Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,011
- 9,879
Baada ya Wizara ya Afya kutoa tahadhari ya kuwepo kwa viashiria vya wimbi la tatu la ugonjwa wa Covid 19, Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) Dk Shedrack Mwaibambe ameshauri Serikali kuweka wazi hali ya ugonjwa huo nchini.
Akizungumza na Mwananchi jana Jumapili Juni 20, 2021 Dk Mwaibambe alisema ipo haja kwa Serikali kuweka wazi kuwa ugonjwa huo upo nchini na taasisi nyingine ziungane kupambana nao.
“Ukisema kuna viashiria mtu anaweza asishtuke na akaendelea na maisha yake kama kawaida, kama ugonjwa upo Serikali ina jukumu la kuwalinda wananchi wake kwa kueleza wazi.
“Pia mapambano dhidi ya Covid 19 hayapaswi kuwa ya Serikali pekee, lazima taasisi nyingine zisaidie, mfano taasisi za dini, elimu na nyingine zinazohusisha mikusanyiko ziwekeze nguvu kuelimisha watu kuchukua tahadhari,” alisema.
Alieleza kuwa endapo takwimu na elimu ya kujikinga itatolewa kila mahala kwa kiasi kikubwa itasaidia watu kuchukua tahadhari.
Akizungumzia hilo, Mkurugenzi wa Kinga wa Wizara ya Afya, Dk Leonard Subi alieleza Serikali itaendelea kutoa taarifa thabiti kuhusu janga hilo.
“Mabadiliko ya tabia yanaweza kuathiriwa na kuendeleza kampeni ya uelimishaji wa umma na elimu, na kwa msaada wa vyombo vya habari tuna imani kuwa watu wangeanza kuchukua suala hili kwa uzito,”
Dk Subi alisema ni wakati wa wadau kutoka sekta ya umma na binafsi kutoa maoni ya hatua sahihi za kufuata ili kujikinga na ugonjwa huo.
Alieleza Serikali kupitia wizara itaendelea kuchukua hatua nyingine dhidi ya ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na kuimarisha usalama wa mipaka na upimaji wa Covid-19 katika viwanja vya ndege na vituo vya mipakani.
Licha ya mara kadhaa viongozi wa Serikali akiwemo Rais Samia Suluhu Hassan kuwataka wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo, watu wamekuwa wazito kuzingatia.
Mwananchi imeshuhudia watu wakiwa katika maeneo yenye misongamano bila kuchukua tahadhari ikiwemo kuvaa barakoa wala kupeana nafasi. Baadhi ya wananchi waliozungumza walieleza suala la ugonjwa huo wameliacha mikononi mwa Mungu kama ambavyo Serikali imekuwa ikielekeza.
Katika maeneo mengi ya biashara, stendi za mabasi hakuna ndoo za maji wala sabuni au matenki yenye maji tiririka kwa ajili ya watu kunawa mikono.