Live: Kizota Dodoma

Live: Kizota Dodoma

  • Thread starter Thread starter MegaPyne
  • Start date Start date
mara nyingi utasikia kwenye kideo, kuna kiongozi nchi fulani katolewa madarakani kwa sababu ya rushwa, huku wengine tunafurahi tunasema demokrasia inafanya kazi, kumbe wale waliomtoa nao wala rushwa vile vile (wamemtoa kwa njama chafu, kumaanisha SIO CHAFU)!
 
Floribert N.N
i knew it you would be after me !(he teh teh )

kwani ukiambiwa mboga, basi wee unajua majani ya maboga ya maboga tu, huangalii kama yameiva, chumvi sawa sawa, maji n.k ?

Jibu swali bana...mbona unajibu kwa mafumbo...kwani wewe umekuwa Yesu?
 
Jibu swali bana...mbona unajibu kwa mafumbo...kwani wewe umekuwa Yesu?

duh ! halafu bana usichanganye mambo ya dini,HAPANA MIE SIO YESU ! ninavyojua mie wanaojibu mafumbo ni waimba taarabu, na hilo jibu nililokupa halijakaa kifumbo, bali ni CTQ (Critical Thinking Question) ! tafuta jibu babu !
 
duh ! halafu bana usichanganye mambo ya dini,HAPANA MIE SIO YESU ! ninavyojua mie wanaojibu mafumbo ni waimba taarabu, na hilo jibu nililokupa halijakaa kifumbo, bali ni CTQ (Critical Thinking Question) ! tafuta jibu babu !

Kwa nini unanipa mimi kazi ya kutafuta jibu wakati swali nimekuuliza wewe? Kama huwezi kujibu sema bana...
 
SIWEZI KUJIBU !
lakini kama wewe ni mvivu kiasi hicho kutafuta hiyo thread, basi hiyo inaweza ikawa sababu tosha kunifanya niamini kwa nini viongozi wetu ni wavivu mno kuleta maendeleo !

wananchi ni reflection ya viongozi, teh teh !
 
SIWEZI KUJIBU !
lakini kama wewe ni mvivu kiasi hicho kutafuta hiyo thread, basi hiyo inaweza ikawa sababu tosha kunifanya niamini kwa nini viongozi wetu ni wavivu mno kuleta maendeleo !

wananchi ni reflection ya viongozi, teh teh !!
 
By the way Field Marshall unaonekana sio fisadi, sasa unapokutana na Mkuu Mbona huonyeshi kumsaidia, kama vitu tunavyosema sisi kupitia JF, na ukaongezea na akili zako, ili mambo yaende mswano

Mkuu wangu huyo ni rais wa jamhuri, sasa kuandika hapa na kukutana naye uso kwa uso ni vitu viwili tofauti, yeye anasoma hapa forum kila siku, na ana watu wake hapa, kwa hiyo siwezi kumwambia jipya asilolijua,

katika viongozi wote wa juu sasa hivi tulionao, ni kiongozi mmoja tu anayeweza kumwambia as it is na akasikia, naye ni makamu aliyeondoka, wengine wote husema ndio mzee, tena utashangaa wengine ni wakubwa kiumri kuliko hata rais wetu, lakini humuamkia anyways! kijana viongozi hugeuka kama watoto wadogo mbele ya rais!


2.
sasa Benjamini kilimshinda nini 2005? Na kama watu wa Zanzibar waliweza kumkataa Salim hivyo leo mbona hatuna watu huku bara ambao wanaweza kumdindia mwenyekiti? au ndio alama za nyakati hizi..?

