matumbo
JF-Expert Member
- Jul 9, 2011
- 7,224
- 3,960
Kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha usiku kucha nimepita baadhi ya mitaa alfajiri hii na kukuta wananchi wakikimbia nyumba zao sababu ya kujaa maji ndani. Inatia huruma kwa kweli, awa watu wanahitaji msaada wa haraka kutoka kwa jamii inayowazunguka sababu Serikali imeshashindwa kuwa msaada kwa Wananchi.
Nimepita maeneo ya Tabata, Buguruni, Vingunguti nimekuja kuiona tena hali hiyo Kigogo na sasa nipo magomeni sijajua kwa ndugu zangu pale Kinondoni kutakuwaje.
=====================
Update
===========================
Update
Nimepita maeneo ya Tabata, Buguruni, Vingunguti nimekuja kuiona tena hali hiyo Kigogo na sasa nipo magomeni sijajua kwa ndugu zangu pale Kinondoni kutakuwaje.
=====================
Update
Watu 8 wamefariki dunia kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha nchini ambapo mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadick, amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo,kinondoni wamefariki watu 6 na Temeke watu wawili.
MAFURIKO DAR - BARABARA YA MOROGORO YAFUNGWA
Kufuatia mvua inayoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam na kusababisha mafuriko ambayo yamepelekea barabara kadhaa kufunikwa na maji; Serikali imetangaza kuifunga Barabara ya Morogoro katika eneo la Jangwani kufuatia daraja kufunikwa na maji.
Aidha, watu wametakiwa kuondoka mapema maeneo ya katikati ya ambako kuna foleni ndefu za magari na kwa mujibu wa utabiri wa hali ya hewa, mvua hizi zitaendelea kunyesha na ambapo madhara yanaweza kuwa makubwa zaidi.
Hadi wakazi wengi wa maeneo ya mabondeni wameripotiwa kuathiriwa na hali hii kwa nyumba zao kujaa maji na mali zao kusombwa na maji.
===========================
Update
Mtu mmoja amefariki Dunia baada ya kusombwa na Maji kutokana na mafuriko yaliyotokana na Mvua zinazoendelea Kunyesha Dar es salaam.
Attachments
Last edited by a moderator: