Bajeti ya Wizara ya Nishati 2024/25 yapunguzwa kwa karibu nusu ya Bajeti ya mwaka 2023/24

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,591
8,800
Wizara ya Nishati imewasilisha Bungeni Bajeti ya Tsh. Trilioni 1.88 kwaajili ya matumizi ya Maendeleo, Matumizi ya Kawaida na Mishara ya Wizara hiyo pamoja na Taasisi zilizo chini yake kwa mwaka 2024/25 ambapo Kati ya Fedha hizo, Tsh. 1,536,020,274,000 ni fedha za ndani na Tsh. 258,846,558,000 ni Fedha za Nje.
FB_IMG_1713982052865.jpg

Akiwasilisha Bajeti hiyo Bunge, Waziri wa Nishati. Dkt. Dotto Biteko, amesema; Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu sasa liidhinishe Bajeti ya jumla ya Shilingi Trilioni Moja, Bilioni Mia Nane Themanini na Tatu, Milioni Mia Saba Hamsini na Tisa, Mia Nne Hamsini na Tano Elfu (Shilingi 1,883,759,455,000) kwa ajili ya matumizi ya Wizara ya Nishati na Taasisi zake.

Hata hivyo Bajeti hiyo imepungua kutoka Tsh. Trilioni 3 zilizozombwa kutumika katika mwaka 2023/24

Mchanganuo wa fedha hizo ni kama ifuatavyo:

(i) Shilingi Trilioni Moja, Bilioni Mia Saba Tisini na Nne, Milioni Mia Nane Sitini na Sita, Mia Nane Thelathini na Mbili Elfu (Shilingi 1,794,866,832,000) sawa na asilimia 95.28 ya Bajeti yote ya Wizara ni21 kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo. Kati ya fedha hizo, Shilingi Trilioni Moja, Bilioni Mia Tano Thelathini na Sita na Milioni Ishirini, Mia Mbili Sabini na Nne Elfu (Shilingi 1,536,020,274,000) ni fedha za ndani na Shilingi Bilioni Mia Mbili Hamsini na Nane, Milioni Mia Nane Arobaini na Sita, Mia Tano Hamsini na Nane Elfu (Shilingi
258,846,558,000) ni fedha za nje; na

(ii) Shilingi Bilioni Themanini na Nane, Milioni Mia Nane Tisini na Mbili, Mia Sita Ishirini na Tatu Elfu (Shilingi 88,892,623,000) sawa na asilimia 4.72 ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida. Kati ya fedha hizo
Shilingi Bilioni Sitini na Tisa, Milioni Mia Tano Ishirini na Nne, Mia Mbili na Moja Elfu (Shilingi 69,524,201,000) ni kwa ajili ya Matumizi Mengineyo (OC) na Shilingi Bilioni Kumi na Tisa, Milioni Mia Tatu
Sitini na Nane, Mia Nne Ishirini na Mbili Elfu (Shilingi 19,368,422,000) ni kwa ajili ya Mishahara (PE) ya Watumishi wa Wizara na Taasisi zilizo chini yake.
FB_IMG_1713982060110.jpg

Mheshimiwa Spika, naomba tena nitoe shukrani zangu za dhati kwako na kwa Waheshimiwa Wabunge wote kwa kunisikiliza. Hotuba hii pia inapatikana katika Tovuti ya Wizara kwa anuani ya www.nishati.go.tz. Vilevile, Hotuba hii ina vielelezo mbalimbali ambavyo vimeambatishwa kwa ajili ya ufafanuzi wa masuala muhimu yanayohusu Sekta ya Nishati.

======

HOTUBA YA NAIBU WAZIRI MKUU NA WAZIRI WA NISHATI MHESHIMIWA DKT. DOTO MASHAKA BITEKO (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA NISHATI KWA MWAKA 2024/25

UTANGULIZI

Mheshimiwa Spika, kufuatia Taarifa iliyowasilishwa leo katika Bunge lako Tukufu na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, naomba kutoa hoja kwamba, Bunge lako Tukufu sasa likubali kupokea, kujadili na kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Taasisi zake kwa mwaka 2024/25.

Mheshimiwa Spika, awali ya yote napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema kwa kunijalia afya njema na fursa ya kusimama mbele ya Bunge lako Tukufu kuwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati kwa Mwaka 2024/25. Aidha, kwa kuwa ni mara yangu ya kwanza kusimama kama Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati katika Serikali ya Awamu ya Sita (6) na kuwasilisha Hotuba hii, kwa namna ya kipekee napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuniamini na kuniteua kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati.

Uteuzi huu ni dhamana na heshima kubwa kwangu katika kuhakikisha kuwa Sekta ya Nishati inakidhi matarajio ya Watanzania ya kupata umeme wa uhakika pamoja na kuendeleza rasilimali za mafuta na gesi kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya nchi yetu. Nitumie fursa hii kuahidi, na kwa kadri Mwenyezi Mungu atakavyoniwezesha, kutekeleza majukumu yangu kwa weledi na uadilifu mkubwa kwa kushirikiana na Bunge lako Tukufu pamoja na wadau wengine katika Sekta ya Nishati.

Mheshimiwa Spika, tarehe 29 Februari, 2024 Taifa letu lilimpoteza aliyekuwa Rais mstaafu wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Ali Hassan Mwinyi. Aidha, kabla ya hapo, tarehe 10 Februari, 2024 Taifa lilimpoteza aliyekuwa Waziri Mkuu mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Edward Ngoyai Lowassa. Kwa masikitiko makubwa naungana na Wabunge wenzangu na wananchi kwa ujumla kutoa pole kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, familia, ndugu, jamaa, marafiki na watanzania wote kwa ujumla kwa kuondokewa na viongozi wetu hawa, tuliwapenda lakini Mwenyezi Mungu amewapenda zaidi. Tunaomba Mwenyezi Mungu azilaze roho za wapendwa wetu mahali pema peponi, Amina.

Mheshimiwa Spika, Julai mosi, 2023, Bunge lako Tukufu lilimpoteza Mhe. Francis Leonard Mtega, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mbarali. Aidha, tarehe 8 Aprili 2024, Bunge lako lilimpoteza Mhe. Ahmed Yahya Abdulwakil aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kwahani, Zanzibar. Naungana na Wabunge wenzangu kutoa pole kwa Bunge lako Tukufu, familia ya marehemu, ndugu, jamaa, marafiki na wote walioguswa na misiba hiyo. Tunaomba Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu wote mahali pema peponi, Amina. Vilevile, naungana na Bunge lako Tukufu na Watanzania kwa ujumla, kuwapa pole watanzania wenzetu waliopatwa na majanga mbalimbali katika mwaka 2023/24, ikiwemo yaliyotokana na mafuriko na maporomoko ya mawe na matope katika maeneo ya Hanang Mkoani Manyara; Kibiti na Rufiji Mkoani Pwani pamoja na Malinyi, Ulanga, Ifakara na Mlimba Mkoani Morogoro.

Mheshimiwa Spika, kipekee nawashukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), kwa uongozi na juhudi zao katika kuleta maendeleo ya Taifa letu na kwa ushirikiano wanaonipa katika kusimamia na kutekeleza majukumu ya Wizara ya Nishati. Nikiri kuwa maelekezo na miongozo ya viongozi wetu hawa ni msingi wa mafanikio ya utekelezaji wa majukumu ya Sekta ya Nishati. Aidha, napenda kumpongeza Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa kuendelea kusimamia kwa umahiri utekelezaji wa shughuli za maendeleo katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Mheshimiwa Spika, napenda kukupongeza kwa dhati wewe binafsi kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU). Hii ni heshima kubwa na Tunu kwa Watanzania wote kwa ujumla kwa kuthaminiwa na kutambuliwa katika medani za kimataifa. Tunakuombea kwa Mwenyezi Mungu ili azidi kukupa nguvu na hekima zaidi katika kutekeleza majukumu yako.

Mheshimiwa Spika, napenda kutumia fursa hii tena kukupongeza wewe binafsi, Naibu Spika na Wenyeviti wa Bunge kwa kuliongoza Bunge letu Tukufu kwa umahiri mkubwa. Aidha, nitumie fursa hii kumpongeza Bi. Nenelwa Mwihambi, Katibu wa Bunge kwa usimamizi wa shughuli za Bunge. Ni dhahiri kuwa, chini ya uongozi wenu Bunge letu limeendelea kutekeleza majukumu yake ya kikatiba ipasavyo katika kuhakikisha kuwa Serikali inatekeleza wajibu wa kuwaletea wananchi maendeleo.

Mheshimiwa Spika, naomba kutumia fursa hii kuwapongeza Mawaziri na manaibu Waziri walioteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan. Nampongeza Mhe. Jerry William Silaa (Mb), aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Mhe. Deogratius John Ndejembi (Mb), aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu); Mhe. Alexander Pastory Mnyeti (Mb), aliyeteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Kilimo; Mhe. David Mwakiposa Kihenzile (Mb), aliyeteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Uchukuzi; Mhe. Dunstan Luka Kitandula (Mb), aliyeteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii; Mhe. Judith Salvio Kapinga (Mb.) aliyeteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Nishati; Mhe. Daniel Baran Sillo (Mb), aliyeteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mhe. Zainab Athuman Katimba (Mb), aliyeteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI. Nawatakia kila la kheri katika utekelezaji wa majukumu yao.

Mheshimiwa Spika, naomba niungane na Waheshimiwa Wabunge wenzangu kumpongeza, Mhe. Bahati Keneth Ndingo, Mbunge wa jimbo la Mbarali kwa kuchaguliwa kwake kwa kishindo kuwa mwakilishi wa wananchi katika jimbo hilo. Hakika ni heshima kubwa uliyopewa na wananchi wa Mbarali na ninakutakia kila la kheri katika kutekeleza jukumu lako la uwakilishi katika Bunge letu Tukufu.

Mheshimiwa Spika, kipekee nampongeza Mhe. Dkt. David Mathayo David (Mb.) kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na Mhe. Kilumbe Shaban Ng’enda (Mb.) kwa kuchaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo. Vilevile, nawashukuru wajumbe wote wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kwa ushauri na maoni yao katika kuendeleza na kusimamia Sekta ya Nishati kwa manufaa ya kiuchumi na kijamii kwa Taifa letu na watu wake.

Mheshimiwa Spika, namshukuru Mhe. Judith Salvio Kapinga (Mb.), Naibu Waziri wa Nishati kwa kuendelea kunisaidia kwa karibu katika kutekeleza majukumu yangu. Aidha, napenda kumshukuru Katibu Mkuu Mha. Felchesmi Jossen Mramba kwa utendaji kazi wake mahiri na ushirikiano anaonipa katika kutekeleza shughuli zangu za kila siku za Wizara. Nampongeza pia, Dkt. James Peter Mataragio kwa kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati. Nawashukuru pia Wakuu wa Idara na Vitengo, Wenyeviti na Wajumbe wa Bodi za Taasisi zilizo chini ya Wizara, Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara na Watumishi wote wa Wizara kwa ujumla kwa ushirikiano na juhudi zao katika kufanikisha kufikiwa kwa malengo ya Wizara.

Mheshimiwa Spika, kipekee kabisa, nitumie fursa hii kuwashukuru wananchi wa Jimbo la Bukombe kwa kuendelea kunipa ushirikiano mkubwa katika kutekeleza majukumu yangu kama Mbunge wao. Kutokana na majukumu ya kitaifa kama Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati kuna wakati wananikosa jimboni, lakini kwa wema wao wanaendelea kunivumilia na kunipa ushirikiano mkubwa. Nawaahidi kuendelea kuwa mtumishi wao mwaminifu katika kutekeleza shughuli za maendeleo. Aidha, namshukuru mke wangu mpendwa Benadetha Clement Mathayo kwa maombi na upendo wake wa dhati kwangu na watoto wetu. Amekuwa mvumilivu katika kipindi chote ninapokuwa natekeleza majukumu yangu ya Ubunge, Uwaziri na Unaibu Waziri Mkuu na kukubali kubeba na kutekeleza baadhi ya majukumu ya kifamilia.

Mheshimiwa Spika, nitumie pia fursa hii kuvishukuru na kuvipongeza Vyombo vya Habari vikiwemo redio, televisheni, magazeti na mitandao ya kijamii kwa ushirikiano mkubwa waliotupatia Wizara ya Nishati kwa mwaka 2023/24. Vyombo hivyo vimekuwa mstari wa mbele katika kufuatilia kwa karibu miradi na shughuli zinazotekelezwa na Wizara ya Nishati na kuelimisha pamoja na kuhabarisha umma kuhusu mafanikio yaliyopatikana. Ni matumaini yangu kuwa, ushirikiano huu utazidi kuimarika katika Mwaka wa Fedha wa 2024/25 kwa manufaa ya Taifa letu na wananchi kwa ujumla katika upatikanaji wa taarifa kuhusu Sekta ya Nishati.

Mheshimiwa Spika, Hotuba hii imeandaliwa kwa kuzingatia maudhui ya Hotuba ya Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu Mapitio ya Utekelezaji wa Kazi za Serikali kwa Mwaka 2023/24 na Mwelekeo wa Kazi za Serikali kwa Mwaka 2024/25.

Mheshimiwa Spika, baada ya utangulizi huo, naomba sasa kuwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara kwa Mwaka 2023/24, pamoja na Mpango na Bajeti ya Wizara kwa Mwaka 2024/25.

B. UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA WIZARA KWA MWAKA 2023/24

Mheshimiwa Spika
, utekelezaji wa majukumu ya Wizara kwa mwaka 2023/24 uliongozwa na vipaumbele mbalimbali vilivyojikita katika kukamilisha miradi mbalimbali ya uzalishaji na usafirishaji wa umeme pamoja na kuendelea kuchukua hatua nyingine za kuimarisha uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa umeme nchini; kuendelea kupeleka umeme vijijini, vitongojini, katika visiwa na maeneo yaliyo mbali na gridi ya Taifa, vituo vya afya na pampu za maji, wachimbaji wadogo wa madini, maeneo ya kilimo na viwanda na katika shule na mahakama za mwanzo vijijini; pamoja na kutekeleza mikakati na programu mbalimbali kuimarisha matumizi ya nishati safi ya kupikia (clean cooking) nchini.

Mheshimiwa Spika, vipaumbele vingine vilikuwa ni kuanza maandalizi ya utekelezaji wa Mradi wa Kuchakata za na Kusindika Gesi Asilia kuwa Kimiminika (Liquefied Natural Gas – LNG); kuendelea na utekelezaji wa Mradi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi kutoka Hoima - Uganda Hadi Tanga – Tanzania (EACOP), shughuli za utafiti wa mafuta na gesi asilia katika vitalu vya Kimkakati, usambazaji wa gesi asilia viwandani, majumbani na nchi jirani, kuimarisha matumizi ya Gesi Asilia Iliyoshindiliwa (Compressed Natural Gas-CNG) katika magari pamoja na kunadi vitalu (licencing round) vilivyo wazi katika maeneo ya nchi kavu na baharini ili viendelezwe.

Mheshimiwa Spika, Wizara ilielekeza pia nguvu katika kuhakikisha nchi yetu inaendelea kuwa na uhakika wa upatikanaji wa bidhaa za mafuta ya petroli, kutokana na umuhimu wake katika ukuaji wa shughuli za kiuchumi na kijamii pamoja kuimarisha ufanisi katika kushughulikia bidhaa hizo. Aidha, Wizara iliendelea kuimarisha Taasisi/Mashirika yaliyo chini ya Wizara ya TANESCO, TPDC, REA, EWURA na PURA pamoja na Kampuni Tanzu ili yatoe huduma bora kwa mujibu wa matarajio ya wadau, kuimarisha mapato pamoja na tija na ufanisi katika uendeshaji. Kwa kuzingatia gharama katika utekelezaji wa miradi ya nishati, Wizara iliendelea pia kuelekeza nguvu katika kuimarisha ushiriki wa Sekta Binafsi katika utekelezaji wa miradi ya nishati.

Bajeti ya Matumizi ya Wizara na Mtiririko wa Fedha kwa Mwaka 2023/24

Mheshimiwa Spika,
katika mwaka 2023/24, Wizara ya Nishati iliidhinishiwa kutumia jumla ya Shilingi Trilioni Tatu na Bilioni Arobaini na

Nane, Milioni Mia Sita Thelathini na Mbili, Mia Tano Kumi na Tisa Elfu
(Shilingi 3,048,632,519,000) ambapo Shilingi Trilioni Mbili, Bilioni Mia Sita na

Tisa, Milioni Mia Moja Hamsini na Sita, Mia Moja Ishirini na Nane Elfu
(Shilingi 2,609,156,128,000) ziliidhinishwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo na Shilingi Bilioni Themanini na

Saba, Milioni Mia Tisa Ishirini na Tisa, Mia Sita Tisini na Nane Elfu (Shilingi 87,929,698,000)
ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida.

Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Machi, 2024, Wizara ilipokea jumla ya Shilingi Trilioni

Moja, Bilioni Mia Nane Kumi na Tatu na Milioni Ishirini na Sita, Mia Moja Arobaini na Saba Elfu, Mia Moja Hamsini na Sita (Shilingi 1,813,026,147,156)
, ambapo Shilingi Bilioni Ishirini na Saba na

Milioni Sabini na Tisa na Ishirini na Sita Elfu, Mia Saba Kumi na Sita
(Shilingi 27,079,026,716) ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida na Shilingi

Trilioni Moja, Bilioni Mia Saba Themanini na Tano, Milioni Mia Tisa Arobaini na Saba, Mia Moja Ishirini Elfu, Mia Nne Arobaini (Shilingi 1,785,947,120,440) ni kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo.

B.1 SEKTA NDOGO YA UMEME NA NISHATI JADIDIFU

B.1.1 HALI YA UZALISHAJI NA UPATIKANAJI WA UMEME NCHINI

Mheshimiwa Spika,
katika mwaka 2023/24 Serikali iliendelea kuchukua hatua za kuimarisha uzalishaji na upatikanaji wa umeme nchini ambapo hadi kufikia Machi, 2024 uwezo wa mitambo ya kufua umeme iliyounganishwa katika mfumo wa Gridi ya Taifa ulifikia jumla ya MW 2,138 ikiwa ni ongezeko la asilimia 14.2 ikilinganishwa na MW 1,872.1 za Mei, 2023. Katika kiasi hicho MW 836.3 (asilimia 39.1) ni umeme unaotokana na nguvu ya maji, MW 1,198.8 (asilimia 56.1) gesi asilia, MW 92.4 (asilimia 4.3) mafuta mazito na MW 10.5 (asilimia 0.5) tungamotaka (biomass) kama inavyofafanuliwa katika Kielelezo Na. 1.
Kielelezo Na.1:Uwezo wa Mitambo ya Kufua Umeme katika
Gridi ya Taifa hadi Machi, 2024 na Hali ya
Uzalishaji
Chanzo
Uwezo wa Mitambo
Hali ya Uzalishaji
MW
Asilimia
MW
Asilimia
Maji
836.3​
39.1%​
755.5​
43.1%​
Gesi Asilia
1,198.8​
56.1%​
935.1​
53.2%​
Mafuta
92.4​
4.3%​
65.8​
3.7%​
Tungamotaka
10.5​
0.5%​
-​
-​
Jumla
2,138.0
100%
1,756.4
100%
Uwezo wa Mitambo (MW)
4.3%​
0.5%​
39.1%​
56.1%​

MajiGesi AsiliaMafutaTungamotaka

Hali ya Uzalishaji (MW)

3.7% 0.0%​

43.1%

53.2%

MajiGesi AsiliaMafutaTungamotaka

Mheshimiwa Spika, Ongezeko la uwezo wa uzalishaji wa umeme limetokana na kuanza kwa uzalishaji wa umeme katika Mradi wa Kuzalisha Umeme wa Julius Nyerere (MW 2,115) ambapo MW 235 zimeanza kuzalishwa kupitia mtambo Namba 9 pamoja na kukamilika kwa Mradi wa Kuzalisha Umeme wa Rusumo ambao unachangia MW 26.7 katika Gridi ya Taifa. Kiambatisho Na. 1 ni mchanganuo wa uwezo wa mitambo ya kuzalisha umeme katika Gridi ya Taifa hadi Machi, 2024.

Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Machi 2024, uwezo wa mitambo ya kuzalisha umeme ambayo haijaungwa katika Gridi ya Taifa ni MW 33.4 ambazo zinajumuisha mitambo inayomilikiwa na TANESCO yenye uwezo wa kufua MW 28.4 na MW 5 zitokanazo na nguvu ya jua kutoka kwa mzalishaji binafsi. Aidha, Wizara kupitia TANESCO inanunua umeme wa MW 31 kati ya hizo MW 21 kutoka Uganda kwa ajili ya Mkoa wa Kagera na MW 10 kutoka Zambia kwa ajili ya Mkoa wa Rukwa.

Mheshimiwa Spika, pamoja na kuongezeka kwa uzalishaji wa umeme katika kipindi cha Julai, 2023 hadi Machi 2024, bado uzalishaji huo ulikuwa haukidhi mahitaji ya nchi ambayo yamekuwa yakiongezeka kwa kasi kutokana na ukuaji wa shughuli za kiuchumi na kijamii pamoja na changamoto za upungufu wa maji na gesi asilia katika vituo vya kufua umeme, hitilafu katika mitambo ya uzalishaji pamoja na kufanyika kwa matengenezo katika mitambo ya uzalishaji wa umeme. Mahitaji ya juu ya umeme nchini yamekua na kufikia MW 1,590.1 zilizofikiwa tarehe 26 Machi, 2024 saa 3.00 usiku sawa na ongezeko la asilimia 8.1 ikilinganishwa na MW 1,470. 5 zilizofikiwa tarehe 12 Juni, 2023 saa 2:00 usiku. Kielelezo Na.2 ni mwenendo wa ukuaji wa mahitaji ya umeme katika mwaka 2022/23 na 2023/24.

Kielelezo Na. 2: Ukuaji wa Mahitaji ya Umeme (Megawati) Nchini kwa Mwaka 2022/23 na Mwaka 2023/24
MWEZI
JULAIAGOSTISEPTEMBAOKTOBANOVEMBADESEMBA
2022/23​
1,302.2​
1,321.0​
1,341.3​
1,336.1
1,315.6​
1,354.6​

JANUARI FEBRUARI MACHI WASTANI

1391.7 1,402.7 1401.9 1351.9
MWAKA
2023/24​
1,466.1​
1,482.8 1413.5​
1399.9​
1389.5​
1339.7​
1434.4​
1,510.3​
1590.1​
1447.4​
ONGEZEKO (%)
11.2
10.9
5.11
4.6
5.3
-1.1
3.0
7.1
11.8
7.1
B.1.2 HALI YA USAFIRISHAJI NA USAMBAZAJI WA UMEME

Mheshimiwa Spika,
kwa upande wa usafirishaji wa umeme, miundombinu ya kusafirisha umeme imeendelea kuimarika na kufikia jumla ya urefu wa kilomita 7,745.4 ikiwa ni ongezeko la asilimia 17.8 ikilinganishwa na kilomita 6,363.3 za mwaka 2022/23. Ongezeko hili limetokana na kukamilika kwa miradi mbalimbali ya njia za kusafirisha umeme, ikiwemo msongo wa Kilovoti 400 kutoka Julius Nyerere Hydro Power Plant hadi Chalinze, Singida- Arusha- Namanga pamoja na msongo wa Kilovoti 220 kutoka Morogoro hadi Dodoma kwa ajili ya uendeshaji wa treni ya umeme (SGR Lot II).

Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kuchukua hatua za kuimarisha miundombinu ya usambazaji umeme nchini ambapo imeongezeka na kufikia kilomita 176,750.9 ikiwa ni ongezeko la asilimia 4.9 ikilinganishwa na kilomita 168,548.5 za mwezi Mei, 2023. Kwa upande wa njia za kusambaza umeme, kilomita 58,886.6 ni za msongo wa Kilovoti 33, kilomita 12,476.6 za msongo wa Kilovoti 11 na kilomita 105,387.7 za msongo wa Kilovoti 0.4. Kielelezo Na.3 ni mwenendo wa miundombinu ya usafirishaji na usambazaji wa umeme.
Kielelezo
Na.3: Njia
za
Kusafirisha na
Kusambaza
Umeme hadi Kufikia Machi, 2024
Na.
Njia za Usafirishaji wa
Urefu (Km)
Umeme
Mei, 2023
Machi, 2024
1.​
Njia za msongo wa kV 400
670.0​
1,244.8​
2.​
Njia za msongo wa kV 220
3,477.7​
4,095.6​
3.​
Njia za msongo wa kV 132
1,672.6​
1,825.0​
4.​
Njia za msongo wa kV 66
543.0​
580.0​
Jumla
6,363.3
7,745.4
Njiaza Usambazajiwa
Umeme
1.​
Njia za msongo wa kV 33
55,045.6​
58,886. 6​
2.​
Njia za msongo wa kV 11
12,986.3​
12,476.6​
3.​
Njia za msongo wa kV 0.4
100,516. 6​
105,387.7​
Jumla
168,548.5
176,750.9

Chanzo: TANESCO

B.1.3 HUDUMA KWA WATEJA

Mheshimiwa Spika,
katika kipindi cha Julai, 2023 hadi Machi, 2024 Serikali kupitia TANESCO imetekeleza mikakati mbalimbali ya kuimarisha utoaji wa huduma ikiwa ni pamoja na:

Kuongeza wigo wa mawasiliano na wateja kwa kuanzisha mfumo unaomuwezesha mteja kuhudumiwa kwa haraka zaidi bila kupiga simu kwa njia ya ujumbe wa simu (CHATBOT). Mfumo huu umekamilika kwa asilimia 95;

Kupanua kituo cha huduma kwa wateja (Call Center) kwa kuongeza vifaa na wapokea simu kutoka mawakala 63 mpaka 100. Kwa sasa, Shirika linakamilisha taratibu za ununuzi wa vifaa;

iii. Kuanzisha mfumo utakaowawezesha wateja kupata taarifa maalumu za hali ya upatikanaji wa umeme kwa haraka kwa njia ya ujumbe wa simu kwenye simu zote janja na simu za kiswaswadu kuhusu Makatizo ya Umeme (Automatic Power Interruption Notification sytem) na hivyo kuwezesha wateja kujipanga ipasavyo na kupunguza malalamiko ya ukosefu wa umeme; na

Kuanzisha mfumo wa benki ya taarifa na elimu (DESA SYTEM knowledge based) ili kuweza kutatua changamoto za wateja kwa kuwapa elimu na taarifa mbalimbali zitakazotatua changamoto zao bila mafundi. Uanzishwaji wa mfumo huu umefikia asilimia 99 ili uweze kuanza kutumika.

B.1.4 MIRADI YA KUZALISHA UMEME

Miradi Iliyopo katika Hatua za Utekelezaji

Mradi wa Kuzalisha Umeme wa Julius Nyerere (JNHPP – MW 2,115)

Mheshimiwa Spika,
Serikali iliendelea na utekelezaji wa mradi wa kimkakati wa Kuzalisha Umeme wa Julius Nyerere wenye uwezo wa kuzalisha umeme wa MW 2,115 katika maporomoko ya maji ya Mto Rufiji, wenye gharama ya Shilingi trilioni 6.55 zinazogharamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa asilimia 100.

Mheshimiwa Spika, naomba nitumie fursa hii kulitaarifu Bunge lako Tukufu kuwa, sasa tupo katika hatua za mwisho za kukamilisha mradi huu ambapo hadi kufikia Machi, 2024 utekelezaji wake ulikuwa umefikia asilimia 97.43 na uzalishaji kuanza kupitia mtambo Namba 9 unaoingiza katika Gridi ya Taifa jumla ya MW 235. Aidha, mtambo Namba 8 wa mradi huu upo katika hatua za mwisho za ukamilishwaji ili uanze uzalishaji wa MW nyingine 235. Kazi zinazoendelea kukamilishwa ni pamoja na ujenzi wa barabara za kudumu katika eneo la mradi ambao umefikia asimilia 85.6, ujenzi wa nyumba za makazi na ofisi ambao umefikia asilimia 98.5, ujenzi wa Daraja la kudumu ambao umefikia asilimia 97.2 na ufungaji wa mitambo saba (7) yenye uwezo wa kuzalisha MW 235 kila mmoja ambayo ipo katika hatua mbalimbali za ufungwaji.

Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Gesi Asilia wa Kinyerezi I Extension– MW 185

Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2023/24, Serikali ilikamilisha ujenzi wa mitambo ya kufua umeme ya Kinyerezi I Extension MW 185 ambapo kwa sasa mitambo yote minne (4) inafua umeme. Aidha, hadi kufika Machi 2024, kazi ya upanuzi wa kituo cha kupoza umeme cha Kinyerezi ilikuwa imefikia asilimia 97.6 ambapo transfoma mbili zenye uwezo wa MVA 175 zilikuwa zimefungwa kwenye misingi yake; na ujenzi wa barabara, ufungaji wa taa na mifumo ya ulinzi ulikuwa unaendelea. Vilevile, vituo vya Mbagala na Gongolamboto vinaongezewa uwezo kufikia MVA 170 kutoka uwezo wa awali wa MVA 50. Pia, ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme yenye urefu wa kilomita 19.2 ya msongo wa Kilovoti 132 kutoka Kinyerezi hadi Mbagala kupitia Gongolamboto umefikia asilimia 55.

Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Maji wa Rusumo – MW 80

Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusisha uzalishaji wa umeme wa MW 80 kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Kagera na umejengwa kwa ushirikiano wa nchi tatu (3) za Tanzania, Burundi na Rwanda kwa mgawanyo sawa wa umeme kwa kila nchi. Mradi umekamilika na kuanza uzalishaji wa umeme ambapo kila nchi inapata MW 27. Aidha, kwa upande wa Tanzania mradi ulihusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme yenye msongo wa Kilovoti 220 kutoka Rusumo hadi Nyakanazi yenye urefu wa kilomita 94.1 pamoja na miradi ya kijamii ambayo imekamilika kwa asilimia 100.

Ukarabati wa Mitambo katika Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Hale

Mheshimiwa Spika, Serikali iliendelea na ukarabati wa miundombinu ya kuzalisha umeme katika Kituo cha Hale chenye uwezo wa kuzalisha MW 21 ambapo kwa sasa kiasi kinachozalishwa ni MW 10.5 kutokana na uchakavu wa miundombinu ya kuzalisha umeme. Hadi kufikia Machi, 2024, utekelezaji wa mradi huu ulikuwa umefikia asilimia 61 na kazi zinazoendelea kutekelezwa ni pamoja na kukamilisha uundaji wa mitambo, matengenezo ya kituo cha kupoza umeme, ujenzi wa barabara mpya yenye urefu wa kilomita 1.3 na uchimbaji wa njia ya chini ya ardhi. Mradi unatarajiwa kukamilika Agosti, 2025.

Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Maji wa Malagarasi – MW 49.5

Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusisha ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme wa MW 49.5 kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Malagarasi pamoja na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 132 yenye urefu wa kilomita 54 kutoka Malagarasi hadi Kidahwe, mkoani Kigoma. Aidha, tayari Mkandarasi ameanza ujenzi wa bwawa la kuzalisha umeme na mradi unatarajiwa kukamilika Oktoba, 2027. Vilevile, Mkandarasi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme anaendelea na kazi za ujenzi ambapo utekelezaji umefikia asilimia 15.6 na mradi unatarajiwa kukamilika Aprili, 2025.

Mradi wa Kuzalisha Umeme wa Jua Mkoani Shinyanga – MW 150

Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa mradi huu unahusisha ujenzi wa mitambo ya kuzalisha umeme wa Megawati 150 kwa kutumia nguvu ya jua Mkoani Shinyanga. Hadi kufikia Machi, 2024 Serikali ilikuwa imekamilisha ulipaji wa fidia ya Shilingi bilioni 2.6 kwa wananchi 109 waliopisha mradi. Aidha, Mkandarasi anaendelea na ujenzi wa miundombinu ya kuzalisha umeme na mradi unatarajiwa kukamilika Januari, 2025.

Miradi ya Kuboresha Upatikanaji wa Umeme Mikoa ya Kusini (Lindi na Mtwara)

Mheshimiwa Spika, Serikali iliendelea na utekelezaji wa Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa kutumia Gesi Asilia wa Mtwara (MW 300) ambapo maandalizi ya malipo ya fidia kwa wananchi watakaopisha eneo la ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme pamoja na njia ya kusafirisha umeme yanaendelea. Aidha, Serikali inaendelea na mazungumzo na JICA kwa ajili ya utekelezaji wa mradi.

Mheshimiwa Spika, ikiwa ni hatua ya kuhakikisha Mikoa ya Lindi na Mtwara inakuwa na umeme wa uhakika na unaoendana na ukuaji wa mahitaji, Serikali iliendelea kuchukua hatua mbalimbali. Hatua hizo ni pamoja na kufunga mtambo wa kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia wa MW 20 katika eneo la Hiyari, Mkoani Mtwara ambao umeanza uzalishaji wa umeme, pamoja na kufufua mtambo Na.13 (MW 4.3) na mtambo Na. 8 (MW 2) mkoani Mtwara na mtambo Na.3 (MW 2.5) Somanga mkoani Lindi. Hatua hizo zimeimarisha upatikanaji wa umeme na kuondoa mgao wa umeme katika mikoa ya Lindi na Mtwara.

Aidha, Serikali inaendelea kuchukua hatua za kuiunganisha Mikoa ya Lindi na Mtwara katika Gridi ya Taifa kwa kukamilisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme ya Songea- Tunduru-Masasi-Mahumbika ifikapo Agosti, 2025. Kielelezo Na. 4 ni mtambo wa kuzalisha umeme kiasi cha MW 20 ukiwa eneo la kufungwa Mkoani Mtwara.​

Kielelezo Na.4: Mtambo wa Kuzalisha Umeme Kiasi cha MW 20 Ukiwa Katika Eneo la Kusimikwa Mkoani Mtwara

Miradi ya Uzalishaji wa Umeme Iliyopo katika Hatua za Utayarishaji

Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Maji wa Ruhudji – MW 358

Mheshimiwa Spika, Serikali iliendelea na utekelezaji wa mradi huu unaohusisha ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme wa MW 358 kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Ruhudji mkoani Njombe na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 400 yenye urefu wa kilomita 170 kutoka Ruhudji hadi kituo cha kupoza umeme cha Kisada mkoani Iringa. Tayari uthamini wa mali za wananchi watakaolipwa fidia ili kupisha eneo la mradi kwa ajili ya ujenzi umekamilika na taratibu za kulipa fidia zinaendelea. Aidha, vyeti vya Tathmini ya Athari za Mazingira na Jamii kwa upande wa kituo cha kuzalisha umeme na njia ya kusafirisha umeme vimeshatolewa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC). Vilevile, tathmini ya gharama za miundombinu wezeshi imekamilika na taratibu za kupata fedha za kutekeleza mradi na ujenzi wa miundombinu hiyo zinaendelea.

Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Maji wa Rumakali – MW 222

Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusisha ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme wa MW 222 kwa kutumia maji ya Mto Rumakali mkoani Njombe na njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa Kilovoti 220 yenye urefu wa kilomita 64.5 kutoka kwenye mitambo hadi kituo cha kupoza umeme cha Iganjo mkoani Mbeya.

Mheshimiwa Spika, hatua zilizochukuliwa katika kutekeleza mradi huu ni pamoja na kukamilisha uthamini wa mali za wananchi watakaolipwa fidia ili kupisha eneo la mradi kwa ajili ya ujenzi ambapo taratibu za kulipa fidia zinaendelea. Aidha, vyeti vya mazingira kutoka NEMC kwa upande wa kituo cha kuzalisha umeme na njia ya kusafirisha umeme vimetolewa na tathmini ya gharama za miundombinu wezeshi zimekamilika ambapo taratibu za kupata fedha za kutekeleza mradi na ujenzi wa miundombinu wezeshi zinaendelea.

Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Maji wa Kakono – MW 87.8

Mheshimiwa Spika, mradi huu unalenga kuongeza uwezo wa uzalishaji wa umeme katika Gridi ya Taifa na upatikanaji wa umeme wa uhakika katika mikoa ya Kanda ya Ziwa. Aidha, mradi utahusisha ujenzi wa bwawa la kuzalisha umeme wa MW 87.8 kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Kagera na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa Kilovoti 220 yenye urefu wa kilomita 38. Hadi kufika Machi, 2024, Serikali ilikuwa inaendelea na tathmini ya mali za wananchi 126 wanaopisha mradi na taratibu za kumpata Mshauri Mwelekezi zinatarajiwa kukamilika Juni, 2024. Aidha, taratibu za kumpata Mkandarasi wa ujenzi zitafuata baada ya kukamilika kwa kazi ya Mshauri Mwelekezi.

(iv) Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Maji wa Kikonge – MW 321

Mheshimiwa Spika,
mradi huu unahusisha ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme wa MW 321 kwa kutumia maporomoko ya maji ya mto Ruhuhu mkoani Ruvuma na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 220 yenye urefu wa kilomita 96 kutoka Kikonge hadi kituo cha kupoza umeme cha Madaba. Serikali inaendelea na taratibu wa kutafuta fedha kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huu pamoja na kukamilisha taarifa muhimu za mradi ikiwemo tathmini ya kina ya Athari za Kijamii na Mazingira (detailed ESIA), uwekaji wa mipaka katika eneo la uzalishaji wa umeme, usanifu wa kina na maandalizi ya nyaraka za zabuni za mradi (bwawa la kuzalisha umeme na njia ya kusafirisha umeme). Aidha, maandalizi ya kufanya tathmini katika eneo la bwawa la uzalishaji umeme yameanza. Vilevile, hatua za awali za kumpata Mshauri Mwelekezi wa kazi za Mazingira zinaendelea.

B.1.5 MIRADI YA KUSAFIRISHA NA KUSAMBAZA UMEME

Miradi ya Kusafirisha na Kusambaza Umeme Iliyopo katika Hatua za Utekelezaji

Mradi wa Kusafirisha Umeme kutoka Julius Nyerere Hydro Power Plant hadi Chalinze – Kilovoti 400 na Kituo cha Kupoza Umeme, Chalinze

Mheshimiwa Spika,
naomba kulitaarifu Bunge lako Tukufu kuwa, ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa Kilovoti 400 yenye urefu wa kilomita 160 kutoka JNHPP hadi Chalinze umekamilika kwa asilimia 99.5 na njia hiyo imeanza kutumika kusafirisha umeme. Aidha, kituo kipya cha kupoza umeme cha Chalinze cha Kilovoti 400/220/132 kimekamilika kwa asilimia 93.1 na kimeanza kutumika kuingiza umeme katika Gridi ya Taifa. Kazi zilizobaki zinatarajiwa kukamilika ifikapo Juni, 2024.

Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa Kilovoti 220 kutoka Geita hadi Nyakanazi

Mheshimiwa Spika, Serikali imekamilisha ujenzi wa miundombinu ya usambazaji umeme katika vijiji 32 vinavyopitiwa na mradi wa kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 220 yenye urefu wa kilomita 144 kutoka Geita hadi Nyakanazi. Aidha, zoezi la uunganishwaji wa wateja linaendelea ambapo wateja 3,046 wameshapata huduma ya umeme kati ya wateja 5,646 na mradi huu unatarajiwa kukamilika ifikapo Juni, 2024.

Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa Kilovoti 400 kutoka Singida – Arusha – Namanga

Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 400 yenye urefu wa kilomita 414 kutoka Singida hadi Namanga kupitia Babati na Arusha ambapo umekamilika kwa asilimia 99.4. Aidha, ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 400 kutoka Arusha hadi Namanga yenye urefu wa kilomita 114.3 umefikia asilimia 97.5 na kituo cha kupoza umeme cha Lemugur kimekamilika kwa asilimia 100 na kuwashwa.

29​

Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa Kilovoti 220 kutoka Rusumo hadi Nyakanazi

Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2023/24 Serikali ilikusudia kukamilisha malipo ya fidia kwa wananchi waliosalia wakati wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 220 yenye urefu wa kilomita 94 kutoka kituo cha kuzalisha umeme cha Rusumo hadi Nyakanazi ambao tayari umekamilika kwa asilimia 100. Hadi kufika Machi 2024, wananchi wote waliosalia walikuwa wamelipwa fidia zao.

Ujenzi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa Kilovoti 400 kutoka Iringa hadi Sumbawanga kupitia Mbeya na Tunduma (TAZA)

Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 400 kutoka Iringa kupitia Mbeya, Tunduma hadi Sumbawanga yenye urefu wa kilomita 620 pamoja na ujenzi wa vituo vya kupoza umeme vya Kisada (Iringa), Iganjo (Mbeya), Tunduma na Sumbawanga. Serikali iliendelea na zoezi la ulipaji wa fidia kwa wananchi watakaopisha mradi ambalo limefikia asilimia 89. Aidha, tayari imesainiwa Mikataba kati ya TANESCO na wakandarasi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme pamoja na vituo viwili vya

30​

kupoza umeme vya Sumbawanga na Tunduma. Vilevile, vituo vya Iringa, Kisada na Mbeya vipo katika hatua za mwisho za kupata idhini ya Benki ya Dunia ya kuendelea na taratibu za kusaini Mikataba. Mradi huu unatarajiwa kukamilika Desemba, 2025 na unalenga pia kuunganisha Gridi ya Taifa na Nchi za Kusini mwa Afrika (Southern African Power Pool – SAPP).

Ujenzi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa Kilovoti 400 kutoka Nyakanazi hadi Kigoma

Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 400 kutoka Nyakanazi hadi Kigoma yenye urefu wa kilomita 280, ujenzi wa kituo cha kupoza umeme Kidahwe Mkoani Kigoma, upanuzi wa kituo cha kupoza umeme cha Nyakanazi pamoja na usambazaji wa umeme katika vijiji 18 vilivyopo katika eneo la mradi. Hadi kufika Machi 2024, utekelezaji wa mradi wa njia ya kusafirisha umeme ulikuwa umefikia asilimia 94.98 na unatarajiwa kukamilika Juni, 2024 kwa mujibu wa Mkataba. Aidha, Mkataba wa ujenzi wa kituo cha kupoza umeme cha Kidahwe na upanuzi wa kituo cha kupoza umeme cha Nyakanazi umesainiwa na utekelezaji unatarajiwa kukamilika Desemba, 2026.

31​

Mheshimiwa Spika, kufuatia kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa njia ya msongo wa Kilovoti 400 kutoka Nyakanazi hadi Kigoma, Serikali imechukua hatua ya dharura ya kufunga transfoma katika kituo cha kupoza umeme cha Kidahwe itakayowezesha kufikisha umeme wa Gridi ya Taifa wa msongo wa Kilovoti 220 katika Mkoa wa Kigoma ifikapo Juni, 2024.

Mradi wa Kuimarisha Gridi ya Taifa (National Grid Stabilization Projects)

– Gridi Imara

Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu uimarishaji wa miundombinu ya umeme katika mikoa mbalimbali ikiwa ni pamoja na ujenzi wa njia za kusafirisha umeme wa msongo wa Kilovoti 220 na 132 na kuongeza uwezo wa nyaya za kusafirisha umeme, ujenzi wa njia za kusambaza umeme msongo wa Kilovoti 33, ujenzi wa vituo vya kupoza umeme na kuongeza uwezo wa baadhi ya vituo pamoja na ujenzi wa vituo vya kupoza umeme katika maeneo ya usambazaji (switching station). Mradi huu unatekelezwa kwa Awamu Tano ambapo Awamu ya Kwanza inahusisha miradi 27.

Mheshimiwa Spika, kwa sasa Serikali inaendelea kutekeleza miradi ya Awamu ya Kwanza kufuatia kusainiwa kwa mikataba baina ya Serikali na Wakandarasi. Aidha, upembuzi yakinifu wa njia

32​

za kusafirisha, kusambaza na vituo vya kupoza umeme umefanyika pamoja na usanifu wa michoro, ununuzi wa vifaa kwa baadhi ya miradi pamoja na kuanza kazi za awali za ujenzi. Vilevile, utambuzi wa miradi ya Awamu ya Pili umefanyika na hatua za awali za utekelezaji zimeanza. Kiambatisho Na.2 ni hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Gridi Imara. Kutokana na umuhimu wa miradi hii katika kuondoa changamoto za upatikanaji wa umeme wa uhakika nchini, Serikali itaendelea kuhakikisha fedha zinazotengwa kila mwaka zinapatikana.

Mradi wa Ukarabati na Uboreshaji wa Gridi ya Taifa (Grid Rehabilitation and Upgrading) TTGRUP

Mheshimiwa Spika, mradi huu unalenga kuimarisha Gridi ya Taifa kwa kukarabati na kuboresha vituo nane (8) vya kupoza umeme, kurefusha Mkongo wa Mawasiliano (Optic Fiber) na kuboresha miundombinu ya mawasiliano kwa kuondoa earth wire na kuweka optical ground wire pamoja na kuimarisha mfumo wa uendeshaji na udhibiti wa Gridi ya Taifa. Mradi huu unafadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) pamoja na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hadi kufikia Machi, 2024, utekelezaji wa mradi wa ukarabati na uboreshaji wa vituo nane (8) ulikuwa umefikia asilimia 21.0; uboreshaji wa miundombinu ya

33​

mawasiliano kwa ujumla umefikia asilimia 70.0 na kazi za kuimarisha mfumo wa uendeshaji na udhibiti wa Gridi ya Taifa kwa ujumla umefikia asilimia 23.4. Mradi unatarajiwa kukamilika Desemba, 2024.

Ujenzi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa Kilovoti 220 kutoka Benaco hadi Kyaka

Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa Kilovoti 220 kutoka Benaco hadi Kyaka yenye urefu wa kilomita 166.2 itakayounganisha Mkoa wa Kagera katika Grid ya Taifa. Serikali kupitia TANESCO imekamilisha uthamini wa mali za wananchi wanaopisha mradi na kazi zinazoendelea ni pamoja na taratibu za kufanya malipo ya fidia na majadiliano na Mshauri Mwelekezi aliyekidhi vigezo ili kusaini mkataba Aprili, 2024. Mradi unatarajiwa kukamilika Desemba, 2026.

Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa Kilovoti 220 kutoka Morogoro hadi Dodoma kwa Ajili ya Uendeshaji wa Treni ya Umeme (SGR Lot II)

Mheshimiwa Spika, Serikali iliendelea kutekeleza mradi huu ambapo tayari umekamilika kwa asilimia 99 na majaribio ya kupitisha umeme

34​

kutoka Msamvu, Morogoro hadi Zuzu, Dodoma yamefanyika kwa mafanikio.

Mradi wa Njia ya Kusafirishi Umeme Msongo wa Kilovoti 220 kutoka Mwanza hadi Isaka kwa Ajili ya Uendeshaji wa Treni ya Umeme (SGR Lot V)

Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 220 yenye urefu wa kilomita 230 kutoka Mwanza hadi Isaka kwa ajili ya uendeshaji wa treni ya umeme. Serikali kupitia TANESCO imekamilisha tathmini ya mali za wananchi watakaopisha mradi na taratibu za malipo ya fidia zinaendelea. Aidha, taratibu za kumpata Mkandarasi Mjenzi zimekamilika na ameanza kufanya kazi za awali za utafiti wa udongo na njia ya kusafirisha umeme. Mradi huu unatarajiwa kukamilika Mei, 2025.

Ujenzi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa Kilovoti 400 kutoka Chalinze - Kinyerezi - Mkuranga (NEG Phase 1)

Mheshimiwa Spika, mradi huu inahusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 400 kutoka Chalinze, Kinyerezi hadi Mkuranga yenye urefu wa kilomita 135 na vituo vya kupoza umeme vya Chalinze, Kinyerezi, Mkuranga na Morogoro. Hadi kufikia Machi 2024, Serikali ilikuwa imekamilisha ununuzi wa Mkandarasi

35​

Mjenzi wa njia ya kusafirisha umeme ambaye anaendelea na utekelezaji wa mradi. Mradi unatarajiwa kukamilika Aprili, 2026.

Ujenzi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa Kilovoti 400 kutoka Chalinze – Dodoma (NEG Phase 2)

Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa mradi huu unahusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 400 kutoka Chalinze hadi Dodoma yenye urefu wa kilomita 345 na upanuzi wa kituo cha kupoza umeme cha Dodoma. Mradi huu utawezesha kusafirisha umeme unaotoka JNHPP kupitia Chalinze kwenda Dodoma na kuusambaza katika Mikoa mbalimbali nchini (power evacuation). Hadi kufikia Machi, 2024, Serikali ilikuwa imekamilisha ulipaji wa fidia kwa wananchi 2,760 kati ya 2,860 wanaopisha mradi sawa na asilimia 92 na taratibu za ulipaji wa fidia zinaendelea. Aidha, Mkandarasi anaendelea na utekelezaji wa mradi na unatarajia kukamilika Desemba, 2025.

Ujenzi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa Kilovoti 400 kutoka Chalinze – Segera na Msongo wa Kilovoti 220 Segera – Tanga

Mheshimiwa Spika, mradi huu unalenga ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 400 kutoka Chalinze – Segera na Msongo

36​

wa Kilovoti 220 kutoka Segera - Tanga na vituo cha kupoza umeme vyenye uwezo wa MVA 800 Segera na Tanga. Kwa sasa Serikali inaendelea na taratibu za kutafuta fedha za utekelezaji wa mradi huu ambao kukamilika kwake kutawezesha kusafirisha umeme kutoka Chalinze kwenda Tanga. Aidha, Serikali imekamilisha kazi ya Upembuzi Yakinifu na inaendelea na taratibu za kutathmini mali za wananchi watakaopisha mradi ili waweze kulipwa fidia.

Mradi wa Kuboresha Utendaji Kazi wa TANESCO (Corporate Management System – CMS)

Mhesimiwa Spika, mradi huu unalenga kuboresha hali ya utendaji kazi wa TANESCO kwa kuweka mifumo itakayowezesha kuongeza tija na ufanisi katika utendaji kazi. Mradi huu unatekelezwa sambamba na mradi wa kusafirisha umeme wa Tanzania – Zambia Interconnector Transmission Project (TAZA) kwa gharama ya Dola za Marekani milioni 34.8 sawa na Shilingi bilioni 81.6.

Mhesimiwa Spika, Serikali kupitia TANESCO inaendelea na utekelezaji wa kazi za ufungaji wa vifaa vya miundombinu ya mradi (data center infrastructure) na kufanyiwa majaribio utendaji wake. Aidha, usimikaji wa mfumo wa taarifa za kijiografia za miundombinu ya umeme na wateja

37​

(GIS) umekamilika pamoja na mafunzo kwa wataalam. Vilevile, miundombinu ya mawasiliano ya mradi (network infrastructure) imekamilika kwa asilimia 80 na hatua ya kwanza ya utengenezaji wa mfumo imefikia asilimia 85 ambapo hatua ya pili ya mradi imefikia asilimia 43. Pia, yamefanyika mafunzo ya matumizi ya mfumo kwa Mameneja na Timu Maalumu (Champions Team) na yanaendelea kwa wafanyakazi wote. Kwa ujumla mradi umetekelezwa kwa asilimia 61 na unatarajiwa kukamilika Agosti, 2024.

Miradi ya Kusafirisha na Kusambaza Umeme Iliyopo Katika Hatua ya Utayarishaji

Ujenzi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa Kilovoti 400 kutoka Segera- Same- Arusha (Lemugur)

Mheshimiwa Spika,
mradi huu unalenga ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 400 kutoka Segera hadi Arusha kupitia Same, kituo cha kupoza umeme cha Same na upanuzi wa vituo vya kupoza umeme vya Segera na Lemugur. Kazi za Upembuzi Yakinifu na Tathmini ya Mazingira na Kijamii zinaendelea na zinatarajika kukamilika Agosti, 2024.

38​

Ujenzi wa Kituo cha Kupoza Umeme cha Ibadakuli, Shinyanga 2x315 MVA

Mhesimiwa Spika, mradi huu unahusisha kujenga kituo kipya chenye uwezo wa Kilovoti 400/220 na kusimika transfoma kubwa mbili zenye ukubwa wa MVA 315 kila moja katika eneo la Ibadakuli mkoani Shinyanga ili kuimarisha upatikanaji wa umeme wa uhakika katika mikoa ya kanda ya Ziwa na maeneo jirani kwa lengo la kuchochea shughuli za kiuchumi, hususan uchimbaji wa madini, usafirishaji kwa kutumia (SGR) na mradi wa Bomba la Mafuta kutoa Uganda hadi Tanga (EACOP). Kwa sasa Mkandarasi anaendelea na usanifu wa kituo.

Ujenzi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa Kilovoti 220 kutoka Makutopora hadi Tabora kwa ajili Uendeshaji wa Treni ya Umeme (SGR Lot 3)

Mhesimiwa Spika, mradi huu unahusu ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 220 yenye urefu wa kilomita 347 kutoka Makutopora hadi Tabora kwa ajili ya uendeshaji wa treni ya umeme (SGR). Gharama za mradi huu zinakadiriwa kuwa Shilingi bilioni 212.58. Hadi kufikia Machi 2024, kazi zilizokuwa zinatekelezwa ni pamoja na Upembuzi Yakinifu ambao umefikia asilimia 25 na taratibu za kumpata Mshauri Mwelekezi wa kufanya usanifu wa kina wa mradi.

39​

Aidha, tathmini ya mali za wananchi watakaopisha mradi zitaanza baada ya kukamilisha Upembuzi Yakinifu.

Ujenzi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa Kilovoti 220 kutoka Tabora hadi Isaka kwa ajili ya Uendeshaji wa Treni ya Umeme (SGR Lot 4)

Mhesimiwa Spika, mradi huu unahusu ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 220 yenye urefu unaokadiriwa kuwa kilomita 195 kutoka Tabora hadi Isaka kwa ajili ya uendeshaji wa treni ya umeme. Gharama za mradi huu zinakadiriwa kuwa Shilingi bilioni 131.66. Hadi kufikia Machi 2024, kazi zilizokuwa zinatekelezwa ni pamoja na Upembuzi Yakinifu ambao umefikia asilimia 12.5 na taratibu za kumpata Mshauri Mwelekezi wa kufanya usanifu wa kina wa mradi. Aidha, tathmini ya mali za wananchi watakaopisha mradi zitaanza baada ya kukamilisha Upembuzi Yakinifu.

Ujenzi wa njia ya Kusafirisha Umeme (Submarine Cable) Msongo wa Kilovoti 220 kutoka Tanzania Bara (Ununio) Hadi Zanzibar (Unguja)

Mhesimiwa Spika, mradi huu unahusu ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 220 kwenda Zanzibar kwa ajili ya

40​

kuimarisha upatikanaji wa umeme Zanzibar. Kukamilika kwa mradi huu kutatatua changamoto ya kuzidiwa kwa miundombinu ya kusafirisha umeme kwenda Zanzibar iliyopo kwa sasa. Kazi zinazoendelea kwa sasa ni kukamilisha taratibu za ununuzi wa Mshauri Mwelekezi atakayefanya Upembuzi Yakinifu wa mradi ambazo zinatarajiwa kukamilika Juni, 2024. Taratibu za utafutaji wa fedha za kutekeleza mradi huu zinaendelea ambapo AfDB imeonyesha nia ya kushirikiana na Serikali katika utekelezaji wa mradi huu.

Ujenzi wa Njia ya Kusafirisha Umeme (Submarine Cable) Msongo wa Kilovoti 132 kutoka Tanzania Bara (Tanga) Hadi Zanzibar (Pemba)

Mhesimiwa Spika, mradi huu unahusu ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 132 kutoka Tanga kwenda Pemba ili kuimarisha upatikanaji wa umeme Pemba. Kukamilika kwa mradi huu kutatatua changamoto ya kuzidiwa kwa miundombinu ya kusafirisha umeme kwenda Pemba iliyopo kwa sasa. Kazi zinazoendelea kwa sasa ni kukamilisha taratibu za ununuzi wa Mshauri Mwelekezi atakayefanya Upembuzi Yakinifu wa mradi. Taratibu za utafutaji wa fedha za kutekeleza mradi huu zinaendelea ambapo AfDB ameonesha nia ya kushirikiana na Serikali katika utekelezaji wa mradi huu.

41​

Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Kupoza Umeme cha Manyoni (Manyoni Substation - MVA 2x30, 220/33kV)

Mhesimiwa Spika, mradi huu unalenga ujenzi wa kituo cha kupoza umeme chenye uwezo wa MVA 60 katika Kata ya Mkwese, Wilaya ya Manyoni, Mkoa wa Singida na unatarajiwa kugharimu Shilingi bilioni 38.05. Hadi kufikia Machi 2024, Tathmini ya Athari kwa Mazingira na Jamii ilikuwa imekamilika na kuwasilishwa NEMC kwa ajili ya kupata cheti cha mazingira. Aidha, tathmini ya mali za wananchi watakaopisha mradi inaendelea ambapo inatarajiwa kukamilika Juni, 2024. Serikali inaendelea na taratibu za utafutaji wa fedha za kutekeleza mradi huu.

Mradi wa Kusafirisha Umeme Msongo wa Kilovoti 400 kutoka Tanzania hadi Uganda (Masaka - Ibadakuli)

Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 400 yenye urefu wa kilomita 617 kutoka Ibadakuli – Nyakanazi – Kyaka hadi Masaka Uganda pamoja na ujenzi wa kituo cha kupoza umeme cha Kyaka. Upembuzi Yakinifu umekamilika na kazi zinazoendelea ni kufanya Tathmini ya Athari za Mazingira pamoja na tathmini ya wananchi watakaopisha mradi.

42​

Taratibu za upatikanaji wa fedha za utekelezaji wa mradi zinaendelea.

Ujenzi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa Kilovoti 220 kutoka Chalinze – Bagamoyo

Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa mradi huu unahusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 220 kutoka Chalinze - Bagamoyo yenye urefu wa kilomita 90 na kituo cha kupoza umeme cha Bagamoyo. Hadi kufikia Machi, 2024 Upembuzi Yakinifu wa mradi ulikuwa umekamilika na kazi zinazoendelea ni pamoja na kufanya tathmini ya mali za wananchi watakaopisha mradi na kutafuta fedha za utekelezaji wa mradi huu.

Ujenzi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa Kilovoti 400 kutoka Sumbawanga hadi Kigoma Kupitia Mpanda (Km 480) na Kituo cha Kupoza Umeme Mpanda

Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 400 kutoka Sumbawanga hadi Kigoma kupitia Mpanda yenye urefu wa kilomita 480. Gharama za mradi huu zinakadiriwa kuwa Dola za Marekani milioni 200.4 sawa na Shilingi bilioni

43​

512.02 kwa upande wa njia ya kusafirisha umeme na Dola za Marekani milioni 50 kwa ajili ya kituo cha kupoza umeme. Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Exim Benki ya Korea zimeonesha nia ya kufadhili mradi huu. Hadi kufikia Machi 2024, Serikali kupitia TANESCO ilikuwa imekamilisha uhuishaji wa Upembuzi Yakinifu na usanifu wa mradi wa awali na inaendelea na taratibu za kutafuta fedha za kutekeleza mradi.

Utekelezaji wa Miradi Mingine na Matengenezo ya Mitambo

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia TANESCO imeendelea kufanya ukaguzi wa miundombinu ya umeme pamoja na kuifanyia matengenezo. Mitambo ya kuzalisha umeme iliyofanyiwa matengenezo kinga makubwa na madogo ni pamoja na kituo cha Tegeta, Kituo cha Kinyerezi II, Kituo cha Ubungo I na Kituo cha Mtera. Matengenezo hayo yaliimarisha uzalishaji wa umeme kwa wastani wa MW 115 kwenye Gridi ya Taifa ambao ulikuwa hauzalishwi kutokana na ubovu wa mitambo. Kiambatisho Na. 3 ni mitambo iliyofanyiwa matengenezo makubwa na madogo.

Mheshimiwa Spika, ili kuongeza uwezo wa miundombinu ya usafirishaji na kupunguza upotevu wa umeme, TANESCO inafanya maboresho kwenye njia mbalimbali za kusafirisha umeme

44​

ikiwemo njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa Kilovoti 132 yenye urefu wa kilomita 97 kutoka Ubungo hadi Chalinze. Kwa sasa njia hiyo ina uwezo wa kusafirisha kiasi cha MW 150, ikilinganishwa na kiasi cha MW 94 kilichokuwa kinasafirishwa awali hivyo kufanya uwezo wa kusafirisha umeme kuongezeka kwa asilimia 78. Aidha, Shirika linabadilisha miundombinu ya msongo wa Kilovoti 11 na kuwa msongo wa Kilovoti 33, pamoja na kuongeza transfoma kwenye maeneo mbalimbali. Kazi ya ukarabati ni endelevu na inaendelea katika mkoa wa Tanga kwa kuboresha njia ya kilomita 172 ya kusafirisha umeme ya msongo wa Kilovoti 132 kutoka Chalinze mpaka Hale.

Mheshimiwa Spika, jitihada nyingine zinazofanyika ili kuimarisha miundombinu ya usafirishaji umeme nchini ni kufanya ukaguzi wa kina ili kubaini maeneo yenye changamoto na kuyafanyia ukarabati. Ukarabati huo unahusisha ubadilishaji wa nyaya chakavu, vikombe vilivyopasuka, vyuma vilivyoibiwa, kuondoa nguzo za miti na kuweka nguzo za zege pamoja na ukarabati wa sehemu zilizoathiriwa na mmomonyoko wa udongo na kusafisha njia tengefu.

Mheshimiwa Spika, kuhusu uboreshaji wa mifumo ya uendeshaji wa Gridi, Serikali kupitia TANESCO ipo katika hatua za mwisho za

45​

kukamilisha mradi wa uboreshaji na kuongeza uwezo wa mitambo ya kuongoza/kuendesha Gridi ya umeme (SCADA/EMS). Mradi huu, wenye lengo la kuongeza ufanisi wa uendeshaji wa gridi kupitia teknolojia ya kidijitali unatarajiwa kukamilika Juni, 2025.

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia TANESCO imefanikiwa kuweka mifumo ya kisasa ya mawasiliano katika vituo tisa (9) vya kupoza umeme ili viendeshwe kidijitali (unmanned substations). Hadi sasa kituo kimoja cha Buzwagi kimekamilika na vituo nane (8) vilivyobaki vinatarajiwa kukamilika Desemba 2024. Vituo hivyo ni New City Centre (Posta), Kurasini, Dege, Mbagala na Gongo la Mboto vilivyopo mkoani Dar es Salaam pamoja na vituo vya Musoma, Geita na Bulyanhulu ambavyo vipo katika majaribio ya kuendeshwa kidijitali. Jitihada za kuweka mifumo ya kidijitali kwenye vituo vingine zinaendelea.

Mheshimiwa Spika, jitihada za maboresho zinafanyika pia katika mifumo ya kisasa ya usambazaji umeme (distribution network automation), ikiwa ni pamoja na kubadilisha mita za wateja wakubwa T2 na T3 kwa kufunga mita zenye ufanisi. Zoezi hili limeanza kwa mkoa wa Dar es Salaam na maeneo mengine yatafuatia. Aidha, TANESCO inakamilisha taratibu za ununuzi wa mfumo wa mita janja (smart meters)

46​

zitakazomuwezesha mteja wa kawaida kununua umeme na kisha mita hiyo kupokea moja kwa moja umeme badala na mfumo wa sasa.

B.1.6 UTENDAJI WA KAMPUNI TANZU ZA TANESCO

Kampuni ya Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Usafirishaji na Usambazaji Umeme (ETDCO)

Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2023/24 ETDCO iliendelea na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya usafirishaji wa umeme. Miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 132 wenye urefu wa kilomita 383 kutoka Tabora hadi Katavi kupitia Sikonge, Ipole na Inyonga unaotarajiwa kukamilika ifikapo Juni, 2024; na mradi wa kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 132 kutoka Tabora hadi Urambo na kutoka Urambo hadi Kidahwe Mkoani Kigoma. Aidha, ETDCO ilikamilisha kwa asilimia 99 ujenzi wa njia nne za kusafirisha umeme msongo wa kilovoti 33 kutoka kituo cha kupoza umeme cha Mpomvu (Geita) hadi kituo cha kupoza umeme cha Mgodi wa Geita Gold Mine ili kuunganisha mgodi na umeme wa Gridi ya Taifa.

47​

Mheshimiwa Spika, ETDCO iliendelea na utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini katika Mikoa ya Geita na Kigoma kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ambapo hadi kufikia Machi, 2024 ilikuwa imekamilika kwa asilimia 40 kwa upande wa Mkoa wa Geita na asilimia 20 kwa upande wa mkoa wa Kigoma. Kazi zilizofanyika ni pamoja na ufungaji wa transfoma 20 kati ya 45 na kuwasha mitaa 20 kati ya 45 kwa upande wa mkoa wa Geita; na kufunga transfoma 6 kati ya 59 na kuwasha umeme mitaa sita kati ya 59 katika mkoa wa Kigoma. Miradi hii kwa ujumla wake inatarajia kukamilika mwishoni mwa Desemba, 2024.

Mheshimiwa Spika, kampuni ya ETDCO iliendelea pia na utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini katika mikoa ya Katavi (REA III, Round II) ambao umekamilika kwa asilimia 96, Mbeya (REA III, Round II) ambao umekamilika kwa asilimia 92, Kigoma (REA III, Round I) ambao umekamilika kwa asilimia 99 na Arusha (REA III, Round I) ambao umekamilika kwa asilimia 100. Pia kampuni hiyo ilianza utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa njia za kusambazia umeme katika nyumba zinazojengwa Msomera wilayani Handeni kwa ajili ya familia zinazohama kutoka Hifadhi ya Ngorongoro ambapo mradi huo pia utahusisha nyumba zitakazojengwa Saunyi wilayani Kilindi na Kitwai B wilayani Simanjiro. Pamoja na hayo, Serikali inaendelea kusimamia kwa karibu utendaji wa Kampuni hii

48​

ikiwemo kuimarisha uongozi wa kampuni ili iweze kufikia malengo ya kuanzishwa kwake.

Kampuni ya Kuzalisha Nguzo za Umeme za Zege Tanzania (TCPM)

Mheshimiwa Spika, ikiwa ni hatua ya kuhakikisha uzalishaji wa nguzo za zege unaimarika nchini, Serikali kupitia TCPM ilianza taratibu za ununuzi wa Mkandarasi wa ujenzi wa kiwanda cha kwanza cha kuzalisha nguzo za zege Mkoani Tabora. Aidha, kazi za ujenzi wa kiwanda zinatarajiwa kuanza Mei, 2024. Vilevile, taratibu za kupata fedha kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha pili Mkoani Mbeya zinaendelea.

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia TCPM itashirikiana na Wawekezaji binafsi walioonyesha nia ya kushirikiana kwa mfumo wa ushirikiano wa joint venture katika uzalishaji wa nguzo za zege. Hadi kufikia Machi, 2024 mazungumzo ya awali yamefanyika na Wawekezaji 17 waliowasilisha maombi ya kushirikiana na TCPM. Aidha, uchambuzi wa taarifa za mapendekezo ya kifedha na kiufundi unaendelea ili kupata wawekezaji wenye uwezo wa kushirikiana nao.

Mheshimiwa Spika, TCPM ilisanifu, kusimamia uzalishaji na kusambaza nguzo za zege 1,482 za mita 17 kwa Kampuni ya ETDCO kwa ajili

49​

ya mradi wa kusafirisha umeme wa msongo wa Kilovoti 132 kutoka Mkoa wa Tabora kwenda Mkoa wa Katavi na Wilaya ya Urambo. TCPM pia ilisambaza nguzo 940 za saizi tofauti kwa ETDCO kwa ajili ya miradi mbalimbali. Aidha, kampuni hii ilisambaza nguzo 4,479 za saizi tofauti kwa mikoa mbalimbali ya TANESCO kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa njia za kusambaza umeme.

Kampuni ya Uendelezaji wa Rasilimali ya Jotoardhi (TGDC)

Mheshimiwa Spika, ili kuimarisha upatikanaji wa umeme nchini kupitia vyanzo mbalimbali, Serikali iliendelea kutekeleza miradi ya kuzalisha umeme kupitia jotoardhi, ambapo kipaumbele kilielekezwa katika miradi mitano (5) ya Ngozi (MW

na Kiejo-Mbaka (MW 60) iliyopo mkoani Mbeya, Songwe (MW 5) mkoani Songwe, Luhoi (MW 5) mkoani Pwani na Natron (MW 60) mkoani Arusha.

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia TGDC inaendelea na taratibu za kuwapata Wakandarasi wa kuchoronga visima vya uhakiki (drilling contractor), tathmini ya visima (well testing services) na ununuzi wa bidhaa/malighafi za uchorongaji wa visima vya uhakiki vya jotoardhi Ngozi na shughuli za uchorongaji wa visima hivyo zinatarajiwa kuanza Juni, 2024. Aidha, mradi wa Ngozi utatekelezwa kwa awamu mbili ambapo

50​

awamu ya kwanza inatarajiwa kuanza na uzalishaji wa MW 30 na inatarajiwa kugharimu Dola za Marekani milioni 144 sawa na takribani Shilingi bilioni 367.9. Kiambatisho Na. 4 ni mtambo wa uchorongaji ukiwa umesimikwa kwa ajili ya uhakiki wa jotoardhi katika eneo la mradi wa jotoardhi wa Ngozi.

Mheshimiwa Spika, kazi nyingine zilizotekelezwa katika miradi ya jotoardhi ni pamoja na:

Kuendelea na taratibu za kuajiri Mshauri Mwelekezi (drilling consultant) kwa ajili ya kusanifu na kusimamia uchorongaji (drilling program) wa visima vya uhakiki vya jotoardhi katika Mradi wa Kiejo–Mbaka pamoja na tathmini ya ardhi na ulipaji fidia kwa wananchi wanaopisha utekelezaji wa mradi. Aidha, maandalizi ya kupata mtambo mdogo wa kuzalisha umeme (well head generator) yanaendelea. Mradi huu utatekelezwa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza inatarajiwa kuanza na MW 10. Gharama za mradi huu ni Dola za Marekani milioni 75 sawa na takribani Shilingi bilioni 191.6;

Taratibu za upatikanaji wa ardhi kwa ajili ya uchorongaji wa visima vya uhakiki vya jotoardhi na kujenga uelewa kwa wananchi na wadau mbalimbali kuhusu manufaa ya

51​

mradi kupitia warsha mbalimbali zimekamilika katika mradi wa Songwe. Maandalizi ya uchoronganji wa visima vya uhakiki katika eneo la mradi yanaendelea. Gharama za kutekeleza mradi huu ni Dola za Marekani milioni 32 sawa na takribani Shilingi bilioni 81.8;

Maandalizi ya uchorongaji wa visima vinne (4) vya uhakiki vya jotoardhi pamoja na kufanya upembuzi yakinikifu wa matumizi mengineyo unaendelea katika mradi wa Luhoi. Gharama za kutekeleza mradi huu ni Dola za Marekani milioni 32 sawa na takribani Shilingi bilioni 81.8; na

Kuendelea na taratibu za kuajiri Mshauri Mwelekezi kwa ajili ya kufanya utafiti wa kina (detailed geoscientific surface exploration) Aprili, 2024 ili kuanza utafiti wa kina wa kijiosayansi katika mradi wa Natron MW 60. Gharama za kutekeleza mradi huu ni Dola za Marekani milioni 288 sawa na takribani Shilingi bilioni 735.8.

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia TGDC ilikamilisha taratibu za kukidhi vigezo vya kupata ruzuku kutoka kwa Washirika wa Maendeleo, ikiwemo mfuko wa Geothermal Risks Mitigation Facility (GRMF) unaoratibiwa na Kamisheni ya

52​

Umoja wa Afrika kwa ajili ya kupata fedha za kuendeleza vyanzo hivyo. Vilevile, Mfuko wa Climate Action Africa kupitia Serikali ya Canada umeridhia kutoa msaada wa kiufundi (Technical Assistance) kwa ajili ya kufanya utafiti wa kina wa kijiosayansi katika eneo la mradi wa Meru Mkoani Arusha na mfuko wa GRMF HEAT umeridhia kutoa Dola za Marekani milioni 1.6 kwa ajili ya utafiti wa kina wa kijiosayansi kwa mradi wa jotoardhi Manyara mkoani Manyara. Jitihada nyingine zinazoendelea ni pamoja na kutoa elimu kwa wananchi na wadau mbalimbali kuhusu manufaa ya miradi ya jotoardhi.

Mheshimiwa Spika, ikiwa ni hatua ya kuhamasiaha uwekezaji na matumizi ya rasilimali za jotoardhi, Tanzania itakuwa mwenyeji wa Kongamano la 10 la Jotoardhi (African Rift Geothermal Conference-ARGeo C10) litakalofanyika Novemba, 2024 Jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo litahusisha Nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki zilizopitiwa na bonde la ufa.

B.1.7 UZALISHAJI WA UMEME KUPITIA SEKTA BINAFSI

Mheshimwa Spika,
Serikali kupitia TANESCO inanunua umeme kutoka kwa wazalishaji wadogo wa umeme ambao wanasaidia kuongeza upatikanaji wa umeme nchini. Wazalishaji hao

53​

wanachangia jumla ya MW 31.8 ambapo MW 26.8 zimeingizwa katika Gridi ya Taifa na MW 5.00 nje ya Gridi ya Taifa. Changamoto wanazokutana nazo wazalishaji hao ni pamoja na upungufu wa malighafi za kuzalisha umeme ikiwemo maji, magome ya miti na mabaki ya miwa kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi na hivyo kuathiri uzalishaji wao. Kiambatisho Na. 5 ni Wazalishaji Wadogo wa Umeme (SPPs) waliosajiliwa.

Mheshimwa Spika, Serikali imeingia mikataba na wawekezaji 20 ambao bado wapo katika hatua ya ujenzi wa miundombinu ya uzalishaji wa umeme ambao kwa ujumla wataongeza uwezo wa uzalishaji wa umeme kiasi cha MW 86.31.

B.1.8 MIRADI YA NISHATI VIJIJINI

Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili (REA III Round II)

Mheshimiwa Spika,
Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini iliendelea kutekeleza Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili unaolenga kukamilisha kupeleka umeme kwenye vijiji 4,071 vilivyobaki kati ya vijiji vyote 12,318. Hadi kufikia Machi 2024, jumla ya vijiji 11,837 sawa na asilimia 96.37 ya

54​

vijiji vyote Tanzania Bara vilikuwa vimepelekewa umeme. Aidha, REA imejenga njia za umeme za Msongo wa Kati zenye urefu wa kilomita 22,578 kati ya kilometa 23,619 sawa na asilimia 95.6 pamoja na njia za umeme wa Msongo Mdogo zenye urefu wa kilomita 8,214 kati ya kilometa 12,159 sawa na asilimia 67. Vilevile, transfoma 3,686 kati ya 4,071 sawa na asilimia 90.54 zimefungwa hivyo kuunganisha wateja 54,626. Kutokana na hatua zinazochukuliwa za kupeleka umeme vijijini, jumla ya taasisi 63,509 zinazotoa huduma kwa ajamii ikiwa ni pamoja na za Elimu, Biashara, Pampu za Maji, Vituo vya Afya na Nyumba za Ibada zilikuwa zimeunganishiwa umeme kama inavyoonekana katika Kiambatisho Na.6 ikilinganishwa na taasisi 43,925 za Aprili, 2023.

Mradi wa Kusambaza Umeme katika Vitongoji – (Hamlet Electrification Project – HEP)

Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2023/24 Serikali iliendelea kutekeleza azma ya kuhakikisha vitongoji vyote nchini vinapatiwa huduma ya umeme ili kuharakisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii vitongojini. Hadi kufikia Machi, 2024 Wakandarasi wa kutekeleza miradi ya kuunganisha umeme katika vitongoji 667 katika Mikoa ya Songwe na Kigoma walikuwa wanaendelea na kazi ya ujenzi wa miundombinu ya umeme katika

55​

vitongoji hivyo. Mradi huu unatarajiwa kukamilika Juni, 2025. Aidha, REA ipo katika hatua za ununuzi wa wakandarasi wa kutekeleza Mradi wa Kupeleka Umeme katika Vitongoji 15 kwa kila Jimbo.

c) Mradi wa Ujazilizi Mzunguko wa Pili B

Mheshimiwa Spika,
mradi huu unalenga kuongeza wigo wa usambazaji umeme kwenye vitongoji ambavyo vimepitiwa na njia ya kusafirisha umeme ya Msongo wa Kati katika mikoa tisa (9) ya Arusha, Geita, Kagera, Katavi, Kigoma, Lindi, Morogoro, Njombe na Songwe. Hadi kufikia Machi 2024, jumla ya kilomita 103 za umeme wa Msongo Mdogo zimejengwa na nguzo kilomita 1,458 zimesimikwa kati ya 3,860. Mradi huu unatarajiwa kukamilika Novemba, 2025.

Mradi wa Ujenzi wa Gridi Ndogo (Mini Grids) katika Maeneo ya Visiwa na Maeneo Yaliyo Mbali na Gridi ya Taifa

Mheshimiwa Spika, mradi unahusisha kupeleka umeme katika visiwa kwa kutumia gridi ndogo zinazozalisha umeme kwa kutumia nishati ya jua kwenye maeneo ya visiwa ambavyo havijafikiwa na Gridi ya Taifa. Hadi kufikia Machi, 2024 kazi zilizotekelezwa ni kuchambua maombi yaliyowasilishwa, kusaini mikataba miwili (2) kati ya saba (7) na kuanza kutekeleza mradi ambapo

56​

wateja 1,403 wameunganishiwa umeme kati ya 14,168 katika vijiji 34 kati ya 85.

Mradi wa Kuwezesha Ujenzi wa Vituo Vidogo vya Kuuzia Bidhaa za Petroli Vijijini kwa Njia ya Mikopo

Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu kusogeza huduma ya bidhaa ya mafuta ya petroli kwa wananchi wanaoishi vijijini kwa kutoa mikopo kwa waendelezaji wa vituo vya mafuta ili waweze kuwekeza katika maeneo ya vijijini. Tayari zoezi la kuwapata waendelezaji wa vituo hivyo vijijini limefanyika kupitia Wakala wa Nishati Vijijini ambapo maombi ya waendelezaji 10 yaliyokidhi vigezo vya kiufundi yamewasilishwa Benki ili kufanyiwa tathmini ya kifedha. Kufuatia uzoefu uliopatikana katika maombi yaliyowasilishwa wakati fursa hii ilipotangazwa awali, vigezo na masharti ya utolewaji wa mikopo hiyo vimepitiwa upya na kuboreshwa ili kuwawezesha waombaji wengi kunufaika na fursa hiyo na hivyo kuimarisha ujenzi wa vituo hivyo vijijini. Aidha, tarehe 25 Machi 2024, Wakala ulitangaza Awamu ya Pili ya fursa za upatikanaji wa mikopo hiyo ambapo kwa sasa hakuna ukomo wa uwasilishwaji wa maombi. Kupitia utaratibu huu, kwa maombi yatakayobainika kutokidhi vigezo, waombaji husika watakuwa na nafasi ya kufanya marekebisho ya maombi yao katika maeneo yenye upungufu na kuyawasilisha tena.

57​

Programu ya Kuwezesha Waendelezaji wa Miradi Midogo ya Nishati Jadidifu Vijijini chini ya Utaratibu wa Kusaidia Uandaaji wa Miradi (PPSF)

Mheshimiwa Spika,
Mradi huu unahusu kuwawezesha waendelezaji miradi ya nishati jadidifu vijijini ambao wana upungufu wa mitaji ili waweze kuandaa maandiko ya miradi ikiwemo Mpango wa Biashara. Hadi kufikia Machi, 2024 kazi zilizotekelezwa ni pamoja na kusaini mikataba miwili (2) iliyopatikana katika Call for Proposal Awamu ya Kwanza na kuendelea na uchunguzi wa kina kwa waendelezaji waliokidhi vigezo baada ya tathmini iliyofanyika (due diligence). Aidha, Wakala unaendelea kuandaa kabrasha kwa ajili ya kutangaza fursa hizo kwa Awamu ya Nne.

Mpango wa Uendelezaji Miradi ya Nishati Jadidifu Inayofua Umeme kwa Kutumia Maporomoko ya Maji

Mheshimiwa Spika, Mpango huu unahusisha Serikali kutoa ruzuku kwa Waendelezaji wa miundombinu ya miradi midogo ya kuzalisha umeme kwa kutumia maporomoko ya maji vijijini ili wapate motisha ya kuiendeleza. Hadi kufikia Machi, 2024 Serikali kupitia REA iliendelea kutoa ruzuku kwa waendelezaji wa Miradi midogo ya kufua umeme kwa kutumia nguvu ya maji. Jumla ya miradi minne (4) imepata ruzuku ikijumuisha Ijangala (kW

58​

uliopo Makete – Shilingi milioni 426; Lupali (kW 317) uliopo Ludewa Shilingi bilioni 2.9; Lugarawa (kW 1,700) uliopo Njombe Shilingi milioni 495 na Kilolo/Maguta (kW 2,400) uliopo Kilolo Iringa Shilingi milioni 969.9. Aidha, ujenzi wa Mradi wa Ijangala umekamilika na kuzinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango Oktoba 2023. Pia, utekelezaji wa Mradi wa Lupali umefikia asilimia 90; Mradi wa Lugarawa asilimia 75; na Mradi wa Kilolo umefikia asilimia 92.

B.1.9 UTEKELEZAJI WA MIKAKATI NA MIPANGO MBALIMBALI YA UENDELEZAJI WA SEKTA NDOGO YA UMEME NA NISHATI JADIDIFU

Mheshimiwa Spika,
Serikali kupitia Wizara ya Nishati imeendelea kuandaa na kutekeleza Mipango na Mikakati mbalimbali ya kuendeleza Sekta ya Nishati kama ifuatavyo:

Uhuishaji wa Mpango Kabambe wa Kuendeleza Sekta Ndogo ya Umeme wa Mwaka 2020 (Power System Master Plan Update 2020)

Mheshimiwa Spika, ikiwa ni hatua ya kuhakikisha uwekezaji katika Sekta Ndogo ya Umeme unaendana na mahitaji yanayotokana na ukuaji wa shughuli za kiuchumi na kijamii, Serikali iliendelea na zoezi la kuhuisha Mpango Kabambe wa

59​

Kuendeleza Sekta Ndogo ya Umeme wa Mwaka 2020. Kazi zilizotekelezwa ni pamoja na ukusanyaji wa mahitaji ya umeme kwa kila mkoa Tanzania Bara na Zanzibar; na utambuzi wa maeneo ya uwekezaji wa miradi ya nishati jadidifu na kiwango cha nishati jadidifu (jua na upepo) kinachotakiwa kuingizwa kwenye Gridi ya Taifa. Kazi hii inafanyika kwa ufadhili wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na inatarajiwa kukamilika Agosti, 2024.

Mkakati wa Nishati Jadidifu na Mpango wa Utekelezaji wa Mkakati (Renewable Energy Strategy and its Implementation Roadmap)

Mheshimiwa Spika, ili kuweza kuimarisha upatikanaji wa umeme nchini, Serikali inaandaa Mkakati na Mpango wa Utekelezaji wa Nishati Jadidifu. Kwa sasa Mshauri Mwelekezi anakamilisha uandaaji wa Mkakati baada ya kupokea maoni ya wadau. Kazi hii inafadhiliwa na Benki ya Dunia kupitia Mradi wa Tanzania Rural Energy Expansion Programme-TREEP na inatarajiwa kukamilika Juni, 2024.

60​

Mkakati wa Matumizi Bora ya Nishati na Uhuishaji wa Mpango Kazi wa Matumizi Bora ya Nishati (Energy Efficiency Strategy and Update of the Energy Efficiency Action Plan)

Mheshimiwa Spika, Serikali inashirikiana na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kuandaa Mkakati na Mpango kazi wa Matumizi Bora ya Nishati. Mkakati huo unaandaliwa ili kukidhi matakwa ya kitaifa na kimataifa ya kupunguza matumizi ya nishati yasiyo ya lazima, upotevu na gharama za nishati, kuhamasisha utunzaji wa mazingira pamoja na kukuza mchango wa nishati katika maendeleo ya nchi. Tayari Mkakati huo umeandaliwa na kuwasilishwa kwa wadau kwa maoni kabla ya kukamilishwa na kuanza kutumika.

Mheshimiwa Spika, zoezi la uandaaji wa Mkakati huo limehusisha pia uaandaji wa viwango vya matumizi ya vifaa vya nishati vinavyoruhusiwa (minimum energy performance standards and labelling); uboreshaji wa taarifa za matumizi na watumiaji wakubwa wa nishati; kuandaa na kutekeleza miongozo ya watumiaji wakubwa wa nishati; kuandaa sifa za wataalamu katika usiamamizi na ukaguzi wa matumizi ya nishati (professional qualification and skills in energy management and audit) na kujenga uelewa kwa

61​

umma kuhusu faida na fursa za matumizi bora ya nishati.

Mkakati wa Kitaifa wa Nishati ya Tungamotaka (Biomass Energy Strategy

– BEST)

Mheshimiwa Spika, Wizara imekamilisha majadiliano na Umoja wa Ulaya ya kuwezesha kupata ufadhili kwa ajili ya kuandaa Mkakati wa Kitaifa wa Nishati ya Tungamotaka ili kuwa na mwongozo thabiti wa uendelezaji wa rasilimali ya tungamotoka ambayo ni endelevu na isiyokuwa na athari kubwa za kiafya na mazingira.

Utekelezaji wa Mpango Kabambe wa Kupeleka Nishati Vijijini (Rural Energy Master Plan-REMP)

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia REA inaendelea na utekelezaji wa Mpango Kabambe wa Nishati Vijijini (Rural Energy Master Plan-REMP) ili kuhakikisha ifikapo mwaka 2030 huduma ya nishati vijijini iwe inapatikana kwa asilimia 100 na asilimia 80 ya Watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupikia.

62​

Mikakati na Mipango Mbalimbali ya Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia

Mheshimiwa Spika, Serikali imeidhinisha Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia wa mwaka 2024 - 2034. Mkakati huu pamoja na mambo mengine, unalenga kukuza matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa watanzania kwa kuimarisha upatikanaji wa malighafi na miundombinu ya uhakika ya nishati safi ya kupikia; kupunguza gharama za nishati safi, vifaa na majiko sanifu ya kupikia; kuandaa, kuhuisha na kuoanisha Sera, Sheria, Kanuni na miongozo wezeshi ya kufanikisha matumizi ya nishati safi ya kupikia; kuhamasisha uwekezaji katika nishati safi ya kupikia; kuongeza wigo wa tafiti na ubunifu wa teknolojia zinazohusu nishati ya kupikia; na kuimarisha uelewa wa jamii kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana na wadau iliratibu na kushiriki katika mkutano wa 28 wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP28) uliofanyika Dubai Novemba-Desemba, 2023. Katika Mkutano huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alizindua Programu ya Nishati Safi ya kupikia itakayowawezesha Wanawake Barani Afrika (African Women Clean Cooking Support Programme-AWCCSP) kutumia nishati safi

63​

ya kupikia. Aidha, Mei, 2024 kutafanyika mkutano wa Wakuu wa Nchi kuhusu Nishati Safi ya Kupikia Barani Afrika, Paris Ufaransa ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan atakuwa Mwenyekiti Mwenza wa mkutano huo kwa kushirikiana na Waziri Mkuu wa Norway, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Nishati Duniani (International Energy Agency-IEA) na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB). Mkutano huo pamoja na mambo mengine, unalenga kujadili na kuweka mikakati ya namna ya kuimarisha Sera, ugharamiaji na ushirikiano katika kuimarisha matumizi ya nishati safi ya kupikia Barani Afrika.

Mheshimiwa Spika, ikiwa ni hatua ya kuhakikisha Umma wa Watanzania unapata elimu kuhusu nishati safi ya kupikia, Wizara iliandaa kongamano la wanawake la nishati safi ya kupikia lililofanyika Mkoani Dodoma tarehe 9 Machi, 2024 katika kipindi cha siku ya wanawake duniani. Kongamano hilo pamoja na mambo mengine, lilihusisha utoaji wa elimu kwa wananchi kuhusu nishati safi ya kupikia, pamoja na ugawaji wa mitaji na vitendea kazi vya nishati safi ya kupikia. Vilevile, Wizara kwa kushirikiana na UNCDF kupitia ufadhili wa Umoja wa Ulaya inaanda mpango wa kuzijengea miundombinu ya nishati safi ya kupikia taasisi za kijamii zinazolisha zaidi ya watu 100 kwa siku katika mikoa ya Mwanza, Dodoma, Morogoro, Pwani na Dar es Salaam.

64​

Mheshimiwa Spika, ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Wizara ya Nishati kupitia Wakala wa Nishati Vijijini, imesaini mkataba wa ushirikiano na Jeshi la Magereza ili kuwezesha Jeshi hilo pamoja na vituo inavyovisimamia ikiwemo Magereza 129, Kambi za Makazi ya Watumishi 47, Ofisi 26, Vyuo vinne (4), Shule moja (1) na Hospitali moja (1) kutumia nishati safi ya kupikia. Katika maeneo hayo, jumla ya mifumo 126 ya bayogesi, 64 ya LPG pamoja na majiko banifu itajengwa na kuwezesha ununuzi wa mashine 61 za kuzalisha mkaa mbadala. Sambamba na hilo, jumla la mitungi 15,920 ya gesi ya LPG itagawiwa kwa Watumishi wa Jeshi hilo. Aidha, Wakala wa Nishati Vijijini unakamilisha taratibu za kuwezesha Jeshi la Kujenga Taifa pamoja na taasisi nyingine hususan za elimu na afya kutumia nishati safi ya kupikia.

Kuridhiwa kwa Mkataba wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati Jadidifu wa Mwaka 2009 (Statute of the International Renewable Energy Agency – IRENA, 2009)

Mheshimiwa Spika, ili kuvutia uwekezaji, utaalamu, teknolojia, utafiti na mitaji katika uendelezaji wa nishati jadidifu, Tanzania ilijiunga na Mkataba wa Wakala wa Kimataifa wa

65​

Nishati Jadidifu wa Mwaka 2009 (Statute of the International Renewable Energy Agency – IRENA, 2009). Hatua hii itaongeza kasi ya uendelezaji wa nishati jadidifu nchini na hivyo mchango wa chanzo hicho katika uzalishaji wa nishati ya umeme iliyo nafuu, ya gharama nafuu na rafiki wa mazingira.

B.2 SEKTA NDOGO YA MAFUTA NA GESI ASILIA

Mheshimiwa Spika,
katika mwaka 2023/24 Serikali iliendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuendeleza Sekta Ndogo ya Mafuta na Gesi Asilia nchini katika maeneo ya utafutaji, uendelezaji, uzalishaji, uchakataji, usafirishaji na usambazaji wa bidhaa za mafuta na gesi, ambapo mafanikio mbalimbali yaliweza kupatikana.

B.2.1 MIRADI YA UTAFUTAJI WA MAFUTA NA GESI ASILIA KATIKA VITALU VYA KIMKAKATI

Kitalu cha Mnazi Bay Kaskazini

Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu utafutaji wa mafuta na gesi asilia katika Kitalu cha Mnazi Bay Kaskazini kilichopo bahari ya kina kifupi Kusini Mashariki mwa Tanzania. Hadi kufika Machi 2024, shughuli zilizotekelezwa ni pamoja na kuanza majadiliano na Kampuni ya Maurel & Prom

66​

(M&P) ambayo imeonesha nia ya kushirikiana na TPDC katika kazi za utafutaji wa mafuta na gesi asilia kwenye kitalu hiki ikiwemo uchorongaji wa visima vya utafiti. Aidha, maombi ya leseni ya utafutaji wa mafuta na gesi asilia katika kitalu husika yapo katika hatua ya uidhinishwaji.

Kitalu cha Eyasi– Wembere

Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusisha utafutaji wa mafuta katika kitalu cha Eyasi – Wembere kilichopo kwenye Bonde la Ufa la Afrika Mashariki, Kaskazini Mashariki mwa Tanzania. Hatua iliyofikiwa ni pamoja na kukamilisha kazi ya kukusanya na kuchakata taarifa za mitetemo za mfumo wa 2D zenye urefu wa kilometa 260 katika awamu ya kwanza, kukamilisha tafsiri ya awali, kuandaa mpango wa awamu ya pili wa ukusanyaji wa taarifa za mitetemo za mfumo wa 2D zenye urefu wa kilomita 1,100; na kukamilika kwa kazi ya ulipaji wa fidia kwa wananchi walioathiriwa na zoezi la ukusanyaji wa taarifa za mitetemo. Aidha, TPDC inaendelea na hatua ya kumpata mkandarasi wa kufanya tafsiri ya tathmini ya kina ya taarifa za awamu ya kwanza na mkandarasi atakayekusanya taarifa za awamu ya pili ya kazi hii.

67​

Kitalu cha Songo Songo Magharibi

Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusisha utafutaji wa mafuta na gesi asilia katika Kitalu cha Songo Songo Magharibi ili kuimarisha upatikanaji, uzalishaji na usambazaji wa gesi asilia kwa matumizi mbalimbali nchini. Kazi zilizotekelezwa ni pamoja na kuanza taratibu za kumpata Mshauri Mwelekezi wa uchorongaji wa visima ambaye atafanya mapitio ya taarifa za kijiolojia na kijiofizikia katika Kitalu na kuandaa rasimu ya Mpango wa Uchorongaji wa visima vya utafiti. Aidha, katika kuimarisha usimamizi na utekelezaji wa mradi husika, TPDC kwa kushirikiana na Kampuni ya Pertamina ya nchini Indonesia inaratibu mafunzo kwa vitendo nchini Indonesia kwa Wataalamu 100 ili kuwajengea uwezo katika masuala ya utafutaji na uendelezaji wa mafuta na gesi asilia. Aidha, awamu ya kwanza Watalaamu watano (5) wameshapelekwa kwenye mafunzo hayo.

Vitalu Namba 4/1B na 4/1C

Mheshimiwa Spika, mradi huu unalenga utafutaji wa mafuta na gesi asilia katika kitalu namba 4/1B na 4/1C ili kuongeza upatikanaji, uzalishaji na usambazaji gesi asilia. Hadi kufikia Machi, 2024 kazi zilizotekelezwa ni pamoja na kukamilisha taratibu za kusaini Makubaliano ya Awali (Memorandum of Understanding – MoU) ya

68​

mashirikiano kati ya TPDC na kampuni ya CNOOC kutoka China. Makubaliano hayo yanalenga kushirikiana katika tafiti za awali kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo vitalu hivyo.

B.2.2 MIRADI YA UTAFUTAJI NA UENDELEZAJI WA MAFUTA NA GESI KATIKA VITALU KUPITIA PSA

Kitalu cha Ruvuma (Ntorya)

Mheshimiwa Spika
, mradi huu unahusisha uendelezaji gesi asilia iliyogunduliwa katika eneo la Ntorya katika kitalu cha Ruvuma. Hadi kufikia Machi, 2024 kazi zilizotekelezwa ni pamoja na kukamilisha tafsiri ya taarifa za mitetemo za mfumo wa 3D zilizokusanywa katika eneo la kilomita za mraba 334.9 na kuendelea na maandalizi ya ukarabati na majaribio ya visima (well tests) kwa visima vya Ntorya 1 na Ntorya 2. Aidha, Mkandarasi anaendelea na hatua za ununuzi wa mtambo wa kuchoronga kisima cha Chikumbi-1. Vilevile, Baraza la Mawaziri limeridhia kutolewa kwa leseni ya uendelezaji wa Kitalu hiki ambapo taratibu za utoaji wa leseni hiyo kwa TPDC kwa niaba ya mwekezaji (Kampuni ya ARA Petroleum) zinakamilishwa.

Mheshimiwa Spika, maandalizi ya ujenzi wa bomba la kutoa gesi Ntorya kupeleka kwenye

69​

kiwanda cha kuchakata gesi cha Madimba yanaendelea ambapo Tathmini ya Athari za Mazingira na Jamii (ESIA) imekamilika na Mshauri Mwelekezi wa uhandisi na ujenzi anakamilisha upembuzi yakinifu wa kihandisi ili kuwezesha zabuni ya ujenzi wa bomba kutangazwa.

B.2.3 MRADI WA KUCHAKATA NA KUSINDIKA GESI ASILIA KUWA KIMIMINIKA (LIQUEFIED NATURAL GAS – LNG)

Mheshimiwa Spika
, mradi huu unatekelezwa katika eneo la Likong’o mkoani Lindi na utahusisha usindikaji wa gesi asilia iliyogunduliwa katika Vitalu Na. 1, 2 na 4 vilivyopo katika kina kirefu cha bahari. Serikali kupitia Timu yake ya Majadiliano (Government Negotiation Team) imekwishafanya uchambuzi wa rasimu za Mkataba wa Nchi Hodhi (Host Government Agreement - HGA) na Mkataba wa Uzalishaji na Ugawanaji Mapato Ulioboreshwa (Amended Production Sharing Agreement – PSA) kwa ajili ya kuboreshwa kupitia majadiliano na wawekezaji kabla ya kuidhinishwa na Serikali kwa kuzingatia maoni yaliyotolewa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na taasisi nyingine za Serikali katika rasimu za awali za Mikataba hiyo.

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia TPDC imeendelea kushirikiana na Kampuni za Shell na Equinor kufanya maandalizi ya kutekeleza

70​

miradi ya uboreshaji wa hali ya maisha kwa wananchi waliopisha eneo la mradi (post compensation livelihood restoration program), ikiwemo kusaini Mkataba wa Makubaliano ya ujenzi wa shule ya msingi ya Likong'o iliyopo Manispaa ya Lindi.

B.2.4 UJENZI WA MIUNDOMBINU YA USAFIRISHAJI NA USAMBAZAJI WA GESI ASILIA

Usambazaji wa Gesi Asilia katika Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani

Mheshimiwa Spika
, mradi huu unahusisha ujenzi wa miundombinu ya kusambaza gesi asilia katika Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani kwa njia ya mabomba. Kazi zilizotekelezwa ni pamoja na ujenzi wa bomba lenye urefu wa kilometa 12.4 kutoka Mwenge hadi Mbezi Beach lililowezesha kuunganishwa kwa miundombinu ya gesi asilia kwenye viwanda viwili (2) vya Chemi and Cotex Industrial Ltd na Cotex Ltd pamoja na kuunganisha miundombinu ya gesi asilia katika hoteli sita (6) za White Sand Hotel, Land Mark Hotel, Serene Beach Resort, Ramada Resort, Giraffe Hotel na Jangwani Sea Breeze. Vilevile, kiwanda cha Sapphire Float Glass (Tanzania) Co. Ltd kiliunganishwa na miundombinu ya gesi asilia katika Mkoa wa Pwani.

71​

Mheshimiwa Spika, kazi nyingine zilizotekelezwa ni kufanya tafiti na kuandaa andiko la mradi wa kuunganisha gesi asilia katika gereza la Ukonga na nyumba za askari katika magereza ya Ukonga na Keko.

Usambazaji wa Gesi Asilia katika Mikoa ya Lindi na Mtwara

Mheshimiwa Spika
, mradi huu unahusisha ujenzi wa miundombinu ya kusambaza gesi asilia kwa njia ya mabomba katika Mikoa ya Lindi na Mtwara. Kazi zilizofanyika ni pamoja na ujenzi wa kituo cha kupunguza msukumo wa gesi (Pressure Reduction Station – PRS) na miundombinu ya umeme yenye urefu wa kilomita 3.8 kutoka makutano ya Mahumbika hadi Valvu Namba 3 (BVS 3) na bomba la kusafirisha gesi asilia kutoka BVS 3 kuelekea Kata za Mnazi Mmoja na Mingoyo mkoani Lindi lenye urefu wa kilomita 10.04. Bomba hilo limewezesha kuunganisha nyumba 209 ambazo zilikuwa na miundombinu ya gesi asilia tangu awali. Kiambatisho Na.7 ni miundombinu ya kusambaza gesi asilia katika maeneo mbalimbali nchini.

Usambazaji wa Gesi Asilia Kupitia Mfuko wa Nishati Vijijini - Awamu ya Kwanza na Pili

72​

Mheshimiwa Spika, mradi huu unatekelezwa na TPDC kwa kushirikiana na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na unalenga kusambaza gesi asilia na kuimarisha upatikanaji wa nishati safi ya kupikia katika maeneo ya vijijini. Kazi zilizotekelezwa ni pamoja na kukamilisha taratibu za kumpata Mkandarasi wa kujenga miundombinu ya kuunganisha nyumba 451 mkoani Lindi (Kata za Mnazi Mmoja na Mingoyo) na nyumba 529 mkoani Pwani (Mkuranga). Mradi huu unatekelezwa kwa ufadhili wa REA kwa gharama ya Shilingi bilioni 6.82 kama sehemu ya utekelezaji wa mkakati wa kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia katika maeneo ya vijijini.

Mheshimiwa Spika, vilevile, TPDC imekamilisha utafiti wa kubaini mahitaji ya gesi asilia katika mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara. Maeneo ya vijijini katika mikoa hiyo yatajengewa miundombinu ya kusambazia gesi asilia kwa ajili ya kupikia ikilenga makazi na taasisi za kibiashara na zisizo za kibiashara ili kupunguza matumizi ya kuni na mikaa kama sehemu ya utekelezaji wa awamu ya pili ya mradi huo.

Ujenzi wa Vituo vya Kujaza Gesi Asilia (Compressed Natural Gas-CNG) katika Magari kwenye Bohari za Dar es Salaam na Dodoma

73​

Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Machi, 2024 TPDC na GPSA ziliendelea na taratibu za kumpata Mshauri Mwelekezi wa kufanya kazi ya upembuzi yakinifu, usanifu wa michoro ya kihandisi na Tathmini ya Athari ya Mazingira na Jamii ili kuwezesha GPSA kujenga vituo vya CNG katika bohari za Dar es Salaam na Dodoma unaotarajiwa kuanza mwaka 2024/25. Lengo la mradi huu ni kuhamasisha matumizi ya gesi asilia katika vyombo vya moto vinavyomilikiwa na Serikali kwa kuongeza upatikanaji wake katika maeneo mbalimbali nchini.

Ushiriki wa Sekta Binafsi katika Ujenzi na Uendeshaji wa Vituo vya Kujaza Gesi Asilia (CNG) katika Magari

Mheshimiwa Spika
, kwa kushirikiana na Sekta Binafsi, vituo viwili vya kujaza gesi asilia (CNG) katika magari vilijengwa na kuanza kutoa huduma Novemba, 2023. Vituo hivyo ni kinachomilikiwa na Kampuni ya TAQA-Dalbit kilichopo pembezoni mwa barabara ya Nyerere karibu na Kiwanja cha Ndege (Terminal II) na kituo kinachomilikiwa na Kampuni ya Dangote kilichopo Mwanambaya, Mkuranga mkoani Pwani.

Mheshimiwa Spika, karakana nane (8) za kubadilisha mifumo ya matumizi ya nishati ya gesi asilia (CNG) kwenye magari ambayo ni nyenzo

74​

muhimu ya kuchochea matumizi ya gesi asilia katika magari zimejengwa na zinamilikiwa Taasisi za Umma na Sekta Binafsi. Karakana hizo ni NK CNG Auto Limited (Mbezi Beach, Dar es Salaam), MOL CNG Limited na TEMESA (Keko, Dar es Salaam), Kleenair CNG (Kigamboni, Dar es Salaam), TAQA Dalbit (Kipawa, Dar es Salaam), DIT (Dar es Salaam), BQ Contractors Limited (Goba, Dar es Salaam) na Kampuni ya Dangote ambayo imejenga karakana yake katika eneo la kiwanda Mkoani Mtwara kwa ajili ya kuhudumia magari ya kiwanda hicho. Jitihada hizi zimewezesha kuongezeka kwa magari yanayotumia mfumo wa gesi asilia kutoka 3,100 hadi 4,500.

Mradi wa Kujenga Uwezo wa Kusimamia Usambazaji wa Gesi Asilia Nchini

Mheshimiwa Spika,
Wizara inashirikiana na JICA kutekeleza mradi wa kujenga uwezo wa kusimamia usambazaji wa gesi asilia nchini (Capacity Development of Natural Gas Utilization in Tanzania). Mradi huu unalenga kuhuisha Mpango Kabambe wa Matumizi ya Gesi Asilia Nchini (Natural Gas Utilization Master Plan - NGUMP), kufanya usanifu wa mtandao wa usambazaji (network design) wa gesi asilia katika Mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma na Pwani na kuwajengea uwezo wataalam wa Wizara na Taasisi. Hadi kufikia Machi, 2024, kazi zilizofanyika ni ukusanyaji wa takwimu

75​

mbalimbali za kuwezesha uhuishaji wa NGUMP ikiwemo mahitaji, uzalishaji na matumizi ya gesi asilia nchini. Mradi huu unatarajiwa kukamilishwa Oktoba, 2025.

B.2.5 MRADI WA BOMBA LA KUSAFIRISHA GESI ASILIA KUTOKA TANZANIA HADI UGANDA

Mheshimiwa Spika,
mradi huu unahusu ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi asilia kutoka Tanzania hadi Uganda. Mradi unalenga kusafirisha gesi asilia pamoja na kuunganisha maeneo yatakayopitiwa na bomba hilo. Hadi kufikia Machi, 2024 kazi zilizotekelezwa ni pamoja na kuridhiwa kwa makubaliano ya mikataba mahsusi kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Uganda (Bilateral Agreement) kwa ajili ya kumpata Mshauri Mwelekezi wa kufanya kazi ya upembuzi yakinifu wa mradi.

B.2.6 MRADI WA KUSAFIRISHA GESI ASILIA KUTOKA DAR ES SALAAM (TANZANIA) HADI MOMBASA (KENYA)

126. Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusisha kusafirisha gesi asilia kutoka Dar es Salaam kwenda Mombasa - Kenya na pia unatarajiwa kunufaisha Mikoa ya Pwani, Tanga, Arusha na Kilimanjaro. Hadi kufikia Machi, 2024

76​

Kamati ya Pamoja ya Wataalamu imekamilisha maboresho ya nyaraka za maridhiano kwa ajili ya kumpata Mshauri Mwelekezi atakayefanya upembuzi yakinifu wa mradi.

B.2.7 MIRADI YA KUHIFADHI NA KUSAFIRISHA MAFUTA

Mradi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi kutoka Hoima - Uganda hadi Tanga - Tanzania (East African Crude Oil Pipeline – EACOP)

Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa mradi huu unaendelea katika mwaka 2023/24 ambapo hadi kufikia Machi, 2024 kazi zilizotekelezwa ni pamoja na kukamilisha malipo ya fidia kwa wananchi ya Shilingi bilioni 34.93 kwa wananchi 9,823 kati ya 9,904 waliopisha utekelezaji wa mradi, sawa na asilimia 99.2; kukamilika kwa ujenzi wa nyumba 340 sawa na asilimia 100 ya makazi mbadala kwa wananchi 294 waliopoteza makazi na kupisha mkuza; kukamilika kwa ujenzi wa karakana ya kuweka mfumo wa upashaji joto kwenye mabomba; na kuendelea na ujenzi wa maeneo 14 ya makambi. Aidha, mabomba yenye urefu wa kilomita 400 yameshawasili nchini na zoezi la kuwekewa mfumo wa kupasha joto, usalama na mawasiliano wa bomba (thermal insulation and fiber optic cables) linaendelea.

77​

Mheshimiwa Spika, shughuli za awali za ujenzi wa matenki zimefikia asilimia 32, usanifu wa kina wa matenki umefikia asilimia 85, ujenzi wa jeti umefikia asimilia 33 na zoezi la upimaji na uwekaji mawe ya mpaka kwenye mkuza wa bomba umekamilika kwa asilimia 100. Aidha, hadi kufikia Machi, 2024, Serikali ilikuwa imelipa jumla ya Dola za Marekani milioni 289.78 sawa na asilimia 94 ya kiasi kinachotakiwa kuchangiwa kama mtaji katika Kampuni ya EACOP Ltd. Utekelezaji wa Mradi kwa ujumla umefikia asilimia 27.1.

Kielelezo Na. 5: Uzinduzi wa Karakana ya Kuweka Mfumo wa Kupasha Joto Mabomba kwenye Kijiji cha Sojo Wilayani Nzega

78

79​

Mradi wa Bomba Jipya la TAZAMA

Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu ujenzi wa bomba jipya la TAZAMA lenye uwezo wa kusafirisha aina mbalimbali za mafuta safi kutoka Dar es Salaam hadi Zambia kwa kutumia mkuza wa bomba la TAZAMA. Tarehe 23 hadi 25 Oktoba, 2023 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alifanya ziara ya kikazi nchini Zambia ambapo pamoja na mambo mengine, alifanya mazungumzo na Rais wa Zambia kuhusu utekelezaji wa mradi huu. Aidha, kupitia mazungumzo hayo ilikubalika mradi utekelezwe sambamba na ujenzi wa matenki ya kuhifadhia mafuta kwa ukubwa wa tani 380,000 kwa upande wa Dar es salaam - Tanzania na tani 120,000 kwa upande wa Ndola – Zambia. Hadi kufikia Machi, 2024, Timu ya Wataalamu imeundwa kwa ajili ya kuangalia namna bora ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bomba jipya. Sambamba na hilo mkutano wa Mawaziri wa Nishati wa nchi hizi mbili umefanyika kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa utekelezaji wa mradi.

Uanzishwaji wa Hifadhi ya Kimkakati ya Mafuta (Strategic Petroleum Reserve - SPR)

Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu uanzishaji wa hifadhi ya kimkakati ya mafuta

80​

ambayo inahitaji pia uwepo wa maghala ya

kuhifadhia mafuta na ununuzi wa mafuta yenyewe. TPDC ipo katika hatua za kutafuta Mshauri Mwelekezi wa kufanya tathmini ya mradi pamoja na uendeshaji utakaoshirikisha Wizara, TPDC na Sekta Binafsi. Maeneo yaliyopo kwa ajili ya uanzishwaji wa SPR ni pamoja na Chongoleani (Tanga), Zuzu (Dodoma), Isaka (Kahama), Makambako (Njombe) na Kigamboni (Dar es Salaam).

81​

B.2.8 MRADI WA KUJENGA UWEZO WA KUSIMAMIA NA KUENDELEZA RASILIMALI ZA NDANI NA UTAWALA WA RASILIMALI ZA ASILI TANZANIA

Mheshimiwa Spika,
mradi huu ulianza kutekelezwa Juni, 2017 kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mfuko wa Maendeleo wa Afrika (AfDB) na umefikia asilimia 86 ya utekelezaji wake. Kazi zilizotekelezwa katika mwaka 2023/24 ni pamoja na kukamilisha uundaji wa mfumo wa uondoshaji shehena mipakani kwa Tanzania Bara na Zanzibar; ununuzi na usimikaji wa vifaa mbalimbali katika bandari ya Dar es Salaam na Zanzibar, uhuishaji wa Mkataba Kifani wa Ugawanaji Mapato (Model Production Sharing Agreement - MPSA) kupitia PURA na kugharamia mafunzo kwa wataalam kutoka Wizara ya Nishati, PIU, PSC, PURA na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Jumla ya watumishi 77 wamenufaika na mafunzo hayo.

B.2.9 UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA KAMPUNI TANZU ZA TPDC

TANOIL Investments Limited (TANOIL)

Mheshimiwa Spika,
TANOIL iliendelea kushiriki katika biashara ya mafuta kama kampuni ya kununua na kuuza mafuta (Oil

82​

Marketing Company - OMC). Aidha, katika kipindi cha Julai, 2023 hadi Machi, 2024, TANOIL iliweza kuagiza kiasi cha lita milioni 34.2 za dizeli ambapo lita milioni 33.1 zimeshauzwa na lita milioni 16.8 za petroli ziliagizwa na zote zimeshauzwa. Katika kipindi hiki, TANOIL imefanikiwa kupata faida ya Shilingi bilioni 6.8. Vilevile, TANOIL katika kipindi husika imekusanya jumla ya Shilingi bilioni 9.8 kati ya Shilingi bilioni 29 za madeni chechefu kutoka kwa wadaiwa sugu na jitihada za kukusanya madeni yaliyosalia zinaendelea.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa ujenzi na ukarabati wa vituo vya mafuta, TANOIL imekamilisha ukarabati wa vituo viwili vya mafuta katika Mikoa ya Singida na Geita. Vituo hivyo vitaendeshwa kwa mtindo wa kukodisha kwa kampuni binafsi zinazofanya biashara ya mafuta (Company Owned Dealer Operated Model -CODO) kwa makubaliano ya kulipa kodi na kununua mafuta kutoka TANOIL. Aidha, ujenzi wa vituo vya Musoma na Tarime (Mara), Segera (Tanga) na Makuyuni (Arusha) vipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji. Hatua hii itaisaidia TANOIL kuweza kushiriki kwenye biashara ya mafuta katika mnyororo wote wa usambazaji na hivyo kuleta tija kwenye ushindani wa sekta.

83​

Mheshimiwa Spika, kufuatia kukamilika kwa uchunguzi dhidi ya watumishi wa TANOIL walioisababishia hasara kampuni hiyo kwa mujibu wa Taarifa za Hesabu za mwaka 2021/22, Serikali tayari imekwishachukua hatua za kinidhamu ambapo watumishi watatu wamefukuzwa kazi na mmoja kupewa adhabu ya kupunguzwa mshahara kwa asilimia 15. Utekelezaji wa adhabu hizo ni kwa mujibu wa taarifa na mapendekezo ya Kamati ya Uchunguzi iliyoundwa na kwa kuzingatia Taratibu na Miongozo katika Utumishi wa Umma. Aidha, TAKUKURU inaendelea na uchunguzi wa tuhuma za kijinai dhidi ya watumishi hao.

GAS Company – GASCO

Mheshimiwa Spika,
GASCO imepewa jukumu la kuendesha na kufanya matengenezo (Operations and Maintenance - O & M) ya miundombinu yote ya Taifa ya gesi asilia (National Natural Gas Infrastructure - NNGI) inayohusisha mitambo ya kuchakata gesi ya Madimba na Songo Songo pamoja na bomba la kusafirisha gesi kutoka Mtwara na Songo Songo hadi Dar es Salaam. GASCO imeendelea kutekeleza jukumu hilo kwa kuzingatia na kufuata viwango vya kitaifa na kimataifa vya usalama mahala pa kazi katika kuhakikisha Usalama wa Watu, Miundombinu na Mazingira (Health Safety and Environment - HSE).

84​

Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Machi, 2024, kazi za uendeshaji na matengenezo zilifanyika kikamilifu bila kupata ajali au kusimamisha shughuli za uzalishaji (Zero Lost Time Injury (LTI =0). Vilevile, jumla ya matenegenezo 21,164 ya mitambo mbalimbali yalifanyika kwa ufanisi sawa na asilimia 95.85 ya mpango kwa kipindi husika. Matengenezo mengine yanaendelea kufanyika baada ya ununuzi wa vipuri kukamilika. Ufanisi huu umewezesha miundombinu yote ya gesi asilia kuwa na utayari (reliability and availability) wa asilimia 100 wa kufikisha gesi asilia kwa wateja wake wote.

B.2.10 USIMAMIZI NA UDHIBITI WA SEKTA YA NISHATI KUPITIA PURA NA EWURA

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) iliendelea kusimamia na kudhibiti Sekta ya Nishati ili kuhakikisha utekelezaji wa shughuli za sekta hiyo unazingatia sheria na taratibu zilizopo pamoja na utoaji wa huduma bora kwa wananchi.

85​

B.2.10.1 MAMLAKA YA UDHIBITI MKONDO WA JUU WA PETROLI (PURA)

Mheshimiwa Spika,
Serikali kupitia PURA imeendelea kusimamia shughuli za utafutaji, uendelezaji na uzalishaji wa gesi asilia katika vitalu mbalimbali nchini kulingana na mikataba ya Uzalishaji na Ugawanaji Mapato (PSA) kama inavyoonekana katika Kiambatisho Na.8. Hadi kufikia Machi 2024, uzalishaji wa gesi asilia umeendelea kuimarika na kufikia wastani wa futi za ujazo milioni 236.21 kwa siku zilizozalishwa katika vitalu vya Songo Songo (120.27 mmscfd) na Mnazi bay (115.94 mmscfd). Gesi hiyo ilitumika katika matumizi mbalimbali ikiwemo viwandani, majumbani, katika taasisi, katika magari na kwa ajili ya uzalishaji wa umeme.

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia PURA inatarajia kunadi vitalu vya utafutaji wa mafuta na gesi asilia kupitia Duru ya Tano (5). Lengo kuu la zoezi hili ni kuwezesha ugunduzi zaidi wa rasilimali za mafuta na gesi asilia nchini kwa kufanya shughuli za utafutaji katika vitalu vilivyowazi vyenye viashiria vya uwepo wa rasilimali hizo. Hadi kufikia Machi, 2024 kazi zilizofanyika ni pamoja na kukamilisha mapitio na maboresho ya Mkataba Kifani wa Ugawanaji Mapato (Model Production Sharing Agreement-MPSA) wa mwaka, 2013 ambapo rasimu ya MPSA (MPSA, 2024)

86​

imeandaliwa; na kukamilishwa kwa Mwongozo wa Kupata Kampuni za Kijiofizikia (Geophysical Multiclient Company) zitakazoshirikiana na PURA katika zoezi la kunadi vitalu ambapo taratibu za kupata kampuni hizo zinaendelea.

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia PURA imekamilisha zoezi la utengaji wa vitalu vinavyopendekezwa kufanyiwa mnada na kwa sasa zoezi linaloendelea ni kuandaa vifurushi vya taarifa (data packages) za vitalu hivyo. Zoezi la kunadi vitalu linatarajiwa kuzinduliwa mara baada ya kuidhinishwa kwa MPSA, 2024 na marekebisho ya Sheria ya Petroli ya mwaka 2015.

Mheshimiwa Spika, kaguzi na usimamizi wa shughuli za utafutaji wa mafuta na gesi asilia umeendelea kufanyika katika vitalu vya Tanga, Namba 1, 2 & 4, Nyuni, Ruvuma, Ruvu na Kiliwani North. Aidha, katika Eneo la Eyasi-Wembere shughuli ya uchakataji wa data zilizochukuliwa za mfumo wa 2D imekamilika na taratibu za kumpata Mkandarasi wa kutafsiri data hizo zinaendelea. Katika Kitalu cha Ruvuma, kazi ya kutafsiri taarifa za mitetemo zilizochukuliwa katika eneo la kilomita za mraba 334 imekamilika na kuanza kwa maandalizi ya uendelezaji wa gesi asilia iliyogunduliwa ikiwemo ukarabati wa visima vya Ntorya-1 na Ntorya-2 vitakavyotumika kuzalisha gesi asilia na uchorongaji wa kisima cha utafutaji cha Chikumbi-1.

87​

Kiambatisho Na. 9 ni ramani inayoonesha hali ya utafutaji, uendelezaji na uzalishaji wa mfuta na gesi asilia nchini.

Mheshimiwa Spika, ili kufikia azma ya Serikali ya kuhakikisha wananchi wananufaika na uwekezaji katika rasilimali zilizopo katika maeneo yao, Serikali kupitia PURA na TPDC imeandaa rasimu ya Miongozo ya Uwajibikaji wa Kampuni kwa Jamii (Corporate Social Responsibility – CSR) katika Sekta Ndogo ya Mafuta na Gesi Asilia nchini inayotarajiwa kukamilika mwishoni mwa Juni, 2024. Aidha, maandalizi ya rasimu yamehusisha wadau kutoka maeneo mbalimbali ikiwemo mikoa ya Lindi, Mtwara na Pwani.

Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha Serikali inapata stahiki zake kwa mujibu wa mikataba iliyoingiwa kati yake na Wawekezaji katika shughuli za utafutaji, uendelezaji na uzalishaji wa mafuta na gesi asilia nchini, PURA imeendelea kufanya kaguzi za gharama katika mikataba ya PSA ambapo hadi kufikia Machi 2024, kaguzi hizo ziliwezesha jumla ya Shilingi bilioni 211 kutolewa kwenye madai ya gharama za uwekezaji na kurudishwa kwenye mfuko wa ugawanaji mapato kati ya Serikali na Wawekezaji.

88​

B.2.10.2 MAMLAKA YA UDHIBITI WA HUDUMA ZA NISHATI NA MAJI (EWURA)

Usimamizi na Udhibiti wa Shughuli za Mkondo wa Kati na Chini wa Gesi Asilia

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia EWURA iliendelea kusimamia na kudhibiti shughuli za gesi asilia kwa kufanya kaguzi za mara kwa mara katika miundombinu ya uchakataji, usafirishaji na usambazaji wa gesi asilia na vituo vya kujazia gesi kwenye magari (CNG) katika mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani na Dar es Salaam.

Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Machi, 2024 jumla ya kaguzi za kawaida 25 kwenye miundombinu ya gesi asilia zilifanyika na kaguzi moja maalum ya kitaalam na kiusalama kwenye vituo vitatu (3) vya kujazia gesi kwenye magari na karakana saba (7) za kuongeza mfumo wa gesi asilia kwenye magari ulifanyika. Ukaguzi huu maalumu ulishirikisha EWURA, Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Bodi ya Usajili wa Wakandarasi (CRB). Lengo ni kuhakikisha usalama kwenye eneo la utaalam, vifaa na mazingira ya utekezaji wa shughuli zinazohusu matumizi ya gesi asilia katika magari. Kupitia kaguzi hizo, imebainika miundombinu na shughuli zote zinazohusisha gesi

89​

asilia hapa nchini zipo katika hali nzuri inayokidhi viwango vya ubora na usalama.

Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Machi 2024, EWURA ilitoa vibali sita (6) kwa ajili ya ujenzi (construction approvals) wa miundombinu ya kusambaza gesi asilia viwandani na vituo vya CNG. Vibali hivyo vilitolewa kwa TPDC kwa ajili ya ujenzi wa kituo kikuu (mother station) cha kuzalisha CNG kwenye eneo la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, vituo vidogo viwili (2) (daughter stations) vya kupokea CNG katika kiwanda cha Kairuki (Kibaha) na hospitali ya Taifa ya Muhimbili na vibali vingine viwili (2) kwa ajili ya ujenzi wa mabomba ya kuunganisha gesi asilia kwenye kituo cha kujazia gesi kwenye magari cha Dangote na kwenye kiwanda cha kampuni ya KEDA vilivyopo Mkuranga. Aidha, EWURA ilitoa kibali cha ujenzi kwa kampuni ya PanAfrican Energy Tanzania (PAET) kwa ajili ya ujenzi wa bomba la gesi la kuunganisha kituo cha kujazia gesi asilia kwenye magari cha kampuni ya TAQA Dalbit - Kipawa.

Mheshimiwa Spika, EWURA pia ilitoa leseni mbili (2) za uendeshaji (operational licence) kwa vituo viwili vya kujazia gesi asilia kwenye
magari (CNG filling station). Vituo hivyo vinamilikiwa na Kampuni za TAQA Dalbit (Kipawa

Dar es Salaam) na Dangote (Mkuranga – Pwani)

90​

vinavyohudumia watumiaji wa nishati ya gesi asilia kwenye maeneo husika.

Shughuli za Bidhaa za Mafuta ya Petroli

Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea na usimamizi wa ubora wa vituo vya mafuta ili kuimarisha upatikanaji, usalama na ubora wa bidhaa za mafuta kwa watumiaji katika maeneo yote nchini. Aidha, imeendelea kusimamia mazingira chanya ya uwekezaji wa ujenzi wa vituo vya mafuta vyenye ubora ambapo hadi kufikia Machi, 2024 jumla ya vituo 2,522 vilivyopo mijini na vijijini vilikidhi vigezo vya ubora na usalama na kupewa leseni ikilinganishwa na vituo 2,297 katika kipindi hicho mwaka 2022/23, sawa na ongezeo la asilimia 9.80. Kati ya vituo hivyo, vituo 434 vimejengwa katika maeneo ya vijijini ikilinganishwa na vituo 287 vilivyojengwa vijijini kwa kipindi hicho mwaka 2022/23 sawa na ongezeko la asilimia 51.22.

Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai 2023 hadi Machi 2024, EWURA ilitoa leseni, vibali, kuboresha Kanuni na kusimamia ubora wa bidhaa za mafuta kama ifuatavyo:

Ilitoa leseni 34 kwa kampuni za mafuta (wholesalers) kwa ajili ya kuagiza na kuuza mafuta kwa jumla, ambapo leseni 30 zilitolewa kwa kampuni mpya;

91

Ilitoa leseni mpya 4 kwa kampuni za kuagiza na kuuza Gesi itokanayo na Petroli (LPG) kwa jumla (LPG Wholesalers). Pia, ilitoa leseni 27 kwa Mawakala wa Kusambaza LPG (LPG Distributors). Kati ya leseni hizo, leseni 26 zilitolewa kwa Mawakala wapya;

Ilitoa leseni saba (7) kwa kampuni zenye miundombinu binafsi ya kuhifadhi na kujaza mafuta (consumer installation facilities). Kati ya leseni hizo, leseni sita (6) zilitolewa kwa kampuni mpya;

Ilitoa leseni mpya moja (1) ya ghala la kuhifadhia mafuta (petroleum storage);

Ilitoa leseni moja (1) ya uwakala wa condensate.

Ilitoa vibali vya ujenzi (construction approvals) 237 ambapo vibali 233 vilikuwa kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya mafuta, kimoja (1) kwa ajili ya miundombinu ya kuhifadhia LPG, viwili (2) kwa ajili ya matumizi binafsi (consumer installations) na kimoja (1) kwa ajili ya ghala ya kuhifadhia mafuta;

Ilisimamia taratibu za uagizaji na usambazaji wa mafuta ili kuhakikisha upatikanaji wa mafuta ya kutosha nchini;

92​

Ilisimamia ubora wa bidhaa za mafuta nchini kwa kufanya kazi ya kuchukua sampuli za mafuta kutoka kwenye vituo vya mafuta na maghala ya kuhifadhia mafuta na kupeleka maabara kwa ajili ya vipimo. Aidha, jumla ya sampuli 318 zilichukuliwa kutoka katika miundombinu tajwa kwa ajili ya kupima ubora na sampuli 303 sawa na asilimia 95.3 zilifaulu kwa kuwa na viwango stahiki vya ubora. EWURA inachukua taratibu za kisheria ikiwemo kufungia wahusika kutoendelea kufanya biashara pindi wanapobainika kuwa na dosari hadi hapo wanapokidhi matakwa ya leseni zao. Pia, EWURA inaendelea kutoa elimu na ushauri kwa wadau ili waendelee kutoa huduma stahiki;

Ilifanya maboresho ya Kanuni zikiwemo The Petroleum (Wholesales Storage Retail and Consumer Installation) Rules, 2023 ili kuimarisha ukusanyaji wa takwimu za
biashara ya mafuta kutoka kwa wafanyabiashara wa mafuta wa jumla pamoja na maghala ya kuhifadhia mafuta; the Petroleum (Retail Operations in Townships and Villages) (Amendment) Rules, 2023 ambazo zilifanyiwa maboresho ili kuwezesha ukusanyaji wa takwimu za biashara ya mafuta kutoka kwenye vituo vya mafuta; na

93​

the Energy and Water Utilities Regulatory Authority (Petroleum Products Price Setting) (Amendment) Rules, 2023 ambazo zilifanyiwa maboresho ya jedwali la ukokotoaji wa bei za mafuta;

Ilikagua ubora wa miundombinu ya mafuta na kuhakikisha upatikanaji wa bidhaa za mafuta kwa wananchi bila kuhatarisha afya, usalama na mazingira. Katika kipindi hiki, ukaguzi ulifanyika kwenye miundombinu ya mafuta 446 na miundombinu ya mafuta 338 sawa na asilimia 75.78 ilikidhi viwango stahiki vya ubora. EWURA inaendelea kutoa elimu kuhusiana na usalama na mazingira ya miundombinu ya mafuta kwa wahusika; na

Ilitoa bei elekezi za mafuta kila mwezi na kusimamia utekelezaji wake.

Udhibiti wa Biashara ya Vilainishi

Mheshimiwa Spika, kwa ujumla upatikanaji na ubora wa vilainishi nchini ni wa kuridhisha. Serikali kupitia EWURA inaendelea na usimamiaji wa ubora wa vilainishi vinavyoingizwa nchini ambapo leseni 99 za wauzaji wa jumla wa vilainishi na leseni 6 za wafanyabiashara wanaotengeneza vilainishi nchini zimetolewa. Vilevile, EWURA inaendelea kushirikiana na Tume

94​

ya Ushindani (FCC) na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) katika kudhibiti ubora wa bidhaa za vilainishi zinazoingizwa nchini kwa kufanya kaguzi kwa pamoja. Aidha, EWURA imeanza kusajili vilainishi vinavyozalishwa na kuagizwa kutoka nje ya nchi kwa lengo la kuhakikisha vilainishi vyenye ubora uliothibitishwa na Taasisi za ndani na kimataifa vinatumika nchini. EWURA inaendelea kutoa elimu kwa watumiaji kununua bidhaa hizo kutoka kwa wauzaji waliothibitishwa.

Uwekaji Vinasaba katika Mafuta

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia EWURA iliendelea na jukumu la kusimamia na kukagua soko la ndani la mafuta ili kuhakikisha kuwa mafuta yanayouzwa nchini yana viwango stahiki vya vinasaba kwa lengo la kudhibiti ubora na kuimarisha mapato ya Serikali kupitia kodi. Uwekaji wa vinasaba kwenye mafuta unafanywa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ambapo hadi kufikia Machi 2024, kiasi cha lita bilioni 1.18 za mafuta ya petroli, lita bilioni 1.70 za mafuta ya dizeli na lita milioni 6.18 za mafuta ya taa ziliwekewa vinasaba nchini. Aidha, katika kipindi hicho EWURA ilipima mafuta kwenye vituo 307 ambapo vituo 299, sawa na asilimia 97.39, vilifaulu kwa kuwa na kiwango stahiki cha vinasaba. Vituo ambavyo vilikutwa na mafuta ambayo hayana

95​

kiwango stahiki cha vinasaba vilichukuliwa hatua za kisheria.

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia TBS inafanya maboresho ya kutumia teknolojia (automation) katika kuweka vinasaba kwenye mafuta na hadi sasa mifumo ya kuweka vinasaba kwa teknolojia hiyo imeunganishwa katika maghala sita na TBS inaendelea na taratibu za kujenga vituo vya kupima vinasaba kwa hiari kabla mafuta hayajafika kituoni (voluntary check points).

Vituo hivi vitawezesha wafanyabiashara kuhakikisha uwepo wa vinasaba kwenye mafuta kabla ya kufikisha mafuta vituoni.

