Mafuriko makubwa yaikumba Dar es Salaam

Mafuriko makubwa yaikumba Dar es Salaam

Tuko page moja Mkuu kamwe siwezi kuitetea hii Serikali dhalimu ambayo ndiyo chanzo kikubwa cha matatizo mbali mbali nchini kwetu.

Niwie radhi kwa swali hili, naamini umeoa. Kwa mfano wako hapo juu ukigombana na mkeo, au kukiwa na matatizo katika ndoa yenu, Serikali pia ni chanzo?
 
Madhara ya Posta ni madogo ukilinganisha na madhara ya watu wanaoishi mabondeni! Wewe umeshawahi kusikia kwamba Posta kuna watu wamekufa kwa mafuriko? Wanaokufa ni wale wale waliojipeleka wenyewe kwenye mikondo ya maji! :sad::yield::A S 114:Lakini kwa upande mwingine, upumbavu wa serikali usiwafanye watu nao wawe wapumbavu! Kati kati ya jiji kutokuwa na miundombinu isiwe sababu ya kufumbia macho upumbavu unaofanywa na watu wa mabondeni kwa makusudi!

Well said, pamoja na serikali kuwa na kila kitu, lakini imeshindwa kuwawekea mipango mizuri tangu enzi za Makamba nyimbo zilezile no changes, wanashindwa nini kuyaweka maeneo hatarishi kama hayo ya msimbazi mikononi mwa JWTZ?
 
huyu angetafutwa apewe adhabu.
attachment.php
 
Isemeni hii ishu kwa ukubwa wake.... madhara si mpaka afe mtu... Wa mabondeni wamekufa .. wa posta uchumi umeathirika... tena ukizingatia foleni inakuwa kubwa kuliko kawaida..
Mimi concern yangu kubwa ni watu wa mabondenikwa sababu madhara ya Posta nitayaacha kwa serikali na upumbavu wake na nitayaacha kwa serikali coz' they don't care. Few years ago nilikuwa nafanya ofisi moja na dada mmoja hivi! Pale ofisini mie nilikuwa new comer; sasa kuna siku tumekaa hivi, mara yule sista akatoka bonge la nduki; watu wakaanza kumcheka! Sikuelewa what's was going on! Mara ya pili tena, ikaanza kushuka mvua from nowhere! Yule dada kama ilivyokuwa awali, akatoka tena nduki! Aliporudi nikakosa uvumilivu nikamuuliza kulikoni huwa anatoka nduki na kupotelea kusikojulikana!? Hapo ndipo akaniambia anaishia Kigogo mabondeni; ndipo nikaja kufunguka macho! Yaani alikuwa anaishi kwa mashaka ile mbaya! Sasa mimi nawazungumzia hawa watu ambao mara nyingi wanatumika kisiasa! Nakumbuka few years ago Zungu alishawahi kuwaambia watu wa Jangwani wasihame hadi serikali iwaoneshe kwa kwenda! That's was stupid manake wanaoumia ni wenyewe wakati hiyo serikali mnayoisimanga wala hawana wasiwasi! Jangwani kila msmimu wa mvua watu wanakufa; fine tuendelee kusema ni uzembe kama sio upumbavu wa serikali! Will it change anything? Na ndio maana nikauliza, there's no doubt kwamba serikali ni wapumbavu; je ina maana na sisi tuwe wapumbavu vile vile wakati tunafahamu fika upumbavu wao watendaji wa serikali wala hauwaathiri wao wenyewe moja kwa moja wakati upumbavu wetu unatuathiri sisi wenyewe moja kwa moja!
 
Unasemaje kuhusu wale watu nyumba zao zipo kwenye kingo za mto ambapo mvua kidogo tu inafika kwenye majumba yao? wale watu wasiilaumu serikali wajilaumu wenyewe.
Wana sehemu kubwa sana ya kulaumiwa kwa kusababisha mafuriko na kuzuia maji kuwa na flow yake....Lakini serikali nayo ina lawama nyingi tu, inaona mtu kajenga eneo lisilopimwa, lipo ukingoni mwa mto lakini utaona huduma za maji na umeme zinawafikia, ina maana gani, kuwa serikali imebariki wao kujenga na kuishi sehemu hatarishi.
 
Jumla ya chanzo cha matatizo yote haya ni ombwe la uongozi, viongozi wasio na maono yaani uwezo wa kuona mbali, viongozi wasio na ubunifu, wasio na uwezo wa kujifunza kutokana na yaliyopita, wasio na fikra na mbinu mpya, wasiotoa kipaumbele kwa taaluma, wasio na uchungu na wananchi, wanaowaza tu juu ya matumbo yao, wanaotembea dunia nzima lakini hawajifunzi kutokana na yale wanayoyaona huko, ....... Uongozi wa CCM unaongoza tu kwa mazoea na desturi, haujui hata lipi jipya la kufanya, umefika mwisho...... CCM ipumzishwe tu!
 