Watu wa bara huwa ni waoga sana, ndio maana lile kundi la G55, ni clear kuwa walikuwa na mkono wa mzito sana, ambaye ni Mwalimu, na baada ya kupewa vyeo wakanyamaza kimyaa, anyways ukweli ni kwamba bara hakuna mtu wa kumdindia mwenyekiti lakini siku zote wapo visiwani, viongozi wengi wa visiwani sio matajiri au masikini, kwa hiyo huwa hawana anything to lose, as opposed na huku kwenye bara ambako kumejaa wanafiki wakubwa wa dunia, wakati wa harusi ya makamu nilimuona kwa macho yangu kiongozi mmoja mkubwa wa nchi akilia machozi kwa kutowekwa kwenye kamati ya maandalizi ya harusi ile, halafu nikamuona kiongozi mwingine akilia machozi kwamba yeye ndiye awe MC, mwingine alidai aruhusiwe kuingiza ng'ombe ndani ya ukumbi wa harusi aliowaleta kama zawadi, I can go on and on....!
 
Mkuu wangu huyo ni rais wa jamhuri, sasa kuandika hapa na kukutana naye uso kwa uso ni vitu viwili tofauti, yeye anasoma hapa forum kila siku, na ana watu wake hapa, kwa hiyo siwezi kumwambia jipya asilolijua,
katika viongozi wote wa juu sasa hivi tulionao, ni kiongozi mmoja tu anayeweza kumwambia as it is na akasikia, naye ni makamu aliyeondoka, wengine wote husema ndio mzee, tena utashangaa wengine ni wakubwa kiumri kuliko hata rais wetu, lakini humuamkia anyways!

Wow, ina maana huwa anatembea na laptop, au anakuwa busy kwenye simu akisoma? au huenda hata tunajibishana naye hapa Mkuu?
 
Haya tuendelee na kumkoma nyani giledi...
Kilitime na FD, wajomba mbona majina ya wasomi wengi yametupwa nje?...
 
Nape Mnauye, amepita ni kijana mwenye ideas nzuri sana za maendeleo, najua kuna siku atapata nafasi ya kuonyesha vitu vyake!
 
Muungwana, ukweli ni kwamba hakufanya research za kutosha wakati akiwa kwenye kampeni, na pia hakujua kuwa watu wote waliomzunguka kuwa ni wajanja, viongozi wengi wazee walimwambia wazi wazi kuwa hauwezi urais, lakini haikuwezekana kumzuia, lakini pia simalumu maana kuna mahali alikubali kuwa yuko radhi kuwa waziri mkuu kwanza, labda hiyo ingemsaidia sana in the future,

Sasa makosa yameshafanyika na ukweli ni kwamba sasa hivi yeye yumo kwenye learning process ya urais, na ni sisi wananchi tuliodai kwa nguvu zote kuwa tunataka vijana, I mean we are in this mess all together wakuu!

Heshima Mbele Mkuu,

Kazi zetu za kawaida hupewa miezi mitatu kama probation period. Huyu mkuu ana miaka miwili sasa bado anajifunza kazi, kulikoni? Ndiyo kusema watu wa chuo wanapomwita kilaza wako right?

Kitu kingine si huwa wanajidai kuwa uwaziri ndiyo sifa ya kuwa rais kwasababu ya uzoefu wa shughuli za serikali. Huyu mkuu amekuwa waziri zaidi ya miaka 15...vipi hakupata uzoefu wa kutosha au ndiyo ukilaza huo?
 
Uwaziri sio urais wa Tanzania, hayo tumeyaona toka enzi za Mkapa maana angalau Mwinyi hakuingia kwa mikogo, aliingia kimya kimya na kuondoka kimya kimya,

Tatizo ni Mkapa na Muungwana, walioingia kwa mikogo mingi, mimi mpaka leo sielewi huko juu kuna nini, maana wakiwa chini wanakuwa na maneno mengi mazuri, lakini wakifika tu basi wanakuwa mabubu,

kabla ya kuingia Ikulu, kuna siku nilikaa chini na Muungwana, ambapo aliniambia kwa uchungu jinsi alivyochoshwa na viongozi wazee, na kanipa mfano clear wa Kibaki, kwamba kazi yake ni kulala tu na kukingiwa kifua na wasaidizi wake,

Alipoingia Ikulu tu, akamchagua Kingunge, ambaye alishaamua kustaafu, na sasa Msekwa, kwa hiyo mkuu wangu huko Ikulu kuna something sijui ni nini kinachowabadili mawazo once wakiingia tu huko! Lakini kabla ya kuingia wanakuwa na maneno mengi mazuri!
 
