Kurudisha kodi ya kichwa nyakati hizi za ulimwengu ulioendelea ni aibu kubwa. Mwigulu Nchemba kuwa na aibu. Mbona kuna vyanzo mbadala vingi

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
6,273
6,637
Kwanza ieleweke wazi kuwa kodi ya itayolipwa na wananchi kupitia manunuzi ya vocha za simu ni sawa na kodi ya kichwa waliokuwa wanatoza wakoloni kisha tukairithi na baadae kuondolewa miaka tisini baada ya kuwa ni kodi inayodhalilisha watu.

Kwamba ukiongeza salio unakatwa pesa ili kuchangia maendeleo hii ni aibu. Yaani hata wanachi wasiojiweza ambao wakiongeza salio la buku watachachangia kodi? Kisa tu tuna miradi mikakati kama Sgr na hatuna pesa

Kama tunahitaji pesa za kukamilisha miradi mkakati kwa nini tusikusanye kodi kupitia uvuvi wa bahari kuu ambako kuna kodi nyingi inapotea kwa kuibiwa na meli kibao za uvuvi toka mataifa ya kigeni?

Kodi ya kichwa ni aibu kubwa karne hii.
 
Uvuvi wa bahari kuu nao ni mradi mwingine wenye kuhitaji uwekezaji mkubwa, hivyo kwa kuwa hapo awali mliimba mapambio kwa sauti kuu na hamkuona dosari, yafaa tuwe watulivu tukubali yote ili miradi ya kimkakati iweze kukamilika, vinginevyo tukubali vyuma virudi kukaza kwa viwango vile.
 
Uvuvi wa bahari kuu nao ni mradi mwingine wenye kuhitaji uwekezaji mkubwa,hivyo kwa kuwa hapo awali mliimba mapambio kwa sauti kuu,na hamkuona dosari,yafaa tuwe watulivu tukubali yote ili miradi ya kimkakati iweze kukamilika,vinginevyo tukubali vyuma virudi kukaza kwa viwango vile.
Acha upuuzi we bwege. Meli kibao zinatoka nje na kuvua bila kulipa kodi .
 
Kuna kada fulani fulani wakiwamo sungu sungu, wapiga debe, boda boda, mama lishe na wa namna hiyo wanataka wengine tu walipe kodi na ikibidi wafilisiwe kabisa!

Wakiwekewa kodi ya hata shs 1 kwa mwaka panachimbika balaa.

Hawa ndiyo wale wanyonge wenye serikali yao iliyokwenda zake.
 
Ingawa ni kweli bado kuna maeneo mengi ambayo hayajaguswa ili kuwa sehemu ya mapato ya serikali,

Lakini kwenye kodi ya Laini, naunga mkono, watu walipie line zao, Kama mtu ataona mzigo abaki na laini moja, maana hizi laini zimekuwa ni kama sehemu za weengi sana kujipatia kipato kwa njia ya udanganyifu, ingawa pia hilo TCRA inaweza kuwa sehemu ya kulaumiwa
 
Nikiweka 1000 inachukuliwa tsh. 152 VAT. Sifahamu hii kodi mpya ya Mwigulu Nchemba ni nini hasa! Eti anasema anatuhurumia; aache kuhurumia familia yake atuhurumie sisi!. Mwanasiasa hubadilika kulingana na wakati na mtawala aliyepo.
 
Tofautisha kodi ya kichwa ambayo ni direct tax na ya bundle la simu indirect tax sawa na VAT unallipa kwa jinsi unavyotumia hakuna physical coercion kwenye ukusanyaji wake.
Fikiria kodi ya majengo ilivyo kuwa,unaacha shughuli zako unaenda benk saa mbili na nusu asubuhi unapata huduma ya kulipa sh.10000 saa nane mchana,umesimama karibu masaa saba, hivi kweli wangapi watakuwa tayari kupata mateso kama hayo bado wanatoa pesa zao kwa mateso ya kiwango hicho, no bora hivi karibuni kuna wakala Ila bado ilikuwa shifts.
 
Idugunde,
TRA na Wizara ya Fedha wanastahili pongezi kwa kutanua "wigo" wa walipa kodi. Maana waTanzania wengi walikuwa hawapo ktk kumbukumbu za TRA hivyo waTanzania wa wachache wa kundi hili Mamlaka ya Mapato Tanzania - Mapato ya watu binafsi ndiyo walikuwa wanabinywa.
Sisi Tanzania tuko milioni 55, walipa kodi ni milioni 2.2 lazima tufike mahali tujiulize, kwa hiyo utaona kwamba kuna mahali tumeshindwa,” amehoji Magufuli : source : Nukta | Sababu za Tanzania kutokuwa na mapato makubwa ya kodi
Nchi za wenzetu mabeberu kila kitu kinacholipiwa serikali lazima ikusanye kodi ili kuweza kulipia huduma za jamii, usalama, ulinzi , elimu, kujenga miundo-mbinu na kysaidia maendeleo ya kimataifa (misaada).

1624041787098.png www.monitor.co.ug
Only 1 million Ugandans are paying taxes, says URA
number of registered ugandan pay taxes 2021 from www.monitor.co.ug
Monday June 14 2021. fina01pix. The number of registered tax payers in the tax register is 1.7 million people but not all

Nchi nyingi za kiAfrika watu wake wazima wengi hawalipi kodi, mfano kwa Uganda ripoti ya mwaka 2021 mwezi Juni inaonesha watu 1,700,000 ndiyo wanalipa kodi kati ya watu 48,000,000. Hivyo watu 1.7million wanawabeba watu wa Uganda 48 millioni, mamlaka ya Ukusanyaji Kodi Uganda URA inasema hii ni asilimia ndogo sana.

Tukirejea kwetu Tanzania ni muhimu TRA na wizara ya fedha chini ya Dr. Mwigulu Nchemba watuambie ni waTanzania wangapi wachache wanaowabeba mzigo wa wengi wenzao na familia zao ili wajifahamu kuwa kodi kama hii ya kupitia voucher za simu zinawafanya na wale wengi wasiolipa kodi kushiriki kuchangia fuko la kodi ili kuwezesha mahospitali, shule, barabara, meli na treni wazitumiazo wachangie ujenzi na uendeshaji wake.

Nadhani mkoloni hakukubali watu wazima na familia zao mijini na vijijini wasilipe kodi, na ndiyo maana tunasoma na kusimuliwa kazi kubwa ya MaDC ilikuwa kukusanya kodi hadi walisaka watu vijijini na kukamata kuku na mayai ya waTanganyika wakaenda kuyapiga mnada ili kupata kodi ya kuendesha serikali alisema Mzee Stephen Masatu Wasira katika kipindi cha Zumari cha Azam TV kilichorushwa mwezi Juni 17 2021.
Stephen Masatu Wasira

Hii kodi ya voucher za simu ni ya kistaarabu na isiyo na bughudha kama kodi ya kichwa kukamata kuku na mayai au kulazimishwa kwenda kuwa manamba kukata mkonge mbali na mikoa yao kwa miezi sita ili waweze kupata mshahara wa kulipia kodi ya kichwa ya Jerumani au Mwingereza kufuatana na simulizi za mababu zetu waliokuwapo enzi za utawala wa kikoloni.

Tuhahitaji kuwa kila mwaka tufahamu watanzania wangapi watu wazima wamechangia kiasi gani cha kodi moja kwa moja kufuata na vipato vyao wawe wafugaji, mama ntilie, wafanyakazi wa umma, machinga n.k na kodi hiyo inachangia asilimia ngapi ya mapato ktk GDP.

Pia makampuni ya madini, simu, viwanda n.k wamechangia kiasi gani cha kodi ya kampuni Corporate tax.

Mwisho taarifa za kodi zingine za VAT, miamala n.k ambazo siyo za moja kwa moja .

Mwisho serikali ituambie imetumia kiasi gani ktk usalama, ulinzi, elimu, afya na miundo-mbinu kwa kutumia jedwali rahisi kila mtanzania ajue kiasi gani kimetumia na hii itawapa morali watanzania kulipa kodi zaidi maana matumizi yake yapo wazi ya serikali kuu na serikali za mitaa.

Mfano wa taarifa kwa watu wa Marekani juu ya kodi yao :
These four categories—national defense, Social Security, healthcare, and interest payments—account for roughly 73% of all federal spending, as Figure 2 shows. The remaining 27% wedge of the pie chart covers all other categories of federal government spending: international affairs; science and technology; natural resources and the environment; transportation; housing; education; income support for the poor; community and regional development; law enforcement and the judicial system; and the administrative costs of running the government.


The pie chart shows that healthcare (including Medicaid) makes up roughly 26% of federal spending; Social Security makes up 24%; national defense makes up 17%; net interest makes up over 6%; and all other spending makes up over 25%.
Figure 2. Slices of Federal Spending, 2014. About 73% of government spending goes to four major areas: national defense, Social Security, healthcare, and interest payments on past borrowing. This leaves about 29% of federal spending for all other functions of the U.S. government. (Source: https://www.whitehouse.gov/omb/budget/Historicals/)

1624044118698.png
 
Hivi ni lazima kila raia alipe kodi? Nini maana ya kuwa na vyanzo vya kodi vyenye nguvu?

Kodi ya voucher ni rahisi kukusanya lakini haina udugu. Maana hata bibi asiye na uwezo akiweka vocha anatozwa kodi.
 
Back
Top Bottom