Je, ni uchawi au saikolojia?

Je, ni uchawi au saikolojia?

Ukishajua uchawi upo tayari maisha yanakua mazuri?
Hahaha nakumbuka enzi zile za utoto tulikuwa tunatishiwa kuna mijitu mirefu natively yalikuwa yanaitwa GABEBA, aisee maisha yalikuwa magumu mnoo...

Haya mambo ya uchawi imebaki kudhani tu, wanaoamini wana imani yao na wale wanaoamini kuna PEPO nao wameendelea kutenda mema ili wakaishi maishi ya PEPONI. Mambo ni mengi mnoo
 
Hahaha nakumbuka enzi zile za utoto tulikuwa tunatishiwa kuna mijitu mirefu natively yalikuwa yanaitwa GABEBA, aisee maisha yalikuwa magumu mnoo...
Ukute nilikua sijazaliwa 🤣
Haya mambo ya uchawi imebaki kudhani tu, wanaoamini wana imani yao na wale wanaoamini kuna PEPO nao wameendelea kutenda mema ili wakaishi maishi ya PEPONI. Mambo ni mengi mnoo
Yes kaka mambo ni mengi lakini tuzidi kupendana kuhurumiana na kutenda mema kwa wengine
 
Ukute nilikua sijazaliwa 🤣

Yes kaka mambo ni mengi lakini tuzidi kupendana kuhurumiana na kutenda mema kwa wengine
Hahaha miaka ya 1996 nipo kijijini aisee kulikuwa na vitisho sana halafu tulijengewa hofu eti ukimuuwa chura utafunikwa na wingu...

Yes kabisa "UPENDO" ndio imani sahihi, hizi Makanisa, Misikiti ni majengo tu
 
Umekosa hoja mpaka unataka kubishana kuhusu jina? Kwani neno uchawi maana yake ni nini kwa kiingereza si ni occultism?
Kwa hivyo vitu visivyo onekana ndio occultsim?
Una elimu gani wewe?

Kama unajua logic, taja hiyo fallacy niliyoifanya na uivunje kwa hoja! Don't just throw words around like a child.
 
Kwa hivyo vitu visivyo onekana ndio occultsim?
Una tatizo la reading comprehension?

Mimi sijasema vitu visivyoonekana ndio occultism, nimesema occultism ni mifumo ya maarifa na matambiko ya siri yanayoshughulika na hidden/invisible forces.

Upepo hauonekani lakini sio occultism, ni meteorology! Jifunze utofauti kati ya kitu kipo kwenye kundi fulani na kila kitu kwenye hilo kundi ndicho hicho kitu. Hiyo ndio basic logic.
 
Umezungumzia swala la uchawi na majini, ni kweli kabisa kuna uhusiano mkubwa sana kati ya uchawi na majini

Wachawi na majini ni wadau muhimu sana wa kufanikiwa kwa uchawi,kwasababu mmoja ni boss na mwingine ni mtumwa

Wachawi wanawatumikia Majini,ndio maana kwenye kitabu cha qur'an Allah anasema majini wanawapoteza watu wengi sana kwenye njia ya Mwenyezi Mungu

Kwasababu ukitaka ufalme wa uchawi, jini nae ana masharti yake,ikiwemo umkane Mwenyezi Mungu,ukufuru na mambo kama hayo

Utaambiwa ua mama yako au baba yao au mwanao,kifupi nao wana ile dhana ya no free lunch

Na wachawi wanapewa uwezo na majini kwa kufanikisha mambo yao,mathalani kupaa,kuingia kwenye nyumba kichawi na mambo kadha wa kadha

Kwahiyo ni sahihi kusema huwezi kutenganisha uchawi na majini
Hatari ipo kubwa, vipi kujlhusu wale majini wazurin hawawapi wachawi maarifa?
 
Una tatizo la reading comprehension?

Mimi sijasema vitu visivyoonekana ndio occultism,
Unajua wewe una shida.

Ulianza kusema uchawi ni occultism.

Ukaja kusema uchawi ni metaphysical science.

Ukaja kusema uchawi ni sayansi ya vitu visivyoonekana.

Nikakuuliza, Kwa hivyo vitu visivyoonekana ndio uchawi?

Unaanza kujiuma uma tena.

nimesema occultism ni mifumo ya maarifa na matambiko ya siri yanayoshughulika hidden/invisible forces.

Sasa define,

Uchawi nini?

Science nini?

Occultism ni nini?

Metaphysical ni nini?

Maana unamix mix tu maneno haya.
Upepo hauonekani lakini sio occultism, ni meteorology! Jifunze utofauti kati ya kitu kipo kwenye kundi fulani na kila kitu kwenye hilo kundi ndicho hicho kitu. Hiyo ndio basic logic.
 
Unajua wewe una shida.

Ulianza kusema uchawi ni occultism.

Ukaja kusema uchawi ni metaphysical science.

Ukaja kusema uchawi ni sayansi ya vitu visivyoonekana.

Nikakuuliza, Kwa hivyo vitu visivyoonekana ndio uchawi?

Unaanza kujiuma uma tena.
Hujui kusoma kwa ufahamu ndio maana unapata shida kunielewa, ili unielewe lazima akili yako iwe sharp, Kama nikisema maji ni H2O, maji ni kimiminika, na maji ni kitu kinachokata kiu, nitakuwa najiumauma au nakupa sifa tofauti za maji?

Occultism ni jina la mfumo wake, Metaphysical Science ni tawi lake la kisayansi, na sayansi ya vitu visivyoonekana ni jinsi inavyofanya kazi. Kila jina linaeleza upande wake. Tatizo unataka ufafanuzi wa neno moja moja kama mwanafunzi wa chekechea!
Science nini?
Science ni systematic knowledge through observation and experimentation.
Uchawi nini?
Haya ni matumizi ya makusudi ya nguvu na maarifa yaliyofichika kubadili au kudhibiti uhalisia kwa kukiuka sheria za kawaida za kifizikia unazozijua wewe.
Occultism ni nini?
Ni jina la jumla la masomo, sayansi, na mifumo ya siri inayoshughulika na mambo yote yaliyofichwa kwa watu wa kawaida. Uchawi ni tawi mojawapo ndani ya occultism.
Metaphysical ni nini?
Ni tawi la falsafa na sayansi linalochunguza vitu vilivyopo beyond the physical realm kama vile uwepo wa akili, roho, nishati, na asili ya ulimwengu.
 
Thibitisha uchawi upo na si hadithi za vijiweni tu.
 
In short, hapa unajifariji tu, ni sawa na mtu anayesema kwa sababu kuna madaktari feki na vyeti feki mitaani, basi elimu ya udaktari haipo kabisa duniani.

Logic haina mashiko hata kidogo.
Mkuu itoshe kusema kuwa. Mimi Edson Kamya (haya ni majina yangu halisia) nimekuruhusu uniroge kwa sharti moja tu.
Ukifanikiwa kuniroga nawe uwe tayari kuweka bayana mchakato uliotumia mpaka ukafanikiwa jambo hilo, na uwe tayari kuwaruhusu watu wengine waitumie njia hiyo kuwaroga wengine then wapate matokeo yaleyale.
 
😅😅
 
Hauna hoja tena, umeamua kuandika utoto sasa, yani ni sawa na mtu asiyejua kuogelea amruhusu papa amng'ate baharini, lakini kwa sharti kwamba papa ampe maelezo kwanza kwa nini meno yake yanauma sana!
 
Thibitisha uchawi upo na si hadithi za vijiweni tu.
Huwa ukizidiwa na kuishiwa hoja unaishiaga kulirudia swali hili hili la kumtaka mtu athibitishe ili tu kumfanya mtu arudie kuandika maelezo yale yale. Huku ni kuchoshana pasipo sababu ya msingi.

Kama umeshindwa kupingana na hoja zangu nilizo toka kukupa, maana yake umekubali kuwa nilicho kueleza ni kweli ndio maana unaishia kutapa tapa tu kurudia swali lile lile.
 
