Waziri wa fedha, Mwigulu Nchemba: Kodi sio jambo la Rais, kodi sio jambo la Waziri wa Fedha, kodi sio jambo la TRA, kodi ni jambo la Nchi

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,115
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba leo June 15,2023 amewasilisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 Bungeni Jijini Dodoma ambapo moja ya mambo aliyoyasema kwenye hotuba yake ni kwamba kuna baadhi ya Wanasiasa wanasema kodi zinatozwa nchini ni za Rais wa Tanzania Dkt. Samia, za Waziri Mwigulu au za TRA ambapo amesema hiyo sio kweli kwakuwa kodi ni jambo la Nchi.

“Kumezuka dhana ya kuona kuwa kodi zinazotozwa ni kubwa bila kujali mzigo mkubwa wa Serikali kwa nchi yetu katika kugharamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo na utoaji wa huduma za jamii, kuna baadhi ya Wanasiasa wanasema kodi hizi ni za Samia, kodi hizi za Mwigulu, kodi hizi za TRA.

“Kodi zote zinazokusanywa huwekwa kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali uliopo Benki kuu ya Tanzania, na baadae kupelekwa kwenye Wizara za Kisekta, fedha hizo ndizo zinazotumika kugharamia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo iliyopo mijini na vijijini ikiwemo miradi ya umeme, maji, barabara, madaraja, vivuko, reli, usafiri wa anga, madarasa, zahanati, ununuzi na usambazaji wa dawa na malipo ya mishahara ya Watumishi kama Walimu, Wauguzi na Madaktari”

“Kila mmoja wetu ajue kuwa, Kodi sio jambo la Rais, kodi sio jambo la Waziri wa Fedha, kodi sio jambo la TRA, kodi ni jambo la Nchi, kodi ndio maendeleo ya Nchi yetu, kila Mtanzania mwenye sifa za kulipa kodi ana wajibu wa kulipa kodi stahiki na halali kwa mujibu wa sheria, ni lazima kulipa kodi, ni lazima tutumie mashine za EFD bila udhuru wowote, ni lazima kila anayeuza atoe risiti na anayenunua adai risiti”
 
CAG kaanisha upotevu wa ma trillion wa pesa, sisi kama walipo Kodi tuna haki ya kujua pesa zetu zinaenda wapi
 
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba leo June 15,2023 amewasilisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa lazima tutumie mashine za EFD bila udhuru wowote, ni lazima kila anayeuza atoe risiti na anayenunua adai risiti”
Punguzeni ma v8 .mnakusanya kodi halafu mnakuja kuzitawanya kwa njia ya ufisadi
 
Kama kawaida maafisa ubashiri (wazee wa mikeka aka wazee wa kubet),wanywaji na wala fegi wanaendelea kuijenga nchi. Yaani hatuna mbadala wa kuongeza mapato kwa kutumia hizi resources zetu.
 
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba leo June 15,2023 amewasilisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 Bungeni Jijini Dodoma ambapo moja ya mambo aliyoyasema kwenye hotuba yake ni kwamba kuna
Nasisitiza yes yes yes.

Lakini tujibiwe swali hili. Kodi inapotafunwa na kuibiwa ni jukumu la nani kuidai ama kuilinda?
 
Kwa hivyo viwango vya kodi wanajiamulia wananchi wenyewe; siyo yeye na ‘Bi Tozo’. Kama ndio hivyo wananchi atutaki tozo za miamala azifute hayo ndio maamuzi yetu.
 
Tozo nayo ni ya nani ?

20230418_074136.jpg
 
Back
Top Bottom