Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,319
33,125
Posti ya Twitter inayodai serikali imesitisha somo la Historia ya Tanzania ya kumtukuza hayati rais John Magufuli SI KWELI.

Posti inakiunganishi kwenda katika tovuti inayoeleza kwa undani juu ya taarifa hizi. Tovuti inaeleza kuwa vitabu vipya vya “Historia ya Tanzania” vilivyokuwa vimechapwa kwa agizo la rais Magufuli, aliyekuwa rais wa awamu ya tano Tanzania, havitatumika tena.

Badala yake, vitaandaliwa vitabu vingine kwa sababu sehemu kubwa ya historia hiyo “ilikuwa imeandikwa kama propaganda za kusifu watawala na kubeba taarifa nyingine zisizokuwa sahihi, hasa katika kuelezea mwenendo wa kuimarika kwa uchumi na maendeleo ya siasa nchini Tanzania”.

Tarehe 12 Februari 2021, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako alitangaza kuandaliwa kwa muhtasari wa vitabu vipya vya somo la historia ya Tanzania kama alivyoagizwa na rais Magufuli.

Prof Ndalichako alidai somo hili litafundishwa sambamba na somo la Historia ambalo bado linaendelea kufundishwa kuanzia Julai 2021. Waziri alieleza vitabu hivi bado vinaendelea kuandikwa, kwa ajili ya vidato vyote yaani darasa la kwanza mpaka darasa la saba.
Hata hivyo, Taasisi ya Elimu Tanzania yenye mamlaka ya kuratibu mitaala ya elimu nchini, imekanusha taarifa hii katika ukurasa wake wa Twitter na kueleza kuwa habari hii ni feki.

Vilevile, kwa mujibu wa matokeo ya kutafuta chanzo cha taarifa kupitia Crowdtangle, taarifa hizi zilianza kusambaa tarehe 11 July 2021, siku ambayo chapisho hili lilitolewa.

PesaCheck imechunguza Posti ya Twitter inayodai serikali yasitisha somo la Historia ya kumtukuza hayati rais John Magufuli, aliyekuwa rais wa awamu ya tano Tanzania, na kugundua SI KWELI.

Chapisho hili ni miongoni mwa muendelezo wa makala ya kuangalia ukweli ya PesaCheck kwa ajili ya kubaini maudhui yanayoweza kua habari za uongo katika mtandao wa Facebook na mitandao mingine ya kijamii.

Kwa kushirikiana na Facebook and mitandao mingine ya kijamii kama hii, Mashirika ya kuangalia ukweli kama PesaCheck yanasaidia kubaini ukweli katika maelezo.Tunafanya hivyo kwa kuwapa umma maelezo kwa upana na undani wa machapisho wanayoyaona katika mitandao yao ya kijamii.

Je, umekutana na habari unazofikiri ni za uzushi au maelezo ya uongo kwenye mtandao wa Facebook? Hii ndo namna unaweza ukaripoti. Na haya ni maelezo zaidi kuhusu njia ambazo PesaCheck inatumia kuangalia maudhui yenyekuzua maswali.

Chapisho hili la kuangalia ukweli limeandikwa na msahili ukweli wa PesaCheck Najma Juma na kuhaririwa na mhariri msaidizi wa PesaCheck Rose Lukalo. Makala hii imepitishwa kwa uchapishaji na mhariri mkuu Enock Nyariki.


SERIKALI YASITISHASOMO LA KUMTUKUZA MAGUFULI.jpeg
 
Tayari mzungu ashapemyeza mkono hapo atuchagulie cha kuweka humo. Hapo wanaandaa mitaala inayoendelea kumshusha mtu mweusi tena
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom