Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,808
11,973
Musoma. Kamati maalum ya kitaifa iliyoundwa na serikali kuchunguza mabadiliko ya maji ndani ya mto Mara, imetoa taarifa ya chanzo cha mabadiliko katika mto huo yaliyosababisha maji kuwa meusi na kutoa harufu, huku samaki wakifa ambapo chanzo kimeelezwa kuwa ni shughuli za binadamu pamoja na nguvu za asili.

Akitoa matokeo ya uchunguzi leo Jumamosi Machi 19, 2022 mjini Musoma, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Profesa Samuel Manyele amesema kuwa hali hiyo imetokana na kuwepo kwa kiwango kikubwa cha kinyesi cha mifugo mtoni pamoja na uozo wa mimea ndani ya mto hasa mimea vamizi kama vile magugu maji na matete.

Amesema kuwa hali hiyo ilisababisha kupungua kwa kiasi kikubwa kiwango cha oksijeni ndani ya mto na hivyo maji kubadilika rangi na kuwa na harufu mbaya huku samaki wakikosa chakula na hivyo kusababisha vifo vyao.

Hata hivyo, amekanusha picha zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zilizokuwa zikionyesha samaki wakiwa wamekufa kwa wingi, akisema sio kutoka mkoani Mara.

Amesema kuwa kwa mujibu wa uchunguzi waliofanyana walibaini kuwa mabadiliko hayo ni matokeo ya mvua kubwa iliyonyesha ghafla kwa muda mfupi katika kipindi cha mwezi huu hivyo kutibua uchafu uliokuwa umejikusanya chini ya mto kwa muda mrefu.

"Mvua zingeendelea kunyesha hali hii ingeisha kwani uchafu ungetiririshwa lakini kwa vile mvua zimenyesha na kukatika ghafla ina maana uchafu ule unatoka taratibu na hii hali inaweza kudumu kwa zaidi ya miezi mitatu hadi minne endapo mvua hazitanyesha hapa katikakati," amesema.

Profesa Manyele amesema kuwa mto huo umeathiriwa kuanzia katika kijiji cha Marasibora wilayani Rorya na kijiji cha Wegero wilayani Butiama huku akisema kuwa mgodi wa dhahabu wa Barrick North Mara hauhusiki na uchafuzi huo.

"Mgodi upo mbali sana na maeneo yaliyoathirika na hata kama uchafu unaozalishwa mgodini pale ungezidishwa mara ishirini na kumwagwa mtoni maji yasingebadilika rangi wala kuwa katika hali iivyo sasa na maji ya mto kelekea kule mgodini ni masafi na hayana shida yoyote," amesema.

Amesema kuwa wamebaini uwepo wa kinyesi cha ng'ombe zaidi ya tani 1.8 milioni pamoja na mkojo wa ng'ombe lita 1.5 bilioni uchafu uliotokana na kuwepo kwa ng'ombe zaidi ya laki 3 waliokuwepo katika eneo oevu la mto Mara kwa kipindi cha miezi minane mwaka jana wakati wa kiangazi.

"Ng'ombe mmoja ana toa kilo 25 za kinyesi kwa siku moja na mkojo lita 21 kwa siku kwahiyo ukizidisha kwa idadi hiyo ya ng'ombe mara miezi minane utapata kiwango hicho na hapo bado hatujaweka kinyesi na mkojo wa kondoo, mbuzi na punda," amesema.

Akizungumza baada ya kupokea taarifa hiyo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Suleiman Jafo ametoa muda wa siku mbili kwa kamati hiyo kuandaa taarifa kamili yenye mpango kazi juu ya nini kifanyike na muhusika ni nani kisha taarifa hiyo ikabidhiwe kwake kwaajili ya utekelezaji.

"Hii taarifa imenipa faraja baada ya uchunguzi kubaini kuwa hakuna kemikali mtoni maana kama kungekuwa na kemikali hii ingekuwa ni habari mbaya sana lakini taarifa hii inaonyesha kuwa tuna kazi kubwa sana ya kufanya ili mto uweze kuendelea kuwepo na tusipochukua hatua za haraka mto unaweza kupotea," amesema Jafo.

Chanzo: Mwananchi

Pia soma;

1).Vifo vya Samaki Mto Mara: Kamati ya Dharura yaundwa kuchunguza Samaki wanaodaiwa kufa kwa Sumu

2). Madai ya sumu Mto Mara kutoka migodini, wananchi wazuiwa kutumia maji, kula samaki, uvuvi, Serikali yatoa tamko
IMG_20220319_184222_465.jpg
 
Ngombe hawa hawa wa mara mmoja anakunya kinyesi cha kg 25 na mkojo lita 21..???

Hivi wanaficha nini kwa manufaa ya nani?..hivi hiyo mifugo imeanza kufungwa mwaka huu maeneo hayo..mbona hayakuwahi kutokea hayo.?

Nadiriki kusema hii ni moja ya kamati za michongo...hivi wanadhani watanzania wasasa ni vilaza sana kwamba hawajui kuhoji au ku reason.

Eti mwenyekiti wa kamati ni professor..daah hii nchi kuna mambo yanakera sana..

Hivi hamna huruma na wananchi kansa kila uchwao zinaongezeka kanda ya ziwa..magonjwa ya ajabu ajabu..sasa hadi samaki wanakufa..ila mnaleta ngonjera.

#MaendeleoHayanaChama
 
Taarifa ya Bodi ya maji bonde la ziwa victoria walisema Chanzo ni mafuta.

Taarifa yao hii hapa chini

Uchunguzi huo umeanza kufanyika Machi 8, 2022 baada ya bodi hiyo kupokea taarifa ya uwepo wa uchafuzi wa maji uliosababisha maji kuwa meusi na kufa kwa samaki katika mto Mara kwenye eneo la Kirumi Darajani.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 12 jijini Mwanza, Mkurugenzi wa bodi hiyo, Renatus Shinhu ametaja vijiji vilivyoathirika kutokana na uchafuzi huo kuwa ni Kirumi, Kwibuse, Marasibora, Ketasakwa na Ryamisanga.

“Uchunguzi wa kimaabara umeonesha mambo mawili ikiwemo kuwepo kwa kiwango kikubwa cha mafuta kuliko kiwango kinachokubalika kwa mujibu wa viwango vya ubora wa maji Tanzania (TZs 2068:2017),” amesema Shinhu.

Amesema sampuli ya maji iliyochukuliwa Machi 8 mwaka huu ilionyesha kuna kiwango sifuri cha Oksijeni katika eneo la Kirumi huku siku tatu baadae kiwango hicho kikiongezeka na kufikia asilimia mbili ambayo inaelea moja kufikia kiwango cha kawaida kinachohitajika kwa viumbe wanaoishi ndani ya mto huo.

"Kiwango kikubwa cha mafuta kwenye maji ndicho kilichosababisha kuisha kwa hewa ya okisijeni kwenye maji na kuathiri viumbe hai ikiwa ni pamoja na samaki hivyo tunaendelea kufanya utafiti kubaini kwa undani yalipotoka mafuta hayo," amesema.

Wakati LVBWB ikitoa taarifa hiyo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Selemani Jaffo ameunda kamati maalum ya kitaifa itakayofanya uchunguzi wa chanzo cha mabadiliko katika mto Mara yaliyosababisha maji ya mto huo kubadilika rangi na kuwa nyeusi.

Chanzo Mwananchi. "Chanzo cha samaki kufa mto Mara chatajwa | Mwananchi" Chanzo cha samaki kufa mto Mara chatajwa | Mwananchi

Hawa wapumbavu wanatugeuza sisi wajinga
 
Ng'mbe mmoja kinyesi 25kg kwa siku + 21 Lita za mkojo???????????? Sijawahi kufuga lakini hapa....Ngumu kumeza
Huyo sio ng'ombe bali ni faru Jon..jamaa wanataka kutufanya sisi wajinga sana...

Tukisema hii nchi imelaaniwa nadhani tumeanza kueleweka sasa..swali moja tu la kuwauliza je hiyo mifugo imeanza kufungwa mwaka huu kandokando ya huo mto?

#MaendeleoHayanaChama
 
Viongozi, wataalamu na wasomi wakitanzania hawalisaidii taifa Bali ndio wakwanza kulizamisha taifa.

Wasomi wengi wamekuwa waroho, wachoyo na kujifanya wajinga ili wapate vyeo waendeleze unafki wapate kuvimbiwa pasipo haki mradi tuu wanasifia viongozi waliopo madarakan
 
Ma proffesa siku hizi wamekuwa washenzi sana sijapata logic yoyote hapo, ngoja nimalize kupata kinywaji hapa nikapitie mafaili yangu kwenye mechanism kadhaa na baadha ya tafiti tuanze kumpinga kwa tafiti.

Bila shaka atakuwa amedhalilisha ma profesa wenzake, na hapa inaonesha moja kwa moja serikali haiko radhi kumsumbua muwekezaji kwa sababu wao wanafikiria kukusanya mapato na si kulinda afya za watanzania na viumbe asilia.

Kwa hii ripoti serikali imepotosha
 
Mtu na pesa zake eeh
Anaweza kuhamisha mito milima na mabonde
Lakini akumbuke Mungu hapokei rushwa
Ni up.umbavu wa hali juu kufikiria kuwa eti kuna sumu za mgodini zingesababisha samaki kufa mto Mara. Ni fikra za kijinga kabisa kutoka kwa wajinga wasiojua chochote kuhusiana na shughuli za mineral processing.

Mgodi wa North Mara, mahali uliko halafu eti ukasababishe vifo vya samaki mto Mara, hata akili ndogo ya kawaida inakataa.

Kwanza ni sumu gani ambayo ingeweza kutembea toka mgodi wa North Mara mpaka ikafike mto Mara ikiwa bado ina nguvu ya kuua viumbe majini? Chemical pekee yenye sumu kali inayotumika kwenye mineral processing ni Sodium cyanide, ambayo kwa muda mfupi ikiwa exposed kwenye hewa hupoteza nguvu yake. Chemicals nyingine ni acids, ambazo zingeingia majini zingekuwa diluted kutokana na uwingi wa maji.
 
Back
Top Bottom