Sidhani Kama unapata muda wa kula na kuongea mada nje ya Jpm, wewe jamaa itakuwa una njaa kali Sana. Participation yako Jf kila Uzi hadi nashangaa pengine hata papuchi sijui unaichakata mda gani.
 
Mabadiliko mara nyingi yanakuja na maumivu! To be honest magufuli kapiga mzigo mkubwa sana! Na ni nature ya viongozi ambao Tanzania ilipaswa kua nao mtu mwenye maamuzi magumu! Dawa ni chungu lakini tutapona! Acha aendeleze alipo ishia
 
Inafika mahali unashindwa kuelewa watanzania wanataka nini hasa?

Kama ni maendeleo yanaonekana kwa macho, tena hayana vyama pande zote za nchi watu wameneemeka.
Huduma za kijamii ikiwemo afya na elimu imeboreshwa mara dufu, miundombinu ndio usiseme.
Treni ya Moshi - Arusha imerejea, ndege kadhalika meli na vivuko vimehuishwa.

Ninapotafakari watu hawa wanataka wafanyiwe nini nakumbuka maneno ya baba wa taifa mwalimu Nyerere kwamba ili nchi iendelee inahitaji Ardhi, Watu, Siasa safi na Uongozi bora.

Watanzania tunafeli wapi hadi kukumbatia siasa za kishabiki?

Au kuna watu wameamuwa kuwa na fikra za kipinzani tu? Maana hata shetani hapingi kila jema liletwalo na Mungu.

Niishie hapo.
Hivi unadhani kuna siasa Safi pamoja na damu nyingi zilizo mwagiga bila maelezo?

Kweli kuna vitu lakini kwa uchache, Kama afya bado ni changamoto dawa hakuna na huduma ni gharama unadhani mwananchi atakosa fikra za upinzani?

Fikiria ajira pamoja na mitaji mingi iliyoanguka ya biashara unadhani hali za wananchi waliowengi ipo katika namna gani?
Hebu fikiria vizuri uone majibu.
 
Inafika mahali unashindwa kuelewa watanzania wanataka nini hasa?

Kama ni maendeleo yanaonekana kwa macho, tena hayana vyama pande zote za nchi watu wameneemeka.
Huduma za kijamii ikiwemo afya na elimu imeboreshwa mara dufu, miundombinu ndio usiseme.
Treni ya Moshi - Arusha imerejea, ndege kadhalika meli na vivuko vimehuishwa.

Ninapotafakari watu hawa wanataka wafanyiwe nini nakumbuka maneno ya baba wa taifa mwalimu Nyerere kwamba ili nchi iendelee inahitaji Ardhi, Watu, Siasa safi na Uongozi bora.

Watanzania tunafeli wapi hadi kukumbatia siasa za kishabiki?

Au kuna watu wameamuwa kuwa na fikra za kipinzani tu? Maana hata shetani hapingi kila jema liletwalo na Mungu.

Niishie hapo.
Tatizo la CCM ni uongo. Sasa watu wameshauchoka kuona na kuusikia.

Hata wajikoshe kwa lipi watu wameshachoka hata kuwasikia wanahisi kiungulia au kichefuchefu ndio maana watu nyongo zinawatoka tu iwe mchana au usiku.
 
Hapo vip!

Binafsi kila nikimuona Rais Magufuli naiyona Tanzania mpya.

Muheshimu Rais Mungu akutie Nguvu na akuongezee Miaka mingi ya kuishi hapa Duniani.

Nakutamkia hivyo kwa niaba ya watanzania wote kwasababu umeiyondolea Tanzania aibu. Sasa hivi Mtanzania anaweza kutembea East Africa. Africa na Duniani kote,akaheshimika.

Nirudi kwenye mada husika,kwanza binafsi nikupongeze kwa mambo makubwa uliyoyafanya katika Nchi hii.

Ni wazi haya mambo uliyoyafanya yanaonekana ndani ya nchi na nje ya nchi pia.

Binafsi naomba nitaje mambo machache uliyoyafanya na nina imani watanzania wenzangu wanzalendo watataja mengine.

1.Ujenzi wa mradi mkubwa wa umeme unayoendea katika nchi yetu..mradi utawezesha nchi yetu iweze hata kuuza umeme Afrika nzima
2.kuondoa tatizo la wafanyakzi hewa waliokuwa wanaingizia nchi hasara ya mabilioni ya fedha.

