Je, unaielewa vipi nchi ya Italy?

Je, unaielewa vipi nchi ya Italy?

Mkuu, dini siyo silaha pekee wanayoitumia hawa jamaa. Walishatambua kitambo kuwa kila zama zitakua na silaha zake, transitioning ya sila ya dini walishaanza kuifanya kitambo nadhani utekelezaji wake ulianza katikati ya miaka ya 70 tena wakati silaha ya dini ikionekana ndiyo nguvu kuu na pekee.
Walifanya transitioning hiyo kuelekea kwenye nyanja za kifedha na kiuchumi. Vatican mbali ya nguvu zake hizo zinazotajwa, isisahaulike pia kuwa ni serikali tajiri sana ambayo imewekeza katika kila mrija wa kiuchumi unaoufahamu.
Na katika ufanikishaji wa hayo yote, Jesuits siyo pekee, kuna Opus dei (Kazi/Mkono wa Mungu), kikundi cha siri cha Vatican kilichoanzishwa huko Spain 1928 na Fr. Josemaría Escrivá, na kuthibitishwa na Pope Pius XII mwaka 1950.
Mbali ya mission za siri za kundi hili, wanachama wa Opus Dei wanaendesha shughuli miradi mbalimbali kama vile .
Pia kikundi hiki hufanya mission nyingi za kijasusi.

Uko sahihi kabisa!
Ila kabla ya Opus Dei kuna kitu kinaitwa The Sovereign Military Order of Malta.
Kama uneangalia Movie ya The God father 3 Pale Papa alikuwa anampa kiapo Al Pacino.
Basi alikuwa anakuwa Knight of Malta.

Masunga Maziku utakuja kushangaa Adam Weishaupt The founder of Illuminati was a Jesuit. Lakini kanisa Katoliki linasema alikuwa ameasi ndiyo akaenda kuanzisha The Illuminati.
This is Yet to be Proved. But most importantly is that Adam Weishaupt was a devout Jesuit.
 
Italy ilishawahi kutawala eneo kubwa la dunia kama dola la Mrumi mnamo karne ya 27 B.C hadi 1453.

  1. Walitawala Ulaya mashariki, Afrika na Mashariki ya kati.
  2. Wao ndiyo wanchukuliwa kuwa waasisi wa utamaduni wa nchi za magharibi.
  3. Baada ya Wagiriki wao ndiyo waliandika kazi nyingi za falsafa.
  4. Waliongoza siasa za kisasa tangu zamani. Walikuwa na mfumo wa bunge na upigaji wa kura.
  5. Wameanza kutumia mfumo wa sarafu kabla ya kuzaliwa kristo.
  6. Wameanzisha dini kubwa sana duniani: Roman Catholic.
  7. Baada ya Wayahudi wao ndiyo wanafuata kupigana vita nyingi za kidini. Waliwatumia wafalme wa Ulaya kama Richard The Lion Heart kupigana na Waislamu wa kiarabu na kituruki.
  8. Wameandika kalenda hii unayoitumia leo: Gregorian Calendar.
  9. Walikuwa wanapenda sana utumwa kama mfumo wao wa maisha.
  10. Wanaongoza kwa kufanya mauji ya wakristo kwa kinyama kuliko dini yoyote ile. Kuwatupia kwenye simba na ndani ya ukumbi unaitwa Colosseum halafu watu wanashangilia.
  11. Kulikuwa na madanguro makubwa ya makahaba na ushoga ulikuwepo sana.
  12. Walikuwa na jeshi kubwa sana lenye silaha za kisasa na walishinda vita karibia zote kasoro vita dhidi ya Dola la Kiajemi la Parthia. Moja ya kitu ambacho kilipelekea kuanguka kwake.
Ngoja weekend nifanye yangu halafu nitarudi.
Ukisema wameanzisha dini kubwa ya kikatoliki unakosea kwa kua katoliki sio dini bali ni dhehebu linalomfata kristo na kila alichkifanya ni sahihi kusema katoliki ni dhehebu la kikristo
Lakini pia ukisema dola ya rumi wakati huo ilianzisha ukatoliki unakosea pia kwa kua
Kwa wakati huo madhehebu ya kikristo yalikua mawili tu
Waothodoks na waothodoksi wa mashariki na katoliki pekee
Katoliki lilianza mwaka wa 30 bk
Na wao waliingia katika dola la rumi kueneza habari njema ya kristo
Waliteswa sana na mfalme wa wakati huo alieitwa kaisari nero mwaka 64bk
Mateso hayo yaliendelea mpaka mwaka 313 bk mfalme wa roma kaisari kostantino mkuu alipotangaza uhuru wa dini kwa kila mwananchi wa dola hilo kubwa kwa wakati huo
Hali hii ilifanya wakristo wa dhehebu la katoliki kueneza ukristo bila woga kwa amani na bila fujo zozote na askari wa dola hilo la kirumi kwa wakati huo
Ndipo katika hali hiyo
Kufikia mwaka 380 bk mfalme wa roma wa wakati huo kaisari theodosius aliongokea katika ukristo wa madhehebu ya katoliki
Na kuamuru dhehebu hilo litakua dhehebu rasmi la kikristo la dola hilo la kirumi kwa wakati huo
Hali iliyofanya ukristo wa dhehebu hilo kukua kwa kasi kutokana na wahubiri wa dhehebu hilo kuhubiri bila woga sehemu mbalimbali zilizomilikiwa na dola hilo la kirumi

