10102ac521314716b0cdeb7f1e57ec04.jpg

Wanajukwaa poleni na misukosuko ya kujibadili kutoka kuwa walaji wa Mwisho kuelekea nchi ya Viwanda.

Uwanja huu ni maalumu kama ule wa Safari za nje za Jakaya kikwete ila huu ni mahususi kukusanya mambo mazuri ya Awamu ya tano chini ya Rais Magufuli juu ya maendeleo yetu hasahasa kauli yake kuu Juu ya Nchi ya Viwanda na Elimu Bure nk.

Unaruhusiwa kugusia miundo mbinu, Afya, Usafiri, Maendeleo ya Majeshi Yetu, Uvuvi,Michezo, Habari, Siasa, Viwanda,Teknolojia, Pato la Taifa nk.
Ila tu iwe kwa tulipotoka na Alipofanikiwa na nini tufanye kumsaidia kujiongeza zaidi.

Mpaka sasa kafanya haya;

Hostel za Chuo cha UDSM.
Hostel za Askari Magereza.
Ununuzi wa Ndege 2 (Nyingine 3 ziko mbioni kuja).
Ujenzi wa Flyover Tazara na Ubungo
Upanuzi wa Airport Mwanza
Upanuzi barabara ya Moroco Dsm
Upanuzi wa Kisasa Airport Dar
Kukomesha Rushwa
Kurejesha nidhamu Makazini.
------------

Na haya ameanza tarehe 12/4/2017;

Uzinduzi ujenzi wa reli kwa ajili ya treni ya Umeme.
Ujenzi wa barabara ya Mtwara-Tandahimba

Kukomesha Watumishi Wenye Feki hivyo kuokoa Mabilioni ya Fedha.

Barabara ya kuunganisha Wilaya za Kibondo kigoma Kaliua huko Tabora.

Miradi Mikubwa ya Maji :

Uwezeshaji Ujenzi Bomba la Mafuta kutoka Hoima mpaka Tanga

============
emie emie posted: Kwa kweli Rais wetu kafanya makubwa sanaa..
Kila upitapo sasa hivi ni ujenzi unaendelea. Dar es Salaam kila kona Barabara ya Tandale-Sinza- Mawasiliano inajengwa
Madaraja yanajengwa

Upanuzi wa barabara kuu ya Ubungo hadi chalinze unafanywa

Daraja Kilombero miaka yote wapigaji walikuwa wanakula hela za wananchi kuwavusha ila sasa limejengwa

Flyovers zinajengwa

Miradi ya umeme inajengwa na miradi mingi ni kwa hela za watanzania wenyewe

Miaka yote maeneo ya Mbezi na kimara walikuwa hawapati maji japo yanapita njia hiyo hiyo lakini sasa maji yamefika mbezi, na bado wanaendelea kutandaza mabomba ili kupeleka maji. Awali waliokuwa wanakula hela za wananchi ni wenye miradi ya kuuza maji kwa magari. Ila sasa wananchi wamekombolewa.

Utendaji kazi umeimarika, sasa hivi kila mmoja anaona cheo akipewa ni kama kakalia kaa la moto..Yale mambo ya kupiga hela na kukaa ofisini kupiga usingizi yameisha watu ni kazi la sivyo unawajibishwa.

Madawa sasa yanapatikana hospitali, ile hali ya madawa ya hospitali yanapelekwa katika Pharmas binafsi imeisha.

Hospitali sasa za serikali ukienda mgonjwa anajaliwa sio kama ilivyokuwa awali.

Taasisi za serikali wafanyakazi wamekuwa wanawajibika, hakika nidhamu imeimarika.
Kwa sasa taasisi za serikali zinajiendesha kibiasara bali si kihasara kama ilivyokuwa awali, ilikuwa ni ulaji tuu wa hela, upigaji dili, taasisi zinakufa, hakuna gawio kwa serikali, ila sasa zinatoa gawio. Hakika kila kitu ni usimamizi imara, ukicheka na kima utavuna mabua.

Awali watu walikuwa wanaulilia uongozi, hata wasio kuwa na elimu walikuwa wanagombea kupata uongozi, sasa uongozi umekuwa mgumu sababu kama wewe si muwajibikaji una ndoto za kupiga tuu, hupati nafasi, Uongozi umekuwa una hadhi kwa sasa.

Hakika namsifu Rais wetu.

Pia soma;
- Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania
Haya no moja ya mafanikio ya utawala wake
 
Amefeli kwa speed ya rocket super sonic speed he will be remembered as the most failed president
 
Si nongwa zetu mnazozileta ilihali mioyo yenu inawatesa na kuwasuta.
kama ilivyo jadi kiongozi lazima ukae mbele kuongoza mapambano, na hata ikibidi kufa basi tumeliona hapa.

Wanaofurahi huku wasijue kiza kinakuja, wasijue kuhusu kesho yao !wakiwa wameitupa mioyo na maisha pamoja na ndoto kwa wengine, bila kujali kwamba hao wengine wana mioyo,ndoto pamoja na maisha yao, na je wapo tayari kuangalia ndoto ,mioyo na maisha ya wengine.

Aghalabu sana mtu kuwa na moyo wa dhati bila kukurupushwa .
Umeme 24/7 ,maji 24/7 , elimu bure, utu na nidhamu kisehemu.
Moyo wa kujituma na kulipenda Taifa. Moyo wa uzalendo. Amani iliyo jengeka nchini kwetu.
 
Si nongwa zetu mnazozileta ilihali mioyo yenu inawatesa na kuwasuta.
kama ilivyo jadi kiongozi lazima ukae mbele kuongoza mapambano, na hata ikibidi kufa basi tumeliona hapa....
Atakayekuja atakuwa mkali kuliko aliyetangulia. That is the principal. Nobody is ready to be referred as a looser.

CCM take note that the late President Magufuli has left a template for you to use for running this Country if you go back to the business as usual era get ready to loose the grip and loose administration forever.
 
Kwanza kabisa natoa salam za rambirambi kwa watanzania wote wazalendo walioguswa na msiba wa jemedari,'nguzo ya Africa',Rais wa mfano wa kuigwa ulimwenguni.Aliyependa wananchi wake kuliko mwenyewe.Pumzika kwa amani 'jembe'.

Ninaamini iwapo uongozi huu upya utaendeleza mfumo aliotuachia jabali utatuwezesha kusonga mbele na kupiga hatua kubwa kama taifa.

Kusiwe na mazoea kama ya zamani watumishi wa umma kunyanyasa wananchi badala ya kuwatumikia.kusiwe kuna matobo katika uongozi na kufanya nchi yetu kuwa 'shamba la bibi'.Nitasikitika kuhamia nchi nyingine kwani nitakua siwezi kuvumilia maovu hayo.
 
Ni wazi sasa kuwa JPM anafahamika kama mtetezi wa wanyonge na masikini. Ebu tujuzane namna masikini tulivyonufaika katika uwepo wake ili Rais Mama Samia Suluhu nae aendeleleze.
 
Bila kuwasahau wanufaika wa bodi ya mikopo ya elimu ya juu Nao ni kundi jingine la wanyonge ambao katika miaka Hii mitano wamekumbukwa kwa kurekebishiwa kikokotoo cha marejesho ya mikopo yao.
 
Back
Top Bottom