Kwanini ndege hutengenezwa kwa kutumia "material" mepesi?

stars

JF-Expert Member
Sep 10, 2020
819
1,111
Kufuatia ajali iliyotokea huko Bukoba, na kuangamiza ndugu zetu wapatao 19 na kujeruhi wengine wengi, yapo maswali ya kujiuliza.

Ndege ilipoibuliwa kutoka majini tuliona uharibifu mkubwa kwa ndege yenyewe na hata kutia mashaka kiasi cha kujiuliza hivi kweli hata kama ni ajali ndio ndege iharibike kiasi hiki?

Swali la kujiuliza hapa ni kuwa, material gani zinatumika kutengeneza ndege? Au wanatumia material "fake" kama za mchina? Baada ya kutolewa majini tumeiona ndege imejikunja kama karatasi, kutoka umbile la kunyooka mpaka umbile la 'el' (L)!

Kama ingetumika material imara kutengenezea ndege hiyo, huenda kusingekuwa na uharibifu tuliouona na hivyo kupunguza maafa yaliyotokea.

Timu ya uchunguzi isiishie kuangalia tu chanzo cha ajali, bali na matengenezo ya ndege yenyewe. Ikibainika material fake ilitumika kutengeneza ndege, basi kampuni iliyotengeneza ndege nayo iwajibike.
 
Ndege mara nyingi haitakiwi kuanguka na ikitokea ni Uzembe wa Binadamu kwa asilimia kubwa.

Ujenzi wake ni kama KIFUA cha Binadamu ambapo Mbavu zipo kulinda Kamoyo kasidhurike pamoja na mapafu bila kuhitaika Minyama kibao kulinda sehemu hizo. Nadhani sababu ni ileile kwamba tuwe wepesi.

Ndege hutumia MAFUTa mengi mno wakati wa kuruka na ikifika kwa mfano 8km au 10km juu, inatulia huko na kuanza kuteleza tu. Huko kuna upepo mdogo na hivyo Wind Resistance ni ndogo pia GRAVITATION inapungua. Kwa wanaotoka Ulaya kwenda USA au USA to EUROPE, wakati mwingine wanautumia upepo unaopuliza kwenye ndege kwa nyuma na na kwenda haraka zaidi pia kutumia mafuta kidogo.

Kwa saabu hiyo, siku zote wanatafuta Material Magumu na mepesi zaidi ili ile NGOZI ya ndege na MBAVU za Ndege ziwe imara na nyepesi zaidi.

1668561515003.png
 
Ndege mara nyingi haitakiwi kuanguka na ikitokea ni Uzembe wa Binadamu kwa asilimia kubwa...
Impact gani iliyotokea pale wakati ndege ilizama tu majini na inasemekana hakukuwa na mwamba (jiwe) wowote. Ina maana impact ya maji tu ndio isababishe uharibifu ule?

Wavuvi wanasema eneo ilipoingia ndege pana mchanga mtupu, kwahiyo impact yake baada ya kukita kwenye mchanga haikuwa kubwa kihivyo.
 
Pamoja na kuwa unasema ni material mepesi(nadhani ukimaanisha laini)

Nikukumbushe airbus a380 ina TANI 560...
Ndiyo, mepesi nilimaanisha laini, yasiyohimili mikiki mikiki. Nadhani wangetumia material isiyoharibika kiwepesi. Nahisi hata ndege za kivita hawatengenezi kwa material mepesi!
 
Impact gani iliyotokea pale wakati ndege ilizama tu majini na inasemekana hakukuwa na mwamba (jiwe) wowote. Ina maana impact ya maji tu ndio isababishe uharibifu ule? Wavuvi wansema eneo ilipoingia ndege pana mchanga mtupu, kwahiyo impact yake baada ya kukita kwenye mchanga haikuwa kubwa kihivyo.
Labda nikufafanulie kidogo tu uelewe. Ule mgongano wa ndege na maji ndio impact inayozungumziwa hapa ndugu. Sio kuzama. Kumbuka maji sio hewa mzee.