Usimamizi na Udhibiti wa Shughuli za Umeme

Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Machi,

2024 Serikali kupitia EWURA ilitekeleza yafuatayo:

Ilitoa leseni tatu (3) za Muda Mfupi (Provisional Licence) zenye uwezo wa kuzalisha Megawati 14.5 kwa Kampuni tatu ambazo ni Bugando Natural Energy Limited MW 5; Lilondi Hydropower Limited MW 4.5; na Tangulf Nakatuta Energy Company Limited MW 5;

96​

Ilitoa leseni 1,163 kwa wataalamu wenye sifa za kufunga mifumo ya umeme nchini ili kusaidia katika juhudi za Serikali za kusambaza umeme kwa mujibu wa kifungu namba 5(a) na 8(1) cha Sheria ya Umeme, Sura ya 131. Kati ya hizo Daraja A (51); Daraja B (105); Daraja C (699); Daraja D (306) na Daraja S1 (2);

Ilikagua miundombinu ya umeme ili kuhakikisha ufanisi katika utendaji, upatikanaji wa huduma bora, na uzingatiwaji wa Sheria kwa mujibu wa kifungu namba 31(2) cha Sheria ya Umeme, Sura ya 131. Miundombinu ya umeme iliyokaguliwa ni:

Miundombinu ya TANESCO ya kusambaza na kugawa umeme katika mikoa 17 nchini. Mikoa hiyo ni; Mwanza, Simiyu, Tabora, Mbeya, Songwe, Arusha, Mtwara, Dodoma, Tanga, Morogoro, Mara, Lindi, Pwani, Kagera, Ruvuma, Rukwa na Songwe. Pia EWURA ilifanya ukaguzi wa miundombinu ya kusamabaza umeme kwa kampuni ya Mwenga Power Services;

97

Mitambo 14 ya kuzalisha umeme. Mitambo hiyo ni Kinyerezi I (MW 150.00), Kinyerezi I Extension (MW
185.00), Kinyerezi II, Ubungo I (MW

102.00), Ubungo II (MW 129.00), Ubungo III (112.50), Tegeta (MW 45.0), Songas (189.0), Mtera (MW

80.00), Andoya Hydro Power Plant

(1.00), Yovi Hydro Power Company Ltd (0.95), Mwenga Hydro Ltd (4.00), Kidatu (204.00) na Kihansi (180.00); na

Miundombinu ya kusafirisha umeme kwenye laini ya Ubungo-Chalinze (Kilovoti 132) pamoja na vituo vyake vya kupozea umeme vya Ubungo, Mlandizi na Chalinze.

Ilikagua miradi ya kuzalisha umeme inayotekelezwa ili kuhakikisha ufanisi katika utekelezaji wake, kwa mujibu wa Sheria ya Umeme. Miradi hiyo ni:

Mradi wa kuzalisha umeme wa Julius Nyerere Hydropower Project (2115MW);
Mradi wa kuzalisha umeme wa Rusumo Hydropower Project (80MW); na

98

Mradi wa kuzalisha umeme wa

Kikagati-Murongo Hydropower Plant (14MW).

Iliridhia mkataba wa mauziano ya umeme (Power Purchase Agreement) wa Megawati 26.67 kati ya TANESCO na Rusumo Power Company Limited (RPCL). Mradi huu umechangia kuimarisha hali ya upatikanaji wa umeme kwenye mfumo wa Gridi ya Taifa;

Iliridhia jumla ya mikataba 14 yenye jumla ya Megawati 79.2 ya kuuziana umeme (Standardized Power Purchase Agreement- SPPA) kati ya TANESCO na wazalishaji wadogo (Kiambatisho Na. 10) ili kuimarisha upatikanaji wa huduma ya nishati ya umeme kwa wananchi waliounganishwa katika Gridi ya Taifa na nje ya Gridi ya Taifa; na

Ilifanya marekebisho ya Kanuni za Shughuli za Ugavi wa umeme na Kanuni za Shughuli za Uzalishaji, Usafirishaji na Usambazaji Umeme za Mwaka 2023 kwa ajili ya kuboresha taratibu za kufanya ukaguzi.

99

B.2.11 USHIRIKI WA SEKTA BINAFSI NA USHIRIKISHWAJI WA WATANZANIA KATIKA SEKTA YA MAFUTA NA GESI ASILIA

Mheshimiwa Spika,
katika kuhakikisha kampuni za wazawa na watalaam wazawa wanashiriki kikamilifu kwenye mnyororo wa Sekta Ndogo ya Mafuta na Gesi Asilia nchini, Serikali kupitia EWURA na PURA zimeendelea kuhuisha kanzidata za watoa huduma na wataalamu wa ndani (Local Suppliers and Service Providers Database (LSSP) na Local Professional Database) kupitia mfumo wa “Common Qualification System – CQS”. Kupitia mfumo huo, EWURA imesajili kampuni za wazawa 2,029 na wataalam wazawa 198 kwenye kanzidata ya EWURA na jumla ya Kampuni 157 zimesajiliwa na zinapata fursa za kuuza bidhaa na kutoa huduma mbalimbali kwenye Miradi inayoendelea na wataalamu 187 wa ndani wenye ujuzi mbalimbali katika tasnia ya mafuta na gesi asilia wamesajiliwa katika mfumo na kanzidata ya shughuli za petroli. Aidha, takribani kampuni 250 zilipata zabuni za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja katika mradi wa EACOP na miradi mingine katika Sekta Ndogo ya Gesi Asilia.

Mheshimiwa Spika, takribani Watanzania 3,227 walikuwa wameajiriwa katika miradi ya mafuta na gesi asilia hususani katika mradi wa

100​

EACOP na Watanzania 212 wameajiriwa katika vitalu vya uzalishaji wa gesi asilia vya Mnazi Bay na Songo Songo. Aidha, shughuli za utafutaji wa gesi asilia pia huzalisha ajira za muda ambapo jumla ya Watanzania 148 waliajiriwa katika kazi ya uchukuaji wa data za mitetemo za 3D katika Kitalu cha Songo Songo na 250 waliajiriwa katika kazi ya uchukuaji wa data za mitetemo za 2D katika Kitalu cha Eyasi Wembere. Sambamba na ajira, takribani Dola za Marekani milioni 44.5 zilitumiwa na kampuni za kigeni zilizowekeza katika shughuli za mafuta na gesi asilia kununua bidhaa na huduma mbalimbali zinazozalishwa na kupatikana nchini.

B.2.12 HALI YA UAGIZAJI NA UPATIKANAJI WA BIDHAA ZA MAFUTA YA PETROLI NCHINI

Mheshimiwa Spika,
ili kuhakikisha upatikanaji wa bidhaa za mafuta ya petroli nchini, Serikali imeendelea kutumia Mfumo wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (Bulk Procurement System - BPS). Mfumo huu ulianzishwa mwaka 2011 na kuanza kutumika rasmi Januari, 2012 ambapo pamoja na uhakika wa upatikanaji wa bidhaa za mafuta ya petroli wakati wote pia uagizaji wa mafuta umeendelea kufanyika kwa ufanisi na hivyo mlaji wa mwisho kulipia mafuta kwa bei stahiki. Aidha, mfumo huu umewezesha upatikanaji wa takwimu sahihi za bidhaa za mafuta ya petroli

101​

yanayoingia nchini na kwenda nchi jirani na pia kurahisisha udhibiti wa ubora wa bidhaa za mafuta ya petroli.

Mheshimiwa Spika, jumla ya lita bilioni 6.28 za bidhaa za mafuta ya petroli ziliingizwa nchini kwa kutumia mfumo wa BPS kwa kipindi cha Julai, 2023 hadi Machi, 2024. Bidhaa hizo ziliingizwa kupitia Bandari za Dar es Salaam, Tanga na Mtwara, ambapo dizeli ilikuwa lita bilioni 3.77, petroli lita bilioni 2.29 na mafuta ya ndege/taa lita milioni 224. Aidha, mafuta kwa ajili ya matumizi ya ndani ya nchi yaliongezeka kwa asilimia 6.07 ikilinganishwa na kiasi kilichoingizwa Julai, 2022 hadi Machi, 2023. Vilevile, kiasi cha mafuta yaliyoingizwa kwa ajili ya kwenda nchi jirani kilipungua kwa asilimia 4.76 kutokana na changamoto ya upatikanaji wa Dola za Marekani. Kati ya mafuta yaliyoingizwa Julai, 2023 hadi Machi, 2024 lita bilioni 3.37 sawa na asilimia 53.7 yalikuwa ni kwa ajili ya matumizi ya ndani na lita bilioni 2.9 sawa na asilimia 46.3 yalikuwa kwa ajili ya nchi jirani. Kielelezo Na. 6 kinaonesha uwiano wa bidhaa za mafuta zilizoingizwa nchini kwa kipindi cha Julai, 2023 hadi Machi, 2024. Kielelezo Na.7 ni jumla ya kiasi cha mafuta kilichoingizwa nchini kwa ajili ya matumizi ya ndani na nchi jirani katika kipindi hicho.

102​

Kielelezo Na.6: Uwiano wa Bidhaa za Mafuta Zilizoingizwa Nchini kwa Kipindi cha Julai, 2023 hadi Machi, 2024

Mafuta Yaliyoingia Julai 2023 hadi Machi 2024

4%

36%

60%

DizeliPetroliMafuta ya Ndege/Taa

Chanzo: PBPA

103​

Kielelezo Na.7: Jumla ya Kiasi cha Mafuta Kilichoingizwa kwa Ajili ya Matumizi ya Ndani na Nchi Jirani, Julai 2023 hadi Machi 2024

Lita Milioni

2,000

1,800

1,600

1,400

1,200

1,000

800

600

400

200

-
Dizeli
Petroli Mafuta ya

Ndege/Taa

Kwenda Nchi Jirani Matumizi ya Ndani

Chanzo: PBPA

Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai 2023 hadi Machi 2024, jumla ya zabuni 88 zilitolewa kwa njia ya ushindani wa kimataifa kwa kigezo cha gharama ndogo za uletaji wa mafuta nchini (premium). Aidha, wastani wa zabuni 9 hadi 12 zilishindanishwa kila mwezi ambapo wastani wa wazabuni wanne (4) hadi sita (6) hushinda zabuni hizo kila mwezi. Katika zabuni hizo TPDC imekuwa ikishiriki na hivyo kuongeza ushindani na kuchangia upatikanaji wa gharama stahiki za uagizaji wa mafuta.

104​

Mheshimiwa Spika, changamoto ya upatikanaji wa Dola za Marekani imeendelea kuikabili nchi yetu kama ambavyo nchi nyingi Duniani zinapitia changamoto hiyo. Makali ya tatizo hili yanatokana na vita baina ya Urusi na Ukraine na mabadiliko ya sera ya fedha za Marekani. Ili kukabiliana na changamoto hiyo, Serikali kupitia Wizara ya Nishati, Wizara ya Fedha, Benki Kuu ya Tanzania, Taasisi zinazohusika katika mnyororo wa biashara ya mafuta pamoja na Sekta Binafsi zilishirikiana kuchukua hatua mbalimbali. Benki Kuu ya Tanzania ilisimamia suala hili ikiwemo kuruhusu benki kuuziana fedha za kigeni hususan Dola za Marekani ili kuchagiza upatikanaji wake katika soko la ndani; kuruhusu ulipiaji wa mafuta kwa kutumia fedha nyingine za kigeni; na kuongeza kiwango cha ukomo wa ukopaji kwa wanunuzi wa mafuta (OMC’s borrowing limit) katika benki za biashara.

Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mpito kuelekea uwekezaji wa miundombinu ya kupokea mafuta kwa pamoja, Serikali imeendelea kutumia miundombinu ya Kampuni ya TIPER kama Kituo cha Kupokea Mafuta kwa Pamoja (Single Receiving Terminal - SRT) ambapo kina uwezo wa kupokea wastani wa meli moja hadi mbili

kwa mwezi. Idadi hii inafikia asilimia kati ya 30 hadi 60 ya meli mbili (2) hadi nne (4) zinazoingia

105​

nchini kila mwezi kushusha shehena ya mafuta ya dizeli. Hivyo meli zinazokosa nafasi ya kushusha mafuta TIPER hutumia muda mrefu kumaliza kushusha mafuta. Ikiwa ni hatua ya kuboresha ufanisi, TIPER inaendelea kusimika pampu za kuhamisha mafuta zenye uwezo mkubwa wa kusukuma hadi lita 800,000 kwa saa ili kuongeza kasi ya kuhamisha mafuta kwenda kwenye maghala ya kampuni za mafuta (OMCs) ambapo kazi hii inatarajiwa kukamilika Januari, 2025.

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia PBPA imekamilisha ufungaji na kuanza kutumia mfumo wa kielektroniki (SCADA) ili kusaidia udhibiti wa upotevu wa mafuta kwenda kwa wafanyabiashara wa mafuta ya jumla (OMCs) wakati wa upakuaji. Mfumo huu una uwezo wa kusoma kiasi cha mafuta yanayopita katika mita (flowmeter) za Serikali zilizopo Kurasini, Kigamboni, Tanga na Mtwara na kulinganisha kiasi cha mafuta yanayopita katika mita zilizopo kwenye maghala ya kuhifadhi mafuta. Upatikanaji wa taarifa hizi kutoka kwenye mita unawezesha Serikali kudhibiti upotevu wa mafuta.

B.2.13 MWENENDO WA BEI ZA MAFUTA KATIKA SOKO LA DUNIA

Mheshimiwa Spika,
Serikali kupitia EWURA imeendelea kufuatilia mwenendo wa bei za mafuta katika soko la dunia ambapo kuanzia Julai

106​

2023 hadi Machi 2024 bei ya pipa la mafuta ghafi kwa wastani ilishuka kwa asilimia 7 na kufika wastani wa Dola za Marekani 84 kwa pipa ikilinganishwa na wastani wa Dola za Marekani 90 kwa pipa kwa kipindi kama hicho katika mwaka 2022/23. Kushuka huko kwa bei za mafuta ghafi katika soko la dunia kulichangiwa na kudorora kwa uchumi wa dunia uliotokana na migororo ya kivita ikiwemo Urusi na Ukraine pamoja na Israel na Palestina. Vilevile, kulichangiwa na kudorora kwa ukuaji wa uchumi wa mataifa makubwa kama China kulikosababishwa na athari zilizotokana na UVIKO- 19. Kielelezo Na.8 ni mwenendo wa bei za mafuta ghafi katika soko la Dunia.

Kielelezo Na.8: Mwenendo wa Bei ya Mafuta Ghafi katika Mwaka 2022/23 na 2023/24

Mwezi
DOLA KWA PIPA
2023/24
2022/23
Julai
80​
105​
Agosti
85​
98​
Septemba
92​
91​
Oktoba
91​
93​
Novemba
83​
87​
Disemba
78​
82​
Januari
80​
80​
Februari
82​
84​
Machi
85​
79​
Wastani
84​
89​
Badiliko
-6%
Chanzo: EWURA

107​

Mheshimiwa Spika, kushuka kwa bei za mafuta ghafi katika soko la dunia, kulisababisha kushuka kwa wastani wa asilimia 8 ya bei za mafuta yaliyosafishwa ambapo bei ya mafuta ya petroli ilishuka kwa asilimia 1, dizeli kwa asilimia 13 na mafuta ya taa/ndege kwa asilimia 10. Hadi kufikia Machi 2024, bei za mafuta yaliyosafishwa katika soko la Dunia kwa wastani zilikuwa Dola za Marekani 785 kwa tani ya petroli, Dola za Marekani 797 kwa tani ya dizeli na Dola za Marekani 832 kwa tani ya mafuta ya taa/ndege ikilinganishwa na wastani wa Dola za Marekani 795 kwa tani ya mafuta ya petroli, Dola za Marekani 919 kwa tani ya dizeli na Dola za Marekani 925 kwa tani ya mafuta ya taa/ndege katika kipindi kama hicho mwaka 2022/23. Kielelezo Na.9 ni wastani wa mwenendo wa bei za mafuta yaliyosafishwa katika Soko la Dunia kwa Mwaka 2022/23 na 2023/24

108​

Kielelezo Na.9: Wastani wa Mwenendo wa Bei za Mafuta Yaliyosafishwa katika Soko la Dunia kwa Mwaka 2022/23 na 2023/24

Dola za Kimarekani Kwa Tani

950

900

850

800

750

700
2023/24​
2022/23​
Petroli
Dizeli​
Mafuta ya Taa/Ndege

Chanzo: EWURA

109​

B.2.14 MWENENDO WA BEI ZA MAFUTA KATIKA SOKO LA NDANI

Mheshimiwa Spika,
Serikali kupitia EWURA iliendelea kupanga bei za ndani za mafuta kwa mujibu wa Sheria na Kanuni. Aidha, bei za mafuta nchini zilionesha kutengamaa ikilinganishwa na mwaka uliopita. Mathalani kwa mkoa wa Dar es Salaam wastani wa bei za mafuta kwa kipindi cha Julai 2023 hadi Machi 2024 zilishuka kwa asilimia 7 kwa mafuta ya taa/ndege, asilimia 2 kwa mafuta ya dizeli; na yalipanda kwa asilimia 2 kwa mafuta ya petroli, ambapo wastani wa bei ya petroli kwa lita ilikuwa Shilingi 3,129, dizeli Shilingi 3,113 na mafuta ya taa Shilingi 3,047 ikilinganishwa na wastani wa bei za mafuta hayo kwa kipindi hicho mwaka 2022/23 ambapo zilikuwa petroli Shilingi 3,081, dizeli Shilingi 3,167 na mafuta ya taa Shilingi 3,282 kwa lita.

Mheshimiwa Spika, kuimarika kwa bei nchini kulitokana na kushuka kwa bei ya mafuta ghafi kwenye soko la Dunia, hatua zilizochukuliwa na Serikali za kutoruhusu kutumia fedha za kigeni zilizopo ndani ya nchi kulipia mafuta yanayokwenda nchi jirani (transit cargoes) pamoja na kuruhusu kutumia aina tofauti za fedha za kigeni kuagiza mafuta yanayotumika nchini. Kielelezo Na. 10 kinaonesha wastani wa mwenendo wa bei za mafuta nchini.

110​

Kielelezo Na.10: Wastani wa Mwenendo wa Bei za Mafuta

Nchini

Chanzo: EWURA

B.2.15 KUIMARISHA UTENDAJI KAZI NA UTOAJI HUDUMA

Mheshimiwa Spika,
Wizara iliendelea kukamilisha Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Ofisi za Wizara katika Mji wa Serikali Mtumba unaotekelezwa na Mkandarasi- Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ambapo hadi kufikia Machi, 2024 ujenzi huo ulifikia asilimia 75.1 na matarajio ya Wizara ni kuhamia katika jengo hilo katika mwaka

111​

2023/24. Ukamilishwaji wa jengo hilo ni hatua ya kuhakikisha Watumishi wanakuwa na mazingira bora ya utekelezaji wa majukumu kwa tija na ufanisi.

Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha Taasisi zilizo chini ya Wizara zinaimarisha utendaji kazi na utoaji wa huduma, Wizara ilisimamia watumishi kujisajili katika mfumo mpya wa Usimamizi na Utendaji kazi katika Utumishi wa Umma (PEPMIS). Aidha, Wizara iliendelea kuwajengea uwezo watumishi wake pamoja na Taasisi zilizo chini yake ambapo jumla ya watumishi 59 walipatiwa mafunzo ya muda mrefu na watumishi 3,048 walipatiwa mafunzo ya muda mfupi katika kada mbalimbali ndani na nje ya nchi. Kati ya hao, watumishi wa Wizara walikuwa 53, TANESCO 2,320, TPDC 248, REA 100, PURA 51, PBPA 48 na EWURA 228.

Mheshimiwa Spika, Serikali iliendelea kuimarisha utendaji wa Taasisi zote zilizo chini ya Wizara ili zifanye kazi kwa tija inayotarajiwa. Kufuatia hatua ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuteua Wenyeviti wa Bodi ya Wakurugenzi ya REA na TANESCO, Wizara iliteua Wajumbe wa Bodi hizo ili kuimarisha usimamizi na utendaji kazi wa Taaasisi hizo.

112​

B.2.16 MAFANIKIO YALIYOPATIKANA KATIKA UTEKELEZAJI WA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA 2023/24

Mheshimiwa Spika,
mafanikio mbalimbali yamepatikana katika utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara ya Nishati kwa mwaka 2023/24. Mafanikio hayo ni pamoja na:

Uwezo wa mitambo ya kufua umeme iliyounganishwa katika mfumo wa Gridi ya Taifa umeongezeka na kufikia MW 2,138 Machi, 2024 kutoka MW 1,872.1 zilizozalishwa mwaka 2022/23, ikiwa ni ongezeko la asimia 14.2;

Kuanza kwa uzalishaji wa umeme kupitia Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Maji wa Julius Nyerere (JNHPP) wenye uwezo wa kuzalisha MW 2,115 ambapo tayari uzalishaji umeanza kwa MW 235 kupitia mtambo Namba 9. Aidha, matarajio ni mradi huu kukamilika Desemba, 2024 kwa mitambo yote nane

yenye uwezo wa kuzalisha MW 235 kila moja kuwa inazalisha umeme;

Kukamilisha ujenzi wa mitambo ya kufua umeme ya Kinyerezi I Extension MW 185 ambapo kwa sasa mitambo yote minne (4) inafua umeme kiasi cha

113​

MW 40 kila mmoja unaoigizwa katika gridi ya Taifa;

Miundombinu ya kusafirisha umeme imeongezeka na kufikia jumla ya urefu wa kilomita 7,745.4 ikiwa ni ongezeko la asilimia 21.7 ikilinganishwa na kilomita 6,363.3 za mwaka 2022/23;

Kuanza kutumika kwa njia ya kusafirisha umeme wa Kilovoti 400 kutoka JNHPP hadi Chalinze pamoja na kituo kipya cha kupoza umeme cha Chalinze cha Kilovoti 400/220/132 kinachotumika kupoza na kusafirisha umeme unaotoka JNHPP na kuingizwa kwenye Gridi ya Taifa;

Kukamilika kwa asilimia 99 kwa Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa Kilovoti 220 kutoka Morogoro hadi Dodoma kwa ajili ya uendeshaji wa treni ya umeme (SGR Lot II);

Kukamilika kwa asilimia 99.4 kwa Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa Kilovoti 400 kutoka Singida
– Arusha – Namanga. Aidha, ujenzi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa Kilovoti 400 kutoka Arusha hadi

114

Namanga yenye urefu wa kilomita 114.3 umefikia asilimia 97.5 na kituo cha kupoza umeme cha Lemugur kimekamilika kwa asilimia 100 na kuwashwa;

Miundombinu ya kusambaza umeme imeongezeka na kufikia kilomita 176,750.9, ikiwa ni ongezeko la asilimia 4.9 ikilinganishwa na kilomita 168,548.5 za mwezi Mei, 2023;

Jumla ya wateja 4,784,297 wameunganishiwa umeme hadi kufikia Machi, 2024 ikiwa ni ongezeko la asilimia 9.4 ikilinganishwa

na wateja 4,319,258 waliokuwa wameunganishiwa umeme Juni, 2023;

Kuweka mifumo ya kisasa ya mawasiliano katika vituo tisa (9) vya kupoza umeme ili viendeshwe kidigitali (unmanned substations) ambapo kituo kimoja cha Buzwagi kimekamilika;

Jumla ya vijiji 11,837 sawa na asilimia 96.37 ya vijiji vyote 12,318 vya Tanzania Bara vimeunganishwa na umeme hadi kufikia Machi, 2024;

Kuandaliwa na kuidhinishwa na Baraza la Mawaziri kwa Mkakati wa Taifa wa

115

Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia wa mwaka 2024 - 2034. Mkakati huu ni nyenzo muhimu ya kuhakikisha angalau asilimia 80 ya watanzania kuwa wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034 kwa kutatua vikwazo mbalimbali vinavyokwamisha matumizi ya nishati hiyo ikiwa ni pamoja na gharama kubwa, upatikanaji hafifu na uhaba wa miundombinu yake; kukosekana kwa elimu ya kutosha kuhusu madhara ya nishati zisizo safi na salama za kupikia pamoja na baadhi ya mila, desturi na tamaduni zinazochochea matumizi ya nishati zisizo safi na salama za kupikia;

Kuzinduliwa kwa Programu ya Nishati

Safi ya Kupikia inayoloenga Kuwawezesha Wanawake Barani Afrika Kutumia Nishati Safi ya Kupikia (African Women Clean Cooking Support Programme – AWCCSP), iliyozinduliwa Desemba 2023 katika Mkutano wa 28 wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP 28) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan; na

116

Kufanikisha ununuzi wa asilimia 20 ya hisa za Kampuni ya Wentworth kwenye Mkataba wa Uendeshaji wa Kitalu cha Uzalishaji gesi asilia cha Mnazi Bay kilichopo Mtwara. TPDC imeongeza uwekezaji katika kitalu hicho kwa asilimia 20;

B.2.17 CHANGAMOTO ZILIZOPO NA UTATUZI WAKE

Mheshimiwa Spika,
pamoja na mafanikio yaliyopatikana katika mwaka 2023/24, Sekta ya Nishati ilikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo zifuatazo:

Uzalishaji wa umeme na gesi asilia kutoendana na mahitaji kutokana na ukuaji wa shughuli za kiuchumi na kijamii. Aidha, uchakavu wa miundombinu ya kusafirisha na kusambaza umeme imekuwa ikichangia pia kutokidhi mahitaji ya upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa wananchi. Kutokana na hatua zilizochukuliwa na Serikali, ikiwemo kuharakisha utekelezaji wa miradi ya uzalishaji wa umeme pamoja na kukarabati na kufanya matengenezo ya miundombinu ya umeme, hali ya upatikanaji wa umeme nchini unaokidhi mahitaji

117​

imeendelea kuimarika hadi kufikia Machi, 2024.

Aidha, Serikali iliendelea kuchukua hatua za kuimarisha upatikanaji wa gesi asilia, ikiwa ni pamoja na kukarabati na kuongeza msukumo wa gesi asilia kwenye visima na mabomba katika Kitalu cha Songo Songo; kutoboa maeneo mapya ya kuzalishia gesi asilia (perforation) katika visima viwili (2) na kuchoronga visima viwili katika kitalu cha Mnazi Bay; pamoja na uendelezaji wa kitalu cha Ruvuma katika eneo la Ntorya.

b) Vitendo vya hujuma/uhalifu katika miundombinu ya umeme. Serikali inaendelea​

kuwachukulia hatua za kisheria wanaobanika kutekeleza vitendo hivyo na inaendelea kutoa wito kwa wananchi wasio na nia njema kuacha vitendo hivyo, kwa kuzingatia hasara na usumbufu mkubwa unaojitokeza kwa watumiaji wa umeme kutokana na vitendo hivyo.

Changamoto ya upatikanaji wa Dola za Marekani kwa ajili ya kulipia mafuta

yaliyoagizwa nchini iliyosababisha wafanyabishara kupunguza kiasi cha mafuta kilichokuwa kinaagizwa. Ili kukabiliana na hali hiyo, Serikali kupitia Wizara ya Nishati

118

kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha, Benki Kuu ya Tanzania na wadau wengine ilichukua hatua mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kufanya mapitio ya mikataba ya kuagiza mafuta na kuruhusu matumizi ya fedha za kigeni zikiwemo fedha ya Uingereza (British Pound), Umoja wa Ulaya (Euro) na Umoja wa Nchi za Uarabuni (Dirham). Aidha, Wizara ya Nishati kupitia EWURA iliimarisha ukaguzi katika vituo vya mafuta ili kuhakikisha mafuta yanapatikana wakati wote katika maeneo yote nchini.

C. MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA 2024/25

Mheshimiwa Spika,
baada ya kutoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Wizara kwa mwaka 2023/24, sasa napenda kuwasilisha Mpango na Bajeti kwa Mwaka 2024/25.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2024/25 utekelezaji wa majukumu ya Wizara

utaongozwa na vipaumbele mbalimbali vinavyojikita katika kuendelea kutekeleza miradi ya uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa umeme ikiwa ni pamoja na kufikisha gridi ya Taifa katika mikoa iliyosalia; kupeleka nishati vijijini, ikiwemo katika vitongoji; kutekeleza miradi ya kielelezo na kimkakati ya mafuta na gesi asilia ikiwemo mradi

119​

wa Kuchakata na Kusindika Gesi Asilia kuwa Kimiminika (Liquefied Natural Gas – LNG Project), ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta kutoka Hoima, Uganda hadi Tanga, Tanzania (East African Crude Oil Pipeline - EACOP) na upelekaji wa gesi asilia katika nchi jirani za Kenya, Uganda, Zambia na Malawi. Aidha, Wizara itaendelea kutekeleza shughuli za utafiti na uendelezaji wa mafuta na gesi asilia katika vitalu vya kimkakati; usambazaji wa gesi asilia viwandani, katika taasisi na majumbani na kuimarisha matumizi ya CNG katika magari.

Mheshimiwa Spika, vipaumbele vingine ni kuendelea kuimarisha matumizi ya nishati safi ya kupikia (clean cooking) nchini pamoja na upatikanaji wa nishati ya mafuta vijijini kupitia uanzishwaji wa vituo vya mafuta katika maeneo hayo; kuhakikisha nchi inaendelea kuwa na uhakika wa upatikanaji wa bidhaa za mafuta ya petroli pamoja na ufanisi katika kushughulikia upatikanaji wa bidhaa hizo; kuimarisha uwekezaji na ushiriki wa Sekta Binafsi katika shughuli za utafutaji na uendelezaji wa mafuta na gesi asilia pamoja na uzalishaji na usambazaji wa umeme na kuendelea kuimarisha utoaji wa huduma, tija na ufanisi katika uendeshaji wa Taasisi/Mashirika yaliyo chini ya Wizara ya TANESCO, TPDC, EWURA, PURA na PBPA pamoja na Kampuni Tanzu. Wizara pia itaendelea kuimarisha ushiriki

120​

wa wazawa katika shughuli za mafuta na gesi asilia pamoja na rasilimali watu ya Wizara ya Taasisi zake na upatikanaji wa vitendea kazi muhimu.

Mheshimiwa Spika, Mpango na Bajeti ya Wizara kwa mwaka 2024/25 pamoja na mambo mengine, umezingatia Dira ya Taifa ya Maendeleo ya Mwaka 2025, Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (FYDP III) 2021/22 – 2025/26, Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa Ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020, Maagizo ya Viongozi wa Kitaifa katika Sekta ya Nishati, Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2024/25 pamoja na Mpango Mkakati wa Wizara wa Miaka Mitano (2021/22 - 2025/26). Miongozo mingine iliyozingatiwa ni Sera, Mikakati na Programu mbalimbali za Kisekta na Kitaifa pamoja na Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (SDGs) ya mwaka 2030 kuhusu masuala ya nishati.

C.1 SEKTA NDOGO YA UMEME NA NISHATI JADIDIFU

C.1.1 MIRADI YA KUZALISHA UMEME

Mheshimiwa Spika,
kama nilivyoeleza awali, moja ya kazi kubwa iliyopo mbele yetu ni kuhakikisha nchi yetu inakuwa na umeme wa kutosha kwa kuzingatia mahitaji ya sasa na ya

121​

baadaye kutokana na kasi ya ukuaji wa uchumi na maendeleo ya kijamii. Ili kutimiza azma hiyo Wizara imepanga kutekeleza miradi mbalimbali ya uzalishaji wa umeme kama ifuatavyo:

Miradi ya Kuzalisha Umeme Iliyopo Katika Hatua za Utekelezaji

Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Maji wa Julius Nyerere

(JNHPP)–MW 2,115

Mheshimiwa Spika,
kazi zilizopangwa kutekelezwa katika mwaka 2024/25 ni pamoja na kukamilisha ujenzi wa jengo la mitambo (power house) na ufungaji wa mitambo saba (7) ambayo ipo katika hatua mbalimbali za ukamilishwaji. Jumla ya Shilingi bilioni 620 fedha za ndani zimetengwa ili kukamilisha mradi huu.

Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Gesi Asilia wa Kinyerezi

Mheshimiwa Spika,
kazi zilizopangwa kutekelezwa kwa mwaka 2024/25 ni pamoja na kukamilisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa kilovoti 132 yenye urefu wa kilomita 19.2 kutoka kituo cha kuzalisha umeme cha Kinyerezi kwenda Gongolamboto hadi Mbagala Jijini Dar es Salaam na kufunga transfoma maeneo

122​

ya Gongolamboto na Mbagala, ikiwemo kukamilisha kazi za mitambo ya uzalishaji zilizobaki kwa uangalizi.

kazi zilizopangwa kufanyika ni pamoja na uangalizi wa njia ya kusafirisha umeme kwa kipindi cha matazamio (defect liability period) hadi Aprili 2025, pamoja na kufanya malipo ya mwisho (retention money). Jumla ya Shilingi Bilioni 4 fedha za ndani zimetengwa.

mradi huu unahusu ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme wa MW 49.5 kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Malagarasi, mkoani Kigoma kwa gharama ya Dola za Marekani Milioni 144.14 (sawa na Shilingi bilioni 364.67) na unatekelezwa kwa ufadhili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB). Serikali inaendelea na ujenzi wa Bwawa la kuzalisha umeme pamoja na njia ya kusafirisha na kusambaza umeme. Jumla ya Shilingi bilioni 5.1

123​

fedha za nje zimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huu.

Mradi wa Kuzalisha Umeme Jua Shinyanga – MW 150

Mheshimiwa Spika,
Serikali itakamilisha ujenzi wa mitambo ya kuzalisha umeme kwa kutumia nishati ya jua wa MW 150. Ujenzi unaendelea na unatarajiwa kamilika Januari, 2025.

Serikali itakamilisha ukarabati wa miundombinu ya kuzalisha umeme katika Kituo cha Hale ili kiwe na uwezo wa kuzalisha MW 21. Jumla ya Shilingi bilioni 1.3 fedha za ndani zimetengwa kwa kazi hiyo.

182. Mheshimiwa Spika, mradi huu unalenga kujenga Bwawa la kuzalisha umeme MW 87.8 kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Kagera, mkoani Kagera na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa Kilovoti 220 yenye urefu wa kilomita 38.7. Kazi zilizopangwa ni

124​

kukamilisha malipo ya fidia kwa wananchi wanaopisha mradi, kupata Mkandarasi Mjenzi na kuanza utekelezaji wa mradi.

Miradi ya Kuzalisha Umeme Iliyopo katika Hatua za Maandalizi

Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Maji ya mto Kikonge–MW 321

Mheshimiwa Spika,
Serikali inalenga kujenga kituo cha kuzalisha umeme wa MW 321 kwa kutumia maporomoko ya maji ya mto Ruhuhu mkoani Ruvuma na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 220 yenye urefu wa kilomita 96 kutoka Kikonge hadi kituo cha kupoza umeme cha Madaba. Kazi zitakazofanyika ni kuendelea na tathmini ya Athari ya Mazingira, uwekaji wa mipaka katika eneo la uzalishaji wa umeme, usanifu wa kina na maandalizi ya nyaraka za zabuni za mradi (bwawa la kuzalisha umeme na njia ya kusafirisha umeme). Jumla ya Shilingi milioni 500 fedha za ndani zimetengwa.

125​

184. Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme wa MW 358 kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Ruhudji na njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa Kiloviti 400 yenye urefu wa kilomita 170 kutoka Ruhudji mkoani Njombe hadi kituo cha kupoza umeme cha Kisada mkoani Iringa. Gharama za ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme zinakadiriwa kuwa Dola za Marekani millioni 867.41 na njia ya kusafirisha umeme Dola za Marekani millioni 100. 9. Kazi zitakazotekelezwa ni pamoja na kulipa fidia kwa wananchi wanaopisha eneo la mradi, ujenzi wa miundombinu wezeshi ya barabara na kuendelea na taratibu za kupata ufadhili wa mradi. Kiasi cha Shilingi bilioni 37 fedha za ndani zimetengwa.

Mheshimiwa Spika, mradi unahusu ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme wa MW 222 kwa kutumia maji ya Mto Rumakali mkoani Njombe na njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 220 yenye urefu wa kilomita 65 kutoka kwenye mitambo hadi kituo cha kupoza umeme cha Iganjo mkoani Mbeya. Gharama za mradi huu

1

kwa pamoja zinakadiriwa kuwa Dola za Marekani milioni 612.78 kwa upande wa mitambo ya kufua umeme. Gharama za njia ya kusafirisha umeme ni Dola za Marekani milioni 21.72. Kazi zitakazotekelezwa ni pamoja na kulipa fidia kwa wananchi wanaopisha eneo la mradi, ujenzi wa miundombinu wezeshi na kuendelea na taratibu za kupata ufadhili wa mradi. Kiasi cha Shilingi bilioni 2 fedha za ndani zimetengwa.​

Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Gesi Asilia wa Mtwara (MW 300)

Mheshimiwa Spika, mradi huu unalenga ujenzi wa mitambo ya kufua umeme wa MW 300 kwa kutumia gesi asilia mkoani Mtwara pamoja na ujenzi wa njia za kusaifirisha umeme ya Kilovoti 400 kutoka Mtwara hadi Somangafungu na vituo vya kupoza umeme ili kuimarisha upatikanaji wa umeme nchini ikiwemo katika mikoa ya Mtwara na Lindi. Kazi zitakazotekelezwa ni pamoja na kukamilisha malipo ya fidia kwa wananchi watakaopisha eneo la ujenzi wa kituo cha kufua umeme pamoja ya njia ya kusafirisha umeme na kutafuta fedha za ujenzi wa mradi. Jumla ya Shilingi bilioni 2.55 fedha za ndani zimetengwa kwa kazi hiyo.

Mradi wa Kinyerezi III wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Gesi Asilia MW 600

Mheshimiwa Spika, mradi huu unalenga kuzalisha umeme wa MW 600 katika eneo la Kinyerezi III. Kwa sasa Serikali inaendelea na taratibu za upatikanaji wa fedha/ufadhili na kuanza taratibu za ununuzi. Jumla ya Shilingi milioni 200 fedha za ndani zimetengwa kwa kazi hiyo.

Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Upepo MW 100 Kititimo Mkoani Singida

Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu ujenzi wa mitambo ya kuzalisha umeme MW 100 kwa kutumia upepo pamoja na njia ya kusafirisha umeme ya kilomita 8 ya msongo wa kilovoti 220 na kituo cha kupoza umeme. Gharama za mradi huu zinakadiriwa kuwa Dola za Marekani milioni 153. Kazi zitakazotekelezwa ni pamoja na upembuzi yakinifu, kufanya tathmini ya mali za wananchi watakaopisha mradi pamoja na kutafuta fedha/ufadhili na kuanza taratibu za ununuzi. Jumla ya Shilingi bilioni 3 fedha za ndani zimetengwa kwa kazi hiyo.

Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Jua MW 100 Wilaya ya Manyoni

Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu ujenzi wa mitambo ya kuzalisha umeme wa MW 100 kwa kutumia jua pamoja na kituo cha kupoza umeme Wilayani Manyoni. Gharama za mradi huu kwa pamoja zinakadiriwa kuwa Dola za Marekani milioni 120. Kazi zitakazotekelezwa ni pamoja na upembuzi yakinifu, kufanya tathmini ya mali za wananchi watakaopisha mradi na kulipa fidia. Serikali inaendelea kutafuta fedha/ufadhili na kuanza taratibu za manunuzi. Jumla ya Shilingi milioni 400 zimetengwa kwa kazi hiyo.

Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa kutumia Jua MW 60 Zuzu Dodoma

Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu ujenzi wa mitambo ya kuzalisha umeme wa MW 60 kwa kutumia jua Mkoani Dodoma. Gharama za mradi huu kwa pamoja zinakadiriwa kuwa Dola za Marekani milioni 77.66. Kazi zitakazotekelezwa ni pamoja na upembuzi yakinifu na kuanza utekelezaji. Serikali inaendelea kutafuta fedha/ufadhili na kuanza taratibu za ununuzi. Jumla ya Shilingi milioni 25 fedha za ndani zimetengwa kwa kazi hiyo.

C.1.2 MIRADI YA KUSAFIRISHA NA KUSAMBAZA UMEME

Mheshimiwa Spika, umeme ukishazalishwa, hauna budi kusafirishwa ili kuweza kuwafikia walaji, hivyo upatikanaji wa umeme wa uhakika ni pamoja na kuwa na miundombinu madhubuti ya usafirishaji na usambazaji wa umeme pamoja na vituo vya kupoza umeme. Kutokana na changamoto ya muda mrefu ya miundombinu chakavu na isiyotosheleza ya kusafirisha na kusambaza umeme, Serikali itaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya usafirishaji na usambazaji wa umeme katika mwaka 2024/25 kama ifuatavyo:

Miradi ya Kusafirisha na Kusambaza Umeme Iliyopo Katika Hatua za Utekelezaji

Mradi wa Kusafirisha Umeme kutoka Julius Nyerere Hydro Power Plant hadi Chalinze – Kilovoti 400 na Kituo cha Kupoza Umeme, Chalinze

Mheshimiwa Spika,
mradi unahusu ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa kilovoti 400 kutoka JNHPP hadi Chalinze na kituo cha kupoza umeme cha Chalinze Kilovoti 400/220/132. Kazi zitakazotekelezwa ni pamoja na kumalizia kazi zilizobaki katika kituo cha kupoza umeme ikiwemo majengo, barabara, njia ya kusafirisha umeme na marekebisho mbalimbali. Shilingi bilioni 2 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya kazi hiyo.

Ujenzi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa Kilovoti 400 kutoka Chalinze – Dodoma

193. Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 400 kutoka Chalinze hadi Dodoma yenye urefu wa kilomita 345 na upanuzi wa vituo vya kupoza umeme vya Chalinze na Dodoma. Kazi zitakazotekelezwa ni pamoja na kuendelea na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme na vituo vya kupoza umeme. Jumla ya Shilingi bilioni 245 fedha za ndani zimetengwa kwa kazi hiyo.

Ujenzi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa Kilovoti 400 kutoka Chalinze - Kinyerezi - Mkuranga

Mheshimiwa Spika, awamu ya kwanza ya mradi huu inahusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 400 kutoka Chalinze, Kinyerezi hadi Mkuranga na vituo vya kupoza umeme vya Chalinze, Kinyerezi, Mkuranga na Morogoro. Kazi zitakazotekelezwa ni pamoja na kuendelea na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme na vituo vya kupoza umeme. Jumla ya Shilingi bilioni 7 fedha za ndani zimetengwa kwa kazi hizo.

Ujenzi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa Kilovoti 400 kutoka Chalinze – Segera na Msongo wa Kilovoti 220 Segera – Tanga

Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 400 kutoka Chalinze – Segera na Msongo wa Kilovoti 220 Segera – Tanga, na ujenzi wa vituo vya kupoza umeme vya Segera na Tanga. Kazi zitakazotekelezwa ni pamoja na kukamilisha malipo ya fidia, kuanza ununuzi wa Wakandarasi na kuanza ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme na vituo vya kupoza umeme. Jumla ya Shilingi bilioni 4.21 zitatumika kwa ajili ya kulipa fidia kwa wananchi watakaopisha mradi.

Ujenzi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa Kilovoti 220 kutoka Chalinze – Bagamoyo hadi Ununio Dar es salaam

Mheshimiwa Spika, mradi unahusu ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 220 kutoka Chalinze – Bagamoyo hadi Ununio na ujenzi wa vituo vya kupoza umeme vya Bagamoyo na Ununio. Kazi zitakazotekelezwa ni pamoja na kukamilisha malipo ya fidia, kuanza manunuzi ya Wakandarasi na kuanza ujenzi wa njia ya kusafirisha na vituo vya kupoza umeme. Jumla ya Shilingi bilioni 4.3 fedha za ndani zimetengwa kwa kazi hiyo.

Ujenzi wa Kituo cha Kupoza Umeme cha Ibadakuli Shinyanga Kilovoti 400/220/33

Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu ujenzi wa kituo cha kupoza umeme cha msongo wa Kilovoti 400/220/33 Ibadakuli - Shinyanga. Gharama ya mradi huu ni Dola za Marekani milioni 50. Serikali itaendelea kutekeleza mradi huu ambapo kazi zilizopangwa kufanyika ni pamoja na ununuzi wa vifaa na nyenzo zote zinazohitajika kwa ajili ya utekelezaji wa mradi. Jumla ya Shilingi bilioni 37.5 fedha za ndani zimetengwa.

Ujenzi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa Kilovoti 400 kutoka Iringa hadi Sumbawanga kupitia Mbeya na Tunduma (TAZA)

Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 400 kutoka Iringa kupitia Mbeya, Tunduma hadi Sumbawanga yenye urefu wa kilomita 620 pamoja na ujenzi wa vituo vya kupoza umeme vya Kisada (Iringa), Iganjo (Mbeya), Tunduma na Sumbawanga. Aidha, mradi huu unalenga pia kuunganisha Gridi ya Taifa na Nchi za Kusini mwa Afrika (Southern African Power Pool

– SAPP)
. Kazi zitakazotekelezwa ni pamoja na kuendelea na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme na vituo vya kupoza umeme ikiwemo kukamilisha ulipaji wa fidia. Jumla ya Shilingi bilioni 51 fedha za nje zimetengwa kwa kazi hizo.

Mradi wa Kuboresha Utendaji Kazi wa TANESCO (Corporate Management System – CMS)

Mhesimiwa Spika, mradi huu unalenga kuboresha hali ya utendaji kazi wa TANESCO kwa kuanzisha mifumo itakayowezesha kuongeza ufanisi wa utendaji kazi. Mradi huu ni sehemu ya Mradi wa Tanzania – Zambia Interconnector Transmission Project (TAZA). Gharama za mradi huu ni Dola za Marekani milioni 34.8 sawa na Shilingi bilioni 81.61. Kazi zilizopangwa kufanyika ni pamoja na kumalizia kazi za ufungaji wa vifaa vya miundombinu vya mradi (data center infrastructure) na kufanyiwa majaribio utendaji wake. Aidha, mafunzo kwa wafanyakazi wote yataendelea kutolewa. Jumla ya Shilingi bilioni 25.9 fedha za nje zimetengwa kwa ajili ya kutekeleza kazi zilizopangwa.

Ujenzi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa Kilovoti 400 kutoka Nyakanazi hadi Kigoma

Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kiloviti 400 kutoka Nyakanazi hadi Kigoma yenye urefu wa kilomita 280, ujenzi wa kituo cha kupoza umeme Kidahwe Mkoani Kigoma, upanuzi wa kituo cha kupoza umeme cha Nyakanazi na usambazaji umeme katika vijiji 18 vilivyopo katika eneo la mradi. Utekelezaji wa mradi wa njia ya kusafirisha umeme umefikia asilimia 94.98. Kazi zitakazotekelezwa ni kuendelea na ujenzi wa kituo cha kupoza umeme cha Nyakanazi na Kidahwe na miundombinu ya usambazaji umeme katika vijiji vinavyopitiwa na mradi.

Mradi wa Kuimarisha Gridi ya Taifa (National Grid Stabilization Project)

– Gridi Imara

Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu utekelezaji wa awamu ya kwanza ya miradi 27 ya uimarishaji wa miundombinu ya umeme katika mikoa mbalimbali ikiwa ni pamoja na ujenzi wa njia za kusafirisha umeme za msongo wa kilovoti 220 na 132 na kuongeza uwezo wa nyaya za kusafirisha umeme (re -conductoring), ujenzi wa njia za kusambaza umeme za msongo wa kilovoti 33, ujenzi wa vituo vya kupoza umeme na kuongeza uwezo wa baadhi ya vituo na ujenzi wa vituo vya kupoza umeme katika maeneo ya

usambazaji (switching station ). Kazi zitakazofanyika ni kuendelea kulipa fidia kwa wananchi wanaopisha miradi, ujenzi wa njia za kusafirisha umeme na vituo vya kupoza umeme. Mradi unatarajiwa kukamilika Desemba 2025. Jumla ya Shilingi bilioni 200 fedha za ndani zimetengwa.

Mradi wa Ukarabati na Uboreshaji wa Gridi ya Taifa (Grid Rehabilitation and Upgrading)-TTGRUP

Mheshimiwa Spika, mradi huu unalenga kuimarisha Gridi ya Taifa kwa kukarabati na kuboresha vituo vya kupoza umeme katika maeneo mbalimbali nchini na unafadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) pamoja na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kazi zitakazofanyika ni ukamilishaji wa usanifu, uagizaji wa vifaa na kukamilisha mradi.

Ujenzi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa Kilovoti 220 kutoka Benaco hadi Kyaka

Mheshimiwa Spika, mradi huu unalenga ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 220 kutoka Benaco hadi Kyaka yenye urefu wa kilomita 166.17. Gharama za mradi ni Dola za Marekani milioni 105.4 sawa na Shilingi bilioni 263.5. Kazi zitakazofanyika ni kulipa fidia, kuanza kazi za usanifu, utafiti wa udongo, uagizaji wa vifaa na kuanza kazi za ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme na vituo vya kupoza umeme vya Benaco na Kyaka. Jumla ya Shilingi bilioni 5.4 fedha za nje na Shilingi bilion 6.2 fedha za ndani zimetengwa.

Ujenzi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa Kilovoti 220 kutoka Makutopora hadi Tabora kwa ajili ya Uendeshaji wa Treni ya Umeme (SGR Lot 3)

Mhesimiwa Spika, mradi huu unahusu ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 220 yenye urefu wa kilomita 347 kutoka Makutopora hadi Tabora kwa ajili ya uendeshaji wa treni ya umeme. Gharama za mradi huu zinakadiriwa kuwa ni Dola za Marekani milioni 90.65 sawa na Shilingi bilioni 212.58. Kazi zitakazofanyika ni pamoja na ukamilishaji wa upembuzi yakinifu ikiwemo tathmini ya mazingira, kufanya uthamini wa mali za wananchi watakaopisha mradi, kulipa fidia na kuanza taratibu za kupata Wakandarasi. Jumla ya Shilingi bilioni 15 zimetengwa kupitia Fungu la SGR.

Ujenzi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa Kilovoti 220 kutoka Tabora hadi Isaka kwa ajili Uendeshaji wa Treni ya Umeme (SGR Lot 4)

Mhesimiwa Spika, mradi huu unahusu ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 220 yenye urefu unaokadiriwa kuwa kilomita 195 kutoka Tabora hadi Isaka kwa ajili ya uendeshaji wa treni ya umeme. Gharama za mradi huu inakadiriwa kuwa Dola za Marekani milioni 56.1 sawa na Shilingi bilioni 131.7. Kazi zitakazofanyika ni pamoja na ukamilishaji wa upembuzi yakinifu ikiwemo tathmini ya mazingira, kufanya uthamini wa mali za wananchi wataopisha mradi, kulipa fidia, na kuanza taratibu za kupata Wakandarasi. Jumla ya Shilingi bilioni 10 zimetengwa kupitia Fungu la SGR.

Mradi wa Njia ya Kusafirishi Umeme Msongo wa Kilovoti 220 kutoka Mwanza hadi Isaka kwa ajili ya Uendeshaji wa Treni ya Umeme (SGR Lot V)

Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 220 yenye urefu wa kilomita 230 kutoka Mwanza hadi Isaka kwa ajili ya uendeshaji wa treni ya umeme. Kazi zitakazotekelezwa ni ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme na kuendelea na malipo ya fidia. Jumla ya Shilingi Bilioni 14 zimetengwa kupitia Fungu la SGR kwa ajili ya malipo ya fidia na Shilingi bilioni 45 za utekelezaji wa mradi.

Miradi ya Kusafirisha na Kusambaza Umeme Iliyopo Katika Hatua za Maandalizi

Ujenzi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa Kilovoti 400 Kutoka Sumbawanga hadi Kigoma Kupitia Mpanda (Km 480) na Kituo cha Kupoza Umeme Mpanda

Mheshimiwa Spika,
kazi zitakazotekelezwa ni pamoja na kufanya tathmini ya mali za wananchi watakaopisha mradi pamoja kuweka mipaka ya mkuza wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Sumbawanga kupitia Mpanda hadi Kigoma, na kutafuta fedha za kutekeleza mradi. Jumla ya Shilingi milioni 600 fedha za ndani zimetengwa kutekeleza kazi hizo.

Ujenzi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa Kilovoti 400 Kutoka Segera – Same – Lemugur (Kisongo) Arusha

Mheshimiwa Spika,
mradi unahusu ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa kilovoti 400 kutoka Segera – Same – Lemugur (Kisongo) Arusha na kituo cha kupoza umeme kilovoti 220/132/33 cha Mwanza. Kazi zilizopangwa kutekelezwa ni kukamilisha Upembuzi Yakinifu, Athari za Mazingira na Jamii (ESIA), usanifu wa mradi, kufanya tathmini ya mali za wananchi watakaopisha mradi, kuanza kulipa fidia na kuendelea kutafuta fedha za utekelezaji wa mradi. Jumla ya Shilingi bilioni 9 fedha za ndani zimetengwa kutekeleza kazi hizo.

Ujenzi wa Njia ya Kusafirisha Umeme (Submarine Cable) Msongo wa Kilovoti 220 Kutoka Tanzania Bara (Ununio) hadi Zanzibar (Unguja)

Mhesimiwa Spika, Serikali kupitia Mshauri Mwelekezi itakamilisha Upembuzi Yakinifu, Athari za Mazingira na Jamii (ESIA) na usanifu wa mradi. Aidha, Serikali itaendelea kutafuta fedha za kutekeleza mradi huu.

Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Kupoza Umeme Manyoni (Manyoni Substation - MVA 60)

Mhesimiwa Spika, Serikali itakamilisha kazi ya tathmini ya mali za wananchi watakaopisha mradi, na kulipa fidia. Aidha, itaendelea na taratibu za kutafuta fedha kiasi cha Dola za Marekani milioni 16.36 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi pamoja na kutafuta Mkandarasi Mjenzi. Jumla ya Shilingi milion 500 fedha za ndani zimetengwa kutekeleza kazi hizo.

Mradi wa Kusafirisha Umeme Msongo wa Kilovoti 400 kutoka Tanzania hadi Uganda (Masaka - Ibadakuli)-UTIP

Mheshimiwa Spika, mradi unahusu ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti kutoka Tanzania hadi Uganda (Masaka - Ibadakuli) yenye urefu wa kilomita 617 na kituo cha kupoza umeme Kilovoti 220/33 cha Kyaka. Serikali itakamilisha kazi ya kufanya uthamini wa mali za wananchi watakaopisha mradi na kuanza kulipa fidia na pia itaendelea na taratibu za kutafuta fedha za utekelezaji wa mradi kiasi cha Dola za Marekani milioni 383.9. Jumla ya Shilingi bilioni 20 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya utekelezaji.

Miradi ya Ujenzi wa Njia ya Kusafirisha Umeme kwa Ajili ya Kuunga Gridi ya Taifa na Nchi za Jirani kwa Msongo wa Kilovoti 400 Kutoka Tanzania Hadi Malawi (TAMA); Kilovoti 400 Kutoka Tanzania Hadi Msumbiji (MOTA) na Kilovoti 400 Kutoka Tanzania hadi DRC

Mheshimiwa Spika, miradi hii inahusu ujenzi wa njia za kusafirisha umeme kwa ajili ya kuunga Gridi ya Taifa na nchi za jirani kwa msongo wa Kilovoti 400 kutoka Tanzania hadi Malawi (TAMA); Kilovoti 400 kutoka Tanzania hadi Msumbiji (MOTA) na Kilovoti 400 kutoka Tanzania hadi DRC. Kazi zitakazofanyika ni kufanya uthamini wa mali na Upembuzi Yakinifu. Serikali itaendelea kutafuta fedha za kutekeleza kazi hizo. Jumla ya Shilingi milioni 800 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya utekelezaji.

Mradi wa Kuboresha Mfumo wa Usambazaji Umeme Msongo wa Kilovoti 220 katika Jiji la Dodoma, Mbeya, Arusha, Mwanza

Mheshimiwa Spika, lengo kuu la mradi huu ni kuandaa Mpango Kabambe wa Usambazaji umeme utakaoiongoza TANESCO kuendelea kutekeleza miradi ya usambazaji umeme ili kukidhi ongezeko la mahitaji ya umeme na kupunguza upotevu wa umeme katika njia za usambazaji katika Majiji hayo. Aidha, mpango huu unalenga kuongeza upatikanaji wa umeme wa uhakika (reliability). Vilevile, mradi huu unahusisha ujenzi wa njia za mzunguko (ring circuirts) za kusafirisha umeme wa msongo wa Kilovoti 220 na ujenzi wa vituo vipya vya kupoza umeme pamoja na upanuzi wa vituo vya kupoza umeme vilivyopo. Kwa kuwa utekelezaji wa miradi hii inahitaji fedha nyingi, maandalizi ya utekelezaji yameanza na Majiji manne ambayo ni Arusha, Mwanza, Dodoma na Mbeya. Kazi zitakazofanyika ni kuendelea na shughuli ya upembuzi yakinifu.​

Mradi wa Kuboresha Mfumo wa Usambazaji Umeme katika Jiji la Dodoma

Mheshimiwa Spika, Serikali imekusudia kulibadilisha jiji la Dodoma kimazingira kwa kuhakikisha miundombinu ya umeme haiwi sehemu ya vitu vinavyolifanya jiji hilo kutokuwa na muonekano mzuri. Kwa kuzingatia hilo, Serikali imeanza maandalizi ya mradi wa kubadilisha miundombinu ya usambazaji umeme kwa kutumia nguzo na kuelekea kwenye miundombinu ya usambazaji inayopita chini ya ardhi. Aidha, mradi huu unalenga kuboresha miundombinu ya usambazaji katika jiji la Dodoma kwa kubadilisha njia za kusambazia umeme pamoja na transfoma zake. Vilevile, katika utekelezaji wa mradi huu, kutakuwa na upanuzi wa vituo vidogo vilivyopo katikati ya jiji ili kuviongezea uwezo. Hatua hii itawezesha kuendelea kusambaza umeme wenye kukidhi mahitaji kwa wateja wapya wanaoongezeka katikati ya jiji. Hata hivyo mradi huu upo katika hatua za awali na tayari Exim Bank ya Korea imeonyesha nia ya kuufadhili na kufanya upembuzi yakinifu. Kazi zinazotarajiwa kufanyika katika mwaka 2024/25 ni upembuzi yakinifu pamoja na kuandaa usanifu wa awali wa mradi. Kiasi cha Shilingi milioni 200 za ndani zimetengwa.

Mradi wa Ujenzi wa Vituo vya Kupoza Umeme katika Kila Wilaya Nchini

Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu ujenzi wa vituo vya kupoza umeme vya Gridi ya Taifa katika Wilaya zote nchini. Mradi utatekelezwa chini ya mradi wa Gridi imara katika awamu tano (5) ambapo katika kila awamu vitajengwa vituo vya kupoza umeme kumi na tano (15). Utekelezaji wa mradi unalenga kuboresha miundombinu ya usambazaji na kupunguza upotevu wa umeme unaotokana na umbali mrefu wa njia za usambazaji umeme katika maeneo mbalimbali nchini. Gharama za mradi zinakadiriwa kuwa Shilingi trilioni 4.20.

216. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2024/25, Serikali kupitia TANESCO itaanza utekelezaji wa mradi huu kwa kufanya Upembuzi Yakinifu wa mradi, Tathmini ya Athari kwa Mazingira na Jamii, tathmini ya mali za wananchi watakaopisha mradi, na kuanza kutafuta fedha za ujenzi wa mradi. Serikali imetenga Shilingi bilioni 5.4 kwa ajili ya utekelezaji wa kazi hizo. Kiambatisho Na.11 ni mchanganuo wa miradi itakayotekelezwa katika kila Wilaya kwa kila awamu.

C.1.3 MIRADI MINGINE ITAKAYOTEKELEZWA

YA MATENGENEZO YA MITAMBO

Mheshimiwa Spika,
TANESCO kupitia mapato yake ya ndani itafanya matengenezo kinga katika vituo vya kuzalisha umeme, kufanya matengenezo makubwa na madogo katika miundombinu ya kusafirisha, kusambaza na vituo vya kupoza umeme. Aidha, Shirika litaendelea kutekeleza miradi inayolenga kuongeza uwezo wa miundombinu ya kusafirisha umeme, kuboresha mifumo ya uendeshaji Gridi, kuweka mifumo ya kisasa ya mawasiliano katika vituo vya kupoza umeme, kujenga vituo vidogo vya kuendesha Gridi (unmanned substations) na kuweka mfumo wa “Advance Metering Infrastructure-AMI” wa kufunga Mita Janja (Smart Meter).

Mheshimiwa Spika, TANESCO pia itatekeleza miradi ya kupeleka umeme katika maeneo mbalimbali pamoja na kufanya maboresho kwenye miundombinu ya usambazaji ili kuondoa adha za kuwa na umeme mdogo kwa wananchi na kuunganisha wateja wapya. Jumla ya Shilingi bilioni 959.792 fedha za ndani zimetengwa kutumika kwa ajili ya kazi hizo ili kuimarisha uwezo wa miundombinu ya kuzalisha, kusafirisha na kusambaza umeme iliyopo.

C.1.4 UTENDAJI WA KAMPUNI TANZU ZA TANESCO (TCPM NA ETDCO)

Kampuni ya Ujenzi na Ukarabati wa

Miundombinu ya Usafirishaji na Usambazaji Umeme (ETDCO)

Mheshimiwa Spika,
Serikali kupitia kampuni tanzu ya TANESCO ya ETDCO, imepanga kukamilisha utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 132 kutoka Tabora hadi Urambo na kutoka Urambo hadi Kidahwe Mkoani Kigoma. Aidha, ETDCO itakamilisha utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini katika Mikoa ya Geita na Kigoma inayosimamiwa na REA. Vilevile, ETDCO imepanga kujenga mradi wa njia ya kusafirisha Umeme Kilovoti 220 Masasi – Mahumbika yenye urefu wa kilometa 128 katika mikoa ya Mtwara na Lindi.

Kampuni ya Kutengeneza Nguzo za Zege Tanzania (TCPM)

Mheshimiwa Spika, Kampuni ya TCPM inatarajia kuzindua kiwanda chake cha kwanza cha kuzalisha nguzo za zege Mkoani Tabora. Kampuni itaendelea kuingia ushirikiano (joint venture) na Wawekezaji binafsi ili kuongeza uzalishaji na upatikanaji wa nguzo za zege na kurahisisha zoezi la usafirishaji wa nguzo hizo katika maeneo mbalimbali nchini.

Kampuni ya Uendelezaji wa Rasilimali ya Jotoardhi (TGDC)

Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2024/25 Serikali kupitia TGDC itatekeleza yafuatayo:

Itakamilisha uchorongaji wa visima vitatu (3) vya uhakiki (exploratory wells) ili kuhakiki hifadhi, kiwango na ubora wa rasilimali ya jotoardhi katika mradi wa Ngozi (Mbeya) wenye uwezo wa kuzalisha MW 30 katika awamu ya kwanza pamoja na kuanza ujenzi wa mtambo mdogo wa kuzalisha umeme (wellhead generator) wa MW 5. Jumla ya Shilingi bilion 2.9 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa kazi hizo.

ii. Itaanza utekelezaji wa programu ya uchorongaji wa visima vinne (4) vya uhakiki, kutekeleza miradi ya matumizi mengineyo pamoja na maandalizi ya upatikanaji wa mtambo wa kuzalisha umeme katika mradi la Kiejo Mbaka (Mbeya) wenye uwezo wa kuzalisha MW 60. Jumla ya Shilingi bilioni 14. 56 zimetengwa kwa ajili ya ukamilishaji wa shughuli hizo;

Itakamilisha taratibu za umiliki wa ardhi na maandalizi ya uchorongaji wa visima vinne (4) vya uhakiki katika mradi wa Songwe (Songwe) wa MW 5. Jumla ya Shilingi milioni 560 zimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa kazi hizo;

Kufanya maandalizi ya programu ya uchorongaji wa visima vitatu (3) vya uhakiki pamoja na kufanya upembuzi yakinifu wa matumizi mengineyo katika eneo la mradi wa Luhoi (Pwani) MW 5. Jumla ya Shilingi milioni 350 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya kutekeleza kazi hizo; Kukamilisha utafiti wa kina wa kijiosayansi wa juu ya ardhi (detailed surface exploration) pamoja na ununuzi wa vifaa vya kufanya tafiti katika eneo la mradi la Natron MW 60 (Arusha) ambapo jumla ya Shilingi bilioni 1.28 zimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa kazi husika;

Kufanya utafiti wa kina wa kijiosayansi wa juu ya ardhi (detailed surface exploration) katika eneo la mradi wa Meru (Arusha) wa MW 60 pamoja na kuajiri Mshauri Mwelekezi kwa ajili ya kufanya kazi ya utafiti huo. Jumla ya Shilingi milioni 700 zimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa kazi husika; na

Kuratibu Kongamano la 10 la Jotoardhi (African Rift Geothermal Conference-ARGeo C-
litakalofanyika Novemba, 2024 Jijini Dar es Salaam.

C.1.5 USHIRIKISHWAJI WA SEKTA BINAFSI KATIKA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA UMEME

Mheshimiwa Spika,
Serikali kupitia TANESCO itaendelea na taratibu za kutekeleza miradi ya kufua umeme inayotarajiwa kutekelezwa na wawekezaji binafsi, ikiwemo miradi ya umeme jadidifu na vyanzo vingine. Wawekezaji binafsi wanaendelea kukaribishwa kujitokeza katika kutekeleza miradi ya upepo, jua, makaa ya mawe, maji na gesi katika maeneo mbalimbali nchini. Kazi zitakazofanyika kwa mwaka 2024/25 ni uchambuzi, uthamini na ulipaji wa fidia katika maeneo ya miradi, kutangaza zabuni na kuingia mikataba ya makubaliano na wawekezaji binafsi pamoja na kufanya upembuzi yakinifu.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa miradi ya usafirishaji wa umeme, Serikali kupitia TANESCO itaendelea kuwashirikisha wawekezaji binafsi katika utekelezaji wa miradi hii, hususan katika maeneo ya viwanda na migodi. Kazi zitakazofanyika ni uchambuzi wa maeneo ya miradi na kuingia makubaliano na wawekezaji binafsi kwa utekelezaji wa miradi hiyo.

