Kwahiyo unataka kuoa single mama?

Nyenyere

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2010
Messages
10,672
Points
2,000

Nyenyere

JF-Expert Member
Joined Sep 9, 2010
10,672 2,000
Basi fahamu haya:

Mwanamke aliyezaa huhamishia mapenzi kwa mwanaye. Hali huwa hivyo hata ndani ya ndoa, kiasi kwamba ndoa nyingi hupoteza mvuto pale tu mtoto anapozaliwa. Kwako wewe kijana unayetaka kujitwika mabomu uoe single mother.

Mwanamke anatakiwa aolewe katika ubikira wake ili mwanamume kujisikia kwamba kweli amepata mtu mwaminifu. Lakini kama hata hilo halikutosha kukushawishi, usithubutu kuoa mwanamke ambaye ni single mama, labda kama una uvumilivu usiopimika. Yako mambo kadhaa ambayo yanamfanya single mama asiwe sehemu ya mtarajiwa wa ndoa.

1. Single mama wengi ni matokeo ya uzinzi ama uasherati. Binti anapojiingiza kwenye mapenzi kabla ya ndoa kwa kigezo cha kutafuta kuolewa ni dalili mbaya hata kama ataolewa kweli. Hii inaonyesha kuwa ana udhaifu kwenye eneo la ndoa kiasi kwamba yuko tayari kuutumia mwili wake kama rushwa ili kufanikisha ndoa. Hii haitofautiani na mwanamke aliye ndani ama nje ya ndoa kutumia tigo yake kama kishawishi cha kumshika mwanamume. Unapotumia ngono kama sehemu ya ushawishi, ama kama silaha ya kumteka mwanamume ujue kwamba unaondoa thamani yako na kuingia kwenye kundi la makahaba. Ni kweli uchi wa mwanamke ndio silaha yake kwenye mahusiano, lakini si kwa kuigawa hovyo, bali kwa kuwanyima wanaoitamani ili apatikane mwenye nia thabiti ya ndoa.

Inapotokea binti kajiingiza kwenye mapenzi mpaka kupata mimba, tayari keshapata muunganiko mwingine na mwanamume aliyempa mimba hiyo, tayari wameunganishwa na mtoto huyo, ingawa bado mwanamume aliona huyu mwanamke hafai kuwa mke, alikiwa anamtumia tu kukidhi kiu yake mpaka pale atakapompata mtu sahihi. Sasa wewe ni nani hata ukajiingize kuoa mwanamke wa aina hii?

2. Single mama hawezi kukupenda kwa jinsi ulivyo, bali kutakuwa na sharti la mtoto. Kwamba iwapo utamtunza mtoto kama single mama atakavyo basi utapewa mapenzi matamu. Ni ukweli usiopingika kuwa mwanamke apatapo mtoto mapenzi yote huhamia huko, hivyo wewe jiandae kuwa chaguo la pili kwake. Haya sio mapenzi na ujue tu kuwa huwezi kuwa na amani kamwe.

3. Mtoto si wako. Hata kama utampenda na kumhudumia kwa namna yoyote ile, ukweli utabaki kuwa huyo si mwanao, sio damu yako. Ni kwamba umejitwika jukumu la kumhudumia mtoto wa mwanaume mwenzako ambaye ndiye ataendelea kutambulika kama baba mzazi. Siku akikua ataanza kumtafuta aliyechangia mbegu mpaka akaja dunuani, sio aliyechangia ugali. Ikitokea mmeachana na single mama, ujue ndio mwisho wa kuonana na mwanao mpenzi uliyekuwa ukimtunza kwa nguvu zako zote.

4. Utatumia nguvu kubwa kulilinda penzi. Ili ujihakikishie kuwa single mama anatulizana na wewe, utahitaji kuishi maisha ya kumfurahisha yeye, kumpa atakacho ili asije akamkumbuka mume wake wa kwanza. Namna pekee ya kumfurahisha ni kuhakikisha mtoto wa mwanamume mwenzako anapata maatunzo mazuri, nguo nzuri, elimu nzuri n.k. Utalazimika kuwa karibu naye kuliko hata baba mzazi anavyokuwa, yote haya ni kutafuta kumfurahisha single mama. Utaishi maisha ya kujipendekeza, yenye stress nyingi.

