Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,329
33,138
MAFUTA-YALIYO-ANDIKWA-VEGETABLE-OIL-HAYAKULINDI-NA-MAGONYWA-YA-MOYO-.jpg

Mafuta mazuri ya kupikia yenye kukulinda na magonjwa ya moyo, hayana cholestrol ndani yake yenye jina la kibiashara “Vegetable oil” kitalamu huitwa “Seed oils” au Polyunsaturated Fatty Acid oils (PUF Oils). Je Kuna ukweli kuhusu hilo?

Kwamba
Mafuta yenye jina la kibiashara “Vegetable oil” Je:
1. Yanakukinga usipate magonjwa ya moyo unapopikia?
2. Je yanapochorwa mboga za majani kama spinach,Kabeji je humaanisha yametokana na mboga hizo au yanaenda kutumika kupikia mboga hizo?

Ukweli ni kwamba mafuta yatokanayo na mbegu za mimea kama Alizeti, Pamba, Mahindi (Corn oil), Soy oil sasa ni vihatarishi vikubwa sana vya magonjwa ya moyo na mashambulizi ya mwili kama Pumu ya kifua, Pumi ya ngozi (Eczema, AD), Baridi yabisi nk.
Swali la Kujiuliza Kwa nini Mwanzo Yalikuwa mazuri na leo tena Rundi la tafiti zinasema ni hatari kwa afya yako?

Sababu ni kwamba kosa kubwa ambalo lilifanywa na Ancel Benjamin Keys kuanzia mwaka 1958 alipo amka na kuja na nadharia ya kwamba “Mafuta yanayo ganda, Huenda kuganda mwilini kama yanavyoganda kwenye mazingira ya kawaida na kukuletea shida mwilini kama magonjwa ya mishipa ya damu ikiwemo moyo kuathiriwa, Lakini pia akasema mafuta yanayoganda kutoka kwa wanyama huongeza Cholestrol na kukuweka hatarini mishipa yako kuziba” Huyu nadharia hii tafiti nyingi zinakanusha na kusema ni tafiti Isiyokuwa na ukweli wowote.

Hakuna Popote katika sayansi panapo onesha mafuta hubadilika kuwa cholestrol, Ndio maana Umbo la cholestrol kikemikali sio sawa na mafuta kabisa. Kwa hio Cholestrol sio mafuta, Bali huwa na sifa zinazofanana kama mafuta, Sifa mojawapo ni kutochangamana na maji. Hio ni “Nadharia ya Kiutafiti, Ambayo ilipitishwa rasmi na kutumika katika mwongozo wa lishe ulitolewa na amerika mwaka 1977, Ambapo dunia nzima tulifuata mwongozo huo”.

Ancel Keys
ndiye aliyesababisha “Tukaanza kuchuja mafuta kwenye maziwa tukaondoa radha asili ya maziwa na badala yake tukaanza kuongeza vanilla,Sukari na yakaitwa low fat, Huku vitamin A,D,E zikiondoka pamoja na mafuta, Ili kutupumbaza walaji wa maziwa hayo kuwa vitamin hazikuondoka, kwamba zoezi hilo halijaathiri kitu, Watalamu wa uchujaji maziwa hayo huongeza vitamin za kiwandani (Artificial vitamin) kama A,D na E tizama maziwa mengi skimmed (Low fat yameandikwa) Enriched with…A,D,E sasa Kwa nini hizo vitamin zinaongezwa wakati Vitamin asili tunategemea ziwemo? Kwa sababu Wamechuja Mafuta hizo ni Fat loving vitamin, Unapoziondoa zinaondoka kwa pamoja.

Huyu ndiye aliyetuambia “Tule nyama iliyo ondolewa mafuta yaani lean meat, Tule Yai tuondoe kiini chake “ Na mengine mengi kwa maana hio sasa Watalamu wengine wamekuwa wakihoji yawezakuwa ndio maana “Kitambi, Kisukari, Presha” Mlipuko ulikuwa wa kasi sana kuanzia mwaka 1980 na yakaanza kuitwa magonjwa ya Mapinduzi ya viwanda, Nyama asili ikawa mbaya ila Yakiwandani ikawa nzuri, Kuku akawa mbaya mpaka uondoe ngozi, Mayai na kiini chake likawa baya , Maziwa ya kienyeji yakawa mabaya yake yaliyochujwa mafuta kiwandani yakawa mazuri, Kila kitu kikawa lazima kipite kiwandani “Ndipo kiitwe kizuri” Unaweza Kufikiria hivyo!

Sasa Kwenye Mafuta ya Kupikia Kimbilio likawa “Mafuta ambayo hayagandi kirahisi kama alizeti, Soya,Mahindi, Pamba nk” Kumbuka kwamba Kabla ya hayo mafuta Binadamu alitumia mafuta kama Siagi, Mzeituni, Nazi, Samli nk ambapo sasa Baada ya Ancel Keys kuja na Elimu yake ya Kufikirika akabadilisha mfumo kabisa kidunia. Na hakukuwa na Taifa lolote enzi hizo ambalo linazalisha Mafuta yatokanayo na mbegu za mimea. Eti mashine ya kukamua mafuta ya soya? Mafuta ya mahindi? Mafuta ya pamba?

Amerika ndio Ilianza kufanya hivyo na sisi duniani kote tulikula kutoka huko. Sisi tumekuja kuanza uzalishaji kwa mashirika ya uma, na ndipo watu binafsi hivi punde ndio Wameanza Kuzalisha mafuta hayo. Ila Amerika ndiyo alikuwa wa kwanza Kufanya hilo.

Yaani Ukisoma kwa kina historia ya Kuibuka kwa mafuta haya yenye jina “Vegitable oil” Utasikitika sana kwani moja ya sababu zilikuwa hizi kuanzia miaka ya 1950s.

1. Mafuta ya Mimea hayana cholestrol, Achana na Mafuta ya wanyama huongeza cholestrol

2. Mafuta ya mimea yana bei ndogo achana na Ghee na butter bei ghali sana

Hizo ndo zilikuwa mada kubwa zilizotumika “KUYADONDOSHA MAFUTA ASILIA YA ENZI NA ENZI KWENYE ULIMWENGU WA BIASHARA”

MAMBO AMBAYO HAWAKUZINGATIA KITALAMU NDIYO YANAANGAMIZA JAMII SASA KIAFYA


1. Hawakujua kwamba kuita “Cholestrol free” hakuna maana yoyote ni sawa na kuchukua Chipsi za viazi Useme “Cholestrol free” au Ugali wako uandike “Cholestrol free Ugali” Maana kwenye Mafuta ya mbegu za mimea hakuna cholestrol kuna “Phytosterol” ambayo binadamu huwa haitumiki, Inaingia na kutoka, Haina kazi yoyote mwilini. Bali cholestrol hupatikana kwenye bidhaa za wanyama na ndege tu kama maziwa, Nyama ,mayai nk.

Ila Chakushangaza Mafuta ambayo nategemea nisikute cholestrol unaandikiwa “Cholestrol free”. Inaleta maana kuandika kwenye maziwa skimmed kwamba “Cholestrol free, Low fat” kwa sababu nategemea hivyo vitu kuvikuta ila sasa sijavikuta. Ila Cholestrol sitegemei kuikuta kwanini useme “Cholestrol free”.

Ipo siku neno hili utalikuta kwenye “Chips viazi” “Kwenye wali” “Kwenye ugali” nk Linatumika Kibiashara sana ukilichunguza kiundani. Soma Haya maneno utakubaliana na mimi siku moja.

2. Hawakuangalia kwamba Mafuta huchanganuliwa kulingana na umbo lake na umbo la mafuta hayo kisayansi ndio yanatofautisha aina moja ya mafuta na mengine.
Mfano Kitalamu unaposema Saturated Fats, Haya ni mafuta yenye sifa ya kuganda kwenye mazingira ya kawaida ya joto, Kwa sababu yameshikamana kiasi kwamba joto la kawaida haliwezi kuvunja muungano wake kikemikali ili kuyafanya yaweze kuyeyuka, Ila endapo ukitumia moto mkali sana unaweza sasa kuyayeusha mafuta haya. Sasa Kuna mafuta mfano Samli, Siagi (Butter), Mafuta ya nazi, nk haya ni mafuta yenye sifa ya kuganda katika Uasili wake.

Pia kuna mafuta unaposema kitalamu “Monounsaturated oil” Haya ni mafuta ambayo yenyewe yapo katikati, Yaani yanastahimili joto na moto kwa wastani. Hapa ndipo utayakuta mafuta ya Mzeituni, Karanga,Parachichi, Mawese nk Chakushangaza Kila mtu anayetumia mafuta ya Olive oil anajua kwamba “Olive oil huwezi kukaangia chips,Samaki na nyama” Kwa sababu hayastahimili moto mkali hasa kwenye kukaanga sana.

Ukiyachoma kwa muda mrefu na moto mkali hutengenesa sumu ziitwazo Free Radicals na kukuweka hatarini kupata msongo wa sumu kitalamu tunaita “Oxidative stress” Ingia kwenye mtandao soma kuhusu magonjwa yanayosababishwa na kinga ya mwili kulemewa na sumu hizi yaani “Oxidative stress”.

Tatu mafuta yenye jina la kitalamu Polyunsaturated oils, Haya ni mafuta ambayo hayastahimili kabisa moto na joto ndio maana hayawezi kuganda hata joto dogo tu linavunja umbo lake na kuyeyuka haraka sana.

Unaweza kuweka hata kwenye friji yasiweze kuganda. Ndio maana moja ya uhifadhi wa mafuta haya katika kundi hili ili yadumu muda mrefu bila kutengeneza sumu “Usiyaweke kwenye jua au mwanga mkali”.

Mafuta ya kundi hili yanatokana na mbegu za Alizeti, Pamba,Mahindi soya nk. Sasa Iweje Olive oil huruhusiwi kukaangia chips nyama walafu mafuta haya ya alizeti, Pamba, Soya mahindi ndiyo yafae kukaangia vitu kama “Chips”?

.Mafuta ambayo hayastahimili moto na joto kitalamu yanapokuwa yanaungua hutengeneza sumu nyingi ziitwazo free Radicals, ambazo kitalamu tunaziita Reactive Oxygen Species (ROS) ,Huleta majeraha na kuvimbisha mwili kibaolojia na mwili kukosa mwelekeo kiutendaji (Yaani shughuli zinavurugika).

Kadri unavyozidi Kumimina sumu hizi mwilini itafikia hatua, Viondoa sumu ambavyo Mungu alituumba navyo vyote vitatumika na mwili utalemewa sumu hizi hatua hio tunasema mwili umeingia kwenye “Oxidative stress” Google neno Oxidative stress halafu bonyeza “Images” kisha soma maelekezo utakuja kuona Uhusiano kati ya magonjwa uliyonayo kama Moyo,Presha kali,Pumu,Kisukari,Uzito kuongezeka kwa kasi, Magonjwa ya ngozi nk ni kwa sababu mwili wako upo kwenye “Oxidative stress”
Kipindi hicho Ancel Keys hakujua kwamba huko mbeleni “Free radicals itakuja kuwa chanzo cha magonjwa ya moyo, na cholestrol itakuwa nadharia mfu na iliyopitwa wakati , kama ilivyo sasa”


Je Unapokuwa unapima Cholestrol je huwa unapima jinsi gani mwili wako umelemewa na Free radicals? Hapana Bado tunashauriwa kupuuzia Athari za free radicals na kukomaa na cholestrol wakati tafiti zinaonesha miili yetu imelemewa free radicals ndio maana magonjwa haya yamekuwa changamoto. Afya ni hazina yako!
3. Hakujua kwamba Baada ya kukimbilia kwenye mapinduzi ya viwanda na kuamua kuleta mafuta na kuyasukuma kwa nguvu zote. Mafuta yenye chanzo kingi cha Omega 6 kama Alizeti,Pamba,Mahindi,soya ,Canola oil yanatuhumiwa kufanya miili yetu kuzidiwa na kiwango kingi kupita kiasi cha Omega 6. Ndio maana shirika la afya duniani WHO linakiri wazi kwamba “Kuna uhusiano mkubwa kati ya mwili kuzidiwa omega 6 ukilinganisha na Omega 3 na magonjwa ya Moyo” Ndio maana hapa duniani utakutana na virutubisho vya “Omega 3 na sio Omega 6” Unajua ni kwa nini? Tunashauriwa kuongeza Omega 3 na Kupunguza omega 6.


