Je, unaielewa vipi nchi ya Italy?

Je, unaielewa vipi nchi ya Italy?

Naomba kufahamu iwapo Italy hutumia watawa zaidi katika shughuli za ujasusi (espionage) katika mataifa mengine!
 
Okay,
Umetia doa mjadala kwa kuingiza mihemko ya kidini.
Mimi siyo mtu wa dini wala sifuati dini hata siku moja.
Naangalia historia kwa vyanzo vya kihistoria siyo vyanzo vya kidini.

Sasa unavyotoa madai kwamba mimi ni Mprotestant you are getting personal and this whole thread becomes pointless.
Tungeendelea kujadili lakini huwa sifagilii hizi Protestant-Catholic sentiments mlizozileta humu.
Haya kukusaidia tu ndugu yangu.
Mimi sina shuruba na Wakatoliki nimesoma shule zao Jesuits , na wala siyo hizi unazozijua wewe.
Hata nikikuambia asilimia kubwa ya elimu yangu nimeipata kwa hawa jamaa hutaelewa mpaka uwe umesoma kwenye vyuo vyao.
Hivyo nawaheshimu sana wakatoliki kama navyoheshimu dini zingine.

Huu mjadala uishe kwasababu hatufiki popote.
Hasa pale unapoanza kuleta Ad Hominen Arguments.

And with San Marino we all know what Pope Niccolo did, so its not something to brag about. We know the role she played during thirty years war prior to West-Phalia.
Ungejua haya usingeuliza hili swali kuhusu Saint Marinus, history of awe still lingers in Europe.
Thanks kwa maelezo mengi ulioyatoa kwenye huu uzi hakika nimejifunza mengi, ninatamani ungeelezea hayo ya san Marino pia tuongeze maarifa/ufahamu.

Huyo jamaa anaekuja na mihemuko ya dhehebu Mpotezee hataki ku-think of the box
 
Lucius Quinctius Cincinnatus alikuwa dikteta wa huko Roma(Italy ya sasa) aliyetawala 458BC na 439BC Huyu jamaa kwanza hakupenda kuwa dikteta ila alilazimishwa na wananchi wa Roma awe dikteta wao baada ya kusaidia kuyapiga vita na kushinda makabila ya Aequians, Sabines na Volscians.

Pamoja na kusaidia kushinda na kupata fursa ya kufanywa dikteta kwa lazima huyu jamaa alikataa na kuamua kurudi zake kijijini kulima na kujifanyia shughuli zake za kujikimu. Kutokana na tukio hilo hadi leo anaenziwa kama alama ya watu wenye kujitoa kutumikia wananchi na taifa na sio kujinufaisha wao.

Kwa heshima yake kuna mji unaitwa Cincinnato, huko Lazio, Italy, Cincinnatus huko New York na Cincinnati huko Ohio ambapo yote imepewa jina lake katika kumuenzi.

Pia kuna sanamu lake kubwa limejengwa katika bustani za Tuileries huko Paris hii yote ni katika kumuenzi huyu jamaa
 
Tofautisha ukristo na ukatoliki, roman catholic maana yake ni iliyokubalika roma na hapo ni baada ya ku edit sana mpaka wakaridhika na maudhui yake enzi za akina Constantine kama sikosei nitarudi kusahihisha kama nimekosea jina la huyo jamaa... Hii thread ni tamu sana hii...
Hii nani alikufundisha ..

Umeenda shule kusomea ujinga..??
 
Umeelezea historia nzuri sana kuwa kaisari kostantino ndie hasa mwaasisi wa ukatoliki. Alipoona watu wanapenda ukristo, akakubaliana nao lakini kwakuchanganya ukristo na upagani. Mungu wao jua alikuwa akiabudiwa siku ya jumapili Sunday. Akaamuru ibada zote zifanyikie jumapili badala ya jumamosi (sabato) sabato ikimaanisha siku ya pumziko 'rest day' ambayo wakristo wote walikuwa wakiabudu km ilivyoandikwa. Kostantino akaizika rasmi na kupeleka ukristo uabudu ktk siku ya ibada ya kipagani Sun day ili kuwavuta wapagani wawe wakristo kwakukana maandiko na kanuni ya Mungu muumbaji. Utabiri wa Daniel ukatimia kuwa ' ...atabadili majira na sheria' (za Mungu) tangu hapo mpk leo jumapili ikawa siku rasmi ya ibada duniani kwa wakatoliki na waprotestanti wengi.
Hivi nani alimlaani Ellen G White..??
 
Hata mi ndugu nashangaa watu kusema konstantino ndo muanzishi wa ukatoliki, hivi hii inakuwaje konstantino kuanzisha ukatoliki? Inabidi tu watu wajue ukatoliki ndio ukristo wenyewe na misingi ya kikatoliki ipo enzi na enzi.
Hawajui historia..Wamelishwa matango pori..
 
Mkuu Lumumba uko deep sana,i like that.Wakristo/wakatoliki wengi hawajui historia ya ukristo/ukatoliki.Wamebaki na waliyokaririshwa tu sunday schools,halafu watakubishia pasi kujua kuwa hawajui wanachokibishia.Wanadhani Ukatoliki ulianza tu ghafla baada ya Yesu kumwita Petro ni mwamba!
Wakristo wote ni Wakatoliki iwapo wanatumia Biblia..Biblia ni ubunifu wa Kanisa..Daah
 
Mkuu upo chaka mbaya tafsiri ndogo sana inakuyumbisha hivi, msikariri kutoka kwa mapadri someni na myachambue maandiko, yesu aliposema hivyo hakumaanisha kujenga ukatoliki bali kupitia petro atalijenga kanisa kwa maana ya kwamba petro alipewa mamlaka ya kutoka Israel na kwenda kwa watu wa mataifa kuhubiri habari njema ya yesu au kueneza injili, ni sawa na hii habari ya kitabu cha matendo, petro anaonyeshwa wanyama pamoja na ndege ambao wengine ni najisi na anaambiwa chinja ule, hapa alikuwa anaambiwa nenda kwa mataifa kahubiri maana kipindi kile wayahudi waliwaterm watu wamataifa ni najisi na injili haikutakiwa kufika kwao, sasa hapa watu wamekaririshwa kuwa petro ameruhusiwa kula vyakula vyote ndo maana watu wanasosi kitimoto kwa sababu ya andiko hili kutafsiri sivyo, mkuu petro aliambiwa kuhubiri kwa watu wote duniani ndo maana yesu akasema hivyo kupitia yeye atalijenga kanisa. Sasa waroma nao wameenda kujenga kanisa sehemu au katika kaburi la petro maana petro aliuliwa italy na kuzikwa hapo ambapo lilipo kanisa la st peter Vatican, lengo ni kuhalalisha kuwa petro ndo muuanzilishi wa ukatoliki hadi kimuita papa wa kwanza wa kanisa katoliki, muanzilishi wa katoliki ni mfalme constantine.
Kwaio watu waamini maneno yako waache mengne...
Very funny....
 
Mkuu huwa nasikia kwamba Ardhi yao kwa asilimia kubwa inafanana na ya Dodoma kwa hapa Tanzania. Na kwakuwa wao ni walimaji wakubwa wa Zabibu walivyofika Tanzania na kufanya tafiti wapi ardhi inayoendana na yao ili zabibu ziweze kustawi wakapata Dodoma. Na kuna ukweli fulani huwa na uona kwamba mji unao pendwa na wataliano hapa Tanzania ni Dodoma. Kuna siku nilisafiri kwenye basi na mtaliano mmoja kutoka Dom kuja Dar na alikuja kama mtalii tu na safari ya Dar ilikuwa anaendelea mpaka Zanzibar akawa ananipa hizo habari kuwa wataliano wengi wapo Dodoma na ndio alienda kuwatembelea jamaa zake. Unajua lolote kuhusu hili?
Soma mabandiko yangu vizuri,
Ukristo ulianzia Uyahudi pale Mashariki ya Kati.
Mashariki ya Kati ilikuwa Chini ya dola ya Mrumi.

Kumbuka sana,
Ukristo haukuanza kwa watu wengine ila Mitume wa Yesu tu na ulikuwa unadhaniwa ni kwa ajili ya Wayahudi tu na siyo mataifa. Hapa hoja ya Orthodox na Ukatoliki haina mashiko kabisa.
Mitume wakiongozwa na Petro walihubiri Injili kwa Wayahudi tu.

