Hivi ni lazima kila raia alipe kodi? Nini maana ya kuwa na vyanzo vya kodi vyenye nguvu?
Kodi ya voucher ni rahisi kukusanya lakini haina udugu. Maana hata bibi asiye na uwezo akiweka vocha anatozwa kodi.
Lazima kila raia alipe kodi ndiyo uzalendo wa kweli ila watoto, vikongwe au walio na ulemavu wa kushindwa kufanya shughuli wao hawawajibiki kulipa kodi.
Mfano Tanzania daftari la wapiga kura mamilioni wenye kazi sekta kama waajiri serikalini, sekta binafsi na waliojiajiri wauza mitumba, wakulima, wavuvi , wafugaji , madalali, mishemishe za mjini n.k ambao wote hawa wanaendesha maisha yao kwa kazi zao lazima walipe kodi inayofanana na ya PAYE. Jumla yao ni 29,000,000 Idadi ya wapiga kura Tanzania waongezeka
Nadhani hakuna namna nyingine hata hawa kina babu na bibi wanatakiwa kuwa wazalendo hawaoni mabarabara, ma-flyover, stendi za mabasi wilaya zote, hospitali za wilaya / rufani, shule zikichipuka kama uyoga kila kona ya nchi lazima kuna ulazima kuvichangia tunaambiwa hatuna mjomba ktk nchi za Mabeberu alete misaada wakati rasilimali watu mamilioni waTanzania wanaoendesha maisha yao kila siku wapo, na bila kusahsu maliasili, utalii, makampuni n.k vipo nchini Tanzania.
Tupewe elimu ya kweli walipa kodi ya "kichwa" tunaofikia watu 29,000,000