Sasa Kibaya zaidi kwenye Lishe yetu ya kawaida mafuta tunayo kumbana nayo kwenye vyakula sio tu yanatumika kukaanga kwenye moto mkali na kurudia rudia yale yale ili mpishi asipate hasara, Lakini pia hayo hayo mafuta yanazidi kutuongezea kitu ambacho tumezidiwa mwilini.
Tafiti zinaoneshwa kwamba uwiano wa omega 3mega 6 sasa unefikia 1:16.7 yaani tumezidisha omega 6 zaidi ya mara 16 kwa nini usiugue maradhi ya moyo?
Kiafya Mwili unapolemewa Omega 6 unapata magonjwa ya mashambulizi ya mwili kama Pumu ya kifua,Pumu ya ngozi, Presha, Kisukari, Baridi yabisi, MAGONJWA YA MOYO (Herufi kubwa) Lakini hakuna Daktari atakayekwambia kuhusu hili, Kwamba mafuta ya kwanza yakuepuka ni “Yenye kukuzalishia free radicals nyingi, na yenye kiwango kingi cha omega 6 ambayo lazima ataje Vegitable oil” Unajua ukweli Lazima uwe hivi ili ujue namna ya kujikinga.

Je ushawahi kuona Daktari akikushauri angalau ufanye kipimo cha kutizama majeraha au uharibifu wa omega 6 kuwa nyingi kuliko omega 3? Kipimo hicho ingawaje sio cha moja kwa moja ila kinaweza kumpatia picha kwamba mashambulizi yanaendelea tunakiita High sensitive C reactive protein. Kulingana na uzoefu wangu wagonjwa wenye huwa wana kiwango sawa cha cholestrol kwenye lipid profile test lakini ukiwapima High sensitive C Reactive protein Unakuta ipo juu sana. Na utanaweza kujua kwa nini mgonjwa anateseka na “Pumu,Ngozi,Presha,Moyo,Viungo kuvimba na kuuma” nk

Sio hivyo tu kuna kipimo cha kuangalia uwiano wa omega 3/Omega 6 kwenye damu na kipimo hiki kina nguvu kuliko lipidi profile test (Kipimo cha cholestrol) Unaweza kuona Jinsi gani tuko nyuma kwenye kuvipima viashiria vya magonjwa ya moyo na presha. Ukienda mataifa yaliyo endelea utapima Uwiano wa omega 3/Omega 6 ili ushauiriwe kuepuka vyanzo vya Omega 6.

Vyanzo Vikubwa vya Omega 6 kwenye lishe yetu ya kila siku, Ni Mafuta ya mbegu za Mimea kama Alizeti,Pamba,Mahindi soya nk
Vyanzo vikubwa vya omega 3 ni Mafuta ya samaki,Samaki mwenyewe, Mayai,Nyama, Kwenye mimea mwili hubadilisha omega 3 ya mimea yaani ALA na kuwa DHA na EPA kisha kutumika mwilini utapata kwenye Karanga za Almonds, Walnuts,Korosho,Pistasho, yaani karanga za mtini tu usiweke karanga hizi za kawaida (Groundnuts) hizi zina kiwango kingi sana cha Omega 6 kuliko omega 3.
4. Hakuelewa kwamba ni vibaya kuyapitisha mafuta ya alizeti,Pamba,Mahindi soya,Mawese kwenye moto mkali na kuyachoma kwa mlolongo mrefu na kututengeneza mafuta ya kisasa ya “Mgando” kama Prestige, margarine nk
Hayo ni mafuta ya mgando yatokanayo ni mimea sio ng’ombe unavyojua rafiki, Mafuta ya mgando yakutengeneza yakawa mazuri kuliko asilia mgando. Lakini mafuta haya yameonesha kuwa na shehena kubwa ya free radicals mwilini kuliko mafuta ya mgando ya kawaida kwa sababu yanazalishwa kwa kutumia moto mkali mlolongo mrefu na yakiwa hayana sifa ya kustahimili moto.

