Luhaga Mpina: Waziri Mwigulu Nchemba anahusika na ufisadi wa trilioni 1.7 mradi wa SGR

USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
9,896
22,666
Waziri wa zamani wa uvuvi Luhaga Mpina ametoa tuhuma kwa Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba kuwa ameiibia Serikali pesa katika miradi wa SGR zaidi ya trilioni1.7 .

Hii ni zaidi ya ile kelele ya trilioni 1.5 ya utawala wa hayati Magufuli na ni nusu ya wizi wote alioutaja CAG katika report yake ya jumla ya trilioni 3.5 kwa wizara yote.

Kumbe yale mabasi na matimu ya mpira ni pesa za walipa kodi

USSR

20230421_132011.jpg
 
Pamoja na haya, ajabu Rais akaishia kuvunja bodi tu ya shirika la Reli, wakati inaonekana kuna uozo mkubwa zaidi unafichwa..

Mwigulu anastahili kufikishwa mahakamani kwa hizi tuhuma kama zikithibitishwa, licha ya kuhusishwa kwake na huu wizi kunakoendana nae kuonekana kuwa na mali nyingi zaidi ya kipato chake, bado yupo ofisini miguu juu akibuni tozo mpya kwa ajili yetu.

Kiongozi kama huyu ingefaa kabisa awekwe pembeni kupisha uchunguzi dhidi yake, bahati yake ni miongoni mwa watoto pendwa wa mama, awamu hii imekuwa incompetent sana.
 
Waziri wa zamani wa uvuvi Ruhaga mpina ametoa tuhuma kwa waziri wa fedha mwigulu Nchemba kuwa ameiibia serkali pesa katika miradi wa SGR zaidi ya trilioni1.7 .

Hii ni zaidi ya ile kelele ya trilioni 1.5 ya utawala wa hayati Magufuli na ni nusu ya wizi wote alioutaja CAG katika report yake ya jumla ya trilioni 3.5 kwa wizara yote.

Kumbe yale mabasi na matimu ya mpira ni pesa za walipa kodi

USSR View attachment 2595078
Zinatakiwa evendence za kutosha kuthibitisha.Sio kupayuka tu Kama mweu.
 
Wizi wa Magufuli tunaoujua ni 1.5 trilioni lakini ule wa Magufuli alioshirikiana na Biswalo Mganga ni zaidi ya hapo labda unaweza kufika trilioni 10 na ushee.

CCM ni walewale na mambo ya wizi na upigaji na matumizi mabaya ya fedha za Wananchi masikini ni yale yale.
 
Back
Top Bottom