Sasa ukisema italy ilianzisha ukatoliki utakua unakosea kwa takwimu hizi zinazojulikana
Labdau ungesema roma iliupokea ukristo wa madhehebu ya kikatoliki ukiacha ule wa waothodoksi ambao ulikuepo pia
 
Italy ya sasa:

  1. Ndiyo walioruhusu Vatican iwe ndani ya Italy kwa kusaini mkataba wa Lateran mwaka 1929 kati ya Benitho Mussolini na Papa Pius wa kumi.
  2. Ndiyo waanzilishi wakuu wa vita ya pili ya dunia.
  3. Ni taifa la Ulaya ambalo limewahi kupigwa vibaya na nchi ya Afrika katika harakati zake za Ukoloni. Vita hiyo Alipigana na Mfalme Menelik 2 wa Abyssinia (Ethiopia) na Jeshi la Italia 1896.
  4. Genge maarufu la kihuni la Mafia limeanzia Italia Sicily.
  5. Ni nchi yenye utamaduni wa kupenda kuweka sana familia mbele na watoto wao hutangulizwa mbele. Wanalingana na Spain kwa hili.
  6. Wanajitahidi sana kwenye utengenezaji wa magari, hili lilianza kabla na baaba ya vita ya pili ya dunia. Thanks to Mussolini.
  7. Ni wa pili kuchukua kombe la dunia mara baada ya brazil wenyewe wakichukua mara nne. Na mwaka 1934 na 1938 walichukua makombe mfululizo baada ya dikteta Benitho Mussolini kuwatishia wachezaji wake wasishindwe.
  8. Watalamu wa kutengeneza nguo za ghali. Kuanzia Gucci, Armani, Renato Balestra, Canali etc yote ni Italia.
  9. Wamechangia sana kuendelea kwa music wa classic huko ulaya.
  10. Mwanamuziki mkubwa wa nyimbo za classic bwana Ennio Morricone ni Muitalia, ametengeneza nyimbo nyingi za kwenye movie ya The Good, The Bad and The Ugly.
Naona unaitaja sana vatikano hii ni nchi huru
Pia kuna san marino iko pia ndani ya italy mkuu
 
1. Wanaume wa kiitaliano 1 kati ya 3 wenye umri wa miaka 30 - 35 bado anaishi na wazazi wake.

2.Trafiki wa Italy ni wa pili duniani kwa kutumia gari za kifahari za Lamborghini baada ya Dubai.

3.Italy ina Barabara ndefu zaidi duniani iliyopita chini ya ardhi (tunnel) inayounganisha na Uswizi yenye urefu wa km 57 na ulichukua miaka 17 kukamilika.

4.Waargentina 37% wanaasili ya italy.

5.Italy ni 8 kwa kuwa na uchumi mkubwa duniani.

6.Ni watengenezaji wakubwa wa Wine duniani.

7.Ni kosa kisheria kwa mwanaume kuvaa sketi hadharani.
 
kwa mujibu wa mafundish niliyoyapa "Catholic" maana yake ni "kwa watu wote", ila pia ningependa unipe tofauti ya Ukatoliki na Ukristo
Hawaelewi wanachokizungumzia catholic ni moja ya madhebu ya kwanza ya kikristo dudiani lilianza mwaka 30bk
Mengine ni madhehebu ya kikristo ya othodoksi na othodoksi wa mashariki
 
History na mipango iliuowekwa siku nyingi Karne ya kwanza baada ya yesu, kabla haijakuwepo hata taasisi yoyote ya kidini duniani. So wale ni wenyeji wa duniani hapa kuliko mtu wala taifa lolote
Hapa uko sawa kabisa mkuu
 
Italia ilitawala hadi mashariki ya kati sehemu ambayo ukristo umezaliwa.
Hata ukosoma barua za Ignatus wa Antiokia utakuja kujua kwamba kulikuwa na ukristo lakini Warumi ndiyo wakaanzisha neno Universal Church na Orthodox kwasababu wao walisema wanafundisha mafundisho asili ya Yesu na kanisa la kwanza.
Japo Kaisari Konstantini mfalme wa Rumi ndiye aliyeifanya dini ya katoliki kuwa dini ya dola la rumi.
Wakaamua watu wasiabudu tena siku ya Sabatho bali Jumapili ambayo ilikuwa mwanzo wa juma.

Sasa kanisa la Katoliki chanzo chake ni ndani ya dola la Mrumi ambalo lilitawala hadi Uyahudi.
Labda ulete sababu nyingine kwamba katoliki imeanzia Moshi ndiyo nitakuelewa.
[emoji23] [emoji23] [emoji115]
 
Christians are those who believe in Jesus Christ as the Son of God and encompass many sects. Catholics are a sect of Christianity led by the pope in Rome and following the teachings of the Roman Catholic Church.
 
Hapo ni story ndefu, na inategemea iwe katika mfumo wa kihistoria,kidini,kisiasa au kiutamaduni.
Huwezi kuitenga dhehebu la kikristo la kikatoliki na hitoria ya ulimwengu iwe kisiasa au kiutamaduni kwa kua kanisa hili lilianzishwa mwaka wa 30bk baada ya wakristo waliokua pamoja kujitenga
Ndio wakazaliwa waothodoks wa mashariki na wakatoliki madhehebu ya kwanza ya kikristo duniani
So waothodoks na wakatoliki walishiriki katika kila kitu hata vita zilizoibuka hawa jamaa walishiriki kwa namna moja au nyingine
 
Ukristo ndiyo ulianzia huko...ukatoliki ni chapter nyingine.
Hivi mkuu unajua kutofautisha dhehebu na ukristo? Mashariki walikuako waothodoksi ambao pia ni wakristo waliojitenga pia baada ya kutoelewna ndio kukaibuka wakristo wa katoliki na wskristo wa kiothodoks hawa ndio chimbuko la madhehebu mengine duniani pamoja na uislam pia
 
Christians are those who believe in Jesus Christ as the Son of God and encompass many sects. Catholics are a sect of Christianity led by the pope in Rome and following the teachings of the Roman Catholic Church.
eden kimario naomba uje na hapa, halafu ufunge mjadala hakuna yoyote anaeyeelewa kuhusu ukatoliki, na wanadhani ukatoliki ni dini nyingine zaidi mbali ya ukristo.
 