Mimi ni Muislam naamini uchawi upo na unadhuru kwa Idhini ya Allah.

Haifai kujifunza wala kuufanyia kazi uchawi.

Uchawi ni Ukafiri na mchawi ni kafiri na hana lake huko Akhera, namuomba Allah Afya na Salama na ninamuomba Allah Aniepushe na ukafiri na ushirikina, Aamiin.

Uthibitisho wa kuwepo kwa uchawi na kwamba una athari kwa Idhini ya Allah, uthibitisho wake upo katika Wahyi (Qur-aan na Sunnah) na hilo kwa tunaomuamini Allah na Mtume wake Muhammad (Swala na Salamu ziwe juu yake) linatosha kwa wao kutuambia hilo na tukaamini kwa sababu Qur-aan na Sunnah ni Haqq na hazina shaka yoyote.

Lakini pia matukio na yale yanayotokea katika maisha yetu ya kila siku na yanayoshuhudiwa ni uthibitisho pia kuwa uchawi upo. Yaani uchawi ni jambo linalowasibu watu pia kila siku, watu wanaliexperience kwa kusibiwa nayo au kuona wengine wakisibiwa nayo. Uchawi ni jambo linaloshuhudiwa na watu katika maisha. Shuhuda kuhusiana na uchawi zimepokelewa katika habari tokea kale mpaka leo na uchawi umeshuhudiwa na wachawi wameshuhudiwa. Habari hizi zipo katika jamii zote hata ambazo sio za Waislam au Wakristo. Utazikuta Afrika, Uarabuni, Bara Hindi, Kwa Waajemi, Wachina, Wazungu, mpaka jamii za ndani ndani kabisa za binAdamu ambao hawakuwa na muingiliano na civilizations kubwa kubwa na wenzao. Mpaka kwa wakaazi wa asili (natives) wa Australia, New Zealand, visiwa vya Bahari ya Pacific huko, natives wa Marekani, watu wa Amazon, nk.

Kote utakuta habari za uchawi na wachawi. Haiwezekani watu wote hawa mbali mbali kabisa waliotofautiana kidini, kijamii, kiutamaduni, nk tokea kale wote wakubaliane kuwepo kwa kitu ambacho hakipo kabisa kabisa na waelezee experiences zao na shuhuda zao kwa namna inayofanana!

Uchawi upo na wachawi wapo katika jamii zote tokea jamii za kale, wawe ni wamisri, wagiriki, warumi, nk mpaka leo. Mpaka katika nchi za magharibi kuna wachawi mpaka leo na kurogwa kupo na hili linathibitishwa kuwepo kwake katika jamii zote za WanaAdamu.

Wachawi wanashirikiana na mashetani kufanya uchawi wao na kuroga wanaingia makubaliano na mashetani kwa kufanya vitendo vya shirki, kufru na madhambi makubwa makubwa kama wanavyoamrishwa na mashetani kisha mashetani wanawatumikia. Hivyo uchawi ni haramu na ni ukafiri na ni katika vichenguzi vya Uislam.

Uchawi unaathiri na unadhuru kwa Idhini ya Allah. Mtu anaweza kufanyiwa uchawi na ukamuathiri kwa Idhini ya Allah. Na hili ni jambo lenye kushuhudiwa. Mtu anaroga wanandoa wanachukiana, yaani ghafla tu mke na mume wanaanza kuchukiana, mtu anarogwa na anakuwa hawezi kufanya tendo la Ndoa na Mwanandoa mwenzie (mkewe au mumewe), anaweza kumuona mbaya kila akimuona au akamuhisi kinyaa ghafla kila akimuona ila akiwa mbali akawa kawaida na wakati mwengine hata akammisi, au akimuona anamuona mbaya anatisha (literally), au mwanaume unakuta ana wake wengi, akiwa kwa mke fulani hawezi kabisa kufanya naye tendo la ndoa kabisa ila kwa wengine kazi inaendelea, hiyo ni mifano mtu anaweza kurogwa yakamsibu hayo.

