Kauli ya Waziri wa fedha kuwataka wananchi wasiotaka Too waende Burundi inamaswali mengi sana ya kifasihi na kimantiki. Kwanini hakutamka Kenya wa nchi nyingine akatamka Burundi?

Hii ni pekee ambayo Mhe. Rais na Makamu wake wamefanya safari za kikazi. Ni nchi pekee ambayo imetembelewa na Mhe. Rais muda mfupi baada ya kusainiwa kwa sheria ya mabadiliko ya sheria mbalimbali ikiwemo sheria ya Kodi.

Kusema tuhamie Burundi kwa tone aliyotumia ni kama ameidharau Burundi, na kitu hiki kinatia doha diplomasia yetu na Taifa ilo hasa inapotoka kauli kwa Waziri wa fedha. Pili inaweza kutafairi Kama nchi isiyo zingatia sheria ndio maana Mhe. Wazir kasema ile ni sheria na asiyetaka kutekeleza basi aende Burundi ambapo hakuna sheria. Tatu inaweza kutafsiriwa Kama dharau kwa viongozi wake wa juu kwamba wanaweza kutumia Kodi za wananchi kwenda eneo la ovyo na lisilofuata sheria Kama Burundi? Anawatumia salama kwamba Burundi ni kwa wasio tii.

Kwa mantiki na kwakuzingatia kwamba Mhe. Rais ametuonyesha kuwa Burundi tunaweza kwenda nadhani Sasa tuseme Mwigulu anatukumbusha Tumeandaliwa Makao tuondoke
 
(Hivi sasa ni saa 2:17 usiku)

Nimesikitishwa sana na kauli ya ndugu yetu mweshimiwa ya kututishia uamisho wa ajabu ajabu hivi.

Ijapokuwa kwa sasa sisi wanywaji wa vitu vyetu kausha figo tunatiliana mashaka sana hasa baada ya kuanza kuwa wawili wawili kichwani, maana hatuchelewi kutunguana sisi.

Ukweli nimepokea kwa masikitiko makubwa mikwara hiyo onevu uku ukizingatia sisi atushindwi kumudu hizo tozo umiza abadani!!! Tunatumia shng: ngapi bwana kunywea mibia na mistarehe lukuki iliyojaa nchini hapa? Kama tunaweza kuchangia sherehe na harusi za kilokole zisizokuwa na bia wala K-vant nini shida kuchangia Kodi kwaajiri ya maendeleo ya taifa??

Shida ni jinsi zinavyopangwa, kupitishwa na hata kulazimishwa na kutupiwa mineno mikavu mikavu, niende Burundi mimi? Yaani sijui kwa nini kachagua Burundi huyu, angalau angesema tukimbilie Paris Ufaransa, binafsi naona ametudhalilisha sisi wakwepa Kodi kwa kiasi kikubwa sana.

Tukiachana na hayo ya makodi na nini...Hivi uko Burundi kuna viwanja vikari kweli ? usalama wetu utakuwepo kweli sisi walevi na wazee wa night kali? Maana isije ikawa kama mambo yanayotokea Sinza huku now days. Kuhusu watoto warembo hilo sina shaka nalo kabisaaa maana ni bora huko kuliko kama ungetuambia tuombe nafasi ya ukimbizi wa kukwepa kodi Kenya.

Ombi langu kwako mweshimiwa. Chonde chonde tunaomba utubadilishia makimbilio, kaa chini na ututafutie nchi nyingine na sio Burundi bwana, walau tuelekee visiwani huko usheri sheri maana naskia kuna starehe za kufa mtu huko, au utuombee nafasi za ukimbizi wapi kule....!¡!¡! nimekumbuka Nigeria angalau tukajifunze utapeli na mengineyo kuhusu Boko Haram.

Na nyie wakuu tusivunjiane heshima, haya mambo ya kukosoana lugha na miandiko yetu achaneni nayo kabisa.
Unakuta jitu kutwa linatafuta wapi wengine wamekosea huku alijui kuwa watu wanatingwa na mambo mengi vichwani mara tozo, mara kodi, sijui mauaji kuchomana moto, ukichanganya na hizi konyagi ndio shida kabisaaa.. 💤💤💤💤💤
 
Back
Top Bottom