Ukisema wameanzisha dini kubwa ya kikatoliki unakosea kwa kua katoliki sio dini bali ni dhehebu linalomfata kristo na kila alichkifanya ni sahihi kusema katoliki ni dhehebu la kikristo
Lakini pia ukisema dola ya rumi wakati huo ilianzisha ukatoliki unakosea pia kwa kua
Kwa wakati huo madhehebu ya kikristo yalikua mawili tu
Waothodoks na waothodoksi wa mashariki na katoliki pekee
Katoliki lilianza mwaka wa 30 bk
Na wao waliingia katika dola la rumi kueneza habari njema ya kristo
Waliteswa sana na mfalme wa wakati huo alieitwa kaisari nero mwaka 64bk
Mateso hayo yaliendelea mpaka mwaka 313 bk mfalme wa roma kaisari kostantino mkuu alipotangaza uhuru wa dini kwa kila mwananchi wa dola hilo kubwa kwa wakati huo
Hali hii ilifanya wakristo wa dhehebu la katoliki kueneza ukristo bila woga kwa amani na bila fujo zozote na askari wa dola hilo la kirumi kwa wakati huo
Ndipo katika hali hiyo
Kufikia mwaka 380 bk mfalme wa roma wa wakati huo kaisari theodosius aliongokea katika ukristo wa madhehebu ya katoliki
Na kuamuru dhehebu hilo litakua dhehebu rasmi la kikristo la dola hilo la kirumi kwa wakati huo
Hali iliyofanya ukristo wa dhehebu hilo kukua kwa kasi kutokana na wahubiri wa dhehebu hilo kuhubiri bila woga sehemu mbalimbali zilizomilikiwa na dola hilo la kirumi

Sasa ukisema italy ilianzisha ukatoliki utakua unakosea kwa takwimu hizi zinazojulikana
Labdau ungesema roma iliupokea ukristo wa madhehebu ya kikatoliki ukiacha ule wa waothodoksi ambao ulikuepo pia

Soma mabandiko yangu vizuri,
Ukristo ulianzia Uyahudi pale Mashariki ya Kati.
Mashariki ya Kati ilikuwa Chini ya dola ya Mrumi.

Kumbuka sana,
Ukristo haukuanza kwa watu wengine ila Mitume wa Yesu tu na ulikuwa unadhaniwa ni kwa ajili ya Wayahudi tu na siyo mataifa. Hapa hoja ya Orthodox na Ukatoliki haina mashiko kabisa.
Mitume wakiongozwa na Petro walihubiri Injili kwa Wayahudi tu.

Aliyeeneza Ukristo kwa mataifa alikuwa ni Mtume Paulo baada ya kubatizwa mnamo mwaka 35 .B.K.
Vyanzo vinaonyesha kuwa ni Mtume Paulo, Barnabas, Cephas na Yakobo ndiyo walipeleka Injili kwa mataifa.
Walenda sehemu kama Korintho, Ufilipi, Antiokia, Galatia, Uyunani na mwishowe Paul alienda kuhukumiwa na Kaisari Nero huko Roma.

Hapa unasemaje kuwa Ukatoliki ulikuwepo wewe?
Mwandishi na mwanafalsafa mashuhuri wa kipindi hicho Josephus aliyezaliwa mwaka 37.B.K anasema Ukristo na Kanisa la Kwanza lilianzia Uyahudi. Hapa mataifa tulikuwa hatujui Ukristo.
Ukatoliki ndiyo umekuja baadae kabisa.