3.kufufua shirika la ndege hivyo inasaidia fasten uchumi wa nchi..na niwazi watu sasa wanapanda ndege kwa bei nafuu hata wapinzani pia...kipato kinachopatikana kwenye sector ya usafiri wa anga ndio inayotumika kuleta elimu bure n.k

4.umerudisha heshima kazini,sasa hamna biashara unanijua mimi no..watu wote ni sawa.

5.Umeondoa giza Tanzania...nikimaanisha mgao wa umeme umekuwa historia.
6.umeleta elimu bure ..watoto wa maskini sasa wanasoma shule
7.umeondo mikatamibovu katika sector ya madine,umezuia makinikia na kujenga ukuta mererani...leo Tanzania ndio nchi ya kwanza Duniani kwa kuuza Tanzanite Duniani..kabla haujaingia madarakani Tanzania ilikuwa nchi ya saba.
8.Umejenga Treni ya Umeme kutoka dar kwenda Dodoma.
9.Umefufua Reli ya kati
10.Umepandisha Uchumi wa nchi mpaka benki ya Dunia imetanganza Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ..sio mchezo.
11.Umenunua Melikubwa na ya kisasa ya kutoka mwanza mpaka bukoba.

12.Umejenga barabara za fly over

13.Umejenga Daraja la kigamboni linalopita baharini.

14.umepambana na Korona kwa imani ya juu na hatimaye umeishinda.
15.umejenga hospitali nyingi sana
16.umejenga Mradi mkubwa wa maji Arusha.
17.umejenga bara imara na za kisasa

Naomba nitaje hizo chache ili niwape pia watanzania wenzangu fursa ya kuzitaja zingine..

Anayesema huyu baba hajaifanyia kitu nchi hii alaaniwe na watanzania.
 
Wanadamu tunasema unaweza kutenda mema 9999 lakini ukikosea moja linafuta mema 9999 yote!!

Kuna intake za kuanzia 2015 ziko mtaani, zinauza chips na nyingine zimeamua kutojulikana zinafanya nini mtaani.

Mheshimiwa Rais aacha kusema yeye ni rais wa wanyonge na masikini, maana watoto wa wanyonge na masikini ndio hao hao wanaosota mtaani na digrii zao kichwani.

Maana watoto wa wenye hela wako makazini na ajira zenyewe anatoa kwa mafungu mafungu, nchi hii ni kubwa na ina watu wengi 55m+ eti sekratalieti ya ajira ihusike kuratibu ajira, wanyonge ndio wanaoonewa, sekretalieti wanachukua watoto wa shangazi zao, na baba zao wakubwa kwa wadogo, sisi wengine lakapompo tuendelee kulima viazi na kuchoma mahindi mitaani.

VIJANA AMBAO AJIRA HAZIJAFIKA, NI WAKATI WA KUANGALI NANI ANAWEZA KUSAIDIA KUFIKA KWENYE KUISHI KWENYE NDOTO ZAKO.

WAKATI NI SASA.
FANYA CHAGUO KWA MASLAHI YAKO KWANZA.

JK Jr
 
Pamoja na madhaifu yake.. lakini Magufuli amedhubutu na anahitaji kupewa miaka mingine 5.. naamini Tanzania itakua mbali sana.

Japo ndani ya hii miaka 5 anahitaji kufanya haya mambo mawili ili kuacha legacy kama Rais Bora.

1. Kuweka mezani mchakato wa katiba
2. Kuwezesha Tanzania kupata katiba mpya isiyo na mizizi ndani ya ccm.

Watu wa Dar msipo mchagua .. mtakua hamna maana kabisa.. dar inamelemeta kwa barabara za mitaani, taa, vituo vya afya, etc.

Huyu hapa ndio Rais wa kumchagua.

FB_IMG_1597818272406.jpeg
 
Dar sio kama ule uchaguzi uliopita ambapo tulimpenda yule mwana CCM mwenzetu. Safari hii tunaweka historia. Tumejipanga! Amefanya mengi makubwa sana. Wagojwa na mabeberu na hao mbuzi wakae pembeni watupishe
 
Mtaji wa JPM uko kwa watu wa hali ya chini, machingaz, bodaboda and the likes. Na JPM kapewa ushindi na wapinzani pale walipojitoa akili kukebehi miuondo msingi/mbinu aliyoijega chini ya kipindi cha miaka 5 ya awamu yake. Hawakusea ingawa wao hawakuliona hilo waliposema atapigiwa kura na miundo mbinu, ni kweli wafaidika hiyo miundo msingi watampigia kura za kufuru.

