Je, ni uchawi au saikolojia?

Je, ni uchawi au saikolojia?

Kama una amini kuna negative energy, basi uchawi upo.
Siamini kwenye kuamini.

Sihitaji kuamini.

Nahitaji kujua kwa uhakika, ushahidi na uthibitisho.

Kama unasema Uchawi upo, Kwanza eleza Uchawi ni nini?

Na unathibitishaje ni uchawi na sio maarifa ambayo wewe umeshindwa kuelewa?
 
Acha kujifanya Thomaso wa karne ya 21, uhakika unaoutaka wewe unaishia kwenye mipaka ya macho yako tu.

Dunia haisubiri wewe uelewe ndio iwepo. Unaishi kwa kukariri machapisho ya wazungu huku ukisahau kuwa misingi mikubwa ya quantum physics yenyewe inakiri uwepo wa nguvu msizoweza kuziona au kuzithibitisha kwa macho (dark matter). You don't need proof, you just need a wider worldview.
 
Kwa hiyo nguvu zisizo thibitishwa kwa macho zinaitwa uchawi?

Nakuuliza hivi, uchawi ni nini?

Usizunguke zunguke!!
 
Uchawi upo tena kwa makundi tofauti na kazi tofauti (wachawi,waloz,wamazingaumbwe,majini,mizimu na hata wazungu wanatambua kwa majina ya kikwao kama gosti,mirako,wichikrafti,)
Hebu tutajia kwa kifupi hayo makundi na kazi zake na faida zake
 
Kwa hiyo nguvu zisizo thibitishwa kwa macho zinaitwa uchawi?

Nakuuliza hivi, uchawi ni nini?

Usizunguke zunguke!!
Uchawi ni sayansi na maarifa yaliyofichika yanayotumia nishati ya asili na nguvu za kiroho kubadili uhalisia bila kufuata sheria za kifizikia unazozijua wewe.
 
Onyesha ni wapi hoja yangu haifuati mantiki badala ya kujificha nyuma ya maneno makubwa unayoyajua maana yake nusu nusu.
Uchawi ni nini?

Sayansi ni nini?

Unasema Uchawi ni sayansi!!

Yani unatumia neno lilelile kudefine lingine.

Huna tofauti na mwanafunzi aliyeulizwa, What is blood pressure? Akajibu; Blood pressure- Is the pressure of the blood.
 
Mimi sijajibu uchawi ni uchawi, mimi nimesema uchawi ni occult science. Neno sayansi maana yake ni knowledge attained through study or practice. Tofauti ni kwamba sayansi unayoijua wewe ni ya vitu vinavyoonekana na uchawi ni metaphysical science.

Ni mifumo miwili tofauti ya maarifa, hapo kuna tautology gani sasa, au umekimbilia kulinganisha mifano ulivyokariri tu?

Huu mfano wako unaonyesha ni jinsi akili yako ilivyo finyu kwenye kuchambua lugha, kama nikiulizwa sayansi ya siasa ni nini? na nikajibu ni sayansi inayochunguza mifumo ya utawala, hapo nitakuwa nimetumia neno lilelile, hiyo itakuwa ni fallacy? Hapana! Kwa sababu sayansi ni broad category na siasa au uchawi ni matawi maalum ndani ya hilo kundi.

Rudi darasani ukajifunze jinsi ya kufanya classification of concepts kabla ya kuleta mifano ya kitoto hapa.
 
Tangu lini vitu visivyo onekana vikaitwa uchawi?

Unafanya fallacy halafu ukibanwa unaanza kuruka ruka hapa!

Tangu vitu visivyo onekana vikaitwa uchawi?
 
Umekosa hoja mpaka unataka kubishana kuhusu jina? Kwani neno uchawi maana yake ni nini kwa kiingereza si ni occultism?

Una elimu gani wewe?
Unafanya fallacy halafu ukibanwa unaanza kuruka ruka hapa!

Tangu vitu visivyo onekana vikaitwa uchawi?
Kama unajua logic, taja hiyo fallacy niliyoifanya na uivunje kwa hoja! Don't just throw words around like a child.
 
Karibu brother

Kaka nimeelewa visa vyako vyote
Umesema kua hua kuna mambo ma 3

1 Tukio
2 Tafsiri
3 Ushahidi

Hiyo no 3 kimsingi ndiyo yenye mantiki
Tunaohoji kuhusu uchawi hua tunataka Ushahidi strong lakini ushahidi unakosekana mwisho mtu unaambiwa haya ni mambo ya rohoni

Kama wewe sio wa rohoni huwezi kuelewa
na hapo ndipo mjaadala unaanza kua mgumu na kukosa mvuto

Sasa nikuulize wewe una elewa vipi maana hapo ni kama umeongea kwa ujumla sana bro
Nimesemauchawi unaweza kueleweka kama imani au vitendo vinavyodhaniwa kutumia nguvu zisizo za kawaida ili kuleta matokeo fulani, kama kumdhuru mtu, kumlinda, kumshawishi au kubadilisha jambo fulani.

Lakini ni Imani au vitendo vinavyokosa tafsiri ya Kisayansi na hapo ndipo inapobakia Kudhania tu.

Kwa kuongezea kwa kadri tunavyokuwa karibia miaka 40 sasa sehemu za Ibada hasa Makanisani siku zote Waumini na Viongozi wao wa Kiroho wamekuwa wakipambana sana na haya mambo pamoja na kujaribu kubadilisha mbinu za kuyashinda lakini bado haya mambo hasa ya Uchawi, majini na mizimu naona ndio yanazidi kupata umaarufu. Na ndio maana nikasema kuna mambo matatu ya kuzingatia. Tukio liinaonekana sio la kawaida na Tafsiri inaonekana ni Uchawi lakini Ushahidi unakosekeana.

Mada ni pana sana na inahitaji ufikirisho mwingi.
 
Aiseee🤔

Dhana ✔️

Shukran brother Asante kwa maoni
Kwa vile umesema mada ni pana basi tutazidi kueleweshana taratibu
 
Vitu kama hivi huoni kama ni matatizo ya akili sasa hapo kuna kitu gani cha furahisha kwa mtu alie timamu ?(kama kweli wanaweza kufanya hayo)

Hivi humu hakuna mchawi atueleze kuhusu haya maumbo ya kichawi ?
Au wewe unayafahamu ebu dokeza ni maumbo ya namna gani?
Watu wanaojua kuwa uchawi upo ndio wanaoishi maisha mazuri hapa duniani. Wanaosema "namuachia Mungu" wana maisha magumu sana.
 
Back
Top Bottom