Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,271
Mh Rais Mama Samia suluhu Hassan bado hujastuka tu kuwa mtu huyu ni hatari katika utawala wako? Waziri wako anadharau amri ya Rais ambayo jana tu asubuhi umemuagiza yeye mwenyewe atwambie kwamba umesikia manung'uniko yetu na kwamba umeziagiza wizara zikae zishughulikie malalamiko yetu wananchi, Kisha siku hiyo hiyo jioni katika kipindi cha tv anazungumza haya?

Idara ya Usalama wa Taifa Tanzania mko wapi mnaacha mtu kama huyu Waziri anakwenda katika Tv kulichafua Taifa na kumchafua Rais wa Nchi? Miiko ya utumishi wa umma na miiko ya viongozi wa Kiserikali juu ya kwenda katika vyombo vya habari iko wapi? Waziri anaongea kwa dharau kuliko hata kibri walichokuwa nacho Makonda, Mnyeti na Sabaya enzi za udikteta?

Waziri anadiriki kusema WANANCHI ambao ndio msingi wa uwepo wa Serikali wanaolalamika tozo hizi wahame nchi waende Burundi? Hivi Mwigulu anajua athari za kidplomasia kusema wananchi wanaolalamika waende Burundi? Kwamba Burundi ni eneo la kishenzi ambalo halina handhi ya utu hivyo yeyote anayolalamika, anayenung'unika au kufedheheka adhabu yake ni kupelekwa Burundi?

Mama umetoka juzi Burundi katika hatua ya kujenga uhusiano wa kidplomasia na nchi washirika na majirani, Kauli hii ya Waziri ni hatari na inadhoofisha juhudi zako zote za kujenga taifa na ushirikiano.

Mwigulu anatakiwa kuondoka katika ofisi ya umma na Serikali ya Tanzania iombe radhi matamshi haya kwamba si msimamo wa serikali bali wa mtu binafsi. Fikiria kesho waziri wa Burundi atangaze kuwa wanaotaka ushoga wote waende Tanzania huko ndio watakuwa mashoga wenye faida, Au Rwanda iseme majambazi wote waende Tanzania huko ndio watafanya ujambazi kwa amani, Au Somali iseme Magaidi wote waende Tanzania huko ndio watafanya ugaidi kwa amani. Nini matokeo ya kauli hizo?

Mama tunakutahadharisha kwa kila kitu juu ya mtu huyu na kundi lake, Maneno huumba, tumeshazungumza mara sita, amini mara ya saba neno litatimia katika umbo kamili. Mwigulu ni hatari kwako Mama na ni hatari kwa usalama wa Tanzania.

 
Ivi kwa nini wana Ccm wamekaa tu bungeni bila upinzani wameanza andaa vikanuni vya kumkandamiza mwananchi wa chini ivi Kwa nin Isifike kipindi wabunge waseme mishahara yao nayoo ikatwe walau 20% Kama kodi na sijui Kama posho zao huwa wanachangia kodi
 
Heeeeh haki ya kujieleza ipo wapi jamani mlioipigania enzi zile🤔! Mwigulu ametumia haki yake ya kikatiba kueleza mtazamo wake! SSH akimtumbua basi ni dictator full stop😡!
 
Mh Rais Mama Samia suluhu Hassan bado hujastuka tu kuwa mtu huyu ni hatari katika utawala wako? Waziri wako anadharau amri ya Rais ambayo jana tu asubuhi umemuagiza yeye mwenyewe atwambie kwamba umesikia manung'uniko yetu na kwamba umeziagiza wizara zikae zishughulikie malalamiko yetu wananchi, Kisha siku hiyo hiyo jioni katika kipindi cha tv anazungumza haya?....
Comment zingine kweli zinachosha, ati anamchafua Rais, hivi anamchfuaje Rais ambaye wala hakuchaguliwa katoka ileile system chafu? Si ndiye alisema hata mkipiga kula upinzani sisi tutatawala? Ana usafi gani huyo?
 
Back
Top Bottom