wenyewe kwenye mikondo ya maji! Lakini kwa upande mwingine, upumbavu wa serikali usiwafanye watu nao wawe wapumbavu! Kati kati ya jiji kutokuwa na miundombinu isiwe sababu ya kufumbia macho upumbavu unaofanywa na watu wa mabondeni kwa makusudi!
 
Leo wakichepuka wakirudi kesho yake anakuta nyumba imejaa maaji au imesombwa na maji ni bora kurudi home mapema

Leo mzee akichepuka usiwe na papara, mpigie cm saa8 usiku Mwambie mtoto amesombwa na mafuriko, utaona anavokuja mbio huku akiwa amekosea amevaa chupi ya mchepuko, tena ameigeuza nje ndani😉
 
Atukatai sisi ni maskini na pengine budget yetu bado finyu lakini this is too much. Kwenye dunia ambayo miji inashindana kuvutia wageni na biashara this explains the lack of creativity on the government part.

Aiwezekani kila mwaka mji mkubwa mvua zikinyesha tuishie na mafuriko ina maana kila mwaka nothing is learned, planned nor thought to be done to tackle the problem, huu sio sasa sio umaskini au kukosekana kwa funds ni uzembe tu kutoka serikarini.

Si kwamba jiji linapata sifa mbaya I am thinking a lot of people loose their valuable possession huko kwenye majumba yao, wafanya biashara wadogo wadogo wanapoteza bidhaa zao, wageni wanaoishi Tanzania watakuwa wanashangaa ata kwa standards za afrika this is below par.

Na haya mambo kila mwaka au msimu wa mvua unapokuja sums uzembe na priority za serikari.

To ridicule us the world has selected our president as the head of dealing with global epidemics. This person is expected to be advised by our national health professions same people who cant to tell him floods are associated with several outbreaks of diseases in communities; you wonder if there are prevention policies in our nation let alone being able to advice the world on epidemics. Only in Tanzania
 
Leo mzee akichepuka usiwe na papara, mpigie cm saa8 usiku Mwambie mtoto amesombwa na mafuriko, utaona anavokuja mbio huku akiwa amekosea amevaa chupi ya mchepuko, tena ameigeuza nje ndani😉

Hhhhhaaaaaaaaaa
 
Mkuu kujiua ni kosa kisheria, na kama utakamatwa ukawa katika harakati za kujiondoa uhai sheria hiyo itakubana, je kwanini hao wanao jenga kingoni mwa mito sheria hiyo isitumike dhidi yao?
Kwahiyo sheria huwezi kuwapata na hatia unless izungumze vinginevyo! Mtu anaweza kukuambia hata kuogelea nako kunahatarisha maisha ya mtu; je itumike hiyo sheria kuwapeleka mahakamani watu wanaoogelea? Wajibu wa serikali ni kutoa tahadhali na pale inapobidi kutumia hata nguvu lakini wananchi wenyewe nao wanatakiwa kuwa responsible na maisha yao badala ya kuwasikiliza wanasiasa! Wanasiasa walivyo wapumbavu usishangae kukuta kuna wengine wanaenda pale na kuwaambia msitoke hadi serikali iwaoneshe mahali pengine pa kujenga utafikiri hapo walioneshwa na serikali huku wakisahau kwamba yakija mafuriko wanaoumia ni wao!
 
Serikali ipo kwaajili ya ninii???
Kama tayari umeshaambiwa huo mto usivuke una mamba na viboko wakali halafu unang'ang'ani kuvuka kwa sababu unadhani serikali ina wajibu na maisha yako then utakufa peke yako na utaacha watu wanaendelea kuponda maisha! Guys, ujinga ama upumbavu wa serikali kutotimiza wajibu wake isiwe ndo sababu ya sisi pia kuwa wapumbavu na kuamua kujenga hata mikondo ya maji ili hata watu wakisema tuje baadae tuseme "kwani kule Posta kuna mkondo wa maji!" Siku vikitokea vifo mia kadhaa Dar es salaam kutokana na mafuriko wala majority ya vifo hivyo havitakuwa city center ambako sio mabondeni lakini hakuna miundo mbinu bali vifo hivyo vitatokea mabondeni kama ambavyo imekuwa ikitokea miaka nenda rudi!
 
Back
Top Bottom