Reading though the strings posted, one comes to several conclusions.

First, those who are in DOM witnessing CCM proceedings are being carried away. And before I go further, I want to make it clear that I am not favoring any part. I am on issues, and on some of the tough questions which are in the public domain in the minds of many Tanzanians, who are still waiting for answers.

I get the impression JF members in Dom are being hurried in posting "strings" and mostly their opinions and NOT either full account/scripts, or in this case an "impartial" summary which could benefit those who have not been privileged to follow. I think JF deserves better; repackaged information that can allow one to give informed comments, and not just a string of yada yada. I am sorry to put it this way.

Now to the issues. Am I getting the wrong impression here? That CCM party Chair who is also President of the country is making a cover up? I mean, he is taking us back to 2005 during the inaugural speech which was overly sweetened and as it turns out it was more of lip-service. And as many JF members are pointing out, there is nothing new, but a well crafted speech to derail Wananchi in focusing on the real issues.

I agree that we are heavily dependant on foreign aid. But we should also agree we are very poor in using that very same foreign aid. Tanzania is among few countries whose budgets are heavily subsidized, yet accountability, embezzlement, is a problem. Corruption is rife, in the end, WHO benefits?

It doesn't make any difference to the majority whether we get donor support or not, THEY don’t benefit. That donor support ends up maintaining a colossal government, such a huge cabinet! Payment for bogus companies, kickbacks, unchecked spending... What trickles down to "Wadanganyika" is peanuts...

Let's face this... and perhaps it is time we got less aid so that we could start thinking of ways of redeeming ourselves from this vicious circle. KAMA TWAFIKIRI TUTAENDELEA KWA MISAADA, TUNAJIDANGANYA. To me, donor aid is "grand corruption", and severe arrest to our capacity to recoup!

A good name abroad... SO WHAT? We get more AID? We now of countries who have even been coined "Axis of Evil" but are enjoying huge economic relationships with the so-called "WORLD" than us who have been singing PEACE and cleanliness...

Let's talk about the serious issues: CHADEMA, CCM, CUF, TLP, whatever, let's cut this party smoke screen. WE ARE ALL Tanzanians...

I think CCM Chair and TG, oh; TZ President forgets that he is a very POWERFUL person in his country. I think he should stop going circles but directly address some of the issues that appear to cripple our economy. CORRUPTION, SHADY DEALS, FAILURE to benefit from our natural resources, and lip-service.

In any case, HE still holds the WHIP, HE is President. WE all dully respect and recognize that. But the public senses there are some figures other than the president who are also above the law. Untouchable, even to the President? Let's clean this country of corrupt leaders, and give it a clean bill of health now...

CCM shouldn't turn into a syndicate... too bad it already appears so... In the times of Nyerere, the Mzee would never mince words; he would say it straight "into your face". He was the President, and Chair of the Chama.

We miss that badly...

And the internet... I think no one can stop this... This is global: you either swim or sink, there is no escape!

So, let's not derail from the core issues maiming TZ... And let those who have first hand of info better inform the rest so that we give proper comments, you never know, if the president is receiving SMS from anyone, he may as well be spending sometime at JF, and when he does, JF should provide good critique...
 
Najivunia,

I am not sure wether I should address my self in English or swahili. But, well I think for the benefit of all swahili will sound better.

Nilipokuwa Dodoma na kuzungumzia yanayoendelea nilikuwa naongea kama nionavyo mimi. Mapungufu yapo I am human being. Alipoongelea mwingine nae alitoa maelezo yake kutokana na alivyoona/kusikia. Magazeti pia yanaandikwa na binadamu.