5. Huna sauti juu ya mtoto. Hata kama utataka umchujue mtoto huyu kuwa mwanao kamili, umpe malezi halisi ya mzazi, kuna mahali utakwama tu. Huwezi kumwadabisha kwa mikono miwili, lazima mmoja utakuwa nyuma na mwingine utakuwa mbele. Mara zote utakaa ukijiuliza, labda nikimfanya hivi mama yake atadhani namchukia, jamii nayo itanifikiria vingine. Utajikuta wewe mwenyewe unajiwekea mipaka hata kabla pilato hajakuhukumu kwa kuvuka mstari!! Pigo kubwa zaidi ni pale single mama atakapokutamkia kuwa unamtendea hivyo kwa sababu mtoto sio wako. Hapo utabaki kama mjinga fulani aliyepigwa bumbuwazi asijue aukabili vipi ukweli huu mchungu.

6. Chanzo cha vurugu kwenye familia. Hata ikitokea mmezaa watoto wengine, bado mapenzi hayawezi kuwa sawa. Single mama wana kawaida ya kuwaandalia mazingira watoto wa baba wengine tofauti hao wa baba waliye naye wakati huo. Hufanya hivyo kwa hofu kuwa watoto hawa mara nyingi hawana urrithi kwa baba aliyewalea. Hii huleta mgawanyiko mkubwa kwenye familia kiasi cha watoto wenyewe kuchukiana. Hata ndugu wa mwanamume hawawezi kamwe kumhesabu mtoto huyu kama sehemu ya familia kwa sabubu sio damu yao na anao ukoo mwingine kabisa. Hawezi kujitambulisha kwa jina la baba wa kambo kwa sabubu hana muunganiko wowote naye. Hata ikitokea baba mlezi amekufa, ukoo wake hauwezi kumhesabu mtoto huyu kama sehemu ya urithi. Tunajifunza kwa wanyama wengine pia kama simba, ambapo anapoinuka dume mwingine kuongoza majike, huua watoto wote àliowakuta kisha huanza upya kusaka watoto wake. Sasa sisi hatuwezi kuua, bali tunaweza kuepuka taabu hii kwa kutokuoa mwanamke mwenye watoto.

7. Mume wa kwanza ana nafasi ya kuendelea kumtafuna single mama atakavyo. Kwa kawaida mwanamke akishazaa na mwanamume, ule muunganiko huwa haufi. Tayari ni mzazi mwenza na hana cha khmficha tena, hivyo kupasha kiporo ni jambo la kawaida tu. Pia mama atataka mtoto amjue baba yake halisi kwa ajili ya siku zijazo, hivyo hawezi kujiweka mbali na mzazi mwenzake. Sasa mzazi mwenza ni juu yake kuamua kuendelea kumla ama la, kwani hakuna kutongozana tena, ni kupanga miadi tu na kukutana kuserebuka. Kidume wewe utageuzwa baba mlishi huku haki nyingine zote zikielekezwa kwa mwenye mwanaye.

Ukweli ni kuwa single mama anapopata mume, focus yake sio ndoa bali ni malezi ya mwanaye. Anataka uhakika tu kuwa mwanae ataishi na atapata matunzo bora ili siku za usoni aje kumsaidia yeye.

Ewe kijana, usijiingize kwenye mtego utakaoharibu maisha yako. Tafuta bikira atakayefunga kiapo nawe, achana na wanawake waliozaa hovyo kwa kukosa mwelekeo.

Hapa sijazungumza juu ya walioolewa kisha waume zao kufariki, kwani kwao hawa yako mambo mengi pia nyuma ya pazia ya kuchunguza.
 

Karma

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2019
Messages
9,099
Points
2,000

Karma

JF-Expert Member
Joined May 20, 2019
9,099 2,000
Huo hapo soma
Nimeshausoma sijaona cha zaidi tofauti na mawazo yako yale yale ya kimisogynist kuna sehemu umesema "mwanaume kujilinganisha na mwanamke ni kujishusha hadhi" yaani kwamba uanamke hauna hadhi ila uanaume ndiyo una hadhi??

