Kwanini ndege hutengenezwa kwa kutumia "material" mepesi?

Kwanini ndege hutengenezwa kwa kutumia "material" mepesi?

Impact gani iliyotokea pale wakati ndege ilizama tu majini na inasemekana hakukuwa na mwamba (jiwe) wowote. Ina maana impact ya maji tu ndio isababishe uharibifu ule?

Wavuvi wanasema eneo ilipoingia ndege pana mchanga mtupu, kwahiyo impact yake baada ya kukita kwenye mchanga haikuwa kubwa kihivyo.

kaka mita 100 kutoka ufukweni ni dhahiri shairi kuwa ndege iligusa ardhi maa ile ndege haipungui tani 40
 
Hata hewa kama ukiweza kuitembeza hiyo ndege kwa km 10,000 kwa saa itaungua kwa moto utaotokana na msuguano kati ya ndege na hewa. Space shuttle Columbia iliteketea kwa staili hiyo ikiingia anga la dunia tokea space station
Mbona space station hailipuki wakati inatembea km 120000/h laki na 20 kwà saa?
 
Swala sio kubadili gia angani, I am responding to what comes in. Halafu, ingekuwa vizuri zaidi na wewe ukatoa mchango wako ili kusupport hicho ulichokiita nondo na kudai kuwa mimi nimekikimbia. Kwa taarifa yako there is nothing which has been spoken here kikawa juu ya uwezo wangu. Kama na wewe unahisi/unajiami, shusha hizo nondo hapa halafu tushindane mimi na wewe halafu tuone nani yuko shallow.
mzee huelewi kitu kuhusu ndege.

kwa akili ya kawaida unaweza ukauliza eti " kwanini material ya ndege haitengenezwi na chuma"

swali lenyewe linaonyesha namna gani ur very shallow katik maada husika...

kamsaidia dada kuchimba viazi aisee[emoji23][emoji23]
 
1. Ulitaka kujua kwanini Ndege inatengenezwa kwa Material mepesi umejibiwa ingetengenezwa kwa material ngumu isingeweza kupaa material mepesi halafu imara yanawezesha kuruka

2 a. Ulitaka kujua kwanini Ndege ilipoibuliwa iliharibika vibaya ukajibiwa ni kutokana na msukumo wa jinsi ilivyotua ukatolewa mfano na wewe upande kwenye muinuko halafu ujirushe kwenye maji kwa tumbo ama mgongo ndio utapata jibu halisi la kwanini Ndege iliharibika vile

2b. Ukataka kuleta hoja ya Rubani hakudondoka bali alitua kwa kukusudia ukaulizwa mbona hakuwatangazia abiria wake kua anatua kwa dharura kwenye maji ili wajiandae kwa kuvaa life jackets?

3. Ukataka kujua material iliyotengeneza Ndege hiyo ni aina gani ukajibiwa ni Aluminium na sifa ya Aluminium ni nyepesi lakini ngumu,

4. Ukawataka wataalam waichunguze ndege hiyo kama ilikua ina kiwango cha kuruka au ilitumika material feki ukajibiwa Ndege zote haziwezi kuruhusiwa kuruka bila wataalam wa Dunia kuithibitisha ubora wake baada ya kutengenezwa kwa maana hiyo Ndege ya Precision haikua na tatizo la material

Na mimi nakuongezea hili,
SUBIRI WATAALAM WAJE NA MAJIBU YA CHANZO CHA AJALI YA NDEGE ACHA KIHEREHERE CHA KUJIFANYA MTAFITI WAKATI YA NYUMBANI KWAKO YANAKUSHINDA.
asante kwa kumpa hoja
 
Ndege mara nyingi haitakiwi kuanguka na ikitokea ni Uzembe wa Binadamu kwa asilimia kubwa.

Ujenzi wake ni kama KIFUA cha Binadamu ambapo Mbavu zipo kulinda Kamoyo kasidhurike pamoja na mapafu bila kuhitaika Minyama kibao kulinda sehemu hizo. Nadhani sababu ni ileile kwamba tuwe wepesi.