C.1.6 MIRADI YA NISHATI VIJIJINI

Mheshimiwa Spika,
Katika Mwaka 2024/25, Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini itaendelea kuchukua hatua za kupeleka nishati vijijini ili kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi na maendeleo ya kijamii katika maeneo hayo. Ili kutekeleza azma hiyo, Serikali kupia Wakala wa Nishati Vijijini itatekeleza miradi ifuatayo:

Mradi wa Kupeleka Umeme katika Vitongoji 20,000

Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusisha ujenzi wa miundombinu ya kusambaza umeme katika vitongoji 20,000 ambavyo bado havijafikiwa na miundombinu ya umeme. Jumla ya Shilingi bilioni 350 fedha za ndani zimetengwa. Kazi zitakazofanyika ni pamoja na kuandaa kabrasha la zabuni, ununuzi wa wakandarasi, kufanya usanifu wa kina wa mradi na kuanza ujenzi wa miundombinu ya mradi.

Mradi wa Kupeleka Umeme Katika Vitongoji katika Mkoa wa Songwe na Kigoma

Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusisha ujenzi wa miundombinu ya kusambaza umeme katika vitongoji 677 vya Mkoa wa Kigoma na Songwe ili kuwezesha ujenzi wa njia za umeme Msongo wa Kati zenye urefu wa kilomita 726.24; ujenzi wa njia za umeme wa Msongo Mdogo zenye urefu wa kilomita 1,308; ufungaji wa transfoma 653 pamoja na kuunganisha wateja wa awali 14,352. Kazi zitakazofanyika ni kukamilisha ujenzi wa miundombinu ya kusambaza umeme Msongo Mdogo, kufunga transfoma na kuunganisha wateja. Jumla ya Shilingi bilioni 26.60 kutoka Shirika la Fedha Duniani (IMF) kupitia dirisha la Extended Credit Facility zimetengwa kwa ajili ya kukamilisha utekelezaji wa mradi.

Mradi wa Kupeleka Umeme katika Vitongoji 3,060

Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusisha ujenzi wa miundombinu ya kusambaza umeme katika vitongoji 3,060 ikiwa ni vitongoji 15 kila Jimbo, ujenzi wa njia za umeme Msongo wa Kati zenye urefu wa kilomita 258; ujenzi wa njia za umeme wa Msongo Mdogo zenye urefu wa kilomita 6,118; ufungaji wa transfoma 3,060 pamoja na kuunganisha wateja wa awali 100,947. Kazi zitakazofanyika ni kuendelea na ujenzi wa miundombinu ya mradi, kufunga transfoma na kuunganisha wateja.

Mradi wa Ujazilizi Awamu ya Pili B ( Densification IIB)

Mheshimiwa Spika, mradi huu unalenga kupeleka umeme kwenye vitongoji 1,686 katika mikoa 9 ya Arusha, Geita, Kagera, Katavi, Kigoma, Lindi, Morogoro, Njombe na Songwe ambapo kazi za ujenzi zinahusisha ujenzi wa njia za msongo mdogo zenye urefu wa kilomita 3,860, ufungaji wa transfoma 1,272 na kuunganisha wateja wa awali 95,334. Katika Mwaka 2024/25, Wakala wa Nishati Vijijini utaendelea kukamilisha kazi za ujenzi wa miundombinu ya mradi, kufunga transfoma na kuunganisha wateja. Jumla ya Shilingi bilioni 25.40 fedha za nje zimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa kazi hizo.

Mradi wa Ujazilizi Awamu ya Pili C (Densification IIC)

Mheshimiwa Spika, mradi huu umelenga kufikisha huduma za umeme kwenye vitongoji 1,880 katika mikoa 7 ya Manyara, Iringa, Rukwa, Mtwara, Ruvuma, Simiyu na Mara ili kujenga kilomita 5,640 za Msongo Mdogo, kufunga transfoma 1,880 na kuunganisha wateja wa awali 94,000. Katika Mwaka 2024/25, Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini itakamilisha kazi za ujenzi wa njia za umeme Msongo Mdogo, kufunga transfoma na kuunganisha wateja. Jumla ya Shilingi bilioni 2.41 fedha kutoka Benki ya Dunia zimetengwa ili kukamilisha kazi hizo.

Mradi wa Kupeleka Umeme Katika Maeneo ya Vijijini-Miji (Peri Urban)

Mheshimiwa Spika, mradi huu unalenga kutekelezwa katika mikoa 8 ya Geita, Kigoma, Kagera, Mbeya, Mtwara, Singida, Tabora na Tanga ambapo jumla ya maeneo 416 yatafikishiwa huduma ya umeme kupitia ujenzi wa njia za umeme wa Msongo wa Kati zenye urefu wa kilomita 379; ujenzi wa njia za umeme wa Msongo Mdogo zenye urefu wa kilomita 753; ufungwaji wa transfoma 314 pamoja na kuunganisha wateja wa awali 16,369 kwa gharama ya Shilingi bilioni 76.9 kutoka Serikali ya Tanzania. Katika Mwaka 2024/25, kazi zilizopangwa kufanyika ni ujenzi wa njia za umeme Msongo wa Kati na Mdogo, kufunga transfoma na kuunganisha wateja ambapo Shilingi bilioni 2 fedha za ndani zimetengwa.

Mradi wa Kusambaza Umeme katika Migodi Midogo, Maeneo ya Kilimo na Viwanda

Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu kupeleka umeme katika maeneo 581 ya wachimbaji wadogo wa madini, maeneo ya kilimo na viwanda Tanzania Bara kupitia ujenzi wa njia za Msongo wa Kati zenye urefu wa kilomita 1,370; ujenzi wa njia za umeme wa Msongo Mdogo zenye urefu wa kilomita 1,097; ufungwaji wa transfoma 517 pamoja na kuunganisha wateja wa awali 17,119. Katika Mwaka 2024/25, Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini itaendelea kukamilisha kazi za kupeleka umeme katika jumla ya maeneo ya migodi, kilimo na viwanda 581 ambapo Shilingi bilioni 5.00 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya kukamilisha kazi hizo.

Mradi wa Kupeleka Umeme Katika Minara ya Mawasiliano ya Simu

Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu kupeleka umeme katika minara 754 ya mawasiliano katika maeneo mbalimbali nchini. Katika Mwaka 2024/25, Wakala wa Nishati Vijijini utaendelea kushirikiana na Universal Communications Services Access Fund (UCSAF) ili kupelekea umeme katika minara ya mawasiliano kwenye maeneno ya vijijini ambapo Shilingi bilioni 12.00 fedha za ndani zimetengwa .

Mradi wa Ufungaji wa Mifumo ya Umeme Jua kwenye Makazi Yaliyopo Visiwani na Yaliyopo Mbali na Gridi ya Taifa

Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu kufunga na kusambaza mifumo itakayozalisha umeme kwa kutumia nishati ya jua katika makazi yaliyo vijijini ambayo hayatafikiwa na gridi ya Taifa kwa kufunga mifumo ipatayo 7,000. Gharama za mradi ni Shilingi bilioni 9.4. Katika Mwaka 2024/25, kazi zitakazotekelezwa ni kutangaza mradi, kufanya tathmini ya maombi yaliyowasilishwa, kufanya due diligence, na kuanza kutekeleza mradi ambapo Shilingi bilioni 3.53 fedha kutoka Benki ya Dunia zimetengwa.

Mradi wa Kusambaza Majiko Banifu kwenye Kaya Zilizopo katika Maeneo ya Vijijini na Vijiji-Miji

Mheshimiwa Spika, mradi huu unalenga kusambaza majiko banifu katika maneo ya vijijini na vijiji-miji (Peri Urban). Mradi utasambaza majiko banifu 70,000 yaliyotengenezwa kwa teknolojia yenye ubunifu wa kupunguza matumizi ya kuni na mkaa pamoja na kupunguza uharibifu wa mazingira. Gharama za mradi ni Shilingi bilioni 14.10. Katika Mwaka 2024/25, Wakala wa Nishati Vijijini utaandaa kabrasha la

mradi na kutangaza ili kuwapata wazalishaji/wasambazaji wa majiko, kufanya tathmini ya maombi yaliyowasilishwa, kufanya due diligence, na kuanza kutekeleza mradi ambapo Shilingi bilioni 4.7 kutoka Benki ya Dunia zimetengwa.

Utekelezaji wa Awamu ya Pili ya Mpango wa Kuhamasisha Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia

Mheshimiwa Spika, Mpango huu unahusisha ujenzi wa miundombinu ya nishati ya kupikia katika taasisi za umma na binafsi ambazo zinahudumia zaidi ya watu 300 kwa siku. Kazi zitakazotekelezwa ni pamoaja na kutoa ruzuku kwa wazalishaji wa mkaa mbadala kwa ajili ya ununuzi

156​

wa mashine zitakazotumika katika uzalishaji; kutoa ruzuku kwa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) ili waweze kununua na kufunga mashine mbili (2) za kuzalisha mkaa bora wa kupikia kutokana na makaa ya mawe, kutoa ruzuku kwa Jeshi la Magereza kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya nishati ya kupkia katika maeneo 211 pamoja na kumpata Mshauri Mwelekezi wa kufanya tathmini ya aina za nishati safi ya kupikia zilizopo Tanzania Bara. Tathmini hii itahusisha pia kuainisha teknolojia zilizopo, nishati safi zilizopo, watoa huduma (waendelezaji au wasambazaji) wa nishati safi ya kupikia waliopo, na kupendekeza aina ya mifumo ya ufadhili ili kufikisha nishati ya kupikia katika maeneo husika.

236. Mheshimiwa Spika, mpango wa kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia utahusisha kutoa elimu kupitia makongamano, semina na vyombo vya habari kuhusu madhara ya nishati chafu na manufaa ya matumizi ya nishati iliyo safi katika kipikia. Jumla ya Shilingi bilioni 24.5 ya fedha ndani zimetengwa.

l) Mpango wa Utoaji Ruzuku kwa Waendelezaji wa Miradi ya Nishati Jadidifu

Mheshimiwa Spika,
Mpango huu unahusisha kuchangia gharama za uendelezaji wa gridi ndogo (mini grids) kwa kutoa ruzuku ili kuzalisha umeme unaotokana na nishati jadidifu. Mpango unahusisha ujenzi wa mitambo ya kufua umeme yenye uwezo wa hadi kufikia Megawati 10 kutoka vyanzo vya maji, jua, upepo na tungamotaka. Jumla ya Shilingi bilioni 10 fedha za ndani zimetengwa.

m) Mradi wa Uwezeshaji Upanuzi wa

Miundombinu ya Msongo Mdogo (Distribution Network ) na Ujenzi wa “Interconnection Line” kwa Waendelezaji Wadogo

Mheshimiwa Spika,
mradi huu unahusisha kutoa ruzuku kwa waendelezaji wa miradi ya nishati vijijini ili waweze kujenga miundombinu ya kuunganisha umeme kutoka kwenye chanzo kwenda kwenye miundombinu ya TANESCO na kusambaza umeme katika vitongoji vinavyoendelezwa na Waendelezaji wa Miradi (Franchaise Area under Standardized Power Purchase Agreement). Kazi zilizopangwa kutekelezwa ni kuchambua maombi yatakayowasilishwa, kufanya due diligence na kusaini mikataba kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya mradi ambapo Shilingi bilioni 15 fedha za ndani zimetengwa.

Ukuzaji na Uhamasishaji wa Ufanisi wa Matumizi Bora ya Nishati Pamoja na Matumizi ya Umeme katika Uzalishaji

Mheshimiwa Spika, kazi hii itahusisha kumpata mtoa huduma wa kukuza na kuhamasisha ufanisi wa matumizi bora ya nishati ikiwemo vifaa vinavyotumia umeme, tabia ya watumiaji kuhusu matumizi sahihi katika uzalishaji mali kwa kutumia umeme. Kazi zitakazotekelezwa ni pamoja na kumtafuta Mshauri Mwelekezi wa kuandaa Mkakati wa kuhamasisha Matumizi bora ya Umeme katika uzalishaji mali katika maeneo yaliyounganishwa na umeme vijijini. Hatua hii itawezesha kuongeza thamani katika maeneo yaliyopelekewa umeme kupitia miradi mbalimbali ya umeme. Jumla ya Shilingi bilioni 2 fedha za ndani na Shilingi bilioni 1.50 fedha kutoka Benki ya Dunia zimetengwa.

Tathmini ya utekelezaji wa Miradi ya Umeme Vijijini

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia REA inatarajia kufanya tathmini mbalimbali ili kuhuisha na kuandaa nyaraka za kitalaamu zitakazoongoza jitihada za uendelezaji na utekelezaji wa miradi ya kusambaza nishati vijijini. Kazi zitakazofanyika ni pamoja na kutafuta Washauri Elekezi kwa ajili ya kuandaa upembezi yakinifu wa kuibua aina za Nishati Jadidifu katika kutekeleza miradi ya umeme vijijini; kufanya tathmini ya vijiji na vitongoji vyote visivyo na umeme na vinavyohitaji ujazilizi katika maeneo yote ya visiwani; na Mshauri Mwelekezi wa kusimamia mradi wa ufungaji wa mifumo midogo ya umeme jua pamoja na gridi ndogo katika maeneo ya vijijini hususan visiwani. Jumla ya Shilingi bilioni 7.5 kutoka Benki ya Dunia zimetengwa.

C.1.6 UTEKELEZAJI WA MIKAKATI NA

MIPANGO MBALIMBALI YA UENDELEZAJI WA SEKTA NDOGO YA UMEME NA NISHATI JADIDIFU

Mheshimiwa Spika,
ili kuendeleza Sekta Ndogo ya Umeme na Nishati Jadidifu nchini, Serikali kupitia Wizara ya Nishati itakamilisha kuandaa mipango na mikakati mbalimbali ili ianze kutekelezwa. Kazi zitakazofanyika ni pamoja na kukamilisha uhuishaji wa Mpango Kabambe wa Kuendeleza Sekta Ndogo ya Umeme (Power System Master Plan 2020) pamoja na kuendelea kutekeleza Mpango Kabambe wa Kupeleka Nishati Vijijini (Rural Energy Master Plan) ambao umejikita katika kupeleka nishati ya umeme katika vitongoji na nishati safi ya kupikia katika maeneo ya vijijini.

Mheshimiwa Spika, kazi nyingine zitakazotekelezwa ni kuendelea kusimamia na kuratibu utekelezaji wa Programu ya Nishati Safi ya Kupikia inayoloenga Kuwawezesha Wanawake Barani Afrika Kutumia Nishati Safi ya Kupikia (African Women Clean Cooking Support Programme – AWCCSP; Mkakati wa Taifa wa Nishati Safi ya Kupikia (2024-2034) pamoja na mradi wa Matumizi Bora ya Nishati na Mkakati wa Maboresho katika Sekta Ndogo ya Umeme (Electricity Supply Industry Reform Strategy and Roadmap – ESI-RSR). Pia Serikali kupitia Wizara ya Nishati itafanya tathmini ya vyanzo vyote vya nishati jadidifu vilivyopo nchini ili kutambua maeneo vilivyopo na uwezo, teknolojia inayohitajika kuviendeleza na kuandaa ramani kwa lengo la kuviendeleza.​

C.2 SEKTA NDOGO YA MAFUTA NA GESI

Mheshimiwa Spika,
Serikali itaendelea kusimamia na kuendeleza Sekta Ndogo ya Mafuta na Gesi kwa kuchukua hatua mbalimbali, lengo likiwa ni kuhakikisha mchango wa sekta hii katika maendeleo ya Taifa letu unaimarika.
C.2.1 MIRADI YA UTAFUTAJI WA MAFUTA NA GESI ASILIA KATIKA VITALU VYA KIMKAKATI

Kitalu cha Mnazi Bay Kaskazini

Mheshimiwa Spika, taarifa za kitaalamu kuhusu kitalu hiki zimeonesha uwepo wa mashapo yenye uwezekano wa kuwa na gesi asilia. Serikali kupitia TPDC imeshampata mbia wa kimkakati (Maurel & Prom (M&P)) ambaye ameonyesha nia ya kushirikiana katika shughuli za utafutaji na uendelezaji wa kitalu hiki. Kazi zilizopangwa kutekelezwa ni pamoja na uchorongaji wa visima vya utafiti pamoja na kukamilisha taratibu za upatikanaji wa leseni ya utafutaji wa mafuta na gesi asilia. Jumla ya Shilingi bilioni 2, fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya kazi hizi.

Kitalu cha Eyasi – Wembere

Mheshimiwa Spika, TPDC itaendelea na shughuli za utafiti wa awali wa mafuta na gesi asilia katika kitalu cha Eyasi – Wembere ambapo kazi zilizopangwa kutekelezwa ni pamoja na kuendelea na uchukuaji wa taarifa za mitetemo za mfumo wa 2D zenye urefu wa kilomita 1,100 ili kutambua maeneo ambayo visima vya utafutaji vitachorongwa, kutafuta mbia wa kimkakati wa kushirikiana naye katika uwekezaji pamoja na kukamilisha taratibu za upatikanaji wa leseni ya utafutaji wa mafuta na gesi. Jumla ya Shilingi bilioni 2 zimetengwa kwa ajili ya kazi hizi.

C.2.3 MRADI WA KUCHAKATA NA KUSINDIKA GESI ASILIA KUWA KIMIMINIKA (LIQUEFIED NATURAL GAS – LNG)

Mheshimiwa Spika,
lengo la mradi huu ni kuchakata na kusindika gesi asilia iliyogunduliwa katika Vitalu Na.1, 2 na 4 vilivyopo katika kina kirefu baharini ili kuwa kimiminika na kuweza kuuzwa katika soko la dunia. Mradi huu pia utasaidia kuongeza upatikanaji, uzalishaji na usambazaji wa gesi asilia kwa matumizi ya ndani ya nchi.

Mheshimiwa Spika, Serikali inatarajia kukamilisha majadiliano ya Mikataba ya mradi huu na Wawekezaji, ikiwemo Mkataba wa Nchi Hodhi (HGA) na Mkataba wa Ugawanaji Mapato (APSA); kuelimisha wananchi kuhusu umuhimu na manufaa ya mradi; kushiriki katika shughuli za ufuatiliaji na tathmini za mradi; na kushiriki katika utafiti na utoaji elimu ya upatikanaji wa huduma na bidhaa za ndani ikiwemo wataalam watakaohitajika katika mradi. Kazi nyingine zitakazotekelezwa ni kuwezesha uanzishwaji wa ofisi ya mradi na ujenzi wa shule ya msingi Likong’o mkoani. Jumla ya Shilingi bilioni 5 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa kazi hizo.

C.2.4 MIRADI YA UENDELEZAJI, UCHAKATAJI, USAFIRISHAJI NA USAMBAZAJI GESI ASILIA

Ujenzi wa Bomba la Kusafirisha Gesi Kutoka Ntorya katika Kitalu cha Ruvuma hadi Madimba

Mheshimiwa Spika,
mradi huu unahusisha kuendeleza gesi asilia iliyogunduliwa katika eneo la Ntorya katika kitalu cha Ruvuma. Kazi zilizopangwa kutekelezwa ni pamoja na kujenga bomba la kusafirisha gesi asilia kutoka kitalu cha Ruvuma (Ntorya) hadi Madimba lenye urefu wa kilomita 34.2 litakalokuwa na uwezo wa kubeba futi za ujazo milioni 140 kwa siku. Aidha, TPDC imeshapata Mshauri Mwelekezi kwa ajili ya usanifu wa kina na kihandisi. Jumla ya Shilingi bilioni 101.6 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya kuwezesha kazi hizo kutekelezwa.

Ujenzi wa Miundombinu ya Usambazaji wa Gesi Asilia katika Mkoa wa Dar es Salaam, Mtwara, Lindi na Pwani

Mheshimiwa Spika,
mradi huu unahusisha ujenzi wa miundombinu ya kusambaza gesi asilia katika Mikoa ya Dar es Salaam, Mtwara, Lindi na Pwani. Kazi zitakazotekelezwa ni pamoja na kufanya tathmini ya athari kwa mazingira na jamii, usanifu wa kihandisi pamoja na ujenzi wa miundombinu ya kusambaza gesi asilia kwenye viwanda vya Mkuranga pamoja na Kongani ya Viwanda ya Kwala Mkoani Pwani; kukamilisha ujenzi wa vituo vya CNG (Kituo Mama katika eneo la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Vituo vidogo vya Kairuki na Muhimbili) mkoani Dar es Salaam; na ununuzi wa vituo vitano (5) vya CNG vinavyohamishika (mobile CNG stations) vitakavyotoa huduma katika Jiji la Dar es Salaam. Aidha, miradi ya ujenzi wa vituo vya CNG inayotekelezwa na Sekta Binafsi itakayokamilika katika mwaka 2024/25 ni pamoja na kituo cha TAQA kitakachojengwa barabara ya Sam Nujoma; kituo cha Energo kinachoendela kujengwa katika eneo la Mikocheni mkabala na Coca Cola; kituo cha BQ Contractors kitakachojengwa Mbezi Beach karibu na Hospitali ya Masana; na vituo sita (6) vya PUMA vitakavyojengwa barabara ya Mandela, makutano ya barabara Mwenge, Mbezi Tanki Bovu, DART Mbagala, DART Ubungo na Tegeta.

Mheshimiwa Spika, TPDC pia itakamilisha awamu ya kwanza ya mradi wa usambazaji wa gesi asilia chini ya ufadhili wa REA ambapo nyumba zitaunganishwa katika mikoa ya Lindi na Pwani; na kuanza awamu ya pili ya mradi huo kwa kuendelea kusambaza gesi asilia maeneo ya Mkuranga, mkoani Pwani. Jumla ya Shilingi bilioni 28.4 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya miradi hii ya usambazaji gesi katika mikoa minne.

C.2.5 MIRADI YA KUSAFIRISHA GESI ASILIA KWENDA NCHI JIRANI

Mradi wa Bomba la Kusafirisha Gesi Asilia kutoka Tanzania hadi Uganda

Mheshimiwa Spika, kazi zitakazofanyika ni pamoja na kukamilisha nyaraka muhimu za miradi ikiwemo Kanuni za Pamoja za Ununuzi (Joint Procurement Rules) na Hadidu za Rejea za kumpata Mshauri Mwelekezi wa kufanya upembuzi yakinifu wa mradi. Jumla ya Shilingi milioni 483.8 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya kufanikisha shughuli hiyo.

Mradi wa Kusafirisha Gesi Asilia Kutoka Dar es Salaam (Tanzania) hadi Mombasa (Kenya)

Mheshimiwa Spika, kazi zilizopangwa kutekelezwa ni pamoja na uandaaji wa nyaraka za mradi zikiwemo Bilateral Agreements, Joint Procurement Rules & Terms of Reference (ToR) na nyaraka za zabuni ya kumpata Mshauri Mwelekezi wa kufanya upembuzi yakinifu. Jumla ya Shilingi milioni 502.2 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya kuwezesha kazi hizo kutekelezwa.

C.2.6 MIRADI YA KUSAFIRISHA NA KUHIFADHI MAFUTA

Mradi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi kutoka Hoima - Uganda hadi Tanga - Tanzania (East African Crude Oil Pipeline – EACOP)

Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa Mradi wa EACOP unaendelea ambapo kazi zitakazotekelezwa ni pamoja na kuendelea kupokea shehena za mabomba, kuendelea na ujenzi wa bomba la mafuta, ujenzi wa matenki ya kuhifadhia mafuta na jeti katika eneo la Chongoleani na kuendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu utekelezaji wa mradi na fursa zilizopo kwa maeneo yanayopitiwa na mradi na kuendelea kuchangia mtaji na kushirikiana na Wanahisa wengine kukamilisha taratibu za upatikanaji wa fedha za mkopo. Jumla ya Shilingi bilioni 50 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya kufanikisha shughuli hizo.

Mradi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Safi kutoka Dar es Salaam - Tanzania hadi Ndola – Zambia

Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta safi kutoka Dar es Salaam hadi Zambia lenye urefu wa takribani kilomita 1,710 ambalo litatumia mkuza wa bomba la kusafirisha mafuta la TAZAMA. Wamiliki wa bomba tajwa ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Zambia. Kazi zilizopangwa kutekelezwa ni pamoja na kukamilisha idhini ya nyaraka muhimu za mradi na kupata Mshauri Mwelekezi wa kufanya uchambuzi wa kina wa mradi. Jumla ya Shilingi milioni 415.8 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya kutekeleza shughuli hizo.

Ujenzi wa Miundombinu ya Hifadhi ya Kimkakati ya Mafuta Pamoja na Miundombinu ya Kuwezesha Biashara ya Mafuta

Mheshimiwa Spika, uanzishaji wa Hifadhi ya Taifa ya Mafuta ya Kimkakati (SPR) unatekelezwa kwa kujenga maghala ya kuhifadhi mafuta (tank farms) katika maeneo ya kimkakati nchini ili kurahisisha usambazaji wa mafuta. Kazi zitakazotekelezwa ni pamoja na kumpata Mshauri Mwelekezi atakayeandaa Mpango wa Kina (Detailed Road Map) kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya SPR. Jumla ya Shilingi bilioni 3.4 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya kutekeleza shughuli hizo.

Ukarabati wa Tenki Namba 8

Mheshimiwa Spika, kazi zitakazotekelezwa ni kukamilisha tathmini ya athari kwa mazingira na jamii na usanifu wa tenki pamoja na kuanza kazi ya ukarabati wa tenki hilo kwa ajili ya hifadhi ya mafuta. Jumla ya Shilingi bilioni 14.4 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya kutekeleza shughuli hizo.

Ujenzi wa Maghala Sita (6) Eneo la Kigamboni

Mheshimiwa Spika, kazi ya ujenzi wa matenki sita (6) katika eneo la Kigamboni itafanyika kwa awamu ambapo awamu ya kwanza itaanza kwa ujenzi wa matenki matatu yenye uwezo wa kuhifadhi tani 81,000. Jumla ya Shilingi bilioni 49.8 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa maghala hayo.

C.2.7 MRADI WA USIMAMIZI WA RASILIMALI ZA NDANI NA UTAWALA WA RASILIMALI ZA ASILI TANZANIA

Mheshimiwa Spika,
kazi zitakazotekelezwa kupitia mradi huu ni pamoja na kuwezesha Duru ya Tano ya kunadi vitalu vilivyo wazi ili kuvutia uwekezaji katika utafutaji wa mafuta na gesi, kufadhili utafiti na maandalizi ya Mkakati wa Uendelezaji na Uhamasishaji wa matumizi ya gesi ya mitungi (Liquefied Petroleum Gas – LPG) na gesi iliyoshindiliwa (Compressed Natural Gas – CNG), kununua kituo kinachotembea cha kujazia gesi kwenye magari (Mobile CNG Station), kufadhili uanzishaji wa vituo vya kujenga uwezo kwa Wananchi chini ya Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) pamoja na kukamilisha awamu ya mwisho ya programu ya kujenga uwezo kwa Wataalam wa Wizara ya Nishati, PURA, TPDC na Watumiaji wa Mfumo wa Uondoshaji Shehena Mipakani.

C.2.8 MAJUKUMU YATAKAYOTEKELEZWA NA KAMPUNI TANZU ZA TPDC (TANOIL & GASCO)

TANOIL Investments Limited (TANOIL)

Mheshimiwa Spika, TPDC kupitia Kampuni yake tanzu ya TANOIL itaendela kushiriki katika biashara ya mafuta kama kampuni ya kununua na kuuza mafuta (Oil Marketing Company
OMC). Kampuni ya TANOIL imepanga kutumia Shilingi bilioni 240.95 katika biashara hiyo na itaendelea kukamilisha ukarabati wa vituo vitatu

(3) vya Musoma, Tarime (Mara) na Segera (Tanga) pamoja na kujenga kituo kipya kimoja (1) Makuyuni (Arusha) kupitia Kampuni mama (TPDC).

Gas Company (GASCO)

Mheshimiwa Spika, TPDC kupitia kampuni Tanzu ya GASCO itaendelea kuendesha miundombinu ya Taifa ya Gesi Asilia nchini. TPDC kupitia GASCO imepanga kutumia Shilingi bilioni 76.41 kwa ajili ya kulipia gharama za uendeshaji na usimamizi wa miundombinu ya kuchakata gesi asilia iliyoko Songo Songo na Madimba, bomba la gesi asilia kutoka Mtwara na Lindi hadi Dar es Salaam na mtandao wa mabomba ya usambazaji gesi asilia iliyopo Mtwara, Lindi, Pwani na Dar es Salaam.

C.2.9 UDHIBITI WA MASUALA YA MKONDO WA

JUU WA PETROLI KUPITIA PURA

Mheshimiwa Spika,
Serikali kupitia PURA inatarajia kutekeleza Duru ya Tano (5) ya kunadi vitalu vya utafutaji wa mafuta na gesi asilia. Zoezi hili lina lengo la kutangaza kwa wawekezaji vitalu vilivyo wazi vinavyopendekezwa katika eneo la bahari na nchi kavu. Kazi zilizopangwa kutekelezwa ni pamoja na; kuandaa nyaraka za zabuni zitakazoongoza mnada wa vitalu, kufanya maonesho ya kitaalamu kuhusu vivutio vya vitalu na kuzindua Duru ya Tano (5) ya kunadi vitalu. Zoezi la kunadi vitalu linatarajiwa kuzinduliwa mwishoni mwa mwaka 2024 baada ya kukamilika kwa maandalizi yote yanayoendelea. Jumla ya Shilingi bilioni 2 zimetengwa.

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia PURA itaendelea kusimamia shughuli za ukarabati wa visima katika vitalu vya uzalishaji wa gesi asilia pamoja na shughuli za uendelezaji katika Kitalu cha Ruvuma, kufanya mapitio ya kanuni mbalimbali, kuendelea kusimamia, kufanya ukaguzi na kuhakikisha ushiriki wa Watanzania katika Vitalu vyote vya utafutaji na uzalishaji wa gesi asilia nchini pamoja na kusimamia shughuli za awali zinazoendelea katika vitalu Namba 1, 2 & 4 vitakavyohusika katika mradi wa LNG. Jumla ya Shilingi bilioni 1.77 fedha za ndani zimetengwa ili kutekeleza kazi hizi.

C.2.10 UDHIBITI WA MASUALA YA NISHATI KUPITIA EWURA

Mheshimiwa Spika,
EWURA itaendelea kusimamia udhibiti wa huduma za nishati nchini kwa kuwasimamia watoa huduma kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na taratibu zilizopo ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma iliyo bora na uhakika. Pia, ili kufikisha huduma karibu na wananchi EWURA imetenga kiasi cha Shilingi bilioni 1.7 kwa ajili ya kuendelea na taratibu za ujenzi wa Ofisi za Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Kaskazini na Kati.

C.2.11 KUIMARISHA UTENDAJI KAZI NA UTOAJI HUDUMA

Mheshimiwa Spika,
Wizara itaendelea kuchukua hatua madhubuti za kuimarisha taasisi zilizo chini yake ili ziweze kujiendesha kwa tija na ufanisi na kutoa huduma bora kwa wananchi na wadau. Aidha, Wizara inatarajia kuajiri watumishi wapya 56 na kuwahamishia Wizarani watumishi 76 ili kukabiliana na upungufu wa watumishi uliopo. Vilevile, Wizara itaendelea kuwajengea uwezo watumishi kwa kutoa mafunzo ya muda mrefu na mfupi kwa watumishi 4,219.

D. USHIRIKIANO

WA

KIKANDA

NA

KIMATAIFA

Mheshimiwa Spika, katika utekelezaji wa majukumu yake, Wizara ya Nishati inashirikiana na Washirika mbalimbali wa Maendeleo, Jumuiya za Kikanda, nchi wahisani na wadau wengine. Kwa niaba ya Serikali, napenda kuwashukuru Washirika wa Maendeleo, Jumuiya na nchi wahisani ambao wameendelea kushiriki katika kufanikisha utekelezaji wa majukumu ya Wizara na maendeleo ya Sekta ya Nishati kwa ujumla. Napenda kutambua mchango wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB); Benki ya Dunia (WB); Arab Bank for Economic Development in Africa (BADEA); Mfuko wa Uendelezaji wa Economic Development Cooperation Fund (EDCF - Korea); Jotoardhi (Geothermal Risk Mitigation Facility - GRMF) pamoja na Taasisi na Mashirika ya JICA (Japan), KfW (Germany), AFD (Ufaransa); Shirika la Fedha Duniani (IMF); Sida (Sweden), NORAD (Norway); Umoja wa Ulaya (EU), Shirika la Mitaji ya Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNCDF), Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Shirika la Maendeleo la Canada (CIDA) na USAID (Marekani); OPEC Fund for International Development; Abu - Dhabi Fund for Development (ADFD); na Saudi Fund for Developmnet (SFD).

Mheshimiwa Spika, nitumie nafasi hii pia kutoa shukrani kwa Serikali za Afrika Kusini, Algeria, Burundi, Canada, China, DRC Congo, Ethiopia, Falme za Kiarabu, Iceland, India, Japan, Kenya, Korea ya Kusini, Malawi, Marekani, Misri, Morocco, Msumbiji, Namibia, Norway, Rwanda, Sweden, Ufaransa, Uganda, Uingereza, Ujerumani, Zambia, na nchi nyingine kwa ushirikiano wao katika kuendeleza Sekta ya Nishati. Nazishukuru pia Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Umoja wa Afrika (AU) kwa ushirikiano katika masuala ya kikanda yanayohusu Sekta ya Nishati

E. HITIMISHO

Mheshimiwa Spika,
kwa kutambua umuhimu wa nishati katika kuchochea na kuharakisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa Taifa letu, katika mwaka 2024/25 Wizara ya Nishati itaendelea kuchukua hatua madhubuti za kusimamia, kuimarisha na kuendeleza Sekta ya Nishati, kwa lengo la kuhakikisha sekta hii inachangia ipasavyo katika maendeleo ya Taifa letu na watu wake kama inavyotarajiwa.

Mheshimiwa Spika, Wizara itaendelea kuimarisha upatikanaji wa nishati safi ya kupikia mijini na vijijini ili kulinda afya za wananchi na mazingira. Aidha, Wizara itaendelea kuipatia suluhu ya kudumu changamoto ya upatikanaji wa umeme wa uhakika nchini, kuimarisha usambazaji wa nishati hiyo pamoja na kuimarisha uzalishaji wa gesi asilia unaoendana na mahitaji, kwa kuzingatia kiwango cha ugunduzi wa nishati hiyo hadi sasa nchini na hatua za utafutaji zinazoendelea kuchukuliwa. Wizara pia itaendelea kuelekeza nguvu katika kuimarisha utoaji wa huduma mbalimbali zinazotolewa na Taasisi zake.

269. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa

hoja kwamba Bunge lako Tukufu sasa liidhinishe Bajeti ya jumla ya Shilingi Trilioni Moja, Bilioni

Mia Nane Themanini na Tatu, Milioni Mia Saba

175​

Hamsini na Tisa, Mia Nne Hamsini na Tano Elfu (Shilingi 1,883,759,455,000) kwa ajili ya matumizi ya Wizara ya Nishati na Taasisi zake. Mchanganuo wa fedha hizo ni kama ifuatavyo:

Shilingi Trilioni Moja, Bilioni Mia Saba Tisini na Nne, Milioni Mia Nane Sitini na Sita, Mia Nane Thelathini na Mbili Elfu (Shilingi 1,794,866,832,000) sawa na asilimia 95.28 ya Bajeti yote ya Wizara ni kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo. Kati ya fedha hizo, Shilingi Trilioni Moja, Bilioni Mia

Tano Thelathini na Sita na Milioni Ishirini, Mia Mbili Sabini na Nne Elfu (Shilingi 1,536,020,274,000) ni fedha za ndani na
Shilingi Bilioni Mia Mbili Hamsini na Nane, Milioni Mia Nane Arobaini na Sita, Mia Tano Hamsini na Nane Elfu (Shilingi 258,846,558,000) ni fedha za nje; na

Shilingi Bilioni Themanini na Nane, Milioni Mia Nane Tisini na Mbili, Mia Sita Ishirini na Tatu Elfu (Shilingi 88,892,623,000)
sawa na asilimia 4.72 ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida. Kati ya fedha hizo Shilingi Bilioni

Sitini na Tisa, Milioni Mia Tano Ishirini na Nne, Mia Mbili na Moja Elfu (Shilingi 69,524,201,000) ni kwa ajili ya Matumizi Mengineyo (OC) na Shilingi Bilioni Kumi na

Tisa, Milioni Mia Tatu Sitini na Nane, Mia

176​

Nne Ishirini na Mbili Elfu (Shilingi 19,368,422,000) ni kwa ajili ya Mishahara (PE) ya Watumishi wa Wizara na Taasisi zilizo chini yake.

Mheshimiwa Spika, naomba tena nitoe shukrani zangu za dhati kwako na kwa Waheshimiwa
Wabunge wote kwa kunisikiliza. Hotuba hii pia inapatikana katika Tovuti ya Wizara kwa anuani ya www.nishati.go.tz. Vilevile, Hotuba hii ina vielelezo mbalimbali ambavyo vimeambatishwa kwa ajili ya ufafanuzi wa masuala muhimu yanayohusu Sekta ya Nishati.

Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.
 
Attachments

  • FINAL CHAPA 20 APRILI 2024 HOTUBA YA WIZARA YA NISHATI .pdf
    19.1 MB · Views: 11
Bilioni 69 mnalipana kama posho
Bilioni 88.89 ni matumizi ya kawaida? Yapi?
Bilioni 19 ndio mishahara?
Trilioni 1.794 ndo za kupigwa zaidi?

Mwamba alipokata hizo OC na matumizi ya kawaida, walibweka sana! Kumbe ndo ilivyo hivyo!
- Mtumishishi analipwa 800k, anaishi nyumba ya 350k kwa mwezi, anasukuma Subaru Forester daily, weekend hakosekani kidimbwi, kwenye gathering za familia, ukoo na jamii yeye ndio don, kwenye kila kona anasema anazo side hustle na kuwashangaa wengine wanaotegemea mshahara....kumbe mambo ya OC na matumizi ya kawaida + Miradi ya maendeleo

Kwanini 69bn isiwe mishahara kisha 19bn ikawa OC?
 
Wizara ya Nishati imewasilisha Bungeni Bajeti ya Tsh. Trilioni 1.88 kwaajili ya matumizi ya Maendeleo, Matumizi ya Kawaida na Mishara ya Wizara hiyo pamoja na Taasisi zilizo chini yake kwa mwaka 2024/25 ambapo Kati ya Fedha hizo, Tsh. 1,536,020,274,000 ni fedha za ndani na Tsh. 258,846,558,000 ni Fedha za Nje.

Akiwasilisha Bajeti hiyo Bunge, Waziri wa Nishati. Dkt. Dotto Biteko, amesema; Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu sasa liidhinishe Bajeti ya jumla ya Shilingi Trilioni Moja, Bilioni Mia Nane Themanini na Tatu, Milioni Mia Saba Hamsini na Tisa, Mia Nne Hamsini na Tano Elfu (Shilingi 1,883,759,455,000) kwa ajili ya matumizi ya Wizara ya Nishati na Taasisi zake.

Hata hivyo Bajeti hiyo imepungua kutoka Tsh. Trilioni 3 zilizozombwa kutumika katika mwaka 2023/24
View attachment 2972823

Mchanganuo wa fedha hizo ni kama ifuatavyo:

(i) Shilingi Trilioni Moja, Bilioni Mia Saba Tisini na Nne, Milioni Mia Nane Sitini na Sita, Mia Nane Thelathini na Mbili Elfu (Shilingi 1,794,866,832,000) sawa na asilimia 95.28 ya Bajeti yote ya Wizara ni21 kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo. Kati ya fedha hizo, Shilingi Trilioni Moja, Bilioni Mia Tano Thelathini na Sita na Milioni Ishirini, Mia Mbili Sabini na Nne Elfu (Shilingi 1,536,020,274,000) ni fedha za ndani na Shilingi Bilioni Mia Mbili Hamsini na Nane, Milioni Mia Nane Arobaini na Sita, Mia Tano Hamsini na Nane Elfu (Shilingi
258,846,558,000) ni fedha za nje; na

(ii) Shilingi Bilioni Themanini na Nane, Milioni Mia Nane Tisini na Mbili, Mia Sita Ishirini na Tatu Elfu (Shilingi 88,892,623,000) sawa na asilimia 4.72 ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida. Kati ya fedha hizo
Shilingi Bilioni Sitini na Tisa, Milioni Mia Tano Ishirini na Nne, Mia Mbili na Moja Elfu (Shilingi 69,524,201,000) ni kwa ajili ya Matumizi Mengineyo (OC) na Shilingi Bilioni Kumi na Tisa, Milioni Mia Tatu
Sitini na Nane, Mia Nne Ishirini na Mbili Elfu (Shilingi 19,368,422,000) ni kwa ajili ya Mishahara (PE) ya Watumishi wa Wizara na Taasisi zilizo chini yake.

Mheshimiwa Spika, naomba tena nitoe shukrani zangu za dhati kwako na kwa Waheshimiwa Wabunge wote kwa kunisikiliza. Hotuba hii pia inapatikana katika Tovuti ya Wizara kwa anuani ya www.nishati.go.tz. Vilevile, Hotuba hii ina vielelezo mbalimbali ambavyo vimeambatishwa kwa ajili ya ufafanuzi wa masuala muhimu yanayohusu Sekta ya Nishati.
Hakuna sababu ya kuwa na Bajeti kubwa Kwa sababu Mradi wa JNHPP imemalizika,malipo yaliyosalia hayazidi hata 1T.

Kazi kubwa ya Tanesco Kwa Sasa ni Kusambaza umeme na Kuunganisha Mikoa ya off grid.
 
Ukiacha posho ndio hapo hapo wanalipa na wale waliowaajiri Kwa mikataba ,uendeshaji wa ofisi.ikiwemo.ununuzi wa magari,Mafuta nk

Mwisho Tanesco Wana matumizi makubwa sana ya hela za OC na ni Kati ya Taasisi ambazo watu wake wanatambua sana huku mtaani.

Hizo pesa ni nyingi sana
 
Ni jambo jema, hizo fedha zilizopunguzwa zipelekwe NHIF kulipia bima za watanzania wanyonge zisiwe posho za majangili ya nchi.
 
Bilioni 69 mnalipana kama posho
Bilioni 88.89 ni matumizi ya kawaida? Yapi?
Bilioni 19 ndio mishahara?
Trilioni 1.794 ndo za kupigwa zaidi?

Mwamba alipokata hizo OC na matumizi ya kawaida, walibweka sana! Kumbe ndo ilivyo hivyo!
- Mtumishishi analipwa 800k, anaishi nyumba ya 350k kwa mwezi, anasukuma Subaru Forester daily, weekend hakosekani kidimbwi, kwenye gathering za familia, ukoo na jamii yeye ndio don, kwenye kila kona anasema anazo side hustle na kuwashangaa wengine wanaotegemea mshahara....kumbe mambo ya OC na matumizi ya kawaida + Miradi ya maendeleo

Kwanini 69bn isiwe mishahara kisha 19bn ikawa OC?
Watapigaje?
 
Hakuna sababu ya kuwa na Bajeti kubwa Kwa sababu Mradi wa JNHPP imemalizika,malipo yaliyosalia hayazidi hata 1T.

Kazi kubwa ya Tanesco Kwa Sasa ni Kusambaza umeme na Kuunganisha Mikoa ya off grid.
Hizo hela watapeleka kununua ndege wapate sehemu ya kupigia badala ya kuelekeza kwenye kugharamia bima za wanyonge pamoja na elimu
 
Wizara ya Nishati imewasilisha Bungeni Bajeti ya Tsh. Trilioni 1.88 kwaajili ya matumizi ya Maendeleo, Matumizi ya Kawaida na Mishara ya Wizara hiyo pamoja na Taasisi zilizo chini yake kwa mwaka 2024/25 ambapo Kati ya Fedha hizo, Tsh. 1,536,020,274,000 ni fedha za ndani na Tsh. 258,846,558,000 ni Fedha za Nje.

Akiwasilisha Bajeti hiyo Bunge, Waziri wa Nishati. Dkt. Dotto Biteko, amesema; Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu sasa liidhinishe Bajeti ya jumla ya Shilingi Trilioni Moja, Bilioni Mia Nane Themanini na Tatu, Milioni Mia Saba Hamsini na Tisa, Mia Nne Hamsini na Tano Elfu (Shilingi 1,883,759,455,000) kwa ajili ya matumizi ya Wizara ya Nishati na Taasisi zake.

Hata hivyo Bajeti hiyo imepungua kutoka Tsh. Trilioni 3 zilizozombwa kutumika katika mwaka 2023/24
View attachment 2972823

Mchanganuo wa fedha hizo ni kama ifuatavyo:

(i) Shilingi Trilioni Moja, Bilioni Mia Saba Tisini na Nne, Milioni Mia Nane Sitini na Sita, Mia Nane Thelathini na Mbili Elfu (Shilingi 1,794,866,832,000) sawa na asilimia 95.28 ya Bajeti yote ya Wizara ni21 kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo. Kati ya fedha hizo, Shilingi Trilioni Moja, Bilioni Mia Tano Thelathini na Sita na Milioni Ishirini, Mia Mbili Sabini na Nne Elfu (Shilingi 1,536,020,274,000) ni fedha za ndani na Shilingi Bilioni Mia Mbili Hamsini na Nane, Milioni Mia Nane Arobaini na Sita, Mia Tano Hamsini na Nane Elfu (Shilingi
258,846,558,000) ni fedha za nje; na

(ii) Shilingi Bilioni Themanini na Nane, Milioni Mia Nane Tisini na Mbili, Mia Sita Ishirini na Tatu Elfu (Shilingi 88,892,623,000) sawa na asilimia 4.72 ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida. Kati ya fedha hizo
Shilingi Bilioni Sitini na Tisa, Milioni Mia Tano Ishirini na Nne, Mia Mbili na Moja Elfu (Shilingi 69,524,201,000) ni kwa ajili ya Matumizi Mengineyo (OC) na Shilingi Bilioni Kumi na Tisa, Milioni Mia Tatu
Sitini na Nane, Mia Nne Ishirini na Mbili Elfu (Shilingi 19,368,422,000) ni kwa ajili ya Mishahara (PE) ya Watumishi wa Wizara na Taasisi zilizo chini yake.

Mheshimiwa Spika, naomba tena nitoe shukrani zangu za dhati kwako na kwa Waheshimiwa Wabunge wote kwa kunisikiliza. Hotuba hii pia inapatikana katika Tovuti ya Wizara kwa anuani ya www.nishati.go.tz. Vilevile, Hotuba hii ina vielelezo mbalimbali ambavyo vimeambatishwa kwa ajili ya ufafanuzi wa masuala muhimu yanayohusu Sekta ya Nishati.

======

HOTUBA YA NAIBU WAZIRI MKUU NA WAZIRI WA NISHATI MHESHIMIWA DKT. DOTO MASHAKA BITEKO (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA NISHATI KWA MWAKA 2024/25

UTANGULIZI

Mheshimiwa Spika, kufuatia Taarifa iliyowasilishwa leo katika Bunge lako Tukufu na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, naomba kutoa hoja kwamba, Bunge lako Tukufu sasa likubali kupokea, kujadili na kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Taasisi zake kwa mwaka 2024/25.

Mheshimiwa Spika, awali ya yote napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema kwa kunijalia afya njema na fursa ya kusimama mbele ya Bunge lako Tukufu kuwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati kwa Mwaka 2024/25. Aidha, kwa kuwa ni mara yangu ya kwanza kusimama kama Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati katika Serikali ya Awamu ya Sita (6) na kuwasilisha Hotuba hii, kwa namna ya kipekee napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuniamini na kuniteua kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati.

Uteuzi huu ni dhamana na heshima kubwa kwangu katika kuhakikisha kuwa Sekta ya Nishati inakidhi matarajio ya Watanzania ya kupata umeme wa uhakika pamoja na kuendeleza rasilimali za mafuta na gesi kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya nchi yetu. Nitumie fursa hii kuahidi, na kwa kadri Mwenyezi Mungu atakavyoniwezesha, kutekeleza majukumu yangu kwa weledi na uadilifu mkubwa kwa kushirikiana na Bunge lako Tukufu pamoja na wadau wengine katika Sekta ya Nishati.

Mheshimiwa Spika, tarehe 29 Februari, 2024 Taifa letu lilimpoteza aliyekuwa Rais mstaafu wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Ali Hassan Mwinyi. Aidha, kabla ya hapo, tarehe 10 Februari, 2024 Taifa lilimpoteza aliyekuwa Waziri Mkuu mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Edward Ngoyai Lowassa. Kwa masikitiko makubwa naungana na Wabunge wenzangu na wananchi kwa ujumla kutoa pole kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, familia, ndugu, jamaa, marafiki na watanzania wote kwa ujumla kwa kuondokewa na viongozi wetu hawa, tuliwapenda lakini Mwenyezi Mungu amewapenda zaidi. Tunaomba Mwenyezi Mungu azilaze roho za wapendwa wetu mahali pema peponi, Amina.

Mheshimiwa Spika, Julai mosi, 2023, Bunge lako Tukufu lilimpoteza Mhe. Francis Leonard Mtega, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mbarali. Aidha, tarehe 8 Aprili 2024, Bunge lako lilimpoteza Mhe. Ahmed Yahya Abdulwakil aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kwahani, Zanzibar. Naungana na Wabunge wenzangu kutoa pole kwa Bunge lako Tukufu, familia ya marehemu, ndugu, jamaa, marafiki na wote walioguswa na misiba hiyo. Tunaomba Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu wote mahali pema peponi, Amina. Vilevile, naungana na Bunge lako Tukufu na Watanzania kwa ujumla, kuwapa pole watanzania wenzetu waliopatwa na majanga mbalimbali katika mwaka 2023/24, ikiwemo yaliyotokana na mafuriko na maporomoko ya mawe na matope katika maeneo ya Hanang Mkoani Manyara; Kibiti na Rufiji Mkoani Pwani pamoja na Malinyi, Ulanga, Ifakara na Mlimba Mkoani Morogoro.

Mheshimiwa Spika, kipekee nawashukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), kwa uongozi na juhudi zao katika kuleta maendeleo ya Taifa letu na kwa ushirikiano wanaonipa katika kusimamia na kutekeleza majukumu ya Wizara ya Nishati. Nikiri kuwa maelekezo na miongozo ya viongozi wetu hawa ni msingi wa mafanikio ya utekelezaji wa majukumu ya Sekta ya Nishati. Aidha, napenda kumpongeza Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa kuendelea kusimamia kwa umahiri utekelezaji wa shughuli za maendeleo katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Mheshimiwa Spika, napenda kukupongeza kwa dhati wewe binafsi kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU). Hii ni heshima kubwa na Tunu kwa Watanzania wote kwa ujumla kwa kuthaminiwa na kutambuliwa katika medani za kimataifa. Tunakuombea kwa Mwenyezi Mungu ili azidi kukupa nguvu na hekima zaidi katika kutekeleza majukumu yako.

Mheshimiwa Spika, napenda kutumia fursa hii tena kukupongeza wewe binafsi, Naibu Spika na Wenyeviti wa Bunge kwa kuliongoza Bunge letu Tukufu kwa umahiri mkubwa. Aidha, nitumie fursa hii kumpongeza Bi. Nenelwa Mwihambi, Katibu wa Bunge kwa usimamizi wa shughuli za Bunge. Ni dhahiri kuwa, chini ya uongozi wenu Bunge letu limeendelea kutekeleza majukumu yake ya kikatiba ipasavyo katika kuhakikisha kuwa Serikali inatekeleza wajibu wa kuwaletea wananchi maendeleo.

Mheshimiwa Spika, naomba kutumia fursa hii kuwapongeza Mawaziri na manaibu Waziri walioteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan. Nampongeza Mhe. Jerry William Silaa (Mb), aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Mhe. Deogratius John Ndejembi (Mb), aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu); Mhe. Alexander Pastory Mnyeti (Mb), aliyeteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Kilimo; Mhe. David Mwakiposa Kihenzile (Mb), aliyeteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Uchukuzi; Mhe. Dunstan Luka Kitandula (Mb), aliyeteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii; Mhe. Judith Salvio Kapinga (Mb.) aliyeteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Nishati; Mhe. Daniel Baran Sillo (Mb), aliyeteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mhe. Zainab Athuman Katimba (Mb), aliyeteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI. Nawatakia kila la kheri katika utekelezaji wa majukumu yao.

Mheshimiwa Spika, naomba niungane na Waheshimiwa Wabunge wenzangu kumpongeza, Mhe. Bahati Keneth Ndingo, Mbunge wa jimbo la Mbarali kwa kuchaguliwa kwake kwa kishindo kuwa mwakilishi wa wananchi katika jimbo hilo. Hakika ni heshima kubwa uliyopewa na wananchi wa Mbarali na ninakutakia kila la kheri katika kutekeleza jukumu lako la uwakilishi katika Bunge letu Tukufu.

Mheshimiwa Spika, kipekee nampongeza Mhe. Dkt. David Mathayo David (Mb.) kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na Mhe. Kilumbe Shaban Ng’enda (Mb.) kwa kuchaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo. Vilevile, nawashukuru wajumbe wote wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kwa ushauri na maoni yao katika kuendeleza na kusimamia Sekta ya Nishati kwa manufaa ya kiuchumi na kijamii kwa Taifa letu na watu wake.

Mheshimiwa Spika, namshukuru Mhe. Judith Salvio Kapinga (Mb.), Naibu Waziri wa Nishati kwa kuendelea kunisaidia kwa karibu katika kutekeleza majukumu yangu. Aidha, napenda kumshukuru Katibu Mkuu Mha. Felchesmi Jossen Mramba kwa utendaji kazi wake mahiri na ushirikiano anaonipa katika kutekeleza shughuli zangu za kila siku za Wizara. Nampongeza pia, Dkt. James Peter Mataragio kwa kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati. Nawashukuru pia Wakuu wa Idara na Vitengo, Wenyeviti na Wajumbe wa Bodi za Taasisi zilizo chini ya Wizara, Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara na Watumishi wote wa Wizara kwa ujumla kwa ushirikiano na juhudi zao katika kufanikisha kufikiwa kwa malengo ya Wizara.

Mheshimiwa Spika, kipekee kabisa, nitumie fursa hii kuwashukuru wananchi wa Jimbo la Bukombe kwa kuendelea kunipa ushirikiano mkubwa katika kutekeleza majukumu yangu kama Mbunge wao. Kutokana na majukumu ya kitaifa kama Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati kuna wakati wananikosa jimboni, lakini kwa wema wao wanaendelea kunivumilia na kunipa ushirikiano mkubwa. Nawaahidi kuendelea kuwa mtumishi wao mwaminifu katika kutekeleza shughuli za maendeleo. Aidha, namshukuru mke wangu mpendwa Benadetha Clement Mathayo kwa maombi na upendo wake wa dhati kwangu na watoto wetu. Amekuwa mvumilivu katika kipindi chote ninapokuwa natekeleza majukumu yangu ya Ubunge, Uwaziri na Unaibu Waziri Mkuu na kukubali kubeba na kutekeleza baadhi ya majukumu ya kifamilia.

Mheshimiwa Spika, nitumie pia fursa hii kuvishukuru na kuvipongeza Vyombo vya Habari vikiwemo redio, televisheni, magazeti na mitandao ya kijamii kwa ushirikiano mkubwa waliotupatia Wizara ya Nishati kwa mwaka 2023/24. Vyombo hivyo vimekuwa mstari wa mbele katika kufuatilia kwa karibu miradi na shughuli zinazotekelezwa na Wizara ya Nishati na kuelimisha pamoja na kuhabarisha umma kuhusu mafanikio yaliyopatikana. Ni matumaini yangu kuwa, ushirikiano huu utazidi kuimarika katika Mwaka wa Fedha wa 2024/25 kwa manufaa ya Taifa letu na wananchi kwa ujumla katika upatikanaji wa taarifa kuhusu Sekta ya Nishati.

Mheshimiwa Spika, Hotuba hii imeandaliwa kwa kuzingatia maudhui ya Hotuba ya Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu Mapitio ya Utekelezaji wa Kazi za Serikali kwa Mwaka 2023/24 na Mwelekeo wa Kazi za Serikali kwa Mwaka 2024/25.

Mheshimiwa Spika, baada ya utangulizi huo, naomba sasa kuwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara kwa Mwaka 2023/24, pamoja na Mpango na Bajeti ya Wizara kwa Mwaka 2024/25.

B. UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA WIZARA KWA MWAKA 2023/24

Mheshimiwa Spika
, utekelezaji wa majukumu ya Wizara kwa mwaka 2023/24 uliongozwa na vipaumbele mbalimbali vilivyojikita katika kukamilisha miradi mbalimbali ya uzalishaji na usafirishaji wa umeme pamoja na kuendelea kuchukua hatua nyingine za kuimarisha uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa umeme nchini; kuendelea kupeleka umeme vijijini, vitongojini, katika visiwa na maeneo yaliyo mbali na gridi ya Taifa, vituo vya afya na pampu za maji, wachimbaji wadogo wa madini, maeneo ya kilimo na viwanda na katika shule na mahakama za mwanzo vijijini; pamoja na kutekeleza mikakati na programu mbalimbali kuimarisha matumizi ya nishati safi ya kupikia (clean cooking) nchini.

Mheshimiwa Spika, vipaumbele vingine vilikuwa ni kuanza maandalizi ya utekelezaji wa Mradi wa Kuchakata za na Kusindika Gesi Asilia kuwa Kimiminika (Liquefied Natural Gas – LNG); kuendelea na utekelezaji wa Mradi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi kutoka Hoima - Uganda Hadi Tanga – Tanzania (EACOP), shughuli za utafiti wa mafuta na gesi asilia katika vitalu vya Kimkakati, usambazaji wa gesi asilia viwandani, majumbani na nchi jirani, kuimarisha matumizi ya Gesi Asilia Iliyoshindiliwa (Compressed Natural Gas-CNG) katika magari pamoja na kunadi vitalu (licencing round) vilivyo wazi katika maeneo ya nchi kavu na baharini ili viendelezwe.

Mheshimiwa Spika, Wizara ilielekeza pia nguvu katika kuhakikisha nchi yetu inaendelea kuwa na uhakika wa upatikanaji wa bidhaa za mafuta ya petroli, kutokana na umuhimu wake katika ukuaji wa shughuli za kiuchumi na kijamii pamoja kuimarisha ufanisi katika kushughulikia bidhaa hizo. Aidha, Wizara iliendelea kuimarisha Taasisi/Mashirika yaliyo chini ya Wizara ya TANESCO, TPDC, REA, EWURA na PURA pamoja na Kampuni Tanzu ili yatoe huduma bora kwa mujibu wa matarajio ya wadau, kuimarisha mapato pamoja na tija na ufanisi katika uendeshaji. Kwa kuzingatia gharama katika utekelezaji wa miradi ya nishati, Wizara iliendelea pia kuelekeza nguvu katika kuimarisha ushiriki wa Sekta Binafsi katika utekelezaji wa miradi ya nishati.

Bajeti ya Matumizi ya Wizara na Mtiririko wa Fedha kwa Mwaka 2023/24

Mheshimiwa Spika,
katika mwaka 2023/24, Wizara ya Nishati iliidhinishiwa kutumia jumla ya Shilingi Trilioni Tatu na Bilioni Arobaini na

Nane, Milioni Mia Sita Thelathini na Mbili, Mia Tano Kumi na Tisa Elfu
(Shilingi 3,048,632,519,000) ambapo Shilingi Trilioni Mbili, Bilioni Mia Sita na

Tisa, Milioni Mia Moja Hamsini na Sita, Mia Moja Ishirini na Nane Elfu
(Shilingi 2,609,156,128,000) ziliidhinishwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo na Shilingi Bilioni Themanini na

Saba, Milioni Mia Tisa Ishirini na Tisa, Mia Sita Tisini na Nane Elfu (Shilingi 87,929,698,000)
ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida.

Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Machi, 2024, Wizara ilipokea jumla ya Shilingi Trilioni

Moja, Bilioni Mia Nane Kumi na Tatu na Milioni Ishirini na Sita, Mia Moja Arobaini na Saba Elfu, Mia Moja Hamsini na Sita (Shilingi 1,813,026,147,156)
, ambapo Shilingi Bilioni Ishirini na Saba na

Milioni Sabini na Tisa na Ishirini na Sita Elfu, Mia Saba Kumi na Sita
(Shilingi 27,079,026,716) ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida na Shilingi

Trilioni Moja, Bilioni Mia Saba Themanini na Tano, Milioni Mia Tisa Arobaini na Saba, Mia Moja Ishirini Elfu, Mia Nne Arobaini (Shilingi 1,785,947,120,440) ni kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo.

B.1 SEKTA NDOGO YA UMEME NA NISHATI JADIDIFU

B.1.1 HALI YA UZALISHAJI NA UPATIKANAJI WA UMEME NCHINI

Mheshimiwa Spika,
katika mwaka 2023/24 Serikali iliendelea kuchukua hatua za kuimarisha uzalishaji na upatikanaji wa umeme nchini ambapo hadi kufikia Machi, 2024 uwezo wa mitambo ya kufua umeme iliyounganishwa katika mfumo wa Gridi ya Taifa ulifikia jumla ya MW 2,138 ikiwa ni ongezeko la asilimia 14.2 ikilinganishwa na MW 1,872.1 za Mei, 2023. Katika kiasi hicho MW 836.3 (asilimia 39.1) ni umeme unaotokana na nguvu ya maji, MW 1,198.8 (asilimia 56.1) gesi asilia, MW 92.4 (asilimia 4.3) mafuta mazito na MW 10.5 (asilimia 0.5) tungamotaka (biomass) kama inavyofafanuliwa katika Kielelezo Na. 1.
Kielelezo Na.1:Uwezo wa Mitambo ya Kufua Umeme katika
Gridi ya Taifa hadi Machi, 2024 na Hali ya
Uzalishaji
Chanzo
Uwezo wa Mitambo
Hali ya Uzalishaji
MW
Asilimia
MW
Asilimia
Maji
836.3​
39.1%​
755.5​
43.1%​
Gesi Asilia
1,198.8​
56.1%​
935.1​
53.2%​
Mafuta
92.4​
4.3%​
65.8​
3.7%​
Tungamotaka
10.5​
0.5%​
-​
-​
Jumla
2,138.0
100%
1,756.4
100%
Uwezo wa Mitambo (MW)
4.3%​
0.5%​
39.1%​
56.1%​

MajiGesi AsiliaMafutaTungamotaka

Hali ya Uzalishaji (MW)

3.7% 0.0%​

43.1%

53.2%

MajiGesi AsiliaMafutaTungamotaka

Mheshimiwa Spika, Ongezeko la uwezo wa uzalishaji wa umeme limetokana na kuanza kwa uzalishaji wa umeme katika Mradi wa Kuzalisha Umeme wa Julius Nyerere (MW 2,115) ambapo MW 235 zimeanza kuzalishwa kupitia mtambo Namba 9 pamoja na kukamilika kwa Mradi wa Kuzalisha Umeme wa Rusumo ambao unachangia MW 26.7 katika Gridi ya Taifa. Kiambatisho Na. 1 ni mchanganuo wa uwezo wa mitambo ya kuzalisha umeme katika Gridi ya Taifa hadi Machi, 2024.

Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Machi 2024, uwezo wa mitambo ya kuzalisha umeme ambayo haijaungwa katika Gridi ya Taifa ni MW 33.4 ambazo zinajumuisha mitambo inayomilikiwa na TANESCO yenye uwezo wa kufua MW 28.4 na MW 5 zitokanazo na nguvu ya jua kutoka kwa mzalishaji binafsi. Aidha, Wizara kupitia TANESCO inanunua umeme wa MW 31 kati ya hizo MW 21 kutoka Uganda kwa ajili ya Mkoa wa Kagera na MW 10 kutoka Zambia kwa ajili ya Mkoa wa Rukwa.

Mheshimiwa Spika, pamoja na kuongezeka kwa uzalishaji wa umeme katika kipindi cha Julai, 2023 hadi Machi 2024, bado uzalishaji huo ulikuwa haukidhi mahitaji ya nchi ambayo yamekuwa yakiongezeka kwa kasi kutokana na ukuaji wa shughuli za kiuchumi na kijamii pamoja na changamoto za upungufu wa maji na gesi asilia katika vituo vya kufua umeme, hitilafu katika mitambo ya uzalishaji pamoja na kufanyika kwa matengenezo katika mitambo ya uzalishaji wa umeme. Mahitaji ya juu ya umeme nchini yamekua na kufikia MW 1,590.1 zilizofikiwa tarehe 26 Machi, 2024 saa 3.00 usiku sawa na ongezeko la asilimia 8.1 ikilinganishwa na MW 1,470. 5 zilizofikiwa tarehe 12 Juni, 2023 saa 2:00 usiku. Kielelezo Na.2 ni mwenendo wa ukuaji wa mahitaji ya umeme katika mwaka 2022/23 na 2023/24.

