Mkuu
stars
Mpaka sasa kuna teknolojia tofauti za uundaji na ujenzi wa body za ndege
Alluminium, hapa inahusika Duralumin ambayo ni mchanganyiko ( alloy) wa allumium, copper na element kadhaa ili kuweza kupata material bora hapa wadau washakujibu sababu za kutumia duralumin ambayo ni teknolojia iliyotumika sana kwenye body za ndege kama ilivyo precision
Ushawahi kujiuliza ni kwanini katika umeme mkubwa wa masafa katika nguzo zinatumika nyaya za allumium badala ya copper jibu ni lilelile
wepesi na gharama
Titanium, hii ndo metal ngumu kuliko zote na utengenezaji wa body za titanium ni gharama mara nyingi hutumika kwenye ndege za kivita (supersonic plane) kama Blackbird SR-71 ambayo inaweza kukimbia kwa speed ya mach 3.(Body za aluminium haziwezi kufikia speed ya mach 2 inaweza kupelekea zikalipuka kwa msuguano wa angani)
Composites, hapa sasa ndo teknolojia ya ya kisasa ya body za ndege ilipofikia. CFRP ni ngumu na gharama rahisi kuliko alluminium. changamoto iliyopo ni kudect katika mifumo ya radar, hivyo basi ndege nyingi za kisasa body zake zinatumia asilimia kubwa composites na allumium kidogo
Kwa mfana boeng 787 body yake imetumia composites isipokuwa kwenye mabawa pekee