Mafuriko makubwa yaikumba Dar es Salaam

Mafuriko makubwa yaikumba Dar es Salaam

Siku zote serikali inapiga vita ujebzi wa mabondeni na katika njia za maji, tatizo watu ni wabishi na wajuaji sana. Leo wewe unasema serikali haijishughulishi vya kutosha katika kuhakikisha ujenzi haufanyiki mabondeni, lakini ikitangaza kuwa inaanza kubomoa nyumba zote zilizojengwa mabondeni, mtabadilika tena na kuanza kuhoji hatua inazochukua dhidi ya ujenzi huo wa holela.

Hujanielewa, kijana, ninachosema ni.kuwa kwa nini usubir kuja kubomoa wakat ulikuwa na uwezo wa kuzuia watu wasijenge? Tahadhar kabla ya hatar
 
Mafuriko kila msimu wa mvua yanatokea lakini serikali ipo tu inashangaa shangaa tu.

Sasa wewe unataka ifanye nini na nyie mabondeni hamtaki kuhama endeleeni kukomaa tu mpaka akili itawakaa sawa hakuna atakae wafukuza
 
ccm ndio wa kulaumiwa kamwe hawawezi kujisafisha katika hili. Ujerumani aliwaachia ramani ya jangwani inaonyesha kuwa jangwani pasijengwe kitu chochote ukiondoa hiyo barabara ya moro.rd. Nyie mkajenga babara ya jangwani mmedharau ramani mlioachiwa sasa hiyo barabara imezuia njia ya maji NA KUSABABISHA MAJI MENGI KUJAA . Je kwa nini ccm msilaumiwe?

Mkuu kuwa mkweli inayozuia maji kupita ni barabara au hayo majumba yaliojengwa hapo jangwani?
 
Ok Ok.. Ok...
1. Na yale maji yanayojaa Azikiwe karibu na Holiday inn alaumiwe nani..?? Wanaoishi mabondeni..??
2. Na hayo maji kupita juu ya madaraja alaumiwe nani..?? Wanaoishi mabondeni..??
3. Na hayo mabarabara yanayojengwa mitaro isiyo na "slop" alaumiwe nani..?? Wanaoishi mabondeni..??
4. Na hayo maofisi ya serikali kuyajaza yote city centre alaumiwe nani..??? Wanaoishi mabondeni..??

Mambo mengine tuseme kweli... kama ingekuwa utashi wa watu ufanye kazi basi hamna maana ya kuwa na serikali..

1. Mbona wezi wanawakamata..?? Wezi hawana utashi wa kujuwa kuwa wizi hauruhusiwi..???
2. Mbona waharifu wanakamatwa..??? Utashi hawna..???

SERIKALI NI KILA KITU... IKIWA LEGELEGE HAKUNA JAMBO LITAKWENDA...

Yes walaumiwe watu wa mabondeni, huwezi ziba njia ya maji halafu ukategemea maji yapate pa kwenda. Kama mmabonde yangekuwa matupu basi maji yangekuwa na makwenda, yasingebakia akiba azikiwe au maeneo mengine.

Soma kuhusu "Archimedes principle". Maji hayana cha kudisplace Bondeni kwani kumeshajaa nyumba (volume) hivyo yata-disperse( floods).

Mifumo yetu ya maji taka si mizuri kihivyo. Kitendo cha watu kujenga mabondeni ni sawa na kumkaba mtu mwenye kigugumizi ili aongee fluently.Seriously?
 
Daaah hii dhahama jaman ata kama haupo bondeni kunammomonyoko wa udongo
 
18.jpg
 
Back
Top Bottom