Kielelezo Na. 2: Ukuaji wa Mahitaji ya Umeme (Megawati) Nchini kwa Mwaka 2022/23 na Mwaka 2023/24
MWEZI
JULAIAGOSTISEPTEMBAOKTOBANOVEMBADESEMBA
2022/23​
1,302.2​
1,321.0​
1,341.3​
1,336.1
1,315.6​
1,354.6​

JANUARI FEBRUARI MACHI WASTANI

1391.7 1,402.7 1401.9 1351.9
MWAKA
2023/24​
1,466.1​
1,482.8 1413.5​
1399.9​
1389.5​
1339.7​
1434.4​
1,510.3​
1590.1​
1447.4​
ONGEZEKO (%)
11.2
10.9
5.11
4.6
5.3
-1.1
3.0
7.1
11.8
7.1
B.1.2 HALI YA USAFIRISHAJI NA USAMBAZAJI WA UMEME

Mheshimiwa Spika,
kwa upande wa usafirishaji wa umeme, miundombinu ya kusafirisha umeme imeendelea kuimarika na kufikia jumla ya urefu wa kilomita 7,745.4 ikiwa ni ongezeko la asilimia 17.8 ikilinganishwa na kilomita 6,363.3 za mwaka 2022/23. Ongezeko hili limetokana na kukamilika kwa miradi mbalimbali ya njia za kusafirisha umeme, ikiwemo msongo wa Kilovoti 400 kutoka Julius Nyerere Hydro Power Plant hadi Chalinze, Singida- Arusha- Namanga pamoja na msongo wa Kilovoti 220 kutoka Morogoro hadi Dodoma kwa ajili ya uendeshaji wa treni ya umeme (SGR Lot II).

Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kuchukua hatua za kuimarisha miundombinu ya usambazaji umeme nchini ambapo imeongezeka na kufikia kilomita 176,750.9 ikiwa ni ongezeko la asilimia 4.9 ikilinganishwa na kilomita 168,548.5 za mwezi Mei, 2023. Kwa upande wa njia za kusambaza umeme, kilomita 58,886.6 ni za msongo wa Kilovoti 33, kilomita 12,476.6 za msongo wa Kilovoti 11 na kilomita 105,387.7 za msongo wa Kilovoti 0.4. Kielelezo Na.3 ni mwenendo wa miundombinu ya usafirishaji na usambazaji wa umeme.
Kielelezo
Na.3: Njia
za
Kusafirisha na
Kusambaza
Umeme hadi Kufikia Machi, 2024
Na.
Njia za Usafirishaji wa
Urefu (Km)
Umeme
Mei, 2023
Machi, 2024
1.​
Njia za msongo wa kV 400
670.0​
1,244.8​
2.​
Njia za msongo wa kV 220
3,477.7​
4,095.6​
3.​
Njia za msongo wa kV 132
1,672.6​
1,825.0​
4.​
Njia za msongo wa kV 66
543.0​
580.0​
Jumla
6,363.3
7,745.4
Njiaza Usambazajiwa
Umeme
1.​
Njia za msongo wa kV 33
55,045.6​
58,886. 6​
2.​
Njia za msongo wa kV 11
12,986.3​
12,476.6​
3.​
Njia za msongo wa kV 0.4
100,516. 6​
105,387.7​
Jumla
168,548.5
176,750.9

Chanzo: TANESCO

B.1.3 HUDUMA KWA WATEJA

Mheshimiwa Spika,
katika kipindi cha Julai, 2023 hadi Machi, 2024 Serikali kupitia TANESCO imetekeleza mikakati mbalimbali ya kuimarisha utoaji wa huduma ikiwa ni pamoja na:

Kuongeza wigo wa mawasiliano na wateja kwa kuanzisha mfumo unaomuwezesha mteja kuhudumiwa kwa haraka zaidi bila kupiga simu kwa njia ya ujumbe wa simu (CHATBOT). Mfumo huu umekamilika kwa asilimia 95;

Kupanua kituo cha huduma kwa wateja (Call Center) kwa kuongeza vifaa na wapokea simu kutoka mawakala 63 mpaka 100. Kwa sasa, Shirika linakamilisha taratibu za ununuzi wa vifaa;

iii. Kuanzisha mfumo utakaowawezesha wateja kupata taarifa maalumu za hali ya upatikanaji wa umeme kwa haraka kwa njia ya ujumbe wa simu kwenye simu zote janja na simu za kiswaswadu kuhusu Makatizo ya Umeme (Automatic Power Interruption Notification sytem) na hivyo kuwezesha wateja kujipanga ipasavyo na kupunguza malalamiko ya ukosefu wa umeme; na

Kuanzisha mfumo wa benki ya taarifa na elimu (DESA SYTEM knowledge based) ili kuweza kutatua changamoto za wateja kwa kuwapa elimu na taarifa mbalimbali zitakazotatua changamoto zao bila mafundi. Uanzishwaji wa mfumo huu umefikia asilimia 99 ili uweze kuanza kutumika.

B.1.4 MIRADI YA KUZALISHA UMEME

Miradi Iliyopo katika Hatua za Utekelezaji

Mradi wa Kuzalisha Umeme wa Julius Nyerere (JNHPP – MW 2,115)

Mheshimiwa Spika,
Serikali iliendelea na utekelezaji wa mradi wa kimkakati wa Kuzalisha Umeme wa Julius Nyerere wenye uwezo wa kuzalisha umeme wa MW 2,115 katika maporomoko ya maji ya Mto Rufiji, wenye gharama ya Shilingi trilioni 6.55 zinazogharamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa asilimia 100.

Mheshimiwa Spika, naomba nitumie fursa hii kulitaarifu Bunge lako Tukufu kuwa, sasa tupo katika hatua za mwisho za kukamilisha mradi huu ambapo hadi kufikia Machi, 2024 utekelezaji wake ulikuwa umefikia asilimia 97.43 na uzalishaji kuanza kupitia mtambo Namba 9 unaoingiza katika Gridi ya Taifa jumla ya MW 235. Aidha, mtambo Namba 8 wa mradi huu upo katika hatua za mwisho za ukamilishwaji ili uanze uzalishaji wa MW nyingine 235. Kazi zinazoendelea kukamilishwa ni pamoja na ujenzi wa barabara za kudumu katika eneo la mradi ambao umefikia asimilia 85.6, ujenzi wa nyumba za makazi na ofisi ambao umefikia asilimia 98.5, ujenzi wa Daraja la kudumu ambao umefikia asilimia 97.2 na ufungaji wa mitambo saba (7) yenye uwezo wa kuzalisha MW 235 kila mmoja ambayo ipo katika hatua mbalimbali za ufungwaji.

Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Gesi Asilia wa Kinyerezi I Extension– MW 185

Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2023/24, Serikali ilikamilisha ujenzi wa mitambo ya kufua umeme ya Kinyerezi I Extension MW 185 ambapo kwa sasa mitambo yote minne (4) inafua umeme. Aidha, hadi kufika Machi 2024, kazi ya upanuzi wa kituo cha kupoza umeme cha Kinyerezi ilikuwa imefikia asilimia 97.6 ambapo transfoma mbili zenye uwezo wa MVA 175 zilikuwa zimefungwa kwenye misingi yake; na ujenzi wa barabara, ufungaji wa taa na mifumo ya ulinzi ulikuwa unaendelea. Vilevile, vituo vya Mbagala na Gongolamboto vinaongezewa uwezo kufikia MVA 170 kutoka uwezo wa awali wa MVA 50. Pia, ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme yenye urefu wa kilomita 19.2 ya msongo wa Kilovoti 132 kutoka Kinyerezi hadi Mbagala kupitia Gongolamboto umefikia asilimia 55.

Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Maji wa Rusumo – MW 80

Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusisha uzalishaji wa umeme wa MW 80 kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Kagera na umejengwa kwa ushirikiano wa nchi tatu (3) za Tanzania, Burundi na Rwanda kwa mgawanyo sawa wa umeme kwa kila nchi. Mradi umekamilika na kuanza uzalishaji wa umeme ambapo kila nchi inapata MW 27. Aidha, kwa upande wa Tanzania mradi ulihusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme yenye msongo wa Kilovoti 220 kutoka Rusumo hadi Nyakanazi yenye urefu wa kilomita 94.1 pamoja na miradi ya kijamii ambayo imekamilika kwa asilimia 100.

Ukarabati wa Mitambo katika Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Hale

Mheshimiwa Spika, Serikali iliendelea na ukarabati wa miundombinu ya kuzalisha umeme katika Kituo cha Hale chenye uwezo wa kuzalisha MW 21 ambapo kwa sasa kiasi kinachozalishwa ni MW 10.5 kutokana na uchakavu wa miundombinu ya kuzalisha umeme. Hadi kufikia Machi, 2024, utekelezaji wa mradi huu ulikuwa umefikia asilimia 61 na kazi zinazoendelea kutekelezwa ni pamoja na kukamilisha uundaji wa mitambo, matengenezo ya kituo cha kupoza umeme, ujenzi wa barabara mpya yenye urefu wa kilomita 1.3 na uchimbaji wa njia ya chini ya ardhi. Mradi unatarajiwa kukamilika Agosti, 2025.

Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Maji wa Malagarasi – MW 49.5

Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusisha ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme wa MW 49.5 kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Malagarasi pamoja na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 132 yenye urefu wa kilomita 54 kutoka Malagarasi hadi Kidahwe, mkoani Kigoma. Aidha, tayari Mkandarasi ameanza ujenzi wa bwawa la kuzalisha umeme na mradi unatarajiwa kukamilika Oktoba, 2027. Vilevile, Mkandarasi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme anaendelea na kazi za ujenzi ambapo utekelezaji umefikia asilimia 15.6 na mradi unatarajiwa kukamilika Aprili, 2025.

Mradi wa Kuzalisha Umeme wa Jua Mkoani Shinyanga – MW 150

Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa mradi huu unahusisha ujenzi wa mitambo ya kuzalisha umeme wa Megawati 150 kwa kutumia nguvu ya jua Mkoani Shinyanga. Hadi kufikia Machi, 2024 Serikali ilikuwa imekamilisha ulipaji wa fidia ya Shilingi bilioni 2.6 kwa wananchi 109 waliopisha mradi. Aidha, Mkandarasi anaendelea na ujenzi wa miundombinu ya kuzalisha umeme na mradi unatarajiwa kukamilika Januari, 2025.

Miradi ya Kuboresha Upatikanaji wa Umeme Mikoa ya Kusini (Lindi na Mtwara)

Mheshimiwa Spika, Serikali iliendelea na utekelezaji wa Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa kutumia Gesi Asilia wa Mtwara (MW 300) ambapo maandalizi ya malipo ya fidia kwa wananchi watakaopisha eneo la ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme pamoja na njia ya kusafirisha umeme yanaendelea. Aidha, Serikali inaendelea na mazungumzo na JICA kwa ajili ya utekelezaji wa mradi.

Mheshimiwa Spika, ikiwa ni hatua ya kuhakikisha Mikoa ya Lindi na Mtwara inakuwa na umeme wa uhakika na unaoendana na ukuaji wa mahitaji, Serikali iliendelea kuchukua hatua mbalimbali. Hatua hizo ni pamoja na kufunga mtambo wa kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia wa MW 20 katika eneo la Hiyari, Mkoani Mtwara ambao umeanza uzalishaji wa umeme, pamoja na kufufua mtambo Na.13 (MW 4.3) na mtambo Na. 8 (MW 2) mkoani Mtwara na mtambo Na.3 (MW 2.5) Somanga mkoani Lindi. Hatua hizo zimeimarisha upatikanaji wa umeme na kuondoa mgao wa umeme katika mikoa ya Lindi na Mtwara.

Aidha, Serikali inaendelea kuchukua hatua za kuiunganisha Mikoa ya Lindi na Mtwara katika Gridi ya Taifa kwa kukamilisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme ya Songea- Tunduru-Masasi-Mahumbika ifikapo Agosti, 2025. Kielelezo Na. 4 ni mtambo wa kuzalisha umeme kiasi cha MW 20 ukiwa eneo la kufungwa Mkoani Mtwara.​

Kielelezo Na.4: Mtambo wa Kuzalisha Umeme Kiasi cha MW 20 Ukiwa Katika Eneo la Kusimikwa Mkoani Mtwara

Miradi ya Uzalishaji wa Umeme Iliyopo katika Hatua za Utayarishaji

Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Maji wa Ruhudji – MW 358

Mheshimiwa Spika, Serikali iliendelea na utekelezaji wa mradi huu unaohusisha ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme wa MW 358 kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Ruhudji mkoani Njombe na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 400 yenye urefu wa kilomita 170 kutoka Ruhudji hadi kituo cha kupoza umeme cha Kisada mkoani Iringa. Tayari uthamini wa mali za wananchi watakaolipwa fidia ili kupisha eneo la mradi kwa ajili ya ujenzi umekamilika na taratibu za kulipa fidia zinaendelea. Aidha, vyeti vya Tathmini ya Athari za Mazingira na Jamii kwa upande wa kituo cha kuzalisha umeme na njia ya kusafirisha umeme vimeshatolewa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC). Vilevile, tathmini ya gharama za miundombinu wezeshi imekamilika na taratibu za kupata fedha za kutekeleza mradi na ujenzi wa miundombinu hiyo zinaendelea.

Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Maji wa Rumakali – MW 222

Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusisha ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme wa MW 222 kwa kutumia maji ya Mto Rumakali mkoani Njombe na njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa Kilovoti 220 yenye urefu wa kilomita 64.5 kutoka kwenye mitambo hadi kituo cha kupoza umeme cha Iganjo mkoani Mbeya.

Mheshimiwa Spika, hatua zilizochukuliwa katika kutekeleza mradi huu ni pamoja na kukamilisha uthamini wa mali za wananchi watakaolipwa fidia ili kupisha eneo la mradi kwa ajili ya ujenzi ambapo taratibu za kulipa fidia zinaendelea. Aidha, vyeti vya mazingira kutoka NEMC kwa upande wa kituo cha kuzalisha umeme na njia ya kusafirisha umeme vimetolewa na tathmini ya gharama za miundombinu wezeshi zimekamilika ambapo taratibu za kupata fedha za kutekeleza mradi na ujenzi wa miundombinu wezeshi zinaendelea.

Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Maji wa Kakono – MW 87.8

Mheshimiwa Spika, mradi huu unalenga kuongeza uwezo wa uzalishaji wa umeme katika Gridi ya Taifa na upatikanaji wa umeme wa uhakika katika mikoa ya Kanda ya Ziwa. Aidha, mradi utahusisha ujenzi wa bwawa la kuzalisha umeme wa MW 87.8 kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Kagera na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa Kilovoti 220 yenye urefu wa kilomita 38. Hadi kufika Machi, 2024, Serikali ilikuwa inaendelea na tathmini ya mali za wananchi 126 wanaopisha mradi na taratibu za kumpata Mshauri Mwelekezi zinatarajiwa kukamilika Juni, 2024. Aidha, taratibu za kumpata Mkandarasi wa ujenzi zitafuata baada ya kukamilika kwa kazi ya Mshauri Mwelekezi.

(iv) Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Maji wa Kikonge – MW 321

Mheshimiwa Spika,
mradi huu unahusisha ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme wa MW 321 kwa kutumia maporomoko ya maji ya mto Ruhuhu mkoani Ruvuma na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 220 yenye urefu wa kilomita 96 kutoka Kikonge hadi kituo cha kupoza umeme cha Madaba. Serikali inaendelea na taratibu wa kutafuta fedha kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huu pamoja na kukamilisha taarifa muhimu za mradi ikiwemo tathmini ya kina ya Athari za Kijamii na Mazingira (detailed ESIA), uwekaji wa mipaka katika eneo la uzalishaji wa umeme, usanifu wa kina na maandalizi ya nyaraka za zabuni za mradi (bwawa la kuzalisha umeme na njia ya kusafirisha umeme). Aidha, maandalizi ya kufanya tathmini katika eneo la bwawa la uzalishaji umeme yameanza. Vilevile, hatua za awali za kumpata Mshauri Mwelekezi wa kazi za Mazingira zinaendelea.

B.1.5 MIRADI YA KUSAFIRISHA NA KUSAMBAZA UMEME

Miradi ya Kusafirisha na Kusambaza Umeme Iliyopo katika Hatua za Utekelezaji

Mradi wa Kusafirisha Umeme kutoka Julius Nyerere Hydro Power Plant hadi Chalinze – Kilovoti 400 na Kituo cha Kupoza Umeme, Chalinze

Mheshimiwa Spika,
naomba kulitaarifu Bunge lako Tukufu kuwa, ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa Kilovoti 400 yenye urefu wa kilomita 160 kutoka JNHPP hadi Chalinze umekamilika kwa asilimia 99.5 na njia hiyo imeanza kutumika kusafirisha umeme. Aidha, kituo kipya cha kupoza umeme cha Chalinze cha Kilovoti 400/220/132 kimekamilika kwa asilimia 93.1 na kimeanza kutumika kuingiza umeme katika Gridi ya Taifa. Kazi zilizobaki zinatarajiwa kukamilika ifikapo Juni, 2024.

Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa Kilovoti 220 kutoka Geita hadi Nyakanazi

Mheshimiwa Spika, Serikali imekamilisha ujenzi wa miundombinu ya usambazaji umeme katika vijiji 32 vinavyopitiwa na mradi wa kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 220 yenye urefu wa kilomita 144 kutoka Geita hadi Nyakanazi. Aidha, zoezi la uunganishwaji wa wateja linaendelea ambapo wateja 3,046 wameshapata huduma ya umeme kati ya wateja 5,646 na mradi huu unatarajiwa kukamilika ifikapo Juni, 2024.

Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa Kilovoti 400 kutoka Singida – Arusha – Namanga

Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 400 yenye urefu wa kilomita 414 kutoka Singida hadi Namanga kupitia Babati na Arusha ambapo umekamilika kwa asilimia 99.4. Aidha, ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 400 kutoka Arusha hadi Namanga yenye urefu wa kilomita 114.3 umefikia asilimia 97.5 na kituo cha kupoza umeme cha Lemugur kimekamilika kwa asilimia 100 na kuwashwa.

29​

Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa Kilovoti 220 kutoka Rusumo hadi Nyakanazi

Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2023/24 Serikali ilikusudia kukamilisha malipo ya fidia kwa wananchi waliosalia wakati wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 220 yenye urefu wa kilomita 94 kutoka kituo cha kuzalisha umeme cha Rusumo hadi Nyakanazi ambao tayari umekamilika kwa asilimia 100. Hadi kufika Machi 2024, wananchi wote waliosalia walikuwa wamelipwa fidia zao.

Ujenzi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa Kilovoti 400 kutoka Iringa hadi Sumbawanga kupitia Mbeya na Tunduma (TAZA)

Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 400 kutoka Iringa kupitia Mbeya, Tunduma hadi Sumbawanga yenye urefu wa kilomita 620 pamoja na ujenzi wa vituo vya kupoza umeme vya Kisada (Iringa), Iganjo (Mbeya), Tunduma na Sumbawanga. Serikali iliendelea na zoezi la ulipaji wa fidia kwa wananchi watakaopisha mradi ambalo limefikia asilimia 89. Aidha, tayari imesainiwa Mikataba kati ya TANESCO na wakandarasi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme pamoja na vituo viwili vya

30​

kupoza umeme vya Sumbawanga na Tunduma. Vilevile, vituo vya Iringa, Kisada na Mbeya vipo katika hatua za mwisho za kupata idhini ya Benki ya Dunia ya kuendelea na taratibu za kusaini Mikataba. Mradi huu unatarajiwa kukamilika Desemba, 2025 na unalenga pia kuunganisha Gridi ya Taifa na Nchi za Kusini mwa Afrika (Southern African Power Pool – SAPP).

Ujenzi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa Kilovoti 400 kutoka Nyakanazi hadi Kigoma

Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 400 kutoka Nyakanazi hadi Kigoma yenye urefu wa kilomita 280, ujenzi wa kituo cha kupoza umeme Kidahwe Mkoani Kigoma, upanuzi wa kituo cha kupoza umeme cha Nyakanazi pamoja na usambazaji wa umeme katika vijiji 18 vilivyopo katika eneo la mradi. Hadi kufika Machi 2024, utekelezaji wa mradi wa njia ya kusafirisha umeme ulikuwa umefikia asilimia 94.98 na unatarajiwa kukamilika Juni, 2024 kwa mujibu wa Mkataba. Aidha, Mkataba wa ujenzi wa kituo cha kupoza umeme cha Kidahwe na upanuzi wa kituo cha kupoza umeme cha Nyakanazi umesainiwa na utekelezaji unatarajiwa kukamilika Desemba, 2026.

31​

Mheshimiwa Spika, kufuatia kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa njia ya msongo wa Kilovoti 400 kutoka Nyakanazi hadi Kigoma, Serikali imechukua hatua ya dharura ya kufunga transfoma katika kituo cha kupoza umeme cha Kidahwe itakayowezesha kufikisha umeme wa Gridi ya Taifa wa msongo wa Kilovoti 220 katika Mkoa wa Kigoma ifikapo Juni, 2024.

Mradi wa Kuimarisha Gridi ya Taifa (National Grid Stabilization Projects)

– Gridi Imara

Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu uimarishaji wa miundombinu ya umeme katika mikoa mbalimbali ikiwa ni pamoja na ujenzi wa njia za kusafirisha umeme wa msongo wa Kilovoti 220 na 132 na kuongeza uwezo wa nyaya za kusafirisha umeme, ujenzi wa njia za kusambaza umeme msongo wa Kilovoti 33, ujenzi wa vituo vya kupoza umeme na kuongeza uwezo wa baadhi ya vituo pamoja na ujenzi wa vituo vya kupoza umeme katika maeneo ya usambazaji (switching station). Mradi huu unatekelezwa kwa Awamu Tano ambapo Awamu ya Kwanza inahusisha miradi 27.

Mheshimiwa Spika, kwa sasa Serikali inaendelea kutekeleza miradi ya Awamu ya Kwanza kufuatia kusainiwa kwa mikataba baina ya Serikali na Wakandarasi. Aidha, upembuzi yakinifu wa njia

32​

za kusafirisha, kusambaza na vituo vya kupoza umeme umefanyika pamoja na usanifu wa michoro, ununuzi wa vifaa kwa baadhi ya miradi pamoja na kuanza kazi za awali za ujenzi. Vilevile, utambuzi wa miradi ya Awamu ya Pili umefanyika na hatua za awali za utekelezaji zimeanza. Kiambatisho Na.2 ni hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Gridi Imara. Kutokana na umuhimu wa miradi hii katika kuondoa changamoto za upatikanaji wa umeme wa uhakika nchini, Serikali itaendelea kuhakikisha fedha zinazotengwa kila mwaka zinapatikana.

Mradi wa Ukarabati na Uboreshaji wa Gridi ya Taifa (Grid Rehabilitation and Upgrading) TTGRUP

Mheshimiwa Spika, mradi huu unalenga kuimarisha Gridi ya Taifa kwa kukarabati na kuboresha vituo nane (8) vya kupoza umeme, kurefusha Mkongo wa Mawasiliano (Optic Fiber) na kuboresha miundombinu ya mawasiliano kwa kuondoa earth wire na kuweka optical ground wire pamoja na kuimarisha mfumo wa uendeshaji na udhibiti wa Gridi ya Taifa. Mradi huu unafadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) pamoja na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hadi kufikia Machi, 2024, utekelezaji wa mradi wa ukarabati na uboreshaji wa vituo nane (8) ulikuwa umefikia asilimia 21.0; uboreshaji wa miundombinu ya

33​

mawasiliano kwa ujumla umefikia asilimia 70.0 na kazi za kuimarisha mfumo wa uendeshaji na udhibiti wa Gridi ya Taifa kwa ujumla umefikia asilimia 23.4. Mradi unatarajiwa kukamilika Desemba, 2024.

Ujenzi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa Kilovoti 220 kutoka Benaco hadi Kyaka

Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa Kilovoti 220 kutoka Benaco hadi Kyaka yenye urefu wa kilomita 166.2 itakayounganisha Mkoa wa Kagera katika Grid ya Taifa. Serikali kupitia TANESCO imekamilisha uthamini wa mali za wananchi wanaopisha mradi na kazi zinazoendelea ni pamoja na taratibu za kufanya malipo ya fidia na majadiliano na Mshauri Mwelekezi aliyekidhi vigezo ili kusaini mkataba Aprili, 2024. Mradi unatarajiwa kukamilika Desemba, 2026.

Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa Kilovoti 220 kutoka Morogoro hadi Dodoma kwa Ajili ya Uendeshaji wa Treni ya Umeme (SGR Lot II)

Mheshimiwa Spika, Serikali iliendelea kutekeleza mradi huu ambapo tayari umekamilika kwa asilimia 99 na majaribio ya kupitisha umeme

34​

kutoka Msamvu, Morogoro hadi Zuzu, Dodoma yamefanyika kwa mafanikio.

Mradi wa Njia ya Kusafirishi Umeme Msongo wa Kilovoti 220 kutoka Mwanza hadi Isaka kwa Ajili ya Uendeshaji wa Treni ya Umeme (SGR Lot V)

Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 220 yenye urefu wa kilomita 230 kutoka Mwanza hadi Isaka kwa ajili ya uendeshaji wa treni ya umeme. Serikali kupitia TANESCO imekamilisha tathmini ya mali za wananchi watakaopisha mradi na taratibu za malipo ya fidia zinaendelea. Aidha, taratibu za kumpata Mkandarasi Mjenzi zimekamilika na ameanza kufanya kazi za awali za utafiti wa udongo na njia ya kusafirisha umeme. Mradi huu unatarajiwa kukamilika Mei, 2025.

Ujenzi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa Kilovoti 400 kutoka Chalinze - Kinyerezi - Mkuranga (NEG Phase 1)

Mheshimiwa Spika, mradi huu inahusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 400 kutoka Chalinze, Kinyerezi hadi Mkuranga yenye urefu wa kilomita 135 na vituo vya kupoza umeme vya Chalinze, Kinyerezi, Mkuranga na Morogoro. Hadi kufikia Machi 2024, Serikali ilikuwa imekamilisha ununuzi wa Mkandarasi

35​

Mjenzi wa njia ya kusafirisha umeme ambaye anaendelea na utekelezaji wa mradi. Mradi unatarajiwa kukamilika Aprili, 2026.

Ujenzi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa Kilovoti 400 kutoka Chalinze – Dodoma (NEG Phase 2)

Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa mradi huu unahusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 400 kutoka Chalinze hadi Dodoma yenye urefu wa kilomita 345 na upanuzi wa kituo cha kupoza umeme cha Dodoma. Mradi huu utawezesha kusafirisha umeme unaotoka JNHPP kupitia Chalinze kwenda Dodoma na kuusambaza katika Mikoa mbalimbali nchini (power evacuation). Hadi kufikia Machi, 2024, Serikali ilikuwa imekamilisha ulipaji wa fidia kwa wananchi 2,760 kati ya 2,860 wanaopisha mradi sawa na asilimia 92 na taratibu za ulipaji wa fidia zinaendelea. Aidha, Mkandarasi anaendelea na utekelezaji wa mradi na unatarajia kukamilika Desemba, 2025.

Ujenzi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa Kilovoti 400 kutoka Chalinze – Segera na Msongo wa Kilovoti 220 Segera – Tanga

Mheshimiwa Spika, mradi huu unalenga ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 400 kutoka Chalinze – Segera na Msongo

36​

wa Kilovoti 220 kutoka Segera - Tanga na vituo cha kupoza umeme vyenye uwezo wa MVA 800 Segera na Tanga. Kwa sasa Serikali inaendelea na taratibu za kutafuta fedha za utekelezaji wa mradi huu ambao kukamilika kwake kutawezesha kusafirisha umeme kutoka Chalinze kwenda Tanga. Aidha, Serikali imekamilisha kazi ya Upembuzi Yakinifu na inaendelea na taratibu za kutathmini mali za wananchi watakaopisha mradi ili waweze kulipwa fidia.

Mradi wa Kuboresha Utendaji Kazi wa TANESCO (Corporate Management System – CMS)

Mhesimiwa Spika, mradi huu unalenga kuboresha hali ya utendaji kazi wa TANESCO kwa kuweka mifumo itakayowezesha kuongeza tija na ufanisi katika utendaji kazi. Mradi huu unatekelezwa sambamba na mradi wa kusafirisha umeme wa Tanzania – Zambia Interconnector Transmission Project (TAZA) kwa gharama ya Dola za Marekani milioni 34.8 sawa na Shilingi bilioni 81.6.

Mhesimiwa Spika, Serikali kupitia TANESCO inaendelea na utekelezaji wa kazi za ufungaji wa vifaa vya miundombinu ya mradi (data center infrastructure) na kufanyiwa majaribio utendaji wake. Aidha, usimikaji wa mfumo wa taarifa za kijiografia za miundombinu ya umeme na wateja

37​

(GIS) umekamilika pamoja na mafunzo kwa wataalam. Vilevile, miundombinu ya mawasiliano ya mradi (network infrastructure) imekamilika kwa asilimia 80 na hatua ya kwanza ya utengenezaji wa mfumo imefikia asilimia 85 ambapo hatua ya pili ya mradi imefikia asilimia 43. Pia, yamefanyika mafunzo ya matumizi ya mfumo kwa Mameneja na Timu Maalumu (Champions Team) na yanaendelea kwa wafanyakazi wote. Kwa ujumla mradi umetekelezwa kwa asilimia 61 na unatarajiwa kukamilika Agosti, 2024.

Miradi ya Kusafirisha na Kusambaza Umeme Iliyopo Katika Hatua ya Utayarishaji

Ujenzi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa Kilovoti 400 kutoka Segera- Same- Arusha (Lemugur)

Mheshimiwa Spika,
mradi huu unalenga ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 400 kutoka Segera hadi Arusha kupitia Same, kituo cha kupoza umeme cha Same na upanuzi wa vituo vya kupoza umeme vya Segera na Lemugur. Kazi za Upembuzi Yakinifu na Tathmini ya Mazingira na Kijamii zinaendelea na zinatarajika kukamilika Agosti, 2024.

38​

Ujenzi wa Kituo cha Kupoza Umeme cha Ibadakuli, Shinyanga 2x315 MVA

Mhesimiwa Spika, mradi huu unahusisha kujenga kituo kipya chenye uwezo wa Kilovoti 400/220 na kusimika transfoma kubwa mbili zenye ukubwa wa MVA 315 kila moja katika eneo la Ibadakuli mkoani Shinyanga ili kuimarisha upatikanaji wa umeme wa uhakika katika mikoa ya kanda ya Ziwa na maeneo jirani kwa lengo la kuchochea shughuli za kiuchumi, hususan uchimbaji wa madini, usafirishaji kwa kutumia (SGR) na mradi wa Bomba la Mafuta kutoa Uganda hadi Tanga (EACOP). Kwa sasa Mkandarasi anaendelea na usanifu wa kituo.

Ujenzi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa Kilovoti 220 kutoka Makutopora hadi Tabora kwa ajili Uendeshaji wa Treni ya Umeme (SGR Lot 3)

Mhesimiwa Spika, mradi huu unahusu ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 220 yenye urefu wa kilomita 347 kutoka Makutopora hadi Tabora kwa ajili ya uendeshaji wa treni ya umeme (SGR). Gharama za mradi huu zinakadiriwa kuwa Shilingi bilioni 212.58. Hadi kufikia Machi 2024, kazi zilizokuwa zinatekelezwa ni pamoja na Upembuzi Yakinifu ambao umefikia asilimia 25 na taratibu za kumpata Mshauri Mwelekezi wa kufanya usanifu wa kina wa mradi.

39​

Aidha, tathmini ya mali za wananchi watakaopisha mradi zitaanza baada ya kukamilisha Upembuzi Yakinifu.

Ujenzi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa Kilovoti 220 kutoka Tabora hadi Isaka kwa ajili ya Uendeshaji wa Treni ya Umeme (SGR Lot 4)

Mhesimiwa Spika, mradi huu unahusu ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 220 yenye urefu unaokadiriwa kuwa kilomita 195 kutoka Tabora hadi Isaka kwa ajili ya uendeshaji wa treni ya umeme. Gharama za mradi huu zinakadiriwa kuwa Shilingi bilioni 131.66. Hadi kufikia Machi 2024, kazi zilizokuwa zinatekelezwa ni pamoja na Upembuzi Yakinifu ambao umefikia asilimia 12.5 na taratibu za kumpata Mshauri Mwelekezi wa kufanya usanifu wa kina wa mradi. Aidha, tathmini ya mali za wananchi watakaopisha mradi zitaanza baada ya kukamilisha Upembuzi Yakinifu.

Ujenzi wa njia ya Kusafirisha Umeme (Submarine Cable) Msongo wa Kilovoti 220 kutoka Tanzania Bara (Ununio) Hadi Zanzibar (Unguja)

Mhesimiwa Spika, mradi huu unahusu ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 220 kwenda Zanzibar kwa ajili ya

40​

kuimarisha upatikanaji wa umeme Zanzibar. Kukamilika kwa mradi huu kutatatua changamoto ya kuzidiwa kwa miundombinu ya kusafirisha umeme kwenda Zanzibar iliyopo kwa sasa. Kazi zinazoendelea kwa sasa ni kukamilisha taratibu za ununuzi wa Mshauri Mwelekezi atakayefanya Upembuzi Yakinifu wa mradi ambazo zinatarajiwa kukamilika Juni, 2024. Taratibu za utafutaji wa fedha za kutekeleza mradi huu zinaendelea ambapo AfDB imeonyesha nia ya kushirikiana na Serikali katika utekelezaji wa mradi huu.

Ujenzi wa Njia ya Kusafirisha Umeme (Submarine Cable) Msongo wa Kilovoti 132 kutoka Tanzania Bara (Tanga) Hadi Zanzibar (Pemba)

Mhesimiwa Spika, mradi huu unahusu ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 132 kutoka Tanga kwenda Pemba ili kuimarisha upatikanaji wa umeme Pemba. Kukamilika kwa mradi huu kutatatua changamoto ya kuzidiwa kwa miundombinu ya kusafirisha umeme kwenda Pemba iliyopo kwa sasa. Kazi zinazoendelea kwa sasa ni kukamilisha taratibu za ununuzi wa Mshauri Mwelekezi atakayefanya Upembuzi Yakinifu wa mradi. Taratibu za utafutaji wa fedha za kutekeleza mradi huu zinaendelea ambapo AfDB ameonesha nia ya kushirikiana na Serikali katika utekelezaji wa mradi huu.

41​

Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Kupoza Umeme cha Manyoni (Manyoni Substation - MVA 2x30, 220/33kV)

Mhesimiwa Spika, mradi huu unalenga ujenzi wa kituo cha kupoza umeme chenye uwezo wa MVA 60 katika Kata ya Mkwese, Wilaya ya Manyoni, Mkoa wa Singida na unatarajiwa kugharimu Shilingi bilioni 38.05. Hadi kufikia Machi 2024, Tathmini ya Athari kwa Mazingira na Jamii ilikuwa imekamilika na kuwasilishwa NEMC kwa ajili ya kupata cheti cha mazingira. Aidha, tathmini ya mali za wananchi watakaopisha mradi inaendelea ambapo inatarajiwa kukamilika Juni, 2024. Serikali inaendelea na taratibu za utafutaji wa fedha za kutekeleza mradi huu.

Mradi wa Kusafirisha Umeme Msongo wa Kilovoti 400 kutoka Tanzania hadi Uganda (Masaka - Ibadakuli)

Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 400 yenye urefu wa kilomita 617 kutoka Ibadakuli – Nyakanazi – Kyaka hadi Masaka Uganda pamoja na ujenzi wa kituo cha kupoza umeme cha Kyaka. Upembuzi Yakinifu umekamilika na kazi zinazoendelea ni kufanya Tathmini ya Athari za Mazingira pamoja na tathmini ya wananchi watakaopisha mradi.

42​

Taratibu za upatikanaji wa fedha za utekelezaji wa mradi zinaendelea.

Ujenzi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa Kilovoti 220 kutoka Chalinze – Bagamoyo

Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa mradi huu unahusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 220 kutoka Chalinze - Bagamoyo yenye urefu wa kilomita 90 na kituo cha kupoza umeme cha Bagamoyo. Hadi kufikia Machi, 2024 Upembuzi Yakinifu wa mradi ulikuwa umekamilika na kazi zinazoendelea ni pamoja na kufanya tathmini ya mali za wananchi watakaopisha mradi na kutafuta fedha za utekelezaji wa mradi huu.

Ujenzi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa Kilovoti 400 kutoka Sumbawanga hadi Kigoma Kupitia Mpanda (Km 480) na Kituo cha Kupoza Umeme Mpanda

Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 400 kutoka Sumbawanga hadi Kigoma kupitia Mpanda yenye urefu wa kilomita 480. Gharama za mradi huu zinakadiriwa kuwa Dola za Marekani milioni 200.4 sawa na Shilingi bilioni

43​

512.02 kwa upande wa njia ya kusafirisha umeme na Dola za Marekani milioni 50 kwa ajili ya kituo cha kupoza umeme. Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Exim Benki ya Korea zimeonesha nia ya kufadhili mradi huu. Hadi kufikia Machi 2024, Serikali kupitia TANESCO ilikuwa imekamilisha uhuishaji wa Upembuzi Yakinifu na usanifu wa mradi wa awali na inaendelea na taratibu za kutafuta fedha za kutekeleza mradi.

Utekelezaji wa Miradi Mingine na Matengenezo ya Mitambo

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia TANESCO imeendelea kufanya ukaguzi wa miundombinu ya umeme pamoja na kuifanyia matengenezo. Mitambo ya kuzalisha umeme iliyofanyiwa matengenezo kinga makubwa na madogo ni pamoja na kituo cha Tegeta, Kituo cha Kinyerezi II, Kituo cha Ubungo I na Kituo cha Mtera. Matengenezo hayo yaliimarisha uzalishaji wa umeme kwa wastani wa MW 115 kwenye Gridi ya Taifa ambao ulikuwa hauzalishwi kutokana na ubovu wa mitambo. Kiambatisho Na. 3 ni mitambo iliyofanyiwa matengenezo makubwa na madogo.

Mheshimiwa Spika, ili kuongeza uwezo wa miundombinu ya usafirishaji na kupunguza upotevu wa umeme, TANESCO inafanya maboresho kwenye njia mbalimbali za kusafirisha umeme

44​

ikiwemo njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa Kilovoti 132 yenye urefu wa kilomita 97 kutoka Ubungo hadi Chalinze. Kwa sasa njia hiyo ina uwezo wa kusafirisha kiasi cha MW 150, ikilinganishwa na kiasi cha MW 94 kilichokuwa kinasafirishwa awali hivyo kufanya uwezo wa kusafirisha umeme kuongezeka kwa asilimia 78. Aidha, Shirika linabadilisha miundombinu ya msongo wa Kilovoti 11 na kuwa msongo wa Kilovoti 33, pamoja na kuongeza transfoma kwenye maeneo mbalimbali. Kazi ya ukarabati ni endelevu na inaendelea katika mkoa wa Tanga kwa kuboresha njia ya kilomita 172 ya kusafirisha umeme ya msongo wa Kilovoti 132 kutoka Chalinze mpaka Hale.

Mheshimiwa Spika, jitihada nyingine zinazofanyika ili kuimarisha miundombinu ya usafirishaji umeme nchini ni kufanya ukaguzi wa kina ili kubaini maeneo yenye changamoto na kuyafanyia ukarabati. Ukarabati huo unahusisha ubadilishaji wa nyaya chakavu, vikombe vilivyopasuka, vyuma vilivyoibiwa, kuondoa nguzo za miti na kuweka nguzo za zege pamoja na ukarabati wa sehemu zilizoathiriwa na mmomonyoko wa udongo na kusafisha njia tengefu.

Mheshimiwa Spika, kuhusu uboreshaji wa mifumo ya uendeshaji wa Gridi, Serikali kupitia TANESCO ipo katika hatua za mwisho za

45​

kukamilisha mradi wa uboreshaji na kuongeza uwezo wa mitambo ya kuongoza/kuendesha Gridi ya umeme (SCADA/EMS). Mradi huu, wenye lengo la kuongeza ufanisi wa uendeshaji wa gridi kupitia teknolojia ya kidijitali unatarajiwa kukamilika Juni, 2025.

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia TANESCO imefanikiwa kuweka mifumo ya kisasa ya mawasiliano katika vituo tisa (9) vya kupoza umeme ili viendeshwe kidijitali (unmanned substations). Hadi sasa kituo kimoja cha Buzwagi kimekamilika na vituo nane (8) vilivyobaki vinatarajiwa kukamilika Desemba 2024. Vituo hivyo ni New City Centre (Posta), Kurasini, Dege, Mbagala na Gongo la Mboto vilivyopo mkoani Dar es Salaam pamoja na vituo vya Musoma, Geita na Bulyanhulu ambavyo vipo katika majaribio ya kuendeshwa kidijitali. Jitihada za kuweka mifumo ya kidijitali kwenye vituo vingine zinaendelea.

Mheshimiwa Spika, jitihada za maboresho zinafanyika pia katika mifumo ya kisasa ya usambazaji umeme (distribution network automation), ikiwa ni pamoja na kubadilisha mita za wateja wakubwa T2 na T3 kwa kufunga mita zenye ufanisi. Zoezi hili limeanza kwa mkoa wa Dar es Salaam na maeneo mengine yatafuatia. Aidha, TANESCO inakamilisha taratibu za ununuzi wa mfumo wa mita janja (smart meters)

46​

zitakazomuwezesha mteja wa kawaida kununua umeme na kisha mita hiyo kupokea moja kwa moja umeme badala na mfumo wa sasa.

B.1.6 UTENDAJI WA KAMPUNI TANZU ZA TANESCO

Kampuni ya Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Usafirishaji na Usambazaji Umeme (ETDCO)

Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2023/24 ETDCO iliendelea na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya usafirishaji wa umeme. Miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 132 wenye urefu wa kilomita 383 kutoka Tabora hadi Katavi kupitia Sikonge, Ipole na Inyonga unaotarajiwa kukamilika ifikapo Juni, 2024; na mradi wa kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 132 kutoka Tabora hadi Urambo na kutoka Urambo hadi Kidahwe Mkoani Kigoma. Aidha, ETDCO ilikamilisha kwa asilimia 99 ujenzi wa njia nne za kusafirisha umeme msongo wa kilovoti 33 kutoka kituo cha kupoza umeme cha Mpomvu (Geita) hadi kituo cha kupoza umeme cha Mgodi wa Geita Gold Mine ili kuunganisha mgodi na umeme wa Gridi ya Taifa.

47​

Mheshimiwa Spika, ETDCO iliendelea na utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini katika Mikoa ya Geita na Kigoma kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ambapo hadi kufikia Machi, 2024 ilikuwa imekamilika kwa asilimia 40 kwa upande wa Mkoa wa Geita na asilimia 20 kwa upande wa mkoa wa Kigoma. Kazi zilizofanyika ni pamoja na ufungaji wa transfoma 20 kati ya 45 na kuwasha mitaa 20 kati ya 45 kwa upande wa mkoa wa Geita; na kufunga transfoma 6 kati ya 59 na kuwasha umeme mitaa sita kati ya 59 katika mkoa wa Kigoma. Miradi hii kwa ujumla wake inatarajia kukamilika mwishoni mwa Desemba, 2024.

Mheshimiwa Spika, kampuni ya ETDCO iliendelea pia na utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini katika mikoa ya Katavi (REA III, Round II) ambao umekamilika kwa asilimia 96, Mbeya (REA III, Round II) ambao umekamilika kwa asilimia 92, Kigoma (REA III, Round I) ambao umekamilika kwa asilimia 99 na Arusha (REA III, Round I) ambao umekamilika kwa asilimia 100. Pia kampuni hiyo ilianza utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa njia za kusambazia umeme katika nyumba zinazojengwa Msomera wilayani Handeni kwa ajili ya familia zinazohama kutoka Hifadhi ya Ngorongoro ambapo mradi huo pia utahusisha nyumba zitakazojengwa Saunyi wilayani Kilindi na Kitwai B wilayani Simanjiro. Pamoja na hayo, Serikali inaendelea kusimamia kwa karibu utendaji wa Kampuni hii

48​

ikiwemo kuimarisha uongozi wa kampuni ili iweze kufikia malengo ya kuanzishwa kwake.

Kampuni ya Kuzalisha Nguzo za Umeme za Zege Tanzania (TCPM)

Mheshimiwa Spika, ikiwa ni hatua ya kuhakikisha uzalishaji wa nguzo za zege unaimarika nchini, Serikali kupitia TCPM ilianza taratibu za ununuzi wa Mkandarasi wa ujenzi wa kiwanda cha kwanza cha kuzalisha nguzo za zege Mkoani Tabora. Aidha, kazi za ujenzi wa kiwanda zinatarajiwa kuanza Mei, 2024. Vilevile, taratibu za kupata fedha kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha pili Mkoani Mbeya zinaendelea.

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia TCPM itashirikiana na Wawekezaji binafsi walioonyesha nia ya kushirikiana kwa mfumo wa ushirikiano wa joint venture katika uzalishaji wa nguzo za zege. Hadi kufikia Machi, 2024 mazungumzo ya awali yamefanyika na Wawekezaji 17 waliowasilisha maombi ya kushirikiana na TCPM. Aidha, uchambuzi wa taarifa za mapendekezo ya kifedha na kiufundi unaendelea ili kupata wawekezaji wenye uwezo wa kushirikiana nao.

Mheshimiwa Spika, TCPM ilisanifu, kusimamia uzalishaji na kusambaza nguzo za zege 1,482 za mita 17 kwa Kampuni ya ETDCO kwa ajili

49​

ya mradi wa kusafirisha umeme wa msongo wa Kilovoti 132 kutoka Mkoa wa Tabora kwenda Mkoa wa Katavi na Wilaya ya Urambo. TCPM pia ilisambaza nguzo 940 za saizi tofauti kwa ETDCO kwa ajili ya miradi mbalimbali. Aidha, kampuni hii ilisambaza nguzo 4,479 za saizi tofauti kwa mikoa mbalimbali ya TANESCO kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa njia za kusambaza umeme.

Kampuni ya Uendelezaji wa Rasilimali ya Jotoardhi (TGDC)

Mheshimiwa Spika, ili kuimarisha upatikanaji wa umeme nchini kupitia vyanzo mbalimbali, Serikali iliendelea kutekeleza miradi ya kuzalisha umeme kupitia jotoardhi, ambapo kipaumbele kilielekezwa katika miradi mitano (5) ya Ngozi (MW

na Kiejo-Mbaka (MW 60) iliyopo mkoani Mbeya, Songwe (MW 5) mkoani Songwe, Luhoi (MW 5) mkoani Pwani na Natron (MW 60) mkoani Arusha.

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia TGDC inaendelea na taratibu za kuwapata Wakandarasi wa kuchoronga visima vya uhakiki (drilling contractor), tathmini ya visima (well testing services) na ununuzi wa bidhaa/malighafi za uchorongaji wa visima vya uhakiki vya jotoardhi Ngozi na shughuli za uchorongaji wa visima hivyo zinatarajiwa kuanza Juni, 2024. Aidha, mradi wa Ngozi utatekelezwa kwa awamu mbili ambapo

50​

awamu ya kwanza inatarajiwa kuanza na uzalishaji wa MW 30 na inatarajiwa kugharimu Dola za Marekani milioni 144 sawa na takribani Shilingi bilioni 367.9. Kiambatisho Na. 4 ni mtambo wa uchorongaji ukiwa umesimikwa kwa ajili ya uhakiki wa jotoardhi katika eneo la mradi wa jotoardhi wa Ngozi.

Mheshimiwa Spika, kazi nyingine zilizotekelezwa katika miradi ya jotoardhi ni pamoja na:

Kuendelea na taratibu za kuajiri Mshauri Mwelekezi (drilling consultant) kwa ajili ya kusanifu na kusimamia uchorongaji (drilling program) wa visima vya uhakiki vya jotoardhi katika Mradi wa Kiejo–Mbaka pamoja na tathmini ya ardhi na ulipaji fidia kwa wananchi wanaopisha utekelezaji wa mradi. Aidha, maandalizi ya kupata mtambo mdogo wa kuzalisha umeme (well head generator) yanaendelea. Mradi huu utatekelezwa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza inatarajiwa kuanza na MW 10. Gharama za mradi huu ni Dola za Marekani milioni 75 sawa na takribani Shilingi bilioni 191.6;

Taratibu za upatikanaji wa ardhi kwa ajili ya uchorongaji wa visima vya uhakiki vya jotoardhi na kujenga uelewa kwa wananchi na wadau mbalimbali kuhusu manufaa ya

51​

mradi kupitia warsha mbalimbali zimekamilika katika mradi wa Songwe. Maandalizi ya uchoronganji wa visima vya uhakiki katika eneo la mradi yanaendelea. Gharama za kutekeleza mradi huu ni Dola za Marekani milioni 32 sawa na takribani Shilingi bilioni 81.8;

Maandalizi ya uchorongaji wa visima vinne (4) vya uhakiki vya jotoardhi pamoja na kufanya upembuzi yakinikifu wa matumizi mengineyo unaendelea katika mradi wa Luhoi. Gharama za kutekeleza mradi huu ni Dola za Marekani milioni 32 sawa na takribani Shilingi bilioni 81.8; na

Kuendelea na taratibu za kuajiri Mshauri Mwelekezi kwa ajili ya kufanya utafiti wa kina (detailed geoscientific surface exploration) Aprili, 2024 ili kuanza utafiti wa kina wa kijiosayansi katika mradi wa Natron MW 60. Gharama za kutekeleza mradi huu ni Dola za Marekani milioni 288 sawa na takribani Shilingi bilioni 735.8.

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia TGDC ilikamilisha taratibu za kukidhi vigezo vya kupata ruzuku kutoka kwa Washirika wa Maendeleo, ikiwemo mfuko wa Geothermal Risks Mitigation Facility (GRMF) unaoratibiwa na Kamisheni ya

52​

Umoja wa Afrika kwa ajili ya kupata fedha za kuendeleza vyanzo hivyo. Vilevile, Mfuko wa Climate Action Africa kupitia Serikali ya Canada umeridhia kutoa msaada wa kiufundi (Technical Assistance) kwa ajili ya kufanya utafiti wa kina wa kijiosayansi katika eneo la mradi wa Meru Mkoani Arusha na mfuko wa GRMF HEAT umeridhia kutoa Dola za Marekani milioni 1.6 kwa ajili ya utafiti wa kina wa kijiosayansi kwa mradi wa jotoardhi Manyara mkoani Manyara. Jitihada nyingine zinazoendelea ni pamoja na kutoa elimu kwa wananchi na wadau mbalimbali kuhusu manufaa ya miradi ya jotoardhi.

Mheshimiwa Spika, ikiwa ni hatua ya kuhamasiaha uwekezaji na matumizi ya rasilimali za jotoardhi, Tanzania itakuwa mwenyeji wa Kongamano la 10 la Jotoardhi (African Rift Geothermal Conference-ARGeo C10) litakalofanyika Novemba, 2024 Jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo litahusisha Nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki zilizopitiwa na bonde la ufa.

B.1.7 UZALISHAJI WA UMEME KUPITIA SEKTA BINAFSI

Mheshimwa Spika,
Serikali kupitia TANESCO inanunua umeme kutoka kwa wazalishaji wadogo wa umeme ambao wanasaidia kuongeza upatikanaji wa umeme nchini. Wazalishaji hao

53​

wanachangia jumla ya MW 31.8 ambapo MW 26.8 zimeingizwa katika Gridi ya Taifa na MW 5.00 nje ya Gridi ya Taifa. Changamoto wanazokutana nazo wazalishaji hao ni pamoja na upungufu wa malighafi za kuzalisha umeme ikiwemo maji, magome ya miti na mabaki ya miwa kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi na hivyo kuathiri uzalishaji wao. Kiambatisho Na. 5 ni Wazalishaji Wadogo wa Umeme (SPPs) waliosajiliwa.

Mheshimwa Spika, Serikali imeingia mikataba na wawekezaji 20 ambao bado wapo katika hatua ya ujenzi wa miundombinu ya uzalishaji wa umeme ambao kwa ujumla wataongeza uwezo wa uzalishaji wa umeme kiasi cha MW 86.31.

B.1.8 MIRADI YA NISHATI VIJIJINI

Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili (REA III Round II)

Mheshimiwa Spika,
Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini iliendelea kutekeleza Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili unaolenga kukamilisha kupeleka umeme kwenye vijiji 4,071 vilivyobaki kati ya vijiji vyote 12,318. Hadi kufikia Machi 2024, jumla ya vijiji 11,837 sawa na asilimia 96.37 ya

54​

vijiji vyote Tanzania Bara vilikuwa vimepelekewa umeme. Aidha, REA imejenga njia za umeme za Msongo wa Kati zenye urefu wa kilomita 22,578 kati ya kilometa 23,619 sawa na asilimia 95.6 pamoja na njia za umeme wa Msongo Mdogo zenye urefu wa kilomita 8,214 kati ya kilometa 12,159 sawa na asilimia 67. Vilevile, transfoma 3,686 kati ya 4,071 sawa na asilimia 90.54 zimefungwa hivyo kuunganisha wateja 54,626. Kutokana na hatua zinazochukuliwa za kupeleka umeme vijijini, jumla ya taasisi 63,509 zinazotoa huduma kwa ajamii ikiwa ni pamoja na za Elimu, Biashara, Pampu za Maji, Vituo vya Afya na Nyumba za Ibada zilikuwa zimeunganishiwa umeme kama inavyoonekana katika Kiambatisho Na.6 ikilinganishwa na taasisi 43,925 za Aprili, 2023.

Mradi wa Kusambaza Umeme katika Vitongoji – (Hamlet Electrification Project – HEP)

Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2023/24 Serikali iliendelea kutekeleza azma ya kuhakikisha vitongoji vyote nchini vinapatiwa huduma ya umeme ili kuharakisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii vitongojini. Hadi kufikia Machi, 2024 Wakandarasi wa kutekeleza miradi ya kuunganisha umeme katika vitongoji 667 katika Mikoa ya Songwe na Kigoma walikuwa wanaendelea na kazi ya ujenzi wa miundombinu ya umeme katika

55​

vitongoji hivyo. Mradi huu unatarajiwa kukamilika Juni, 2025. Aidha, REA ipo katika hatua za ununuzi wa wakandarasi wa kutekeleza Mradi wa Kupeleka Umeme katika Vitongoji 15 kwa kila Jimbo.

c) Mradi wa Ujazilizi Mzunguko wa Pili B

Mheshimiwa Spika,
mradi huu unalenga kuongeza wigo wa usambazaji umeme kwenye vitongoji ambavyo vimepitiwa na njia ya kusafirisha umeme ya Msongo wa Kati katika mikoa tisa (9) ya Arusha, Geita, Kagera, Katavi, Kigoma, Lindi, Morogoro, Njombe na Songwe. Hadi kufikia Machi 2024, jumla ya kilomita 103 za umeme wa Msongo Mdogo zimejengwa na nguzo kilomita 1,458 zimesimikwa kati ya 3,860. Mradi huu unatarajiwa kukamilika Novemba, 2025.

Mradi wa Ujenzi wa Gridi Ndogo (Mini Grids) katika Maeneo ya Visiwa na Maeneo Yaliyo Mbali na Gridi ya Taifa

Mheshimiwa Spika, mradi unahusisha kupeleka umeme katika visiwa kwa kutumia gridi ndogo zinazozalisha umeme kwa kutumia nishati ya jua kwenye maeneo ya visiwa ambavyo havijafikiwa na Gridi ya Taifa. Hadi kufikia Machi, 2024 kazi zilizotekelezwa ni kuchambua maombi yaliyowasilishwa, kusaini mikataba miwili (2) kati ya saba (7) na kuanza kutekeleza mradi ambapo

56​

wateja 1,403 wameunganishiwa umeme kati ya 14,168 katika vijiji 34 kati ya 85.

Mradi wa Kuwezesha Ujenzi wa Vituo Vidogo vya Kuuzia Bidhaa za Petroli Vijijini kwa Njia ya Mikopo

Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu kusogeza huduma ya bidhaa ya mafuta ya petroli kwa wananchi wanaoishi vijijini kwa kutoa mikopo kwa waendelezaji wa vituo vya mafuta ili waweze kuwekeza katika maeneo ya vijijini. Tayari zoezi la kuwapata waendelezaji wa vituo hivyo vijijini limefanyika kupitia Wakala wa Nishati Vijijini ambapo maombi ya waendelezaji 10 yaliyokidhi vigezo vya kiufundi yamewasilishwa Benki ili kufanyiwa tathmini ya kifedha. Kufuatia uzoefu uliopatikana katika maombi yaliyowasilishwa wakati fursa hii ilipotangazwa awali, vigezo na masharti ya utolewaji wa mikopo hiyo vimepitiwa upya na kuboreshwa ili kuwawezesha waombaji wengi kunufaika na fursa hiyo na hivyo kuimarisha ujenzi wa vituo hivyo vijijini. Aidha, tarehe 25 Machi 2024, Wakala ulitangaza Awamu ya Pili ya fursa za upatikanaji wa mikopo hiyo ambapo kwa sasa hakuna ukomo wa uwasilishwaji wa maombi. Kupitia utaratibu huu, kwa maombi yatakayobainika kutokidhi vigezo, waombaji husika watakuwa na nafasi ya kufanya marekebisho ya maombi yao katika maeneo yenye upungufu na kuyawasilisha tena.

57​

Programu ya Kuwezesha Waendelezaji wa Miradi Midogo ya Nishati Jadidifu Vijijini chini ya Utaratibu wa Kusaidia Uandaaji wa Miradi (PPSF)

Mheshimiwa Spika,
Mradi huu unahusu kuwawezesha waendelezaji miradi ya nishati jadidifu vijijini ambao wana upungufu wa mitaji ili waweze kuandaa maandiko ya miradi ikiwemo Mpango wa Biashara. Hadi kufikia Machi, 2024 kazi zilizotekelezwa ni pamoja na kusaini mikataba miwili (2) iliyopatikana katika Call for Proposal Awamu ya Kwanza na kuendelea na uchunguzi wa kina kwa waendelezaji waliokidhi vigezo baada ya tathmini iliyofanyika (due diligence). Aidha, Wakala unaendelea kuandaa kabrasha kwa ajili ya kutangaza fursa hizo kwa Awamu ya Nne.

Mpango wa Uendelezaji Miradi ya Nishati Jadidifu Inayofua Umeme kwa Kutumia Maporomoko ya Maji

Mheshimiwa Spika, Mpango huu unahusisha Serikali kutoa ruzuku kwa Waendelezaji wa miundombinu ya miradi midogo ya kuzalisha umeme kwa kutumia maporomoko ya maji vijijini ili wapate motisha ya kuiendeleza. Hadi kufikia Machi, 2024 Serikali kupitia REA iliendelea kutoa ruzuku kwa waendelezaji wa Miradi midogo ya kufua umeme kwa kutumia nguvu ya maji. Jumla ya miradi minne (4) imepata ruzuku ikijumuisha Ijangala (kW

58​

uliopo Makete – Shilingi milioni 426; Lupali (kW 317) uliopo Ludewa Shilingi bilioni 2.9; Lugarawa (kW 1,700) uliopo Njombe Shilingi milioni 495 na Kilolo/Maguta (kW 2,400) uliopo Kilolo Iringa Shilingi milioni 969.9. Aidha, ujenzi wa Mradi wa Ijangala umekamilika na kuzinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango Oktoba 2023. Pia, utekelezaji wa Mradi wa Lupali umefikia asilimia 90; Mradi wa Lugarawa asilimia 75; na Mradi wa Kilolo umefikia asilimia 92.

B.1.9 UTEKELEZAJI WA MIKAKATI NA MIPANGO MBALIMBALI YA UENDELEZAJI WA SEKTA NDOGO YA UMEME NA NISHATI JADIDIFU

Mheshimiwa Spika,
Serikali kupitia Wizara ya Nishati imeendelea kuandaa na kutekeleza Mipango na Mikakati mbalimbali ya kuendeleza Sekta ya Nishati kama ifuatavyo:

Uhuishaji wa Mpango Kabambe wa Kuendeleza Sekta Ndogo ya Umeme wa Mwaka 2020 (Power System Master Plan Update 2020)

Mheshimiwa Spika, ikiwa ni hatua ya kuhakikisha uwekezaji katika Sekta Ndogo ya Umeme unaendana na mahitaji yanayotokana na ukuaji wa shughuli za kiuchumi na kijamii, Serikali iliendelea na zoezi la kuhuisha Mpango Kabambe wa

59​

Kuendeleza Sekta Ndogo ya Umeme wa Mwaka 2020. Kazi zilizotekelezwa ni pamoja na ukusanyaji wa mahitaji ya umeme kwa kila mkoa Tanzania Bara na Zanzibar; na utambuzi wa maeneo ya uwekezaji wa miradi ya nishati jadidifu na kiwango cha nishati jadidifu (jua na upepo) kinachotakiwa kuingizwa kwenye Gridi ya Taifa. Kazi hii inafanyika kwa ufadhili wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na inatarajiwa kukamilika Agosti, 2024.

Mkakati wa Nishati Jadidifu na Mpango wa Utekelezaji wa Mkakati (Renewable Energy Strategy and its Implementation Roadmap)

Mheshimiwa Spika, ili kuweza kuimarisha upatikanaji wa umeme nchini, Serikali inaandaa Mkakati na Mpango wa Utekelezaji wa Nishati Jadidifu. Kwa sasa Mshauri Mwelekezi anakamilisha uandaaji wa Mkakati baada ya kupokea maoni ya wadau. Kazi hii inafadhiliwa na Benki ya Dunia kupitia Mradi wa Tanzania Rural Energy Expansion Programme-TREEP na inatarajiwa kukamilika Juni, 2024.

60​

Mkakati wa Matumizi Bora ya Nishati na Uhuishaji wa Mpango Kazi wa Matumizi Bora ya Nishati (Energy Efficiency Strategy and Update of the Energy Efficiency Action Plan)

Mheshimiwa Spika, Serikali inashirikiana na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kuandaa Mkakati na Mpango kazi wa Matumizi Bora ya Nishati. Mkakati huo unaandaliwa ili kukidhi matakwa ya kitaifa na kimataifa ya kupunguza matumizi ya nishati yasiyo ya lazima, upotevu na gharama za nishati, kuhamasisha utunzaji wa mazingira pamoja na kukuza mchango wa nishati katika maendeleo ya nchi. Tayari Mkakati huo umeandaliwa na kuwasilishwa kwa wadau kwa maoni kabla ya kukamilishwa na kuanza kutumika.

Mheshimiwa Spika, zoezi la uandaaji wa Mkakati huo limehusisha pia uaandaji wa viwango vya matumizi ya vifaa vya nishati vinavyoruhusiwa (minimum energy performance standards and labelling); uboreshaji wa taarifa za matumizi na watumiaji wakubwa wa nishati; kuandaa na kutekeleza miongozo ya watumiaji wakubwa wa nishati; kuandaa sifa za wataalamu katika usiamamizi na ukaguzi wa matumizi ya nishati (professional qualification and skills in energy management and audit) na kujenga uelewa kwa

61​

umma kuhusu faida na fursa za matumizi bora ya nishati.

Mkakati wa Kitaifa wa Nishati ya Tungamotaka (Biomass Energy Strategy

– BEST)

Mheshimiwa Spika, Wizara imekamilisha majadiliano na Umoja wa Ulaya ya kuwezesha kupata ufadhili kwa ajili ya kuandaa Mkakati wa Kitaifa wa Nishati ya Tungamotaka ili kuwa na mwongozo thabiti wa uendelezaji wa rasilimali ya tungamotoka ambayo ni endelevu na isiyokuwa na athari kubwa za kiafya na mazingira.

Utekelezaji wa Mpango Kabambe wa Kupeleka Nishati Vijijini (Rural Energy Master Plan-REMP)

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia REA inaendelea na utekelezaji wa Mpango Kabambe wa Nishati Vijijini (Rural Energy Master Plan-REMP) ili kuhakikisha ifikapo mwaka 2030 huduma ya nishati vijijini iwe inapatikana kwa asilimia 100 na asilimia 80 ya Watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupikia.

62​

Mikakati na Mipango Mbalimbali ya Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia

Mheshimiwa Spika, Serikali imeidhinisha Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia wa mwaka 2024 - 2034. Mkakati huu pamoja na mambo mengine, unalenga kukuza matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa watanzania kwa kuimarisha upatikanaji wa malighafi na miundombinu ya uhakika ya nishati safi ya kupikia; kupunguza gharama za nishati safi, vifaa na majiko sanifu ya kupikia; kuandaa, kuhuisha na kuoanisha Sera, Sheria, Kanuni na miongozo wezeshi ya kufanikisha matumizi ya nishati safi ya kupikia; kuhamasisha uwekezaji katika nishati safi ya kupikia; kuongeza wigo wa tafiti na ubunifu wa teknolojia zinazohusu nishati ya kupikia; na kuimarisha uelewa wa jamii kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana na wadau iliratibu na kushiriki katika mkutano wa 28 wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP28) uliofanyika Dubai Novemba-Desemba, 2023. Katika Mkutano huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alizindua Programu ya Nishati Safi ya kupikia itakayowawezesha Wanawake Barani Afrika (African Women Clean Cooking Support Programme-AWCCSP) kutumia nishati safi

63​

ya kupikia. Aidha, Mei, 2024 kutafanyika mkutano wa Wakuu wa Nchi kuhusu Nishati Safi ya Kupikia Barani Afrika, Paris Ufaransa ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan atakuwa Mwenyekiti Mwenza wa mkutano huo kwa kushirikiana na Waziri Mkuu wa Norway, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Nishati Duniani (International Energy Agency-IEA) na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB). Mkutano huo pamoja na mambo mengine, unalenga kujadili na kuweka mikakati ya namna ya kuimarisha Sera, ugharamiaji na ushirikiano katika kuimarisha matumizi ya nishati safi ya kupikia Barani Afrika.