Aliyeeneza Ukristo kwa mataifa alikuwa ni Mtume Paulo baada ya kubatizwa mnamo mwaka 35 .B.K.
Vyanzo vinaonyesha kuwa ni Mtume Paulo, Barnabas, Cephas na Yakobo ndiyo walipeleka Injili kwa mataifa.
Walenda sehemu kama Korintho, Ufilipi, Antiokia, Galatia, Uyunani na mwishowe Paul alienda kuhukumiwa na Kaisari Nero huko Roma.

Hapa unasemaje kuwa Ukatoliki ulikuwepo wewe?
Mwandishi na mwanafalsafa mashuhuri wa kipindi hicho Josephus aliyezaliwa mwaka 37.B.K anasema Ukristo na Kanisa la Kwanza lilianzia Uyahudi. Hapa mataifa tulikuwa hatujui Ukristo.
Ukatoliki ndiyo umekuja baadae kabisa.

Cha kujiuliza,
Siku ya Ibada ilikuwa ni Jumamosi lakini Warumi walitawala Uyahudi yote hadi kufanya siku ya Ibada iwe Jumapili.
Rumi yote ikafanya ibada iwe Jumapili, kuanzia Roma hadi Uyahudi.
Nakubali katoliki ni dhehebu lakini limekuja baadae sana na limeanzishwa na Warumi.
Hapana unakosea...Katoliki ndio dhehebu la kwanza kabisa...Labda tuseme jina Katoliki lilianza kutumila lini...

Hili jina la Katoliku kama sijakosea lilianza kutumila baada ya Mtaguso wa Nicea ukijikita zaidi kutafuta ni creed gani itumike kwa wakristo wote kukiri...

Ndio hapo kanisa likawa ni moja, kila kitu ni kimoja, ibada ni moja, lugha ni moja(Kilatini) imani moja....Hivyo likawa ni kanisa la wote(Universal)

Likapatikana neno moja la Kigiriki Katoliko's maana yake moja au iliyooenea kila maali
...Hapo ndio Kanisa likaamua kujiita Katoliki la Mitume....Ni kanisa Lile la Mitume kina Petro na Paulo na Wenzake..

Soma tena historia...Jina Katoliki lilichelewa kidogo kutumika ila Kanisa ni lile lile la mwanzo
 
Sometimes mtu anaweza kuiita Cr7 ilmradi afurahishe nafsi yake....
Wakat sio kweli
 
Uko sawa, na ndio hoja yangu hiyo, labda sijaeleweka vizuri. Kimsingi nilikua najaribu kuonyesha chanzo cha ukristo ambao later ulitekwa na waroma na hatimaye kuzaliwa kanisa katoliki. Pia nikatika kutofautisha ukristo na ukatoliki kupitia historia. Ukiisoma vizuri comment yangu utaona haitofautiani na yako nilichosema ndio ulichosema with even more details on the reason of why Jesus was crucified.
Wewe ndo unachanganya mambo....
 
Ok.....this time nitafanya maamuzi magumu........
Nataka kupanda tax aina ya boat.......
Pretta mrembo uko wapi?,nimekimiss mpaka nakosa amani jamani,unitumie hata kiss moja hewani jamani mwaaaaaaah.
 
Hapana unakosea...Katoliki ndio dhehebu la kwanza kabisa...Labda tuseme jina Katoliki lilianza kutumila lini...

Hili jina la Katoliku kama sijakosea lilianza kutumila baada ya Mtaguso wa Nicea ukijikita zaidi kutafuta ni creed gani itumike kwa wakristo wote kukiri...

Ndio hapo kanisa likawa ni moja, kila kitu ni kimoja, ibada ni moja, lugha ni moja(Kilatini) imani moja....Hivyo likawa ni kanisa la wote(Universal)

Likapatikana neno moja la Kigiriki Katoliko's maana yake moja au iliyooenea kila maali
...Hapo ndio Kanisa likaamua kujiita Katoliki la Mitume....Ni kanisa Lile la Mitume kina Petro na Paulo na Wenzake..

Soma tena historia...Jina Katoliki lilichelewa kidogo kutumika ila Kanisa ni lile lile la mwanzo

Nakosea kivipi?
Hivi mitume kama Petro, Paulo, Yohana na Yakobo walikuwa Wakatoliki?
Ukatoliki umeanza lini na Ukristo umeanza lini?
 
Back
Top Bottom