DOKEZO Kasulu: Eneo la NYAKITONTO, Kamchape wanahatarisha usalama wa raia na Polisi wapo kimya!

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mchawi hapaswi kuishi,maana anafanya kazi isiyo na faida kwake Wala kwa jamii zaidi ya kuwa mateka wa shetani.
 
Subiri hao unaowatetea wakikuulia mwana family yako ksa wivu wa maendeleo ndo akili itakukaa sawa.
 
Hata humu Kuna mijitu pori mingi tu, kupitia comments za Wadau bado tuna Safari kama taifa kufika nchi ya ahadi.
Uchawi, Ujinga, Nyege, Chuki, Magonjwa n.k zimezijaza sana akili zetu waafrica.

Ndio mana wahuni wa kuuza mafuta, keki, maji na chumvi wanajipigia tu pesa
 
Wachawi ni adui wa maendeleo na hawa KAMCHAPE nasikia iliasisiwa na rais baada ya kufanyiwa mazingara alivotembelea Kigoma, ndo akawapa mamlaka ya kuwakomesha wachawi. Sasa hawa wanaowapinga KAMCHAPE itakuwa ndo wachawi wenyewe wanaogopa kuachishwa uchawi wao
 
Ni muda sasa kumekuwepo na hili wimbi la watu wanaojiita kamchape kiboko ya kutoa uchawi katika wilaya ya kasulu.

Mwanzoni Serikali kupitia jeshi la polisi walitoa maonyo kuhusu hawa watu lakini wananchi wengi waliyapuuza.

Kinachotokea sasa wanadhalilisha watu, wanatengeneza chuki dhidi ya wanajamii kupitia ramli yao chonganishi, Wanadhulumu watu pesa zao kidogo kwa ahadi watawasafishia nyumba zao zisiwe na uchawi, wanasambaza magonjwa ya zinaa ikiwemo kaswende na gono.

Kinachotokea katika kata ya Nyakitonto
Watu wanadhalilishwa, wanaibiwa pesa zao ,ndoa zinavunjika, maelewano katika familia yanapotea, raia wasio na hatia wanapigwa, watu wanavunjiwa nyumba zao.

Askari polisi kama walinzi wa usalama wako kimya kuhusu hali hii. Juzi kuna raia asiye na hatia kutokea Kitema kapigwa manusura ya kufa, jana mwananchi asiye na hatia kidogo avunjiwe nyumba yake.

Jeshi la Polisi liko wapi kupinga dhulma hii na uonevu huu au na wenyewe ni sehemu ya kamchape?

Waziri wa Mambo ya Ndani, sikiliza kilio cha hawa wanachi wasio na hatia. Kinachopaliliwa sasa hivi ipo siku kitatoa matunda na matunda hayo itakua ngumu kuyateketekeza.

RPC Kigoma angalia suala hili ni jipu linaloiva litakua kidonda ndugu siku moja. OCD Kasulu umewatelekeza raia wema ambao kila siku wanakupa ushirikiano kudhibiti uhalifu
Wachawi mpigwe tu
 
Wanasambazaje magonjwa ya zinaa mkuu?
 
Back
Top Bottom