Nawasalimu wakuu!

Kiukweli kilio hiki kimetutia simanzi wengi saana aswaa wale tunaoelewa tu tafsiri ya msiba. Kimsingi katika maisha yangu ya jeshini, nilifundishwa vitu vingi saana lakini nilichokizingatia hadi leo ni pale tulipoambiwa katika unatakiwa kupigia saluti maiti yeyote ile iwe ya Mwanajeshi, Raia, mwizi, na hata mheshimiwa ili mradi iwe ya binadamu. Hii ilikuwa ni kwa ajili ya kuonyesha respect na kwa mtu yeyote aliyefariki.

Mwalimu Nyerere wakati anang'atuka aliwahi kusema hivi "Kwenye uongozi wangu nimefanya mengi, mengine mema mengine ya kijinga lakini fuateni yale mema ya kijinga myaache"

Vivyo hivyo kwa Magufuli! Kafanya mengi mengine mema mengine ya kijinga.

Mema yake ndio dhumuni la uzi huu.

Kwanza namsifu kwa kuyaishi maneno yake angetaka kwenda kokote Duniani kutibiwa angeweza lakini katibiwa kwenye hospitali ya nchini kwake na kufariki hapo hapo Mzena hospital. Viongozi wengi vigeugeu lakini sio Magufuli.

Alizilinda rasilimali za Taifa kwa kumaanisha.

Weka na za kwako tuone.
 
Usafi wa jiji

IMG_0521.jpg
 
Chuma Magufuli

Akipatia Jambo, amepatia. Tulifurahi.

Akikosea Jambo, amelikosea. Tuliumia!

Mazuri yake ni mengi. Kitabu cha walau kurasa 500 kinaweza kubeba mema machache aliyotenda kwa nchi yetu.

MHSRIP
 
Magufuli aligeuza nchi na kuifanya kuwa ya vitendo, siyo ya maneno maneno na njia za mkato mkato tu. Nina wasiwasi nchi itarudi kwenye maneno mingi na misheni town zitazaliwa upya tena.

Katika line up iliyopo, sioni mtu ambaye ni wa matendo decisively kama alivyokuwa Magufuli, labda Kassim Majaliwa tu. Huyu Mama Samia kwa vile position yake ilikuwa ni ya kivulini, siwezi kuelewa philosophy na approach yake ya uongozi, lakini in the end, maneno mingi na misheni town vinarudi nchini.
 
Kwa kweli sijafurahi kabisa kumpoteza kiongozi mahiri kama john pombe magufuli alikua hodari sana katika uongozi wake mianya ya rushwa alikomesha, uonevu, huduma katika taasisi za kiserikali zilikua zikitolewa kwa heshima na bila ubaguzi, kajenga miradi mingi sana nchini, elimu bure, miundombinu, hudumu hospitalini ziliboreshwa, huduma za maji mikoa mbalimbali alitoa fedha miradi ikamilishwe, uwanja wa ndege wa mwl Julius Nyerere aliukarabati kwa ufupi Rais wangu kifo chako John Pombe Magufuli umeniachia simanzi moyoni mwangu,
Umesahau Umeme
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom