JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,308
- 5,458
Juzi kati niliona memba humu JF akiandika juu ya taarifa za kemikali zenye sumu kutoka mgodini zilivyoharibu mazingira kwenye Mto Mara na kusababisha vifo vya samaki na pamoja maji kuwa meusi.
Baadaye habari hiyo ikasambaa na kuwa kubwa mwisho Serikali ikiingilia kati na kufanya uchunguzi kuhusu taarifa hizo.
Ripoti ya awali ikatolewa, wakagusia kuwa hakuna sumu bali ni mafuta ndiyo maana Oksijeni ikawa ndogo kwenye maji, wakasema wanaendelea kuchunguza kwa nini maji yamekuwa meusi.
……………………
NANUKUU KILICHOSEMWA SIKU HIYO…
“Akizungumza na waandishi wa habari Machi 12, 2022 jijini Mwanza, Mkurugenzi wa Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria (LVBWB), Renatus Shinhu ametaja vijiji vilivyoathirika kutokana na uchafuzi huo kuwa ni Kirumi, Kwibuse, Marasibora, Ketasakwa na Ryamisanga.
“Uchunguzi wa kimaabara umeonesha mambo mawili ikiwemo kuwepo kwa kiwango kikubwa cha mafuta kuliko kiwango kinachokubalika kwa mujibu wa viwango vya ubora wa maji Tanzania (TZs 2068:2017),” amesema Shinhu.
MWISHO WA KUNUKUU
…………………….
Sasa baada ya ripoti hiyo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Selemani Jaffo akaunda kamati maalum ya kitaifa kuchunguza chanzo cha mabadiliko katika Mto Mara yaliyosababisha maji ya mto huo kubadilika rangi na kuwa nyeusi.
Ndipo ripoti hiyo ya leo Jumamosi Machi 19, 2022 ikatolewa ikiwa na sababu nyingine tofauti, yenyewe ikisema kuwa eti wingi wa kinyesi cha ng’ombe na mkojo ndiyo sababu ya maji kuwa meusi na hatimaye kusababisha vifo vya Samaki wengi.
Inafikirisha kidogo, sasa kufikia hapo tumuamini nani, wale waliosema Samaki wanakufa kwa sababu ya mafuta kuwa mengi tena wakataja kabisa kuwa ni Dizel na Petrol, hawa wengine wanatuaminia kinyesi…
…………………….
NANUKUU RIPOTI YA KAMATI MAALUM YA KITAIFA ILIYOUNDWA NA SERIKALI
Akitoa matokeo ya uchunguzi Jumamosi Machi 19, 2022 mjini Musoma, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Profesa Samuel Manyele amesema kuwa hali hiyo imetokana na kuwepo kwa kiwango kikubwa cha kinyesi cha mifugo mtoni pamoja na uozo wa mimea ndani ya mto hasa mimea vamizi kama vile magugu maji na matete.
Amesema kuwa hali hiyo ilisababisha kupungua kwa kiasi kikubwa kiwango cha oksijeni ndani ya mto na hivyo maji kubadilika rangi na kuwa na harufu mbaya huku samaki wakikosa chakula na hivyo kusababisha vifo vyao.
MWISHO WA KUNUKUU
…………………………………..
Baada ya hapo nimewatafuta wataalamu wawili wa masuala ya ufugaji, mmoja ni kutoka Serikalini na mwingine ni sekta binafsi na kuwauliza kuhusu uwezekano wa samaki kufa wengi kutokana na kinyesi na mkono wa ng’ombe, hawa hapa wanafafanua…
Mtaalam wa kwanza
“Kwa kawaida kinyesi cha ng’ombe huwa ni sehemu ya chakula kwa Samaki na viumbe wengine kwenye maji, ndiyo maana kwenye mabwawa yanayofuga Samaki huwa ni kawaida kuona wafugaji wakitumia kinyesi hicho kwa ajli ya chakula cha Samaki.
“Ikitokea kwenye bwawa unalofugia kinyesi kikawa kingi kupitiliza kinaweza kusababisha kukosekana kwa oksijeni kutokana na kuziba njia kwa juu, hali hiyo ikiendelea kwa muda inaweza kusababisha samaki wakafa kweli.
“Lakini kwa sehemu kama mto au ziwa au bwawa kubwa mara nyingi kinyesi kikiwa kingi kinasambaa hivyo kinayeyushwa, tena kwenye mto au ziwa ni ngumu zaidi kusema kinyesi kimeziba na kukosekana kwa oksijeni.
“Ni ngumu kuona kinyesi kimeziba oksijeni kwenye mto wakati unajua maji ni mengi na kadiri kinyesi kinavyoingia kwenye maji ndivyo kinavyosambaa.
“Kingine ni kuwa kama kweli hali hiyo imetokea unatakiwa kujiuliza imetokea kwa muda gani, yaani imechukua muda mrefu kiasi gani hadi hali hiyo ikatokea, kama ni ndani ya muda mfupi basi hilo ni tatizo lingine, kama ni muda mrefu inamaanisha mlundikano huo ulitakiwa kuonekana mapema na siyo ghafla.
“Kitaalam ikitokea samaki wengi wamekufa kwenye mto au ziwa au bahari ndani ya muda mfupi basi hapo kuna tatizo, ama kuna sumu au kuna kemikali ambao haziendani na samaki.”
Mtaalam wa pili
“Inapotokea kuna magugu au majani mengi kwenye maji kisha kukawa na kinyesi kingi kinajaa kwenye maji, oksijeni itakosekana na itahatarisha maisha ya samaki.
“Hilo linaweza kutokea lakini iwe ni katika sehemu ndogo ya maji ambayo inakuwa na mrundikano wa vitu nilivyoeleza hapo juu, lakini kusema tu ni kinyesi na mkono, swali ni kuwa hali hiyo imetokea kwa muda gani yaani namaanisha mrundikano umechukua miezi mingapi?
“Kingine kinachonipa wasiwasi kuhusu hiyo ripoti ni kuwa maji yamekuwa meusi, hilo kitaalamu sina hakika nalo, ingekuwa imetokea kwenye kibwawa kidogo nisingekuwa na wasiwasi, lakini maji kuwa meusi kwenye mto kisa mikojo na kinyesi nafikiri nahitaji kujifunza zaidi kutoka kwa hao wataalam.”
Pia soma...
Madai ya sumu Mto Mara kutoka migodini, wananchi wazuiwa kutumia maji, kula samaki, uvuvi, Serikali yatoa tamko
Vifo vya Samaki Mto Mara: Kamati ya Dharura yaundwa kuchunguza Samaki wanaodaiwa kufa kwa Sumu