Mungu tuepushe na madhara ya miili, nafsi na roho zetu!.


Lawama zote ziiendee Ccm na serikali yake kwa kushindwa kuwa proactive wala reactive. Serikali ina wataalam wa miundombinu wengi ambao wamesoma vizuri wakahitimu (achana na wale wakupasishwa wa sasa), wameajiriwa na wanalipwa mishahara - kodi zetu kwa kazi hiyo.

Ni nini kinaifanya serikali ishindwe kuwatumia katika kuhakikisha miundo mbinu yetu iko vizuri ili kuepusha fedheha hii ya kurudia rudia kwa majanga ambayo yamepoteza uahi wa ndugu zetu, mali, na kuleta magonjwa ya milipuko yanayotugharimu fedha nyingi za kigeni na kudidimiza uchumi wetu? Ninaamini wataalam wana majibu sahihi ya kuboresha na kuimarisha miundo mibnu ili watanzania tuishi kwa amani na tuone mvua ni baraka na si laana ila serikali haitaki kuwatumia ama kwa kutokujali shida za wananchi ama kwa kutokujua thamani na maana halisiya utaalamu.

Ujenzi holela ambao ndio chimbuko kubwa linasopelekea athari za mvua kuwa mbaya na kwa kiwango kikubwa, unalelewa na serikali kutokuzingatia na kumaanisha kufanya kazi kwa ufanisi na kwa malengo ya kuboresha ustawi wa taifa.

Tuna mipango miji, upimaji na ramani wanalipwa mishahara kila mwezi january to december, na hadi marehemu wako kwenye payrolls za serikali. Lakini hawa watu, wanakuwa desk officers ama private dealers!.
Kuna ugumu gani wa kusurvey viwanja na maeneo kwa wingi ili anayehitaji kujenga aonyeshwe eneo lake kama vile route za magari ya abilia?
Ajabu hawa wataalam, kazi yao ni kwenda kupima maeneo kwa maombi ya watu binafsi baada ya ujenzi holela bila considerations za mahitaji muhimu ya general public, wanalipwa fedha sawa na private surveyors, kitu kinachokithirisha ukosefu wa miundo mbinu sahihi na mwisho ni kama tunavyoona.

Ni jambo lisilofikirika kwamba watu wanajenga mchana, serikali inaona haichukui hatua yoyote, badala yake inakwenda kuweka namba kwenye zile nyumba holela, inachukua kodi, wakati huo huo, umeme wanawekewa, na maji ya serikali wanapelekewa, bills wanalilpa kwa serikali kila mwezi, na soko wanajengewa, local Governments wanachukua levy, kodi wengine wanalipa na baraka zote za serikali kama vile hakuna kosa lolote lipo. Ni jambo la ajabu mvua zinaanza kunyesha, mafuriko yanaanza, serikali inawageuka eti wahame wamejenga mabondeni, mara wamejenga bila mifereji, mara eneo walilojenga si la makazi, mara walipo ni mkondo wa mto hivyo wameziba mto na hadhithi nyingi kibao.

SWALI LA KUJIULIZA, NIA THABITI YA SERIKALI KULINDA NA KUSIMAMIA MASLAHI NA USTAWI WA UMMA IKO WAPI?
KWA UZEMBE HUU, BILA KUBADILISHA UTAWALA, TANZANIA ITAKUWA BADO IPO KWA MIAKA MICHACHE IJAYO?
TAFAKARI!.
 
Kwa miji mikubwa ya Tanzania panatakiwa kuwa na mamlaka ya uendelezaji miji,ukitaka kujenga lazima uwe na kibali cha ujenzi,hata kama unajenga choo. Mamlaka ijilidhishe kama panapojengwa je panastahili?
 
Acheni kulalamika.
Huku kwetu Zanzibar mvua zimesababisha mafuriko na watu wamekufa kabisa
Na taarifa ya hali ya hewa kwa Zanzibar ni kwamba kiwango cha mvuo kimevunja record ya miaka ya 80s.
Hembu mkiwa mnaenda kwenye nyumba za ibada msiwe mnawaza mkitoka muishie Bar.Ila mnatakiwa ujumbe ukae kichwani.
Gharka kama hizi au majanga ya kidunia haya kwepeki,na hadi kwenye Biblia na Qur`aan yameandikwa.Na ndio maana hayachagui nchi,hadi Marekani wamekiona cha moto itakuwa sie.
Cha msingi ni kuwa na utayari wa kukabiliana nayo na kusaidiana.Sasa janga kama hili unailaumu serikali si wendawazim huu?
Mungu alishusha dharuba zaidi ya hizi na wakati huo Manabii/Mitume wake wapo,Sasa kati ya Serikali na Mitume nani mwenye uwezi wa kuomba kwa mungu moja kwa moja na akajibiwa hapo hapi.Ila Mungu ana hekma zake kwa kila janga.
Ujumbe ni kwamba Mungu anataka tusaidiane kwenye maafa,hapa watu wanalalamika,hata mtu kwenda kupeleka hata Elfu moja au suruali moja kwa muathirika hakuna.Kazi zogo tu.