Sisemi mwanaume ajilinganishe na mwanamke lakini asifanye hivyo siyo kwa sababu eti jinsia fulani ndiyo ina hadhi kuliko nyingine bali kwa sababu yeye aliumbwa hivyo na anatakiwa awe hivyo ni sawa na kusema "tajiri asijifananishe na masikini anajishusha hadhi" kwamba tajiri ndiyo bora sana kuliko masikini siyo??

Na haya yote yanayoendelea kwenye jamii ni matokeo ya wanaume kuwadharau wanawake hakuna jinsia inayopenda kudharauliwa na mliambiwa mtutawale hamkuambiwa mtudharau sasa kama ndicho mlichoelewa kutoka kwa Mungu basi nina mashaka akili zenu yaani nashangaa eti wanaume wanawadharau wanawake kwa sababu ya maovu ambayo hata wanaume nao wanayafanya??

Yaani dhambi akiifanya mwanaume ni sawa ila akiifanya mwanamke ni kosa eti kwa sababu tu mwanaume hapotezi ila mwanamke anapoteza msilazimishe tofauti kwenye kila kitu dhambi ni dhambi tu haijalishi kaifanya mwanaume au mwanamke iko hivi kama ambavyo mnaona ni sawa kuwa na wanaume wazuri na wabaya basi pia acheni iwe sawa kuwa na wanawake wazuri na wabaya dunia ndivyo ilivyo ili ibalance lazima kila kitu kiwe na kinyume chake sasa ninyi mnataka kwa wanaume kuwe na wazuri na wabaya ila kwa wanawake kuwe na wazuri tu hata kwa kutumia akili ya kawaida inawezekana kweli hiyo??
 

Karma

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2019
Messages
9,099
Points
2,000

Karma

JF-Expert Member
Joined May 20, 2019
9,099 2,000
Na kwanini jamii itengeneze stigma hii??
Kulingana na mila NA desturi za mwafrika, suala LA kuwasemasema single moms haliwezi kukoma wala kukomeshwa KWA sababu ktk jamii zetu inaonekana dhahiri hao single moms tayari wamejikomesha wenyewe kwa kutaka balaa LA kuandamwa NA stigma hii kutokana na kuzaa nje ya ndoa, tena bila ya mpango au utaratibu.
 

Easy Chair Mark III

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2019
Messages
910
Points
1,000

Easy Chair Mark III

JF-Expert Member
Joined Aug 19, 2019
910 1,000
Anayeomba ndiyo chanzo cha kila kitu hakuna effects bila causes haijalishi effects zitakuwaje ila siku zote tunatakiwa kudeal na causes kwanza
Nashauri utumie nguvu NA juhudi hizi hizi ktk kufanya kampeni kubwa kabisa ya kufa NA kuona ktk kuwaelimisha wanawake wenzako NA wasichana ili wajitambue, wawe NA ufahamu wa kutosha kabisa kuhusiana na masuala ya ndoa, pamoja na kuheshimu miiko ya ndoa.Ukitilia mkazo zaidi juu ya umuhimu wa mwanamke kujitunza, kuwa na watoto wakati tu akiwa kwenye ndoa, KUACHA KABISA TABIA YA KUZAA WATOTO AKIWA NJE YA NDOA TENA BILA UTARATIBU WALA ANGO UNAOELEWEKA.
Kuzaa nje ya ndoa KWA mwanamke ni kitendo cha kujifedhehesha sana kupita kiasi, washauri wanawake wenzako NA wasichana kuwa wajitunze, wasizae nje ya ndoa, ili kuepuka fedheha itokanayo NA kudhalilishwa ktk jamii. Mjitunze ili mheshimike ktk maisha yenu, epukeni fedheha?!
 

Baraja

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2015
Messages
212
Points
250

Baraja

JF-Expert Member
Joined Dec 28, 2015
212 250
Singo madhaz

Watu wengi tumekuwa tukikoseshwa imani na watu hawa kutokana na matendo yao ndani ya jamii tunamoishi nao, kiukweli huwa wanadiscourage sana katika mahusiano. Hata hivyo kila mmoja achague analoona lamfaa,

Ila singo madhaz, mnh!
 

