Kuanguka kwa Kingunge, lilikuwa ni suala la wakati tu, maana huko nyuma niliwahi kusema kuwa kwenye kikao cha kamati kuu cha kwanza chini ya Muungwana kama mwenyekiti, jinsi alivyomkaripia Kingunge kama mtoto mdogo, pale Kingunge alipodai Mahita afukuzwe kazi mara moja, nikawakumbusha tena majuzi kwenye kikao cha cc ambapo tena Kingunge alipotaka wabunge wawili wale wa "rushwa" wafukuzwe, alivyoshushuliwa na Muungwana,
Na pia nikawakumbusha kuwa mwenyekiti wa ccm ndiye huwapigania watu anaowataka kuingia cc, asiowataka hawawezi kuingia huko hata kama noma na iwe, na katika siasa za ccm, hata uwe na nguvu kiasi gani, kama huingii cc, wewe ni msindikizaji tu,
Swali la msingi hapa ni je Kingunge atakasirika na kugeuka mpinzani ndani ya ccm?, au atajiunga na asilia? Ataingia Chadema? Kumbuka hii ni mara yake ya kwanza kupigwa chini katika siasa, au naye atajiunga na kina Sumaye, na Salim kwenda kupewa counselling kwa Malecela, ya namna ya kuishi baada ya kushindwa uchaguzi?