Hakuna sehem yenye Upinzani wa vyama kama Zanzibar,lakini kwa hili watu wote wamekuwa wamoja.Na viongozi wote wameenda kuwapa pole wahanga na wafiwa,na misaada mbali mbali imetolewa na inaendelea kutolewa na pande zote.
Na husikii hata Kiongozi mmoja akilalamikia serikali.
Mkiendekeza sana Siasa ndani yake ina ushetani,na Mungu alisema kwamba kuna vitu vitakuja na vitakuwa upande mmoja salam na upande mmoja sio salama.Ndio hayo sasa
 

Hoja ni kuwa serikali inafanya uzembe kwenye jambo hili... Mafuriko si mara ya kwanza kutokea... Na kila yanapotokea akina nyie maneno yenu ndo haya.... Hii ishu uzembe upo hapa...
1. Mipango miji.... Hii inapelekea kila muda fulani foleni zipo direction moja eg. asubuhi wote kwenda city centre, jioni tunajipanga kurudi majumbani.... Huduma zote muhimu zimejazwa sehemu moja
2. Mitaro almost yote haina 'slop'... Mtaro hauna tofauti na septic tanks... Maana almost kila mtaro maji yanatuama...
3. Mabarabara mengine maji yanatuama.... mfano Akiba, posta mpya, milenium tower, bamaga... etc
4. Watoa vibali vya ujenzi wanaruhusu watu kujenga kwenye njia za maji bila kutoa altenative route ya maji. Kumbuka maji hayazuiliwi bali yanabadilishiwa uelekeo... Mfano wa hili ni apartment nyuma ya Mayfair plaza... Zile zimejengwa kwenye njia ya maji na hawajayapa hayo maji njia mbadala
5. Huduma za kijamii kubwa kubwa zote zipo concentrated city centre.... check soko la kariakoo, mahospitali almost yote, maofisi ya serikali almost yote (wizara, mamlaka etc), mabenki huku pembeni vi-ATM tu....
6. Kambi za majeshi zipo mjini.... JKT, JWT, etc...

Na uzembe mkubwa sana upo hapa...

Kwa TAnzania, siku zote wananchi wanaanza kuishi eneo fulani na baadaye huduma zinafuata....

Nchi zingine, serikali inaingia sehemu kama Goba inapima viwanja inatengeneza njia inapele utilities zote (maji, umeme etc) halafu wananchi mtavuntika tu kwenda...

In Tanzania, hakuna communications kati ya wizara mbalimbali za serikali... Leo hii ujenzi wanamaliza tu kujenga lami, kesho wizara ya maji inabomoa kupitisha bomba...

NB: Usipoelewa hapa, we basii tenaa

CC

Dinazarde

  1. Foleni za magari zinasababishaje mafuriko? Kuna uhusiano gani kati ya mvua kunyesha kwa wingi kiasi cha kusababisha mafuriko na uwepo wa foleni za magari?
  2. Slop ya mitaro haipimwi kwa macho, inapimwa kwa darubini. Macho yako yanaweza kukuonyesha kama mitaro haina slop ila slop ipo. Tatizo ni uchafu wa wakazi wa eneo husika ambao wanataka kila kitu wafanyiwe na serikali, ndio maana wanadiriki hata kutiririsha maji ya chooni mitaani pindi mvua zikinyesha.
  3. Kutuama kwa maji barabarani sehemu kubwa ni matatizo ya mitaro kujaa uchafu unaowekwa na wananchi wenye mawazo ya kwamba usafi wa mji ni jukumu la serikali peke yake.
  4. Badala ya kuilaumu serikali, naona wapuuzi ni wale wanaokwenda kujenga kwenye njia za maji kwa kigezo kwamba wana vibali huku wanasahau kuwa maji hayaangalii mwenye kibali au asiye na kibali.
  5. Hili linachangiaje mafuriko?
  6. Mfano kambi ipi ya jeshi iliyopo mjini?
 
Majangaa
 

Attachments

  • 1431011746614.jpg
    1431011746614.jpg
    13.4 KB · Views: 569
  • 1431011771926.jpg
    1431011771926.jpg
    56.6 KB · Views: 542
  • 1431011793551.jpg
    1431011793551.jpg
    9.1 KB · Views: 534
  • 1431011810580.jpg
    1431011810580.jpg
    11.4 KB · Views: 534
  • 1431011846570.jpg
    1431011846570.jpg
    10.7 KB · Views: 531
Back
Top Bottom