Mheshimiwa Spika, ikiwa ni hatua ya kuhakikisha Umma wa Watanzania unapata elimu kuhusu nishati safi ya kupikia, Wizara iliandaa kongamano la wanawake la nishati safi ya kupikia lililofanyika Mkoani Dodoma tarehe 9 Machi, 2024 katika kipindi cha siku ya wanawake duniani. Kongamano hilo pamoja na mambo mengine, lilihusisha utoaji wa elimu kwa wananchi kuhusu nishati safi ya kupikia, pamoja na ugawaji wa mitaji na vitendea kazi vya nishati safi ya kupikia. Vilevile, Wizara kwa kushirikiana na UNCDF kupitia ufadhili wa Umoja wa Ulaya inaanda mpango wa kuzijengea miundombinu ya nishati safi ya kupikia taasisi za kijamii zinazolisha zaidi ya watu 100 kwa siku katika mikoa ya Mwanza, Dodoma, Morogoro, Pwani na Dar es Salaam.

64​

Mheshimiwa Spika, ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Wizara ya Nishati kupitia Wakala wa Nishati Vijijini, imesaini mkataba wa ushirikiano na Jeshi la Magereza ili kuwezesha Jeshi hilo pamoja na vituo inavyovisimamia ikiwemo Magereza 129, Kambi za Makazi ya Watumishi 47, Ofisi 26, Vyuo vinne (4), Shule moja (1) na Hospitali moja (1) kutumia nishati safi ya kupikia. Katika maeneo hayo, jumla ya mifumo 126 ya bayogesi, 64 ya LPG pamoja na majiko banifu itajengwa na kuwezesha ununuzi wa mashine 61 za kuzalisha mkaa mbadala. Sambamba na hilo, jumla la mitungi 15,920 ya gesi ya LPG itagawiwa kwa Watumishi wa Jeshi hilo. Aidha, Wakala wa Nishati Vijijini unakamilisha taratibu za kuwezesha Jeshi la Kujenga Taifa pamoja na taasisi nyingine hususan za elimu na afya kutumia nishati safi ya kupikia.

Kuridhiwa kwa Mkataba wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati Jadidifu wa Mwaka 2009 (Statute of the International Renewable Energy Agency – IRENA, 2009)

Mheshimiwa Spika, ili kuvutia uwekezaji, utaalamu, teknolojia, utafiti na mitaji katika uendelezaji wa nishati jadidifu, Tanzania ilijiunga na Mkataba wa Wakala wa Kimataifa wa

65​

Nishati Jadidifu wa Mwaka 2009 (Statute of the International Renewable Energy Agency – IRENA, 2009). Hatua hii itaongeza kasi ya uendelezaji wa nishati jadidifu nchini na hivyo mchango wa chanzo hicho katika uzalishaji wa nishati ya umeme iliyo nafuu, ya gharama nafuu na rafiki wa mazingira.

B.2 SEKTA NDOGO YA MAFUTA NA GESI ASILIA

Mheshimiwa Spika,
katika mwaka 2023/24 Serikali iliendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuendeleza Sekta Ndogo ya Mafuta na Gesi Asilia nchini katika maeneo ya utafutaji, uendelezaji, uzalishaji, uchakataji, usafirishaji na usambazaji wa bidhaa za mafuta na gesi, ambapo mafanikio mbalimbali yaliweza kupatikana.

B.2.1 MIRADI YA UTAFUTAJI WA MAFUTA NA GESI ASILIA KATIKA VITALU VYA KIMKAKATI

Kitalu cha Mnazi Bay Kaskazini

Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu utafutaji wa mafuta na gesi asilia katika Kitalu cha Mnazi Bay Kaskazini kilichopo bahari ya kina kifupi Kusini Mashariki mwa Tanzania. Hadi kufika Machi 2024, shughuli zilizotekelezwa ni pamoja na kuanza majadiliano na Kampuni ya Maurel & Prom

66​

(M&P) ambayo imeonesha nia ya kushirikiana na TPDC katika kazi za utafutaji wa mafuta na gesi asilia kwenye kitalu hiki ikiwemo uchorongaji wa visima vya utafiti. Aidha, maombi ya leseni ya utafutaji wa mafuta na gesi asilia katika kitalu husika yapo katika hatua ya uidhinishwaji.

Kitalu cha Eyasi– Wembere

Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusisha utafutaji wa mafuta katika kitalu cha Eyasi – Wembere kilichopo kwenye Bonde la Ufa la Afrika Mashariki, Kaskazini Mashariki mwa Tanzania. Hatua iliyofikiwa ni pamoja na kukamilisha kazi ya kukusanya na kuchakata taarifa za mitetemo za mfumo wa 2D zenye urefu wa kilometa 260 katika awamu ya kwanza, kukamilisha tafsiri ya awali, kuandaa mpango wa awamu ya pili wa ukusanyaji wa taarifa za mitetemo za mfumo wa 2D zenye urefu wa kilomita 1,100; na kukamilika kwa kazi ya ulipaji wa fidia kwa wananchi walioathiriwa na zoezi la ukusanyaji wa taarifa za mitetemo. Aidha, TPDC inaendelea na hatua ya kumpata mkandarasi wa kufanya tafsiri ya tathmini ya kina ya taarifa za awamu ya kwanza na mkandarasi atakayekusanya taarifa za awamu ya pili ya kazi hii.

67​

Kitalu cha Songo Songo Magharibi

Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusisha utafutaji wa mafuta na gesi asilia katika Kitalu cha Songo Songo Magharibi ili kuimarisha upatikanaji, uzalishaji na usambazaji wa gesi asilia kwa matumizi mbalimbali nchini. Kazi zilizotekelezwa ni pamoja na kuanza taratibu za kumpata Mshauri Mwelekezi wa uchorongaji wa visima ambaye atafanya mapitio ya taarifa za kijiolojia na kijiofizikia katika Kitalu na kuandaa rasimu ya Mpango wa Uchorongaji wa visima vya utafiti. Aidha, katika kuimarisha usimamizi na utekelezaji wa mradi husika, TPDC kwa kushirikiana na Kampuni ya Pertamina ya nchini Indonesia inaratibu mafunzo kwa vitendo nchini Indonesia kwa Wataalamu 100 ili kuwajengea uwezo katika masuala ya utafutaji na uendelezaji wa mafuta na gesi asilia. Aidha, awamu ya kwanza Watalaamu watano (5) wameshapelekwa kwenye mafunzo hayo.

Vitalu Namba 4/1B na 4/1C

Mheshimiwa Spika, mradi huu unalenga utafutaji wa mafuta na gesi asilia katika kitalu namba 4/1B na 4/1C ili kuongeza upatikanaji, uzalishaji na usambazaji gesi asilia. Hadi kufikia Machi, 2024 kazi zilizotekelezwa ni pamoja na kukamilisha taratibu za kusaini Makubaliano ya Awali (Memorandum of Understanding – MoU) ya

68​

mashirikiano kati ya TPDC na kampuni ya CNOOC kutoka China. Makubaliano hayo yanalenga kushirikiana katika tafiti za awali kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo vitalu hivyo.

B.2.2 MIRADI YA UTAFUTAJI NA UENDELEZAJI WA MAFUTA NA GESI KATIKA VITALU KUPITIA PSA

Kitalu cha Ruvuma (Ntorya)

Mheshimiwa Spika
, mradi huu unahusisha uendelezaji gesi asilia iliyogunduliwa katika eneo la Ntorya katika kitalu cha Ruvuma. Hadi kufikia Machi, 2024 kazi zilizotekelezwa ni pamoja na kukamilisha tafsiri ya taarifa za mitetemo za mfumo wa 3D zilizokusanywa katika eneo la kilomita za mraba 334.9 na kuendelea na maandalizi ya ukarabati na majaribio ya visima (well tests) kwa visima vya Ntorya 1 na Ntorya 2. Aidha, Mkandarasi anaendelea na hatua za ununuzi wa mtambo wa kuchoronga kisima cha Chikumbi-1. Vilevile, Baraza la Mawaziri limeridhia kutolewa kwa leseni ya uendelezaji wa Kitalu hiki ambapo taratibu za utoaji wa leseni hiyo kwa TPDC kwa niaba ya mwekezaji (Kampuni ya ARA Petroleum) zinakamilishwa.

Mheshimiwa Spika, maandalizi ya ujenzi wa bomba la kutoa gesi Ntorya kupeleka kwenye

69​

kiwanda cha kuchakata gesi cha Madimba yanaendelea ambapo Tathmini ya Athari za Mazingira na Jamii (ESIA) imekamilika na Mshauri Mwelekezi wa uhandisi na ujenzi anakamilisha upembuzi yakinifu wa kihandisi ili kuwezesha zabuni ya ujenzi wa bomba kutangazwa.

B.2.3 MRADI WA KUCHAKATA NA KUSINDIKA GESI ASILIA KUWA KIMIMINIKA (LIQUEFIED NATURAL GAS – LNG)

Mheshimiwa Spika
, mradi huu unatekelezwa katika eneo la Likong’o mkoani Lindi na utahusisha usindikaji wa gesi asilia iliyogunduliwa katika Vitalu Na. 1, 2 na 4 vilivyopo katika kina kirefu cha bahari. Serikali kupitia Timu yake ya Majadiliano (Government Negotiation Team) imekwishafanya uchambuzi wa rasimu za Mkataba wa Nchi Hodhi (Host Government Agreement - HGA) na Mkataba wa Uzalishaji na Ugawanaji Mapato Ulioboreshwa (Amended Production Sharing Agreement – PSA) kwa ajili ya kuboreshwa kupitia majadiliano na wawekezaji kabla ya kuidhinishwa na Serikali kwa kuzingatia maoni yaliyotolewa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na taasisi nyingine za Serikali katika rasimu za awali za Mikataba hiyo.

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia TPDC imeendelea kushirikiana na Kampuni za Shell na Equinor kufanya maandalizi ya kutekeleza

70​

miradi ya uboreshaji wa hali ya maisha kwa wananchi waliopisha eneo la mradi (post compensation livelihood restoration program), ikiwemo kusaini Mkataba wa Makubaliano ya ujenzi wa shule ya msingi ya Likong'o iliyopo Manispaa ya Lindi.

B.2.4 UJENZI WA MIUNDOMBINU YA USAFIRISHAJI NA USAMBAZAJI WA GESI ASILIA

Usambazaji wa Gesi Asilia katika Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani

Mheshimiwa Spika
, mradi huu unahusisha ujenzi wa miundombinu ya kusambaza gesi asilia katika Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani kwa njia ya mabomba. Kazi zilizotekelezwa ni pamoja na ujenzi wa bomba lenye urefu wa kilometa 12.4 kutoka Mwenge hadi Mbezi Beach lililowezesha kuunganishwa kwa miundombinu ya gesi asilia kwenye viwanda viwili (2) vya Chemi and Cotex Industrial Ltd na Cotex Ltd pamoja na kuunganisha miundombinu ya gesi asilia katika hoteli sita (6) za White Sand Hotel, Land Mark Hotel, Serene Beach Resort, Ramada Resort, Giraffe Hotel na Jangwani Sea Breeze. Vilevile, kiwanda cha Sapphire Float Glass (Tanzania) Co. Ltd kiliunganishwa na miundombinu ya gesi asilia katika Mkoa wa Pwani.

71​

Mheshimiwa Spika, kazi nyingine zilizotekelezwa ni kufanya tafiti na kuandaa andiko la mradi wa kuunganisha gesi asilia katika gereza la Ukonga na nyumba za askari katika magereza ya Ukonga na Keko.

Usambazaji wa Gesi Asilia katika Mikoa ya Lindi na Mtwara

Mheshimiwa Spika
, mradi huu unahusisha ujenzi wa miundombinu ya kusambaza gesi asilia kwa njia ya mabomba katika Mikoa ya Lindi na Mtwara. Kazi zilizofanyika ni pamoja na ujenzi wa kituo cha kupunguza msukumo wa gesi (Pressure Reduction Station – PRS) na miundombinu ya umeme yenye urefu wa kilomita 3.8 kutoka makutano ya Mahumbika hadi Valvu Namba 3 (BVS 3) na bomba la kusafirisha gesi asilia kutoka BVS 3 kuelekea Kata za Mnazi Mmoja na Mingoyo mkoani Lindi lenye urefu wa kilomita 10.04. Bomba hilo limewezesha kuunganisha nyumba 209 ambazo zilikuwa na miundombinu ya gesi asilia tangu awali. Kiambatisho Na.7 ni miundombinu ya kusambaza gesi asilia katika maeneo mbalimbali nchini.

Usambazaji wa Gesi Asilia Kupitia Mfuko wa Nishati Vijijini - Awamu ya Kwanza na Pili

72​

Mheshimiwa Spika, mradi huu unatekelezwa na TPDC kwa kushirikiana na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na unalenga kusambaza gesi asilia na kuimarisha upatikanaji wa nishati safi ya kupikia katika maeneo ya vijijini. Kazi zilizotekelezwa ni pamoja na kukamilisha taratibu za kumpata Mkandarasi wa kujenga miundombinu ya kuunganisha nyumba 451 mkoani Lindi (Kata za Mnazi Mmoja na Mingoyo) na nyumba 529 mkoani Pwani (Mkuranga). Mradi huu unatekelezwa kwa ufadhili wa REA kwa gharama ya Shilingi bilioni 6.82 kama sehemu ya utekelezaji wa mkakati wa kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia katika maeneo ya vijijini.

Mheshimiwa Spika, vilevile, TPDC imekamilisha utafiti wa kubaini mahitaji ya gesi asilia katika mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara. Maeneo ya vijijini katika mikoa hiyo yatajengewa miundombinu ya kusambazia gesi asilia kwa ajili ya kupikia ikilenga makazi na taasisi za kibiashara na zisizo za kibiashara ili kupunguza matumizi ya kuni na mikaa kama sehemu ya utekelezaji wa awamu ya pili ya mradi huo.

Ujenzi wa Vituo vya Kujaza Gesi Asilia (Compressed Natural Gas-CNG) katika Magari kwenye Bohari za Dar es Salaam na Dodoma

73​

Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Machi, 2024 TPDC na GPSA ziliendelea na taratibu za kumpata Mshauri Mwelekezi wa kufanya kazi ya upembuzi yakinifu, usanifu wa michoro ya kihandisi na Tathmini ya Athari ya Mazingira na Jamii ili kuwezesha GPSA kujenga vituo vya CNG katika bohari za Dar es Salaam na Dodoma unaotarajiwa kuanza mwaka 2024/25. Lengo la mradi huu ni kuhamasisha matumizi ya gesi asilia katika vyombo vya moto vinavyomilikiwa na Serikali kwa kuongeza upatikanaji wake katika maeneo mbalimbali nchini.

Ushiriki wa Sekta Binafsi katika Ujenzi na Uendeshaji wa Vituo vya Kujaza Gesi Asilia (CNG) katika Magari

Mheshimiwa Spika
, kwa kushirikiana na Sekta Binafsi, vituo viwili vya kujaza gesi asilia (CNG) katika magari vilijengwa na kuanza kutoa huduma Novemba, 2023. Vituo hivyo ni kinachomilikiwa na Kampuni ya TAQA-Dalbit kilichopo pembezoni mwa barabara ya Nyerere karibu na Kiwanja cha Ndege (Terminal II) na kituo kinachomilikiwa na Kampuni ya Dangote kilichopo Mwanambaya, Mkuranga mkoani Pwani.

Mheshimiwa Spika, karakana nane (8) za kubadilisha mifumo ya matumizi ya nishati ya gesi asilia (CNG) kwenye magari ambayo ni nyenzo

74​

muhimu ya kuchochea matumizi ya gesi asilia katika magari zimejengwa na zinamilikiwa Taasisi za Umma na Sekta Binafsi. Karakana hizo ni NK CNG Auto Limited (Mbezi Beach, Dar es Salaam), MOL CNG Limited na TEMESA (Keko, Dar es Salaam), Kleenair CNG (Kigamboni, Dar es Salaam), TAQA Dalbit (Kipawa, Dar es Salaam), DIT (Dar es Salaam), BQ Contractors Limited (Goba, Dar es Salaam) na Kampuni ya Dangote ambayo imejenga karakana yake katika eneo la kiwanda Mkoani Mtwara kwa ajili ya kuhudumia magari ya kiwanda hicho. Jitihada hizi zimewezesha kuongezeka kwa magari yanayotumia mfumo wa gesi asilia kutoka 3,100 hadi 4,500.

Mradi wa Kujenga Uwezo wa Kusimamia Usambazaji wa Gesi Asilia Nchini

Mheshimiwa Spika,
Wizara inashirikiana na JICA kutekeleza mradi wa kujenga uwezo wa kusimamia usambazaji wa gesi asilia nchini (Capacity Development of Natural Gas Utilization in Tanzania). Mradi huu unalenga kuhuisha Mpango Kabambe wa Matumizi ya Gesi Asilia Nchini (Natural Gas Utilization Master Plan - NGUMP), kufanya usanifu wa mtandao wa usambazaji (network design) wa gesi asilia katika Mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma na Pwani na kuwajengea uwezo wataalam wa Wizara na Taasisi. Hadi kufikia Machi, 2024, kazi zilizofanyika ni ukusanyaji wa takwimu

75​

mbalimbali za kuwezesha uhuishaji wa NGUMP ikiwemo mahitaji, uzalishaji na matumizi ya gesi asilia nchini. Mradi huu unatarajiwa kukamilishwa Oktoba, 2025.

B.2.5 MRADI WA BOMBA LA KUSAFIRISHA GESI ASILIA KUTOKA TANZANIA HADI UGANDA

Mheshimiwa Spika,
mradi huu unahusu ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi asilia kutoka Tanzania hadi Uganda. Mradi unalenga kusafirisha gesi asilia pamoja na kuunganisha maeneo yatakayopitiwa na bomba hilo. Hadi kufikia Machi, 2024 kazi zilizotekelezwa ni pamoja na kuridhiwa kwa makubaliano ya mikataba mahsusi kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Uganda (Bilateral Agreement) kwa ajili ya kumpata Mshauri Mwelekezi wa kufanya kazi ya upembuzi yakinifu wa mradi.

B.2.6 MRADI WA KUSAFIRISHA GESI ASILIA KUTOKA DAR ES SALAAM (TANZANIA) HADI MOMBASA (KENYA)

126. Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusisha kusafirisha gesi asilia kutoka Dar es Salaam kwenda Mombasa - Kenya na pia unatarajiwa kunufaisha Mikoa ya Pwani, Tanga, Arusha na Kilimanjaro. Hadi kufikia Machi, 2024

76​

Kamati ya Pamoja ya Wataalamu imekamilisha maboresho ya nyaraka za maridhiano kwa ajili ya kumpata Mshauri Mwelekezi atakayefanya upembuzi yakinifu wa mradi.

B.2.7 MIRADI YA KUHIFADHI NA KUSAFIRISHA MAFUTA

Mradi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi kutoka Hoima - Uganda hadi Tanga - Tanzania (East African Crude Oil Pipeline – EACOP)

Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa mradi huu unaendelea katika mwaka 2023/24 ambapo hadi kufikia Machi, 2024 kazi zilizotekelezwa ni pamoja na kukamilisha malipo ya fidia kwa wananchi ya Shilingi bilioni 34.93 kwa wananchi 9,823 kati ya 9,904 waliopisha utekelezaji wa mradi, sawa na asilimia 99.2; kukamilika kwa ujenzi wa nyumba 340 sawa na asilimia 100 ya makazi mbadala kwa wananchi 294 waliopoteza makazi na kupisha mkuza; kukamilika kwa ujenzi wa karakana ya kuweka mfumo wa upashaji joto kwenye mabomba; na kuendelea na ujenzi wa maeneo 14 ya makambi. Aidha, mabomba yenye urefu wa kilomita 400 yameshawasili nchini na zoezi la kuwekewa mfumo wa kupasha joto, usalama na mawasiliano wa bomba (thermal insulation and fiber optic cables) linaendelea.

77​

Mheshimiwa Spika, shughuli za awali za ujenzi wa matenki zimefikia asilimia 32, usanifu wa kina wa matenki umefikia asilimia 85, ujenzi wa jeti umefikia asimilia 33 na zoezi la upimaji na uwekaji mawe ya mpaka kwenye mkuza wa bomba umekamilika kwa asilimia 100. Aidha, hadi kufikia Machi, 2024, Serikali ilikuwa imelipa jumla ya Dola za Marekani milioni 289.78 sawa na asilimia 94 ya kiasi kinachotakiwa kuchangiwa kama mtaji katika Kampuni ya EACOP Ltd. Utekelezaji wa Mradi kwa ujumla umefikia asilimia 27.1.

Kielelezo Na. 5: Uzinduzi wa Karakana ya Kuweka Mfumo wa Kupasha Joto Mabomba kwenye Kijiji cha Sojo Wilayani Nzega

78

79​

Mradi wa Bomba Jipya la TAZAMA

Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu ujenzi wa bomba jipya la TAZAMA lenye uwezo wa kusafirisha aina mbalimbali za mafuta safi kutoka Dar es Salaam hadi Zambia kwa kutumia mkuza wa bomba la TAZAMA. Tarehe 23 hadi 25 Oktoba, 2023 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alifanya ziara ya kikazi nchini Zambia ambapo pamoja na mambo mengine, alifanya mazungumzo na Rais wa Zambia kuhusu utekelezaji wa mradi huu. Aidha, kupitia mazungumzo hayo ilikubalika mradi utekelezwe sambamba na ujenzi wa matenki ya kuhifadhia mafuta kwa ukubwa wa tani 380,000 kwa upande wa Dar es salaam - Tanzania na tani 120,000 kwa upande wa Ndola – Zambia. Hadi kufikia Machi, 2024, Timu ya Wataalamu imeundwa kwa ajili ya kuangalia namna bora ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bomba jipya. Sambamba na hilo mkutano wa Mawaziri wa Nishati wa nchi hizi mbili umefanyika kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa utekelezaji wa mradi.

Uanzishwaji wa Hifadhi ya Kimkakati ya Mafuta (Strategic Petroleum Reserve - SPR)

Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu uanzishaji wa hifadhi ya kimkakati ya mafuta

80​

ambayo inahitaji pia uwepo wa maghala ya

kuhifadhia mafuta na ununuzi wa mafuta yenyewe. TPDC ipo katika hatua za kutafuta Mshauri Mwelekezi wa kufanya tathmini ya mradi pamoja na uendeshaji utakaoshirikisha Wizara, TPDC na Sekta Binafsi. Maeneo yaliyopo kwa ajili ya uanzishwaji wa SPR ni pamoja na Chongoleani (Tanga), Zuzu (Dodoma), Isaka (Kahama), Makambako (Njombe) na Kigamboni (Dar es Salaam).

81​

B.2.8 MRADI WA KUJENGA UWEZO WA KUSIMAMIA NA KUENDELEZA RASILIMALI ZA NDANI NA UTAWALA WA RASILIMALI ZA ASILI TANZANIA

Mheshimiwa Spika,
mradi huu ulianza kutekelezwa Juni, 2017 kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mfuko wa Maendeleo wa Afrika (AfDB) na umefikia asilimia 86 ya utekelezaji wake. Kazi zilizotekelezwa katika mwaka 2023/24 ni pamoja na kukamilisha uundaji wa mfumo wa uondoshaji shehena mipakani kwa Tanzania Bara na Zanzibar; ununuzi na usimikaji wa vifaa mbalimbali katika bandari ya Dar es Salaam na Zanzibar, uhuishaji wa Mkataba Kifani wa Ugawanaji Mapato (Model Production Sharing Agreement - MPSA) kupitia PURA na kugharamia mafunzo kwa wataalam kutoka Wizara ya Nishati, PIU, PSC, PURA na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Jumla ya watumishi 77 wamenufaika na mafunzo hayo.

B.2.9 UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA KAMPUNI TANZU ZA TPDC

TANOIL Investments Limited (TANOIL)

Mheshimiwa Spika,
TANOIL iliendelea kushiriki katika biashara ya mafuta kama kampuni ya kununua na kuuza mafuta (Oil

82​

Marketing Company - OMC). Aidha, katika kipindi cha Julai, 2023 hadi Machi, 2024, TANOIL iliweza kuagiza kiasi cha lita milioni 34.2 za dizeli ambapo lita milioni 33.1 zimeshauzwa na lita milioni 16.8 za petroli ziliagizwa na zote zimeshauzwa. Katika kipindi hiki, TANOIL imefanikiwa kupata faida ya Shilingi bilioni 6.8. Vilevile, TANOIL katika kipindi husika imekusanya jumla ya Shilingi bilioni 9.8 kati ya Shilingi bilioni 29 za madeni chechefu kutoka kwa wadaiwa sugu na jitihada za kukusanya madeni yaliyosalia zinaendelea.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa ujenzi na ukarabati wa vituo vya mafuta, TANOIL imekamilisha ukarabati wa vituo viwili vya mafuta katika Mikoa ya Singida na Geita. Vituo hivyo vitaendeshwa kwa mtindo wa kukodisha kwa kampuni binafsi zinazofanya biashara ya mafuta (Company Owned Dealer Operated Model -CODO) kwa makubaliano ya kulipa kodi na kununua mafuta kutoka TANOIL. Aidha, ujenzi wa vituo vya Musoma na Tarime (Mara), Segera (Tanga) na Makuyuni (Arusha) vipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji. Hatua hii itaisaidia TANOIL kuweza kushiriki kwenye biashara ya mafuta katika mnyororo wote wa usambazaji na hivyo kuleta tija kwenye ushindani wa sekta.

83​

Mheshimiwa Spika, kufuatia kukamilika kwa uchunguzi dhidi ya watumishi wa TANOIL walioisababishia hasara kampuni hiyo kwa mujibu wa Taarifa za Hesabu za mwaka 2021/22, Serikali tayari imekwishachukua hatua za kinidhamu ambapo watumishi watatu wamefukuzwa kazi na mmoja kupewa adhabu ya kupunguzwa mshahara kwa asilimia 15. Utekelezaji wa adhabu hizo ni kwa mujibu wa taarifa na mapendekezo ya Kamati ya Uchunguzi iliyoundwa na kwa kuzingatia Taratibu na Miongozo katika Utumishi wa Umma. Aidha, TAKUKURU inaendelea na uchunguzi wa tuhuma za kijinai dhidi ya watumishi hao.

GAS Company – GASCO

Mheshimiwa Spika,
GASCO imepewa jukumu la kuendesha na kufanya matengenezo (Operations and Maintenance - O & M) ya miundombinu yote ya Taifa ya gesi asilia (National Natural Gas Infrastructure - NNGI) inayohusisha mitambo ya kuchakata gesi ya Madimba na Songo Songo pamoja na bomba la kusafirisha gesi kutoka Mtwara na Songo Songo hadi Dar es Salaam. GASCO imeendelea kutekeleza jukumu hilo kwa kuzingatia na kufuata viwango vya kitaifa na kimataifa vya usalama mahala pa kazi katika kuhakikisha Usalama wa Watu, Miundombinu na Mazingira (Health Safety and Environment - HSE).

84​

Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Machi, 2024, kazi za uendeshaji na matengenezo zilifanyika kikamilifu bila kupata ajali au kusimamisha shughuli za uzalishaji (Zero Lost Time Injury (LTI =0). Vilevile, jumla ya matenegenezo 21,164 ya mitambo mbalimbali yalifanyika kwa ufanisi sawa na asilimia 95.85 ya mpango kwa kipindi husika. Matengenezo mengine yanaendelea kufanyika baada ya ununuzi wa vipuri kukamilika. Ufanisi huu umewezesha miundombinu yote ya gesi asilia kuwa na utayari (reliability and availability) wa asilimia 100 wa kufikisha gesi asilia kwa wateja wake wote.

B.2.10 USIMAMIZI NA UDHIBITI WA SEKTA YA NISHATI KUPITIA PURA NA EWURA

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) iliendelea kusimamia na kudhibiti Sekta ya Nishati ili kuhakikisha utekelezaji wa shughuli za sekta hiyo unazingatia sheria na taratibu zilizopo pamoja na utoaji wa huduma bora kwa wananchi.

85​

B.2.10.1 MAMLAKA YA UDHIBITI MKONDO WA JUU WA PETROLI (PURA)

Mheshimiwa Spika,
Serikali kupitia PURA imeendelea kusimamia shughuli za utafutaji, uendelezaji na uzalishaji wa gesi asilia katika vitalu mbalimbali nchini kulingana na mikataba ya Uzalishaji na Ugawanaji Mapato (PSA) kama inavyoonekana katika Kiambatisho Na.8. Hadi kufikia Machi 2024, uzalishaji wa gesi asilia umeendelea kuimarika na kufikia wastani wa futi za ujazo milioni 236.21 kwa siku zilizozalishwa katika vitalu vya Songo Songo (120.27 mmscfd) na Mnazi bay (115.94 mmscfd). Gesi hiyo ilitumika katika matumizi mbalimbali ikiwemo viwandani, majumbani, katika taasisi, katika magari na kwa ajili ya uzalishaji wa umeme.

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia PURA inatarajia kunadi vitalu vya utafutaji wa mafuta na gesi asilia kupitia Duru ya Tano (5). Lengo kuu la zoezi hili ni kuwezesha ugunduzi zaidi wa rasilimali za mafuta na gesi asilia nchini kwa kufanya shughuli za utafutaji katika vitalu vilivyowazi vyenye viashiria vya uwepo wa rasilimali hizo. Hadi kufikia Machi, 2024 kazi zilizofanyika ni pamoja na kukamilisha mapitio na maboresho ya Mkataba Kifani wa Ugawanaji Mapato (Model Production Sharing Agreement-MPSA) wa mwaka, 2013 ambapo rasimu ya MPSA (MPSA, 2024)

86​

imeandaliwa; na kukamilishwa kwa Mwongozo wa Kupata Kampuni za Kijiofizikia (Geophysical Multiclient Company) zitakazoshirikiana na PURA katika zoezi la kunadi vitalu ambapo taratibu za kupata kampuni hizo zinaendelea.

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia PURA imekamilisha zoezi la utengaji wa vitalu vinavyopendekezwa kufanyiwa mnada na kwa sasa zoezi linaloendelea ni kuandaa vifurushi vya taarifa (data packages) za vitalu hivyo. Zoezi la kunadi vitalu linatarajiwa kuzinduliwa mara baada ya kuidhinishwa kwa MPSA, 2024 na marekebisho ya Sheria ya Petroli ya mwaka 2015.

Mheshimiwa Spika, kaguzi na usimamizi wa shughuli za utafutaji wa mafuta na gesi asilia umeendelea kufanyika katika vitalu vya Tanga, Namba 1, 2 & 4, Nyuni, Ruvuma, Ruvu na Kiliwani North. Aidha, katika Eneo la Eyasi-Wembere shughuli ya uchakataji wa data zilizochukuliwa za mfumo wa 2D imekamilika na taratibu za kumpata Mkandarasi wa kutafsiri data hizo zinaendelea. Katika Kitalu cha Ruvuma, kazi ya kutafsiri taarifa za mitetemo zilizochukuliwa katika eneo la kilomita za mraba 334 imekamilika na kuanza kwa maandalizi ya uendelezaji wa gesi asilia iliyogunduliwa ikiwemo ukarabati wa visima vya Ntorya-1 na Ntorya-2 vitakavyotumika kuzalisha gesi asilia na uchorongaji wa kisima cha utafutaji cha Chikumbi-1.

87​

Kiambatisho Na. 9 ni ramani inayoonesha hali ya utafutaji, uendelezaji na uzalishaji wa mfuta na gesi asilia nchini.

Mheshimiwa Spika, ili kufikia azma ya Serikali ya kuhakikisha wananchi wananufaika na uwekezaji katika rasilimali zilizopo katika maeneo yao, Serikali kupitia PURA na TPDC imeandaa rasimu ya Miongozo ya Uwajibikaji wa Kampuni kwa Jamii (Corporate Social Responsibility – CSR) katika Sekta Ndogo ya Mafuta na Gesi Asilia nchini inayotarajiwa kukamilika mwishoni mwa Juni, 2024. Aidha, maandalizi ya rasimu yamehusisha wadau kutoka maeneo mbalimbali ikiwemo mikoa ya Lindi, Mtwara na Pwani.

Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha Serikali inapata stahiki zake kwa mujibu wa mikataba iliyoingiwa kati yake na Wawekezaji katika shughuli za utafutaji, uendelezaji na uzalishaji wa mafuta na gesi asilia nchini, PURA imeendelea kufanya kaguzi za gharama katika mikataba ya PSA ambapo hadi kufikia Machi 2024, kaguzi hizo ziliwezesha jumla ya Shilingi bilioni 211 kutolewa kwenye madai ya gharama za uwekezaji na kurudishwa kwenye mfuko wa ugawanaji mapato kati ya Serikali na Wawekezaji.

88​

B.2.10.2 MAMLAKA YA UDHIBITI WA HUDUMA ZA NISHATI NA MAJI (EWURA)

Usimamizi na Udhibiti wa Shughuli za Mkondo wa Kati na Chini wa Gesi Asilia

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia EWURA iliendelea kusimamia na kudhibiti shughuli za gesi asilia kwa kufanya kaguzi za mara kwa mara katika miundombinu ya uchakataji, usafirishaji na usambazaji wa gesi asilia na vituo vya kujazia gesi kwenye magari (CNG) katika mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani na Dar es Salaam.

Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Machi, 2024 jumla ya kaguzi za kawaida 25 kwenye miundombinu ya gesi asilia zilifanyika na kaguzi moja maalum ya kitaalam na kiusalama kwenye vituo vitatu (3) vya kujazia gesi kwenye magari na karakana saba (7) za kuongeza mfumo wa gesi asilia kwenye magari ulifanyika. Ukaguzi huu maalumu ulishirikisha EWURA, Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Bodi ya Usajili wa Wakandarasi (CRB). Lengo ni kuhakikisha usalama kwenye eneo la utaalam, vifaa na mazingira ya utekezaji wa shughuli zinazohusu matumizi ya gesi asilia katika magari. Kupitia kaguzi hizo, imebainika miundombinu na shughuli zote zinazohusisha gesi

89​

asilia hapa nchini zipo katika hali nzuri inayokidhi viwango vya ubora na usalama.

Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Machi 2024, EWURA ilitoa vibali sita (6) kwa ajili ya ujenzi (construction approvals) wa miundombinu ya kusambaza gesi asilia viwandani na vituo vya CNG. Vibali hivyo vilitolewa kwa TPDC kwa ajili ya ujenzi wa kituo kikuu (mother station) cha kuzalisha CNG kwenye eneo la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, vituo vidogo viwili (2) (daughter stations) vya kupokea CNG katika kiwanda cha Kairuki (Kibaha) na hospitali ya Taifa ya Muhimbili na vibali vingine viwili (2) kwa ajili ya ujenzi wa mabomba ya kuunganisha gesi asilia kwenye kituo cha kujazia gesi kwenye magari cha Dangote na kwenye kiwanda cha kampuni ya KEDA vilivyopo Mkuranga. Aidha, EWURA ilitoa kibali cha ujenzi kwa kampuni ya PanAfrican Energy Tanzania (PAET) kwa ajili ya ujenzi wa bomba la gesi la kuunganisha kituo cha kujazia gesi asilia kwenye magari cha kampuni ya TAQA Dalbit - Kipawa.

Mheshimiwa Spika, EWURA pia ilitoa leseni mbili (2) za uendeshaji (operational licence) kwa vituo viwili vya kujazia gesi asilia kwenye
magari (CNG filling station). Vituo hivyo vinamilikiwa na Kampuni za TAQA Dalbit (Kipawa

Dar es Salaam) na Dangote (Mkuranga – Pwani)

90​

vinavyohudumia watumiaji wa nishati ya gesi asilia kwenye maeneo husika.

Shughuli za Bidhaa za Mafuta ya Petroli

Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea na usimamizi wa ubora wa vituo vya mafuta ili kuimarisha upatikanaji, usalama na ubora wa bidhaa za mafuta kwa watumiaji katika maeneo yote nchini. Aidha, imeendelea kusimamia mazingira chanya ya uwekezaji wa ujenzi wa vituo vya mafuta vyenye ubora ambapo hadi kufikia Machi, 2024 jumla ya vituo 2,522 vilivyopo mijini na vijijini vilikidhi vigezo vya ubora na usalama na kupewa leseni ikilinganishwa na vituo 2,297 katika kipindi hicho mwaka 2022/23, sawa na ongezeo la asilimia 9.80. Kati ya vituo hivyo, vituo 434 vimejengwa katika maeneo ya vijijini ikilinganishwa na vituo 287 vilivyojengwa vijijini kwa kipindi hicho mwaka 2022/23 sawa na ongezeko la asilimia 51.22.

Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai 2023 hadi Machi 2024, EWURA ilitoa leseni, vibali, kuboresha Kanuni na kusimamia ubora wa bidhaa za mafuta kama ifuatavyo:

Ilitoa leseni 34 kwa kampuni za mafuta (wholesalers) kwa ajili ya kuagiza na kuuza mafuta kwa jumla, ambapo leseni 30 zilitolewa kwa kampuni mpya;

91

Ilitoa leseni mpya 4 kwa kampuni za kuagiza na kuuza Gesi itokanayo na Petroli (LPG) kwa jumla (LPG Wholesalers). Pia, ilitoa leseni 27 kwa Mawakala wa Kusambaza LPG (LPG Distributors). Kati ya leseni hizo, leseni 26 zilitolewa kwa Mawakala wapya;

Ilitoa leseni saba (7) kwa kampuni zenye miundombinu binafsi ya kuhifadhi na kujaza mafuta (consumer installation facilities). Kati ya leseni hizo, leseni sita (6) zilitolewa kwa kampuni mpya;

Ilitoa leseni mpya moja (1) ya ghala la kuhifadhia mafuta (petroleum storage);

Ilitoa leseni moja (1) ya uwakala wa condensate.

Ilitoa vibali vya ujenzi (construction approvals) 237 ambapo vibali 233 vilikuwa kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya mafuta, kimoja (1) kwa ajili ya miundombinu ya kuhifadhia LPG, viwili (2) kwa ajili ya matumizi binafsi (consumer installations) na kimoja (1) kwa ajili ya ghala ya kuhifadhia mafuta;

Ilisimamia taratibu za uagizaji na usambazaji wa mafuta ili kuhakikisha upatikanaji wa mafuta ya kutosha nchini;

92​

Ilisimamia ubora wa bidhaa za mafuta nchini kwa kufanya kazi ya kuchukua sampuli za mafuta kutoka kwenye vituo vya mafuta na maghala ya kuhifadhia mafuta na kupeleka maabara kwa ajili ya vipimo. Aidha, jumla ya sampuli 318 zilichukuliwa kutoka katika miundombinu tajwa kwa ajili ya kupima ubora na sampuli 303 sawa na asilimia 95.3 zilifaulu kwa kuwa na viwango stahiki vya ubora. EWURA inachukua taratibu za kisheria ikiwemo kufungia wahusika kutoendelea kufanya biashara pindi wanapobainika kuwa na dosari hadi hapo wanapokidhi matakwa ya leseni zao. Pia, EWURA inaendelea kutoa elimu na ushauri kwa wadau ili waendelee kutoa huduma stahiki;

Ilifanya maboresho ya Kanuni zikiwemo The Petroleum (Wholesales Storage Retail and Consumer Installation) Rules, 2023 ili kuimarisha ukusanyaji wa takwimu za
biashara ya mafuta kutoka kwa wafanyabiashara wa mafuta wa jumla pamoja na maghala ya kuhifadhia mafuta; the Petroleum (Retail Operations in Townships and Villages) (Amendment) Rules, 2023 ambazo zilifanyiwa maboresho ili kuwezesha ukusanyaji wa takwimu za biashara ya mafuta kutoka kwenye vituo vya mafuta; na

93​

the Energy and Water Utilities Regulatory Authority (Petroleum Products Price Setting) (Amendment) Rules, 2023 ambazo zilifanyiwa maboresho ya jedwali la ukokotoaji wa bei za mafuta;

Ilikagua ubora wa miundombinu ya mafuta na kuhakikisha upatikanaji wa bidhaa za mafuta kwa wananchi bila kuhatarisha afya, usalama na mazingira. Katika kipindi hiki, ukaguzi ulifanyika kwenye miundombinu ya mafuta 446 na miundombinu ya mafuta 338 sawa na asilimia 75.78 ilikidhi viwango stahiki vya ubora. EWURA inaendelea kutoa elimu kuhusiana na usalama na mazingira ya miundombinu ya mafuta kwa wahusika; na

Ilitoa bei elekezi za mafuta kila mwezi na kusimamia utekelezaji wake.

Udhibiti wa Biashara ya Vilainishi

Mheshimiwa Spika, kwa ujumla upatikanaji na ubora wa vilainishi nchini ni wa kuridhisha. Serikali kupitia EWURA inaendelea na usimamiaji wa ubora wa vilainishi vinavyoingizwa nchini ambapo leseni 99 za wauzaji wa jumla wa vilainishi na leseni 6 za wafanyabiashara wanaotengeneza vilainishi nchini zimetolewa. Vilevile, EWURA inaendelea kushirikiana na Tume

94​

ya Ushindani (FCC) na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) katika kudhibiti ubora wa bidhaa za vilainishi zinazoingizwa nchini kwa kufanya kaguzi kwa pamoja. Aidha, EWURA imeanza kusajili vilainishi vinavyozalishwa na kuagizwa kutoka nje ya nchi kwa lengo la kuhakikisha vilainishi vyenye ubora uliothibitishwa na Taasisi za ndani na kimataifa vinatumika nchini. EWURA inaendelea kutoa elimu kwa watumiaji kununua bidhaa hizo kutoka kwa wauzaji waliothibitishwa.

Uwekaji Vinasaba katika Mafuta

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia EWURA iliendelea na jukumu la kusimamia na kukagua soko la ndani la mafuta ili kuhakikisha kuwa mafuta yanayouzwa nchini yana viwango stahiki vya vinasaba kwa lengo la kudhibiti ubora na kuimarisha mapato ya Serikali kupitia kodi. Uwekaji wa vinasaba kwenye mafuta unafanywa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ambapo hadi kufikia Machi 2024, kiasi cha lita bilioni 1.18 za mafuta ya petroli, lita bilioni 1.70 za mafuta ya dizeli na lita milioni 6.18 za mafuta ya taa ziliwekewa vinasaba nchini. Aidha, katika kipindi hicho EWURA ilipima mafuta kwenye vituo 307 ambapo vituo 299, sawa na asilimia 97.39, vilifaulu kwa kuwa na kiwango stahiki cha vinasaba. Vituo ambavyo vilikutwa na mafuta ambayo hayana

95​

kiwango stahiki cha vinasaba vilichukuliwa hatua za kisheria.

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia TBS inafanya maboresho ya kutumia teknolojia (automation) katika kuweka vinasaba kwenye mafuta na hadi sasa mifumo ya kuweka vinasaba kwa teknolojia hiyo imeunganishwa katika maghala sita na TBS inaendelea na taratibu za kujenga vituo vya kupima vinasaba kwa hiari kabla mafuta hayajafika kituoni (voluntary check points).

Vituo hivi vitawezesha wafanyabiashara kuhakikisha uwepo wa vinasaba kwenye mafuta kabla ya kufikisha mafuta vituoni.

Usimamizi na Udhibiti wa Shughuli za Umeme

Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Machi,

2024 Serikali kupitia EWURA ilitekeleza yafuatayo:

Ilitoa leseni tatu (3) za Muda Mfupi (Provisional Licence) zenye uwezo wa kuzalisha Megawati 14.5 kwa Kampuni tatu ambazo ni Bugando Natural Energy Limited MW 5; Lilondi Hydropower Limited MW 4.5; na Tangulf Nakatuta Energy Company Limited MW 5;

96​

Ilitoa leseni 1,163 kwa wataalamu wenye sifa za kufunga mifumo ya umeme nchini ili kusaidia katika juhudi za Serikali za kusambaza umeme kwa mujibu wa kifungu namba 5(a) na 8(1) cha Sheria ya Umeme, Sura ya 131. Kati ya hizo Daraja A (51); Daraja B (105); Daraja C (699); Daraja D (306) na Daraja S1 (2);

Ilikagua miundombinu ya umeme ili kuhakikisha ufanisi katika utendaji, upatikanaji wa huduma bora, na uzingatiwaji wa Sheria kwa mujibu wa kifungu namba 31(2) cha Sheria ya Umeme, Sura ya 131. Miundombinu ya umeme iliyokaguliwa ni:

Miundombinu ya TANESCO ya kusambaza na kugawa umeme katika mikoa 17 nchini. Mikoa hiyo ni; Mwanza, Simiyu, Tabora, Mbeya, Songwe, Arusha, Mtwara, Dodoma, Tanga, Morogoro, Mara, Lindi, Pwani, Kagera, Ruvuma, Rukwa na Songwe. Pia EWURA ilifanya ukaguzi wa miundombinu ya kusamabaza umeme kwa kampuni ya Mwenga Power Services;

97

Mitambo 14 ya kuzalisha umeme. Mitambo hiyo ni Kinyerezi I (MW 150.00), Kinyerezi I Extension (MW
185.00), Kinyerezi II, Ubungo I (MW

102.00), Ubungo II (MW 129.00), Ubungo III (112.50), Tegeta (MW 45.0), Songas (189.0), Mtera (MW

80.00), Andoya Hydro Power Plant

(1.00), Yovi Hydro Power Company Ltd (0.95), Mwenga Hydro Ltd (4.00), Kidatu (204.00) na Kihansi (180.00); na

Miundombinu ya kusafirisha umeme kwenye laini ya Ubungo-Chalinze (Kilovoti 132) pamoja na vituo vyake vya kupozea umeme vya Ubungo, Mlandizi na Chalinze.

Ilikagua miradi ya kuzalisha umeme inayotekelezwa ili kuhakikisha ufanisi katika utekelezaji wake, kwa mujibu wa Sheria ya Umeme. Miradi hiyo ni:

Mradi wa kuzalisha umeme wa Julius Nyerere Hydropower Project (2115MW);
Mradi wa kuzalisha umeme wa Rusumo Hydropower Project (80MW); na

98

Mradi wa kuzalisha umeme wa

Kikagati-Murongo Hydropower Plant (14MW).

Iliridhia mkataba wa mauziano ya umeme (Power Purchase Agreement) wa Megawati 26.67 kati ya TANESCO na Rusumo Power Company Limited (RPCL). Mradi huu umechangia kuimarisha hali ya upatikanaji wa umeme kwenye mfumo wa Gridi ya Taifa;

Iliridhia jumla ya mikataba 14 yenye jumla ya Megawati 79.2 ya kuuziana umeme (Standardized Power Purchase Agreement- SPPA) kati ya TANESCO na wazalishaji wadogo (Kiambatisho Na. 10) ili kuimarisha upatikanaji wa huduma ya nishati ya umeme kwa wananchi waliounganishwa katika Gridi ya Taifa na nje ya Gridi ya Taifa; na

Ilifanya marekebisho ya Kanuni za Shughuli za Ugavi wa umeme na Kanuni za Shughuli za Uzalishaji, Usafirishaji na Usambazaji Umeme za Mwaka 2023 kwa ajili ya kuboresha taratibu za kufanya ukaguzi.

99

B.2.11 USHIRIKI WA SEKTA BINAFSI NA USHIRIKISHWAJI WA WATANZANIA KATIKA SEKTA YA MAFUTA NA GESI ASILIA

Mheshimiwa Spika,
katika kuhakikisha kampuni za wazawa na watalaam wazawa wanashiriki kikamilifu kwenye mnyororo wa Sekta Ndogo ya Mafuta na Gesi Asilia nchini, Serikali kupitia EWURA na PURA zimeendelea kuhuisha kanzidata za watoa huduma na wataalamu wa ndani (Local Suppliers and Service Providers Database (LSSP) na Local Professional Database) kupitia mfumo wa “Common Qualification System – CQS”. Kupitia mfumo huo, EWURA imesajili kampuni za wazawa 2,029 na wataalam wazawa 198 kwenye kanzidata ya EWURA na jumla ya Kampuni 157 zimesajiliwa na zinapata fursa za kuuza bidhaa na kutoa huduma mbalimbali kwenye Miradi inayoendelea na wataalamu 187 wa ndani wenye ujuzi mbalimbali katika tasnia ya mafuta na gesi asilia wamesajiliwa katika mfumo na kanzidata ya shughuli za petroli. Aidha, takribani kampuni 250 zilipata zabuni za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja katika mradi wa EACOP na miradi mingine katika Sekta Ndogo ya Gesi Asilia.

Mheshimiwa Spika, takribani Watanzania 3,227 walikuwa wameajiriwa katika miradi ya mafuta na gesi asilia hususani katika mradi wa

100​

EACOP na Watanzania 212 wameajiriwa katika vitalu vya uzalishaji wa gesi asilia vya Mnazi Bay na Songo Songo. Aidha, shughuli za utafutaji wa gesi asilia pia huzalisha ajira za muda ambapo jumla ya Watanzania 148 waliajiriwa katika kazi ya uchukuaji wa data za mitetemo za 3D katika Kitalu cha Songo Songo na 250 waliajiriwa katika kazi ya uchukuaji wa data za mitetemo za 2D katika Kitalu cha Eyasi Wembere. Sambamba na ajira, takribani Dola za Marekani milioni 44.5 zilitumiwa na kampuni za kigeni zilizowekeza katika shughuli za mafuta na gesi asilia kununua bidhaa na huduma mbalimbali zinazozalishwa na kupatikana nchini.

B.2.12 HALI YA UAGIZAJI NA UPATIKANAJI WA BIDHAA ZA MAFUTA YA PETROLI NCHINI

Mheshimiwa Spika,
ili kuhakikisha upatikanaji wa bidhaa za mafuta ya petroli nchini, Serikali imeendelea kutumia Mfumo wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (Bulk Procurement System - BPS). Mfumo huu ulianzishwa mwaka 2011 na kuanza kutumika rasmi Januari, 2012 ambapo pamoja na uhakika wa upatikanaji wa bidhaa za mafuta ya petroli wakati wote pia uagizaji wa mafuta umeendelea kufanyika kwa ufanisi na hivyo mlaji wa mwisho kulipia mafuta kwa bei stahiki. Aidha, mfumo huu umewezesha upatikanaji wa takwimu sahihi za bidhaa za mafuta ya petroli

101​

yanayoingia nchini na kwenda nchi jirani na pia kurahisisha udhibiti wa ubora wa bidhaa za mafuta ya petroli.

Mheshimiwa Spika, jumla ya lita bilioni 6.28 za bidhaa za mafuta ya petroli ziliingizwa nchini kwa kutumia mfumo wa BPS kwa kipindi cha Julai, 2023 hadi Machi, 2024. Bidhaa hizo ziliingizwa kupitia Bandari za Dar es Salaam, Tanga na Mtwara, ambapo dizeli ilikuwa lita bilioni 3.77, petroli lita bilioni 2.29 na mafuta ya ndege/taa lita milioni 224. Aidha, mafuta kwa ajili ya matumizi ya ndani ya nchi yaliongezeka kwa asilimia 6.07 ikilinganishwa na kiasi kilichoingizwa Julai, 2022 hadi Machi, 2023. Vilevile, kiasi cha mafuta yaliyoingizwa kwa ajili ya kwenda nchi jirani kilipungua kwa asilimia 4.76 kutokana na changamoto ya upatikanaji wa Dola za Marekani. Kati ya mafuta yaliyoingizwa Julai, 2023 hadi Machi, 2024 lita bilioni 3.37 sawa na asilimia 53.7 yalikuwa ni kwa ajili ya matumizi ya ndani na lita bilioni 2.9 sawa na asilimia 46.3 yalikuwa kwa ajili ya nchi jirani. Kielelezo Na. 6 kinaonesha uwiano wa bidhaa za mafuta zilizoingizwa nchini kwa kipindi cha Julai, 2023 hadi Machi, 2024. Kielelezo Na.7 ni jumla ya kiasi cha mafuta kilichoingizwa nchini kwa ajili ya matumizi ya ndani na nchi jirani katika kipindi hicho.

102​

Kielelezo Na.6: Uwiano wa Bidhaa za Mafuta Zilizoingizwa Nchini kwa Kipindi cha Julai, 2023 hadi Machi, 2024

Mafuta Yaliyoingia Julai 2023 hadi Machi 2024

4%

36%

60%

DizeliPetroliMafuta ya Ndege/Taa

Chanzo: PBPA

103​

Kielelezo Na.7: Jumla ya Kiasi cha Mafuta Kilichoingizwa kwa Ajili ya Matumizi ya Ndani na Nchi Jirani, Julai 2023 hadi Machi 2024

Mafuta Yaliyoingia Julai 2023 hadi Machi 2024

Lita Milioni

2,000

1,800

1,600

1,400

1,200

1,000

800

600

400

200

-
Dizeli
Petroli Mafuta ya

Ndege/Taa

Kwenda Nchi Jirani Matumizi ya Ndani

Chanzo: PBPA

Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai 2023 hadi Machi 2024, jumla ya zabuni 88 zilitolewa kwa njia ya ushindani wa kimataifa kwa kigezo cha gharama ndogo za uletaji wa mafuta nchini (premium). Aidha, wastani wa zabuni 9 hadi 12 zilishindanishwa kila mwezi ambapo wastani wa wazabuni wanne (4) hadi sita (6) hushinda zabuni hizo kila mwezi. Katika zabuni hizo TPDC imekuwa ikishiriki na hivyo kuongeza ushindani na kuchangia upatikanaji wa gharama stahiki za uagizaji wa mafuta.

104​

Mheshimiwa Spika, changamoto ya upatikanaji wa Dola za Marekani imeendelea kuikabili nchi yetu kama ambavyo nchi nyingi Duniani zinapitia changamoto hiyo. Makali ya tatizo hili yanatokana na vita baina ya Urusi na Ukraine na mabadiliko ya sera ya fedha za Marekani. Ili kukabiliana na changamoto hiyo, Serikali kupitia Wizara ya Nishati, Wizara ya Fedha, Benki Kuu ya Tanzania, Taasisi zinazohusika katika mnyororo wa biashara ya mafuta pamoja na Sekta Binafsi zilishirikiana kuchukua hatua mbalimbali. Benki Kuu ya Tanzania ilisimamia suala hili ikiwemo kuruhusu benki kuuziana fedha za kigeni hususan Dola za Marekani ili kuchagiza upatikanaji wake katika soko la ndani; kuruhusu ulipiaji wa mafuta kwa kutumia fedha nyingine za kigeni; na kuongeza kiwango cha ukomo wa ukopaji kwa wanunuzi wa mafuta (OMC’s borrowing limit) katika benki za biashara.

Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mpito kuelekea uwekezaji wa miundombinu ya kupokea mafuta kwa pamoja, Serikali imeendelea kutumia miundombinu ya Kampuni ya TIPER kama Kituo cha Kupokea Mafuta kwa Pamoja (Single Receiving Terminal - SRT) ambapo kina uwezo wa kupokea wastani wa meli moja hadi mbili

kwa mwezi. Idadi hii inafikia asilimia kati ya 30 hadi 60 ya meli mbili (2) hadi nne (4) zinazoingia

105​

nchini kila mwezi kushusha shehena ya mafuta ya dizeli. Hivyo meli zinazokosa nafasi ya kushusha mafuta TIPER hutumia muda mrefu kumaliza kushusha mafuta. Ikiwa ni hatua ya kuboresha ufanisi, TIPER inaendelea kusimika pampu za kuhamisha mafuta zenye uwezo mkubwa wa kusukuma hadi lita 800,000 kwa saa ili kuongeza kasi ya kuhamisha mafuta kwenda kwenye maghala ya kampuni za mafuta (OMCs) ambapo kazi hii inatarajiwa kukamilika Januari, 2025.

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia PBPA imekamilisha ufungaji na kuanza kutumia mfumo wa kielektroniki (SCADA) ili kusaidia udhibiti wa upotevu wa mafuta kwenda kwa wafanyabiashara wa mafuta ya jumla (OMCs) wakati wa upakuaji. Mfumo huu una uwezo wa kusoma kiasi cha mafuta yanayopita katika mita (flowmeter) za Serikali zilizopo Kurasini, Kigamboni, Tanga na Mtwara na kulinganisha kiasi cha mafuta yanayopita katika mita zilizopo kwenye maghala ya kuhifadhi mafuta. Upatikanaji wa taarifa hizi kutoka kwenye mita unawezesha Serikali kudhibiti upotevu wa mafuta.

B.2.13 MWENENDO WA BEI ZA MAFUTA KATIKA SOKO LA DUNIA

Mheshimiwa Spika,
Serikali kupitia EWURA imeendelea kufuatilia mwenendo wa bei za mafuta katika soko la dunia ambapo kuanzia Julai

106​

2023 hadi Machi 2024 bei ya pipa la mafuta ghafi kwa wastani ilishuka kwa asilimia 7 na kufika wastani wa Dola za Marekani 84 kwa pipa ikilinganishwa na wastani wa Dola za Marekani 90 kwa pipa kwa kipindi kama hicho katika mwaka 2022/23. Kushuka huko kwa bei za mafuta ghafi katika soko la dunia kulichangiwa na kudorora kwa uchumi wa dunia uliotokana na migororo ya kivita ikiwemo Urusi na Ukraine pamoja na Israel na Palestina. Vilevile, kulichangiwa na kudorora kwa ukuaji wa uchumi wa mataifa makubwa kama China kulikosababishwa na athari zilizotokana na UVIKO- 19. Kielelezo Na.8 ni mwenendo wa bei za mafuta ghafi katika soko la Dunia.

Kielelezo Na.8: Mwenendo wa Bei ya Mafuta Ghafi katika Mwaka 2022/23 na 2023/24

Mwezi
DOLA KWA PIPA
2023/24
2022/23
Julai
80​
105​
Agosti
85​
98​
Septemba
92​
91​
Oktoba
91​
93​
Novemba
83​
87​
Disemba
78​
82​
Januari
80​
80​
Februari
82​
84​
Machi
85​
79​
Wastani
84​
89​
Badiliko
-6%
Chanzo: EWURA

107​

Mheshimiwa Spika, kushuka kwa bei za mafuta ghafi katika soko la dunia, kulisababisha kushuka kwa wastani wa asilimia 8 ya bei za mafuta yaliyosafishwa ambapo bei ya mafuta ya petroli ilishuka kwa asilimia 1, dizeli kwa asilimia 13 na mafuta ya taa/ndege kwa asilimia 10. Hadi kufikia Machi 2024, bei za mafuta yaliyosafishwa katika soko la Dunia kwa wastani zilikuwa Dola za Marekani 785 kwa tani ya petroli, Dola za Marekani 797 kwa tani ya dizeli na Dola za Marekani 832 kwa tani ya mafuta ya taa/ndege ikilinganishwa na wastani wa Dola za Marekani 795 kwa tani ya mafuta ya petroli, Dola za Marekani 919 kwa tani ya dizeli na Dola za Marekani 925 kwa tani ya mafuta ya taa/ndege katika kipindi kama hicho mwaka 2022/23. Kielelezo Na.9 ni wastani wa mwenendo wa bei za mafuta yaliyosafishwa katika Soko la Dunia kwa Mwaka 2022/23 na 2023/24

108​

Kielelezo Na.9: Wastani wa Mwenendo wa Bei za Mafuta Yaliyosafishwa katika Soko la Dunia kwa Mwaka 2022/23 na 2023/24

Dola za Kimarekani Kwa Tani

950

900

850

800

750

700
2023/24​
2022/23​
Petroli
Dizeli​
Mafuta ya Taa/Ndege

Chanzo: EWURA

109​

B.2.14 MWENENDO WA BEI ZA MAFUTA KATIKA SOKO LA NDANI

Mheshimiwa Spika,
Serikali kupitia EWURA iliendelea kupanga bei za ndani za mafuta kwa mujibu wa Sheria na Kanuni. Aidha, bei za mafuta nchini zilionesha kutengamaa ikilinganishwa na mwaka uliopita. Mathalani kwa mkoa wa Dar es Salaam wastani wa bei za mafuta kwa kipindi cha Julai 2023 hadi Machi 2024 zilishuka kwa asilimia 7 kwa mafuta ya taa/ndege, asilimia 2 kwa mafuta ya dizeli; na yalipanda kwa asilimia 2 kwa mafuta ya petroli, ambapo wastani wa bei ya petroli kwa lita ilikuwa Shilingi 3,129, dizeli Shilingi 3,113 na mafuta ya taa Shilingi 3,047 ikilinganishwa na wastani wa bei za mafuta hayo kwa kipindi hicho mwaka 2022/23 ambapo zilikuwa petroli Shilingi 3,081, dizeli Shilingi 3,167 na mafuta ya taa Shilingi 3,282 kwa lita.

Mheshimiwa Spika, kuimarika kwa bei nchini kulitokana na kushuka kwa bei ya mafuta ghafi kwenye soko la Dunia, hatua zilizochukuliwa na Serikali za kutoruhusu kutumia fedha za kigeni zilizopo ndani ya nchi kulipia mafuta yanayokwenda nchi jirani (transit cargoes) pamoja na kuruhusu kutumia aina tofauti za fedha za kigeni kuagiza mafuta yanayotumika nchini. Kielelezo Na. 10 kinaonesha wastani wa mwenendo wa bei za mafuta nchini.

110​

Kielelezo Na.10: Wastani wa Mwenendo wa Bei za Mafuta

Nchini

Chanzo: EWURA

B.2.15 KUIMARISHA UTENDAJI KAZI NA UTOAJI HUDUMA

Mheshimiwa Spika,
Wizara iliendelea kukamilisha Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Ofisi za Wizara katika Mji wa Serikali Mtumba unaotekelezwa na Mkandarasi- Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ambapo hadi kufikia Machi, 2024 ujenzi huo ulifikia asilimia 75.1 na matarajio ya Wizara ni kuhamia katika jengo hilo katika mwaka

111​

2023/24. Ukamilishwaji wa jengo hilo ni hatua ya kuhakikisha Watumishi wanakuwa na mazingira bora ya utekelezaji wa majukumu kwa tija na ufanisi.

Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha Taasisi zilizo chini ya Wizara zinaimarisha utendaji kazi na utoaji wa huduma, Wizara ilisimamia watumishi kujisajili katika mfumo mpya wa Usimamizi na Utendaji kazi katika Utumishi wa Umma (PEPMIS). Aidha, Wizara iliendelea kuwajengea uwezo watumishi wake pamoja na Taasisi zilizo chini yake ambapo jumla ya watumishi 59 walipatiwa mafunzo ya muda mrefu na watumishi 3,048 walipatiwa mafunzo ya muda mfupi katika kada mbalimbali ndani na nje ya nchi. Kati ya hao, watumishi wa Wizara walikuwa 53, TANESCO 2,320, TPDC 248, REA 100, PURA 51, PBPA 48 na EWURA 228.

Mheshimiwa Spika, Serikali iliendelea kuimarisha utendaji wa Taasisi zote zilizo chini ya Wizara ili zifanye kazi kwa tija inayotarajiwa. Kufuatia hatua ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuteua Wenyeviti wa Bodi ya Wakurugenzi ya REA na TANESCO, Wizara iliteua Wajumbe wa Bodi hizo ili kuimarisha usimamizi na utendaji kazi wa Taaasisi hizo.