Mtu anaweza kurogwa akapatwa na hali katika mwili wake au maradhi na mwengine mpaka anakufa

Ila yote hayo hayamsibu mtu ila kwa Idhini ya Allah.

Sisi Waislam tumefundishwa namna ya kujikinga na Uchawi kwa Ruqyah ya Kishari'ah. Mtume wetu (Swala na Salamu ziwe juu yake) katufundisha namna ya kujitibu tunaposibiwa na uchawi na namna ya kujikinga usitusibu. Na Akatukataza Mtume (Swala na Salamu ziwe juu yake) kuuchomoa uchawi kwa kutumia uchawi mwengine, Mtume katukataza hilo.

Yangu hayo tu katika uzi huu.
 
Huwa ukizidiwa na kuishiwa hoja unaishiaga kulirudia swali hili hili la kumtaka mtu athibitishe ili tu kumfanya mtu arudie kuandika maelezo yale yale. Huku ni kuchoshana pasipo sababu ya msingi.

Kama umeshindwa kupingana na hoja zangu nilizo toka kukupa, maana yake umekubali kuwa nilicho kueleza ni kweli ndio maana unaishia kutapa tapa tu kurudia swali lile lile.
Hakuna hoja uliyotoa zaidi ya blah blah tu!

Hicho unacho kiita uchawi, ulijuaje ni uchawi na si maarifa ambayo wewe umeshindwa kuyaelewa?
 
Hauna hoja tena, umeamua kuandika utoto sasa, yani ni sawa na mtu asiyejua kuogelea amruhusu papa amng'ate baharini, lakini kwa sharti kwamba papa ampe maelezo kwanza kwa nini meno yake yanauma sana!
Irrelevant, huwezi kueleza inachokifanya wewe ni tapeli tu.
Narudia kama unaweza kaniroge. Najua huwezi ......nitakuuliza uthibitishe ulivyoniroga na hautaweza.
 
Hello jamii intelligence 👋

Wakuu hii habari ya uchawi nadhani sio jambo geni
Uchawi ulitajwa kwenye vitabu vya dini hasa hivi maarufu Bible&Qur'an

Kwa bible mfano Kutoka 22:18 inasema:

Usimwache mchawi kuishi
Huu ni ushahidi kua Bible inatambua uchawi

Uchawi umetajwa pia kwenye Qur’an, hasa Al-Baqarah 2:102 ambapo inazungumzia habari ya uchawi na watu kujifunza mambo hayo
Huu nao ni ushahidi Qur'an inatambua habari za uchawi

kwa mantiki hii dhana ya uchawi ni ya kale sana

Huku Africa watu bado wamekumbatia hii imani sana, sijui huko Ulaya ikoje

Utasikia mtu anasema
👇
Mtoto huyu karogwa, sio akili zake.

Hapa tunaona uchawi unatajwa kama kitu ambacho kinaweza kubadilisha hali ya mtu
Alikuwa mzima, ghafla akawa kichaa au mtu asie sawa kama alivyokua kabla

Mtu anaumwa, unaambiwa karogwa

Sasa najiuliza...

Uchawi umetengenezwa au umeundwa kwa kufanya vitu negative tu?

Hakuna namna huo uchawi kama upo unaweza kutumika kwa njia positive?

Yaani tukaamua kutumia akili ya mtu kilaza akawa genius, kama vile inavyoaminika kwamba uchawi unaweza kumbadilisha genius kuwa kilaza?

Kuna hii pia👇

Ooh, wachawi wanapaa usiku...

Kwanini sasa kama hiyo technology ipo tusiitumie kupunguza foleni?

Huo usafiri wa kupaa uwe official sasa

Nyie wachawi wa JF(jokes)
haiwezekani kuwa hivi yaani huu uchawi ukawa na tija?

Hivi uchawi unafanya kazi kweli au ni mambo ya nadharia tu?

Niliwahi kua na matatizo ya kupata maumivu ya kicwa nakizunguzungu

Basi kuna mtu akamwambia mama:

Huyu ShesRise_1 amelogwa asifanye vizuri shuleni na si haba shuleni nilikua najitahidi kwahiyo huyo mama akamuambia mama angu huenda nimelogwa ili nirudi nyuma kimasomo🤔

Heh! 🤔

Nikastuka

Nikawaza, haya yatakuwa mambo gani?

Basi nikaanza kufanyiwa zile zinazoitwa tiba za Kisunna, visomo na mambo mengine

Ajabu ni kwamba kuanzia pale ndiyo kwanza nikaanza kupata maruerue.

Usiku naogopa kulala mwenyewe.

Naota ndoto za ajabu, heh... tafrani mtindo mmoja

Kumbe ile issue ya kuanza kuota mauza uza ni kwa sababu
ya saikolojia bana
Yaani saikolojia kwa maana baada ya kusikia nimelogwa na kupelekwa kwenye visomo

Ndiyo ubongo ukaanza kuniundia mapicha picha

So nilivyoambiwa tu vile, akili yangu na ubongo wangu vikaanza kujishughulisha na hayo mambo

Mara nione hiki...

Mara nisikie kile...

Mara nianze kujiuliza, Hivi huu ni uchawi gani?

Asieee!

Nikakaa nikasema:

Hapana, hizi mbona kama fix?

Na mimi by nature nina kaubishi fulani sipendi kumezeshwa mambo japo mwanzo wali ni win

Nikaacha kabisa huo upuuzi

Nikaamua ku-clean akili yangu

Kuanzia hapo nikiambiwa

Njoo kwenye visomo

Nawaambia

Mimi sina tatizo lolote

Na kweli, nilifanya vipimo hospitali nikambiwa kicwa kilikuwa kinauma kwa sababu sikuwa na damu ya kutosha, na ndiyo maana nilikuwa naumwa kicwa na kizunguzungu

Na hata sijui ilikuaje na mama akaingia kwenye mtego wa rafiki yake akaacha kunipeleka hospital kwanza akaanzia kwenye imani huku

Nikatumia zangu dawa nikawa fresh

Sijaumwa tena kicwa, labda cha mafua tu

Sioni mauza mauza wala nini

Naishi vizuri kabisa

Ndipo nikaja kugundua kumbe mambo mengine ni saikolojia tu

Wala hakuna cha uchawi wala nini

Na kuna hii pia ya majini kutaja uchawi bila majini sio sawa ni mtu na shoga yake

Sasa imagine eti mtu anapandisha mashetani anataka dhahabu...

Heh! Dhahabu sasa inatoka wapi yani?

Mashetani wana migodi yao huko?

Nimetoa mtazamo wangu kuhusu hii dhana ya uchawi

Je, uchawi ni nguvu halisi?

Au wakati mwingine tunaita kitu uchawi kumbe kuna sababu za kiafya, kisaikolojia au mazingira ambazo hatujazijua?

Na kama kweli uchawi una uwezo wa kumbadilisha mtu kutoka kuwa genius mpaka kilaza...

Kwanini usitumike kinyume chake?

Au kama wachawi wanaweza kupaa...

Kwanini bado tunakaa kwenye foleni?

Kama hii dhana ya uchawi haina tija kwanini tuna ing'ang'ania?

ShesRise_1 ✋️
Nakupa hii CODE na uizingatie

Kitu chochote ambacho ni IMANI basi ujie ni kitu ambacho HAKIPO au huna UHAKIKA nacho………. So Uchawi na vitabu ulivyo vinukuu vyote ni IMANI

Kitu chochote ambacho KIPO hakiwezi kuwa IMANI…….. Huwezi kusema NAAMINI Trump ni Rais wa Marekani au kusema naamini kuna Bahari ina maji mengi kwasababu ipo na hawezi kuwa IMANI

Ukisema NAAMINI chumba namba 5 kina Nyoka…… kikifunguliwa ikawa yupo huwezi tena kusema UNAAMINI kuna nyoka, utasema chumba kina nyoka sababu ni uhalisia(fact)
 
Back
Top Bottom