Idugunde
JF-Expert Member
- May 21, 2020
- 6,273
- 6,637
Kwanza ieleweke wazi kuwa kodi ya itayolipwa na wananchi kupitia manunuzi ya vocha za simu ni sawa na kodi ya kichwa waliokuwa wanatoza wakoloni kisha tukairithi na baadae kuondolewa miaka tisini baada ya kuwa ni kodi inayodhalilisha watu.
Kwamba ukiongeza salio unakatwa pesa ili kuchangia maendeleo hii ni aibu. Yaani hata wanachi wasiojiweza ambao wakiongeza salio la buku watachachangia kodi? Kisa tu tuna miradi mikakati kama Sgr na hatuna pesa
Kama tunahitaji pesa za kukamilisha miradi mkakati kwa nini tusikusanye kodi kupitia uvuvi wa bahari kuu ambako kuna kodi nyingi inapotea kwa kuibiwa na meli kibao za uvuvi toka mataifa ya kigeni?
Kodi ya kichwa ni aibu kubwa karne hii.