eden kimario
JF-Expert Member
- Jun 13, 2015
- 10,235
- 16,205
Italy ina eneo la kilomita 301,338.
Mji mkuu wake ni roma mji wenye historia ya dunia nzima.
Kwa mujibu wa sensa yao ya mwaka 2013 ina wakazi 60, 782, 668
Italy pia ni ya 12 kwa uchumi duniani.
Italy pia ina rais aitwae Sergio Mattarela.
Wimbo wa taifa ni fratell d italy au ndugu wa Italy
Pesa inayotumia ni Euro
Sikukuu yao ya jamhuri huisherekea kila june 2 kila mwaka
Sikukuu ya taifa husherekewa kila aprili 25 kila mwaka
Simu ya kimataifa ni+39
Italy iko katikati ya bahari
Italy iko Ulaya ya Kusini
Italy ni moja ya nchi 6 za mwanzo zilizoanzisha umoja wa ulaya
Italy pia ina nchi 2 huru zinazozungukwa na eneo la italy pande zote
Nazo ni san Marino na Vaticano
Je wewe unaifahamu vipi Italy
Karibu uongezee kwa ufahamu zaidi kwa wengine