Mafuriko makubwa yaikumba Dar es Salaam

Mafuriko makubwa yaikumba Dar es Salaam

Poleni wakazi wa dar kuna dugu zangu pia huko

Hapa mwanza hali ni shwari sana
 
Kiswahili kweli kigumu hivi nyumba inatelekezwa vipi.
 
Wakuu heshima kwenu;

Wakazi wa jiji la Dar es Salaam wamejikuta tena kwenye sintofahamu kubwa kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha tangia jana.

Maeneo mengi hali ni mbaya kutokana na mvua kunyesha kwa wastani wa saa 14 mfululizo!

Nimetokea maeneo ya Tegeta hali ni mbaya. Nyumba zimejaa maji. Maeneo ya Mbezi kutokea Goba kuna magari yametelekezwa njiani kutokana na maji mengi. Kuna gari dogo ya Toyota (jamii ya saloon kama sikosei) Imetelekezwa hapa Mbezi tangi bovu na imefunikwa na maji yanayotokea huku ukanda wa juu! Pia nyumba nyingi maeneo haya ya Mbezi beach zimezingirwa na maji na zimetelekezwa!

Nimepita Sinza hali ni mbaya sana. Maji yapo kila kona, njia hazipitiki!

Stendi ya Makumbusho asubuhi ya leo ilikuwa na daladala chache sana.

Barabara nyingi zinaongozwa na mataa badala ya askari wa trafic. Mfano mataa ya Chang'ombe kitu ambacho ni nadra sana na ni kutokana na magari kuwa machache sana!

Nasikia pia huko Mbagala hali ni tete kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha.

Emb tujuzane na kwa wale ambao mnaweza kuweka picha pia itasaidia.

Katuangalizie Na Nyumba Yetu Kubwa Watanzania Ya Magogoni Pia Je Hakujafurika Napo? Otherwise Tunashukuru Kwa Taarifa Yako Japo Umesema Mbezi Beach Hali Ni Tete ILA Mbezi Beach Nilipo Mimi Hali Si Kama Hiyo Uliyoisema Japo Ni Kweli Kuna Mvua Kubwa Tu Inanyesha.
 
Hivi wewe kama c yingo ni nini?au umbea?yani mitaa yote umepita wewe tena subuhi hii na foleni hizi...tegeta ushapita,mbezi beach umepita...goba umepita...sinza,makumbusho umepita yote hii asubuhi...hadi chang'ombe??sasa embu nikuulize wewe mwandishi wa habari au??au mitaa yote hiyo ni junction ya kueleka ofisini kwako.
Nimalizie kwa kutoa pole kwa wakazi wote wa dar walioathirika na hizi mvua za kuanzia jana.
 
Hakuna ugumu wa Kiswahili, sema tu wewe haujaelewa.Kutelekezwa nyumba ni kitendo cha watumiaji wa hiyo nyumba kuikimbia na kuiacha bila uangalizi.
 
Katuangalizie Na Nyumba Yetu Kubwa Watanzania Ya Magogoni Pia Je Hakujafurika Napo? Otherwise Tunashukuru Kwa Taarifa Yako Japo Umesema Mbezi Beach Hali Ni Tete ILA Mbezi Beach Nilipo Mimi Hali Si Kama Hiyo Uliyoisema Japo Ni Kweli Kuna Mvua Kubwa Tu Inanyesha.

Mkuu, syo lazima liwe ni eneo ulilopo ila ukweli ni kuwa maeneo mengi yamezingirwa na maji! Labda bado hujatoka ukajionea hali halisi!
 
Ngoja Nichungulie Dirishani Na Nitakujuza Mkuu.
 
Sehemu sinza napo ni balaa,tandale kwa tumbo napo hakufai
 
Wakuu heshima kwenu;

Wakazi wa jiji la Dar es Salaam wamejikuta tena kwenye sintofahamu kubwa kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha tangia jana.

Maeneo mengi hali ni mbaya kutokana na mvua kunyesha kwa wastani wa saa 14 mfululizo!

Nimetokea maeneo ya Tegeta hali ni mbaya. Nyumba zimejaa maji. Maeneo ya Mbezi kutokea Goba kuna magari yametelekezwa njiani kutokana na maji mengi. Kuna gari dogo ya Toyota (jamii ya saloon kama sikosei) Imetelekezwa hapa Mbezi tangi bovu na imefunikwa na maji yanayotokea huku ukanda wa juu! Pia nyumba nyingi maeneo haya ya Mbezi beach zimezingirwa na maji na zimetelekezwa!

Nimepita Sinza hali ni mbaya sana. Maji yapo kila kona, njia hazipitiki!

Stendi ya Makumbusho asubuhi ya leo ilikuwa na daladala chache sana.

Barabara nyingi zinaongozwa na mataa badala ya askari wa trafic. Mfano mataa ya Chang'ombe kitu ambacho ni nadra sana na ni kutokana na magari kuwa machache sana!

Nasikia pia huko Mbagala hali ni tete kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha.

Emb tujuzane na kwa wale ambao mnaweza kuweka picha pia itasaidia.

Asikudanganye mtu!! hii mvua ina mkono wa CHADEMA! mgomo wa madereva umewashinda sasa wameingia kwenye mvua ilimradi tu watu wasiende makazini!! hivi hawa jamaa tukiwakabidhi nchi hali itakuwaje!?? nchi nzima si itafunikwa na theluji!! hahahahahahahahaaaa.... LOL..
 
Hivi wewe kama c yingo ni nini?au umbea?yani mitaa yote umepita wewe tena subuhi hii na foleni hizi...tegeta ushapita,mbezi beach umepita...goba umepita...sinza,makumbusho umepita yote hii asubuhi...hadi chang'ombe??sasa embu nikuulize wewe mwandishi wa habari au??au mitaa yote hiyo ni junction ya kueleka ofisini kwako.
Nimalizie kwa kutoa pole kwa wakazi wote wa dar walioathirika na hizi mvua za kuanzia jana.

Aiseee!!! Jf umekuja kufanya nini?
 
wakuu hii ni noma nipo mitaa ya bamaga barabara ya sinza..maji si mchezo
 
Mafuriko kila msimu wa mvua yanatokea lakini serikali ipo tu inashangaa shangaa tu.
 
Acheni kulalamikia kila kitu, wakiondolewa ni nyie wananchi mnasema wameonewa, serikali ya ccm ni waonevu sana, wanatumia mabavu, wakiambiwa waondoke kwa hiyari hawataki, sasa ccm ifanyeje???? wacha cha moto kiwapate ndio akili ziwakae sawa.

Laiti ungefikiria kidogo tu ungejua serikali yako inahusika vipi na mipango miji. Lazima kuwe na master plan ya mji, lazima kabla hujaamza kujenga uwe na ramani na approval ya wizara, lazima kabla ya kujenga eneo lako lipimwe na kuonekana linafaa na kukidhi ujenzi, lazima wizara ijidhihirishe kuwa drainage system pale unapokenga inakubaliana na system ya mji, lazima sewage system ya nyumba yako iendane na sewage system ya jiji.
Unaposema sisiem isilaimiwe sijui unaangalia vigezo gani.
 
Back
Top Bottom