42774277
JF-Expert Member
- Aug 24, 2018
- 6,835
- 8,914
Kwanza unapaswa kujua kwamba ndege kama hiyo iliyopata ajali (ATR42 500) ina uzito wa tani 11.5 bila abiria wala mizigo.Kufuatia ajali iliyotokea huko Bukoba, na kuangamiza ndugu zetu wapatao 19 na kujeruhi wengine wengi, yapo maswali ya kujiuliza.
Ndege ilipoibuliwa kutoka majini tuliona uharibifu mkubwa kwa ndege yenyewe na hata kutia mashaka kiasi cha kujiuliza hivi kweli hata kama ni ajali ndio ndege iharibike kiasi hiki?
Swali la kujiuliza hapa ni kuwa, material gani zinatumika kutengeneza ndege? Au wanatumia material "fake" kama za mchina? Baada ya kutolewa majini tumeiona ndege imejikunja kama karatasi, kutoka umbile la kunyooka mpaka umbile la 'el' (L)!
Kama ingetumika material imara kutengenezea ndege hiyo, huenda kusingekuwa na uharibifu tuliouona na hivyo kupunguza maafa yaliyotokea.
Timu ya uchunguzi isiishie kuangalia tu chanzo cha ajali, bali na matengenezo ya ndege yenyewe. Ikibainika material fake ilitumika kutengeneza ndege, basi kampuni iliyotengeneza ndege nayo iwajibike.
Ikiwa full loaded inakuwa na tani almost 18.
Hapo wakiweka material magumu uzito unaweza fika hata tani 30 au zaidi ikiwa full loaded.