Lakini wako watu wa maisha ya hali ya nchi ambao hata mpayujaji Lissu anajua siri hii kuwa hapo JPM alicheza karata zake vizuri pale aliponza kuzunguka nchi na kila mahali alipopita aliwapa heshima na umuhimu wa kuwasikiliza katika utendaji wake wa siku kwa siku. Na kuhakikisha juhudi za JPM na watendaji wengine chini yake katika kutatua kero za wananchi zitaleta maajabu ya wingi wa kura watakazozipata hapo oktoba.

Lissu na wenzaka kwa nini wanasema JPM atapigiwa kura na madaraja tu? Waache huu unafiki ulio kubuhu, waseme pia na ukweli mwingine kwamba JPM atapigiwa kura na machingaz, wachimbaji wadogo wa madini, wagonjwa waliopona na wanarndelea kutibiwa katika huduma za afya na miondombinu iloyoboreshwa, wazazi wenye watoto wanao pata elimu bure na shule zilizoboreshwa na madawati ya kutosheleza kwa kiwango cha kuridhisha. Raia wema ambao haki zao zilizokuwa zinadhulumiwa walitetewa na wakati mwingine Rais kuzisimamia na kuzishuhulikia mwenyewe tena kwa mtu ambaye hadhi yake katika jamii ni ya chini mno. Hii halikumpa Rais taabu maana anajua nini wajibu wake hata pale wasaidizi wake walipotaka kuzuia maskini hawa wasipate fursa ya kufikisha kilio chao wote tulimuona Rais JPM hadharani akiwasihi kuwapa nafasi awasikilize maana yeye ni kiongozi wa wote maskini na matajiri waaminifu si mafisadi na wezi lakini.
 
Mbali na matatizo kadha wa kadha yaliyosababishwa na utawala wake lakini ni ukweli kuwa Magufuli ni kiongozi jasiri na mwenye maono juu ya taifa hili.
Mh Rais ameondoa ule umwinyi uliokuwa umeanza kuota mizizi kwenye taifa hili, mfano baadhi ya viongozi kujiona miungu watu.

Kitendo cha kuwakata Pasi kuwa na hofu baadhi ya wababe kama Chenge ni ishara njema kwa kiongozi mkuu wa nchi. Lakini pia namna serikali yake ilivyolikabiri suala la CORONA ni ishara mojawapo ya kiongozi anayejali watu wake. Nilijiuliza sana hivi kama tungeingia lockdown (whether partial or complete) maisha yetu yangekuwaje haswa? Watumishi wa umma na binafsi tungeendelea kuwalipa kweli? Na maisha y mama ntilie, bodaboda, na vijana wetu wanaojipatia riziki kwa kazi za kutwa maisha yao yangekuwaje?

Kwa ufupi Haya ndiyo mafanikio matano muhimu ya awamu ya tano.
1. Kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi wanaoandikishwa darasa la kwanza, kidato cha kwanza na wanaodahiliwa vyuo vya kati na vyuo vikuu nchini.

2. Kuongezeka kwa uzalishaji wa mazao mbalimbali ya chakula na biashara. Ikumbukwe kuwa ndani ya kipindi cha miaka mitano ya kwanza ya utawala huu taifa halijashuhudia upungufu mkubwa was chakula kama awamu zilizopita hii ni kwa ya slogani ya hapa kazi tu.
3. Namna ilivyolitatua suala la korona nchini na kutoharibu mipango ya maendeleo iliyokuwepo kabla janga hill halijatufikia.
4. Kukiimarisha chama chake kama mwenyekiti kwa kutomuonea mtu aibu. Kitendo cha Kuwaita mbele ya kamati kuu kuwahoji waliokuwa viongozi na makada wandamizi wa chama hicho Mzee Yusuf Makamba, Abdurahiman Kinana na Bernard Membe ni ishara kuwa chama hikina mwenyewe kitu ambacho awali kilitoweka.
5. Kupungua kwa migogoro kati ya wafanya biashara wadogo wadogo, wachimbaji madini wadogo, migogoro ya wanafunzi wa elimu ya juu na serikali ni ishara nyingine serikali yake imetatua changamoto kadhaa ambazo zilipelekea migogoro kati ya makundi hayo na serikali.
 
Back
Top Bottom