Easy Chair Mark III

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2019
Messages
910
Points
1,000

Easy Chair Mark III

JF-Expert Member
Joined Aug 19, 2019
910 1,000
Na kwanini jamii itengeneze stigma hii??
Kitendo cha mwanamke kuzaa nje ya ndoa tena bila utaratibu au mpango maalumu unaoeleweka anahesabika kuwa ni mwanamke asiyekuwa anajitunza.Mwanamke huyo anahesabika kuwa ni mzinzi, asiye NA msimamo, dira wala mwelekeo, hajui kutunza unyumba ndio maana ameweza kutapeliwa kimapenzi kirahisi, hivyo upo uwezekano mkubwa wa kuweza kutapeliwa tena zaidi NA zaidi ktk maisha yake yote, ni mwanamke asiyefaa, n.k., n.k.

Suluhisho pekee ni KUJITUNZA, USIZAE NJE YA NDOA
 

Karma

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2019
Messages
9,099
Points
2,000

Karma

JF-Expert Member
Joined May 20, 2019
9,099 2,000
Yale yale, hivi hao wanawake wanajizalisha wenyewe??

Hivi tukisema tushikie bango wanawake tu kujitunza halafu tukawaacha wanaume kuona kuwa wanayofanya ni sawa unadhani wanawake watapona na wataweza kukwepa vishawishi vyote kweli??
Nashauri utumie nguvu NA juhudi hizi hizi ktk kufanya kampeni kubwa kabisa ya kufa NA kuona ktk kuwaelimisha wanawake wenzako NA wasichana ili wajitambue, wawe NA ufahamu wa kutosha kabisa kuhusiana na masuala ya ndoa, pamoja na kuheshimu miiko ya ndoa.Ukitilia mkazo zaidi juu ya umuhimu wa mwanamke kujitunza, kuwa na watoto wakati tu akiwa kwenye ndoa, KUACHA KABISA TABIA YA KUZAA WATOTO AKIWA NJE YA NDOA TENA BILA UTARATIBU WALA ANGO UNAOELEWEKA.
Kuzaa nje ya ndoa KWA mwanamke ni kitendo cha kujifedhehesha sana kupita kiasi, washauri wanawake wenzako NA wasichana kuwa wajitunze, wasizae nje ya ndoa, ili kuepuka fedheha itokanayo NA kudhalilishwa ktk jamii. Mjitunze ili mheshimike ktk maisha yenu, epukeni fedheha?!
 

Easy Chair Mark III

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2019
Messages
910
Points
1,000

Easy Chair Mark III

JF-Expert Member
Joined Aug 19, 2019
910 1,000
Yale yale, hivi hao wanawake wanajizalisha wenyewe??

Hivi tukisema tushikie bango wanawake tu kujitunza halafu tukawaacha wanaume kuona kuwa wanayofanya ni sawa unadhani wanawake watapona na wataweza kukwepa vishawishi vyote kweli??
KWA nini ukubali kushawishiwa kizembe?Kudanganywa au kurubumiwa kirahisi tena kizembe kabisa kama mtoto mdogo wa umri wa miaka mitano???
Mwanamke kukubali kudanganywa kizembe ni udhaifu mkubwa NA tena inaonyesha wazi kuwa hauna msimamo ktk maisha yako, mama huduma NA matokeo yake ni kuzalishwa nje ya ndoa na hatimaye kudhalilishwa KWA kuitwa majina mabaya yasiyofaa ktk jamii.

Shikeni msimamo, hakuna ndoa hakuna kuzaa mtoto!
Mkiwa NA msimamo huu, mkijitunza NA kujiheshimu lazima wanaume tutawaoeni, NA mtazaa watoto mkiwa ktk ndoa.
 

Karma

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2019
Messages
9,099
Points
2,000

Karma

JF-Expert Member
Joined May 20, 2019
9,099 2,000
Lakini single fathers hawana matendo mabaya??
Singo madhaz

Watu wengi tumekuwa tukikoseshwa imani na watu hawa kutokana na matendo yao ndani ya jamii tunamoishi nao, kiukweli huwa wanadiscourage sana katika mahusiano. Hata hivyo kila mmoja achague analoona lamfaa,

Ila singo madhaz, mnh!
 

Forum statistics

Threads 1,344,030
Members 515,307
Posts 32,805,550
Top