Ndege hutumia MAFUTa mengi mno wakati wa kuruka na ikifika kwa mfano 8km au 10km juu, inatulia huko na kuanza kuteleza tu. Huko kuna upepo mdogo na hivyo Wind Resistance ni ndogo pia GRAVITATION inapungua. Kwa wanaotoka Ulaya kwenda USA au USA to EUROPE, wakati mwingine wanautumia upepo unaopuliza kwenye ndege kwa nyuma na na kwenda haraka zaidi pia kutumia mafuta kidogo.

Kwa saabu hiyo, siku zote wanatafuta Material Magumu na mepesi zaidi ili ile NGOZI ya ndege na MBAVU za Ndege ziwe imara na nyepesi zaidi.

View attachment 2418116
Umeeleza katika lugha rahisi mpaka mimi tabularasa nimeelwa
 
Kufuatia ajali iliyotokea huko Bukoba, na kuangamiza ndugu zetu wapatao 19 na kujeruhi wengine wengi, yapo maswali ya kujiuliza.

Ndege ilipoibuliwa kutoka majini tuliona uharibifu mkubwa kwa ndege yenyewe na hata kutia mashaka kiasi cha kujiuliza hivi kweli hata kama ni ajali ndio ndege iharibike kiasi hiki?

Swali la kujiuliza hapa ni kuwa, material gani zinatumika kutengeneza ndege? Au wanatumia material "fake" kama za mchina? Baada ya kutolewa majini tumeiona ndege imejikunja kama karatasi, kutoka umbile la kunyooka mpaka umbile la 'el' (L)!

Kama ingetumika material imara kutengenezea ndege hiyo, huenda kusingekuwa na uharibifu tuliouona na hivyo kupunguza maafa yaliyotokea.

Timu ya uchunguzi isiishie kuangalia tu chanzo cha ajali, bali na matengenezo ya ndege yenyewe. Ikibainika material fake ilitumika kutengeneza ndege, basi kampuni iliyotengeneza ndege nayo iwajibike.
Material nzito ndege itashindwa kupaa, itakua nzito sana. Na ndege haitengenezwi kwa mategemeo itadondoka... so inatengenezwa ili iweze kupaa
Na pia Material ngumu mfano chuma, haiwezi kustahimili zile turbulence ndege inakutana nazo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Impact gani iliyotokea pale wakati ndege ilizama tu majini na inasemekana hakukuwa na mwamba (jiwe) wowote. Ina maana impact ya maji tu ndio isababishe uharibifu ule?

Wavuvi wanasema eneo ilipoingia ndege pana mchanga mtupu, kwahiyo impact yake baada ya kukita kwenye mchanga haikuwa kubwa kihivyo.
Hivi unajua ukitokea mita kadhaa juu ukadondoka ndan ya maji bado utavunjika tu kama ambavo ungevunjika ukiwa nchi kavu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mzee huelewi kitu kuhusu ndege.

kwa akili ya kawaida unaweza ukauliza eti " kwanini material ya ndege haitengenezwi na chuma"

swali lenyewe linaonyesha namna gani ur very shallow katik maada husika...

kamsaidia dada kuchimba viazi aisee[emoji23][emoji23]
Sio kutengeneza material, bali material ya kutengenezea ndege
 
Material nzito ndege itashindwa kupaa, itakua nzito sana. Na ndege haitengenezwi kwa mategemeo itadondoka... so inatengenezwa ili iweze kupaa
Na pia Material ngumu mfano chuma, haiwezi kustahimili zile turbulence ndege inakutana nazo

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama unaongelea turbulence, nadhani kitu kizito ndio kinahimili turbulence kuliko chepesi. Kama umewahi kusafiri kwa kutumia ndege kubwa na ndogo, bila shaka utakuwa unalielewa hili.
 
Kama unaongelea turbulence, nadhani kitu kizito ndio kinahimili turbulence kuliko chepesi. Kama umewahi kusafiri kwa kutumia ndege kubwa na ndogo, bila shaka utakuwa unalielewa hili.
ww jamaa mbna hueleweki??

yani umeuuliza swali ili ujibiwe ila sasa kila anayeleta hoja na jibu unabishaa..

Nini kusudio la kuanzisha thread hii.?
 
Kama unaongelea turbulence, nadhani kitu kizito ndio kinahimili turbulence kuliko chepesi. Kama umewahi kusafiri kwa kutumia ndege kubwa na ndogo, bila shaka utakuwa unalielewa hili.
Nope. Kuna somo nilisoma chuoni linaitwa properties of metals. So nitakuelekeza kwa urahisi.
Chuma ikiwa kama kitu kizito, ni moja kati ya metals ambavyo havikunjiki. Chuma ukiikunja unaikata na ili kusudi. N dege iwe safe zaidi tunahitaji material yenye uwezo wa kukunjika sana iwe flexible vya kutosha bila kukatika. Mabawa yanaact kama spring inavokua kweny. e miguu ya magari. Kwenye turbulence ili ndege iweze kua controlled vzr unahitaji material flexible ndiomaana wanatumia aluminum na composite materials kama carbon fibers etc..
Na materials kua nzito haimaanishi ndio imara, hapana. Kila metal ina sifa zake na zinawekwa sehem kulingana na kazi inayotakiwa. Ndiomaana utakuta malory yanachasis ya chuma na magari ya madogo yana aluminum.
Kitu kingine, uzito kwenye ndege ni disadvantage kubwa sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lakini ujue maji yanasave kama cushion!
Maji yanakua kama cushion ukiwa distance ndogo... siku ukiwa unaogelea jaribu kuchapa kofi juu ya surface ya maji uone, utaumia kiganja.
Sasa imagine ni kitu kimedondoka mita kadhaa kutoka angani kwa spidi kali.
Pia ndege zimetengenezwa kana kwamba ziwe na uwezo wa kutua kwenye maji na kuzama taratibu, sasa ukiweka material nzito zitakua zinazama moja kwa moja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ww jamaa mbna hueleweki??

yani umeuuliza swali ili ujibiwe ila sasa kila anayeleta hoja na jibu unabishaa..

Nini kusudio la kuanzisha thread hii.?
Ni kwelj nimeuliza swali na kutaka majibu, lakini hii haimaanishi nikubaliane au nisihoji pale ninapoana kuna mashaka. Wewe unakubali kulishwa matango pori?
 
Nope. Kuna somo nilisoma chuoni linaitwa properties of metals. So nitakuelekeza kwa urahisi.
Chuma ikiwa kama kitu kizito, ni moja kati ya metals ambavyo havikunjiki. Chuma ukiikunja unaikata na ili kusudi. N dege iwe safe zaidi tunahitaji material yenye uwezo wa kukunjika sana iwe flexible vya kutosha bila kukatika. Mabawa yanaact kama spring inavokua kweny. e miguu ya magari. Kwenye turbulence ili ndege iweze kua controlled vzr unahitaji material flexible ndiomaana wanatumia aluminum na composite materials kama carbon fibers etc..
Na materials kua nzito haimaanishi ndio imara, hapana. Kila metal ina sifa zake na zinawekwa sehem kulingana na kazi inayotakiwa. Ndiomaana utakuta malory yanachasis ya chuma na magari ya madogo yana aluminum.
Kitu kingine, uzito kwenye ndege ni disadvantage kubwa sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa hiyo unataka kusema effect ya turbulence itakayopata ndege ndogo na kubwa zilizotengenezwa kwa material sawa haitakuwa tofauti (namaanisha myumbisho)? Kwa ndege tunaongelea air turbulence, na kwa meli tunasema water turbulence, sasa mbona meli kubwa inavumilia turbulence kuliko meli ndogo? Does it not apply to planes as well?
 
Back
Top Bottom