Nchi 16 zaungana kulinda Gaza Flotilla

Nchi 16 zaungana kulinda Gaza Flotilla

Zacht

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2020
Posts
1,124
Reaction score
2,471
Gaza flotilla ni msafara wa meli ulioandaliwa na wanaharakati wa kimataifa, mashirika ya kiraia, na watu binafsi wenye lengo la kupeleka misaada ya kibinadamu moja kwa moja kwa watu wa Gaza.

Umeungwa mkono na mataifa 16 ambayo yametoa wito wa kulindwa kwake na kuheshimiwa kwa sheria za kimataifa.

Mataifa hayo ni:
Türkiye, Qatar, Bangladesh, Brazil, Colombia, Indonesia, Ireland, Libya, Malaysia, Maldives, Mexico, Pakistan, Oman, Slovenia, South Africa, na Spain.

Hatua hii imekuja baada ya misafara kushambuliwa na drones wakati ikielekea ikipeleka chakula na dawa kwa raia wa Palestina.

Pia, Italy na Spain zimetuma meli za kijeshi baharini kulinda na kusaidia raia wao waliopo ndani ya msafara huo.

Gaza Flotilla ni ishara ya mshikamano wa kimataifa dhidi ya mzingiro wa Gaza, na kila mwaka hufanyika ili kupeleka misaada moja kwa moja licha ya vizuizi vya Israel.
 
Back
Top Bottom