Cha kujiuliza,
Siku ya Ibada ilikuwa ni Jumamosi lakini Warumi walitawala Uyahudi yote hadi kufanya siku ya Ibada iwe Jumapili.
Rumi yote ikafanya ibada iwe Jumapili, kuanzia Roma hadi Uyahudi.
Nakubali katoliki ni dhehebu lakini limekuja baadae sana na limeanzishwa na Warumi.
 
mbona china kule wameenda kitambo sana 1582. Mtafute mtu anayeitwa MAtteo Ricci.
Huyu ndio kapeleka china science, masomo kama ya hesabu na unajimu etc, Hadi hawa majesuit wakawa ndio top valuable and trusted advisors wa utawala uliokuwepo wakichukua nafasi kubwa katika utawala na wachina wengi wakajiunga n a jesuits. Wamekuwepo huko katikati ya vita wakeneza dini vipindi tofauti tofauti. Kumbuka vita vinavyoitwa TAIPING REBELLION iloua watu zaidi ya

image52552.jpg
hawa china sio lolote kabisa, dalai lama mwenyew anaanguka na kusujudu.
Hahahaa hiyo ni heshima tu ndugu sio kusujudu
Kama ile watoayo watu wa kijijini ya kushuka kidogo wanaposalimiana na mkubwa
 
Christians are those who believe in Jesus Christ as the Son of God and encompass many sects. Catholics are a sect of Christianity led by the pope in Rome and following the teachings of the Roman Catholic Church.
Kuna kitu hapa watu hawataki kukubali, wayahudi walimkataa yesu kuwa ni mesiha wakamshitaki kwa herode lakini kwa kuwa kipindi hicho wako chini ya roma ilibidi hukumu itolewe na pilato ambaye ni mroma, kwa wanaofuatilia watakumbuka kuwa pilato hakuona kosa la yesu na ikamlazimu kunawa mikono ishara ya kwamba hakitaka ahusishwe na adhabu hiyo.

Wayahudi walimchukia yesu kiasi kwamba walitaka yule mshenzi barnaba aachwe huru lakini sio yesu hivyo, yesu akateswa na kusurubiwa msalabani kwa shinikizo la wayahudi wenzake, adhabu za mijeredi na misalaba ni adhabu zq kiroma tangu zamani hata yesu kazikuta.

Baada ya yesu kufa na kifufuka ndipo ukristo ukaanza, yani kuwa mkristo ni ile kuamini katika yesu na mafundisho yake, ukristo sio dhehebu, ni attribute ya kisema fulani ni mkristo kwa maana fulani anaamini katika yesu na mafundisho yake na yu tayari hata kufa pia.

Wakati petro anaoambana kuimarisha kanisa, waroma walikuwa ni wapagani tupu, ni waroma wachache sana walianza kumuelewa petro na wafuasi wake, na hakuna kitu kilichikuwa kinawaigopesha sana waroma enzi hizo kama atokee mtu awe na ushawishi kwa public, hofu yao kubwa ni mtu huyo anaweza kubalika mpaka awe mfalme pengine, hivyo waroma wakafitini mpaka wakamuua petro, enzi za akina Constantine na inasemekana petro kifo chake kilikua ni cha kujitoa muhanga ili kukomboa wakristo wengi waliokuwa wameshaamini, waroma wakamsimika petro kuwa papa wa kwanza na wakachukua kanisa.

Baada yakuridhika kwamba wamesha ingiza ibada zao za kipagani ndani ya kanisa la petro, wakalibatiza kanisa hilo kuwa Roman Catholic Church, na bishop wa roma akapewa cheo cha upapa.

Harakati hizi ziliendelea katika kulikuza na kukieneza kanisa hili, na ukifuatilia utagundua maasi mengi yakifanywa kwa mwamvuli wa kanisa.

Kimsingi tujifunze, hivi vitu vina historical facts nyingi, mimi mwenyewe ni mkatoliki lakini nimefuatilia mengi sana juu ya dhehebu hili, pamoja na ukweli huu nalikubali na wala sitoki, hakuna dhehebu linalojielewa duniani kama hili na ndio kila kitu.
 
