Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,812
- 11,989
Fuatilia yanayojiri kwenye Bunge la 12, Mkutano wa 11, Kikao cha 55, leo Juni 26, 2023.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mwigulu Nchemba amesema fedha zinazopelekwa kwenye Mikopo ya Elimu ya juu ndani ya mwaka mmoja wa fedha kwa sasa ni kubwa zaidi kuwahi kutolewa tangu uhuru. Hali ipo hivyo pia kwenye Sekta ya Kilimo, Afya, Uvuvi na mifugo na Maji.
Aidha, fedha za mafao ya wastaafu, Maslahi ya watumishi wa Umma, kuvutia uwekezaji, Ulinzi na Usalama pamoja na miradi ya kimikakati ni nyingi kuliko kipindi chochote kile.
Amesema hoja zote zilizotolewa na wabunge wakati wa kuchangia mjadala wa Bajeti ikiwemo ujenzi wa uwanja wa ndege wa Mwanza na Barabara mbalimbali nchini zitashughulikiwa.
Suala la kulipa kodi linaitambulisha nchi kwenye uhuru, uwezo wa kutekeleza miradi ya maendeleo na uwezo wa kujitegemea. Wabunge wanapaswa kuwahimiza wananchi wote kulipa kodi ili nchi iweze kushushwa. Aidha, Waziri Mwigulu amesema kodi zinazotozwa nchini ni kubwa kwa sababu watu wengi hawalipi kodi, mzigo wa kulipa kodi hudondoka kwa watu wachache.
Kuhusu hoja ya mafuta ya kula, Waziri Nchemba amesema wametoa unafuu kwa wazalishaji wa ndani kama motisha kwao, na mabadiliko hayo yatatolewa kwenye jedwali la mabadiliko (Schedule of Amendments). Pia, Serikali itadhibiti uingizwaji holela wa mafuta nchini kama sehemu ya kuwajali wakulima wa ndani.
Amemshauri Mbunge wa Kisesa Lugaha Mpina kuwa si ubingwa wala si ustaarabu kupinga kila kitu hata visipopaswa kupingwa, badala yake anaweza kuuliza kwa namna nzuri ili aeleweshwe. Ameyasema haya wakati akirejea hoja ya Mpina iliyokata biashara zifungiwe.
Ametolea mfano alivyokuwa anafunga viwanda, kuchoma nyavu akiwa Waziri kuwa matendo hayo hayakuwa ya kistaarabu. Watu wa Sekta binafsi sio maadui, ni washirika wa maendeleo.
Katika kufungia biashara za watu ni muhumu kuzingatia mitaji yao, uwekezaji na muda wanaotumia kuwekeza na kufanya biashara hizo. Hauwezi kukaa na mtaji wa mtu umeushikilia huku yeye akiumia.