Dodoma: Vyama vingine 6 vyajitokeza kupinga maandamano yaliyoitishwa na Chadema

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
617
1,800
Vyama 6.jpg

Wakati zikiwa zimesalia siku sita kabla ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kufanya maandamano, vyama vya ACT Wazalendo, CUF, NCCR Mageuzi, AAFP, ADC na Demokrasia Makini vimesema havitashiriki na haviungi mkono kufanyika kwake.

Wakizungumza mbele ya waandishi wa habari leo Alhamisi, Januari 19, 2014 Jijini Dodoma, wenyeviti wa vyama hivyo mkoani hapa wamesema kuwa hawaungi mkono maandamano hayo kwani vyama hivyo vina njia zake za kudai haki nje ya maandamano.

Juzi vyama 13, vilijitokeza kupinga maandamano yaliyoitishwa na Chadema, hivyo kujitokeza kwa vyama hivi sita mkoani Dodoma ni mwendelezo wa kutounga mkono kilichosemwa siku chache zilizopita na Mwenyekiti wa Chadema Freeman, Mbowe aliyetangaza mpango huo.

Kati ya vyama hivyo sita vilivyojitokeza jana mkoani Dodoma, ni CUF peke yake yenye diwani mmoja kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Chemba na diwani mmoja Kondoa Vijiji.

Mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo Mkoa wa Dodoma, Yohana Musa amesema chama chake hakiungi mkono maandamano hayo, kwani chama hicho kina njia zake za kudai haki kwa mujibu wa katiba ya nchi.

Musa amesema hawatashiriki kwenye maandamano hayo, kwani mpaka sasa bado haijafahamika kama maoni waliyoyatoa kwenye kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria yamechukuliwa au yameachwa.

“Hayo ni maoni ya Chadema ya kudai haki kwa njia ya maandamano, lakini sisi tunajua Taifa kwanza leo na kesho na kama itatokea maoni yetu hayajachukuliwa tutajua namna ya kufanya na siyo kuiga wenzetu wanachokifanya,” amesema Musa na kuongeza:

“Sasa wewe ukimuona jirani yako anampiga mkewe kwa sababu amemfumania au anatembea nusu uchi na wewe utarudi nyumbani uanze kumpiga mkeo bila sababu eti kwa sababu tu jirani anampiga mkewe?”

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CUF Mkoa wa Dodoma, Steven Chitema amesema chama hicho hakiungi mkono maandamano ya Chadema, kwani mpaka muda huu hawajapata ujumbe wowote kuhusu maandamano hayo kutoka ngazi ya juu.

Amesema chama hicho kina mfumo mzuri wa kupeana taarifa pale linapotokea jambo lakini mpaka sasa hawajapokea taarifa zozote kuhusu maandamano hayo.

Amewataka wanachama wa CUF kujiandaa na uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika mwaka huu na Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwaka 2025 ili waweze kushiriki kikamilifu.

Naye Laila Tivuta kutoka chama cha ADC, amesema chama hicho kinaunga mkono maoni yaliyotolewa na viongozi wa kitaifa wa chama hicho kuhusu miswada iliyowasilishwa bungeni Novemba mwaka jana na wanaamini kamati itayafanyia kazi maoni yao waliyoyatoa bila kuyaacha.

Baraka Machumu kutoka chama cha Demokrasia Makini, amesema maoni yao kuhusu wakurugenzi na makatibu kata kutosimamia uchaguzi yazingatiwe kwani hawatendi haki katika kuwatangaza washindi na maandalizi hayo yaanze mapema kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa haujafanyika.

Hata hivyo jana, Kamati ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imewasilisha serikalini awamu ya kwanza ya rasimu ya uchambuzi wa sheria tatu za uchaguzi baada ya kupokea maoni kutoka kwa makundi mbalimbali.

Mwananchi

==========For English Audience Only=========
6 Opposition Parties Distance Themselves from Upcoming CHADEMA Protests

As one of the oppostion political party CHADEMA (Chama Cha Mapinduzi) prepares for national wide peaceful protests in 6 days to come. Six other opposition parties including ACT Wazalendo, CUF, NCCR Mageuzi, AAFP, ADC and Demokrasia Makini, have announced their decision of not participating and they have disapproved the scheduled demonstrations.

During a press conference in Dodoma on Thursday, January 19, 2014, the chairpersons of these parties declared that their parties are not will not be a part of the upcoming protests, emphasizing that their respective parties have alternative avenues for demanding justice outside of public demonstrations.

This follows the recent stance taken by 13 opposition parties against CHADEMA's call for protests, making the participation of these six parties in Dodoma a continuation of the trend.

Yohana Musa, the Chairman of ACT Wazalendo in Dodoma, stated that his party does not support the planned demonstrations, as they believe in pursuing their rights through constitutional means. He affirmed that they will not participate in the protests, emphasizing that it remains unclear whether the opinions presented to the Parliamentary Permanent Committee on Administration, Constitution, and Legal Affairs have been considered.

Chitema, the Chairman of CUF in Dodoma, echoed the sentiment, stating that CUF does not endorse CHADEMA's protests, as they have not received any official communication regarding the demonstrations from higher party authorities.

Laila Tivuta from ADC expressed support for the national leaders' opinions on the bills presented to parliament last November, expressing confidence that their input would be considered by the committee.

Baraka Machumu of Demokrasia Makini urged that their concerns about directors and ward secretaries not overseeing elections be addressed, emphasizing the need for fairness in declaring winners, and called for early preparations ahead of local elections.

However, the Bunge Committee on Administration, Constitution, and Legal Affairs presented the first phase of the analysis of three election-related bills to the government after receiving input from various groups.
 
Kwani maandamao ni ya vyama vyote au CHADEMA?
Halafu Ccm wanavyo ufanya wajinga ni hapo. Sheria hairuhusu muungano wa vyama vya siasa. Ila kwenye matamko ya kishenzi, Ccm ina kusanya mataei yake, ina wanunulia suti, inanwalipia press na kuwapa hela, na kuwaambia watoe tamko. Msajili feki ambae ni Ccm kindakindaki ana kaa kimya. Haoni wala hasikii.
 
Hivyo vyama Sita, ukiondoa Act wazalendo Zanzibar, havifikishi wanachama hata laki 2 kwa ujumla wake 🤔
 
View attachment 2876303

Wakati zikiwa zimesalia siku sita kabla ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kufanya maandamano, vyama vya ACT Wazalendo, CUF, NCCR Mageuzi, AAFP, ADC na Demokrasia Makini vimesema havitashiriki na haviungi mkono kufanyika kwake.

Wakizungumza mbele ya waandishi wa habari leo Alhamisi, Januari 19, 2014 Jijini Dodoma, wenyeviti wa vyama hivyo mkoani hapa wamesema kuwa hawaungi mkono maandamano hayo kwani vyama hivyo vina njia zake za kudai haki nje ya maandamano.

Juzi vyama 13, vilijitokeza kupinga maandamano yaliyoitishwa na Chadema, hivyo kujitokeza kwa vyama hivi sita mkoani Dodoma ni mwendelezo wa kutounga mkono kilichosemwa siku chache zilizopita na Mwenyekiti wa Chadema Freeman, Mbowe aliyetangaza mpango huo.

Kati ya vyama hivyo sita vilivyojitokeza jana mkoani Dodoma, ni CUF peke yake yenye diwani mmoja kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Chemba na diwani mmoja Kondoa Vijiji.

Mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo Mkoa wa Dodoma, Yohana Musa amesema chama chake hakiungi mkono maandamano hayo, kwani chama hicho kina njia zake za kudai haki kwa mujibu wa katiba ya nchi.

Musa amesema hawatashiriki kwenye maandamano hayo, kwani mpaka sasa bado haijafahamika kama maoni waliyoyatoa kwenye kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria yamechukuliwa au yameachwa.

“Hayo ni maoni ya Chadema ya kudai haki kwa njia ya maandamano, lakini sisi tunajua Taifa kwanza leo na kesho na kama itatokea maoni yetu hayajachukuliwa tutajua namna ya kufanya na siyo kuiga wenzetu wanachokifanya,” amesema Musa na kuongeza:

“Sasa wewe ukimuona jirani yako anampiga mkewe kwa sababu amemfumania au anatembea nusu uchi na wewe utarudi nyumbani uanze kumpiga mkeo bila sababu eti kwa sababu tu jirani anampiga mkewe?”

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CUF Mkoa wa Dodoma, Steven Chitema amesema chama hicho hakiungi mkono maandamano ya Chadema, kwani mpaka muda huu hawajapata ujumbe wowote kuhusu maandamano hayo kutoka ngazi ya juu.

Amesema chama hicho kina mfumo mzuri wa kupeana taarifa pale linapotokea jambo lakini mpaka sasa hawajapokea taarifa zozote kuhusu maandamano hayo.

Amewataka wanachama wa CUF kujiandaa na uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika mwaka huu na Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwaka 2025 ili waweze kushiriki kikamilifu.

Naye Laila Tivuta kutoka chama cha ADC, amesema chama hicho kinaunga mkono maoni yaliyotolewa na viongozi wa kitaifa wa chama hicho kuhusu miswada iliyowasilishwa bungeni Novemba mwaka jana na wanaamini kamati itayafanyia kazi maoni yao waliyoyatoa bila kuyaacha.

Baraka Machumu kutoka chama cha Demokrasia Makini, amesema maoni yao kuhusu wakurugenzi na makatibu kata kutosimamia uchaguzi yazingatiwe kwani hawatendi haki katika kuwatangaza washindi na maandalizi hayo yaanze mapema kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa haujafanyika.

Hata hivyo jana, Kamati ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imewasilisha serikalini awamu ya kwanza ya rasimu ya uchambuzi wa sheria tatu za uchaguzi baada ya kupokea maoni kutoka kwa makundi mbalimbali.

Mwananchi
Hiyo ni misukule ya CCM
 
Msikilize mzee Mkongwe kwenye Siasa mzee wa Ubwabwa kashabariki hivi ndo vyama hata bikipinga vinafahamika
 
Kwani maandamano yanafanyika Dar es salaam au Ni NChi Nzima..
Maana maandamano ya DAR anayejibu wa Dodoma
 
Kwani maandamao ni ya vyama vyote au CHADEMA?

Hawa na wametumwa kusaidia CCM. Wanachotaka kufanya hawa maCCM ni kujaribu kuonyesha kuwa CDM ni wakorofi ndiyo maana hakuna chama kinacho wamsupport. Maandamano yanafanyika Dar wao Dodoma wanareact.....!!?

Mbona CCM wakiwa na maandamano yao ya amani ya kumoongeza Rais huwa haeatoi matamko...!!?
 
View attachment 2876303

Wakati zikiwa zimesalia siku sita kabla ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kufanya maandamano, vyama vya ACT Wazalendo, CUF, NCCR Mageuzi, AAFP, ADC na Demokrasia Makini vimesema havitashiriki na haviungi mkono kufanyika kwake.

Wakizungumza mbele ya waandishi wa habari leo Alhamisi, Januari 19, 2014 Jijini Dodoma, wenyeviti wa vyama hivyo mkoani hapa wamesema kuwa hawaungi mkono maandamano hayo kwani vyama hivyo vina njia zake za kudai haki nje ya maandamano.

Juzi vyama 13, vilijitokeza kupinga maandamano yaliyoitishwa na Chadema, hivyo kujitokeza kwa vyama hivi sita mkoani Dodoma ni mwendelezo wa kutounga mkono kilichosemwa siku chache zilizopita na Mwenyekiti wa Chadema Freeman, Mbowe aliyetangaza mpango huo.

Kati ya vyama hivyo sita vilivyojitokeza jana mkoani Dodoma, ni CUF peke yake yenye diwani mmoja kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Chemba na diwani mmoja Kondoa Vijiji.

Mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo Mkoa wa Dodoma, Yohana Musa amesema chama chake hakiungi mkono maandamano hayo, kwani chama hicho kina njia zake za kudai haki kwa mujibu wa katiba ya nchi.

Musa amesema hawatashiriki kwenye maandamano hayo, kwani mpaka sasa bado haijafahamika kama maoni waliyoyatoa kwenye kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria yamechukuliwa au yameachwa.

“Hayo ni maoni ya Chadema ya kudai haki kwa njia ya maandamano, lakini sisi tunajua Taifa kwanza leo na kesho na kama itatokea maoni yetu hayajachukuliwa tutajua namna ya kufanya na siyo kuiga wenzetu wanachokifanya,” amesema Musa na kuongeza:

“Sasa wewe ukimuona jirani yako anampiga mkewe kwa sababu amemfumania au anatembea nusu uchi na wewe utarudi nyumbani uanze kumpiga mkeo bila sababu eti kwa sababu tu jirani anampiga mkewe?”

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CUF Mkoa wa Dodoma, Steven Chitema amesema chama hicho hakiungi mkono maandamano ya Chadema, kwani mpaka muda huu hawajapata ujumbe wowote kuhusu maandamano hayo kutoka ngazi ya juu.

Amesema chama hicho kina mfumo mzuri wa kupeana taarifa pale linapotokea jambo lakini mpaka sasa hawajapokea taarifa zozote kuhusu maandamano hayo.

Amewataka wanachama wa CUF kujiandaa na uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika mwaka huu na Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwaka 2025 ili waweze kushiriki kikamilifu.

Naye Laila Tivuta kutoka chama cha ADC, amesema chama hicho kinaunga mkono maoni yaliyotolewa na viongozi wa kitaifa wa chama hicho kuhusu miswada iliyowasilishwa bungeni Novemba mwaka jana na wanaamini kamati itayafanyia kazi maoni yao waliyoyatoa bila kuyaacha.

Baraka Machumu kutoka chama cha Demokrasia Makini, amesema maoni yao kuhusu wakurugenzi na makatibu kata kutosimamia uchaguzi yazingatiwe kwani hawatendi haki katika kuwatangaza washindi na maandalizi hayo yaanze mapema kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa haujafanyika.

Hata hivyo jana, Kamati ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imewasilisha serikalini awamu ya kwanza ya rasimu ya uchambuzi wa sheria tatu za uchaguzi baada ya kupokea maoni kutoka kwa makundi mbalimbali.

Mwananchi
Tabia ya chama tawala kuanzisha vyama na kuviita vyama vya upinzani ni ya siku nyingi sana.
Hivyo vyama sanamu vya upinzani vinajiandaa na uchaguzi vikijua kuwa vinasindikiza tu wala haviendi kushindana. Ndio maana Kenya wametuacha mbali na wanatucheka.
 
Hao wote ni machawa wanaotumiwa na Samia kudhihirisha uchu wake wa madaraka
 
Back
Top Bottom