112​

B.2.16 MAFANIKIO YALIYOPATIKANA KATIKA UTEKELEZAJI WA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA 2023/24

Mheshimiwa Spika,
mafanikio mbalimbali yamepatikana katika utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara ya Nishati kwa mwaka 2023/24. Mafanikio hayo ni pamoja na:

Uwezo wa mitambo ya kufua umeme iliyounganishwa katika mfumo wa Gridi ya Taifa umeongezeka na kufikia MW 2,138 Machi, 2024 kutoka MW 1,872.1 zilizozalishwa mwaka 2022/23, ikiwa ni ongezeko la asimia 14.2;

Kuanza kwa uzalishaji wa umeme kupitia Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Maji wa Julius Nyerere (JNHPP) wenye uwezo wa kuzalisha MW 2,115 ambapo tayari uzalishaji umeanza kwa MW 235 kupitia mtambo Namba 9. Aidha, matarajio ni mradi huu kukamilika Desemba, 2024 kwa mitambo yote nane

yenye uwezo wa kuzalisha MW 235 kila moja kuwa inazalisha umeme;

Kukamilisha ujenzi wa mitambo ya kufua umeme ya Kinyerezi I Extension MW 185 ambapo kwa sasa mitambo yote minne (4) inafua umeme kiasi cha

113​

MW 40 kila mmoja unaoigizwa katika gridi ya Taifa;

Miundombinu ya kusafirisha umeme imeongezeka na kufikia jumla ya urefu wa kilomita 7,745.4 ikiwa ni ongezeko la asilimia 21.7 ikilinganishwa na kilomita 6,363.3 za mwaka 2022/23;

Kuanza kutumika kwa njia ya kusafirisha umeme wa Kilovoti 400 kutoka JNHPP hadi Chalinze pamoja na kituo kipya cha kupoza umeme cha Chalinze cha Kilovoti 400/220/132 kinachotumika kupoza na kusafirisha umeme unaotoka JNHPP na kuingizwa kwenye Gridi ya Taifa;

Kukamilika kwa asilimia 99 kwa Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa Kilovoti 220 kutoka Morogoro hadi Dodoma kwa ajili ya uendeshaji wa treni ya umeme (SGR Lot II);

Kukamilika kwa asilimia 99.4 kwa Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa Kilovoti 400 kutoka Singida
– Arusha – Namanga. Aidha, ujenzi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa Kilovoti 400 kutoka Arusha hadi

114

Namanga yenye urefu wa kilomita 114.3 umefikia asilimia 97.5 na kituo cha kupoza umeme cha Lemugur kimekamilika kwa asilimia 100 na kuwashwa;

Miundombinu ya kusambaza umeme imeongezeka na kufikia kilomita 176,750.9, ikiwa ni ongezeko la asilimia 4.9 ikilinganishwa na kilomita 168,548.5 za mwezi Mei, 2023;

Jumla ya wateja 4,784,297 wameunganishiwa umeme hadi kufikia Machi, 2024 ikiwa ni ongezeko la asilimia 9.4 ikilinganishwa

na wateja 4,319,258 waliokuwa wameunganishiwa umeme Juni, 2023;

Kuweka mifumo ya kisasa ya mawasiliano katika vituo tisa (9) vya kupoza umeme ili viendeshwe kidigitali (unmanned substations) ambapo kituo kimoja cha Buzwagi kimekamilika;

Jumla ya vijiji 11,837 sawa na asilimia 96.37 ya vijiji vyote 12,318 vya Tanzania Bara vimeunganishwa na umeme hadi kufikia Machi, 2024;

Kuandaliwa na kuidhinishwa na Baraza la Mawaziri kwa Mkakati wa Taifa wa

115

Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia wa mwaka 2024 - 2034. Mkakati huu ni nyenzo muhimu ya kuhakikisha angalau asilimia 80 ya watanzania kuwa wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034 kwa kutatua vikwazo mbalimbali vinavyokwamisha matumizi ya nishati hiyo ikiwa ni pamoja na gharama kubwa, upatikanaji hafifu na uhaba wa miundombinu yake; kukosekana kwa elimu ya kutosha kuhusu madhara ya nishati zisizo safi na salama za kupikia pamoja na baadhi ya mila, desturi na tamaduni zinazochochea matumizi ya nishati zisizo safi na salama za kupikia;

Kuzinduliwa kwa Programu ya Nishati

Safi ya Kupikia inayoloenga Kuwawezesha Wanawake Barani Afrika Kutumia Nishati Safi ya Kupikia (African Women Clean Cooking Support Programme – AWCCSP), iliyozinduliwa Desemba 2023 katika Mkutano wa 28 wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP 28) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan; na

116

Kufanikisha ununuzi wa asilimia 20 ya hisa za Kampuni ya Wentworth kwenye Mkataba wa Uendeshaji wa Kitalu cha Uzalishaji gesi asilia cha Mnazi Bay kilichopo Mtwara. TPDC imeongeza uwekezaji katika kitalu hicho kwa asilimia 20;

B.2.17 CHANGAMOTO ZILIZOPO NA UTATUZI WAKE

Mheshimiwa Spika,
pamoja na mafanikio yaliyopatikana katika mwaka 2023/24, Sekta ya Nishati ilikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo zifuatazo:

Uzalishaji wa umeme na gesi asilia kutoendana na mahitaji kutokana na ukuaji wa shughuli za kiuchumi na kijamii. Aidha, uchakavu wa miundombinu ya kusafirisha na kusambaza umeme imekuwa ikichangia pia kutokidhi mahitaji ya upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa wananchi. Kutokana na hatua zilizochukuliwa na Serikali, ikiwemo kuharakisha utekelezaji wa miradi ya uzalishaji wa umeme pamoja na kukarabati na kufanya matengenezo ya miundombinu ya umeme, hali ya upatikanaji wa umeme nchini unaokidhi mahitaji

117​

imeendelea kuimarika hadi kufikia Machi, 2024.

Aidha, Serikali iliendelea kuchukua hatua za kuimarisha upatikanaji wa gesi asilia, ikiwa ni pamoja na kukarabati na kuongeza msukumo wa gesi asilia kwenye visima na mabomba katika Kitalu cha Songo Songo; kutoboa maeneo mapya ya kuzalishia gesi asilia (perforation) katika visima viwili (2) na kuchoronga visima viwili katika kitalu cha Mnazi Bay; pamoja na uendelezaji wa kitalu cha Ruvuma katika eneo la Ntorya.

b) Vitendo vya hujuma/uhalifu katika miundombinu ya umeme. Serikali inaendelea​

kuwachukulia hatua za kisheria wanaobanika kutekeleza vitendo hivyo na inaendelea kutoa wito kwa wananchi wasio na nia njema kuacha vitendo hivyo, kwa kuzingatia hasara na usumbufu mkubwa unaojitokeza kwa watumiaji wa umeme kutokana na vitendo hivyo.

Changamoto ya upatikanaji wa Dola za Marekani kwa ajili ya kulipia mafuta

yaliyoagizwa nchini iliyosababisha wafanyabishara kupunguza kiasi cha mafuta kilichokuwa kinaagizwa. Ili kukabiliana na hali hiyo, Serikali kupitia Wizara ya Nishati

118

kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha, Benki Kuu ya Tanzania na wadau wengine ilichukua hatua mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kufanya mapitio ya mikataba ya kuagiza mafuta na kuruhusu matumizi ya fedha za kigeni zikiwemo fedha ya Uingereza (British Pound), Umoja wa Ulaya (Euro) na Umoja wa Nchi za Uarabuni (Dirham). Aidha, Wizara ya Nishati kupitia EWURA iliimarisha ukaguzi katika vituo vya mafuta ili kuhakikisha mafuta yanapatikana wakati wote katika maeneo yote nchini.

C. MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA 2024/25

Mheshimiwa Spika,
baada ya kutoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Wizara kwa mwaka 2023/24, sasa napenda kuwasilisha Mpango na Bajeti kwa Mwaka 2024/25.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2024/25 utekelezaji wa majukumu ya Wizara

utaongozwa na vipaumbele mbalimbali vinavyojikita katika kuendelea kutekeleza miradi ya uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa umeme ikiwa ni pamoja na kufikisha gridi ya Taifa katika mikoa iliyosalia; kupeleka nishati vijijini, ikiwemo katika vitongoji; kutekeleza miradi ya kielelezo na kimkakati ya mafuta na gesi asilia ikiwemo mradi

119​

wa Kuchakata na Kusindika Gesi Asilia kuwa Kimiminika (Liquefied Natural Gas – LNG Project), ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta kutoka Hoima, Uganda hadi Tanga, Tanzania (East African Crude Oil Pipeline - EACOP) na upelekaji wa gesi asilia katika nchi jirani za Kenya, Uganda, Zambia na Malawi. Aidha, Wizara itaendelea kutekeleza shughuli za utafiti na uendelezaji wa mafuta na gesi asilia katika vitalu vya kimkakati; usambazaji wa gesi asilia viwandani, katika taasisi na majumbani na kuimarisha matumizi ya CNG katika magari.

Mheshimiwa Spika, vipaumbele vingine ni kuendelea kuimarisha matumizi ya nishati safi ya kupikia (clean cooking) nchini pamoja na upatikanaji wa nishati ya mafuta vijijini kupitia uanzishwaji wa vituo vya mafuta katika maeneo hayo; kuhakikisha nchi inaendelea kuwa na uhakika wa upatikanaji wa bidhaa za mafuta ya petroli pamoja na ufanisi katika kushughulikia upatikanaji wa bidhaa hizo; kuimarisha uwekezaji na ushiriki wa Sekta Binafsi katika shughuli za utafutaji na uendelezaji wa mafuta na gesi asilia pamoja na uzalishaji na usambazaji wa umeme na kuendelea kuimarisha utoaji wa huduma, tija na ufanisi katika uendeshaji wa Taasisi/Mashirika yaliyo chini ya Wizara ya TANESCO, TPDC, EWURA, PURA na PBPA pamoja na Kampuni Tanzu. Wizara pia itaendelea kuimarisha ushiriki

120​

wa wazawa katika shughuli za mafuta na gesi asilia pamoja na rasilimali watu ya Wizara ya Taasisi zake na upatikanaji wa vitendea kazi muhimu.

Mheshimiwa Spika, Mpango na Bajeti ya Wizara kwa mwaka 2024/25 pamoja na mambo mengine, umezingatia Dira ya Taifa ya Maendeleo ya Mwaka 2025, Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (FYDP III) 2021/22 – 2025/26, Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa Ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020, Maagizo ya Viongozi wa Kitaifa katika Sekta ya Nishati, Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2024/25 pamoja na Mpango Mkakati wa Wizara wa Miaka Mitano (2021/22 - 2025/26). Miongozo mingine iliyozingatiwa ni Sera, Mikakati na Programu mbalimbali za Kisekta na Kitaifa pamoja na Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (SDGs) ya mwaka 2030 kuhusu masuala ya nishati.

C.1 SEKTA NDOGO YA UMEME NA NISHATI JADIDIFU

C.1.1 MIRADI YA KUZALISHA UMEME

Mheshimiwa Spika,
kama nilivyoeleza awali, moja ya kazi kubwa iliyopo mbele yetu ni kuhakikisha nchi yetu inakuwa na umeme wa kutosha kwa kuzingatia mahitaji ya sasa na ya

121​

baadaye kutokana na kasi ya ukuaji wa uchumi na maendeleo ya kijamii. Ili kutimiza azma hiyo Wizara imepanga kutekeleza miradi mbalimbali ya uzalishaji wa umeme kama ifuatavyo:

Miradi ya Kuzalisha Umeme Iliyopo Katika Hatua za Utekelezaji

Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Maji wa Julius Nyerere

(JNHPP)–MW 2,115

Mheshimiwa Spika,
kazi zilizopangwa kutekelezwa katika mwaka 2024/25 ni pamoja na kukamilisha ujenzi wa jengo la mitambo (power house) na ufungaji wa mitambo saba (7) ambayo ipo katika hatua mbalimbali za ukamilishwaji. Jumla ya Shilingi bilioni 620 fedha za ndani zimetengwa ili kukamilisha mradi huu.

Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Gesi Asilia wa Kinyerezi

Mheshimiwa Spika,
kazi zilizopangwa kutekelezwa kwa mwaka 2024/25 ni pamoja na kukamilisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa kilovoti 132 yenye urefu wa kilomita 19.2 kutoka kituo cha kuzalisha umeme cha Kinyerezi kwenda Gongolamboto hadi Mbagala Jijini Dar es Salaam na kufunga transfoma maeneo

122​

ya Gongolamboto na Mbagala, ikiwemo kukamilisha kazi za mitambo ya uzalishaji zilizobaki kwa uangalizi.

Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Maji wa Rusumo – MW 80

Mheshimiwa Spika,
kazi zilizopangwa kufanyika ni pamoja na uangalizi wa njia ya kusafirisha umeme kwa kipindi cha matazamio (defect liability period) hadi Aprili 2025, pamoja na kufanya malipo ya mwisho (retention money). Jumla ya Shilingi Bilioni 4 fedha za ndani zimetengwa.

Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Maji wa Malagarasi – MW 49.5

Mheshimiwa Spika,
mradi huu unahusu ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme wa MW 49.5 kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Malagarasi, mkoani Kigoma kwa gharama ya Dola za Marekani Milioni 144.14 (sawa na Shilingi bilioni 364.67) na unatekelezwa kwa ufadhili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB). Serikali inaendelea na ujenzi wa Bwawa la kuzalisha umeme pamoja na njia ya kusafirisha na kusambaza umeme. Jumla ya Shilingi bilioni 5.1

123​

fedha za nje zimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huu.

Mradi wa Kuzalisha Umeme Jua Shinyanga – MW 150

Mheshimiwa Spika,
Serikali itakamilisha ujenzi wa mitambo ya kuzalisha umeme kwa kutumia nishati ya jua wa MW 150. Ujenzi unaendelea na unatarajiwa kamilika Januari, 2025.

Ukarabati wa Mitambo katika Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Hale

Mheshimiwa Spika,
Serikali itakamilisha ukarabati wa miundombinu ya kuzalisha umeme katika Kituo cha Hale ili kiwe na uwezo wa kuzalisha MW 21. Jumla ya Shilingi bilioni 1.3 fedha za ndani zimetengwa kwa kazi hiyo.

Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Maji wa Kakono – MW 87.8

182. Mheshimiwa Spika, mradi huu unalenga kujenga Bwawa la kuzalisha umeme MW 87.8 kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Kagera, mkoani Kagera na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa Kilovoti 220 yenye urefu wa kilomita 38.7. Kazi zilizopangwa ni

124​

kukamilisha malipo ya fidia kwa wananchi wanaopisha mradi, kupata Mkandarasi Mjenzi na kuanza utekelezaji wa mradi.

Miradi ya Kuzalisha Umeme Iliyopo katika Hatua za Maandalizi

Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Maji ya mto Kikonge–MW 321

Mheshimiwa Spika,
Serikali inalenga kujenga kituo cha kuzalisha umeme wa MW 321 kwa kutumia maporomoko ya maji ya mto Ruhuhu mkoani Ruvuma na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 220 yenye urefu wa kilomita 96 kutoka Kikonge hadi kituo cha kupoza umeme cha Madaba. Kazi zitakazofanyika ni kuendelea na tathmini ya Athari ya Mazingira, uwekaji wa mipaka katika eneo la uzalishaji wa umeme, usanifu wa kina na maandalizi ya nyaraka za zabuni za mradi (bwawa la kuzalisha umeme na njia ya kusafirisha umeme). Jumla ya Shilingi milioni 500 fedha za ndani zimetengwa.

125​

Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Maji wa Ruhudji – MW 358

184. Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme wa MW 358 kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Ruhudji na njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa Kiloviti 400 yenye urefu wa kilomita 170 kutoka Ruhudji mkoani Njombe hadi kituo cha kupoza umeme cha Kisada mkoani Iringa. Gharama za ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme zinakadiriwa kuwa Dola za Marekani millioni 867.41 na njia ya kusafirisha umeme Dola za Marekani millioni 100. 9. Kazi zitakazotekelezwa ni pamoja na kulipa fidia kwa wananchi wanaopisha eneo la mradi, ujenzi wa miundombinu wezeshi ya barabara na kuendelea na taratibu za kupata ufadhili wa mradi. Kiasi cha Shilingi bilioni 37 fedha za ndani zimetengwa.

Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Maji wa Rumakali – MW 222

Mheshimiwa Spika, mradi unahusu ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme wa MW 222 kwa kutumia maji ya Mto Rumakali mkoani Njombe na njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 220 yenye urefu wa kilomita 65 kutoka kwenye mitambo hadi kituo cha kupoza umeme cha Iganjo mkoani Mbeya. Gharama za mradi huu

126​

kwa pamoja zinakadiriwa kuwa Dola za Marekani milioni 612.78 kwa upande wa mitambo ya kufua umeme. Gharama za njia ya kusafirisha umeme ni Dola za Marekani milioni 21.72. Kazi zitakazotekelezwa ni pamoja na kulipa fidia kwa wananchi wanaopisha eneo la mradi, ujenzi wa miundombinu wezeshi na kuendelea na taratibu za kupata ufadhili wa mradi. Kiasi cha Shilingi bilioni 2 fedha za ndani zimetengwa.

Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Gesi Asilia wa Mtwara (MW 300)

Mheshimiwa Spika, mradi huu unalenga ujenzi wa mitambo ya kufua umeme wa MW 300 kwa kutumia gesi asilia mkoani Mtwara pamoja na ujenzi wa njia za kusaifirisha umeme ya Kilovoti 400 kutoka Mtwara hadi Somangafungu na vituo vya kupoza umeme ili kuimarisha upatikanaji wa umeme nchini ikiwemo katika mikoa ya Mtwara na Lindi. Kazi zitakazotekelezwa ni pamoja na kukamilisha malipo ya fidia kwa wananchi watakaopisha eneo la ujenzi wa kituo cha kufua umeme pamoja ya njia ya kusafirisha umeme na kutafuta fedha za ujenzi wa mradi. Jumla ya Shilingi bilioni 2.55 fedha za ndani zimetengwa kwa kazi hiyo.

127​

Mradi wa Kinyerezi III wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Gesi Asilia MW 600

Mheshimiwa Spika,
mradi huu unalenga kuzalisha umeme wa MW 600 katika eneo la Kinyerezi III. Kwa sasa Serikali inaendelea na taratibu za upatikanaji wa fedha/ufadhili na kuanza taratibu za ununuzi. Jumla ya Shilingi milioni 200 fedha za ndani zimetengwa kwa kazi hiyo.

Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Upepo MW 100 Kititimo Mkoani Singida

Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu ujenzi wa mitambo ya kuzalisha umeme MW 100 kwa kutumia upepo pamoja na njia ya kusafirisha umeme ya kilomita 8 ya msongo wa kilovoti 220 na kituo cha kupoza umeme. Gharama za mradi huu zinakadiriwa kuwa Dola za Marekani milioni 153. Kazi zitakazotekelezwa ni pamoja na upembuzi yakinifu, kufanya tathmini ya mali za wananchi watakaopisha mradi pamoja na kutafuta fedha/ufadhili na kuanza taratibu za ununuzi. Jumla ya Shilingi bilioni 3 fedha za ndani zimetengwa kwa kazi hiyo.

128​

Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Jua MW 100 Wilaya ya Manyoni

Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu ujenzi wa mitambo ya kuzalisha umeme wa MW 100 kwa kutumia jua pamoja na kituo cha kupoza umeme Wilayani Manyoni. Gharama za mradi huu kwa pamoja zinakadiriwa kuwa Dola za Marekani milioni 120. Kazi zitakazotekelezwa ni pamoja na upembuzi yakinifu, kufanya tathmini ya mali za wananchi watakaopisha mradi na kulipa fidia. Serikali inaendelea kutafuta fedha/ufadhili na kuanza taratibu za manunuzi. Jumla ya Shilingi milioni 400 zimetengwa kwa kazi hiyo.

Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa kutumia Jua MW 60 Zuzu Dodoma

Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu ujenzi wa mitambo ya kuzalisha umeme wa MW 60 kwa kutumia jua Mkoani Dodoma. Gharama za mradi huu kwa pamoja zinakadiriwa kuwa Dola za Marekani milioni 77.66. Kazi zitakazotekelezwa ni pamoja na upembuzi yakinifu na kuanza utekelezaji. Serikali inaendelea kutafuta fedha/ufadhili na kuanza taratibu za ununuzi. Jumla ya Shilingi milioni 25 fedha za ndani zimetengwa kwa kazi hiyo.

129​

C.1.2 MIRADI YA KUSAFIRISHA NA KUSAMBAZA UMEME

Mheshimiwa Spika,
umeme ukishazalishwa, hauna budi kusafirishwa ili kuweza kuwafikia walaji, hivyo upatikanaji wa umeme wa uhakika ni pamoja na kuwa na miundombinu madhubuti ya usafirishaji na usambazaji wa umeme pamoja na vituo vya kupoza umeme. Kutokana na changamoto ya muda mrefu ya miundombinu chakavu na isiyotosheleza ya kusafirisha na kusambaza umeme, Serikali itaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya usafirishaji na usambazaji wa umeme katika mwaka 2024/25 kama ifuatavyo:

Miradi ya Kusafirisha na Kusambaza Umeme Iliyopo Katika Hatua za Utekelezaji

Mradi wa Kusafirisha Umeme kutoka Julius Nyerere Hydro Power Plant hadi Chalinze – Kilovoti 400 na Kituo cha Kupoza Umeme, Chalinze

Mheshimiwa Spika,
mradi unahusu ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa kilovoti 400 kutoka JNHPP hadi Chalinze na kituo cha

kupoza umeme cha Chalinze Kilovoti 400/220/132. Kazi zitakazotekelezwa ni pamoja na kumalizia kazi zilizobaki katika kituo cha kupoza

130​

umeme ikiwemo majengo, barabara, njia ya kusafirisha umeme na marekebisho mbalimbali. Shilingi bilioni 2 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya kazi hiyo.

Ujenzi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa Kilovoti 400 kutoka Chalinze – Dodoma

193. Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 400 kutoka Chalinze hadi Dodoma yenye urefu wa kilomita 345 na upanuzi wa vituo vya kupoza umeme vya Chalinze na Dodoma. Kazi zitakazotekelezwa ni pamoja na kuendelea na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme na vituo vya kupoza umeme. Jumla ya Shilingi bilioni 245 fedha za ndani zimetengwa kwa kazi hiyo.

Ujenzi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa Kilovoti 400 kutoka Chalinze - Kinyerezi - Mkuranga

Mheshimiwa Spika, awamu ya kwanza ya mradi huu inahusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 400 kutoka Chalinze, Kinyerezi hadi Mkuranga na vituo vya kupoza umeme vya Chalinze, Kinyerezi, Mkuranga na Morogoro. Kazi zitakazotekelezwa ni pamoja na

131​

kuendelea na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme na vituo vya kupoza umeme. Jumla ya Shilingi bilioni 7 fedha za ndani zimetengwa kwa kazi hizo.

Ujenzi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa Kilovoti 400 kutoka Chalinze – Segera na Msongo wa Kilovoti 220 Segera – Tanga

Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 400 kutoka Chalinze – Segera na Msongo wa Kilovoti 220 Segera – Tanga, na ujenzi wa vituo vya kupoza umeme vya Segera na Tanga. Kazi zitakazotekelezwa ni pamoja na kukamilisha malipo ya fidia, kuanza ununuzi wa Wakandarasi na kuanza ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme na vituo vya kupoza umeme. Jumla ya Shilingi bilioni 4.21 zitatumika kwa ajili ya kulipa fidia kwa wananchi watakaopisha mradi.

Ujenzi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa Kilovoti 220 kutoka Chalinze – Bagamoyo hadi Ununio Dar es salaam

Mheshimiwa Spika, mradi unahusu ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 220 kutoka Chalinze – Bagamoyo hadi Ununio na ujenzi wa vituo vya kupoza umeme vya

132​

Bagamoyo na Ununio. Kazi zitakazotekelezwa ni pamoja na kukamilisha malipo ya fidia, kuanza manunuzi ya Wakandarasi na kuanza ujenzi wa njia ya kusafirisha na vituo vya kupoza umeme. Jumla ya Shilingi bilioni 4.3 fedha za ndani zimetengwa kwa kazi hiyo.

Ujenzi wa Kituo cha Kupoza Umeme cha Ibadakuli Shinyanga Kilovoti 400/220/33

Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu ujenzi wa kituo cha kupoza umeme cha msongo wa Kilovoti 400/220/33 Ibadakuli - Shinyanga. Gharama ya mradi huu ni Dola za Marekani milioni 50. Serikali itaendelea kutekeleza mradi huu ambapo kazi zilizopangwa kufanyika ni pamoja na ununuzi wa vifaa na nyenzo zote zinazohitajika kwa ajili ya utekelezaji wa mradi. Jumla ya Shilingi bilioni 37.5 fedha za ndani zimetengwa.

Ujenzi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa Kilovoti 400 kutoka Iringa hadi Sumbawanga kupitia Mbeya na Tunduma (TAZA)

Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 400 kutoka Iringa kupitia

133​

Mbeya, Tunduma hadi Sumbawanga yenye urefu wa kilomita 620 pamoja na ujenzi wa vituo vya kupoza umeme vya Kisada (Iringa), Iganjo (Mbeya), Tunduma na Sumbawanga. Aidha, mradi huu unalenga pia kuunganisha Gridi ya Taifa na Nchi za Kusini mwa Afrika (Southern African Power Pool

– SAPP)
. Kazi zitakazotekelezwa ni pamoja na kuendelea na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme na vituo vya kupoza umeme ikiwemo kukamilisha ulipaji wa fidia. Jumla ya Shilingi bilioni 51 fedha za nje zimetengwa kwa kazi hizo.

Mradi wa Kuboresha Utendaji Kazi wa TANESCO (Corporate Management System – CMS)

Mhesimiwa Spika, mradi huu unalenga kuboresha hali ya utendaji kazi wa TANESCO kwa kuanzisha mifumo itakayowezesha kuongeza ufanisi wa utendaji kazi. Mradi huu ni sehemu ya Mradi wa Tanzania – Zambia Interconnector Transmission Project (TAZA). Gharama za mradi huu ni Dola za Marekani milioni 34.8 sawa na Shilingi bilioni 81.61. Kazi zilizopangwa kufanyika ni pamoja na kumalizia kazi za ufungaji wa vifaa vya miundombinu vya mradi (data center infrastructure) na kufanyiwa majaribio utendaji wake. Aidha, mafunzo kwa wafanyakazi wote yataendelea kutolewa. Jumla ya Shilingi bilioni

134​

25.9 fedha za nje zimetengwa kwa ajili ya kutekeleza kazi zilizopangwa.

Ujenzi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa Kilovoti 400 kutoka Nyakanazi hadi Kigoma

Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kiloviti 400 kutoka Nyakanazi hadi Kigoma yenye urefu wa kilomita 280, ujenzi wa kituo cha kupoza umeme Kidahwe Mkoani Kigoma, upanuzi wa kituo cha kupoza umeme cha Nyakanazi na usambazaji umeme katika vijiji 18 vilivyopo katika eneo la mradi. Utekelezaji wa mradi wa njia ya kusafirisha umeme umefikia asilimia 94.98. Kazi zitakazotekelezwa ni kuendelea na ujenzi wa kituo cha kupoza umeme cha Nyakanazi na Kidahwe na miundombinu ya usambazaji umeme katika vijiji vinavyopitiwa na mradi.

Mradi wa Kuimarisha Gridi ya Taifa (National Grid Stabilization Project)

– Gridi Imara

Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu utekelezaji wa awamu ya kwanza ya miradi 27 ya uimarishaji wa miundombinu ya umeme katika mikoa mbalimbali ikiwa ni pamoja na ujenzi wa njia za kusafirisha umeme za msongo

135​

wa kilovoti 220 na 132 na kuongeza uwezo wa nyaya za kusafirisha umeme (re -conductoring), ujenzi wa njia za kusambaza umeme za msongo wa kilovoti 33, ujenzi wa vituo vya kupoza umeme na kuongeza uwezo wa baadhi ya vituo na ujenzi wa vituo vya kupoza umeme katika maeneo ya

usambazaji (switching station ). Kazi zitakazofanyika ni kuendelea kulipa fidia kwa wananchi wanaopisha miradi, ujenzi wa njia za kusafirisha umeme na vituo vya kupoza umeme. Mradi unatarajiwa kukamilika Desemba 2025. Jumla ya Shilingi bilioni 200 fedha za ndani zimetengwa.

Mradi wa Ukarabati na Uboreshaji wa Gridi ya Taifa (Grid Rehabilitation and Upgrading)-TTGRUP

Mheshimiwa Spika, mradi huu unalenga kuimarisha Gridi ya Taifa kwa kukarabati na kuboresha vituo vya kupoza umeme katika maeneo mbalimbali nchini na unafadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) pamoja na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kazi zitakazofanyika ni ukamilishaji wa usanifu, uagizaji wa vifaa na kukamilisha mradi.

136​

Ujenzi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa Kilovoti 220 kutoka Benaco hadi Kyaka

Mheshimiwa Spika, mradi huu unalenga ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 220 kutoka Benaco hadi Kyaka yenye urefu wa kilomita 166.17. Gharama za mradi ni Dola za Marekani milioni 105.4 sawa na Shilingi bilioni 263.5. Kazi zitakazofanyika ni kulipa fidia, kuanza kazi za usanifu, utafiti wa udongo, uagizaji wa vifaa na kuanza kazi za ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme na vituo vya kupoza umeme vya Benaco na Kyaka. Jumla ya Shilingi bilioni 5.4 fedha za nje na Shilingi bilion 6.2 fedha za ndani zimetengwa.

Ujenzi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa Kilovoti 220 kutoka Makutopora hadi Tabora kwa ajili ya Uendeshaji wa Treni ya Umeme (SGR Lot 3)

Mhesimiwa Spika, mradi huu unahusu ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 220 yenye urefu wa kilomita 347 kutoka Makutopora hadi Tabora kwa ajili ya uendeshaji wa treni ya umeme. Gharama za mradi huu zinakadiriwa kuwa ni Dola za Marekani milioni 90.65 sawa na Shilingi bilioni 212.58. Kazi

137​

zitakazofanyika ni pamoja na ukamilishaji wa upembuzi yakinifu ikiwemo tathmini ya mazingira, kufanya uthamini wa mali za wananchi watakaopisha mradi, kulipa fidia na kuanza taratibu za kupata Wakandarasi. Jumla ya Shilingi bilioni 15 zimetengwa kupitia Fungu la SGR.

Ujenzi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa Kilovoti 220 kutoka Tabora hadi Isaka kwa ajili Uendeshaji wa Treni ya Umeme (SGR Lot 4)

Mhesimiwa Spika, mradi huu unahusu ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 220 yenye urefu unaokadiriwa kuwa kilomita 195 kutoka Tabora hadi Isaka kwa ajili ya uendeshaji wa treni ya umeme. Gharama za mradi huu inakadiriwa kuwa Dola za Marekani milioni 56.1 sawa na Shilingi bilioni 131.7. Kazi zitakazofanyika ni pamoja na ukamilishaji wa upembuzi yakinifu ikiwemo tathmini ya mazingira, kufanya uthamini wa mali za wananchi wataopisha mradi, kulipa fidia, na kuanza taratibu za kupata Wakandarasi. Jumla ya Shilingi bilioni 10 zimetengwa kupitia Fungu la SGR.

138​

Mradi wa Njia ya Kusafirishi Umeme Msongo wa Kilovoti 220 kutoka Mwanza hadi Isaka kwa ajili ya Uendeshaji wa Treni ya Umeme (SGR Lot V)

Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 220 yenye urefu wa kilomita 230 kutoka Mwanza hadi Isaka kwa ajili ya uendeshaji wa treni ya umeme. Kazi zitakazotekelezwa ni ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme na kuendelea na malipo ya fidia. Jumla ya Shilingi Bilioni 14 zimetengwa kupitia Fungu la SGR kwa ajili ya malipo ya fidia na Shilingi bilioni 45 za utekelezaji wa mradi.

Miradi ya Kusafirisha na Kusambaza Umeme Iliyopo Katika Hatua za Maandalizi

Ujenzi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa Kilovoti 400 Kutoka Sumbawanga hadi Kigoma Kupitia Mpanda (Km 480) na Kituo cha Kupoza Umeme Mpanda

Mheshimiwa Spika,
kazi zitakazotekelezwa ni pamoja na kufanya tathmini ya mali za wananchi watakaopisha mradi pamoja kuweka mipaka ya mkuza wa njia ya kusafirisha umeme kutoka

139​

Sumbawanga kupitia Mpanda hadi Kigoma, na kutafuta fedha za kutekeleza mradi. Jumla ya Shilingi milioni 600 fedha za ndani zimetengwa kutekeleza kazi hizo.

Ujenzi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa Kilovoti 400 Kutoka Segera – Same – Lemugur (Kisongo) Arusha

Mheshimiwa Spika,
mradi unahusu ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa kilovoti 400 kutoka Segera – Same – Lemugur (Kisongo) Arusha na kituo cha kupoza umeme kilovoti 220/132/33 cha Mwanza. Kazi zilizopangwa kutekelezwa ni kukamilisha Upembuzi Yakinifu, Athari za Mazingira na Jamii (ESIA), usanifu wa mradi, kufanya tathmini ya mali za wananchi watakaopisha mradi, kuanza kulipa fidia na kuendelea kutafuta fedha za utekelezaji wa mradi. Jumla ya Shilingi bilioni 9 fedha za ndani zimetengwa kutekeleza kazi hizo.

Ujenzi wa Njia ya Kusafirisha Umeme (Submarine Cable) Msongo wa Kilovoti 220 Kutoka Tanzania Bara (Ununio) hadi Zanzibar (Unguja)

Mhesimiwa Spika, Serikali kupitia Mshauri Mwelekezi itakamilisha Upembuzi Yakinifu, Athari za Mazingira na Jamii (ESIA) na usanifu wa

140​

mradi. Aidha, Serikali itaendelea kutafuta fedha za kutekeleza mradi huu.

Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Kupoza Umeme Manyoni (Manyoni Substation - MVA 60)

Mhesimiwa Spika, Serikali itakamilisha kazi ya tathmini ya mali za wananchi watakaopisha mradi, na kulipa fidia. Aidha, itaendelea na taratibu za kutafuta fedha kiasi cha Dola za Marekani milioni 16.36 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi pamoja na kutafuta Mkandarasi Mjenzi. Jumla ya Shilingi milion 500 fedha za ndani zimetengwa kutekeleza kazi hizo.

Mradi wa Kusafirisha Umeme Msongo wa Kilovoti 400 kutoka Tanzania hadi Uganda (Masaka - Ibadakuli)-UTIP

Mheshimiwa Spika, mradi unahusu ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti

kutoka Tanzania hadi Uganda (Masaka - Ibadakuli) yenye urefu wa kilomita 617 na kituo cha kupoza umeme Kilovoti 220/33 cha Kyaka. Serikali itakamilisha kazi ya kufanya uthamini wa mali za wananchi watakaopisha mradi na kuanza kulipa fidia na pia itaendelea na taratibu za kutafuta fedha za utekelezaji wa mradi kiasi cha Dola za Marekani milioni 383.9. Jumla ya Shilingi

141​

bilioni 20 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya utekelezaji.

Miradi ya Ujenzi wa Njia ya Kusafirisha Umeme kwa Ajili ya Kuunga Gridi ya Taifa na Nchi za Jirani kwa Msongo wa Kilovoti 400 Kutoka Tanzania Hadi Malawi (TAMA); Kilovoti 400 Kutoka Tanzania Hadi Msumbiji (MOTA) na Kilovoti 400 Kutoka Tanzania hadi DRC

Mheshimiwa Spika, miradi hii inahusu ujenzi wa njia za kusafirisha umeme kwa ajili ya kuunga Gridi ya Taifa na nchi za jirani kwa msongo wa Kilovoti 400 kutoka Tanzania hadi Malawi (TAMA); Kilovoti 400 kutoka Tanzania hadi Msumbiji (MOTA) na Kilovoti 400 kutoka Tanzania hadi DRC. Kazi zitakazofanyika ni kufanya uthamini wa mali na Upembuzi Yakinifu. Serikali itaendelea kutafuta fedha za kutekeleza kazi hizo. Jumla ya Shilingi milioni 800 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya utekelezaji.

Mradi wa Kuboresha Mfumo wa Usambazaji Umeme Msongo wa Kilovoti 220 katika Jiji la Dodoma, Mbeya, Arusha, Mwanza

142​

Mheshimiwa Spika, lengo kuu la mradi huu ni kuandaa Mpango Kabambe wa Usambazaji umeme utakaoiongoza TANESCO kuendelea kutekeleza miradi ya usambazaji umeme ili kukidhi ongezeko la mahitaji ya umeme na kupunguza upotevu wa umeme katika njia za usambazaji katika Majiji hayo. Aidha, mpango huu unalenga kuongeza upatikanaji wa umeme wa uhakika (reliability). Vilevile, mradi huu unahusisha ujenzi wa njia za mzunguko (ring circuirts) za kusafirisha umeme wa msongo wa Kilovoti 220 na ujenzi wa vituo vipya vya kupoza umeme pamoja na upanuzi wa vituo vya kupoza umeme vilivyopo. Kwa kuwa utekelezaji wa miradi hii inahitaji fedha nyingi, maandalizi ya utekelezaji yameanza na Majiji manne ambayo ni Arusha, Mwanza, Dodoma na Mbeya. Kazi zitakazofanyika ni kuendelea na shughuli ya upembuzi yakinifu.

Mradi wa Kuboresha Mfumo wa Usambazaji Umeme katika Jiji la Dodoma

Mheshimiwa Spika, Serikali imekusudia kulibadilisha jiji la Dodoma kimazingira kwa kuhakikisha miundombinu ya umeme haiwi sehemu ya vitu vinavyolifanya jiji hilo kutokuwa na muonekano mzuri. Kwa kuzingatia hilo, Serikali imeanza maandalizi ya mradi wa kubadilisha miundombinu ya usambazaji umeme kwa kutumia

143​

nguzo na kuelekea kwenye miundombinu ya usambazaji inayopita chini ya ardhi. Aidha, mradi huu unalenga kuboresha miundombinu ya usambazaji katika jiji la Dodoma kwa kubadilisha njia za kusambazia umeme pamoja na transfoma zake. Vilevile, katika utekelezaji wa mradi huu, kutakuwa na upanuzi wa vituo vidogo vilivyopo katikati ya jiji ili kuviongezea uwezo. Hatua hii itawezesha kuendelea kusambaza umeme wenye kukidhi mahitaji kwa wateja wapya wanaoongezeka katikati ya jiji. Hata hivyo mradi huu upo katika hatua za awali na tayari Exim Bank ya Korea imeonyesha nia ya kuufadhili na kufanya upembuzi yakinifu. Kazi zinazotarajiwa kufanyika katika mwaka 2024/25 ni upembuzi yakinifu pamoja na kuandaa usanifu wa awali wa mradi. Kiasi cha Shilingi milioni 200 za ndani zimetengwa.

Mradi wa Ujenzi wa Vituo vya Kupoza Umeme katika Kila Wilaya Nchini

Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu ujenzi wa vituo vya kupoza umeme vya Gridi ya Taifa katika Wilaya zote nchini. Mradi utatekelezwa chini ya mradi wa Gridi imara katika awamu tano (5) ambapo katika kila awamu vitajengwa vituo vya kupoza umeme kumi na tano (15). Utekelezaji wa mradi unalenga kuboresha miundombinu ya usambazaji na kupunguza

144​

upotevu wa umeme unaotokana na umbali mrefu wa njia za usambazaji umeme katika maeneo mbalimbali nchini. Gharama za mradi zinakadiriwa kuwa Shilingi trilioni 4.20.

216. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2024/25, Serikali kupitia TANESCO itaanza utekelezaji wa mradi huu kwa kufanya Upembuzi Yakinifu wa mradi, Tathmini ya Athari kwa Mazingira na Jamii, tathmini ya mali za wananchi watakaopisha mradi, na kuanza kutafuta fedha za ujenzi wa mradi. Serikali imetenga Shilingi bilioni 5.4 kwa ajili ya utekelezaji wa kazi hizo. Kiambatisho Na.11 ni mchanganuo wa miradi itakayotekelezwa katika kila Wilaya kwa kila awamu.

C.1.3 MIRADI MINGINE ITAKAYOTEKELEZWA

YA MATENGENEZO YA MITAMBO

Mheshimiwa Spika,
TANESCO kupitia mapato yake ya ndani itafanya matengenezo kinga katika vituo vya kuzalisha umeme, kufanya matengenezo makubwa na madogo katika miundombinu ya kusafirisha, kusambaza na vituo vya kupoza umeme. Aidha, Shirika litaendelea kutekeleza miradi inayolenga kuongeza uwezo wa miundombinu ya kusafirisha umeme, kuboresha mifumo ya uendeshaji Gridi, kuweka mifumo ya kisasa ya mawasiliano katika vituo vya kupoza

145​

umeme, kujenga vituo vidogo vya kuendesha Gridi (unmanned substations) na kuweka mfumo wa “Advance Metering Infrastructure-AMI” wa kufunga Mita Janja (Smart Meter).

Mheshimiwa Spika, TANESCO pia itatekeleza miradi ya kupeleka umeme katika maeneo mbalimbali pamoja na kufanya maboresho kwenye miundombinu ya usambazaji ili kuondoa adha za kuwa na umeme mdogo kwa wananchi na kuunganisha wateja wapya. Jumla ya Shilingi bilioni 959.792 fedha za ndani zimetengwa kutumika kwa ajili ya kazi hizo ili kuimarisha uwezo wa miundombinu ya kuzalisha, kusafirisha na kusambaza umeme iliyopo.

C.1.4 UTENDAJI WA KAMPUNI TANZU ZA TANESCO (TCPM NA ETDCO)

Kampuni ya Ujenzi na Ukarabati wa

Miundombinu ya Usafirishaji na Usambazaji Umeme (ETDCO)

Mheshimiwa Spika,
Serikali kupitia kampuni tanzu ya TANESCO ya ETDCO, imepanga kukamilisha utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 132 kutoka Tabora hadi Urambo na kutoka Urambo hadi Kidahwe Mkoani Kigoma. Aidha, ETDCO itakamilisha utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini katika Mikoa ya Geita na Kigoma

146​

inayosimamiwa na REA. Vilevile, ETDCO imepanga kujenga mradi wa njia ya kusafirisha Umeme Kilovoti 220 Masasi – Mahumbika yenye urefu wa kilometa 128 katika mikoa ya Mtwara na Lindi.

Kampuni ya Kutengeneza Nguzo za Zege Tanzania (TCPM)

Mheshimiwa Spika, Kampuni ya TCPM inatarajia kuzindua kiwanda chake cha kwanza cha kuzalisha nguzo za zege Mkoani Tabora. Kampuni itaendelea kuingia ushirikiano (joint venture) na Wawekezaji binafsi ili kuongeza uzalishaji na upatikanaji wa nguzo za zege na kurahisisha zoezi la usafirishaji wa nguzo hizo katika maeneo mbalimbali nchini.

Kampuni ya Uendelezaji wa Rasilimali ya Jotoardhi (TGDC)

Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2024/25 Serikali kupitia TGDC itatekeleza yafuatayo:

Itakamilisha uchorongaji wa visima vitatu (3) vya uhakiki (exploratory wells) ili kuhakiki hifadhi, kiwango na ubora wa rasilimali ya jotoardhi katika mradi wa Ngozi (Mbeya) wenye uwezo wa kuzalisha MW 30 katika awamu ya kwanza pamoja na kuanza ujenzi wa mtambo mdogo wa kuzalisha umeme

147​

(wellhead generator) wa MW 5. Jumla ya Shilingi bilion 2.9 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa kazi hizo.

ii. Itaanza utekelezaji wa programu ya uchorongaji wa visima vinne (4) vya uhakiki, kutekeleza miradi ya matumizi mengineyo pamoja na maandalizi ya upatikanaji wa mtambo wa kuzalisha umeme katika mradi la Kiejo Mbaka (Mbeya) wenye uwezo wa kuzalisha MW 60. Jumla ya Shilingi bilioni 14. 56 zimetengwa kwa ajili ya ukamilishaji wa shughuli hizo;

Itakamilisha taratibu za umiliki wa ardhi na maandalizi ya uchorongaji wa visima vinne (4) vya uhakiki katika mradi wa Songwe (Songwe) wa MW 5. Jumla ya Shilingi milioni 560 zimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa kazi hizo;

Kufanya maandalizi ya programu ya uchorongaji wa visima vitatu (3) vya uhakiki pamoja na kufanya upembuzi yakinifu wa matumizi mengineyo katika eneo la mradi wa Luhoi (Pwani) MW 5. Jumla ya Shilingi milioni 350 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya kutekeleza kazi hizo;

148​

Kukamilisha utafiti wa kina wa kijiosayansi wa juu ya ardhi (detailed surface exploration) pamoja na ununuzi wa vifaa vya kufanya tafiti katika eneo la mradi la Natron MW 60 (Arusha) ambapo jumla ya Shilingi bilioni 1.28 zimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa kazi husika;

Kufanya utafiti wa kina wa kijiosayansi wa juu ya ardhi (detailed surface exploration) katika eneo la mradi wa Meru (Arusha) wa MW 60 pamoja na kuajiri Mshauri Mwelekezi kwa ajili ya kufanya kazi ya utafiti huo. Jumla ya Shilingi milioni 700 zimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa kazi husika; na

Kuratibu Kongamano la 10 la Jotoardhi (African Rift Geothermal Conference-ARGeo C-
litakalofanyika Novemba, 2024 Jijini Dar es Salaam.

C.1.5 USHIRIKISHWAJI WA SEKTA BINAFSI KATIKA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA UMEME

Mheshimiwa Spika,
Serikali kupitia TANESCO itaendelea na taratibu za kutekeleza miradi ya kufua umeme inayotarajiwa kutekelezwa na wawekezaji binafsi, ikiwemo miradi ya umeme jadidifu na vyanzo vingine. Wawekezaji binafsi

149​

wanaendelea kukaribishwa kujitokeza katika kutekeleza miradi ya upepo, jua, makaa ya mawe, maji na gesi katika maeneo mbalimbali nchini. Kazi zitakazofanyika kwa mwaka 2024/25 ni uchambuzi, uthamini na ulipaji wa fidia katika maeneo ya miradi, kutangaza zabuni na kuingia mikataba ya makubaliano na wawekezaji binafsi pamoja na kufanya upembuzi yakinifu.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa miradi ya usafirishaji wa umeme, Serikali kupitia TANESCO itaendelea kuwashirikisha wawekezaji binafsi katika utekelezaji wa miradi hii, hususan katika maeneo ya viwanda na migodi. Kazi zitakazofanyika ni uchambuzi wa maeneo ya miradi na kuingia makubaliano na wawekezaji binafsi kwa utekelezaji wa miradi hiyo.

C.1.6 MIRADI YA NISHATI VIJIJINI

Mheshimiwa Spika,
Katika Mwaka 2024/25, Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini itaendelea kuchukua hatua za kupeleka nishati vijijini ili kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi na maendeleo ya kijamii katika maeneo hayo. Ili kutekeleza azma hiyo, Serikali kupia Wakala wa Nishati Vijijini itatekeleza miradi ifuatayo:

150​

Mradi wa Kupeleka Umeme katika Vitongoji 20,000

Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusisha ujenzi wa miundombinu ya kusambaza umeme katika vitongoji 20,000 ambavyo bado havijafikiwa na miundombinu ya umeme. Jumla ya Shilingi bilioni 350 fedha za ndani zimetengwa. Kazi zitakazofanyika ni pamoja na kuandaa kabrasha la zabuni, ununuzi wa wakandarasi, kufanya usanifu wa kina wa mradi na kuanza ujenzi wa miundombinu ya mradi.

Mradi wa Kupeleka Umeme Katika Vitongoji katika Mkoa wa Songwe na Kigoma

Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusisha ujenzi wa miundombinu ya kusambaza umeme katika vitongoji 677 vya Mkoa wa Kigoma na Songwe ili kuwezesha ujenzi wa njia za umeme Msongo wa Kati zenye urefu wa kilomita 726.24; ujenzi wa njia za umeme wa Msongo Mdogo zenye urefu wa kilomita 1,308; ufungaji wa transfoma 653 pamoja na kuunganisha wateja wa awali 14,352. Kazi zitakazofanyika ni kukamilisha ujenzi wa miundombinu ya kusambaza umeme Msongo Mdogo, kufunga transfoma na kuunganisha wateja. Jumla ya Shilingi bilioni 26.60 kutoka Shirika la Fedha Duniani (IMF) kupitia dirisha la Extended Credit Facility zimetengwa kwa ajili ya kukamilisha utekelezaji wa mradi.

151​

Mradi wa Kupeleka Umeme katika Vitongoji 3,060

Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusisha ujenzi wa miundombinu ya kusambaza umeme katika vitongoji 3,060 ikiwa ni vitongoji 15 kila Jimbo, ujenzi wa njia za umeme Msongo wa Kati zenye urefu wa kilomita 258; ujenzi wa njia za umeme wa Msongo Mdogo zenye urefu wa kilomita 6,118; ufungaji wa transfoma 3,060 pamoja na kuunganisha wateja wa awali 100,947. Kazi zitakazofanyika ni kuendelea na ujenzi wa miundombinu ya mradi, kufunga transfoma na kuunganisha wateja.

Mradi wa Ujazilizi Awamu ya Pili B ( Densification IIB)

Mheshimiwa Spika, mradi huu unalenga kupeleka umeme kwenye vitongoji 1,686 katika mikoa 9 ya Arusha, Geita, Kagera, Katavi, Kigoma, Lindi, Morogoro, Njombe na Songwe ambapo kazi za ujenzi zinahusisha ujenzi wa njia za msongo mdogo zenye urefu wa kilomita 3,860, ufungaji wa transfoma 1,272 na kuunganisha wateja wa awali 95,334. Katika Mwaka 2024/25, Wakala wa Nishati Vijijini utaendelea kukamilisha kazi za ujenzi wa miundombinu ya mradi, kufunga transfoma na kuunganisha wateja. Jumla ya

152​

Shilingi bilioni 25.40 fedha za nje zimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa kazi hizo.

Mradi wa Ujazilizi Awamu ya Pili C (Densification IIC)

Mheshimiwa Spika, mradi huu umelenga kufikisha huduma za umeme kwenye vitongoji 1,880 katika mikoa 7 ya Manyara, Iringa, Rukwa, Mtwara, Ruvuma, Simiyu na Mara ili kujenga kilomita 5,640 za Msongo Mdogo, kufunga transfoma 1,880 na kuunganisha wateja wa awali 94,000. Katika Mwaka 2024/25, Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini itakamilisha kazi za ujenzi wa njia za umeme Msongo Mdogo, kufunga transfoma na kuunganisha wateja. Jumla ya Shilingi bilioni 2.41 fedha kutoka Benki ya Dunia zimetengwa ili kukamilisha kazi hizo.

Mradi wa Kupeleka Umeme Katika Maeneo ya Vijijini-Miji (Peri Urban)

Mheshimiwa Spika, mradi huu unalenga kutekelezwa katika mikoa 8 ya Geita, Kigoma, Kagera, Mbeya, Mtwara, Singida, Tabora na Tanga ambapo jumla ya maeneo 416 yatafikishiwa huduma ya umeme kupitia ujenzi wa njia za umeme wa Msongo wa Kati zenye urefu wa kilomita 379; ujenzi wa njia za umeme wa Msongo Mdogo zenye urefu wa kilomita 753; ufungwaji wa

153​

transfoma 314 pamoja na kuunganisha wateja wa awali 16,369 kwa gharama ya Shilingi bilioni 76.9 kutoka Serikali ya Tanzania. Katika Mwaka 2024/25, kazi zilizopangwa kufanyika ni ujenzi wa njia za umeme Msongo wa Kati na Mdogo, kufunga transfoma na kuunganisha wateja ambapo Shilingi bilioni 2 fedha za ndani zimetengwa.

Mradi wa Kusambaza Umeme katika Migodi Midogo, Maeneo ya Kilimo na Viwanda

Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu kupeleka umeme katika maeneo 581 ya wachimbaji wadogo wa madini, maeneo ya kilimo na viwanda Tanzania Bara kupitia ujenzi wa njia za Msongo wa Kati zenye urefu wa kilomita 1,370; ujenzi wa njia za umeme wa Msongo Mdogo zenye urefu wa kilomita 1,097; ufungwaji wa transfoma 517 pamoja na kuunganisha wateja wa awali 17,119. Katika Mwaka 2024/25, Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini itaendelea kukamilisha kazi za kupeleka umeme katika jumla ya maeneo ya migodi, kilimo na viwanda 581 ambapo Shilingi bilioni 5.00 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya kukamilisha kazi hizo.

154​

Mradi wa Kupeleka Umeme Katika Minara ya Mawasiliano ya Simu

Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu kupeleka umeme katika minara 754 ya mawasiliano katika maeneo mbalimbali nchini. Katika Mwaka 2024/25, Wakala wa Nishati Vijijini utaendelea kushirikiana na Universal Communications Services Access Fund (UCSAF) ili kupelekea umeme katika minara ya mawasiliano kwenye maeneno ya vijijini ambapo Shilingi bilioni 12.00 fedha za ndani zimetengwa .

Mradi wa Ufungaji wa Mifumo ya Umeme Jua kwenye Makazi Yaliyopo Visiwani na Yaliyopo Mbali na Gridi ya Taifa

Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu kufunga na kusambaza mifumo itakayozalisha umeme kwa kutumia nishati ya jua katika makazi yaliyo vijijini ambayo hayatafikiwa na gridi ya Taifa kwa kufunga mifumo ipatayo 7,000. Gharama za mradi ni Shilingi bilioni 9.4. Katika Mwaka 2024/25, kazi zitakazotekelezwa ni kutangaza mradi, kufanya tathmini ya maombi yaliyowasilishwa, kufanya due diligence, na kuanza kutekeleza mradi ambapo Shilingi bilioni 3.53 fedha kutoka Benki ya Dunia zimetengwa.

155​

Mradi wa Kusambaza Majiko Banifu kwenye Kaya Zilizopo katika Maeneo ya Vijijini na Vijiji-Miji

Mheshimiwa Spika, mradi huu unalenga kusambaza majiko banifu katika maneo ya vijijini na vijiji-miji (Peri Urban). Mradi utasambaza majiko banifu 70,000 yaliyotengenezwa kwa teknolojia yenye ubunifu wa kupunguza matumizi ya kuni na mkaa pamoja na kupunguza uharibifu wa mazingira. Gharama za mradi ni Shilingi bilioni 14.10. Katika Mwaka 2024/25, Wakala wa Nishati Vijijini utaandaa kabrasha la

mradi na kutangaza ili kuwapata wazalishaji/wasambazaji wa majiko, kufanya tathmini ya maombi yaliyowasilishwa, kufanya due diligence, na kuanza kutekeleza mradi ambapo Shilingi bilioni 4.7 kutoka Benki ya Dunia zimetengwa.

Utekelezaji wa Awamu ya Pili ya Mpango wa Kuhamasisha Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia

Mheshimiwa Spika, Mpango huu unahusisha ujenzi wa miundombinu ya nishati ya kupikia katika taasisi za umma na binafsi ambazo zinahudumia zaidi ya watu 300 kwa siku. Kazi zitakazotekelezwa ni pamoaja na kutoa ruzuku kwa wazalishaji wa mkaa mbadala kwa ajili ya ununuzi

156​

wa mashine zitakazotumika katika uzalishaji; kutoa ruzuku kwa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) ili waweze kununua na kufunga mashine mbili (2) za kuzalisha mkaa bora wa kupikia kutokana na makaa ya mawe, kutoa ruzuku kwa Jeshi la Magereza kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya nishati ya kupkia katika maeneo 211 pamoja na kumpata Mshauri Mwelekezi wa kufanya tathmini ya aina za nishati safi ya kupikia zilizopo Tanzania Bara. Tathmini hii itahusisha pia kuainisha teknolojia zilizopo, nishati safi zilizopo, watoa huduma (waendelezaji au wasambazaji) wa nishati safi ya kupikia waliopo, na kupendekeza aina ya mifumo ya ufadhili ili kufikisha nishati ya kupikia katika maeneo husika.

236. Mheshimiwa Spika, mpango wa kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia utahusisha kutoa elimu kupitia makongamano, semina na vyombo vya habari kuhusu madhara ya nishati chafu na manufaa ya matumizi ya nishati iliyo safi katika kipikia. Jumla ya Shilingi bilioni 24.5 ya fedha ndani zimetengwa.

l) Mpango wa Utoaji Ruzuku kwa Waendelezaji wa Miradi ya Nishati Jadidifu

Mheshimiwa Spika,
Mpango huu unahusisha kuchangia gharama za uendelezaji wa gridi ndogo (mini grids) kwa kutoa ruzuku ili

157​

kuzalisha umeme unaotokana na nishati jadidifu. Mpango unahusisha ujenzi wa mitambo ya kufua umeme yenye uwezo wa hadi kufikia Megawati 10 kutoka vyanzo vya maji, jua, upepo na tungamotaka. Jumla ya Shilingi bilioni 10 fedha za ndani zimetengwa.

m) Mradi wa Uwezeshaji Upanuzi wa

Miundombinu ya Msongo Mdogo (Distribution Network ) na Ujenzi wa “Interconnection Line” kwa Waendelezaji Wadogo

Mheshimiwa Spika,
mradi huu unahusisha kutoa ruzuku kwa waendelezaji wa miradi ya nishati vijijini ili waweze kujenga miundombinu ya kuunganisha umeme kutoka kwenye chanzo kwenda kwenye miundombinu ya TANESCO na kusambaza umeme katika vitongoji vinavyoendelezwa na Waendelezaji wa Miradi (Franchaise Area under Standardized Power Purchase Agreement). Kazi zilizopangwa kutekelezwa ni kuchambua maombi yatakayowasilishwa, kufanya due diligence na kusaini mikataba kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya mradi ambapo Shilingi bilioni 15 fedha za ndani zimetengwa.

158​

Ukuzaji na Uhamasishaji wa Ufanisi wa Matumizi Bora ya Nishati Pamoja na Matumizi ya Umeme katika Uzalishaji

Mheshimiwa Spika, kazi hii itahusisha kumpata mtoa huduma wa kukuza na kuhamasisha ufanisi wa matumizi bora ya nishati ikiwemo vifaa vinavyotumia umeme, tabia ya watumiaji kuhusu matumizi sahihi katika uzalishaji mali kwa kutumia umeme. Kazi zitakazotekelezwa ni pamoja na kumtafuta Mshauri Mwelekezi wa kuandaa Mkakati wa kuhamasisha Matumizi bora ya Umeme katika uzalishaji mali katika maeneo yaliyounganishwa na umeme vijijini. Hatua hii itawezesha kuongeza thamani katika maeneo yaliyopelekewa umeme kupitia miradi mbalimbali ya umeme. Jumla ya Shilingi bilioni 2 fedha za ndani na Shilingi bilioni 1.50 fedha kutoka Benki ya Dunia zimetengwa.

Tathmini ya utekelezaji wa Miradi ya Umeme Vijijini

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia REA inatarajia kufanya tathmini mbalimbali ili kuhuisha na kuandaa nyaraka za kitalaamu zitakazoongoza jitihada za uendelezaji na utekelezaji wa miradi ya kusambaza nishati vijijini. Kazi zitakazofanyika ni pamoja na kutafuta Washauri Elekezi kwa ajili ya kuandaa upembezi

159​

yakinifu wa kuibua aina za Nishati Jadidifu katika kutekeleza miradi ya umeme vijijini; kufanya tathmini ya vijiji na vitongoji vyote visivyo na umeme na vinavyohitaji ujazilizi katika maeneo yote ya visiwani; na Mshauri Mwelekezi wa kusimamia mradi wa ufungaji wa mifumo midogo ya umeme jua pamoja na gridi ndogo katika maeneo ya vijijini hususan visiwani. Jumla ya Shilingi bilioni 7.5 kutoka Benki ya Dunia zimetengwa.

C.1.6 UTEKELEZAJI WA MIKAKATI NA

MIPANGO MBALIMBALI YA UENDELEZAJI WA SEKTA NDOGO YA UMEME NA NISHATI JADIDIFU

Mheshimiwa Spika,
ili kuendeleza Sekta Ndogo ya Umeme na Nishati Jadidifu nchini, Serikali kupitia Wizara ya Nishati itakamilisha kuandaa mipango na mikakati mbalimbali ili ianze kutekelezwa. Kazi zitakazofanyika ni pamoja na kukamilisha uhuishaji wa Mpango Kabambe wa Kuendeleza Sekta Ndogo ya Umeme (Power System Master Plan 2020) pamoja na kuendelea kutekeleza Mpango Kabambe wa Kupeleka Nishati Vijijini (Rural Energy Master Plan) ambao umejikita katika kupeleka nishati ya umeme katika vitongoji na nishati safi ya kupikia katika maeneo ya vijijini.

160​

Mheshimiwa Spika, kazi nyingine zitakazotekelezwa ni kuendelea kusimamia na kuratibu utekelezaji wa Programu ya Nishati Safi ya Kupikia inayoloenga Kuwawezesha Wanawake Barani Afrika Kutumia Nishati Safi ya Kupikia (African Women Clean Cooking Support Programme – AWCCSP; Mkakati wa Taifa wa Nishati Safi ya Kupikia (2024-2034) pamoja na mradi wa Matumizi Bora ya Nishati na Mkakati wa Maboresho katika Sekta Ndogo ya Umeme (Electricity Supply Industry Reform Strategy and Roadmap – ESI-RSR). Pia Serikali kupitia Wizara ya Nishati itafanya tathmini ya vyanzo vyote vya nishati jadidifu vilivyopo nchini ili kutambua maeneo vilivyopo na uwezo, teknolojia inayohitajika kuviendeleza na kuandaa ramani kwa lengo la kuviendeleza.

C.2 SEKTA NDOGO YA MAFUTA NA GESI

Mheshimiwa Spika,
Serikali itaendelea kusimamia na kuendeleza Sekta Ndogo ya Mafuta na Gesi kwa kuchukua hatua mbalimbali, lengo likiwa ni kuhakikisha mchango wa sekta hii katika maendeleo ya Taifa letu unaimarika.

161​

C.2.1 MIRADI YA UTAFUTAJI WA MAFUTA NA GESI ASILIA KATIKA VITALU VYA KIMKAKATI

Kitalu cha Mnazi Bay Kaskazini

Mheshimiwa Spika, taarifa za kitaalamu kuhusu kitalu hiki zimeonesha uwepo wa mashapo yenye uwezekano wa kuwa na gesi asilia. Serikali kupitia TPDC imeshampata mbia wa kimkakati (Maurel & Prom (M&P)) ambaye ameonyesha nia ya kushirikiana katika shughuli za utafutaji na uendelezaji wa kitalu hiki. Kazi zilizopangwa kutekelezwa ni pamoja na uchorongaji wa visima vya utafiti pamoja na kukamilisha taratibu za upatikanaji wa leseni ya utafutaji wa mafuta na gesi asilia. Jumla ya Shilingi bilioni 2, fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya kazi hizi.

Kitalu cha Eyasi – Wembere

Mheshimiwa Spika, TPDC itaendelea na shughuli za utafiti wa awali wa mafuta na gesi asilia katika kitalu cha Eyasi – Wembere ambapo kazi zilizopangwa kutekelezwa ni pamoja na kuendelea na uchukuaji wa taarifa za mitetemo za mfumo wa 2D zenye urefu wa kilomita 1,100 ili kutambua maeneo ambayo visima vya utafutaji vitachorongwa, kutafuta mbia wa kimkakati wa kushirikiana naye katika uwekezaji pamoja na

162​

kukamilisha taratibu za upatikanaji wa leseni ya utafutaji wa mafuta na gesi. Jumla ya Shilingi bilioni 2 zimetengwa kwa ajili ya kazi hizi.

C.2.3 MRADI WA KUCHAKATA NA KUSINDIKA GESI ASILIA KUWA KIMIMINIKA (LIQUEFIED NATURAL GAS – LNG)

Mheshimiwa Spika,
lengo la mradi huu ni kuchakata na kusindika gesi asilia iliyogunduliwa katika Vitalu Na.1, 2 na 4 vilivyopo katika kina kirefu baharini ili kuwa kimiminika na kuweza kuuzwa katika soko la dunia. Mradi huu pia utasaidia kuongeza upatikanaji, uzalishaji na usambazaji wa gesi asilia kwa matumizi ya ndani ya nchi.

Mheshimiwa Spika, Serikali inatarajia kukamilisha majadiliano ya Mikataba ya mradi huu na Wawekezaji, ikiwemo Mkataba wa Nchi Hodhi (HGA) na Mkataba wa Ugawanaji Mapato (APSA); kuelimisha wananchi kuhusu umuhimu na manufaa ya mradi; kushiriki katika shughuli za ufuatiliaji na tathmini za mradi; na kushiriki katika utafiti na utoaji elimu ya upatikanaji wa huduma na bidhaa za ndani ikiwemo wataalam watakaohitajika katika mradi. Kazi nyingine zitakazotekelezwa ni kuwezesha uanzishwaji wa ofisi ya mradi na ujenzi wa shule ya msingi Likong’o

163​

mkoani. Jumla ya Shilingi bilioni 5 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa kazi hizo.

C.2.4 MIRADI YA UENDELEZAJI, UCHAKATAJI, USAFIRISHAJI NA USAMBAZAJI GESI ASILIA

Ujenzi wa Bomba la Kusafirisha Gesi Kutoka Ntorya katika Kitalu cha Ruvuma hadi Madimba

Mheshimiwa Spika,
mradi huu unahusisha kuendeleza gesi asilia iliyogunduliwa katika eneo la Ntorya katika kitalu cha Ruvuma. Kazi zilizopangwa kutekelezwa ni pamoja na kujenga bomba la kusafirisha gesi asilia kutoka kitalu cha Ruvuma (Ntorya) hadi Madimba lenye urefu wa kilomita 34.2 litakalokuwa na uwezo wa kubeba futi za ujazo milioni 140 kwa siku. Aidha, TPDC imeshapata Mshauri Mwelekezi kwa ajili ya usanifu wa kina na kihandisi. Jumla ya Shilingi bilioni 101.6 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya kuwezesha kazi hizo kutekelezwa.

Ujenzi wa Miundombinu ya Usambazaji wa Gesi Asilia katika Mkoa wa Dar es Salaam, Mtwara, Lindi na Pwani

Mheshimiwa Spika,
mradi huu unahusisha ujenzi wa miundombinu ya kusambaza gesi asilia katika Mikoa ya Dar es Salaam, Mtwara, Lindi na

164​

Pwani. Kazi zitakazotekelezwa ni pamoja na kufanya tathmini ya athari kwa mazingira na jamii, usanifu wa kihandisi pamoja na ujenzi wa miundombinu ya kusambaza gesi asilia kwenye viwanda vya Mkuranga pamoja na Kongani ya Viwanda ya Kwala Mkoani Pwani; kukamilisha ujenzi wa vituo vya CNG (Kituo Mama katika eneo la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Vituo vidogo vya Kairuki na Muhimbili) mkoani Dar es Salaam; na ununuzi wa vituo vitano (5) vya CNG vinavyohamishika (mobile CNG stations) vitakavyotoa huduma katika Jiji la Dar es Salaam. Aidha, miradi ya ujenzi wa vituo vya CNG inayotekelezwa na Sekta Binafsi itakayokamilika katika mwaka 2024/25 ni pamoja na kituo cha TAQA kitakachojengwa barabara ya Sam Nujoma; kituo cha Energo kinachoendela kujengwa katika eneo la Mikocheni mkabala na Coca Cola; kituo cha BQ Contractors kitakachojengwa Mbezi Beach karibu na Hospitali ya Masana; na vituo sita (6) vya PUMA vitakavyojengwa barabara ya Mandela, makutano ya barabara Mwenge, Mbezi Tanki Bovu, DART Mbagala, DART Ubungo na Tegeta.

