Unajua mkanganyiko uko wapi mkuu ni kwamba ukiacha kuamini hizo issue za uchawi wala hutouona kabisa kwenye maisha yako
Huoni hapo kama kuna walakini?
Kama ipi share basi tujifunze
1.Kijana A alimtukana kijana B halafu kijana A(Mtukanaji) akapindishwa mdomo on the spot na kijana B(Mtukanwaji) tena alimwambia kabisa "Mimi huwa situkanwi"
2. Kuna mchawi mmoja mwaka huu huu alijaribu kutunishiana misuli na mimi kwa kujaribu kuniua kwa kunisababishia ajali mbaya ya gari. Ajali haikutokea kwa sababu ya Ulinzi ninaolindwa nao 24/7. Nikiri tu kwamba under normal circumstances mimi sikupaswa kuwa hai. Nimekingwa na mashambulizi ya kichawi mengi sana na mengine ni kutoka kwa ndugu zangu wa damu!
3. Mwingine alinijia usiku mnene nikiwa nimelala ili aniwangie akidhani simuoni kumbe namuona fully. Nilichofanya ni kumkata jicho tu kisha akatokomea kwa hofu
Yatosha kwa leo!
UJUMBE: Kuna tofauti kati ya kuamini uwepo wa Uchawi na kuishi kwa kuutumainia uchawi. Wengi huwa wanachanganya Kati ya haya mawili. Wapo ambao wanaamini kwamba kutoamini uwepo wa Uchawi ni Njia ya wao kuwa salama dhidi ya Uchawi jambo ambalo si kweli.
Ukweli ni kwamba kama mtu hana Ulinzi wa Kristo Yesu ndani yake basi hata ajilinde vipi hayupo 100% safe dhidi ya hatari mbalimbali za kiroho ukiwemo Uchawi na za kimwili pia
ZABURI 91
10 Mabaya hayatakupata wewe, Wala tauni haitaikaribia hema yako.
11 Kwa kuwa atakuagizia malaika zake Wakulinde katika njia zako zote.
12 Mikononi mwao watakuchukua, Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.
13 Utawakanyaga simba na nyoka, Mwana-simba na joka utawaseta kwa miguu.
14 Kwa kuwa amekaza kunipenda Nitamwokoa; na kumweka palipo juu, Kwa kuwa amenijua Jina langu.
15 Ataniita nami nitamwitikia; Nitakuwa pamoja naye taabuni, Nitamwokoa na kumtukuza;
16 Kwa siku nyingi nitamshibisha, Nami nitamwonyesha wokovu wangu.
YOHANA 10
10 Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.