Nakomea hapo leo, Nilipita sehemu wanachoma mafuta yamekuwa meusi lakini bado nyama zinakaangwa tu, na sio sehemu moja ni sehemu nyingi sana. Ndio maana nimeandika haya usome ukaongeze elimu nyingine ujue namna ya kujikinga, Jamii inaangamia kwa kukosa maarifa.

MAFUTA YENYE JINA LA KIBIASHARA VEGITABLE OILS YANAWEZA KUKUONGEZEA UHATARI WEWE KUPATA MAOGONJWA YA MOYO, PRESHA,PUMU, KUTOKANA NA HOJA YENYE TAFITI RUNDO HADI SASA YAANI FREE RADICALS NA WINGI WA OMEGA 6 NDANI YAKE AMBAYO TUNASHAURIWA TUPUNGUZE KIAFYA.NA NENO “CHOLESTROL FREE, HALINA UZITO WOWOTE JUU YA KUKUKINGA WEWE USIPATE MAGONJWA YA MOYO”
 
Nakomea hapo leo, Nilipita sehemu wanachoma mafuta yamekuwa meusi lakini bado nyama zinakaangwa tu, na sio sehemu moja ni sehemu nyingi sana. Ndio maana nimeandika haya usome ukaongeze elimu nyingine ujue namna ya kujikinga, Jamii inaangamia kwa kukosa maarifa.


Huo ni uongo ulio kubuu, mafuta kuwa meusi haitokani na kukaangia sana, nyama zinaungua na ndo zinasababisha mafuta kuwa meusi yawe alizeti yawe ya wanyama, au ujui kupika na Wala ujawahi pika.
 
Nimejifunza kuhusu vitu viwili ambavyo ni:
1. FACTS za kisayansi na
2. TRUTH za Neno la Mungu
Mimi huzipima Fact zote kama zinakubaliana na Neno la Mungu zikikinzana huchagua UKWELI isemavyo Biblia na Mafunuo mengine maana huu ndio mwongozo wa yote
Fact za kisayansi ambazo tafiti zake huendelea kujipinga kwa tafiti zingine ni za kuogopa .kama kuna mtu alidanganya watu kipindi kirefu ni Dalton na nadharia yake ya atomi. Mimi hunywa maziwa sana tu na samli maana Biblia HAIJAKATAZA ila huepuka mafuta ya Wanayama maana Biblia IMEKATAZA. Mafuta mengine hata biblia haikuyataja mfano mafuta yatokanayo na mchele, mahindi n.k ambavyo tunalazimisha kupata mafuta wakati zipo mbegu zenye mafuta kama Karanga, korosho, Maboga n.k
Ukaangaji wa vyakula kwenye mafuta Biblia HAIJASEMA.

Bora tufuate Mwongozo wa "Bwana amesema"
 
Halafu muuza chipsi yeye utasikia anatumia mafuta ya transformer kwa kukaangia.
Halafu utasikia babe mbona hunambi I love you Nita kwambiaje I love you wakati moyo ushachomwa hata hisia hauna😂
 
Tafiti za kisayansi hubadilika kulingana na maendeleo ya teknolojia hivyo yawezekana ni kweli hakua sahihi kutokana na uduni wa teknolojia ya kipindi hicho katika kufanya tafiti.
 
Kesho utasikia ugali haufai, kesho kutwa wali, bas tuache kula kabisa ili tusipate magonjwa

Napo utaletewa utafiti wa madhara ya kutokula.

Ni shida sana, tafiti Moja inakwambia kahawa ni nzuri, nyingine inakusisitiza usitumie.

Mara ule matunda kabla ya chakula, shida sana.

Sasa hapa kwenye mafuta Kwa wengi wetu hawaangalii sijui mafuta ya Kenge, mchicha au ya kambale, anachouliza je, ni mafuta ya kupika? Anapimiwa vibaba vyake anaenda kuandaa maakuli.

Kuna wale unanunua Alizet au olive oil wakati mchana unaenda kula mafuta usiyoyajua.

Sisemi tusiwe makini kuzingatia tunakula nini ila afya zetu ni kudra zaidi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom