Mafuriko makubwa yaikumba Dar es Salaam

Mafuriko makubwa yaikumba Dar es Salaam

Ifike wakati watu waende nje ya mji, kwani lazima kuonekana unakaa mjini ili hali unaishi kwenye bwawa la maji ya chooni???????? nyumba nyingine ni kinyaa lakini mtu anang'ang'ania hapo hapo kisa yupo karibu na kariakoo ni ujinga huo sasa. hapo serikali ya ccm haihusiki.
 
Tatizo waTz wabishi maana hii sio mara ya kwanza wala haitakuwa ya mwisho. Mi nawapa pole tu.
 
Nimepita hapa ubungo darajani karibu MTO umejaa maji
 
Ni kweli serikali haileti mvua inasingiziwa kwa hilo, ila yenyewe ndio msimamizi wa wananchi na maeneo, ifike mahali ikisema jambo ilitekeleze, imezembea upande wa idara ya mipango mji, sio dar pekee hata mikoani pia kuna uzembe na kutowajibika, Tangu miaka ya 80 walikuwa wanaangalia tu mfumuko wa makazi holela, hamna miundo mbinu sahihi ambayo ingesaidia nyakati kama hizi. Bado haijachelewa sana kurekebisha ili kulitatua tatizo in long term, suala tu ni kujipanga na kutanguliza utaalamu kwanza siasa baadae sana.
 
Mvua imenyesha usiku kucha. Sipati picha huko mjini kunafananaje
 
Jamani tupeane updates za mvua kila mtu kutoka eneo alipo,mimi namalizia chai soon ntawapasha hali ikoje.

Nimepita jangwani nyumba zimefunikwa na maji......... baadhi ya wakazi wanahamisha

mizigo yao na kuondoka hayo maeneo
 
Hali ya taharuki imetoka baada ya daraja lililokuwa linaunganisha watu wa kutoka mongolandege na mombasa (ukonga) kusombwa na maji; bodaboda hazipiti, watu hawawezi kuvuka maji ni mengi watu wanaishia kutazamana walioko pande 2 tofauti
 
Poleni sana wananchi wa huko. Serikali sikivu ya CCM itafanya jambo punde

Mzee Tupatupa
 
Poleni, nilijua kutakuwa na madhara makubwa! ngoja tusubiri updates zaidi
 
Tanzania ni sehemu pekee duniani mafuriko yanatokea makubwa,ukienda bombani hamna maji yanatoka hata kuosha miguu.

Tuendeleeni kuchagua watu wasiojali. Haya mambo ni aibu na yameshapitwa na wakti. Lakni utakuta mijitu waliotufikisha hapa wanarudi ofisini
 
Tatizo kujenga ovyo bila mpangilio, kujenga mabondeni na ukosefu wa miundo mbinu ya kutolea maji wakati wa mvua,,,
tatizo hii nchi imelaaniwa siku nyingi! Tangu tumepata uhuru hakuna mipango miji endelevu iliyofanyika! Tuna wizara ya ardhi ila haijui majukumu tangu kuanzishwa kwake! Watu wanapiga deal tu hapo! Alipoingia mama wa escrow nilijua nyumba imepata mpangaji! Kumbe alikuwa anatafuta hela za mboga tu! Poor my country tanzania, hata tunavyoona watu wanajenga hakuna provision ya barabara hii yote ni majukumu ya wizara ya ardhi! But they have no idea! Ndio sasa naona tulidai uhuru kabla ya muda kufikia! Au akili zetu zimedumaa
 
Hakuna anaependa kujenga bondeni ni maisha tu, mtu hela ya kujenga pazuri hana na kachoka kupanga.
Hapana mkuu si kweli unachosema,ujenzi wa bondeni gharama yake ni kubwa sana! Na ujenzi wa bondeni haukomi ni kila wakati wa mvua. Watanzania wengi wanafanya vitu bila kufanya hesabu.
 
Ifike wakati watu waende nje ya mji, kwani lazima kuonekana unakaa mjini ili hali unaishi kwenye bwawa la maji ya chooni???????? nyumba nyingine ni kinyaa lakini mtu anang'ang'ania hapo hapo kisa yupo karibu na kariakoo ni ujinga huo sasa. hapo serikali ya ccm haihusiki.

serikali ya ccm ndio imeleta uzembe kwa kushindwa kusimamia sheria maana wao ndio wanadhamana ya kuongoza kwa sasa,ccm na serikali yake imeshindwa kupanga matomizi bora ya ardhi ndio matokeo yake haya
 
serikali ya ccm ndio imeleta uzembe kwa kushindwa kusimamia sheria maana wao ndio wanadhamana ya kuongoza kwa sasa,ccm na serikali yake imeshindwa kupanga matomizi bora ya ardhi ndio matokeo yake haya

Acheni kulalamikia kila kitu, wakiondolewa ni nyie wananchi mnasema wameonewa, serikali ya ccm ni waonevu sana, wanatumia mabavu, wakiambiwa waondoke kwa hiyari hawataki, sasa ccm ifanyeje???? wacha cha moto kiwapate ndio akili ziwakae sawa.
 
Wakuu heshima kwenu;

Wakazi wa jiji la Dar es Salaam wamejikuta tena kwenye sintofahamu kubwa kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha tangia jana.

Maeneo mengi hali ni mbaya kutokana na mvua kunyesha kwa wastani wa saa 14 mfululizo!

Nimetokea maeneo ya Tegeta hali ni mbaya. Nyumba zimejaa maji. Maeneo ya Mbezi kutokea Goba kuna magari yametelekezwa njiani kutokana na maji mengi. Kuna gari dogo ya Toyota (jamii ya saloon kama sikosei) Imetelekezwa hapa Mbezi tangi bovu na imefunikwa na maji yanayotokea huku ukanda wa juu! Pia nyumba nyingi maeneo haya ya Mbezi beach zimezingirwa na maji na zimetelekezwa!

Nimepita Sinza hali ni mbaya sana. Maji yapo kila kona, njia hazipitiki!

Stendi ya Makumbusho asubuhi ya leo ilikuwa na daladala chache sana.

Barabara nyingi zinaongozwa na mataa badala ya askari wa trafic. Mfano mataa ya Chang'ombe kitu ambacho ni nadra sana na ni kutokana na magari kuwa machache sana!

Nasikia pia huko Mbagala hali ni tete kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha.

Emb tujuzane na kwa wale ambao mnaweza kuweka picha pia itasaidia.
 
Kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha usiku kucha nimepita baadhi ya mitaa alfajiri hii na kukuta wananchi wakikimbia nyumba zao sababu ya kujaa maji ndani. Inatia huruma kwa kweli, awa watu wanahitaji msaada wa haraka kutoka kwa jamii inayowazunguka sababu serikali imeshashindwa kuwa msaada kwa wananchi.

Nimepita maeneo ya Tabata, Buguruni, Vingunguti nimekuja kuiona tena hali hiyo Kigogo na sasa nipo magomeni sijajua kwa ndugu zangu pale Kino kutakuwaje.

Hivi wewe ungekuwa ndio kiongozi mkuu wa serikali (rais) ungewasaidiaje? Kwa mwendo huu kuiongoza Tanzania kweli ni pasua kichwa
 
Back
Top Bottom