Lets come back to the president speech. JK aliongelea rushwa, akasema kuna viongozi wa serikali au waliowahi kuwa viongozi 38 wanahojiwa walipopata mali zao, ikionekana wana matatizo watafikishwa mahakamani. Lets give him a benefit of doubt, tusubiri.

Rushwa ndani ya chama aliizungumzia.

Mani point yako ni rushwa kubwa kubwa ambazo baadhi ya mawaziri wanatuhumiwa. Najivunia ndugu yangu, rushwa kubwa kubwa sio rahisi kuzi track, zinatakiwa muda mrefu na uchunguzi wa kina, huwezi kukurupuka kuchukua hatua, WATAKUSHINDA MAHAKAMANI KIRAHISI SANA. Mfano kama PM kama tunavyomshutumu alihusika na Richmonduli, usifikiri (kama ni kweli) aliandika barua kuwa wachagueni hawa la sivyo nawafukuza kazi! wala usifikiri hela (kama ni kweli) za rushwa zilipelekwa kwenye account yake ya CRDB pale Azikiwe!

Guys running the country is not like running a joint or a business, It is much more complicated than we think.

Put your self in Muungwana's shoes. What would you do on fighting corruption? what are your basis for that decision?.

Bila kujali imetoka wapi kila anayetoa taarifa anatoa kuendana na anataka msomaji au msikilizaji asikie/asome nini, PERIOD.

Unedited
 
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, (Takukuru), imekamilisha upelelezi wa tuhuma za rushwa kuhusina na utata wa ununuzi wa rada na mmoja wa watuhumiwa katika kashfa hiyo, Shailesh Pragji Vithlani, amefunguliwa mashitaka katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar salaam, ili kujibu tuhuma zinazomkabili.


Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za taasisi hiyo, Mkurugunzi wa Idara ya Elimu kwa Umma wa Takukuru, Mary Mosha, alisema mshitakiwa huyo alibainika kushiriki katika mlolongo wa ununuzi wa rada kutokana na uchunguzi uliofanywa na taasisi hiyo.


Alisema taasisi hiyo imeshafungua kesi namba 1474/2007 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu dhidi ya mtuhumiwa huyo, itakayokuwa chini ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi, Sivangilwa Mwangesi.


?Kwa sasa natangaza rasmi kuwa mshitakiwa popote alipo duniani anatafutwa kwa ajili ya kujibu mashitaka yanayomkabili na asipofanya hivyo tutamkamata kwa vile hati ya kumkamata imeshatolewa na mahakama? alisisitiza Mosha


Mosha alisema Mshitakiwa huyo anayetafutwa ana uraia wa Tanzania na Uingereza, hivyo wamewasiliana na Polisi wa Kimataifa (Interpol), ili popote alipo duniani aweze kukamatwa na kujibu tuhuma zinazomkabili.


Hata hivyo Mkurugenzi huyo alipotakiwa kuwataja watuhumiwa wengine waliobainika kuhusika na ununuzi huo wa rada, alikataa kwa madai kuwa taasisi hiyo imeanza kumfungulia mashitaka mtuhumiwa mmoja kwa kufuata taratibu na sheria za Takukuru na kwamba baadaye wataendelea kuwashughulikia wengine.


Source Gazeti Mwananchi

MNATAKA MUUNGWANA AFANYE NINI ZAIDI YA HAYA???!!!
 
Mosha alisema Mshitakiwa huyo anayetafutwa ana uraia wa Tanzania na Uingereza, hivyo wamewasiliana na Polisi wa Kimataifa (Interpol), ili popote alipo duniani aweze kukamatwa na kujibu tuhuma zinazomkabili

Kumbe kuna watanzania wengine wana uraia wa nchi mbili siku hizi? This is news to me.
 
Back
Top Bottom