Naona unaitaja sana vatikano hii ni nchi huru
Pia kuna san marino iko pia ndani ya italy mkuu

Mkuu sasa unabisha nini?
Umeusoma huo mkataba nilioandika hapo juu?
Vatican ilikuwa chini ya Italia hadi mwaka 1929 na wala haikuwa nchi huru kabla ya hapo.
Ni Benitho Mussolini ambaye aliiruhusu iwe nchi huru.

Read between the lines ,
Nimeandika kwamba hata hiyo Vatican ilikuwa ndani ya Ancient Italy ambayo ilikuwa ndiyo Rumi.
Kabla ya hapo Papal states were never free from Italy.
 
Hata Kitabu cha SUN TZU (THE ART OF WAR) kwa mara ya kwanza walikipata kabla ya dunia nzima alikuwa ni Jesuit father J.Amiot . Yeye alikitafsiri kwa lugha ya kifaransa mwaka 1782. Sasa kama wao walishatafsiri kitu ambacho sisi tumekijua miaka ya 2000 tu utawaweza kirahisi hawa watu?

Vitabu na maandishi ya Plato na Aristotle yalipotea duniani hapa,
Ila kumbe Waruni na Waarabu walikuwa nayo.
Sasa falsafa yetu hii tunayoisoma imeandikwa upya na hawa jamaa.

Tena hata biblia kabla ya kina Wycleff kufanya tafsiri,
Ilikuwa katika lugha ya kigiriki ambayo ilikuwa lugha ya dola la mrumi kabla ya kilatini.
Basi ilikuwa imepotea ila ilikuwepo kwenye maktaba ya Rumi na Martin Luther anakwambia hukuruhusiwa kuisoma.
Walisoma tu viongozi wakubwa wa kanisa.

Hawa jamaa ni walewale,
na ndiyo dola pekee ambayo imekaa zaidi ya miaka 2000 kwa kweli.
Japo iko Vatican ndogo ila mhhhh hakuna ufalme unaweza kuishi kwa muda hivi.
Vatikani sio ufalme ndugu ni nchi huru ya wakristo wa madhehebu ya kikatoliki ambapo imepewa mamlaka na wakatoliki wote duniani kusimamia mambo yao
Mungu pia yuko nao kwa kua pamoja na mafarakano yote bado lipo tu inaonekana kilichoanzishwa na mungu ni vigumu kufa ila wakatoliki mi nawakubali sana wao na mambo yao tu hawana habari na watu wanaowakashifu
 
Mmmh Mimi bado naamini kuna kitu kimefichwa hapa, huu uwezo sio wa kawaida. Hili kanisa ni zaidi ya taasisi ya dini.
Mungu atakua anahusika hapa sio bure kwa kua mungu pia hajitengi na siasa yupo pia halafu hawa jamaa wanapinga sana ushoga duniani hata mashoga waliojificha ndani yake wanaanza kuondoka mmoja mmoja UN wanapiga kelele we lakini wapi
 
Vatikani sio ufalme ndugu ni nchi huru ya wakristo wa madhehebu ya kikatoliki ambapo imepewa mamlaka na wakatoliki wote duniani kusimamia mambo yao
Mungu pia yuko nao kwa kua pamoja na mafarakano yote bado lipo tu inaonekana kilichoanzishwa na mungu ni vigumu kufa ila wakatoliki mi nawakubali sana wao na mambo yao tu hawana habari na watu wanaowakashifu

Wapi nimeandika ni ufalme?
Mbona unatoa vitu hewani tu mkuu?
Au hujui The Capital of The Holly Roman Empire was the Vatican?

Halafu Vatican haikupewa mandate na Wakatoliki,
Ni Dikteta Musollini ndiye aliiruhusu iwe nchi huru baada ya makubaliano ya Lateran Mwaka 1929.

Yes you are a Catholic and i respect that its your constitutional right to be so.
But your beliefs should not try to pervert the true cause of history.
Historia itabaki kuwa historia tu, haikimbiliki.
 
Back
Top Bottom