Inapokuja mada ya uchawi huwa kuna kuchanganya kati kuwepo ama kutokuwepo huo uchawi, nguvu ya huo uchawi ama manufaa ya huo uchawi, na imani kuhusu uchawi hapa afrika kulinganisha na jamii zengine hasa wazungu.
Kwa mfano unakuta mtu anapinga kuwepo uchawi halafu yale madhara yenye kuhusishwa na uchawi husema ni suala la saikolojia tu, au tabia tu za mtu mwenyewe ila si uchawi, lakini mtu huyo huyo anajenga hoja kwamba kama kweli uchawi upo mbona hatuoni hiki na kile kuonyesha kuwa kama uchawi ungekuwepo basi ungetumika kuleta athari ama kufanikisha hivyo vitu.
Hapo utaona kumechanganywa kati ya uhalisia wa uwepo wa uchawi na nguvu ama manufaa ya huo uchawi, sidhani kama ni sahihi kuweka vigezo kwamba lazima huo uchawi uweze kufanya hiki na kile ndio tukubali kuwa kweli huo uchawi upo wakati hata hayo mengine yote yaliyokuwepo yenye kuhusishwa na uchawi(iwe kwenye tiba, mali, kesi, mapenzi n.k) yanakataliwa kwa sababu hakuna uthibitisho, sasa huko kuweka vigezo kwamba kama uchawi ungekuwepo kungetakiwa kuwe na hiki na kile sioni kama ni hoja ya msingi naona ni kuchanganya uwepo wa uchawi wenyewe na nguvu ya huo uchawi.