Mheshimiwa Spika, TPDC pia itakamilisha awamu ya kwanza ya mradi wa usambazaji wa gesi asilia chini ya ufadhili wa REA ambapo nyumba

zitaunganishwa katika mikoa ya Lindi na Pwani; na kuanza awamu ya pili ya mradi huo kwa kuendelea kusambaza gesi asilia maeneo ya

165​

Mkuranga, mkoani Pwani. Jumla ya Shilingi bilioni 28.4 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya miradi hii ya usambazaji gesi katika mikoa minne.

C.2.5 MIRADI YA KUSAFIRISHA GESI ASILIA KWENDA NCHI JIRANI

Mradi wa Bomba la Kusafirisha Gesi Asilia kutoka Tanzania hadi Uganda

Mheshimiwa Spika, kazi zitakazofanyika ni pamoja na kukamilisha nyaraka muhimu za miradi ikiwemo Kanuni za Pamoja za Ununuzi (Joint Procurement Rules) na Hadidu za Rejea za kumpata Mshauri Mwelekezi wa kufanya upembuzi yakinifu wa mradi. Jumla ya Shilingi milioni 483.8 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya kufanikisha shughuli hiyo.

Mradi wa Kusafirisha Gesi Asilia Kutoka Dar es Salaam (Tanzania) hadi Mombasa (Kenya)

Mheshimiwa Spika, kazi zilizopangwa kutekelezwa ni pamoja na uandaaji wa nyaraka za mradi zikiwemo Bilateral Agreements, Joint Procurement Rules & Terms of Reference (ToR) na nyaraka za zabuni ya kumpata Mshauri Mwelekezi wa kufanya upembuzi yakinifu. Jumla ya Shilingi milioni

166​

502.2 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya kuwezesha kazi hizo kutekelezwa.

C.2.6 MIRADI YA KUSAFIRISHA NA KUHIFADHI MAFUTA

Mradi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi kutoka Hoima - Uganda hadi Tanga - Tanzania (East African Crude Oil Pipeline – EACOP)

Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa Mradi wa EACOP unaendelea ambapo kazi zitakazotekelezwa ni pamoja na kuendelea kupokea shehena za mabomba, kuendelea na ujenzi wa bomba la mafuta, ujenzi wa matenki ya kuhifadhia mafuta na jeti katika eneo la Chongoleani na kuendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu utekelezaji wa mradi na fursa zilizopo kwa maeneo yanayopitiwa na mradi na kuendelea kuchangia mtaji na kushirikiana na Wanahisa wengine kukamilisha taratibu za upatikanaji wa fedha za mkopo. Jumla ya Shilingi bilioni 50 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya kufanikisha shughuli hizo.

167​

Mradi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Safi kutoka Dar es Salaam - Tanzania hadi Ndola – Zambia

Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta safi kutoka Dar es Salaam hadi Zambia lenye urefu wa takribani kilomita 1,710 ambalo litatumia mkuza wa bomba la kusafirisha mafuta la TAZAMA. Wamiliki wa bomba tajwa ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Zambia. Kazi zilizopangwa kutekelezwa ni pamoja na kukamilisha idhini ya nyaraka muhimu za mradi na kupata Mshauri Mwelekezi wa kufanya uchambuzi wa kina wa mradi. Jumla ya Shilingi milioni 415.8 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya kutekeleza shughuli hizo.

Ujenzi wa Miundombinu ya Hifadhi ya Kimkakati ya Mafuta Pamoja na Miundombinu ya Kuwezesha Biashara ya Mafuta

Mheshimiwa Spika, uanzishaji wa Hifadhi ya Taifa ya Mafuta ya Kimkakati (SPR) unatekelezwa kwa kujenga maghala ya kuhifadhi mafuta (tank farms) katika maeneo ya kimkakati nchini ili kurahisisha usambazaji wa mafuta. Kazi zitakazotekelezwa ni pamoja na kumpata Mshauri Mwelekezi atakayeandaa Mpango wa Kina (Detailed

168​

Road Map) kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya SPR. Jumla ya Shilingi bilioni 3.4 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya kutekeleza shughuli hizo.

Ukarabati wa Tenki Namba 8

Mheshimiwa Spika, kazi zitakazotekelezwa ni kukamilisha tathmini ya athari kwa mazingira na jamii na usanifu wa tenki pamoja na kuanza kazi ya ukarabati wa tenki hilo kwa ajili ya hifadhi ya mafuta. Jumla ya Shilingi bilioni 14.4 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya kutekeleza shughuli hizo.

Ujenzi wa Maghala Sita (6) Eneo la Kigamboni

Mheshimiwa Spika, kazi ya ujenzi wa matenki sita (6) katika eneo la Kigamboni itafanyika kwa awamu ambapo awamu ya kwanza itaanza kwa ujenzi wa matenki matatu yenye uwezo wa kuhifadhi tani 81,000. Jumla ya Shilingi bilioni 49.8 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa maghala hayo.

C.2.7 MRADI WA USIMAMIZI WA RASILIMALI ZA NDANI NA UTAWALA WA RASILIMALI ZA ASILI TANZANIA

Mheshimiwa Spika,
kazi zitakazotekelezwa kupitia mradi huu ni pamoja na kuwezesha Duru ya Tano ya kunadi vitalu vilivyo wazi ili kuvutia

169​

uwekezaji katika utafutaji wa mafuta na gesi, kufadhili utafiti na maandalizi ya Mkakati wa Uendelezaji na Uhamasishaji wa matumizi ya gesi ya mitungi (Liquefied Petroleum Gas – LPG) na gesi iliyoshindiliwa (Compressed Natural Gas – CNG), kununua kituo kinachotembea cha kujazia gesi kwenye magari (Mobile CNG Station), kufadhili uanzishaji wa vituo vya kujenga uwezo kwa Wananchi chini ya Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) pamoja na kukamilisha awamu ya mwisho ya programu ya kujenga uwezo kwa Wataalam wa Wizara ya Nishati, PURA, TPDC na Watumiaji wa Mfumo wa Uondoshaji Shehena Mipakani.

C.2.8 MAJUKUMU YATAKAYOTEKELEZWA NA KAMPUNI TANZU ZA TPDC (TANOIL & GASCO)

TANOIL Investments Limited (TANOIL)

Mheshimiwa Spika, TPDC kupitia Kampuni yake tanzu ya TANOIL itaendela kushiriki katika biashara ya mafuta kama kampuni ya kununua na kuuza mafuta (Oil Marketing Company
OMC). Kampuni ya TANOIL imepanga kutumia Shilingi bilioni 240.95 katika biashara hiyo na itaendelea kukamilisha ukarabati wa vituo vitatu

(3) vya Musoma, Tarime (Mara) na Segera (Tanga) pamoja na kujenga kituo kipya kimoja (1)

170​

Makuyuni (Arusha) kupitia Kampuni mama (TPDC).

Gas Company (GASCO)

Mheshimiwa Spika, TPDC kupitia kampuni Tanzu ya GASCO itaendelea kuendesha miundombinu ya Taifa ya Gesi Asilia nchini. TPDC kupitia GASCO imepanga kutumia Shilingi bilioni 76.41 kwa ajili ya kulipia gharama za uendeshaji na usimamizi wa miundombinu ya kuchakata gesi asilia iliyoko Songo Songo na Madimba, bomba la gesi asilia kutoka Mtwara na Lindi hadi Dar es Salaam na mtandao wa mabomba ya usambazaji gesi asilia iliyopo Mtwara, Lindi, Pwani na Dar es Salaam.

C.2.9 UDHIBITI WA MASUALA YA MKONDO WA

JUU WA PETROLI KUPITIA PURA

Mheshimiwa Spika,
Serikali kupitia PURA inatarajia kutekeleza Duru ya Tano (5) ya kunadi vitalu vya utafutaji wa mafuta na gesi asilia. Zoezi hili lina lengo la kutangaza kwa wawekezaji vitalu vilivyo wazi vinavyopendekezwa katika eneo la bahari na nchi kavu. Kazi zilizopangwa kutekelezwa ni pamoja na; kuandaa nyaraka za zabuni zitakazoongoza mnada wa vitalu, kufanya maonesho ya kitaalamu kuhusu vivutio vya vitalu na kuzindua Duru ya Tano (5) ya kunadi vitalu. Zoezi la kunadi vitalu linatarajiwa kuzinduliwa

171​

mwishoni mwa mwaka 2024 baada ya kukamilika kwa maandalizi yote yanayoendelea. Jumla ya Shilingi bilioni 2 zimetengwa.

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia PURA itaendelea kusimamia shughuli za ukarabati wa visima katika vitalu vya uzalishaji wa gesi asilia pamoja na shughuli za uendelezaji katika Kitalu cha Ruvuma, kufanya mapitio ya kanuni mbalimbali, kuendelea kusimamia, kufanya ukaguzi na kuhakikisha ushiriki wa Watanzania katika Vitalu vyote vya utafutaji na uzalishaji wa gesi asilia nchini pamoja na kusimamia shughuli za awali zinazoendelea katika vitalu Namba 1, 2 & 4 vitakavyohusika katika mradi wa LNG. Jumla ya Shilingi bilioni 1.77 fedha za ndani zimetengwa ili kutekeleza kazi hizi.

C.2.10 UDHIBITI WA MASUALA YA NISHATI KUPITIA EWURA

Mheshimiwa Spika,
EWURA itaendelea kusimamia udhibiti wa huduma za nishati nchini kwa kuwasimamia watoa huduma kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na taratibu zilizopo ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma iliyo bora na uhakika. Pia, ili kufikisha huduma karibu na wananchi EWURA imetenga kiasi cha Shilingi bilioni 1.7 kwa ajili ya kuendelea na taratibu za ujenzi wa Ofisi

172​

za Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Kaskazini na Kati.

C.2.11 KUIMARISHA UTENDAJI KAZI NA UTOAJI HUDUMA

Mheshimiwa Spika,
Wizara itaendelea kuchukua hatua madhubuti za kuimarisha taasisi zilizo chini yake ili ziweze kujiendesha kwa tija na ufanisi na kutoa huduma bora kwa wananchi na wadau. Aidha, Wizara inatarajia kuajiri watumishi wapya 56 na kuwahamishia Wizarani watumishi 76 ili kukabiliana na upungufu wa watumishi uliopo. Vilevile, Wizara itaendelea kuwajengea uwezo watumishi kwa kutoa mafunzo ya muda mrefu na mfupi kwa watumishi 4,219.

D. USHIRIKIANO

WA

KIKANDA

NA

KIMATAIFA

Mheshimiwa Spika, katika utekelezaji wa majukumu yake, Wizara ya Nishati inashirikiana na Washirika mbalimbali wa Maendeleo, Jumuiya za Kikanda, nchi wahisani na wadau wengine. Kwa niaba ya Serikali, napenda kuwashukuru Washirika wa Maendeleo, Jumuiya na nchi wahisani ambao wameendelea kushiriki katika kufanikisha utekelezaji wa majukumu ya Wizara na maendeleo ya Sekta ya Nishati kwa ujumla. Napenda kutambua mchango wa Benki ya

173​

Maendeleo Afrika (AfDB); Benki ya Dunia (WB); Arab Bank for Economic Development in Africa (BADEA); Mfuko wa Uendelezaji wa Economic Development Cooperation Fund (EDCF - Korea); Jotoardhi (Geothermal Risk Mitigation Facility - GRMF) pamoja na Taasisi na Mashirika ya JICA (Japan), KfW (Germany), AFD (Ufaransa); Shirika la Fedha Duniani (IMF); Sida (Sweden), NORAD (Norway); Umoja wa Ulaya (EU), Shirika la Mitaji ya Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNCDF), Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Shirika la Maendeleo la Canada (CIDA) na USAID (Marekani); OPEC Fund for International Development; Abu - Dhabi Fund for Development (ADFD); na Saudi Fund for Developmnet (SFD).

Mheshimiwa Spika, nitumie nafasi hii pia kutoa shukrani kwa Serikali za Afrika Kusini, Algeria, Burundi, Canada, China, DRC Congo, Ethiopia, Falme za Kiarabu, Iceland, India, Japan, Kenya, Korea ya Kusini, Malawi, Marekani, Misri, Morocco, Msumbiji, Namibia, Norway, Rwanda, Sweden, Ufaransa, Uganda, Uingereza, Ujerumani, Zambia, na nchi nyingine kwa ushirikiano wao katika kuendeleza Sekta ya Nishati. Nazishukuru pia Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Umoja wa Afrika (AU) kwa ushirikiano katika masuala ya kikanda yanayohusu Sekta ya Nishati.

174​

E. HITIMISHO

Mheshimiwa Spika,
kwa kutambua umuhimu wa nishati katika kuchochea na kuharakisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa Taifa letu, katika mwaka 2024/25 Wizara ya Nishati itaendelea kuchukua hatua madhubuti za kusimamia, kuimarisha na kuendeleza Sekta ya Nishati, kwa lengo la kuhakikisha sekta hii inachangia ipasavyo katika maendeleo ya Taifa letu na watu wake kama inavyotarajiwa.

Mheshimiwa Spika, Wizara itaendelea kuimarisha upatikanaji wa nishati safi ya kupikia mijini na vijijini ili kulinda afya za wananchi na mazingira. Aidha, Wizara itaendelea kuipatia suluhu ya kudumu changamoto ya upatikanaji wa umeme wa uhakika nchini, kuimarisha usambazaji wa nishati hiyo pamoja na kuimarisha uzalishaji wa gesi asilia unaoendana na mahitaji, kwa kuzingatia kiwango cha ugunduzi wa nishati hiyo hadi sasa nchini na hatua za utafutaji zinazoendelea kuchukuliwa. Wizara pia itaendelea kuelekeza nguvu katika kuimarisha utoaji wa huduma mbalimbali zinazotolewa na Taasisi zake.

269. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa

hoja kwamba Bunge lako Tukufu sasa liidhinishe Bajeti ya jumla ya Shilingi Trilioni Moja, Bilioni

Mia Nane Themanini na Tatu, Milioni Mia Saba

175​

Hamsini na Tisa, Mia Nne Hamsini na Tano Elfu (Shilingi 1,883,759,455,000) kwa ajili ya matumizi ya Wizara ya Nishati na Taasisi zake. Mchanganuo wa fedha hizo ni kama ifuatavyo:

Shilingi Trilioni Moja, Bilioni Mia Saba Tisini na Nne, Milioni Mia Nane Sitini na Sita, Mia Nane Thelathini na Mbili Elfu (Shilingi 1,794,866,832,000) sawa na asilimia 95.28 ya Bajeti yote ya Wizara ni kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo. Kati ya fedha hizo, Shilingi Trilioni Moja, Bilioni Mia

Tano Thelathini na Sita na Milioni Ishirini, Mia Mbili Sabini na Nne Elfu (Shilingi 1,536,020,274,000) ni fedha za ndani na
Shilingi Bilioni Mia Mbili Hamsini na Nane, Milioni Mia Nane Arobaini na Sita, Mia Tano Hamsini na Nane Elfu (Shilingi 258,846,558,000) ni fedha za nje; na

Shilingi Bilioni Themanini na Nane, Milioni Mia Nane Tisini na Mbili, Mia Sita Ishirini na Tatu Elfu (Shilingi 88,892,623,000)
sawa na asilimia 4.72 ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida. Kati ya fedha hizo Shilingi Bilioni

Sitini na Tisa, Milioni Mia Tano Ishirini na Nne, Mia Mbili na Moja Elfu (Shilingi 69,524,201,000) ni kwa ajili ya Matumizi Mengineyo (OC) na Shilingi Bilioni Kumi na

Tisa, Milioni Mia Tatu Sitini na Nane, Mia

176​

Nne Ishirini na Mbili Elfu (Shilingi 19,368,422,000) ni kwa ajili ya Mishahara (PE) ya Watumishi wa Wizara na Taasisi zilizo chini yake.

Mheshimiwa Spika, naomba tena nitoe shukrani zangu za dhati kwako na kwa Waheshimiwa
Wabunge wote kwa kunisikiliza. Hotuba hii pia inapatikana katika Tovuti ya Wizara kwa anuani ya www.nishati.go.tz. Vilevile, Hotuba hii ina vielelezo mbalimbali ambavyo vimeambatishwa kwa ajili ya ufafanuzi wa masuala muhimu yanayohusu Sekta ya Nishati.

Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.

177​

VIAMBATISHO

Kiambatisho Na. 1:
Uwezo wa Mitambo ya Kuzalisha Umeme

Iliyounganishwa katika Gridi ya Taifa
hadi mwezi Machi, 2024
A. Mitambo ya Maji
MW
1.JNHPP
235.00​
2.Kidatu
204.00​
3.Kihansi
180.00​
4.Mtera
80.00​
5.New Pangani Falls
68.00​
6.Rusumo
26.67​
7.Hale
21.00​
8.Nyumba ya Mungu
8.00​
9.Uwemba
0.84​
10Mwenga
4.00​
11Yovi
0.95​
12Matembwe
0.59​
13Darakuta
0.32​
14Luponde
0.90​
15Andoya
1.00​
16Tulila
5.00​
Jumla ya Uwezo wa Mitambo ya Maji
836.27
Mitambo ya Gesi Asilia
1.SONGAS
189.00​
2.Ubungo I
102.00​
3.Tegeta
45.00​
4.Ubungo II
129.00​
5.Ubungo III
92.50​
6.Kinyerezi I
335.00​
7.Kinyerezi II
248.22​
8.Mtwara I
30.60​
9.Mtwara 2 (TM16)
20.00​
10Somanga
7.50​
Jumla ya Uwezo wa Mitambo ya
Gesi Asilia
1,198.8

Mitambo ya Mafuta

178​

A.Mitambo ya Maji
MW
1.Zuzu
7.44​
2.Nyakato Plant
63.00​
3.Biharamulo
2.72​
4.Songea
5.74​
5.Liwale
0.85​
6.Tunduru
1.05​
7.Ludewa
1.27​
8.Mbinga
1.00​
9.Loliondo
1.00​
10Ngara
1.25​
11Kasulu
4.55​
12Kibondo
2.50​
Jumla ya Uwezo wa Mitambo ya
Mafuta
92.37
Tungamotaka
1.TAWNWAT
1.50​
2.TPC
9.00​
Jumla ya Tungamotaka
10.50
JUMLA YA GRIDI YA TAIFA
2,138.0

Chanzo: TANESCO

179​

Kiambatisho Na.2: Hatua Iliyofikiwa katika Utekelezaji wa Miradi Mbalimbali ya Gridi Imara

NA
. MAELEZO YA MRADI WA GRIDI IMARA

Ujenzi wa njia kuu ya kusafirisha umeme ya msongo wa Kilovolti 132 yenye urefu wa kilomita 7 kutoka Ilala hadi Kurasini chini ya ardhi. Mradi huu umeanza utekelezaji Januari, 2023 na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa Mei, 2024 na umefikia asilimia 82.
Mradi wa upanuzi wa kituo cha kupoza umeme cha Dege Kigamboni kwa kuongeza transfoma moja yenye uwezo wa MVA 120 ya msongo wa kilovolti 132/33. Mradi huu umeanza utekelezaji Machi, 2023 na unatarajia kukamilika Januari, 2025 na umefikia asilimia 42.

Ujenzi wa njia kuu ya kusambaza umeme ya msongo wa Kilovoti 33 kutoka Nyakanazi hadi Kakonko yenye urefu wa kilomita 56 na kutoka Nyakanazi hadi Lusahunga (Ngara) yenye urefu wa kilomita 10. Mradi huu ulianza utekelezaji Agosti, 2022 na umekamilika Januari, 2023.
Kuimarisha gridi ya taifa kwa kuongeza uwezo au ukubwa wa nyaya za umeme mkubwa wa kilovolti 132 wenye urefu wa kilomita 19.7 kutoka Gongolamboto hadi Mbagala na kuongeza uwezo wa transfoma zenye uwezo wa 100MVA za msongo wa kilovolt 132/33 katika kituo cha kupoza umeme cha Gongolamboto na Mbagala. Mradi huu ulianza utekelezaji Julai, 2022 na unatarajia kukamilika Septemba, 2025 na utekelezaji wake umefikia asilimia 51.03.
Ujenzi wa njia kuu ya kusafirisha umeme ya msongo wa Kilovoti 132 kutoka Tabora hadi Katavi yenye urefu wa kilomita 383 na vituo vya kupooza umeme vyenye uwezo wa 2x15MVA Ipole na Inyonga na 1x35MVA Mpanda vya msongo wa Kilovolti 132/33. Mradi huu ulianza utekelezaji Septemba, 2021 na unatarajiwa kukamilika Juni, 2024 na mradi huu umefikia asilimia 47 kwa lot 1 na asilimia 87 kwa lot 2.

Ujenzi wa kituo cha kupooza umeme chenye transfoma mbili zenye uwezo wa 60MVA cha msongo wa Kilovoti 132/33 katika eneo la Mkata Tanga na ujenzi wa njia ya kusambaza umeme ya msongo wa Kilovoti 33 yenye urefu

180​

NA. MAELEZO YA MRADI WA GRIDI IMARA

wa kilomita 45 kutoka Mkata hadi Kwamsisi. Mradi huu ulianza utekelezaji Machi, 2023 na unatarajiwa kukamilika Januari, 2025 na utekelezaji umefikia asilimia 10.

Ujenzi wa njia kuu ya kusafirisha umeme ya msongo wa Kilovoti 220 yenye urefu wa kilomita 5.02 eneo la viwandani Zegereni na ujenzi wa kituo cha kupooza umeme cha msongo wa Kilovoti 220/33 chenye uwezo wa 2x120MVA maeneo ya viwanda Zegereni. Mradi huu ulianza utekelezaji Desemba, 2023 na unatarajiwa kukamilika Juni, 2025. Utekelezaji wa mradi huu umefikia asilimia 1.5.

Ujenzi wa Switching Station yenye msongo wa Kilovoti 33 katika eneo la Msigani Dar es Salaam. Mradi huu ulianza utekelezaji Machi, 2023 na unatarajiwa kukamilika mwezi Mei 2024. Mradi huu umekamilika kwa asilimia 87.

Ujenzi wa njia kuu ya kusafirisha umeme ya msongo wa Kilovoti 220 na urefu wa kilomita 110 kutoka Shinyanga hadi Simiyu, pamoja na ujenzi wa kituo cha kupoza umeme kitakachokuwa na transfoma mbili zenye uwezo wa 90MVA kila moja, ya msongo wa Kilovoti 220/33 katika eneo la Imalilo, Simiyu. Mradi huu ulianza utekelezaji Septemba, 2023 na unatarajia kukamilika Julai, 2025 na umekamilika kwa asilimia 32 kwa Lot 1(njia ya kusafirisha umeme) na asilimia 5 kwa Loti 2 (kituo cha kupoza umeme).

Ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa Kilovoti 132 yenye urefu wa kilomita 37 kutoka kituo cha kupoza umeme cha Kasiga hadi Lushoto, ujenzi wa kituo kipya cha kupoza umeme chenye uwezo wa 2x30MVA msongo wa kilovolti 132/33 eneo la Lushoto na upanuzi wa kituo cha kupooza umeme cha Kasiga. Mradi huu ulianza utekelezaji Septemba, 2023 na unatarajia kukamilika Machi, 2025 na umekamilika kwa asilimia 13.

Ujenzi wa njia kuu ya kusafirisha umeme ya msongo wa Kilovoti 132 yenye urefu wa kilomita 143 kutoka Mkata hadi Kilindi na ujenzi wa kituo cha kupoza umeme cha Kilindi cha msongo wa Kilovoti 132/33 chenye uwezo wa 2x60MVA katika eneo la Kilindi. Ujenzi wa mradi huu ulianza Machi,

181​

NA. MAELEZO YA MRADI WA GRIDI IMARA

2023 na unatarajiwa kukamilika Septemba, 2024. Kwa sasa utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 30 kwa Lot 1 (njia ya kusafirisha umeme) na asilimia 40 kwa Loti 2(kituo cha kupoza umeme).

Ujenzi wa njia kuu ya kusafirisha umeme ya msongo wa Kilovoti 132 yenye urefu wa kilomita 395 kutoka Tabora hadi Kigoma kupitia Urambo na vituo vya kupooza umeme vya Urambo (35MVA) na Nguruka (15MVA), msongo wa kilovolti 132/33. Mradi huu ulianza utekelezaji Agosti, 2022 na unatarajia kukamilia Juni, 2024. Mradi umekamilika kwa asilimia 21 kwa Lot 1 (njia ya kusafirisha umeme) na asilimia 84 kwa lot 2 (vituo cha kupoza umeme).
Kubadilisha nyaya za umeme za msongo wa Kilovoti 132 kwenye njia ya umeme kutoka Ubungo kupitia Chalinze yenye urefu wa kilomita 97 na kilomita 172 kutoka Chalinze hadi Hale ili kuongeza uwezo wa kusafirisha umeme na kupunguza upotevu wa umeme katika Gridi ya Taifa. Mradi huu ulianza utekelezaji Julai, 2022 na unatarajiwa kukamilika Aprili, 2024. Mradi huu umekamilika kwa asilimia 35.82.

Ujenzi wa njia ya kusambaza umeme wa msongo wa kilovoti 33 wenye urefu wa kilomita 208 kutoka kituo cha kupoozea umeme cha Lemugur mkoani Arusha. Mradi huu ulianza utekelezaji Machi 2023 na unatarajiwa kukamilika Oktoba, 2024 na umekamilika kwa asilimia 59.7.
Ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa Kilovoti 33 kutoka kituo cha kupoza umeme cha Zuzu hadi Mbande yenye urefu wa kilomita 92 na kufunga regulating transfoma zenye uwezo wa 20MVA na 15MVA za kuongeza uwezo katika maeneo ya Mbande mkoani Dodoma na Misenyi mkoani Kagera. Mradi huu ulianza utekelezaji Machi, 2023 na unatarajiwa kunamilika April, 2024. Mradi huu umeshakamilika kwa asilimia 40

Uwekaji wa regulating transfoma mbili zenye uwezo wa 10MVA za msongo wa Kilovoti 33 ili kuongeza nguvu ya umeme katika eneo la Songwe Mkwajuni na Mbangala mkoani Songwe. Mradi huu ulianza utekelezaji Machi, 2023 na unarajiwa kukamilika April 2024 na umeshakamilika kwa

182​

NA. MAELEZO YA MRADI WA GRIDI IMARA

asilimia 80.

Ujenzi wa njia ya kusambaza umeme ya msongo wa kilovoti 33 yenye urefu wa Kilomita 60 kutoka kituo cha kupoza umeme cha Nyamongo hadi Mugumu Serengeti pamoja na ujenzi wa kituo cha kubadilishia umeme (switching station) cha msongo wa kati wa Kilovoti 33 eneo ka Mugumu. Mradi huu umeanza utekelezaji Juni, 2023 na unatarajiwa kukamilika Mei 2024, ujenzi wa njia ya kusambaza umeme umekamilika kwa asilimia 29.45 na ujenzi wa kituo cha kubadilishia umeme umekamilika kwa asilimia 7.

Ujenzi wa njia kuu ya kusafirisha umeme ya msongo wa Kilovoti 220 yenye urefu wa kilomita 47 kutoka Pugu hadi Dundani. Mradi huu ulianza utekelezaji Februari, 2024 na unatarajiwa kukamilika Agosti 2025. Mradi huu umekamilika kwa asilimia 2.7.

Ujenzi wa kituo cha kupoozea umeme cha msongo wa Kilovoti 220/33 chenye uwezo wa 2X120MVA katika eneo la Dundani wilaya ya Mkuranga. Mradi huu ulianza utekelezaji Agosti, 2023 na unatarajiwa kukamilika Februari, 2025. Mradi huu umekamilika kwa asilimia 05.
Ujenzi wa njia ya kusambaza umeme ya msongo wa Kilovoti 33 yenye urefu wa kilomita 16 utakaounganisha vituo vya kupooza umeme vya Nyakanazi na Bulyankulu. Mradi huu ulianza kutekelezwa Juni, 2023 na umekamilika Septemba, 2023

Kuboresha njia kuu ya kusafirisha umeme ya msongo wa Kilovoti 220 yenye urefu wa kilomita 16.5 kutoka Kinyerezi hadi Ilala kupitia Ubungo na Mabibo pamoja na kituo cha kupooza umeme cha Mabibo chenye uwezo wa Kilovoti 220/132/33, 2×200MVA, na kilovoti 132/33, 2×90MVA, na uboreshaji wa vituo vya Ilala na Ubungo kwa kuweka transfoma moja yenye uwezo wa 300MVA, 220/132/33kV eneo la Ubungo. Mradi huu ulianza utekelezaji Septemba 2023 na unatarajiwa kukamilika Februari, 2025. Mradi huu upo katika hatua za utekelezaji ambapo njia ya kusafirisha

183​

NA. MAELEZO YA MRADI WA GRIDI IMARA

umeme (Lot 1) imefikia asilimia 8.26 na Kituo cha kupoza umeme (Lot 2) kimefikia asilimia 10.

Kuiongezea uwezo njia kuu ya kusafirisha umeme kutoka Kilovoti 66 hadi Kilovoti 132 inayoanzia Bunda kupitia Kibara hadi Ukerewe yenye urefu wa kilomita 98.6, upanuzi wa kituo cha kupoza umeme cha Bunda pamoja na ujenzi wa kituo kipya cha kupooza umeme cha Ukerewe chenye uwezo wa 2x45MVA, na msongo wa kilovolti 132/33. Mradi huu ulianza utekelezaji Septemba, 2023 na unatarajiwa kukamilika Februari, 2025 na umeshakamilika kwa asilimia 10 kwa lot 1 (njia ya kusafirisha umeme) na asilimia 17 kwa lot 2 (kituo cha kupooza umeme).

Ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme yenye msongo wa kilovoti 132 na urefu wa kilomita 61.31 kutoka Kiyungi hadi Rombo na ujenzi wa kituo cha kupoza umeme cha Rombo chenye uwezo wa 2x45MVA, na msongo wa kilovolti 132/66/33. Mradi huu unatarajiwa kukamilika Machi, 2025 na umeshakamilika kwa asilimia 2.

Ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa Kilovoti 220 yenye urefu wa kilomita 18.43 kutoka Ubungo kupitia Kunduchi hadi Ununio na kujenga kituo cha kupooza umeme cha msongo wa kilovoti 220/132/33 katika eneo la Ununio chenye uwezo wa 2x120MVA. Mradi huu ulianza utekelezaji Februari, 2023 na unatarajiwa kukamilika Machi, 2025. Ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme (Lot 1) umefikia asilimia 17 na Kituo cha kupoza umeme (Lot 2) kimefikia asilimia 2.
Ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa Kilovoti 220 yenye urefu wa kilomita 214.5 kutoka Songea hadi Tunduru na kituo cha kupooza umeme chenye uwezo wa 2x60 MVA na msongo wa Kilovoti 220/33 katika eneo ya Tunduru. Mradi huu ulianza utekelezaji Machi 2023 na unatarajiwa kukamilika Septemba, 2024 na umefikia asilimia 51.

Ujenzi wa njia kuu ya kusafirisha umeme ya msongo wa Kilovoti 220 yenye urefu wa kilomita 179 kutoka Tunduru hadi Masasi na ujenzi wa kituo cha kupooza umeme chenye uwezo wa 2x60MVA na msongo wa Kilovoti 220/33

184​

NA. MAELEZO YA MRADI WA GRIDI IMARA

katika eneo la Masasi. Mradi huu ulianza utekelezaji Juni, 2023 na unatarajiwa kukamilika Desemba, 2024 na umeshakamilika kwa asilimia 5.

Ujenzi wa kituo cha kupooza umeme cha Ibadakuli mkoani Shinyanga cha msongo wa Kilovoti 400/220kV chenye uwezo wa 2x315MVA. Mradi huu ulianza utekelezaji mwezi Julai, 2023 na unatarajiwa kukamilika Novemba, 2025. Mradi upo katika hatua za awali za utekelezaji.

Ujenzi wa njia kuu ya kusafirisha umeme ya msongo wa Kilovoti 220 yenye urefu wa kilomita 128 kutoka Masasi hadi Mahumbika na ujenzi wa kituo cha kupooza umeme chenye uwezo wa 2x60MVA na msongo wa Kilovoti 220/33 katika eneo la Mahumbika. Mradi huu upo katika hatua za awali ambapo mkataba unatarajiwa kusainiwa Aprili, 2024.

Chanzo: TANESCO

185​

Kiambatisho Na.3: Mitambo iliyofanyiwa Matengenezo Makubwa na Madogo

Mitambo ya Mafuta na Gesi (Thermal Power Plants)

Na.
Jina laNamba yaMatengezo Yaliyofanyika
KituoMtambo
1.​
Kinyerezi IIGT23Matengenezo
makubwa​
ya​
ukaguzi hop parts inspection
2.​
Kinyerezi IGT 5,6 naMatengenezo
madogo​
ya​
7masaa 8,000 ya ukaguzi wa
jumla katika mtambo
EG2, EG5,Matengenezo
madogo​
ya​
EG7 namasaa 12,000
3.​
Ubungo IEG12
EG6 &Matengenezo ya masaa 2,000
EG9Level
D
4.​
Ubungo IIGT2Matengenezoya
yamekamilika
5.​
Ubungo IIILM6000Upgradesyamtambo
ili​
kuongeza uwezo wake kutoka
26MW – 32MW
6.​
TegetaEG5Matengenezo makubwa kutokana
na mtambo kuvuja oil
8Kubadilisha cylinder heads
6Kutatuachangamoto
ya​
mtambokutofikia
frequency
7.​
Mtwarainayotakiwa
11Matengenezo
makubwa​
na​
bado yanaendelea
1Kubadilisha cylinder heads
8.​
Somanga2Matengenezo
upande​
wa​
beringi bado yanaendelea
9.​
Nyakato3Matengenezo
madogo​
ya​
pampu
za mafuta katika​
mtambo

186​

Mitambo ya Mafuta na Gesi (Thermal Power Plants)

Mitambo ya Nguvu za Maji (Hydro Power Plants)

Na.
Jina laNamba yaMatengenezo Yaliyofanyika
KituoMtambo
1.​
Kidatu
1,2,3&4​
Kubadilisha pampu za kutoa
maji yanayovuja
(drainage
pumps)
1​
Matengenezoyamfumo
wa​
kufua umeme (replacement of
slip ring and DC field winding
connecting rod)
2​
Kubadilisha vipooza hewa vya
jenereta (replacement of generator air
coolers)
1 & 2​
Kubadilishakabari
kwenye​
milango ya tubini (replacement of
shear pins on guide vanes)
3 & 4​
i. Kubadilishaberingi
za​
tubini (replacement of turbine
brearings)
ii. Kubadilishavidhibiti
maji​
yanayovujakupitia
kwenye​
tubini (replacement of shaft
seals)
2.​
Kihansi
1​
i. Matengenezoya
kikata​
umeme cha mtambo (generator
circuit breaker)
ii. Matengenezo kwenye gavana ya
tubini(calibration
of​
deflectors and replacement
of needle bolts)

187​

Mitambo ya Mafuta na Gesi (Thermal Power Plants) iii. Ukarabati wa waya wa

mfumo wa kufua umeme

(excitation system)

2​
Matengenezo
kwenye gavana​
ya tubini(replacement
of​
needle bolts)
3​
i. Kubadilishapampu
za​
kutoa
maji​
yanayovuja​
(drainage pumps)
ii. Matengenezo ya gavana ya
tubini (replacement of turbine
governor needle bolts)
iii. Matengenezo ya beringi ya​
chini ya jenereta (adjustment of
the lowerguide
bearing
pumping ring)
3.​
Mtera
2​
i. Kutenganisha
jenerata​
pamoja
na​
kukarabati​
sehemukuuza
jenereta​
(generaorstator
winding
and rotor repair)
ii. Kubadilisha kikata umeme​
cha jenereta namba 1 na​
mfumowamsongo
wa​
kilovolti220
(replacement
of generator circuit breaker
and buscoupler)
4.​
New
1​
i. Kubadilishaberingi
ya​
Panganitubini(replacement
of
Fallsturbine bearing)
ii. Matengenezo ya gavana ya​
tubini (overhaul of turbine
governor servomotor)

188​

Mitambo ya Mafuta na Gesi (Thermal Power Plants) iii. Matengenezo mfumo wa

uendedshaji, (maintenance

on main contro system
)

2 i. Matengenezo kwenye gavana ya tubini (repalcement of turbine governor accumulator)

ii. Mfumo wa uendeshaji

(maintenance on main

contro system)

Chanzo: TANESCO

189​

Kiambatisho Na. 4: Mtambo wa Uchorongaji Ukiwa Umesimikwa kwa Ajili ya Uhakiki wa Jotoardhi katika Eneo la Mradi wa Jotoardhi wa Ngozi

190​

Kiambatisho Na. 5:

Wazalishaji Wadogo wa Umeme Waliosajiliwa na Kuuza Umeme (SPPs)

Wazalishaji Wadogo (SPPs) Wanaozalisha Umeme

Wazalishaji Wadogo Waliopo katika Hatua ya Ujenzi wa Miundombinu

Na.Jina la MradiEneo la Mradi
Chanzo
Uwezo
1.​
Pinyinyi Hydropower PlantArusha
Maji​
1.90​
2.​
Diwale projectMvumero
Maji​
5.00​
3.​
SSI projectsShinyanga
Maji​
10.00​
4.​
MagutaIringa
Maji​
1.20​
5.​
Lwega projectKatavi
Maji​
3.00​
6.​
Nakatuta projectSongea
Maji​
5.00​
7.​
Nkwillo ProjectRukwa
Maji​
0.95​
8.​
Igola projectNjombe
Maji​
2.00​
9.​
Suma projectTukuyu
Maji​
4.00​
10.​
LuswiswiSongwe
Maji​
4.70​
11.​
IFUMBO HPPMorogoro
Maji​
1.00​
12.​
Mabuki SolarMwanza
Jua​
5.00​
13.​
Mdunku (Kiteto) SolarKiteto
Jua​
6.00​
14.​
Nyasoro (Rorya) SolarRorya
Jua​
8.00​
15.​
Bugando Solar PVBugando
Jua​
5.00​
16.​
Isangawana SolarMbeya
Jua​
8.00​
17.​
Gua SolarMbeya
Jua​
5.00​
18.​
Illundo ProjectMbeya
Maji​
0.56​
19.​
Lumuma ProjectDodoma
Jua​
2.00​
20.​
Mkulazi Holdings limitedMorogoro
Tungamotaka​
8.00​
Jumla
86.31

Chanzo: TANESCO

191

Kiambatisho Na 6: Taasisi Zilizounganishiwa Umeme hadi Kufikia Machi 2024

Na.
Mradi
Taasisi Zilizounganishiwa Umeme
Elimu
Biashara
Pampu
Afya
Nyumba
za maji
za Ibada
1.​
Miradi ya Awali
1,099​
2,648​
64​
412​
813​
Kusambaza
Umeme
Vijijini​
Awamuya
Pili​
2.​
(REA II)
1,947​
4,943​
513​
1,069​
212​
Kusambaza
Umeme
Vijijini​
Awamuya
Tatu​
Mzunguko
wa​
3.​
Kwanza
4,233​
8,113​
1,879​
1,816​
2,706​
Kusambaza
Umeme
kwenye​
njiakuu
ya​
Msongo
wa​
Kilovoti
400​
(BTIP-VEI)
Iringa,​
Dodoma, Singida,
Tabora
na​
4.​
Shinyanga
125​
323​
11​
513​
97​
Ujazilizi
Awamu​
ya I (Densification
5.​
I)
226​
3,570​
928​
507​
1,279​
Kusambaza
Umeme
katika​
Mkuza wa Njia ya
Umeme
Kilovoti​
220
(Makambako-
6.​
Songea)
99​
134​
5​
79​
73​
Makontena
ya​
7.​
Umeme Jua
6​
36​
0​
6​
27​
Kusambaza
Umeme
Pembezoni
mwa​
Miji/MajijiI
(Peri
8.​
Urban I)
249​
428​
36​
64​
312​
Ujazilizi
Awamu​
ya II
Fungu A​
9.​
(Densification IIA)
311​
536​
62​
213​
425​

192​

Na.
Mradi
Taasisi Zilizounganishiwa Umeme
Elimu
Biashara
Pampu
Afya
Nyumba
Kusambaza
za maji
za Ibada
Umeme
Pembezoni
mwa​
Miji/Majiji II (Peri
10.​
Urban II)
258​
212​
22​
97​
66​
Kituo cha kupoza
Umeme Ifakara -
(usambazaji
umeme
katika​
wilaya ya Kilombero
11.​
na Ulanga)
16​
43​
9​
16​
39​
Kusambaza
Umeme
katika​
Vituo vya afya na
pampu za maji ili
kukabilianana
magonjwa
ambukizi ikiwemo
12.​
UVIKO19
0​
0​
310​
58​
0​
Kusambaza
Umeme
Vijijini​
Awamu ya
Tatu​
13.​
Mzunguko wa Pili
4,336​
8,308​
1,934​
1,865​
2,773​

Chanzo: REA

193​

Kiambatiosho Na.7: Miundombinu ya Kusambaza Gesi Asilia Nchini

MkoaNa.Jina
Umbali (Km)
1.Dangote Awamu ya Kwanza
2.70​
2.Dangote Awamu ya Pili
0.10​
3.Majumbani Awamu ya
16.60​
MtwaraKwanza
4.Majumbani Awamu ya Pili
8.60​
Jumla Ndogo
28.00
1.Trunk line
7.10​
2.Goodwill
1.65​
Pwani3.Lodhia
3.70​
4.Knauf
0.20​
5.Raddy
0.75​
Jumla Ndogo
13.40
1.Majumbani Aamu ya
18.30​
LindiKwanza
Jumla Ndogo
18.30
1.Ubungo - Mikocheni
7.20​
2.NNGI - Ubungo Mikocheni
1.42​
3.Mitambo ya kuzalisha
6.50​
umeme
4.Coca Cola
0.15​
Dar es5.Majumbani UDSM
10.52​
6.Majumbani - Mikocheni
4.30​
Salaam
7.Majumbani - Sinza
7.50​
8.Majumbani - Kurasini
4.50​
9.Viwandani (TPDC & PAET)
53.00​
Jumla Ndogo
95.09
JUMLA KUU
154.79

Chanzo: TPDC

194​

Kiambatiosho Na.8: Mikataba ya Uzalishaji na Ugawanaji wa Mapato (PSA) kwenye Gesi Asilia

Na.​
MKATABAHALI YA
LESENI
1.​
Block 1Awamu ya
(Baharini)pili ya
Leseni ya
utafutaji
2.​
Block 2Awamu ya
(Baharini)pili ya
Leseni ya
utafutaji
3.​
Block 4Awamu ya
(Baharini)pili ya
Leseni ya
utafutaji
4.​
NyuniAwamu ya
Areakwanza ya
(NchiLeseni ya
kavu)utafutaji
5.​
RuvumaAwamu ya
(Nchipili ya
kavu)Leseni ya
utafutaji
6.​
RuvuAwamu ya
Blockpili ya
(NchiLeseni ya
kavu)utafutaji
7.​
Kilosa –Awamu ya
Kilomberokwanza ya
(NchiLeseni ya
kavu)utafutaji
8.​
Mnazi BayLeseni ya
(NchiUendelezaji
kavu)

MWENDESHAJISHUGHULI
NA WABIAZINAZOENDELEA
Shell (Operator),Majadiliano
kati​
Ophir Energy naya Serikali
na​
PavilionMakampuni
yaliyogundua
gesi​
Equinorkuhusu
Tanzania
AS​
utekelezaji
wa​
(Operator)
na​
mradi
wa​
Exxon MobilKuchakata
na​
Shell (Operator),Kusindika
Gesi​
Ophir Energy naAsilia
kuwa​
PavillionKimiminika
yanaendelea.
NdovuUtafutaji
Resources
Ltd​
(Operator)
na​
Bounty Oil & Gas
ARA
Petroleum​
Utafutaji
Tanzania
Ltd​
(Operator) na Ndovu
Resources Ltd
DodsalUtafutaji
Hydrocarbon and
Power (Tanzania) Pvt
Limited (Operator)
TPDCUtafutaji
M&PUzalishaji
Exploration
and​
Production
TZ​
Ltd
(Operator)​

na TPDC

195​

Na.MKATABAHALI YAMWENDESHAJISHUGHULI
LESENINA WABIAZINAZOENDELEA
9.SongoLeseni yaPanAfricanUzalishaji
songoUendelezajiEnergy Tanzania
(NchiLtd (Operator)
kavu)
10.Nyuni-Leseni yaNdovuUzalishaji
KiliwaniUendelezajiResources
Ltd​
North(Operator), RAK
(NchiGas, Solo
na​
kavu)BountyOil
&​
Gas
11.TangaAwamu yaOctanct
Energy​
Utafutaji
Blockpili yaTanzania
(NchiLeseni yaLimited
kavu)utafutaji

Chanzo: PURA

196​

Kiambatisho Na. 9: Ramani ya Shughuli za Utafutataji, Uendelezaji na Uzalishaji wa Mafuta na Gesi Asilia Hadi Machi,2024

Chanzo: PURA

197​

Kiambatisho Na.10: Mikataba ya Kuuziana Umeme kati ya TANESCO na Wazalishaji Wadogo Iliyoridhiwa na EWURA Hadi Machi, 2023 katika Mwaka 2023/24

Na.Jina la MzalishajiEneo la MradiChanzo
Uwezo
(MW)
1.ZBS
Investments​
Nyasoro,Wilaya
ya​
Jua
8.0​
LimitedRorya, Mkoa wa Mara
2.ZBS
Investments​
Mdunku,Wilaya
ya​
Jua
6.0​
LimitedKiteto, Mkoa wa Arusha
3.ConviviumMabukiWilaya
ya​
Jua
5.0​
Investments TanzaniaMisungwi,Mkoa
wa​
LimitedMwanza
4.Ninety-Two LimitedPinyinyi,Wilaya
ya​
Maji
2.9​
Ngorongoro, Mkoa
wa​
Arusha
5.SSI Energy TanzaniaKahama,Wilaya
ya​
10​
LimitedKahama,Mkoa
wa​
Shinyanga
6.Africa
Power​
Kikuletwa II, Wilaya yaMaji
8.0​
Investment LimitedHai,Mkoa
wa​
Shinyanga
7.Lilondi
Hydropower​
Lingatunda, Wilaya
ya​
Maji
4.5​
LimitedMadaba,Mkoa
wa​
Ruvuma
8.LUCSEC
Company​
Lunyamacho, Wilaya ya
3.0​
LimitedLudewa,Mkoa
wa​
Njombe
9.Maximum
Power​
Paramawe,Wilaya
ya​
Jua
5.0​
Tanzania LimitedNkasi, Mkoa wa Rukwa
10.BXC Tanzania LimitedKayenze,Wilaya
ya​
Jua
5.0​
Ushetu

198​

Na.Jina la MzalishajiEneo la MradiChanzoUwezo
(MW)
11.BXC Tanzania LimitedLyambamgongo, WilayaJua
5.0​
ya Bukombe, Mkoa wa
Geita
12.FGS
Eco-energy​
Nkungwe,Mkoa
wa​
Maji
6.0​
LimitedKigoma
13.FGS
Eco-energy​
Kamwana,Wilaya
ya​
Maji
5.0​
LimitedMuleba,Mkoa
wa​
Kagera
14.CESNE
Energy (T)​
Mabeshi, Wilaya Uyui,Jua
5.8​
LimitedMkoa wa Tabora
Jumla
79.2

Chanzo: (EWURA)

199​

Kiambatisho Na.11: Vituo vya Kupoza Umeme Vitakavyojengwa katika Kila Wilaya Nchini

A.
Awamu ya Kwanza

Eneo la

Kituo
Na. Mkoa cha
Kupooza

Umeme

Morogoro Ulanga

Morogoro Mvomero

3 Mbeya Chunya

Songwe Songwe

Dodoma Kongwa

SingidaManyoni

Mtwara Masasi

Njia ya Kusafirisha Umeme

220kV Ifakara - Ulanga

220kV Msamvu -

Mvomero
220kV

Mwakibete -
Chunya
220kV Chunya -

Songwe
220kV Ihumwa

SGR Ext. -
Kongwa

220kV Manyoni

underline Pie

S/S
220kV Tunduru - Masasi

Urefu wa
Uwezo
Njia ya
wa Kituo
Kusafirisha
cha
Umeme
Kupooza
(Km)
Umeme
95​
2x45MVA​
54​
2x30MVA​
70​
2x60MVA​
83​
2x60MVA​

2x30MVA 2x30MVA​

174 2x30MVA

Gharama
Jumla (TZS)
(USD)
27,800,000.00​
64,913,000,000.00​
16,580,000.00​
38,714,300,000.00​
27,570,000.00​
64,375,950,000.00​
27,740,000.00​
64,772,900,000.00​
30,130,000.00​
70,353,550,000.00​
11,450,000.00​
26,735,750,000.00​
45,500,000.00​
106,242,500,000.00​

200

Eneo la

Kituo
Na. Mkoa cha
Kupooza

Umeme

8 Manyara Simanjiro

9 Kagera Muleba

Ruvuma Mbinga

TaboraIgunga

12​
GeitaBukombe
13​
ArushaLongido
14​
SingidaManyoni
15​
DodomaChamwino

Njia ya Kusafirisha Umeme

220kV

Lemuguru -
Simanjiro
220kV Chato -

Muleba
220kV Songea -

Mbinga
220kV Igunga

underline Pie

S/S
220kV Buzwagi -

Ushirombo
220kV Njiro -

Longido

220kV Manyoni -

Mitundu
220kV Zuzu -

Msalato -
Ihumwa

Urefu wa
Uwezo
Njia ya
wa Kituo
Kusafirisha
cha
Umeme
Kupooza
(Km)
Umeme
105​
2x30MVA​
150​
2x30MVA​

2x60MVA 2x30MVA​

120​
2x30MVA
56​
2x30MVA

2x30MVA

492x100MVA

Gharama
Jumla (TZS)
(USD)
29,870,000.00​
69,746,450,000.00​
45,600,000.00​
106,476,000,000.00​
28,100,000.00​
65,613,500,000.00​
12,460,000.00​
29,094,100,000.00​
35,510,000.00​
82,915,850,000.00​
25,350,000.00​
59,192,250,000.00​
34,500,000.00​
80,557,500,000.00​
34,900,000.00​
81,491,500,000.00​

Jumla-Awamu ya Kwanza

433,060,000.00
1,011,195,100,000.00

201​

B. Awamu ya Pili

Eneo la
Kituo
Na.
Mkoa
cha
Kupooza
Umeme
1​
DodomaDodoma
2​
GeitaChato

Dodoma Mpwapwa
Njombe Njombe
Njombe Ludewa
Manyara Hanang
Morogoro Gairo

8​
PwaniKisarawe
9​
PwaniKibiti

Njia ya Kusafirisha Umeme

220kV Msalato Underline Pie S/S 220kV Bwanga underline Pie S/s 220kV Kongwa - Mpwapwa 220kV Njombe Underline Pie S/s 220kV Madaba - Ludewa

220kV Underline Pie S/S Katesh 220kV Kongwa - Gairo

220kV Pugu SGR Extension 220kV Mkuranga - Kibiti

Urefu wa
Uwezo
wa
Njia ya
Kituo
Kusafirisha
Gharama (USD)
Jumla (TZS)
cha
Umeme
Kupooza
(Km)
Umeme
0​
2x50MVA​
17,800,000.00​
41,563,000,000.00​
0​
2x30MVA​
12,460,000.00​
29,094,100,000.00​
90​
2x45MVA​
27,780,000.00​
64,866,300,000.00​
0​
2x45MVA​
12,460,000.00​
29,094,100,000.00​
55​
2x30MVA​
28,400,000.00​
66,314,000,000.00​
0​
2x30MVA​
12,460,000.00​
29,094,100,000.00​
56​
2x45MVA​
22,712,000.00​
53,032,520,000.00​
0​
2x90MVA​
10,700,000.00​
24,984,500,000.00​
66.7​
2x90MVA​
25,140,000.00​
58,701,900,000.00​

202

Na. Mkoa

Mbeya

Kigoma
Kigoma

Iringa
Singida

Arusha

Eneo la
Urefu wa
Uwezo
wa
Kituo
Njia ya
Njia ya
Kituo
cha
Kusafirisha
Kusafirisha
cha
Kupooza
Umeme
Umeme
Kupooza
Umeme
(Km)
Umeme
220kV
MbaraliMakambako -
66​
2x30MVA​
Mbarali
Buhigwe220kV Kigoma -
60​
2x30MVA​
Buhigwe
Kasulu220kV Buhigwe -
60​
2x30MVA​
Kasulu
Kilolo220kVTagamenda
79​
2x30MVA​
- Kilolo
Iramba220kV Misigiri
0​
2x30MVA​
Underline Pie S/S
Ngorongoro220kV Longido -
149​
2x30MVA​
Ngorongoro

Jumla-Awamu ya Pili

Gharama (USD)
Jumla (TZS)
23,710,000.00​
55,362,850,000.00​
19,800,000.00​
46,233,000,000.00​
20,570,000.00​
48,030,950,000.00​
28,400,000.00​
66,314,000,000.00​
19,300,000.00​
45,065,500,000.00​
28,500,000.00​
66,547,500,000.00​

310,192,000.00 682,735,320,000.00

203​

C. Awamu ya Tatu

Eneo la
Na.
Mkoa
Kituo cha
Kupooza
Umeme
1​
RukwaNkasi
2​
KataviMlele
3​
LindiRuangwa
4​
TangaMkinga
5​
KigomaKibondo
6​
MaraSerengeti

Morogoro Mvuha

8 Lindi Nachingwea

Njia ya Kusafirisha Umeme

220kV

Sumbawanga -

Namanyere
220kV

Sumbawanga -

Kibaoni
132kV

Mahumbika -

Luangwa
132kV Tanga -

Mkinga
220kV

Nyakanazi -

Kibondo
132kV

Nyamongo -

Serengeti
132kV Msamvu

Mvuha 220kV Masasi - Nachingwea

Urefu wa
Uwezo
wa Kituo
Njia ya
cha
Gharama (USD)
Jumla (TZS)
Kusafirisha
Kupooza
Umeme (Km)
Umeme
120​
2x30MVA​
38,000,000.00​
88,730,000,000.00​
150​
2x30MVA​
28,500,000.00​
66,547,500,000.00​
97​
2x30MVA​
27,110,000.00​
63,301,850,000.00​
0​
2x30MVA​
16,850,000.00​
39,344,750,000.00​
134​
2x30MVA​
37,508,000.00​
87,581,180,000.00​
49.5​
2x30MVA​
15,245,000.00​
35,597,075,000.00​
75​
2x15MVA​
21,400,000.00​
49,969,000,000.00​
104​
2x45MVA​
39,430,000.00​
92,069,050,000.00​

204

Eneo la
Na.Mkoa
Kituo cha
Kupooza
Umeme
9​
MtwaraNewala
10​
NjombeMakete
11​
RuvumaNamtumbo
12​
SimiyuMaswa
13​
MbeyaKyela
14​
MbeyaRungwe
15​
DodomaChemba

Jumla-Awamu ya Tatu

Njia ya Kusafirisha Umeme

220kV Masasi -

Newala
220kV Kyela -

Makete
220kV

Underline Pie

Namtumbo s/s

220kV

Underline Pie

Maswa s/s
220kV

Mwakibete -

Kyela
220kV

Underline
Tukuyu pie S/s

220kV Zuzu -

Chemba

Urefu wa Njia ya Kusafirisha Umeme (Km)

60

54

0

0

105

0

98​

Uwezo
wa Kituo
cha
Gharama (USD)
Jumla (TZS)
Kupooza
Umeme
2x30MVA​
22,400,000.00​
52,304,000,000.00​
2x30MVA​
21,400,000.00​
49,969,000,000.00​
2x30MVA​
20,360,000.00​
47,540,600,000.00​
2x30MVA​
12,050,000.00​
28,136,750,000.00​
2x30MVA​
31,460,000.00​
73,459,100,000.00​
2x30MVA​
9,570,000.00​
22,345,950,000.00​
2x30MVA​
29,200,000.00​
68,182,000,000.00​
370,483,000.00
776,347,805,000.00

D. Awamu ya Nne

205​

Eneo la
Kituo
Na.
Mkoa
cha
Kupooza
Umeme
1​
PwaniRufiji
2​
KilimanjaroMwanga
3​
KigomaKakonko
4​
SongweMbozi
5​
KageraKyerwa
6​
KageraKaragwe
7​
MorogoroMalinyi
8​
MorogoroKilosa

Njia ya Kusafirisha Umeme

220kV Kibiti -

Ikwilili
132kV

Underline
Mwanga pie

S/s
220kV

Underline -
Kakonko Pie

S/s
220kV

Mwakibete -

Mbozi
132kV Kyaka-

Kyerwa
220kV Kyaka -

Karagwe
220kV Ulanga -

Malinyi
220kV

Mpwapwa -
Kilosa

Urefu wa
Uwezo
Njia ya
wa Kituo
Kusafirisha
cha
Gharama (USD)
Jumla (TZS)
Umeme
Kupooza
(Km)
Umeme
47​
2x30MVA
20,100,000.00​
46,933,500,000.00​
2x15MVA
11,170,000.00​
26,081,950,000.00​
2x30MVA
11,170,000.00​
26,081,950,000.00​
62​
2x30MVA
20,400,000.00​
47,634,000,000.00​
40​
2x30MVA
14,230,000.00​
33,227,050,000.00​
30​
2x30MVA
16,580,000.00​
38,714,300,000.00​
75​
2x30MVA
29,800,000.00​
69,583,000,000.00​
58​
2x30MVA
23,170,000.00​
54,101,950,000.00​

206

Eneo la

Kituo
Na. Mkoa cha
Kupooza

Umeme

Urefu wa
Uwezo
Njia ya
Njia ya
wa Kituo
Kusafirisha
Kusafirisha
cha
Umeme
Umeme
Kupooza
(Km)
Umeme

Gharama (USD) Jumla (TZS)

9​
GeitaMbogwe
10​
ManyaraKiteto
11​
SimiyuMeatu
12​
PwaniMafia
13​
SongweIleje
14​
RukwaKalambo
15​
ArushaMonduli

Jumla-Awamu ya Nne

220kV

Bulyanhulu -

Mbongwe
220kV Kongwa

-Kiteto
220kV Kishapu

Meatu 220kV Kibiti - Mafia 220kV Kyela - lleje
220kV Sumbawanga - kalambo 220kV Lemuguru - Monduli

39​
2x30MVA
78.2​
2x30MVA
66​
2x30MVA
86.6​
2x30MVA

2x30MVA

2x30MVA

2x30MVA

16,840,000.0039,321,400,000.00
37,600,000.0087,796,000,000.00
25,000,000.0058,375,000,000.00
81,300,000.00189,835,500,000.00
19,200,000.0044,832,000,000.00
27,920,000.0065,193,200,000.00
19,100,000.0044,598,500,000.00
373,580,000.00872,309,300,000.00

207​

E. Awamu ya Tano
Eneo la
a.
Mkoa
Kituo cha
Kupooza
Umeme
1​
GeitaNyang’wale
2​
LindiLiwale
3​
LindiKilwa
4​
MaraButiama
5​
MaraRorya
6​
MtwaraTandahimba
7​
MtwaraNanyumbu

Njia ya Kusafirisha Umeme

220kV Mabuki -

Nyang’wale
220kV

Nachingwea -

Liwale
220kV

Mahumbika -

Nangu- rukuru

132kV Bunda -

Butiama
132kV Musoma

- Rorya
220kV Newala -

Tandahimba

220kV

Underline
Nanyumbu Pie

S/s

Urefu wa
Uwezo
Njia ya
wa Kituo
Kusafiri-
cha
Gharama (USD)
Jumla (TZS)
sha
Kupooza
Umeme
Umeme
(Km)
68​
2x30MVA​
24,510,000.00​
57,230,850,000.00​
115.1​
2x30MVA​
32,070,000.00​
74,883,450,000.00​
160​
2x30MVA​
46,200,000.00​
107,877,000,000.00​
77​
2x15MVA​
28,500,000.00​
66,547,500,000.00​
48​
2x15MVA​
17,910,000.00​
41,819,850,000.00​
33​
2x30MVA​
17,180,000.00​
40,115,300,000.00​
0​
2x30MVA​
12,870,000.00​
30,051,450,000.00​

208​

Urefu wa
Eneo la
Njia ya
Njia ya
Kituo cha
Kusafiri-
a.Mkoa
Kusafirisha
Kupooza
sha
Umeme
Umeme
Umeme
132kV
(Km)
8​
MwanzaMaguUnderline Pie
0​
Magu s/s
9​
SingidaMkalama220kV Hanang-
82​
Mkalama
220kV
10​
SingidaIkungiUnderline S/S
0​
Ikungi
11​
SingidaManyoni220kV Mitundu
130​
- Rungwa
12​
TaboraUyui220kV Iramba -
100​
Uyui
13​
KilimanjaroSiha132kV Kiyungi -
52.2​
Siha
220kV
14​
SimiyuMaswaUnderline
0​
Maswa Pie S/S
15​
RukwaNkasi220kV Kalambo
106​
- Nkasi

Jumla-Awamu ya Tano

Jumla Kuu- Awamu Zote Tano

Uwezo
wa Kituo
cha
Gharama (USD)
Jumla (TZS)
Kupooza
Umeme
2x15MVA​
11,550,000.00​
26,969,250,000.00​
2x30MVA​
35,450,000.00​
82,775,750,000.00​
2x30MVA​
11,550,000.00​
26,969,250,000.00​
2x30MVA​
34,550,000.00​
80,674,250,000.00​
2x30MVA​
31,460,000.00​
73,459,100,000.00​
2x15MVA​
19,500,000.00​
45,532,500,000.00​
2x30MVA​
12,050,000.00​
28,136,750,000.00​
2x30MVA​
30,340,000.00​
70,843,900,000.00​
365,690,000.00
853,886,150,000.00
1,853,005,000.00
4,196,473,675,000.00

209

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mha. Felchesmi J. Mramba, akipokea mtambo wa kuzalisha umeme wa Megawati 20 kwa kutumia gesi asilia wa aina ya TM16 uliofungwa katika Kijiji cha Hiari, Wilaya ya Mtwara Vijijini. Mtambo huo umeimarisha upatikanaji wa umeme katika mikoa ya Mtwara na Lindi.

210​
2023/2024 tulikuwa na wizara ya NISHATI au NISHATI NA MADINI?
 
hongera kwa Mh waziri, ingawa sijaona mapendekezo ya kushusha bei za nishati hasa umeme na gesi.

Tumeambiwa tunaumeme wa ziada hadi mitambo imezimwa. Tushushe bei kuchochea matumizi makubwa ya hiyo nishati huku tukiendelea kulinda mazingira.

Pamoja nafasi ya uwaziri ni ya uongozi zaidi lakini natoa wito tupate mawaziri competent katka wizara husika, watu wenye ujuzi na masuala wanayoyaongoza.

Maana hata huko tuna watu wenye uwezo wa kiuongozi. Italeta tija zaidi hasa anapopatikana mtu mwaminifu na mzalendo.
 
Hizo hela watapeleka kununua ndege wapate sehemu ya kupigia badala ya kuelekeza kwenye kugharamia bima za wanyonge pamoja na elimu
Mkuu, huwa kunakuwa na makadirio tu ya bajeti peke yake?
  • Hakuna(ga) ripoti ya matumizi halisi ya mwaka mzima?
  • CAG huwa asemi labda eneo fulani lilitengewa bajeti hii, mpaka mwisho wa mwaka wa fedha wamepokea kiasi hiki na kiasi hiki ndicho walichofanyia uchawa kama zawadi ya kusifu kizimkazi?

Muhimu sana kujua hilo, haiwezekani OC ikaizidi wage bill ya wizara nzima kwa takribani mara 4!
- Ukiuliza kwa utendaji gani walio nao hao watumishi, hupewi jibu la maana zaidi ya watu kuanza kukuambia...itakuwa ni takwa la kisheria, wafanyakazi wasiminywe kwenye haki zao!

Unaingia kazini saa 3asbh, saa 6mchana mpaka saa 8.30mchana uko lunch, saa 9.30 muda wa kazi umeisha! Saa 10 unabeba file moja toka ofisi A kwenda B ndani ya jengo moja, mara siku 15, OC hilo.
  • Kuna wale wengine, mshahara 900k, posho ya chakula 950k...sasa unajiuliza, kama ulidhani 900k inamtosha, vipi ufikiri chakula cha kwake pekee kinagharimu zaidi ya mshahara wake? 900k pengine analisha familia ya 4 pipo!
  • Wekeni kima cha chini tzs 1,500,000 ili tujue moja!
 
Hatari sn mkuu
 
Ni jambo jema, hizo fedha zilizopunguzwa zipelekwe NHIF kulipia bima za watanzania wanyonge zisiwe posho za majangili ya nchi.
Inaweza kuwa vizuri kuzipeleka huko , lakini tatizo la Wizara ya Afya Kwa sasa ni uongozi wake , haujui au hawana Nia ya kutenda KAZI Yao Kwa ufanisi , hivyo hizo hela zinaweza zisi tatue tatizo, ndio maana NHIF na MSD kuna ufisudi na hakuna Mipango yenye ufanisi
 
Mbona sioni uwekezaji umeme wa jua, big opportunity kumaliza matatizo ya umeme nchini, tunahitaji visionary leaders kuona hili inaonekana
 
Back
Top Bottom