Ukitaka kuelewa maana ya mchangiaji hapo juu, nenda ziwani au baharini. Panda kwenye kingo yenye mwinuko (yaweza kuwa kwenye jiwe au ukingo lakini kuwe na mwinuko ambao unaweka kuingia majini kwa kuruka) kisha jitupe kwenda kwenye maji ukiwa umetanguliza tumbo.

Halafu rudi hapa utuambie ulijisikiaje tumbo lilipotua kwenye maji kwa kasi ya mruko wako.
 
Kufuatia ajali iliyotokea huko Bukoba, na kuangamiza ndugu zetu wapatao 19 na kujeruhi wengine wengi, yapo maswali ya kujiuliza.

Ndege ilipoibuliwa kutoka majini tuliona uharibifu mkubwa kwa ndege yenyewe na hata kutia mashaka kiasi cha kujiuliza hivi kweli hata kama ni ajali ndio ndege iharibike kiasi hiki...

Mkuu kwa wastani ndege hugusa chini ikitua salama salimini ikiwa katika speed kati ya 210km/h - 260km/h. Fikiria gari katika mwendo huo. Fikiria mazingira ya uwanja inapotua.

Sasa kumbuka ndege hii haikutua uwanjani bali Ili crash land ziwani ambako terrain ni aijuaye mola.

Kwa hakika hata ingekuwa imetengenezwa kwa chuma cha pua ingepasuka tu wala kusingekuwa na ujanja.
 
Ndege ikitengenezwa kwa zege si itakuwa MNARA!!
Kufuatia ajali iliyotokea huko Bukoba, na kuangamiza ndugu zetu wapatao 19 na kujeruhi wengine wengi, yapo maswali ya kujiuliza.

Ndege ilipoibuliwa kutoka majini tuliona uharibifu mkubwa kwa ndege yenyewe na hata kutia mashaka kiasi cha kujiuliza hivi kweli hata kama ni ajali ndio ndege iharibike kiasi hiki?

Swali la kujiuliza hapa ni kuwa, material gani zinatumika kutengeneza ndege? Au wanatumia material "fake" kama za mchina? Baada ya kutolewa majini tumeiona ndege imejikunja kama karatasi, kutoka umbile la kunyooka mpaka umbile la 'el' (L)!

Kama ingetumika material imara kutengenezea ndege hiyo, huenda kusingekuwa na uharibifu tuliouona na hivyo kupunguza maafa yaliyotokea.

Timu ya uchunguzi isiishie kuangalia tu chanzo cha ajali, bali na matengenezo ya ndege yenyewe. Ikibainika material fake ilitumika kutengeneza ndege, basi kampuni iliyotengeneza ndege nayo iwajibike.
 
Impact gani iliyotokea pale wakati ndege ilizama tu majini na inasemekana hakukuwa na mwamba (jiwe) wowote. Ina maana impact ya maji tu ndio isababishe uharibifu ule? Wavuvi wanasema eneo ilipoingia ndege pana mchanga mtupu, kwahiyo impact yake baada ya kukita kwenye mchanga haikuwa kubwa kihivyo.

Ukitaka kujua kuwa maji yana impact panda sehem ya juu sana then dive hovyo kwenye maji uone yanavyo kuchapa kutokana na uzito wako na gravity. Uki-dive vizuri hutoweza ona impact yake kubwa. Na ile ndege it is said kuwa ali land vibaya if not nose dive. Ndomana damage ilkuwa kubwa na maji kuingia ndan ya ndege haraka na wengi kupoteza maisha.

Muwe mmafanya na research na pia kufikili tu kwa akili ya haraka hata kama hutokuwa right lakini utasogea kidogo kwa ukweli. Size ya ndege pia inaweza changia. Ile pale ndege i think kama angetuisha kwenye maji kama unavyo tuisha kwenye runway damage isingekuwa vile.

Mfano ile ndege iliyotua Hudson River ili tua kama anatua runway, so ili elea kwa muda kidogo before sinking, na pia na hisi ukubwa wa ndege naamanisha surface ya ndege ilkuwa kubwa so ili sababisha ku elea na pia waka deploy ile milango ya exit kwa kutumia slides za boya. So mambo ni mengi ya ku consider.
Correct me if I’m wrong!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom