Mbunge wa Ukonga Jerry Slaa, amesema imefikia hatua Wabunge waanze kulipa kodi kupitia mishahara yao ili wapate uwezo wa kuwaambia Wananchi na wao walipe kodi.

Silaa ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara uliowashirikisha wananchi wa Mzinga Ukonga jijini Dar es Salaam wakati akizungumzia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Maendeleo jimboni kwake.

"Mie nimeanza Ubunge juzi mwaka jana mwezi wa 11, kwahiyo nimekuta hayo yanayosemwa mengine yameshapitishwa tayari Bungeni na katika hili niungane na Mbunge wa Kinondoni, Abbas Tarimba kwamba vikiliwa vya Mwali na vya Kungwi viliwe”

“Ni wakati muafaka sisi Waheshimiwa Wabunge ili tupate uwezo wa kuwaambia Watu waanze kulipa kodi na sisi tuanze kulipa kodi katika mishahara yetu, hakuna sababu ya kuwa wengine wanalipa wengine hawalipi ukishakuwa haulipi unakosa ile nguvu ya kumwambia mwenzako alipe”

“Kwahiyo niseme tu kwamba kazi kubwa inayotakiwa tuifanye sisi kama viongozi ni kutowadanganya Watanzania kwamba tunaweza kuiendesha nchi bila Kodi, haitowezekana”-Jerry Silaa
View attachment 1864641

Sanamu lake lichongwe na kuwekwa makao makuu ya nchi Dodoma.
 
Hili kwA kweli liikua na bado ni jambo la aib,,,hebu nisaidieni awamu zote tokea ya kwanza,wabunge walikua hawalipi kodi?
 
Namuunga mkono Mh.Mbunge wangu......

It's a waking up call.....

Wabunge waanze kukatwa Kodi katika mishahara yao!

#NikoNaMbungeWanguMh.Silaa
#KaziIendelee
Jitahidi lakini huko CCM wenzio hawataki akili hizo. Kwanza hilo halimo kwenye ilani yenu.
 
Mbunge wa Ukonga Jerry Slaa, amesema imefikia hatua Wabunge waanze kulipa kodi kupitia mishahara yao ili wapate uwezo wa kuwaambia Wananchi na wao walipe kodi.

Silaa ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara uliowashirikisha wananchi wa Mzinga Ukonga jijini Dar es Salaam wakati akizungumzia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Maendeleo jimboni kwake.

"Mie nimeanza Ubunge juzi mwaka jana mwezi wa 11, kwahiyo nimekuta hayo yanayosemwa mengine yameshapitishwa tayari Bungeni na katika hili niungane na Mbunge wa Kinondoni, Abbas Tarimba kwamba vikiliwa vya Mwali na vya Kungwi viliwe”

“Ni wakati muafaka sisi Waheshimiwa Wabunge ili tupate uwezo wa kuwaambia Watu waanze kulipa kodi na sisi tuanze kulipa kodi katika mishahara yetu, hakuna sababu ya kuwa wengine wanalipa wengine hawalipi ukishakuwa haulipi unakosa ile nguvu ya kumwambia mwenzako alipe”

“Kwahiyo niseme tu kwamba kazi kubwa inayotakiwa tuifanye sisi kama viongozi ni kutowadanganya Watanzania kwamba tunaweza kuiendesha nchi bila Kodi, haitowezekana”-Jerry Silaa
View attachment 1864641
Bora huyu lakini inatakiwa hiyo hoja yake aipeleke kabisa bungeni
 
Hivi kigezo gani kilitumika ili kusema wabunge wasilipe kodi?
This is very unfair kwa wananchi wengine. Wote tulipe kodi bila kubagua.
Si wanadai kuwa mishahara yao (wabunge) inatumika kulipia mahitaji ya wapiga kura wao, suala ambalo halina ukweli wowote. Hawana aibu hata kusema wapiga kura wao huwafuata mpaka bungeni kuwapelekea shida zao.
 
Nimependa hapo kwenye parandesi

Vikiliwa vya Mwali nadhan hapa anazungumzia k bila Shaka bas muoji atest na k ya kungwi pia Kama kwel kungwi alikuwa na viwango vya kumfunda mwali

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Bwana mdogo muhuni sana anatumia kigezo cha kodi ili kudai kupanda mishahara ya wabunge apo lazima watadai mishahara ipande kwanza ili waweze kulipa kod
 
Mbunge wa Ukonga Jerry Slaa, amesema imefikia hatua Wabunge waanze kulipa kodi kupitia mishahara yao ili wapate uwezo wa kuwaambia Wananchi na wao walipe kodi.

Silaa ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara uliowashirikisha wananchi wa Mzinga Ukonga jijini Dar es Salaam wakati akizungumzia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Maendeleo jimboni kwake.

"Mie nimeanza Ubunge juzi mwaka jana mwezi wa 11, kwahiyo nimekuta hayo yanayosemwa mengine yameshapitishwa tayari Bungeni na katika hili niungane na Mbunge wa Kinondoni, Abbas Tarimba kwamba vikiliwa vya Mwali na vya Kungwi viliwe”

“Ni wakati muafaka sisi Waheshimiwa Wabunge ili tupate uwezo wa kuwaambia Watu waanze kulipa kodi na sisi tuanze kulipa kodi katika mishahara yetu, hakuna sababu ya kuwa wengine wanalipa wengine hawalipi ukishakuwa haulipi unakosa ile nguvu ya kumwambia mwenzako alipe”

“Kwahiyo niseme tu kwamba kazi kubwa inayotakiwa tuifanye sisi kama viongozi ni kutowadanganya Watanzania kwamba tunaweza kuiendesha nchi bila Kodi, haitowezekana”-Jerry Silaa
View attachment 1864670
Wanafiki wakubwa hawa, wakiwa bungeni wanakaa kimya wakija huku nje wanabwabwaja
 
Kwani alipoliongelea hapo HATASIKIWA NA WABUNGE WENZAKE?!!

Hayo ni maandalizi ya KULIONGEA BUNGENI.....

It's a waking up call....

#HayaNdiyoMambo
#NchiKwanza
#KaziInaendelea
 
Back
Top Bottom