10102ac521314716b0cdeb7f1e57ec04.jpg


Wanajukwaa poleni na misukosuko ya kujibadili kutoka kuwa walaji wa Mwisho kuelekea nchi ya Viwanda.

Uwanja huu ni maalumu kama ule wa Safari za nje za Jakaya kikwete ila huu ni mahususi kukusanya mambo mazuri ya Awamu ya tano chini ya Rais Magufuli juu ya maendeleo yetu hasahasa kauli yake kuu Juu ya Nchi ya Viwanda na Elimu Bure nk.

Unaruhusiwa kugusia miundo mbinu, Afya, Usafiri, Maendeleo ya Majeshi Yetu, Uvuvi,Michezo, Habari, Siasa, Viwanda,Teknolojia, Pato la Taifa nk.
Ila tu iwe kwa tulipotoka na Alipofanikiwa na nini tufanye kumsaidia kujiongeza zaidi.

Mpaka sasa kafanya haya;

Hostel za Chuo cha UDSM.
Hostel za Askari Magereza.
Ununuzi wa Ndege 2 (Nyingine 3 ziko mbioni kuja).
Ujenzi wa Flyover Tazara na Ubungo
Upanuzi wa Airport Mwanza
Upanuzi barabara ya Moroco Dsm
Upanuzi wa Kisasa Airport Dar
Kukomesha Rushwa
Kurejesha nidhamu Makazini.
------------

Na haya ameanza tarehe 12/4/2017;

Uzinduzi ujenzi wa reli kwa ajili ya treni ya Umeme.
Ujenzi wa barabara ya Mtwara-Tandahimba

Kukomesha Watumishi Wenye Feki hivyo kuokoa Mabilioni ya Fedha.

Barabara ya kuunganisha Wilaya za Kibondo kigoma Kaliua huko Tabora.

Miradi Mikubwa ya Maji :

Uwezeshaji Ujenzi Bomba la Mafuta kutoka Hoima mpaka Tanga
Mkuu naomba kukuuliza; kati ya hiyo miradi ulitotaja hakuna miradi ambayo ni on going project?? nikiwa na maana ilianzishwa na mtangulizi wake?? na bajeti ilikuwepo mezani? naomba tu kufahamu hilo
 
Magufuli akitumia akili yake kidogo hapa tulipo tunaenda mbal kiuchumi
 
Hakuna kipindi rushwa imekomaa kama wakati huu, tumewazidi hata Kenya kwa rushwa, kaamua kuendesha nchi kama bar yake mambo anajiamulia tu anayoona yeye, ukweli kufeli kuna kiwango huyu kafeli kwa kiwango cha mwisho,
Muongo wewe huna jipya to a mifano
 
Hostel DSM zinanyufa ni hatarishi kwa maisha.
Ndege zimeshikiliwa na ufisadi umetika kuzinunua.
Flyover imepaaa paaa hakuna fedha izo
Upanuz airport mwanza ufisadi na utoa zabun kimagumashi
Barabara moro co mbwembwe za fedha zetu kumbe wajapan
Uwanja Wa dar lini ulipanuliwa
Kujenda uoga Wa kuogopa makada Wa ccm na watu wasiojulikana. Ujenz Wa reli kimagumashi,
Kaokoa fedha ambazo haujaona zimeenda wapi
Watu wanakunywa maji machafu
Hakuna kitu cha maana bombs LA Mafuta ni mpango Wa kikwete
 
Haya aliyoyafanya na kwa muda aliyoutumia, yule mzee mwenye mvi hata robo asingeweza kuyafanya.

Bombardier used, nyinyi wanafiki ndio mliokuwa mkipiga kelele kwamba nchi yenye watu milioni 50 haina ndege, zinakuja mnaanza kuongea kama walevi wa pombe za kienyeji.

Tatizo lenu la kukaa mbele ya laptop zeni Dar ndio hilo, hamjui wala hamtaki kufungua macho na kuona yanayoendelea nchi nzima. Mkoa wa Mbeya umebakiza vijijini chini ya kumi ambavyo havina umeme.
Hiyo ni project ya mwaka 2007. Lowassa alivyokuwa waziri mkuu alikuja Mbeya pia alitembelea kijiji chetu cha Mababu kwenye mhadhara alisema 'ntahakikisha umeme unafika vijiji vingi vya Mbeya, kikiwamo kijiji chenu' na utekelezaji ulianza 2008 mwanzoni.
Ko hoja ya umeme kwa Mbeya haijakaa sawa.
Kwa upande wangu, Magufuli huwa anaanza vizuri kwa kila kitu lakini pia anamaliza vibaya sana kwa kila kitu. Mfano ni Flowmeter pale bandarin, hostel chini ya kiwango za udsm, mchakato wa vyeti feki wenye upendeleo, kutuaminisha hela za standard gauge n hela za ndani kumbe mkopo na currently umepigaji kwenye sakata la e-migration.
Ko shida yake ni kushindwa kumaliza vizuri mipango yake na hii inatokana na tabia yake ya 'I know all' ambayo inapelekea kutosikiliza ushauri wa kitaalamu kwa watu mahususi (mfano makinikia watu walitoa ushauri wa kisheria, lilikuwa jambk jema kwa taifa ila kwa upande wangu sijui limekomea wapi maana lilianza hadharani na kuelekea sirini)
Kwa mipango hake angekuwa mshirikishaji (demokrasia) ni mizuri na ingetufikisha mbali.
 
Baadhi ya miradi ambayo mtangulizi hajaianzisha.
1. Uwanja wa michezo dodoma (kazi imeanza).

2. Ukarabati wa viwanja 11 katika mikoa 11.

3. Ujenzi wa uwanja mkubwa wa ndege dodoma .

4. Ujenzi wa ofisi za Nec, twakwimu, makamu wa rais, etc makao makuu dodoma

5. Ujenzi wa barabara ya njia 6 kutoka dar hadi kibaha.

6. Ujenzi wa barabara ya arusha kuanganisha kenya.

7. Ukarabati wa shule kongwe

8. Ukarabati wa vyuo vya ualimu vikongwe.

9. Ujenzi wa bomba la mafuta.

10. Ukarabati wa reli ya kaskazini.
 
Yote hayo yamemsaidia vipi mwananchi alieko Tandahimba?
Mkuu barabara itasaidia mama anaeenda kuifungua afike haraka na salama, pesa zake za ada za watoto wake hatazipeleka tena shuleni ila atanunulia mahitaji mengine kwani ada serikali imefuta na vilevile upatikanaji wa huduma za afya na kwenye mashirika ya umma ni mzuri sasa hivi mwananchi hanyanyaswi tena kwani wafanyakazi wasio na maadiri waliokuwa wanafanya kwa mazoea tu (vyeti) hawapo tena wamebaki wale walio somea fani husika, hakuna kutumbuliwa.
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.
 
Ha ha imebidi nicheke. na kelele zote hizi haya ndio kayafanya. Kukomesha rushwa how , nidhamu makazini unaweza kuniambia how, airport mwanza na Dar pamoja na flyovers ni on going projects alizikuta. Alichofanya yeye ni kununua bombardier used 2 ,kujenga hostels ya wanafunzi na kupanua hicho kipande cha barabara ya moroko.
Nyingine tunasikia kila siku ni mikwara , vitisho na ubabe ,kabaki kusema fanyeni kazi. Tutaona hiyo 2020. Hajaanza hata km 50 ya lami toka aingie ikulu
Ushabiki na chuki ni sumu mbaya sana.
Unaweza kuelezea kuhusu bombadia USED!
 
Back
Top Bottom