Chagu wa Malunde
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 8,708
- 5,711
Nauliza hili swali sababu kama wananchi tunataka kufahamu ukweli juu ya hili janga. Tunataka waziri wa afya, au msemaji mkuu wa serikali kila siku awe anatoa taarifa zilizo rasmi.
Mbona nchi za wenzetu ambazo zimekumbwa na hili janga kila siku lazima watoe taarifa rasmi kuhusu maambukizi,waliopona na waliofariki.
Au hapa Tanzania ndio kusema mambo yanaenda kimya kimya? Maana watu kila kukicha ni kutishwa tu na habari ambazo sio rasmi.
Mara tunasikia watu wanazikwa usiku, mara tunasikia rubani wa Tanapa alikufa kwa Covid-19,mara kuna maiti imekaa siku mbili mtaa wa Lumumba. Lakini hatusikii serikali ikikanusha wala kuwaambia ukweli wananchi.
Kwa jinsi hili janga lilivyo serious ilipaswa waziri wa afya au msemaji wa serikali angekuwa kila siku anakaa na wanahabari na kutoa takwimu na taarifa rasmi.
Lakini mtu mmoja ambae anamiliki jarida la mtandaoni (Pambazuka) anapoachiwa awe anaandika habari za uongo kuwa watu wanazikwa usiku kimya kimya ni jambo baya maana watu hofu inazidi kwa wananchi.
Inatoka habari kuwa madereva wanne watanzania wamepimwa huko Uganda na kukutwa na ugonjwa wa Covid-19. Hofu inazidi kuwa kubwa kwa wananchi.
Hivyo ili kuondoa hofu lazima mtupatie taarifa rasmi,kama nchi tupo wapi?
Maambukizi ni mengi? Yamepungua? Na wanaopona ni kiasi gani? Hii iwe kila siku na mruhusu kupigwa maswali na waandishi wa habari kama Andrew Cuomo gavana wa New York anavyofanya kila siku. Maana hatulali ni hofu tu.