Naona Kama EPL inataka kukukimbia hivi ..maana Jana umedrop point mbili vs Spurs na City kafumua mtu tano uko.
UEFA final uko na Madirid na siyo game nyepesi hiyo.
FA final uko na Chelsea na pia ni 50,50 maana kwa Sasa tunachechemea Ila lolote laweza kutokea.
Je, ikitokea umekosa makombe yote matatu utamlaumu Nani? Maana kikosi chenu kwa Sasa kipo 🔥🔥 ..tusubiri tuone msimu huu mutavuna nini.
#CFC💙💙💙
Aisee ngumu kumeza lakini kwenye mpira yote yanawezekana kabisa kwamba tukaambulia Carabao tu na nisishangae kabisa.
Kwanza fainali hua haina mwenyewe kabisa inakua open gemu kila mmoja kwa mbinu zake na utayari wa wachezaji anashinda kabisa kombe hivyo tusubiri burudani kwanza fainali FA itakua gemu ngumu japo unasema mnachechemea lakini Liverpool vs Chelsea haijawai kua rahisi na pazuri hata utulivu sasa mtapata kwani mmiliki mpya kashapatikana wamebakisha kuwakilisha seriakalini wajiridhishe hivyo mtapata stability kwa taarifa hizo.
Jana gemu ya Tottenham sijaangalia nitaisaka marudio nione namna gani Conte kaja na mbinu ipi. Baada ya ile sare ya Liverpool vs Manchester City Klopp alihojiwa na kuulizwa anaone aje hizi mbio na alijibu ni ngumu kushinda mechi zote nadhani zilikua zimekua 7 kipindi kile ila akasema atapambana kuwapa burudani mashabiki na pia kuona kama tutakua kwenye mix ya ubingwa na so far vijana mpaka sasa wamejitahidi mno mpaka tulipo msimu huu ni kwa juhudi zao sio rahisi kama tunavyoona sisi mashabiki kucheza fainali kila baada ya siku 3 au 4 na tutegemee ushindi kila gemu ni ngumu.
Nani wa kulaumiwa duuh sioni mchezaji mmoja mmoja wa kumnyooshea kidole jumla ila kuna baadhi ya gemu wachezaji walituangusha kwa mfano Milner gemu yetu kwenu mara mbili anampiga kiatu Pulisc refa akaona ujinga katoa free kick ikapigwa kuokolewa ikatua kwa Kovac mkapata goli la kwanza. Ukipata muda ebu tazama clip za hio gemu utaona.
Sare msimu huu zimekua nyingi kwetu na hizo ndio zimetuangusha tuna sare na Brighton, sare na Brentford, sare na Chelsea, sare na Manchester City, sare na Tottenham hapo mkuu tunakosa pointi 15 za ubishi ama hata 10 ambazo mpaka sasa ingekua ubingwa tunaunusa. Kwenye mbio hizi Pep amekua bora mpaka sasa maana leo na goal difference ameifuta kibishi.
Matokeo ya Everton vs Manchester City nayo yamechangia tulipo kama tukitazama matokeo ya wengine kwenye hizi mbio za EPL.
Kingine ubora wa EPL ni dhahiri ni level zingine ingekua zamani Spurs Anfield alikua hana jibu lake lakini kocha Conte ujue hajampiga Pep kwa kubahatisha wala hajatoa sare kwa kubahatisha mbali ni kwa mbinu.
Ni msimu wa mafanikio kwetu tumepata burudani murwa sana bado tuna gemu 5 mpaka msimu kuisha so let's all enjoy tjis beautiful game.
YNWA